Roketi ya Vigo yashindwa kuingia kwenye orbit

Mzawa_G

JF-Expert Member
Feb 27, 2014
667
1,467
Kama chombo kitafikia kasi inayohitajika katika eneo fulani anga za mbali basi moja kwa moja chombo hicho kitaingia katika orbit husika huko anga za mbali ila kama chombo kitashindwa kufikia kasi hiyo moja kwa moja chombo huanguka.

Masaa machache yaliyopita shirika la anga za mbali ya Umoja wa Ulaya lilijikuta likiingia katika hasara ambayo ilitokana na chombo chao kushindwa kufikia katika eneo lengwa la orbit na kujikuta likibaki angani kama uchafu kama ilivyo kwa satellite zilizokufa au kuisha muda wake.

Mara baada ya second stage ya rocket hiyo kuanza kusukuma mzigo ambao ulikuwa ni satellite ya shirika la ndege za Airbus NEO 5 na 6 dakika kadhaa engine za second stage za rocket hiyo zilizima na kuacha kuzalisha thrusters na kupelekea chombo hicho kushindwa kusukuma kuelekea mbele na huo ndio ulikuwa mwisho wa mission hiyo.

Tunahitaji kasi kubwa ili chombo kiweze kubaki katika orbit kasi kubwa itakayoweza kushinda kani ya uvutano wa Dunia yetu na kupelekea chombo bila ya kujalisha uzito wake wa kiasi chochote kuendelea kubaki katik orbit kwa kuzunguka Dunia yetu.

Kwa eneo la orbit ya kwanza ya Dunia yetu huwa tunahitaji kiasi cha kasi 7.2 kilomita kwa sekunde moja hivyo kama chombo kitaweza kufikia kiasi hicho cha kasi basi moja kwa moja kitabaki katika orbit ya kwanza ya Dunia yetu.

Mahesabu makali huwa yanafanywa na wanasayansi kabla ya chombo kutaka kwenda anga za mbali ili waweze kufahamu ni kiasi cha engine ngani ambazo zinahitajika kuweza kunyanyua mzigo uliolengwa kwenda anga za mbali.

Gerald
geraldchristopher1@gmail.com
FB_IMG_1671646671297.jpg
 
Duh, najaribu kufikiria, kama kilikuwa ni chombo kilichobeba wanaanga kwenda anga za mabali, halafu inatokea situation kama hiyo; mahesabu yamefeli, hapo itakuwaje?
 
Ngoja tusubiri kina Mwakyembe wenye fani muhimu zaidi waje kuwaps mawazo ya namna ya kukikwamua.

"Law is not for everybody" - alisikika mwamba huyo akijishasha.
 
Back
Top Bottom