Angalia picha hii kwa umakini halafu ueleze umegundua nini

Mzawa_G

JF-Expert Member
Feb 27, 2014
667
1,467
Utakuta watu wamebeba huku huyu wa chini akiwa na hali fulani kama ya kuelea kabisa bila ya kujali mzigo alioubeba mgongoni ila bado hakukuwa na chance ya yeye kuanguka hadi chini

Inatuaminisha kutokuwepo kwa kani ya uvutano katika eneo fulani au kani ya uvutano kuwa ndogo zaidi haya ni moja ya matokeo yake ambapo kitu au binadamu hupoteza kabisa uzito au tuseme hujihisi kuwa mwepesi kiasi kwamba huepelekea yeye kuelea katika eneo lolote huko anga za mbali ndani ya chombo

Katika eneo la Low earth orbit uwepo wa kani ya uvutano ni mkubwa sana ambapo kasi ya chombo pekee ndio huitajika kuweza kushindana na kani ya uvutano ya dunia yetu na kuwezesha chombo hicho kuweza kubaki katika eneo hilo kikizunguka dunia yetu

Angalia wanaanga wote wamekuwa wepe si kiasi kwamba hata wakibebana bado hawawezi kuhisi aina yoyote ya uzito

Moudyswema
Tanzaniascienceyetu
AstronomyKiswahili


FB_IMG_1675283176155.jpg
 
Wanaanga wakiwa katika chombo cha ISS wanakuwa na majukumu makubwa mawili.

Mosi, kufanya majaribio ya vitu walivyoenda navyo ili kupata majibu sahihi, pili kihakikisha usalama wa chombo chao ili wazidi kuishi huko salama.

Wanaanga wanaoenda huko huwa wabobezi wa Sayansi katika nyanja zote. Ila binafsi nimegundua licha ya kuwa wao ni wabobezi wa Sayansi bali pia sehemu kubwa huwa na mafunzo ya kijeshi, tena sio wanajeshi wadogo bali ni wakubwa hasa.

Kazi ya kushughulikia ISS imegawanyika, kuna mitambo ya Ndani na kuna mitambo ya nje. Kutoka nje sio kazi ndogo hata siku moja( spacewalk) kunahitaji ujasiri mkubwa na lazima uwe na mavazi maalum.

Mpk sasa hakuna mtu aliyewahi kutoka nje ya dunia na kujaribu kuvuta hewa moja kwa moja ya anga la nje ya dunia. Ingawa kuna mwanaanga mmoja alishasema anga linanuka kama kuni zinazoungua.

Ukiwa huko anga la nje ya Dunia hakuna juu wala chini. Unaweza kudondosha kitu ukashangaa kinapaa zaidi kuliko kishuka chini, ukashangaa kinaenda mbele yako zaidi, ndio kimedondoka hicho.

Hao wanaanga wenyewe wakidondoka si kweli watadondokea huku duniani, wanaweza kwenda sehemu nyingine yoyote huko angani.

Pichani hapo mjuba huyo akiwa ameshika mavazi yake kabla haja ya vaa, na picha zingine hapo akiwa nje anafanya kazi.

Haya mavazi ni mazito kwa kilo, yanazaidi ya kilo 35. Ila kwa kuwa huko hakuna kani basi yamepoteza uzito.
 
Bendera ya US na Israel..
Yeah!

Katika safari hii kulikuwa na Mwisraeli wa kwanza kwenda anga za juu - kanali wa jeshi la anga la Israeli aliyeitwa Ilan Ramon. Ndiyo maana waliweka bendera ya Israeli katika safari hii.

918533450.jpg


Kwa bahati mbaya hii ilikuwa ndiyo safari yake ya kwanza na ya mwisho maana wakati wa kurudi duniani shuttle yao (Columbia) ilisambaratika huko Texas dakika 16 tu kabla hawajatua kwenye kituo cha NASA cha kurushia vyombo na maroketi ya anga za juu cha Cape Canaveral huko Florida.

Screenshot_20230202-092557_Chrome.jpg
 
Yeah!

Katika safari hii kulikuwa na Mwisraeli wa kwanza kwenda anga za juu - kanali wa jeshi la anga la Israeli aliyeitwa Ilan Ramon. Ndiyo maana waliweka bendera ya Israeli katika safari hii.

View attachment 2503353

Kwa bahati mbaya hii ilikuwa ndiyo safari yake ya kwanza na ya mwisho maana wakati wa kurudi duniani shuttle yao (Columbia) ilisambaratika huko Texas dakika 16 tu kabla hawajatua kwenye kituo cha NASA cha kurushia vyombo na maroketi ya anga za juu cha Cape Canaveral huko Florida.

View attachment 2503358
Bila kusahau kuwa ilo tukio lilitokea miaka 20 iliyopita
 
Hawa wanaandaliwa wakiwa wadogo , naona hata sura zao zinaonesha ni mabarobaro kabisa
Wengi wao huwa ni marubani wa ndege za kivita jeshini huko kwa hivyo wana uzoefu na hekaheka za kuruka na haya mavyombo ya hatari. Hata hivyo mara moja moja NASA huchukua hata raia wa kawaida ambao hawana uzoefu wo wote. Ila ni lazima wawe physically fit maana hupitia mafunzo makali na ya muda mrefu kabla hawajaweza kwenda huko anga za juu.

Elon Musk na mabilionea wenzake ndiyo wanajaribu kubadilisha hiyo hali kwa kuanzisha utalii wa watu wa kawaida ambapo hata mimi na wewe tutaweza kutalii huko anga za juu ali mradi tuwe na uwezo wa kujilipia nauli na gharama zingine (dola milioni 20+) kwa kila abiria...
 
Back
Top Bottom