Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 280,547
- 729,426
Tuna tafsiri roho kama moyo na moyo kama roho! Ni makosa makubwa tunafanya...!
Roho si kitu cha kuona kwa macho kusikia kwa masikio wala kushika kwa mikon. Roho haina mfano bali ni jambo la kufikirika zaidi kuliko uhalisia. wengi wetu huchanganya roho na moyo, lakini ukweli ni kwamba moyo ni kasha tu la roho katika mwili.
Roho ni nguvu ambayo huleta uhai popote, nguvu hii sio solid state kwamba unaweza kuiona na kuishika..kamwe huwezi fanya hivyo. Roho ni kiasili cha namna yake hivyo kutaka kudili nayo usiwaze wala kuwa na kitu kinachoonekana kwa macho.
Matunzo ufahamu uelewa na utunzaji wa roho ni kitu kimoja tuu PUMZI
PUMZI kivipi? Tafakuri jadidi tafakuri maizi tafakuri pumzi kwa kupitia hapa ndio utaweza kuifahamu na kuielewa roho yak.
Miili yetu si chochote bila roho maisha yetu si lolote bila roho vitu na mawazo yetu si chochote bila roho roho ndio uhai roho ndio ufahamu roho ndio maisha