Mkomawatu
JF-Expert Member
- Oct 13, 2012
- 277
- 135
Habari zenu ndugu wanaukumbi! Awali ya yote nitoe pole kwa familia ya Al-marhum mzee Ally Sykes kwa kuondekewa na kipenzi chao, lakini pia msiba huu ni wetu sote Watanzania kwani hakika marehemu ni miongoni mwa makamaradi waliopigania uhuru wa Nchi yetu, Mungu amlaze mahali pema peponi.
Ndugu zangu binafsi kiasili ni mtu Kilosa ndiko chimbuko la wazazi wangu, ijapokuwa nimekulia Dar, wilaya yetu ya kilosa ni kongwe mno hapa nchini tangu enzi ya utawala wa Wajerumani na hata Waingereza Kilosa ilikuwa mbele kwa viwanda vya malighafi na hata miundombinu ya barabara, lakini miaka 51 ya uhuru wetu ikiwa chini ya uwakilishi wa Wabunge wa CCM katika vipindi vyote hadi sasa chini ya Mustafa Mkulo, wilaya yangu kipenzi imeendelea kuadhibiwa kwa kudunishwa bila kujua kosa lake, Kilosa mjini hakuna hata barabara ya lami, miundombinu mibovu, huduma za afya hazikidhi mahitaji, halmashauri imejaa wizi kila mwaka hati chafu, elimu imeshuka, mafuriko yameacha watu kama yatima walioachiwa magofu bila uangalizi wowote!, kilosa nakulilia hivi tulikosa nini sisi mbele ya Mungu? Nadhani imefika hatua mapinduzi yafanyike ili kuondoa laana hii ya kukosa maendeleo, nia tunayo, uwezo tunao, vijana wenye uwezo wa kusimamia na kutetea wilaya yetu tupo naomba kuwasilisha.