Kocha Rogath John Stephen Akhwari Ashinda urais wa shirikisho la riadha Tanzania -RT kwa kura 27 na kumbwaga mpinzani wake Nsolo Malongo Mlozi aliyepata kura 20.
Mpinzani wake baada ya kushindwa aliandika hivi kwenye mitandao ya kijamii
" Kura hazikutosha kushinda, nimeshika nafasi ya 2 (kura 20). Mshindi ni Rogath John (kura 27) baada ya kurudiwa mzunguko wa 2 kikatiba. Namshukuru Mungu na kheri kwa washindi. Shukrani pia kwa wajumbe" alisema Nsolo Mlozi.