Rocket ya China ndio inategemewa kugongana na 'Moon' /Mwezi na siyo Falcon 9 kutoka kampuni la SpaceX.

Kichwa Kichafu

JF-Expert Member
Apr 13, 2017
44,629
188,885
Habari,

Hivi karibuni kulisambaa habari za roketi inayotarajiwa kugongana na Mwezi/Moon mwezi ujao march ambazo kulikuwa na makosa ya kutambua roketi hiyo kwa kusema ni aina ya Falcon 9 inayomilikiwa na kampuni la SpaceX.

Taarifa za mwanzo ilitambulika kama ni Falcon 9 za mwanzoni kabisa kurushwa angani mwaka 2015 ambayo ilibeba satellite ya kuchunguza hali ya hewa ya anga katika orbit iliyokaribu kabisa na pointi ya kwanza ya Lagrange, DSCOVR "Deep Space Climate Observatory Satellite"

Kumbe rocket ambayo inategemewa kugongana na Mwezi ni ilirushwa kutoka China ambayo inafahamika kama Chinese Long March 3C Rocket.

Bill Gray ambaye ni mnajimu na mtafati wa kujitegemea aliwahi kuitambua rocket ya SpaceX mwaka 2015 kwa kutumia software ya kufatilia vitu angani vilivokaribu na dunia.

Gray anasema rocket hiyo mwanzo ilipewa jina la WE0913A ilipishana na mwezi siku mbili tu baada ya kurushwa kwa DSCOVR.

"Mimi na wengine wote tumeweza kukubaliana kwenye kutambua mgawanyiko katika hatua ya pili ya Falcon 9 kwa usahihi kabisa. Tulitambua namna ya mwanga ulivyotokea kama tulivyotegemea pia muda wake vile vile kama tulivyotegemea kwenye orbit husika" Gray alinukuliwa kwenye mazungumzo.

Gary anasema baada ya taarifa hizi za utafiti wake kuchapishwa Jon Giorgini kutoka NASA's Jet Propulsion Laboratory (JPL) alimtafuta Gray na kuulizwa maswali machache juu ya utafiti wake huo.

Jon Giorgini alikuwa na shauku zaidi kwenye hoja za Gray za kusema DSCOVR zilipishana kwa ukaribu na mwezi siku mbili tu tangu ilirushwe toka duniani. Na alihoji kwa maoni ya kusingewezekana trajectory ya rocket Ilivyokuwa imebeba satellite hiyo kuwa na ukaribu kupita kiasi kuelekea kwenye mwezi.

"Ni kitu cha kushangaza kama ni kweli hatua ya pili ya Falcon 9 ipite karibu kabisa na mwezi wakati huo huo DSCOVR iwe upande mwingine wa pili kabisa wa anga. Tunafahamu ndio uwa kuna mgawanyiko ila hili linaleta mashaka maana ni utofauti mkubwa kama Ilitokea" Ameeleza Gray muda si mrefu kupitia website yake kutoa matukio yanayoendelea.

Baada ya kufahamu ili Gray alienda kutazama data za mwanzoni na kupelekea kuja na hitimisho jipya "Kitu hicho kinachotegemewa kugonga mwezi ni kifaa cha hatua ya tatu ya mgawanyiko wa Chinese Chang'e 5-T1 mission iliyorushwa October 2014 na roketi ya China ambayo ni Long March 3C Rocket.

Njia/Trajectory Iliyorushwa Na Muda zilikaribia kufanana sana na DSCOVR mission hivyo kusababisha mkanganyiko kwenye kutambua roketi ipi inayotegemewa kugongana na Mwezi.

Taarifa kutoka NASA zinasema Collision hiyo inategemewa kutokea March 4 saa 07:26EST kwetu itakuwa kama saa tisa mchana hivi na Rocket hiyo kwa sasa imejulikana kama Chinese Chang'e 5-T1 booster iliyorushwa mwaka 2014.

Matokeo ya mgongano huo hautoweza kuonekana kutokea duniani ila inakadiliwa mgongano huo utasababisha crater yenye urefu wa kuanzia 10mita hadi 20mita. Mashimo hayo yatakuja kusaidia na kudhihirisha vyema kwa watakao kuja kujifunza mambo ya geology vizazi na vizazi.

Nawasilisha Mzee Mkoloni.

Cc: Kichwa Kichafu
 
Back
Top Bottom