Road licence kuwekwa kwenye mafuta sio uamuzi sahihi na athari yake ni kubwa zaidi ya tatizo

wametumia neno linalopunguza makali kwa watanzania

siyo road license ni ongezeko la kodi kwenye mafuta. kwa maana kwamba road license imefutwa na mafuta yameongezewa kodi kwa jina la road license

na athari za kupanda gharama za mafuta kwa kuongezea uliyoweka ni kwamba kwa utility machinery lazima waongeze bei ya huduma na ya bidhaa, gari linalobeba nyanya au mahindi lazima mmiliki aongeze bei ambapo mlipaji wa mwisho ni mlaji (consumer)

nitarudi baadaye
 
mbona ewura tunawalipa kwa kila lita na hujalalamika..hizo mashine na generator ewura wanahusoka naz???!!...huu mfumo ni mzuri kwa nchi nyingi sana na uko poa tu...achen mawazo ya kimaskini...
Hujui kuwa hata EWURA wanakwenda kufaidika kwa kuongeza bei ya mafuta?
 
Hujui kuwa hata EWURA wanakwenda kufaidika kwa kuongeza bei ya mafuta?
wanafaidika siku zote..mleta mada kayatetea sana magenerator na mashine za nafaka..ndo nikauliza mbona huko nyuma hawakulalamika au ewura wanahusoka pia na hizo mashine!?....ain hii ya ulipaji ni mzuro swma tu labda hiyo tsh 40ipunguzwe....
 
Hujui kuwa hata EWURA wanakwenda kufaidika kwa kuongeza bei ya mafuta?
wanafaidika siku zote..mleta mada kayatetea sana magenerator na mashine za nafaka..ndo nikauliza mbona huko nyuma hawakulalamika au ewura wanahusoka pia na hizo mashine!?....ain hii ya ulipaji ni mzuro swma tu labda hiyo tsh 40ipunguzwe....
 
Ata kama road license ingebaki mafuta yangeongezwa kodi tu,bongo kila kitu bahati mbaya ata kila mtz apewe gari bure bado tutajadili
 
Watu wenye majenereta wanasumbua sana na kuleta visababu kupinga utaratibu mpya wa Road Licence. Nawaomba mkae kimya maana na nyie tunawavumilia sana na makelele yenu mtaani na mijini. Pia mnapaswa kuchangia kwa sababu mnachafua mazingira kwa moshi wa vijenereta vyenu. Tulieni sindano iwaingie.
 
Ikiwa mfumo utakua hivyo inamaana serikali itajiongezea mapato na ndicho serikal ya awamu hii wanachoitaji ....ina maana mtumiaji wa gari atalipa pesa nyingi kuliko ile ada ya kila mwaka akilipa road licence katika mafuta. .......
 
Hata sekta ya usafiri ina multiplier effect. Tatizo hatuna takwimu. Haina maana kuweka kodi ambayo inakuwa ngumu kukusanya. Kuna watu kwa Road Licence ya laki 3 kwa mwaka, wamelimbikiza wanadaiwa mpaka milioni 10. Sasa hapo serikali inanufaika vipi na mfumo huo wa kutoza kodi? Tukitaka kujua ukweli wa jambo hili tujiulize ni asilimia ngapi ya wenye magari wanalipa road licence? Naamini haizidi 50%.

Kuhusu utaratibu unaoshauri wa kutoa taarifa TRA kama gari haitumiki/mbovu ili usidaiwe hiyo kodi: unachoshauri kimekaa kinadharia sana,kiuhalisia kinaleta mwanya mkubwa sana wa kukwepa kodi na kufanya administration ya hiyo kodi kuwa ngumu sana. Kuna watu wanapaki magari kwa sababu wanaenda nje ya wilaya, mkoa, au nchi. Kuna wanaopaki magari sababu ya vipuri, kuna wanaopaki sababu ya ubovu wa gari kiujumla. Ni mfumo gani unatumika kumtambua msema kweli na muongo?

Mbona hatuwalalamikii EWURA kwa kuweka makato yao kwenye umeme na mafuta wakati umeme bado ni ghali kwa mtanzania wa kawaida? Kodi yoyote ni mbaya sana, lakini lazima ilipwe.
 
Mtoa mada na Watanzania wengine wanaolalamikia bajeti hii nawaombeni tujifunze kuheshim Mitazamo ya wengine.

Naamini uamuzi wa kuondoa kodi ya road licence utakuwa umefanyiwa tafiti na wataalam. Kama ndiyo basi tujifunze kuheshim maono na taaluuma za wenzetu. Si vema kupinga kila kitu cha Serikali. Hebu tujifunze kujifunza toka kwa Watanzania wenzetu pia.
 

Kwa lugha rahisi ni kuwa, road license imefutwa, kilichobaki ni kodi ya vyombo vinavyotumia nishati ya mafuta

Mfumo wa kutoa taarifa TRA kuwa chombo hakitumiki ni too mechanical, na unatengeneza mianya ya rushwa na kuikosesha serikali mapato na mfumo huo umeonesha kutokuwa na ufanisi na una usumbufu mkubwa,
 
Poorest analysis.. This is the best way ever to pay road licence.. Maana yake sasa hakuna uongo uongo, kodi stahiki italipwa sasa, uchambuzi wako hauna mantiki hata kidogo, huu ndio mfumo almost dunia nzima wanalipa hivyo.. Wewe kama hutaki kaishi mwezini au tembea kwa miguu usiharibu barabara zetu..

 
Road license haikuwa kodi rafiki, mtu alitozwa kodi kwa kosa la kumiliki hata gari chakavu. Hivi kuna faida gani ya kulipishwa kodi ya kitu usichokitumia? Inawezekana uamuzi wa kuihamishia kwenye mafuta unaweza kuwa sio sahihi, lkn uamuzi wa kuiondoa ni sahihi.

Vv
 
Usiporidhika wewe, wengine wamerudhika. Tena walioridhika ni wengi zaidi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…