Road licence kuwekwa kwenye mafuta sio uamuzi sahihi na athari yake ni kubwa zaidi ya tatizo

bowlibo

JF-Expert Member
Dec 10, 2011
3,182
2,000
wametumia neno linalopunguza makali kwa watanzania

siyo road license ni ongezeko la kodi kwenye mafuta. kwa maana kwamba road license imefutwa na mafuta yameongezewa kodi kwa jina la road license

na athari za kupanda gharama za mafuta kwa kuongezea uliyoweka ni kwamba kwa utility machinery lazima waongeze bei ya huduma na ya bidhaa, gari linalobeba nyanya au mahindi lazima mmiliki aongeze bei ambapo mlipaji wa mwisho ni mlaji (consumer)

nitarudi baadaye
 

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
41,856
2,000
mbona ewura tunawalipa kwa kila lita na hujalalamika..hizo mashine na generator ewura wanahusoka naz???!!...huu mfumo ni mzuri kwa nchi nyingi sana na uko poa tu...achen mawazo ya kimaskini...
Hujui kuwa hata EWURA wanakwenda kufaidika kwa kuongeza bei ya mafuta?
 

jf expert

Member
Jun 5, 2017
14
45
Hujui kuwa hata EWURA wanakwenda kufaidika kwa kuongeza bei ya mafuta?
wanafaidika siku zote..mleta mada kayatetea sana magenerator na mashine za nafaka..ndo nikauliza mbona huko nyuma hawakulalamika au ewura wanahusoka pia na hizo mashine!?....ain hii ya ulipaji ni mzuro swma tu labda hiyo tsh 40ipunguzwe....
 

jf expert

Member
Jun 5, 2017
14
45
Hujui kuwa hata EWURA wanakwenda kufaidika kwa kuongeza bei ya mafuta?
wanafaidika siku zote..mleta mada kayatetea sana magenerator na mashine za nafaka..ndo nikauliza mbona huko nyuma hawakulalamika au ewura wanahusoka pia na hizo mashine!?....ain hii ya ulipaji ni mzuro swma tu labda hiyo tsh 40ipunguzwe....
 

harder king

JF-Expert Member
Jan 21, 2017
3,889
2,000
Ata kama road license ingebaki mafuta yangeongezwa kodi tu,bongo kila kitu bahati mbaya ata kila mtz apewe gari bure bado tutajadili
 

Sooth

JF-Expert Member
Apr 27, 2009
3,921
2,000
Watu wenye majenereta wanasumbua sana na kuleta visababu kupinga utaratibu mpya wa Road Licence. Nawaomba mkae kimya maana na nyie tunawavumilia sana na makelele yenu mtaani na mijini. Pia mnapaswa kuchangia kwa sababu mnachafua mazingira kwa moshi wa vijenereta vyenu. Tulieni sindano iwaingie.
 

fenisher

JF-Expert Member
Apr 27, 2017
292
1,000
Ikiwa mfumo utakua hivyo inamaana serikali itajiongezea mapato na ndicho serikal ya awamu hii wanachoitaji ....ina maana mtumiaji wa gari atalipa pesa nyingi kuliko ile ada ya kila mwaka akilipa road licence katika mafuta. .......
 

Sooth

JF-Expert Member
Apr 27, 2009
3,921
2,000
Ninadhani siku ukija kuelewa multiplying effect ya hili jambo utajua it is not about wanaomiliki generators...na hata wanayomiliki hawamikili kwa anasa au kwamba wanayapenda. Ingeelewa kwama bado tuna kazi ya kufanya na so kukomoana kama unavyojenga hoja yako. Bahata mbaya utakua umechelewa sana na hutakua na njia ya kubadilisha.
Hata sekta ya usafiri ina multiplier effect. Tatizo hatuna takwimu. Haina maana kuweka kodi ambayo inakuwa ngumu kukusanya. Kuna watu kwa Road Licence ya laki 3 kwa mwaka, wamelimbikiza wanadaiwa mpaka milioni 10. Sasa hapo serikali inanufaika vipi na mfumo huo wa kutoza kodi? Tukitaka kujua ukweli wa jambo hili tujiulize ni asilimia ngapi ya wenye magari wanalipa road licence? Naamini haizidi 50%.

Kuhusu utaratibu unaoshauri wa kutoa taarifa TRA kama gari haitumiki/mbovu ili usidaiwe hiyo kodi: unachoshauri kimekaa kinadharia sana,kiuhalisia kinaleta mwanya mkubwa sana wa kukwepa kodi na kufanya administration ya hiyo kodi kuwa ngumu sana. Kuna watu wanapaki magari kwa sababu wanaenda nje ya wilaya, mkoa, au nchi. Kuna wanaopaki magari sababu ya vipuri, kuna wanaopaki sababu ya ubovu wa gari kiujumla. Ni mfumo gani unatumika kumtambua msema kweli na muongo?

Mbona hatuwalalamikii EWURA kwa kuweka makato yao kwenye umeme na mafuta wakati umeme bado ni ghali kwa mtanzania wa kawaida? Kodi yoyote ni mbaya sana, lakini lazima ilipwe.
 

m2020

JF-Expert Member
Jul 10, 2016
971
1,000
Mtoa mada na Watanzania wengine wanaolalamikia bajeti hii nawaombeni tujifunze kuheshim Mitazamo ya wengine.

Naamini uamuzi wa kuondoa kodi ya road licence utakuwa umefanyiwa tafiti na wataalam. Kama ndiyo basi tujifunze kuheshim maono na taaluuma za wenzetu. Si vema kupinga kila kitu cha Serikali. Hebu tujifunze kujifunza toka kwa Watanzania wenzetu pia.
 

marxlups

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
15,364
2,000
Unapoweka road licence kwenye mafuta inamaanisha hata generator unalotumia nyumbani kwako unalipia kodi ya kutumia barabara. Magenereta mengi yaliyo kwenye taasisi za umma ikiwa ni pamoja na pale bungeni yanayotoa backup ya umeme unapokatika, yatalipa road licence. Mwananchi anayetumia machine ya kukata miti au kufyeka majani na fensi nyumbani kwake atakua analipia road licence ya magari. Wanaotumia mitambo ya ujenzi kutengeneza zege au kazi nyingine yoyote ile ya mitambo sasa wanakwenda kulipia road licence. Wanaondesha boats za injini kwenye maji nao watalipia road licence. Kifaa chochote kitakachotumia matufa ya diesel au petrol kitakua kimelazimika kulipia road licence sawa na mwendesha shangingi na mbaya zaidi wote watalipia kwa kiwango kinachofananaIli kuzuia gari ambalo haliendeshwi kwa muda mrefu kwa ubovu au sababu nyingine yoyote ile kuendelea kulipa road licence,


TRA walitakiwa kuweka mfumo ambao mwenye gari atatoa taarifa kwamba gari lake halitumiki kwa kipindi fulani na hivyo kuondolewa kwenye mfumo wa kodi hadi litakaporudi barabarani.

Kwa lugha rahisi ni kuwa, road license imefutwa, kilichobaki ni kodi ya vyombo vinavyotumia nishati ya mafuta

Mfumo wa kutoa taarifa TRA kuwa chombo hakitumiki ni too mechanical, na unatengeneza mianya ya rushwa na kuikosesha serikali mapato na mfumo huo umeonesha kutokuwa na ufanisi na una usumbufu mkubwa,
 

Jay One

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
14,304
2,000
Poorest analysis.. This is the best way ever to pay road licence.. Maana yake sasa hakuna uongo uongo, kodi stahiki italipwa sasa, uchambuzi wako hauna mantiki hata kidogo, huu ndio mfumo almost dunia nzima wanalipa hivyo.. Wewe kama hutaki kaishi mwezini au tembea kwa miguu usiharibu barabara zetu..

 

Vyamavingi

JF-Expert Member
Oct 3, 2014
5,246
2,000
Road license haikuwa kodi rafiki, mtu alitozwa kodi kwa kosa la kumiliki hata gari chakavu. Hivi kuna faida gani ya kulipishwa kodi ya kitu usichokitumia? Inawezekana uamuzi wa kuihamishia kwenye mafuta unaweza kuwa sio sahihi, lkn uamuzi wa kuiondoa ni sahihi.

Vv
 

Congo

JF-Expert Member
Mar 13, 2008
1,664
2,000
Usiporidhika wewe, wengine wamerudhika. Tena walioridhika ni wengi zaidi.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom