Naomba mambo yafuatayo yafahamike.
Mosi, Chadema kwa mujibu wa katiba yake haina udini wala haibagui dini ya mtu yo yote, kwa hiyo, Kiongozi yo yote wa Chadema atakayembagua mtu kwa msingi wa jinsia,dini,kabila nk anakwenda kinyume na Katiba na kanuni zetu. Ktk hilo sihitaji ruhusa yaMbowe au Slaa kuwaelezea. Liko wazi ndani ya katiba.
Pili, nijuavyo, hakuna kiongozi wala mwanachama ye yote wa Chama chetu anayefanya hivyo. Kama kuna mtu yo yote mwenye ushahidi wa jambo kama hilo auweke hapa au anipigie my namba is open. Mimi nitapeleka hoja hiyo ktk baraza kuu la Taifa lijalo ila asilete majungu.
Tatu, kati ya viongozi 6 wa juu kabisa wa Chadema, mkiti Taifa na makamu 2 katibu mkuu na manaibu 2 na Mwenezi. Waislamu ni 4 na wakristo ni 3. Hoja ya udini mtaijadili ktk kikao gani? Kamati kuu imejaa waislamu. Baraza kuu wanataka kila wilaya za bara na visiwani. Je, hoja za udini utajadili ktk kikao gani? Mimi nashauri propaganda hizi za udini ni hatari sana kwa mustakabali wa Taifa letu. Nawashauri kwa upendo na kwa nia njema tuiache vinginevyo tunatafuta balaa.