Riwaya za Greyson

Riwaya za Greyson

bepari tata

Member
Joined
Jan 21, 2014
Posts
7
Reaction score
0
Journey to hell (SAFARI YA KUZIMU)
Mtunzi: Greyson H Mtingwa
Contact: 0742893359

Sehemu ya kwanza

Baada ya kumaliza masomo yangu ya udactari katika chuo kikuu kilichopo katika mji wa California nchini Marekani. Nilikuwa nafanya maandalizi ili nirudi nyumbani Tanzania kutumikia nchi yangu iliogarimika kwa kiasi kikubwa kunisomesha ili nije kuokoa maisha ya watanzania wenzangu wanao teseka na magonjwa sugu especially upande magonjwa ya kina mama na watoto. Majonzi yalitawala maana kutengana na watu niliokuwa naishi nao kwa miaka takribani sita. Ilikuwa zaidi ya ndugu jinsi tulivyo kuwa tumezoeana na wanafunzi wenzangu. Mtu ambaye niliumia kwa kiasi kikubwa kutengana nae si mwingine bali ni Catherine. Catherine alikuwa zaidi ya rafiki kwangu nilimpenda na yeye alinipenda sana japo ote tulikutana chuoni. Catherine alikuwa anatokea katika nchi ya Netherland. Alikuwa msichana mzuri sana mwenye mchanganyiko wa asili ya kiafrika na kizungu. Baba yake na Catherine alikuwa mtanzania lakini mama yake ndio alikuwa mnetherland. Piga picha mchanganyiko wa mwafrika ma mzungu afu angalia mtoto mzuri anavyo tokeza.

"I will miss you so much Greyson" aliongea Catherine huku akiwa kanikumbatia tukiwa chumbani kwangu. Tulikuwa tumekumbatiana huku mikono yangu nikipapasa mgongoni mwake.

"Grey najua unaenda home Tz ila kumbuka kuwa kuna mtu unamuacha huku nyuma anakupendaga sa,,,,,!" Aliongea Catherine kwa kiswahili cha kusuasua ambacho kilikuwa kimeanza kukomaa kutokana na kumfundisha lugha yetu ya kiswahili.

"Usijali mpenzi wangu mimi niko pamoja nawe japo natoka kwenda kufanya kazi nyumba. Acha nikaokoe maisha ya watanzania na waafrika kwa ujumla."
Gafla nilihisi kama ubaridi katika mabega yangu, ndipo nilipo msogeza nyuma kidogo Catherine. Nilikuta akiwa analia machozi yakimtoka kama maji toka yatokayo katika chemichemi zilizo kolea.

"Vipi tena Catherine mbona unalia mimi niwako nyamaza acha kulia. Tuombe mungu one day atatukutanisha mpenzi pia kumbuka our promise tuliokubaliana. Siku itafika na tutaoana na kuishi ote mpenzi." Nilimbembeleza Catherine huku nikimfuta machozi kwa kutambaa

"This is the sensitive issue kuwa mbali na wewe sizani kama ntaweza nimekuzoea Greyson wangu. I fill pain in my heart." Alizidi kulalamika Catherine.

"Sawa usijali mpenzi tutazidi kuwasiliana email zipo na hii globalisation hakuta alibika kitu ila ukipata likizo fanya uje nyumbani Tanzania." Nilimbembeleza sana mpaka akanielewa.
Baada ya maongezi nilielekea bafuni kuoga na kumwacha Catherine akiwa anakunja nguo zangu na kuzipanga katika begi. Mpaka namaliza kuoga alikuwa kasha maliza kila kitu. Tulitoka out na Catherine ikiwa ndio sehemu ya kuagana na mpenzi wangu. Catherine alionekana mtu asie na furaha hata kidogo japo mara kibao nilimfanyia vituko na utani wa hapa na pale ili kumjengea furaha, jambo ambalo kiasi furani nilikuwa linashika nafasi na kupotea tuliongea mengi sana na Catherine aliekuwa akiniasa sana sana nisije kumsaliti. Maana ndie mwanaume niliemfundisha na kumwingiza katika sayari ya mapenzi.

"Nitajituza na kukutunzia penzi lako na kamwe sitampa mtu mwingine zaidi yako."

Majira ya saa tano usiku tulirudi katika chumba nilichokuwa nikiishi, tulilala asubuhi na mapema Catherine aliamka na kuniamsha kwa ajiri ya safari. Safari ilikuwa inaanza saa nne asubuhi. Nilifanya maandalizi saa tatu kamili tulikuwa katika uwanja wa ndege nikulisubili safari ianze tuliagana na Catherine aliyezidi kulia. Sikua na jinsi nilimuacha na kuingia ndani ya ndege kwa ajili ya safari ya kurudi Tanzania. Ndege ilikuwa inaruti ya kupita Sweden, Paris, Ethiopia and then Tanzania. Niliingia ndani ya ndege kisha sauti ya kututaka tufunge mikanda kwa ajili ya safari baada kama ya dakika tano ndege ilianza kuiacha aridhi na kushika anga ilianza. Ndani ya ndege nilikuwa bize nikichati na Catherine nilikuwa nimemwacha nchini Marekani kwa mda wa masaa majira ya saa kumi na moja jioni ndege ilitua katika uwanja wa kimataifa wa Sweden. Tulipumzika pale kwa mda wa dakika 45 kisha safari iliendelea, sasa ilikuwa route ya Paris. Usingizi ulinichukua na nilikuja kushitushwa na sauti ya mwanamke aliekuwa akitangaza kuwa abiria tufunge mikanda yetu na tuzime simu zetu ndege inaenda kutua katika uwanja wa ndege wa Paris. Ilikuwa ni usiku sana katika jiji la Paris lakini mataa yalikuwa yanang'a misili kama mchana vile. watu walipata chakula na safari iliendelea. Kwenye siti yangu nilibaki pekeangu baada ya abiria niliekuwa nimekaa nae siti ya ujirani kushuka katika mji wa parks. Mpaka saa kumi na mbili asubuhi ndege ilitua katika uwanja wa kimataifa wa ndege wa Ethiopia. Walipanda watu wengine hata siti iliokuwa imeachwa wazi ya pembeni yangu ilikaliwa na abiria. Safari iliendelea. Mpaka tunafika katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa mwalimu Nyerere nilikuwa nimechoka sana. Lakini furaha ililejea tena baada ya kukanyaga arithi ya Tanzania. Abiria tulishuka na kuanza kutoka katika uwanja wa ndege. Ndugu, jamaa na marafiki walikuwa wamekuja kunipokea walikuwa wengi kiasi. Sio wao tu pia watu wa hospital ya taifa ya mhimbili walikuwepo pia kuja kunipokea. Nilisalimiana na ndugu zangu kisha tukaagana nao maana nilikuwa naitajika nikaripoti kwanza katika kituo cha kazi.

*************ITAENDELEA***********

Maoni yenu yanakaribishwa.
 
Back
Top Bottom