Riwaya ya Kombora Kiotani

Riwaya ya Kombora Kiotani

KOMBORA KIOTANI-11
BONIFACE BIRAGE
“Defcon1 bado sijaridhika nayo.Na lazima kiongozi yeyote atakayekuja ajue tupo katika hali gani ya kiusalama.Hii inathibitisha kwamba eneo letu si salama kiusalama maana tutakuwa vitani!Msiba huu ni sehemu ya kuimarisha uhusiano wetu kidiplomasia.Wageni watakuja wengi.Hatuwezi kuwa na viwango vya Defcon 1 no sishauri hilo.”mwingine akasema.

“Lakini cha muhimu ni nini kulinda nchi yetu au?Mheshimiwa ukidanganya umma kwamba nchi ipo salama halafu hao maadui wakaja nakuhakikishia vita ikitokea utakuwa hatiani kwa uzembe uliochukua wa viwango vya usalama.”Mambosasa hachelewi kila pembe yeye huwepo.Na lazima hoja zake ziwe na mashiko nakuongoza.Swala la msiba bado lilileta utata.Mambo kadhaa yapo mezani yanahitaji uamuzi wa rais lakini tayari mabishano yamechukua nafasi yake.

“Jamani mimi sioni umuhimu wa kuhatarisha usalama wa taifa letu.Marehemu wanahitaji kuzikwa kwa heshma.Hawa ni viongozi wa taifa wapewe heshma yao.”

“Lakini bado kamati ya msiba haijaundwa na itakapoundwa majibu yatahitajika kuhusiana na viwango vya usalama!”alisema Serambovu kuokoa jahazi.Ilishaanza kuonekana kwamba watu hapa mezani hawakubaliani na mamlaka aliyopewa Kilua.Na walimtafuta kila kwenye uamuzi wake kuingiza propaganda zao ilimradi wa mmalize kabisa!

Kilua muda mwingi alikuwa kimya akisikiliza hoja zao.Bado alikuwa kwenye mshtuko.Alitamani siku ile iishe.Kichwani alikumbuka file namba 13:14.Lilikuwa jambo zito mpaka amepigiwa simu ilitakiwa aliangalie.Lakini nchi ilihitaji umakini wa rais kwa wakati ule.

Kilua akapiga mkono mezani kuonesha anataka kuongea.Wote wakamgeukia huku kila mmoja akitaka kujua kauli yake wakijiandaa kumpingaa!

“Nahitaji viongozi wa kijeshi haraka sana.The situation in Kibatari needs more attention.Kuongeza viwango vya usalama ni priority number moja kwa upande wangu.Kabla hatujaweka uamuzi wa haraka natoa amri we are moving not to any level of defcon condition until futher notice.Then nataka kuongea na rais wa Savanna Lands pili namtaka balozi ikulu ndani ya nusu saa.Majeshi yetu yote yawe tayari lakini hakuna wakuinua mkono kumpiga mtu.Walinde mipaka yetu kama wanavyofanya siku zote.Nimemaliza next ajenda ije mezani!”Kilua aliongea kwa ukali kidogo.Bado hali yake haikushawishi alitamani kuondoka pale aende kupumzika.Kauli hiyo iliwashtua kidogo wajumbe wale wakashangaa.

Kwa namna alivyotoa kauli waliona mwanga kidogo lakini wapo waliobeza kauli zake.Hawakumpatiliza alikuwa mwanamke atawafanza nini?Walijiambia wenyewe kwenye vichwa vyao.

“Lakini mheshimiwa…unajua hili ja…”alikuwa Mambosasa.

“Bwana Mambosasa nadhani nimetoka kwenye hilo.Nimeshamalizana na hilo nataka twende kwenye ajenda nyingine hatuwezi kalia kitu kimoja kuna mambo mengine yanahitaji macho yetu.”alikuwa Kilua.

“Ndiyo mheshimiwa gavana…ooh sorry mheshimiwa rais.Nilikuwa na maanisha issue kuu ni huo ulinzi wa taifa…”alijisahau kiasi cha kuwafanya wenzake wacheke kidogo.Kilua akamwangalia alishaanza kuona ukimbelembele wake.Ila kwenye uongozi lazima ukutane na mambo kama hayo.

“Tafadhali bwana Mambosasa naomba twende ajenda nyingine.”

Ilibidi Mambosasa amuweke rais kiporo kwa hilo.Hakuwa ameridhika kabisa na uamuzi rais aliouchukua.

Wakati bado wanajadili pale Kilua aliona simu yake ikiita.Hakuwa tayari kuipokea lakini alipokumbuka kuna mtu alizungumza naye aliamua kufanya jambo moja.

Alimwita mpambe wake nakumwambia,”Mwambie wakala wa mawasiliano wai-track hii namba sasa hivi nataka majibu.”mpambe hakuwa na ruhusa yakuwa mbali na rais alimpa maelekezo mlinzi mwingine aliyeenda hadi chumba cha mawasiliano akawapa taarifa kwamba namba ile ifuatiliwe.Kilua aliamua kupokea wakati akimzubaisha mpigaji.

“Ndiyo bwana.Rais Kilua anaongea.”
“Nimesema nataka file namba 13:14 naona upoupo tu ajenda zangu huzifuatilii?”sauti ilisema upande wa pili Kilua akaitambua ni ya nani?

“Nimesema sijui kuhusu hicho kitu.”

“You are the president you have the power to get anything I need file number 13:14 now or else?”sauti ilikuwa ya ukali kidogo.Haikuwa na masihara.

“Utafanya nini?”Kilua aliuliza.Aliongea kwa mtindo ambao hakuna aliyehisi ni simu mbaya lakini muda wote huo Serambovu alikuwa anamkazia macho.

“Nadhani ni muda muafaka uonje joto ya jiwe!Unajua mahali mumeo na mwanao walipo?”sauti ilisema kwa ukali tena.

Kilua moyo ulimwenda mbio.Alihisi kichwa kutaka kumpasuka!

“Unasemaje?”aliuliza kwa sauti ya juu kidogo lakini akakumbuka masharti watu wengi hawatakiwi kujua mazungumzo hayo.Kilua akajikoki ili wote wasigundua ni kama wawili ndo walimwangalia.Wakajua kuwa rais lazima uwe na mengi.

“Mumeo yumo mahali namuona alivyo na mawazo mengi.Mwanao mrembo katoto kamevaa gauni la zambarau.Nywele zake tena rasta hizi alisukwa saluni ya Manka Fwaa!...”

Kilua aliijikuta akiinuka kwa haraka!

“Halo?...Halo…?”Kilua alihofu!Sasa alijua simu hii si ya mchezo na yeye ndo alifanya mchezo dhidi ya simu hii.Alipoinuka aliwashtua waliokuwa kwenye kikao.

“Mheshimiwa kuna nini?”

“Sijisikii vizuri naombeni nipumue kidogo.”alijitetea.

“Lakini mheshimiwa tunakuhitaji hapa.Kiota inakuhitaji hapa siokupumzika kwako.”

“Sikubaliani na mapumziko yako au kazi ngumu?”Mambosasa aliropoka.

Kilua alimwangalia tu bila kumpatia ufumbuzi!Aliona ataanzisha mengine.Tayari kesha thibitishiwa kuwa mumewe na mwanaye wanaonekana kwa macho ya sauti ile.Bila shaka hili ni tishio kubwa la kumuweka sawa.

“This meeting shall continue without me.”’alisema Kilua akijiandaa kuondoka.Alihisi presha ikimpanda na alijua akizidisha ataanguka chini.

“Ha!Ha!Ha!”alicheka Mambosasa,halafu akasema,”Tuendelee na kikao cha usalama wa taifa bila rais?Hiki ni kituko.Hebu kaa hapa madam tushughulikie nchi.”kauli ya Mambosasa ikawashtua ilikuwa kama mzaha flani.Na huyo ndo Mambosasa hakopeshi kauli anakurarua mara moja.Ilikuwa mzaha wa kumshtua tu.

Wengine waliomjua walimzoea.

Kilua alimeza hilo lakini alichotaka kujua ni usalama wa famlilia yake kwanza!Ni usiku wake wa kwanza akiwa ikulu zimwi la matatizo limemuandama.Alijikaza kwa kweli.

“Muda simrefu nataka kuongea na balozi wa Savanna Lands na baada ya hapo nitaongea na rais wao.Naombeni mniache kwanza pia nitahitajiika kusema na taifa punde kamati ya msiba itakaapokuwa tayari.”alisema bimkubwa wan chi.

Mara mlango ukafunguliwa akaingia wakala wa taarifa,”Mheshimiwa rais kuna taarifa kutoka ubalozi wa Savanna Lands!”wote waka taharuki.

“Balozi wa Savanna Lands yupo wapi?”

“Hakuwepo ubalozini.Watu wote wa Savanna Lands waliokuwepo ubalozini wa hapo hawapo.Yaani the embassy is empty!”wakal a alitoa taarifa.Kilua akaduwaa.Hiyo ilikuwa na maana nzito.

Bila shaka rais alihitajika mezani.Kuna file namba 13:14,kuna tishio la kumfuta Kilua halafu kuna taarifa ya uwepo wa familia yake matatani.Hii ya kutoweka kwa balozi wa Savanna Lands na watumishi wote wa ubalozini ilikuwa hatari kubwa sana!Ukilinganisha mambo utajua fika taifa la Savanna lilikuwa limeondoa watu wake ubalozini.

“Ni kwamba hawapo wote.Tuna jaribu kuangalia rekodi ya ndege lakini inaonekana hakupanda ndege yeyote.Tumecheki mipakani bado hakuna data za uwepo wa balozi wa Savanna Lands katika ardhi ya Kiota!”wakala aliwasilisha.Kilua akatumbua macho.

“Simu zake hazijafanyiwa tracking?”

“Kama ubalozini hayupo una dhani simu zake atakuwa ameziacha wapi?

“Nipigieni simu Savanna Lands sasa hivi!”alisema Kilua.Muda uleule simu ilipigwa kuelekea Savanna Lands Kilua alizidi kuwa na hali mbaya.Alichanganyikiwa zaidi.Gavana wa Savanna Lands hajulikani alipo.Hiyo ilikuwa tafsiri mbaya sana kwake.

Baada ya mawasiliano kuungwanishwa Kilua alichukua simu,”Huyu ni rais Kilua.”

“Ndiyo bi Kilua naskia umechukua nchi.Hongera.”ilikuwa sauti ya rais wa Savanna Lands.

“Asante mheshimiwa.Naomba kujua kama unataarifa zozote za balozi wako?”

“Hapana niliongea naye mchana.Nikamtumia salamu za rambirambi kwako.”

“Nashkuru kwa salamu.Ila balozi wako katoweka ubalozini hayupo sehemu yeyote.Tumejaribu kupitia kona zote za usafiri lakini hayupo!”

“Mheshimiwa Rais Kilua kwa heshma zote namtaka balozi wangu akiwa hai!”rais wa Savanna Lands alitoa kauli ya vitisho. “Sifahamu alipo balozi.Kwanza majeshi yako yameanza kutilia macho anga langu.Nina taarifa za kiintelijensia kwamba wanajiandaa baada ya kusikia taifa letu limepatwa na msiba!Amri inatoka kwa nani?”
 

Attachments

  • kombora kiotani cover page.jpg
    kombora kiotani cover page.jpg
    37.7 KB · Views: 77
KOMBORA KIOTANI-12

BONIFACE BIRAGE

Kwa sekunde kadhaa rais wa Savanna lands alichelewa kujibu maswali hayo.Simu kama zile mtu alitakiwa awe makini na kauli kosa dogo tu unajimaliza!Kauli zilikuwa tat asana kiasi bimkubwa Kilua alijaribu kudhibitin kauli zake.

“Mheshimiwa sina la kukujibu.”

“Tafadhali kwa heshma zote naomba uniambie kwanini majeshi yako yanajongea kwenye mipaka ya nchi yangu!Mnaajenda gani na taifa la Kiota.Isitoshe balozi wako kapotea na watendaji wote wa ubalozini.Huoni kama hapa kuna swali lakujiuliza?”

“Mheshimiwa kumbuka huku kwenu kuna ubalozi wenu.Kama mmeamua kuuvamia wa kwangu nakuteka watu wangu hii nikutangaza vita!Nakupa mpaka asubuhi nataka majibu yupo wapi balozi wangu la sivyo majeshi yangu yataendelea kujongea kuja kwako.Halafu sina budi bali na mimi nitauangalia ubalozi wako hapa kwa macho ya tatu!”

Ilikuwa kauli moja hatari sana kuwahi kusemwa.Haikuwa yaki rafiki kabisa.Ina maana tayari vitisho vimetoka kinywani mwa rais wa Savanna LANDS.Hakuhitaji maelezo kwa yeyote.Ni kweli Savanna Lands wanatuma vikosi vyao vije mpakani mwake.Lakini swali linakuja ni kweli hawajui balozi wao aliopo?Au ni mtego unachezwa?Hilo lilikuwa swali gumu kujibu kiasi likamfanya rais Kilua kujikuta akiwa kwenye wakati mgumu!Palepale akajua fika hatari imetangazwa na uhusiano wa kidiplomasia kati ya Kiota na Savanna Lands umeingia dosari moja kubwa sana!Ilihitajika kuwa makini.Kilua alijikusanya kutumia busara.

“Mheshimiwa kwa heshma zote naomba tusifikie kwenye swala la kutishiana mataifa yetu yamekuwa na uhusiano mzuri kwa muda sasa…”

“Uhusiano mzuri?...Wewe unasemaje au kuona tumekaa kimya ndo mnajua mambo ni mazuri?Mlichukua eneo letu nabado tunalitaka.Mheshimiwa kwa heshma zote tusirudi tusipopata sisi wote.Nimesema kama balozi wangu hajapatikana mpaka kesho nitalazimika kuchukua hatua…”

Kilua akameza.Mazungumzo hayakuwa mazuri.Na tayari rais wa Savanna Lands alishaelewa saikolojia ya Kilua nakujua atampelekesha anavyotaka.Tayari ulikuwa uadui mwingine anaoneshwa mwanamke huyu na bila shaka alitakiwa kuchukua hatua haraka iwezeka navyo la sivyo angepoteza taifa lake kwa uzembe!Busara zaidi ilitakiwa kutumika.

“Sawa mheshimiwa nimekuelewa nitalifanyia kazi swala lako.”alijibu Kilua akivuta pumzi ndefu na kuzishusha.Palepale kitu kilimtuma ajiuzulu maana anachokutana nacho sikitu cha kuchezea.Upinzani uliopo baina ya watendaji wa serikali ulimthibitishia kwamba kazi ni ngumu.Alijuta kubeba kijiti kile.

“Mpaka asubuhi nahitaji majibu!”alisema rais wa Savanna Lands.Palepale wakakata mawasiliano.Kilua akazimia!Purukushani tena zilianza!Ilibidi achukuliwe aingizwe ndani akapumzike.Kikao kilihairishwa!

Ilikuwa siku ndefu sana.Ilibidi wwatu waende wapumzike kutafakari!


***

Ubichi wa asubuhi hakuleta tabasamu katika taifa hili la Kiota.Mambo yaliyojiri siku iliyopita yalikuwa kwenye kitabu kikubwa cha maombolezo.Tayari hali tete ilikuwa inaendelea.Kilua aliamka nakukuta aliye pembeni yake alikuwa ni Serambovu.Chumba cha ikulu alicholala kilikuwa tofauti na cha kwake.Mbele yake alikuwepo Serambovu na tabasamu la jua la asubuhi.

“Hello my love.”alianza Serambovu.Kilua alimwangalia halafu akamvuta karibu nakumwelekeza aingie kwenye blanketi.Ndani ya muda mfupi tai ya Serambovu ilikuwa pembeni.Huku shati na suruale zikifuatiwa nakutandazwa chini.Joto la mwili wa Kilua lilikuwa la kufariji kwa asubuhi ile.Alihitaji kitu cha kumchangamsha na mchangamshaji mzuri alikuwa kwa asubuhi ile yenye ubichi alikuwa ni Serambovu.Kuna kitu huwa kina mchanganya sana Kilua hasa anapokuwa faragha na bwana Serambovu,hujikuta mwili ukichemka na kuwa na msisimko wa haraka nakujikuta akisahau mambo mengi yenye msingi.Na kweli alisahau.Walizungushana kwenye godoro lile.Kilua alikuwa amepotelea kwenye mahaba ya bwana huyu.Alimuondoa mavazi yake na sasa walikuwa dunia yao wakipeana vile wao tu walivyovijua.

Miguno ya mahaba kati ya Kilua na bwana Serambovu ilisikika kwenye blanketi lile lenye joto pale ikulu.Wakiwa bize kwenye mapenzi yao.Mlango ulifunguliwa kwa haraka bila wao kutarajia.Alikuwa ni binti wa usafi wa pale ikulu.Binti aliona msuguano pale kwenye kitanda wala hakutaka kufikiri mara mbili alijua fika Kilua atakuwa na mwanaume lakini jana rais alipoletwa ikulu hakuja na mumewe na mpaka sasa familia yake haijaonekana.Huyu atakuwa nani?Udadisi ule ulimfanya Yule msichana arudi nje lakini kabla hajatoka alikuwa ameshawashtua Kilua na Serambovu ambao waliinuka ghafla.

“Samahani mheshimiwa sikujua.”alijitetea.

“Funga mlango na utupishe.” aliwahi kuzungumza Serambovu.Lilikuwa kosa kubwa sana kwa rais kufumaniwa akiwa ikulu.Tena mtu asiye mume wake!Hii ilitakiwa kudhibitiwa kwa haraka sana.Aliwaza Serambovu akimrudia bimkubwa.

“Nataka kwenda.”alisema Kilua akiwa amezongwa na joto lamahaba.

“Lakini bado sijatosheka?”

“No kuna majukumu yanatusubiri bora twende na hivi huyu binti katuona lazima twende.Nafikiria kuachia madaraka muda huu.”

“What?”

“Ndiyo kwani lazima kazi yenyewe ngumu na lawama kibao.”

Serambovu alijikuta akimzaba Kilua kofi la shavu!

Halafu akagundua amefanya kosa kubwa sana alijikuta akimshika mkono nakumwambia kwa pupa,”Samahani my dear nimepitiwa naomba uniwie radhi mwandani wangu.”
Kilua moyo wake mtama hasa linapokuja swala la mapenzi kati yake na Serambovu.Kuna kitu huwa akikumbuka kati yake na bwana huyu basi yeye huchanganyikiwa kabisa nakujua kuna mapenzi flani lakini hakujua yapo kiasi gani.

“Nisamehe mumy,Kilua wangu.Tafadhali.”

Kilua hakusema kitu zaidi ya kumshika mabegani akamvutia mdomoni.Serambovu aliamua kumpa penzi zito asubuhi ile yakumchangamsha mwili hadi Kilua akatoa machozi ya furaha.Japo kichwani mwake alimfikiria mumewe pamoja na mwanaye lakini hakujua wapo katika hali gani.Ilikuwa ni saa kumi na mbili asubuhi.

Kilua alienda kuoga pamoja na Serambovu hapohapo chumbani kwake.Ilitakiwa iwe siku akiwa na mumewe lakini bahati mbaya imemkuta akiwa na mchepuko wake wakizini.Baada ya kuoga.Serambovu alivaa nguo zake akatangulia.Kilua hakuwa amekuja na nguo ilibidi abonyeze kitufe Fulani pale wakaja wajakazi wa ikulu.

“Nahitaji mavazi kwa leo.”alisema Kilua akimwangalia.Ndani ya muda mfupi mavazi kwaajili yake yaliletwa akavaa.Japo kichwani alikuwa na mawazoo mengi lakini wazo lakuachia madaraka halikukosekana.Baada ya kuvaa alitoka chumbani nakukutana na walinzi wake wakiwa wanamngoja.

“Habari zenu?”aliwasabahi Kilua.

“Salama mheshimiwa.”

Serambovu akawahi kujumuika kana kwamba hakuwa naye chumbani muda mfupi uliopita.

“Tunaelekea wapi?”aliuliza Kilua.

Sekretari wake akafika pale,”Mheshimiwa utaenda kupata staftahi halafu twende kikao na kamati ya ulinzi.”

Aliondoka moja kwa moja hadi mahali kupata mlo wa asubuhi.Alistaftahi pamoja na Serambovu.Meza ilikuwa kubwa na ilipangwa kwa makockocho mengi hata hakujua aanzie wapi nakumalizia wapi.Watumishi waliovalia vizuri walikuwa wakimhudumia.Kilua alipata chai wakizungumza machache na Serambovu lakini aligeukia watumishi wale.

“Wewe unaitwa nani?”

“Naitwa Maua Shaka.”

Kilua alikuwa akitengeneza urafiki nao awajue.Wengine walimjua alipokuwa anakuja ikulu kwa shughuli za kiserikali na pia kwa mialiko mbalimbali kutoka kwa hayati rais Kisusi.

“Tuna kukaribisha sana mheshimiwa tupo kwaajili yako.”alisema kiongozi wa wawajakazi.Nyuso zao zilionesha matumaini kwa Kilua nakuona kuna watu wanaoonesha Tumaini kwake.Hapo aliridhika kidogo sio wale wajumbe waliomkalia kooni.Alijitahidi kula lakini hakuwa na hamu alijilazimisha maana tangu jana hajaweka kitu tumboni.

Baada ya kupiga zogo na watumishi wale huku akipata chai yake safi Kilua aliondoka nakuelekezwa chumba cha mikutano.Leo alikuwa kachoka hasa kwa shughuli aliyopewa na Serambovu maana kila muda alikuwa anamtizama asijue ampe nini.Bwana huyu alikuwa akigusa sana hasa kwenye sekta ya mahaba.Lakini kabla hajafika kwenye kikao aliambiwa kuna simu kadhaa anatakiwa kuzijibu.Kilua aliingia ofisini kwake kwanza kupokea simu hizo.


Kilua alipokea simu moja ya wapo,”Halo?”
“Mheshimiwa nataka file namba 13:14 bado hujalipata!”mwili wake ukaingiwa na mshtuko kidogo.Sura ya mumewe pamoja na mwanaye vikamjia kichwani.Kilua akaikata ile namba akamwita wakala wa mawasiliano.

“Ndiyo mkuu.”

“Vipi kuhusu ile namba niliyokupa jana ufutailie?
“Mheshimiwa ile namba nimeshindwa kuitrack.Anatumia teknolojia ngumu kwa sisi kuidhibiti!”
 

Attachments

  • kombora kiotani cover page.jpg
    kombora kiotani cover page.jpg
    37.7 KB · Views: 77
KOMBORA KIOTANI-13

BONIFACE BIRAGE

“Kivipi?”

“Mazungumzo yote hatuwezi kutrace hiyo namba.Anatumia secured line!”

“Ina maana hakuna IT anayeweza kuidhibiti hiyo namba?Simu itaingiaje ikulu bila kutrace huo ni upuuzi!”Kilua akawa mkali sana.

“Mheshimiwa hawa watu wanajificha sana.Yaani hata rekodi ya mazungumzo hatuwezi kuipata!”
“What?”Kilua akashtuka zaidi.Kabla hajafanya mengi akaingia mtumishi mwingine akaleta bahasha kwa mheshimiwa rais.Ile bahasha Kilua aliipokea nakuifungua akakutana na picha iliyomtisha sana!Mumewe alikuwa kafungwa kamba pamoja na mwanaye!Kilua alihis kupotea akili!

Walinzi wake waliona jambo lile wote waka taharuki familia ya rais ilikuwa imetekwa!Walinzi walikuwa na wakati mgumu kwani punde tu Kilua alipoapishwa kuna kikosi kilitumwa mahususi kuwalinda familia yake lakini mpaka sasa hawajapata mrejesho ni vile hawakuwa wameuliza.Huo ulikuwa uzembe kwa sheria zao!Kila mmoja alijiandaa kukabiliana na lawama.

“Mheshimiwa tutawatafuta popote walipo watapatikana.”alijaribu moja ya walinzi wale.

“Kwanza sitaki mtu yeyote ajue kwamba familia yangu imetekwa hicho sitaki kijulikane kabisa.Kufanya hivyo ni kuwahatarisha.”alisema akijikaza asiangushe machozi.

“Mheshimiwa lak…”
“Hakuna wakujua kama mume wangu na mwanangu katekwa.Hiyo ni oda!”alisema mheshimiwa rais.

“Lakini.”alitaka kusema kitu Yule wakala wa mawasiliano.

“Hii ni binafsi nisingependa litumike kama ajenda kwa taifa.Tayari tuna matatizo mengi hili litagusa pabaya.”
“Ok mheshimiwa tuambie unachojua kuhusu utekaji huu.Maana wewe pekee ndo umeongea na mtekaji.”aliuliza kiongozi wa ulinzi.

“Siwezi kusema lolote lakini maelezo yote nitatoa mwenyewe.Yoyote anayechezea familia yangu anajua anachokifanya ni kama ameniweka kiganjani.Siamini yeyote.Jana tu ananitajia hadi majina ya watu niliokaa nao mkutanoni!Hadi nguo nilizovaa!”Kilua ni kama alitaka kulia lakini akajikaza tu!Walinzi wakagundua mwanamke huyu anapitia kipindi kigumu sana.Umepewa nchi ghafla unakutana na hali ngumu bado familia yako imetekwa.Hakika ilihitaji ujasiri wa hali ya juu.

“Mheshimiwa tutampata huyu asidi.Wameigusa familia ya kwanza.”walijaribu kumhakikishia uimara wao katika kushughulika na hali kama zile.

“No.Msifanye chochote familia yangu ipo hatarini hata siamini kama ikulu ni sehemu salama kwa upande wangu.”

Walinzi walibaki kimya.Lilikuwa tukio la kufedhehesha na lazima hatua zichukuliwe haraka iwezekanavyo.

“Narudia tena nawapa amri hakuna wakujua habari hii zaid yenu.Nahitaji kujua adui aliyepo ikulu ni nani?”Kilua alisema akijikaza kulia.Ina maana nyendo zake zilikuwa zinakaguliwa kw asana.Walinzi walimwelewa.

“Nahitaji mpelelezi makini aweze kujua ni nani aliyefanikisha mume wangu na mtoto wa tekwe.”alisema Kilua akiwa anamaanisha kwa umakini.Walinzi walisikitika kila mmoja akipandisha hasira nakuapa wakimkamata huyo aliyeiteka familia ya rais basi hatakuwa na msalia mtume nikumfutilia mbali.Lazima baadae watajadiliana maana wao ndo watakaoulizwa kuhusu tukio ilo la kutekwa kwa familia ya rais.

“Mheshimiwa tumepokea agizo lake tutalifanyia kazi tutakagua kila eneo hadi tujue.Lakini kama huamini vikosi vya taifa basi tutaomba sisi wenyewe tufuatilie jambo hili tutawatuma watu wafanye ukaguzi na kweli tutampata mumeo.We are the best on this issue.”alisema chifu Ditu kiongozi wa ulinzi wa rais.
“Naomba usiri katika hili.”
“Hapana mheshimiwa hutakiwi kutuomba umeshatoa oda na sisi tunafuata oda tu.”Ditu alisisitiza.Kabla hajatoka akasema.

“Kuna file nalitaka.”

“Kama ni mambo ya siri kuna mtu wa kushughulika nalo.”alisema Dittu.

“Nani?”

“Katibu mkuu.”
“Namtaka ofisini kwangu haraka iwezekanavyo.”

“Alikufa kwenye tukio la jana.”sekretari alisema.Kilua akasugua kichwa.Palepale akamgeukia sekretari.Uzuri Serambovu hakuwepo hapo alikuwa ametangulia chumba cha mkutano.

“Nani anaweza kunipa hilo file?”

“Mimi nina uwezo huo.”alisema sekretari Sada.

Kilua aliwapa ishara walinzi wake wampishe.Walitii nakutoka nje,Kilua akabaki na Sada mule ndani,”Nataka file namba 13:14”

Sada alishtuka sana!Alibadilika ndani yamuda mfupi nakuonesha hofu ambayo hata Kilua aliweza kuiona,”Kuna nini Sada?”

Sada alizunguka pale ofisini huku akiwa kwenye mawazo mazito sana.Kitu hicho hakutaka aulizwe kabisa au kiangukie kwenye uamuzi wake kwamba kipo wapi.Alitamani katibu mkuu angekuwepo pale ajibu hayo mambo lakini sio yeye.

“Sada kuna kitu gani ambacho unaogopa kunitajia hilo file nimeomba nipewe kwani kuna ugumu gani?”

“Mheshimiwa naomba niache kazi tafadhali sana.”alisema Sada akiwa na wasiwasi sana.

Kilua akazidi kupatwa na hofu,”Uache kazi wakati nafikiria kukuteua kuwa katibu mkuu?”

“Hapana hilo file limeteketeza watu.Kila aliyetaka kuingilia amekuwa akiishia pabaya.Makatibu takribani watatu walipoteza nafasi zao kisa hilo file!”

“Hebu niambie vizuri?”habari ilimteka Kilua kusikia kwamba file nambari 13:14 lina kiza kinene.
“Ilianza awamu zilizopita kila aliyetaka kugusa hilo file alidhibitiwa sana.Hata rais Kisusi jambo hilo lilimpa wakati mgumu sana.Wakati alipotaka kuingilia ndo ikaja taarifa kauawa kwenye maonesho ya uhuru.”

Kilua akawa anameza yale maelezo,”Kwani hilo file lina nini hadi rais asiweze kuliingilia?”aliuliza Kilua.Huku akijaribu kukumbuka vitisho vya Yule bwana aliyemwambia anajua hadi watu aliokaa nao mezani.

“Hilo file sijabahatika kuliona.Kulipata linahitaji password ya katibu mkuu au sekretari halafu ifuate ya rais.Lakini Theory inayolizunguka siielewi yasemekana uongozi uliopita ndo wenye hiyo password na mpaka uombe hiyo password ndo uweze kulifungua.Theory pekee ninayoiamini ni ya kwamba viongozi wa awamu Fulani ndo walianzisha hilo file na ajenda halisi ya file hilo tatizo ni kwamba wao wenyewe hakutaka kabisa file hilo liguswe na uongozi ujao.Hivyo likawekewa password na jina pekee linalotambulika kuhusu file hilo ni hiyo namba 13:14.”aliendelea kuchuja nakupembua mwana Sada.

“Linaweza kuwa nini?”
“Ni kama mkataba wa kitu Fulani cha siri sana.Mara kadhaa nilimsikia rais Kisusi akizungumza hilo jambo.Lilimsumbua sana na kila alipotaka kutupia jicho alipata vizuizi vingi!”

“Mhh.”aliguna Kilua tafakari ikiwa ngumu kuelewa.

“Kwani mheshimiwa imekuwaje?Nilifarijika sana nilipojua unachukua madaraka nikajua hakuna atakayekuja na ajenda ya hili file na mambo yataenda kawaida.Lakini siku ya kwanza tu ofisini umeanza kuulizia hili file.Au ndo maana familia yako imetekwa?”aliuliza Mwana Sada.Kilua alitikisa kichwa haikujulikana kama alisema ndio au hapana.Lakini tayari kapokea maelezo mazito kuhusu file nambari 13:14.Sasa ameanza kuunganisha doti zote hadi ajue hilo file lina umuhimu gani kiasi cha kusababisha familia yake iingie kwenye majaribu makubwa sana.Wakati anawaza hilo simu tena ya ofisini kwake.Akaipokea.

“Ni rais wa Savanna Lands natumai una majibu ya wapi balozi wangu yupo?”

“Mheshimiwa sina jibu la kuridhisha kuhusu balozi wako.Kupotea kwake sijui kitu chochote kile.Wewe ndo mwenye majibu sahihi.”Kilua alizungumza kwa ukali kidogo.Habari ya file lile ilimnyima hadi amani yake akiwaza mwanae na mumewe na tayari kuna tishio kubwa la ndani.

“Mheshimiwa kwa heshma zote nataka balozi apatikane la sivyo nitachukua hatua ikiwezekana majeshi yangu yaje kwako yamtafute balozi wangu!”alisema kwa ukali rais wa Savanna Lands.Kilua alikosa jibu ilibidi akate simu palepale!

Kabla hajafikiria simu yake ya mkononi ikaita tena bila kujishauri sana akaipokea,”Halo?”
“Tuma majeshi yako katika jimbo la Kibatari.Halafu ambia kikosi cha anga kuna ndege ya jeshi la Savanna LANDS imeruka hadi kwenye anga letu hiyo ndege itungue sasa hivi!”ilikuwa sauti ile ya mtu asiyemjua.Ina maana huyu mtu anaintelijensia gani kujua haya mambo?Alijua anaongea na rais wa Savanna Lands.

“Kwanini nifanye hivyo?”

“Wewe ni rahisi na sasa hivi huna mkuu wa majeshi wewe ndo amiri unauwezo wa kuongozi amri hiyo.”
Kilua akavuta pumzi ndefu nakuzishusha,”Lakini nina uhakika gani?”
“Unataka mumeo na mwanao wapate mlo wa leo?”sauti ikauliza.

Ina maana familia yake inanyimwa hata chakula?Roho ikamuuma sana!Bila hata kuwaza.Akamgeukia sekretari,”Nataka simu ya kambi ya jeshi ya Kibatari?”bila hata kujishauri kwa mara nyingine akajikuta akicheza ngoma hiyo.
“Kuna simu maalum inayotumiwa na amiri jeshi pekee.Ngoja nikuunganishe.”alisema Sada akasogea kwenye meza a rais akaingia kwenye droo kuna simu flani hivi kubwa akaitoa halafu akampa na Kilua.
 

Attachments

  • kombora kiotani cover page.jpg
    kombora kiotani cover page.jpg
    37.7 KB · Views: 82
KOMBORA KIOTANI-17

BONIFACE BIRAGE

Aliinua mkono uliokuwa umefunikwa na blanketi lenye uzito.Aliupeleka hadi kwenye meza ilikuwa pembeni kisha akaichukua simu iliyokuwa na mtetemesho wenye kuashiria kwamba ilikuwa inaita.Aliipokea nakusikia sauti ya upande wa pili kulikuwa na maelekezo Fulani ambayo yalimzindua fahamu za mwili zilizokuwa bado na wingu la usingizi nay eye kuamka kabisa.Sasa alihisi mwili wa mwanamke aliyekuwa pembeni yake huku joto la mwili wake ukimfariji.Harufu ya mwili wa mwanamke huyu aliyejikwatua kwa tarabizuna ilisababisha utuli wenye kufariji!Hata habari aliyopokea ilizidi kumtatiza sana!

“No hakuna yeyote zaidi ya mduara wetu…Impossible kuwe na inspection…No!Listen Mr Zungu nakuhakikishia hakuna yeyote…just finish her…”alitoa maelezo bwana huyu kisha simu akaikata bila shaka aliyekuwa anaongea naye hakumpa nafasi yay eye kutamka chochote alimdhibiti kimaelezo!

Alirudia kuvuta harufu ya mwanamke aliyepembeni yake nakuupapasa mgongo wake ulikuwa wazi kiasi cha kutuma msisimko kwa mwanamke huyo unaoshtua!Yule mwanamke alizinduka kutoka usingizini nakujikuta akitamka neno,”Oh Dedani?”

“Shss!Ni Serambovu siyo Dedani.”alijitambulisha mwanaume Yule.Kilua alimkumbatia kwa nguvu mwanaume Yule nakujilaza kifuani mwake huku akivuta hisia kwa nguvu lakini ombwe kubwa liliukumba moyo wake akahisi kama anasaliti kitu katika maisha yake alijikuta akimuachia mwanaume Yule kwa haraka.

“Bado unaweweseka na njozi za familia yako?”

“Ndiyo naziona sura zao kila nikifumba macho nahisi wananitazama nakunililia moyoni mwao.”
“Kwani imekuwaje?”

“Tangu atufumanie sijamtia machoni!”

Serambovu alihisi moyo ukienda mbio kwa muda kidogo lakini akakosa jibu.

“Najua wametekwa.”

“What?”Kilua akashtuka.

“Ndiyo najua ametekwa.”

“How did you know that?”

“Najua tu!”

Kilua alihisi kitu iweje Serambovu ajue ishu ya familia yake kutekwa wakati muda huo wote ni yeye na walinzi wake na sio rahisi siri ile ivuje hata kwa dawa!Hapana kuna kitu kizito nyuma ya pazia!Hili jambo kalijuaje?Wakati akiwaza hayo aliamka muda ule ilikuwa saa tisa usiku.Alienda moja kwa moja hadi bafuni akafungulia maji nakuanza kuoga.Alijiandaa kwa muda wa dakika 30 za uhakika kisha alivaa.Alitoka nje ya chumba bila kumsemesha Serambovu kitu chochote kile.Alikutana na walinzi wake wenye zamu ya usiku.Aliongozana nao hadi ofisini kwake.Walinzi walianza kugutusha watendaji wengine wa mkuu wajue yupo macho.Aliingia ofisini akachukua mafaili kadhaa.Leo kazi ilikuwa ngumu kweli kujua atakabiliana vipi na tishio la kuingia vita na Savanna Lands hapohapo anatakiwa kuhakikisha usalama unapatikana.Bila shaka amejua mpaka sasa kwamba serikali ya Kisusi iliondolewa kwa mauaji ya nguvu na bila shaka kuna mikono ya watu.Idara zote zimekuwa katika kizungumkuti kikubwa sana!

Alimfikiria sana mkuu wa idara ya usalama wa taifa.Alifikiria pia hatua za kuchukua kama rais.Hakupendelea kuanza kukamata watu nakuwasweka ndani hasa katikam kipindi kile japo wengi walihitaji majibu ya haraka kuona kama kuna mkono wa mtu basi waadhibiwe.Alihitaji kukamilisha msiba mkubwa wa taif kwa kuwapumzisha marehemu wote.

Akiwa pale alisikia mlango wake ukigongwa kisha mgongaji akaona bora afungue tu.Akaingia ndani nakumkuta Bi Kilua amejaa tele ka pishi la mchele kwenye shughuli.

Alikuwa ni Director Masha,”Habari Mheshimiwa.”

“Salama.”

“Nimekuja nataka msaada wako.”
“Upi tena.”
“Nataka tumuingize mkuu wa idara ya usalama katika uchunguzi huu.”alisema bwana Masha.

“Kuna nini?”
“Kuna majibu atatupa.”

“Ni sawa ila kuna jambo nahitaji msaada wako.Hadi tunavyoongea sijui hatma ya familia yangu.”alisema Kilua akiwa na masikitiko makubwa.

“Ni vipi kwani?”
Kilua alifikiri kidogo kabla hajajibu mlango ulifunguliwa akaingia mjakazi wa ikulu akaingia nakuleta kahawa akawapa wote wawili.Alipomaliza kuwatengea aliwakaribisha kisha akaondoka.Kilua alimwangalia director Masha kisha akasema,”Some people think I am weak.”

“Hapana mheshimiwa wewe sio dhaifu tena nimegundua hakuna rais jasiri kama wewe.Kuchukua nchi katika hali kama hii sio kitu rahisi.Wakati mwingine hali ndizo zinazoamua maamuzi yetu.Ninaamini unaweza prove them wrong and lead the country madam President.”

“Hiki kiti kimekuwa mzigo kwangu wengine wanaona nimepata bahati lakini imekuwa kama mkosi but I will play their game!Nitawafuata kulekule wanapotaka twende.”

Kilua alikunywa kahawa iliyopenyeza joto kwenye mwili wake kisha akaendelea,”Wameiteka familia yangu na wanataka kitu ambacho siwezi kupata.”

“What?”

“Nahitaji usiri wako chunguza jambo hili nataka usalama wa familia yangu simuamini mtu yeyote katika hili.Naomba usiri wako.”

“Ilitokeaje?”

“Siku ileile niliyoapishwa ndo familia yangu ilitekwa.”
“Wanataka nini?”
“Nitakwambia muda ukifika but first nahitaji usiri.Hawa watu wanajua kila ninachofanya hata ikulu.Siajabu hata ninavyokushirikisha itakuwa wanajua hili jambo.”

“Niamini mheshimiwa siwezi kukuangusha.”

“Hatua ya kwanza nataka mumfanyie Serambovu upelelezi wa siri.Dukua mawasiliano yake na kila baada ya muda nahitaji taarifa ujue anaongea na nani na kipi wanachoongea.”alitamka Kilua akiwa anajiamini.Masha alikuwa makini kuhusu maagizo haya.

“Unadhani adui atakuwa humu ikulu?”

“Ndiyo adui yangu anaweza kuwa anatumia watu.”

“Pili nataka upeleleze kuhusu file namba 13:14.”

Masha akashtuka sana kusikia faili hilo.Mshtuko wake ukamgusa bi Kilua,”Mbona umeshtuka.”

“Hilo faili liliwapa idara ya usalama taabu sana.Kuna viongozi walitimuliwa kazi kisa hili file.”

Kilua alitikisa kichwa kumuelewa nakuona anatakiwa alivalie njunga swala lile.Bila kuenda na umakini wakiakili inawezekana akapoteza vita ile.Kwa sasa alitakiwa kuwa kama rais wan chi na si ule udhaifu wa kuonesha alipewa madaraka ghafla bin vuu bila kujiandaa kwa lolote.Alitakiwa awe makini sana bila kupepesa huku wala kule.Tayari kesha mwambia director Masha kwamba familia yake imetekwa.

“Ni file lenye mambo mazito sana na hadi kujua hili jambo inahitajika nguvu ya ziada.Wanahusika na jambo hili wapo ndani ya serikali kila sekta ni rahisi kujua yeyote anayetaka kutafuta nyaraka hizo.”

Kilua alikunywa kahawa yake tena.

“Kwa majibu machache nimeskia hizo nyaraka ni kuhusu mkataba Fulani wa kitu ambaol ulipita serikali zilizopita na haupaswi kuingiliwa na yeyote.Lakini sasa nalazimishwa kufanya upekuzi maana…”alikwama kidogo.

“Wataidhuru familia yako kama hutawapa nyaraka hizo ambazo hata wewe hauna!”alijibu director Masha akiwa na umakini wa hali ya juu.Hatua hiyo ikatihibitisha kile ambacho Kilua hakuwa tayari kukisema kwa wakati huo.Familia yake imetekwa.Kisha anatakiwa kuwasilisha nyaraka za faili namba 13:14 au familia yake idhuriwe.Ilibidi aeleze kila kitu kilivyo tangu alipoingia madarakani ni vitisho alivyopokea kwa director Masha ambaye alipandwa na hasira kuona rais wake anatishiwa aliapa kutumia ujuzi wake wote kudhibiti kila kitu hadi atakapo dhibiti jambo hilo.

“Ndiyo hivyo ilivyotokea.”
“Usijali nitahakikisha tunadhibiti uzandiki huu nakuufutilia mbali.Ila najua tutapitia vikwazo lakini nakuahidi nitadhibiti hili swala.”alisema director Masha.Makubaliano ilikuwa kuanza kupeleleza dhidi ya faili namba 13:14 pamoja na familia ya rais.

“Pia nataka kufanyike upembuzi wa mikataba yote iliyoingiwa awamu zilizopita nakuwe na vigezo ilikujua ni mkataba gani huo uliopo kwenye hizo nyaraka.”alishauri rais Kilua akimalizia kikombe cha kahawa.

“Tupo pamoja.”
Masha aliondoka kutoka kwa rais.Sasa alijua fika kupata wepesi wakupitia mikataba hiyo ni lazima aende kwa mkuu wa idara ya usalama wa taifa huyo anaweza akajua ni mikataba ipi itakayozua utata hadi aweze kuoanisha nyaraka zile muhimu zinazomnyima usingizi rais Kilua.Akiwa anatoka ikulu kuna ujumbe uliingia kwenye simu yake alipotizama alikuta ni kutoka kwa mhariri ambaye ni mchapaji wa gazeti la Alfajiri.Gazeti pendwa kwa habari nyeti tena nzito na zile zenye udaku ndani yake unaokaribiana na ukweli.Mida ilikuwa saa kumi na moja alfajiri.Aliamua kuelekea moja kwa moja hadi ofisi za gazeti hilo maana ujumbe ulimtaka aweze kufika kwa siku ile.Mwendo ulikuwa wa dakika kama 40.Hadi inafika saa kumi na moja asubuhi tayari alikuwa alikuwa viunga vya mjini akiifuata ofisi ya gazeti la Alfajiri.Aliingia hadi ofisini kwa mhariri nakukutana nakala moja iliyochapishwa ikiwa na kichwa cha habari kizito chenye kumtisha hata mwendawazimu.RAIS KILUA NA MCHEPUKO WAKE!Hilo lilitosha kabisa kuona hizi si habari njema kwa rais Kilua nizakumpaka doa!
 

Attachments

  • kombora kiotani cover page.jpg
    kombora kiotani cover page.jpg
    37.7 KB · Views: 92
KOMBORA KIOTANI-38

BONIFACE BIRAGE

TULIISHIA RAIS KILUA KESHA PATA USHAURI WAKUUNDA BARAZA LAKE LA MAWAZIRI PAMOJA NAKUMTEUA MAKAMU WA RAIS NA WAZIRI MKUU.VILEVILE RAIS KILUA ANAHITAJIKA KUTEUA TEUZI MPYA ILIKUUSIMIKA UTAWALA HASA AKIJUA ANAKIBARUA KIKUBWA CHA KUIRUDISHA TAIFA LA KIOTA KATIKA RAMANI YA KIUUTAWALA BAADA YA KUUAWAWA KWA RAIS KISUSI.KILUA ANAPATA MSAADA MKUBWA MUME WAKE KATIKA HATUA MPYA YA KUUWEEKEA MIZIZI UTAWALA WAKE.LAKINI ANAPOKEA VITISHO VYA KUTAKIWA KUMRUDISHA MUMEWE KWAWATEKAJI ILIKUMNUSURU MWANAE AMBAYE BADO YUPO MATEKANI.VILEVILE DEDANI ANAAMRIWA KUMSHAWISHI RAIS KILUA AMTEUE MTU ANAITWA TWALIPO KUWA MAKAMU WA RAIS DEDANI ANAHISI KUNDI LA THE BIG BOYS WANATAKA KUPACHIKA MTU WAO SERIKALINI.JE,TWALIPO NI NANI?UPPANDE WA PILI MWANAUSALAMA SHUNIE ALIYEMKOMBOA MUME WA RAIS KILUA MATEKANI ANAAMUA KUSITISHA HARUSI YAKE NA PABLO AKIAMINI HAMPENDI NA ANATAKA KUWA NA MAHUSIANO NA DEDANI.RAIS KILUA ANA UJAUZITO WA CHIFU WAKE WA STAFU JE,ATAMWELEZA MUMEWE?TUWE SOTE PAMOJA.

Alipiga hatua kutoka pale katika uwepo wa Pablo.Nyuma alihisi kutizamwa kwa macho makali na wake zake.Shunie alijua ametengeneza vita kubwa sana kati yake na Pablo na kama ikija kugundulika bila sababu za yeye za yeye kukwepa harusi hata kuwa na msalia mtume.Hata anaweza akaleta mengine magumu yatakayozidi kumdhibiti kw asana.Shunie alikubali jambo moja moyoni mwake kwamba ni kweli amejikuta akimpenda mume wa rais Kilua bwana Dedani.Amempenda sana kiasi cha kushindwa kujidhibiti na hata akahisi kama kweli akiolewa na Pablo ni kuisaliti nafsi yake hasa kwa kipindi hiki upendo wake kwa Dedani ukiwa bado mchanga wenye joto na nguvu za kutaka kuthibitisha kwamba ni kweli anampenda Dedani kiukweli na kuwa na mtu mwingine kujilisha upepo.Penzi hilo ni batili.Alimpenda kwa penzi lililo jenga ukuta wa kuamini kwamba moyo wake una milikiwa na Dedani nasio mtu mwingine hata kufikia hatua ya kusitisha harusi yake kwa kisingizio cha kazi.

“Shunie mpenzi wangu unaniambiaje?”aliuliza Pablo kwa sauti iliyo na mawimbi ya kekefu za kilio.

“Sihitaji ndoa kwa sasa.”alijikaza na neno kumtoka huku akikwepesha macho kumkabili Pablo.

“Unasemaje?”aliuliza Pablo kwa mshangao!

“Samahani sana najua nitakuwa nimewakera sana.Baba mkwe pamoja na ndugu wote mlio hapa.Kweli nilipenda kuwa sehemu ya famiilia kwa njia ya ndoa.Nilitamani sana kuwa mke wa Pablo nakukubaliana na ahadi hiyo lakini mambo yamebadilika na kwa jinsi hali ilivyo sioni kama nitaweza kutimiza ndoto hii.Kwasasa mimi sio mke wa kumfaa Pablo.Sioni maisha yangu yakiwa na Pablo.Naomba mnisamehe kwa kuwakwaza.Najua uamuzi wangu utawadhoofisha wengi sana lakini ndo hivyo naomba mniwie radhi kwa hatua hii.”Shunie alisema maneno hayo akitizama chini.Alimsogelea Pablo nakupiga magoti mbele zake.Alimtizama usoni akijitahidi kuwa na ujasiri.

“Pablo nakuomba…ndani ya uvungu wa moyo wako unielewe kwamba Shunie kwa sasa hawezi kuwa mkeo.Tafadhali kwa heshma uliyonipa naomba kwa heshma hiyohiyo unipe nafasi hii ya mimi kujitenga na taratibu za ndoa.Sipo tayari kuolewa na wewe.”ulikuwa ujumbe mzito sana kwa Pablo kuusikia hata akaanza kuhisi maumivu tena ya risasi kwenye mwili wake na sasa alihisi ni kama risasi zilipigwa kwenye moyo wake.Alihisi maumivu ya kisaikolojia tena makali sana katika kusitishwa nafasi ya kumpata Shunie kama mkewe.Alimwangalia usoni na uzuri wake na macho mazuri lakini sasa yametiwa huzuni.Pabli hakuwa na mpango wa kumpoteza Shunie hata iweje.Alikumbuka penzi lake lilivyo tamu na joto la mwili wake picha zote zilipita kichwani mwake kama mkanda nakujua kweli alimpenda sana mchumba wake.Kitu kilimwambia kichwani kwamba mwanamke huyu kapata mtu mwingine.Au kutakuwa na operesheni zao lakini hiyo siyo suluhu.Makubaliano yao hayakuwathiriwa na kazi zao.

“Shunie usiseme hivyo.Unauchoma moyo wangu.Tafadhali sana naomba nafasi tutarekebisha kama kuna tatizo.Pamoja tutapata suluhu ya jaambo hili.”Pabli alijikuta akiropoka bila kujua hasa anategemea kueleweka au la!Jazba ilimpanda na alikuwa tayari kusema na kufanya lolote ili mwanamke huyu amuelewe.

“Pablo Pablito please naomba usiufanye uamuzi wangu kuwa mgumu zaidi.Naomba uelewe.You are strong.Agent please understand what I need.”alisema Shunie akimhimiza kwa kumhini Pablo.

“Shunie haiwezekani.Nina malengo na wewe.”alisisitiza bwana Pablo.

“Asante kwa wema wako lakini siwezi.Kufanya hvi ni kuisaliti nafsi yangu.Naomba tuachane na utaratibu wa ndoa.Pia nasitisha uchumba kati yangu na wewe kwa sasa.We need some space a lot of things took place we need time to think.”ulikuwa ujumbe mzito sana.

“Hivi Shunie una moyo kweli?”

“Ninao lakini haiwezekani kabisa kwa sasa mimi na wewe kuwa mke na mume.”

Shunie alihuzunika lilikuwa jambo gumu sana kwa yeye kulifanya.Alimuona Pablo akiwa ameumia sana.

Shunie aliinuka nakuanza kusimama.Alipeleka mkono nakuvua Pete ya uchumba kati yake na Pablo akampa.Ndugu za kina Pablo walishindwa kuvumilia,dada wa Pablo alikuja kwa haraka akamshika Shunie nakumvuta akimtoa,”Ondoka hapa hatukutaki!Toka!”

Shunie alijua kimenuka akaanza kujitoa kwenye fujo zile akitaka kukimbia aondoke.Alitamani ardhi ipasuke atumbukie nakufukiwa kabisa.

“Dada Manka tulia acha hasira.”aliomba Pablo.

“Huyu mbwa ana nini hadi anitesee mdogo wangu kwani yeye ni nani?Aondoke Malaya mkubwaa!Na wewe Pablo achana na huyu kahaba asiye na shukrani!Mtu imebaki mwezi harusi ifungwe yeye anatuletea season zake za kifilipino eti nyoko siwezi kuolewa I need some space!Atoe pumba zake hapa.Shunie potea kabisa sitaki kukuona tena karibu na mdogo wangu.Shenzi kabisa!”dada Manka alikuwa amekasirika sana.Ilibidi wazee waingilie kati kutuliza ghasia.

“Mdogo wangu usijali wanawake wapo wengi achana na huyu kahaba!Watu tunaangaika kuandaa shughuli tunatumia gharama na heshma zetu halafu pumbavu nyingine inakuja hapa kutuletea isidingo.Aondoke hapa!”Dada wa Pablo alizidi kukaripia nakutukana hadi matusi ya nguoni.Shunie aliumia zaidi moyoni mwake.Aliona hapa ataumbuka.Alitumia utaalamu wake wa kijasusi nakupotea eneo lile.

***

Dedani alimtizama mkewe kwa makini sana.Hakutaka kumwambia hofu yake ni nini?Aliona atamzidishia hofu zaidi.

Kilua naye hakutaka kabisa kuonesha ni kitu gani amepokea.Anatakiwa amtoe mumewe sadaka ilikumnusuru mwanae.Alifikiria sana.

“Kwani mke wangu imekuwaje?”
“Hapana nimepokea ujumbe ni kuhusu mtumishi Fulani wa serikali yangu amepatwa na tatizo.”alisema Kilua.Alijaribu kupotezea na kweli Dedani alinunua uongo huo nakuamini.Wasichokijua wote walipokea vitisho.Dedani alipokea kitisho cha kushawishi bwana Twalipo ateuliwe kuwa makamu wa rais.

“Usijali mke wangu uwe imara.”alishauri Dedani huku akiwa na kibarua kigumu.Walielekea ofisini kwa rais Kilua alikuwa na mkutano na balozi wa China aliyekuja kumtembelea.Dedani aliitwa ofisini kwa Serambovu.Hakupenda lakini alienda kuonana na bwana huyo.Japo hakumpenda ilibidi aende maana kwa sasa imeshaonekana Dedani kuwa karibu sana na mkewe kiasi kila mtu anahitaji kuonana naye kiushauri.

Aliachana na mkewe yeye alikatiza korido za ikulu hadi kumfikia bwana Serambovu.

Walitizamana kwa hasira sana,”Unasemaje?”

“Naona umekuwa na sauti sana katika kuunda serikali ya rais Kilua.Kila mtu anamtaja Dedani.”alizungumza bwana Serambovu kwa kejeli akimpa sifa hewa mtu huyu.

“Kwa hiyo unasemaje.”

“Hapana sina maana mbaya ila kama chifu wa staffu wa ikulu lazima niwe nawasiliana na wewe hasa nipatapo jambo lolote.Kwa sasa tupo kwenye mchakato wa kuunda serikali hivyo kila mtu anatakiwa kuriopoti kwako.”

“So what?”

“Kuna ujumbe nimepokea kuna mtu anahitaji muonane kujadili kuhusu mchakato huu.Hakunipa maelezo sana ingawa natamani kujua kuna jambo gani.Ni vile Serambovu hapendi kuingilia vya watu.”

Dedani kidogo amrukie lakini akajidhibiti,”Kuwa makini na kauli zako.”

“Kwa vyote umesikia hii ya kuwa siingilii vya watu?Mtu wa aajabu.Kwa taarifa tu mkeo namjua kiundani.Nilikuwa wa kwanza kwake na hata ufanyeje bado nitakuwa mwanaume wa kwanza maishani mwake.Mimi ndiye niliyeondoa usichana wake.Put this in your thick head I was the first na daima utakula makombo!”yalikuwa maneno makali sana.Ilionekana dhahiri Serambovu hawezi kuudhibiti ulimi wake.Cha msingi ni kuendelea kukoleza chuki kwa Dedani.

“Serambovu chunga ulimi wako!”alionya Dedani.

“Hahaha!”alicheka kicheko cha dharau,kisha akaendelea,”Ohh!Dedani hujui ni kiasi gani zile nyakati aligugumia kwa Ohh!Papa Sera unanifikisha!My name she will always remember.”

Dhihaka ilivuka mipaka sasa.Dedani alikuwa amefika kikomo ila akajikaza kwa heshma ya mkewe.Alijikuta mikono ikimtetemeka nay eye kutamani kumshughulikia vizuri bwana huyu lakini alijirudi.

“Nipe ujumbe.”

“Mtu anaitwa Twalipo kaomba kuonana nawe.Mkutane Chemchem Hotel aanakusubiri fanya juhudi umfikie.”
Dedani alikuwa amekasirika sana lakini ile kkutajiwa mtu anaitwa Twalipo kulimgutusha nakumfanya asisimke mwili mzima kwamba mtu huyu ni nani?Iweje aombe nafasi yakuzungumza naye?Ana ajenda gani hadi aweze kutuma ujumbe huo wakuomba kikao kupitia Serambovu?Huu ulikuwa mzizi mwingine wenye kichefuchefu!

Dedani alijikuta akiduwaa!

***

Kilua baada ya mkutano na balozi wa uchina alitoka nakuelekea sehemu nyingine ya ikulu.Akiwa katika bustani za ikulu alipokea tena ujumbe.

“TUNAMTAKA DEDANI NDIPO TUMUACHIE MWANAO.HATUTAKI AHUSIKE NA MCHAKATO WA KUUNDA SERIKALI YAKO.”

Kilua alishtuka sana!Ina maana tayari wameshajua uwepo wa Dedani katika uundaji wa serikali?Moyo ulipiga paa!Aligutuka kutoka alipokuwa nakupiga simu kwa mumewe?

“Uko wapi?”aliuliza Kilua baada ya mumewe kupokea simu ile.

“Naelekea Chemchem Hotel.”

“Unaenda na nani?”

“Nitakuwa mwenyewe.”

“Ok chukua gari lenye namba za ikulu.Na waambie wakupe level F bodyguard mmoja.”alisema Kilua akijua fika anamuandaa mumewe kwa jambo bay asana.Alikata simu kisha Kilua alituma ujumbe kuijibu ile namba iiliyompigia awali.

***

Zee Kavu aliitengeneza tai yake vizuri baada ya kusoma ujumbe ulioingia kwenye simu yake.

“Kasemaje?”

“Kasema mumewe yupo Chemchem Hotel.Tutume vijana wetu.”

“Siatakuwa na ulinzi mkali sana.”

“Hapana alipunguza kiwango cha ulinzi kampa mlinzi level F tena mmoja.Huyu tutaweza kumdhibiti..”alisema Kavu sasa alinyoosha mikono ya koti lake huku uso wenye ukavu ukiachia kwa tabasamu la ushindi.

“Timu ipo tayari?”

“Yes.The president has just offered her husband tumbadilishe kwa binti yake.”alisema Zee Kavu.Aligeuka na kumwangalia Bwana Tufe wote walitabasamu vizuri.

“Dedani ni problem hatuna imani kama ataweza kumuingiza bwana Twalipo.Watu kama Dedani ni wajanja sana anaweza hata kumuua Twalipo akiwa tayari ni makamu wa rais.”

“Hivyo tumfanyeje?”

“Ni simple tu Dedani afutiliwe mbali.Yeye atakuwa mfano kwamba Kilua hana ubavu kwetu sisi.”

TUKUTANE TOLEO LIJALO.
 

Attachments

  • kombora kiotani cover page - copy.jpg
    kombora kiotani cover page - copy.jpg
    18.2 KB · Views: 56
Kombora kiotani-39


Boniface birage


Tulipoishia baada ya shunie kupinga ndoa yake na pablo ugomvi mzito umezuka na shunie kutimuliwa ukweni.upande wa pili dedani anapewa taarifa za kukutana na mtu anayeitwa twalipo kwa lengo la kupiga ushawishi bwana huyu ateuliwe kuwa makamu wa rais.dedani amekuwa na hisia za mbaya dhidi ya mkutano huu na tayari hofu ikiwa kujipenyeza kwa kundi baya la the big boys katika serikali ya mkewe.dedani kapokea vitisho na sasa mkewe kapokea kitisho akamilishe njama za kumfanya dedan akamatwe na kundi la mzee kavu anayesadikiwa kuwa kibaraka wa the big boys.rais kilua anashiriki kwa kupunguza ulinzi wa mumewe akijua yupo katika hatari.je,dedani atakamatwa?

“ni simple tu dedani afutiliwe mbali.yeye atakuwa mfano kwamba kilua hana ubavu kwetu sisi.”





“Dedani ni tatizo sana kwa upande wetu.”
“Tudhibiti hili jambo just make sure tuna best team ndo itamshughulikia.”

Makubaliano yalikuwa yamefikiwa na sasa ilikuwa ni hatari kubwa sana.Walionekana vijana wa kazi wakiondoka kuelekea Chemchem hotel kumshughulikia Dedan katika mkutano wake.Lakini kulikuwa na maswali kama Dedani anaenda kutekwa kwanini wampe mkutano na Twalipo?Ikiwa Dedani ni mshauri mkuu wa Kilua ambaye anategemewa kuonekana kama na sauti kwanini wamteke?Ushauri wake utakuwa na maana gani kama akiwa mikononi mwao kuliko akiwa kwa Kilua?

Jua lilikuwa utosini.Mji ukiwa na pilikapilika na tayari kamata kamata ilianza kwa wale walioshukiwa kwa namna moja au nyingine kushiriki kummaliza rais Kisusi na serikali yake.Hii kamata kamata ilienda kimya kimya huku watu wakijishtukia wakipotea bila kuwa na maelezo wala nyayo za kufuata.Taharuki ilikwisha pita kila pembe na kila mwenye ndugu aliyepotezwa alikuwa na mkururo wa maswali ya sintofahamu kuhusu mwenzake aliyepotea.

Japo serikali ya Kilua ilijua vyema jambo hili litaleta mushkeli na umma ungetegemea majibu ya kuridhisha.Lakini aliona vyema yeye binafsi kukamata mnyororo wa hawa wahusika wa chini ilikuondoa uozo huo kotekote.Japo alijua kwa njia hii wakubwa wa ule mtandao watajitahidi kubadili mbinu na njia ilikudhorotesha hatua zake.Ila alijipa moyo kwa njia ile angefanikiwa tu japo kwa mbine na hata kama asingefika anapotaka lakini atakuwa amefanikiwa kutikisa nyavu zilizoonekana ni chuma!

Katika hotel ya Chem chem lilikuja gari lenye namba za ikulu nakusimama mbele ya hoteli hiyo kisha alishuka bwana Dedani.Kwa kuwa alijua umuhimu wa mkutano huo aliona ni vyema angeenda peke yake kukutana na Bwana Twalipo ili kuwe na uhuru wa kutosha wakumfanya yeye binafsi aweze kumpeleleza bwana huyu.Alihisi uwepo wa mlinzi ungemwondolea ujasiri wa yeye kuzungumza na Twalipo.Pengine mazungumzo yangebebwa na mlinzi japo walinzi hawa walikuwa wamekula viapo kutotoa siri za wanaowalinda lakini kwa jinsi alivyoona mkewe kazungukwa na wasaliti allijikuta akikosa imani na hata walinzi waliohodari kutunza siri.

Dedani alimuelekeza mlinzi kulinda gari na yeye kuingia ndani.Alielekea moja kwa moja hadi mapokezi.Alijitambulisha nakuuliza kama kuna ujumbe wowote uanohusiana na jina lake.Msichana wa mapokezi aliangalia kwenye kumbukumbu nakukuta bwana Dedani kawekwa kwenye miadi na tayari kuna meza ilishatengwa maalum na muhusika anamsubiri.Msichana wa mapokezi alimwita mhudumu wa pale hotelini kisha akamwelekeza amuoneshe bwana Dedani wapi pa kwenda.Hotel ilikuwa tulivu wakionekana watu waliostaarabika wenye ukwasi wakipata huduma katika hotel hiyo.Dedani alfikishwa kwenye meza iliyoandaliwa.Alimkuta bwana mmoja hivi ameketi.Alikuwa mtu mzima mwenye mvi za busara.Dedani alikaribishwa na mtu yule kisha yeye binafsi akaketi.

Walisalimiana kwa bashasha.Japo bashasha la Dedani lilikuwa batli.Moyoni alikereka akijua watu hawa wamekuwa mwiba kwenye familia yake na badala ya mkewe kulitumikia taifa bila wasiwasi watu hawa wamekuwa wasiwasi kwa mkeo!

“Bwana Dedani mimi ndo Mr Twalipo.”alisema Mzee huyo akionesha tabasamu lake.Kisha alitoa makadabrasha yake akaweka mezani.

“Hili ni faili langu unaweza kuliangalia kwa muda wako kupata maelezo kunihusu mimi.Rekodi yangu ni nzuri isiyo na dosari.Ni naamini nina uwezo wa kulitumikia taifa letu kama naibu rais wa taifa letu.”alisema mzee huyo kisha akampa Dedani faili lake.

Dedani alichukua mafaili ya bwana yule.

“Lakini bwana Twalipo siunajua utaratibu wa kumteua naibu rais lazima uchunguzwe na usalama wa taifa?”

Hilo kidogo lilionekana kumlemea bwana Twalipo kiasi alijikohoza kidogo kurekebisha koo lake.

“Ningependa usalama wa taifa wasifanye upelelezi kunihusu.Nina rekodi safi kitaifa na hata ndani ya chama chetu tawala wanalijua hilo.Hakuna aliyeomba hadi sasa kupewa nafasi.Najua rais ndiyo anapendekeza ni nani wa kumteua.Ila mimi nimeamua kujitokeza mwenyewe nitoe ombi langu ili jina langu lipigiwe debe kisha niteuliwe na rais kuwa makamu wake.”alishauri bwana Twalipo.

Dedani alifikiri kidogo kisha akasema,”Kuna wakati inabidi tuache utani.Hivi unanichezea ngonjera wakati unajua wewe ni kibaraka unayetaka kupandikizwa kwa serikali ya Kilua ili mje kulinda maslahi yenu?”

“Bosi lakini siumeshapewa maelezio?”
“Tuache kuigiza!”alisema Dedani kwa sauti iliyopanda kidogo.

Twalipo alinywea kiasi akitizama kwa mshangao.Ni dhahiri Uso wa Dedani ulibeba hasira ambayo haikujificha hata kidogo.

“Hatuigizi mkuu.”alijitetea bwana Twallipo.
“Huu upuuzi wa kunipa mafaili yako ni ujinga tu.Mimi ninajua kabisa kwanini hutaki kuchunguzwa.Yawezekana wewe ni msafi huna dosari ila shida moja ni kuwa wewe ni kibaraka ni hicho ndicho unachokiogopa sana.They will brand you as a traitor to the nation and people like you are to be eliminated from authority!”alitamka kwa hasira sana.

“Lakini bosi hatuna haja ya kufika huko.”
“Nisikilize kwa umakini sana wewe ni mpuuzi!Tena hufikirii.Unajua hali halisi ilivyo kwa sasa kwenye taifa hili?Makamu wa rais sio mtu wa mchezomchezo tu.Unaleta utani.Mimi siwezi kupendekeza jina lako liwepo kirahisirahisi tu.”
“Dedani inabidi ukubali.Unajua kama mkiniweka kwenye wadhfa huo na wahakikishia kabisa mtoto wenu mtampata akiwa salama.Endapo mtaenda kinyume na hilo tusije laumiana.”alisema bwana Twalipo.

“Hahaha wewe unaleta utani ndugu.”

“Hapana sitanii kwa kweli.”

“Kwanza nataka nikuhakikishie endapo mwanangu atadhurika zaidi ya vile mlivyomfanya.”alisema Dedan kwa sauti iliyobebwa na hisia,kisha akaongeza,”Nitakuua kwa mikono yangu!”

“Unanitishia?”aliuliza bwana Twalipo

“Sikutishii bali ni onyo nakupa dhidi ya hatua zako!”Dedani alishikwa na hasira.Urais wa mkewe ulikuwa kama mwiba hvi hadi sasa familia yake haieleweki.

“Kwa hiyo nataka nikwambie jina langu linatakiwa kugeuka Vice-president Twalipo!Naona hapa hatuelewani tutaelewana kibabe zaidi.”alisema bwana Twalipo.

Dedani alikereka sana na matisho hayo kiasi cha kuchefukwa kabisa na maelezo hayo.Huyu wa mtu alioneka kuwadhibiti na sasa aliona kabisa kwamba wapo kwenye kizuizi.

“Utahakikisha jina langu linapita nategemea kuapishwa ndani ya muda mfupi sana maana kuna ofisi nyingi sana zipo bure.

Dedani alivuta pumzi ndefu na kuzishusha alitamani kwenda msalani kwanza anawe uso kuondoa jinamizi lililompata.Dedani aliinuka nakuelekea moja kwa moja hadi mlani.Alinawa uso kisha akajifuta kisha alitizama kioo mbele yake akijitahidi kujidhibiti alitamani amtungue yule bwana kwa ngumi kadhaa lakini akashindwa.

Akiwa pale alishtukia mlango ukifunguliwa kisha akaingia yule bwana.Dedani aliona huu ndo mwanya wake wa kumshughulikia bwana huyu.Alichofanya nikumrukia nakuanza kumshushia kipigo.Alimkwida na kwenda kumpigiza kwenye karo la kunawia.Alimpigiza mara kadhaa kwenye paji la usoo!Kwa kila pigizo lilimfanya bwana Twalipo kuhisi kishindo kizito kikipiga na kichwa kumtikisika hadi ubongo wa ndani hali iliyofanya kuona taswira ya kuona ikififia na kupoteza kabisa ufahamu wake.Damu zilianza kutota kwenye paji la uso na tayari alikuwa amempasua sehemu kubwa.Dedani alimuachia bwana huyo.Alijua huyu mtu hata aamka.Alichofanya alinawa mikono kisha akatoka nje.Alikatiza korido kadhaa akaja kutokea ukumbi wa hoteli kwenye mgahawa kisha akanyoosha kutoka nje.Ile alikatiza hapo nakuelekea mahali gari lilipo.Wakati analiona kwa mbali alishangaa kuona kuna watu wanamfuata kwa nyuma ile kugeuka aliona mabwana wawili waliovalia suti nyeusi wakimjia.Dedani alijifanya kutowapatiliza kisha akaenda kwenye gari lake.Alipotaka kuufungua alihisi kusimamiwa na wale watu wawili.

“Samahni bwana tunaomba mazungumzo na wewe.”alisema mmoja wao.Dedani alishtuka sana na nywele kumsimama.

“Kuna nini?”

“Tunaomba usiondoke.”wa pili alijibu.

“Nina haraka na wahi kwenye shughuli zangu muhimu.”alijitetea.

“Hili lina umuhimu sana na bila shaka unapaswa kuwa mtaratibu.Tunaamini wewe ni mtu mstaarabu.”

Dedani hakuona kheri kwenye hizo kauli na kwa namna moja au nyingine machale yalimcheza na kama angebweteka basi angepoteza.Hawa wanataka nini.Lakini kuna jambo lilimshtua,alimuona mlinzi wake akiwa kwenye usukani ameketi kwa kuwa alivalia mawani meusi bila kujigusa Dedani alihisi huyu bwana atakuwa amelala.Na kama angekuwa maccho bila shaka angesaidia kukabiliana na hawa watu.

Dedani alivuta pumzi ndefu nakuzishusha.

“Ok.Natakiwa niwasubiri kwa hapa au wapi?”
“Ingekuwa vyema kama ungekuja ofisini kwetu.”

Dedani alitikisa kichwa kukubali kisha alisogea hadi kwenye gari kumtaarifu mlinzi wake.Alienda upande wa pili wa dereva.Kioo kilikuwa kimeshushwa alimgusa bega lakini mlinzi hakushtuka!Alipotizama maeneo ya tumbo aliona michirizi ya damu ambayo bado ilikuwa ikitoka tena bado mbichi kuonesha tukio hio limetokea mida hiyo!Dedani alichichimkwa!Ilibidi awageukie wale watu wawili.Hakutaka kuwaonesha kama kuna dosari kwenye gari lake.

Walianza kuelekea kurudi hotelini.

“Tukio ulilofanya chooni tumeliona lote.Tutakuweka chini ya ulinzi.Polisi wanakuja!”

Dedani alihisi nywele kumsimama!Hilo lilikuwa tatizo kubwa sana.Dedani alisita kwanza kupiga hatua alipsoikia jambo hilo.
 

Attachments

  • kombora kiotani cover page.jpg
    kombora kiotani cover page.jpg
    37.7 KB · Views: 67
KOMBORA KIOTANI-43

BONIFACE BIRAGE


“Kwanza nataka kutangaza hali ya hatari before anything.”alisema Serambovu akimtizama jenerali Lupogo aliyesimama hatua chache kutoka pale.Jenerali alimsikiliza.

“Ungetangaza kwamba umechukua nchi kisha utangaze hali ya hatari.Ni safari ngumu nap engine utegemee ugumu kutoka mataifa mengine.Kamata kituo cha taifa cha utangazaji.Majeshi yapo tayari ni wewe tu uingie kilingeni kwa amri!”

“Nafikiri tuandae matangazo ya mimi kulishika taifa.”

“Vikosi vipo tayari kwaajili yako.”
“Tuelekee huko kwa haraaka japo nilipenda kutolea maamuzi nikiwa hapa ikulu.”

“No bado una nafasi salama.”

“Jenerali?”
“Mr President?”

“Unafikiri ni hatua sahihi tunayochukua?”
“Wote tuna nafasi ya kufanya maamuzi nasio kila uamuzi utampendeza kila mtu ila mwisho wa siku inabidi tuufuate njia tuliyochagua.Kila uamuzi una matokeo na lazima tujifunze kuishi kwa matokeo yenyewe.”ulikuwa ujumbe mzito sana toka kwa jenerali Lupogo.

Serambovu alijiandaa kisaikolojia kwa upepo mpya na uzembe wowote ule ungefikia pabaya sana ikiwa hajajipanga.

“Ok Jenerali tunaanza daraja la kwanza.Ikulu ipo salama?”

“Ndiyo ipo salama ni wewe tu ila kwa muda mfupi kuna walinzi wa rais wanatakiwa kufutiliwa mbali wale waliopo kwenye chumba cha upasauaji.”alisema jenerali.

“Kikosi kazi kipo tayari kukabiliana nao?”aliuliza bwana Serambovu.

“Ndiyo.Utawadhibiti kwanza wao kisha tutaikamata handaki la silaha hadi hapo tutakuwa salama kuiteka ikulu.Vikosi kadhaa vimepewa maelezo kuwa katika hali ya hatari it will take time kabla wajue wewe ndo unaendesha nchi ila lazima tujiandae kwa lolote.”alisema Jeneral Lupogo.

“Kwanini tusimlazimishe Kilua ajiuzulu kuliko kuingia kwa rabsha namna hii?”

“Mkuu wote tuna mategemeo sio kila uamuzi nikuchukua.She won’t resign!”alihakikisha bwana jenerali.

Serambovu aivuta hisia kali akijiandaa kisaikolojia kupambana na mtiririko huo mpya.Alijiahakikishia kwa hatua anayoenda kuichukua bila shaka atakuwa na uhakika wa kum,uondoa bi Kilua madarakani kwa haraka sanaa.

“Ok.Give the order tuanze kazi!”alisema Serambovu ambapo muda uleule tu jenerali alikamata redio call yake kisha akaanza kutoa maelekezo kwa vijana wake wa kazi.Ikulu ilikuwa si salama tena kwa rais Kilua na ndani ya dakika vilionekana vikosi vilivyovalia tofauti na wanajeshi vikiingia ikulu.Walikuwa na silaha zilizo tayari kwaajili ya shughuli hiyo maalum.Walipofika ujio wao uliwafanya walinzi wa ikulu kushtuka nakuanza kujibishana nao hali iliyoleta mapigano mazito.Dakika tano mbele vikaingia vifaru viwili vya kijeshi pamoja na magari kadhaa yakiwa tayari kuendeleza mapambano.Tofauti na walinzi walivyo dhani kwani baada ya vikosi vile kuingia tu vilitulia bila kufanya lolote wakiacha wale jamaa waliovalia mavazi tofauti na sare za jeshi la Kiota.

Ilikuwa mitutu mizito sana kwa wakati ule na bila shaka hali haikuwa sawa.Wala kuridhisha.Ikulu ilingiia katika mhanga mkubwa sana.

***

Umbali Fulani kutoka ikulu mlikuwa na jengo kubwa.Katika ofisi ya juu kabisa walikuwepo vibosile kadhaa wakiangalia usawa wa ikulu kwenye vioo wadunguaji wao walikuwa na silaha zao wakilenga shabaha ikulu.

“Sniper in position?”aliuliza mzungu mmoja aliyekuwa hatua chache na pale wadunguaji walipo.

“Eye eye sir!”

“Alpha team send the drones.”alisema mzungu Yule akiwa kavalia suti nyeusi.Hiki kilikuwa kikosi cha siri mahsusi kuondoa utawala wa Kilua.Hakikumilikiwa na serikali yoyote.

“Drones in position.”
“Shoot on my command!”alisema Mzungu Yule.

Mzungu Yule alimgeukia mtu aliyekuwa pembeni na tarakilishi mpakato.Alimuangalia kwa umakini kisha akamwambia,”Ingilia mawasiliano ya vikosi vya ulinzi vya rais.”

“Eye eye sir!”alisema bwana Yule akaendelea kubofya tarakilishi yake kisha kupitia kifaa chake cha kupokea nakutuma sauti akasema,”All team in Redcode condition submit to omega king as your identity whosoever doesn’t possess the code is unworthy!”

“Umehakikisha imeenda kwa kundi tofauti?”

“Ndiyo mkuu.”

Mzungu alirudisha macho kwenye kioo.

Drone vifaa maalum vya kupaa hewani vikiwa vimebeba silaha vilikuwa hewani kuelekea ikulu tayari kwa mashambulizi ikiwa tu anayeviongoza atafanikiwa kubofya vitufe vya kulipulia.Rais Kilua alikuwa matatani na bila shaka alikuwa mbioni kufurushwa na wavamizi.

Drones kwa kuwa zilikuwa hewani ilikuwa rahisi kuona vikosi vya ulinzi vya ikulu na kwa haraka vikaanza kurusha makombora kuwalipua walinzi wa ikulu.Walinzi wengi waliuawa kwa haraka wakati mapigano yamezuka.Ilikuwa jino kwa jino!Vita kuu!Hadi hapo haikujulikana ni kiasi gani sserikali ilikuwa imesalitika.Mpango wao kumtikisa Kilua ulikuwa umewadia.Na sasa hali ilikuwa tete!

***

Zee Kavu alimtoa Shani kule alipokua kwenye chumba.Alimleta hadi nje kisha kulikuwa na kamera ambazo zilikuwa zikichukua tukio zima linavyo tokea.Zee huyu alichukua kisu nakukielekeza kwenye shingo ya mtoto.Uoga ulikuwa umemtafuna Shani kiasi cha kumnyima imani yake.Japo mzee huyu alikwisha tia najisi utu wake na kumnyima dhamana ya imani yake.Kulikuwa bado na woga kwenye mwili wake.Woga uliobebwa kwenye kingo za moyo wake.

Shani pamoja na uoga lakini hakutoa sauti!Mikono ya zee Kavu kwenye mwili wake ilitosha kumuangamiza.Picha ya zee lile kiuononi mwake ilimnyima imani ya kuishi pia.

“Shani tunaenda kuangamiza familia yako.Nilimwambia mama ako kwamba ipo siku hata iona sura yako tena nafikiri ni leo.”alisema zee lile kwa sauti yake kavu huku uso wake ukibeba mashaka ya moyo wake.

Shingo aliikamata huku Shani akikodoa macho bila kufanza lolote ulikuwa umewadia muda wake.Zee Kavu alipitisha ulimi kwenye papi za mido yake tayari kummaliza mwana wa Kilua.Alichofanya ni unyama uliopitiliza alimdunga kisu mgongoni badala ya kumchinja kama alivyodhamiria.Alikishindilia kwa umakini mkubwa kisha akakichomoa.Shani alihisi nguvu kumuishia akatua chini!Zee Kavu aligeuka na kuwapa ishara vijana wake.

Waliuchukua mwili wa Shani kisha wakauweka kwenye gunia nakuondoka nao kwenye gari.

***

“Ina maana hamsikii milio ya risasi?”aliuliza Dedani.Ofisa usalama aliyepo pembeni yake alimuangalia kwa umakini.

“Tunaisikia response team ipo kazini.”alijibu bwana Yule.Lakini wakiwa pale wakaingia wanausalama wengine wa rais.

“Identify yourself?”

“Una maanisha nini?”

“Give me the new code?Walinzi wote wa rais tumepewa code mpya nataka unitajie?”alisema mwana usalama Yule.Palepale kile kikosi kilichokuwa kinamlinda Dedani wakashtukia wakichomolewa bastola na wenzao.

“Code ipi?Code iliyopo Eagle fly Redcode condition.”alijibu bwana Yule.

Wanausalama wenzao wakaangaliana nakupeana ishara kuwa hawa wasio na code ndo wavamizi na wale walio nacode wakaonekana kama wao ndo wenye makosi.Punde sipunde walianza kurushiana risasi huku wengine wakiingia kwenye mapigano mazito sana.Dedani alichopoka kwa haraka kisha akajibiringisha chini.Akainuka wakati wanausalama wakikabiliana.Dedan aliinuka kwa ustadi wa ajabu.Alisimama akatoka nje.Dedani alipita kwenye korido za ikulu nakukuta watu wakikimbia huku na kule.Walinzi wa rais walikuwa wakirushiana risasi na wengine wakitwangana makonde mazito.Ndani ya muda mfupi hakuna mlinzi aliyemuamini mwenzake.Lengo lakuwachanganya lilifanikiwa baaada ya kuchanganywa na kikosi haramu kilichovamia ikulu ya rais Kilua.

Dedani alitoa simu yake mfukoni ili anataka kupiga alishtushwa na risasi iliyopita nakumchubua sikio.Wakati anaweweseka alishangaa mtu kumsukuma wakaangikia mlango nakuingia chumba kingine.Kwa kasi ya ajabu aliyemsukuma aliwahi mlangoni na bastola yake akiwa amechutama akafyatua risasi mbili nakufanikiwa kummaliza aliyemfyatulia Dedani.

Ile Dedani anageuka anakutana na sura ya Shunie.Shunie alimkimbilia Dedani nakumkumbatia kwa nguvu zote huku akimbusu.

“Uwe makini ikulu imevamiwa.Wanataka kumuondoa Kilua madarakani.Hadi sasa nahisi kuna uzembe mkubwa sana umefanyika hadi kufikia hatua hii.Tulijua kuna hatari kwa utawala wa Kilua lakini sio kwa namna hii.Hakuna aliyetegemea.Kwa upembuzi nimegundua hata walinzi wamechanganywa.Kuna mtu anatoa amri za uongo.Ana wa-confuse ndo maaana wanapigana.”alisema Shunie.
 
KOMBORA KIOTANI-44

BONIFACE BIRAGE

Dedani,”Mke wangu siwatamuua?”
“Kuna uwezekano huo.Nimeshangaa kumuona jenerali yupo hapa.Kuna vikosi tofauti vimeingia hapa.Kimoja kimeanza kushambulia walinzi.Kingine kimekuja na vifaru viwili cha ajabu hawaonekani kama wanatoa msaada.Huu ni uvamizi mbaya sana.”

“Shunie nakuomba jambo moja tena.”
“Ndiyo.”

‘Utakubali nimsaidie Kilua kwa mara ya mwisho?”

“Dedani kwanini tusitumie mwanya huu kuondoka kabisa eneo hili?Twende tuanze maisha mapya mimi na wewe.Penzi changa juani?”alisisitiza Shunie.

“Tafadhali tumsaidie.”
“Dedani ushahidi gani tena unataka umeshaambiwa na zee Kavu kwamba mkeo ni msaliti tena nini unataka kwake?Hao wanaovamia watahakikisha wanakumaliza na wewe.”

“No she is still my wife pia tunarudisha heshma ya taifa letu hakuna wakulichezea.”alisema Dedani kisha akashika simu yake.Akafya namba Fulani akaweka simu masikioni.

“This is special team commandor am activating the silent hunter for the glory of our nation.100911 We are going in full attack!”alitamka maneno yale bwana Dedani.Na palepale kikosi cha SILENT HUNTER mahususi kwa ukombozi wa taifa kilipata ujumbe ule.Kikosi hiki kiliundwa kwa wazalendo wan chi na mashujaa ambao maisha yao yote hawakujulikana hovyo.Walikuwa wasiri sana.Na leo ilikuwa siku yao maalum kuingia kazini.Kikosi cha Destruction Control Unit kilikuwa macho kwa matukio yaliyokuwa yakiendelea.

“So it is true?”aliuliza Shunie akimwangalia Dedani machoni.

“Kuhusu nini?”
“Kwamba SILENT HUNTER ni kikosi kilichopo nilidhani DCU ndo vikosi vya mwisho?”

Dedani akatabasamu,”Ni heshma kuwepo ila tunaruhusiwa kuingia kazini ikiwa tukio limetokea kama mmoja wetu ameshuhudia mbali na hapo we remain silent forever.Hata baada ya uamuzi huu nitatakiwa kutoa majibu.”

Dedani na Shunie walingia kazini Shunie,”Chukua silaha.”

“SILENT HUNTER hawatumii silaha.Sisi wenyewe ni silaha.Sisi ni wananchi wa kawaida sana.”alisema Dedani kisha kwa haraka ya ajabu alitoka mbio nakumuwahi moja vile vikosi vilivyovamia ikulu.Dedani alikuwa na ukomavu wa mafunzo na mwenye uimara wa ajabu namna alivyodhibti kwa mapigano mazito ilimfanya Shunie aduwae!Dedani alwashangaza wale kwa haraka alienda moja kwa moja hadi kilipo chumba cha rais Kilua alipokuwa akitibiwa.Alikuta madaktari wakiwa wamemaliza shughuli yao.Ilibidi wamfanyie operesheni maana pigo l;a Dedani lilileta hitilafu kubwa kwenye tumbo lake la uzazi.Upasuaji ulifanikiwa kurekebisha madhara yaliyojitokeza.s

Kufika pale aliupiga teke mlango akaingia nao nakukutana walinzi wa rais Kilua pamoja na timu ya madaktari.Walinzi walitaka kumkabili Dedani lakini kwa kasi ya ajabu Dedani alifanikiwa kuwadhibiti na kumnyang’anya mmoja silaha kisha akaiweka kwenye kichwa cha rais KIlua ambapo alitoa amri walinzi wengine washushe silaha zao la sivyo angeondoa ubongo wa Kilua.Ilibidi wazishushe lakini wakichukizwa maana Dedani aliwashtukiza na hawakuwa na jeuri ya kupiga risasi mgonjwa hakutakiwa kelele.

“Nisikilizeni ikulu imevamiwa na simuamini mtu mbele ya mke wangu.Wenzenu huko nje wanapigana na nyie mlioingia kwenye chumba cha upasuaji ndo mmesalimika.Nataka nimuondoe mke wangu hapa.”

“Una uhakika?”
“Ndiyo.Kwanini ni danganya.I Just need my family hii kazi inaleta shida.”
“Kwanza tuambie wewe ulipata wapi mafunzo haya?”aliuliza bwana Dittu mkuu wa ulinzi wa rais.

“Hilo halina maana kwa sasa.Mtu lazima ajiandae kulinda familia yake.”alisema Dedani akiwaangalia.Kisha alitoa bastola akawarudishia.Lilikuwa kosa kubwa sana.Kwani walinzi hakukoma hapo waliziokota zao na kwa kasi ya ajabu wakamshambulia Dedani kwa risasi nyingi!

“NOOO!”alipiga kelele Shunie ambaye aliwahiwa kwa kupigwa teke la kuruka likatua kwenye paji la uso!Shunie alianguka kifuani kwa Dedani!Dittu aliamuru rais Kilua aondolewe paleKilua hakuwa anaelewa ni kitu gani kinaendelea hadi muda yeye.Alikuwa usingizi maana dawa za usingizi zilimsafirisha mbali sana!Wakasukuma kitanda chenye magurudumu wakamuingiza kwenye lifti kisha ikashuka hadi chini ya handaki la ikulu.

Ndani ya muda mfupi walikuwa kwenye njia iliyochimbwa chini tayari kumtorosha rais Kilua.

“Tuna hitaji vikosi zaidi.”alisema moja ya walinzi wake.

“Hapana simuamini mtu tena!Ulinzi wa rais umeingia doa.Yeyote anayefanya hivi katushtukiza.”

“Tunaenda wapi mkuu?”

“Tunamuondoa rais Kilua katika ardhi ya Kiota.”alisema bwana Dittu.Lakini ghafla akawafyetulia walinzi wenzake risasi pamoja na madaktari.Dittu aliwaua wote na sasa alikuwa amebadilika na kudhihirisha yeye ni nan?Mbele yake walittokea watu wamevalia nguo kama za jeshi.Walimsaidia kusukuma kitanda wakarudi nacho kwenye ile lifti nakukiweka kisha wakapanda pamoja wakarudi juu.Walimpitisha rais Kilua njia za siri wakamuondoa rais Kilua eneo la ikulu.Kiota haikuwa salama tena tayari ilikuwa mikononi mwa ghasia na mchanganyo usioisha.

Wakiwa kwenye magari yao walitengeneza msafara wa rais.Ikujulikana kwamba Kilua yumo ndani ya moja ya magari yale.Mwendo ulikuwa mkali sana.Wapo waliokuwa katika msafara ule lakini hawakujua kwamba ule ni mtego mbaya sana kuwahi kutokea.

***

“Mkuu msafara wa rais Kilua unaelekea sehemu salama.”aliambiwa Serambovu aliyekuwa katika ofisi ya rais Kilua.

“Hakikisheni anatoroshwa nchini.Pia kila nyumba ya mbunge nahitaji vikosi vya usalama vivamie huko.Kila ofisi ya kiongozi wa serikali nataka kuwe na watu wetu.”

“Kila kitu kitapangwa kama kilivyo.”

Lakini ghafla Serambovu anapokea simu.Aliipokea,”Ndiyo Zee Kavu.”

“Sikiliza kwa makini kijana!Huo msafara unatunguliwa na mabomu.Kilua hatakiwi kupumua ulikuwa na nafasi ya kummaliza lakini naona unarembesha.Huyu akiomba msaada kutoka ummoja wa mataifa hakika hatutatoboa.Tayari kontena letu limeondolewa bandarini.”

“NO!Niachine Kilua mimi?”

“Seramboviu Kilua hana umuhimu mwanae tumeshamuua maiti yake tutaitupa popote pale au tuichome kwa aside!Huna haja umeshakula sana huyo Malaya.Yatosha sasa!”

“Etiii?”Serambovu alihisi tai kumkaba akawa anailegeza.

“Shani tumemuua!”

Serambovu kichwa kikawaka moto.

“Ile ni damu yangu jamani mnasemaje mmeua?Acha utani!”

“Kuna gharama kwa kila jambo.Huyu angekuja kutusumbua huko mbeleni.Tunafuta na ukoo wake wote!”Ulikuwa ujumbe mzito sana kwa wao kuupokea.

“Nchi ni ya kwako.”

Simu ikakatwa muda uleule.

Serambovu alijua amekabidhiwa madaraka mazito kwa ncha ya upanga.Kilua hakuwepo tena na sasa Kiota ipo mikononi mwake!Serambovu aliduwaa.

“What have I done?”

***

“Target acquired?”

“Eye eye sir!”

“Release the missile destroy the president’s convoy!”

Mshambuliaji akiwa kwenye tarakilishi yake alikuwa akiongoza drine kifaa kisichotumia rubani.Alikuwa anaona msafara wa rais Kilua ambao ulikuwa unaelekea sehemu salamu ambapo angepanda ndege kisha wamuondoe eneo lile.Huu sasa ulikuwa wakati mgumu sana kuliko vile walivyodhani.Walikuwa mbioni kumuondoa uhai rais Kilua.

“Goodbye madam president.BOOM!”Alisema nakubofya.Kisha kombora likaachiwa kutoka kwenye drone likaenda kwa kasi nakudungua msafara wa rais Kilua.BOOOM!KOMBORA KIOTANI.

MAWIMBI

Serambovu alikuwa amejishika kichwa asijue afanye nini?Alikuwa amezungukwa na wanajeshi.Simu zilikuwa zinaita kila sekunde akawa hapokei.Msafara wa rais Kilua ulikuwa umedunguliwa.Wote walimuangalia wakisubiri kauli yake kuondoa utata uliokuwemo.Serambovu hakuelewa hatua ya kuchukua.

“Acha kushika kichwa.Upepo umebadilika.Kiota imetikiswa ni wakati wako.Hatukutegemea ila imetokea sasa kubaliana na hali halisi.Hotuba yako isome kuhusu hatma ya Kilua.Kuna mengi ya kufanya kudhibiti utawala wako.”

Serambovu aliinua kichwa akaona karatasi nyeupe ikiw na maandishi pengine hayo maandishi hayakuwepo kwa jinsi msongo wa mawazo ulivyokuwa umemtafuna.Aliinua nakuhisi ni nzito.Mkutano na waandishi wa habari ulikuwa umewadia kwa yeye kutoa hotuba yake kwamba Kilua hayupo.Yeye kama chifu wa ikulu kaamua kutwaa madaraka mwenyewe.Kayashika kwa mikono yake na sasa yupo tayari kuiongoza Kiota.Kuna mataifa ya nje ambayo yangetakiwa kumsikia.Je,ni wangapi wangekuwa tayari kumuunga mkono?Alijiuliza bila kupata majibu.Ataweza kuwatuliza wananchi wake?Nchi imetoka katika vuguvugu la kuuawa kwa serikali ya rais Kisusi.Sasa hata ya Kilua imeondolewa na mnadhimu mkuu wa ikulu.Huu ulikuwa usaliti wa hali ya juu kuliko wote uliowahi kutokea!Alitakiwa kuyatuliza majeshi yote na kila sekta ya serikali ya Kiota ijifunze kumtii yeye!Bwana Serambovu alihisi ubovu alioingia nao.Mlango wa ofisi ukafunguka wakaingia watu Fulani wamevalia suti nadhifu.Wote walionesha umakini.Walikuwa wane.Wazungu wa tatu na mtu mweusi mmoja.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom