Riwaya ya Kipelelezi: Hatari

Riwaya ya Kipelelezi: Hatari

gilbert35

JF-Expert Member
Joined
Nov 20, 2021
Posts
253
Reaction score
476
RIWAYA: HATARI
Imeandikwa na Halfani SUDY
SIMU 0629 360357

Hii ni sehemu ya kwanza.

MLANGO wa ofisi yake ulisukumwa kwa nguvu, kwa haraka, macho mawili ya Daniel Mwaseba yaliangalia pale mlangoni. Na kwa haraka ileile ya macho, mkono wake wa kuume ulikuwa umeshafika kiunoni kwake na kuichomoa bastola yake ndogo, nyeusi, mdomo wa bastola ulikuwa umeelekea pale mlangoni, huku kidole chake cha shahada kikiwa kimekigusa kibonyazio.

“Ni nani wewe?” Daniel Mwaseba aliuliza kwa pupa baada ya macho yake kumtazama mtu aliyeingia kwa ghafla ofisini kwake. Hakulipata jibu la swali lake, aliupata mshangao, kwa maana ghafla yule mtu alidondoka chini, huku akitoa mguno mkubwa kuonesha kwamba alikuwa anapitia katika maumivu makali sana.

Kwa umakini mkubwa, Daniel alikisukuma kiti alichokuwa amekikalia kwa kutumia paja lake la mguu wa kulia. Akapata nafasi ya kupita kuelekea pale mlangoni alipoangukia yule mtu. Huku mkono wake wa kulia ulioishika imara bastola yake ukielekea katika mlango, wakati macho yake yakimtazama yule mtu aliyelala kifudifudi mbele kidogo ya mlango.

Ndipo macho yake yalipoona, michirizi ya damu kutoka kwa yule mtu ilikuwa inaelekea chini ya meza yake. Daniel hakuamini kwamba lile anguko ndilo lililosababisha ile michirizi ya damu!

“Ni nini hiki kinatokea?” Daniel alijiuliza mwenyewe huku kwa umakini mkubwa akimsogelea yule mtu. Hakukuwa na wa kumjibu swali lake, kwa maana mle ndani alikuwa yeye na yule mtu aliyekuwa hajiwezi kwa lolote.

Hatua za Daniel zilimfikisha mahali alipolala yule mtu, kwa mkono wake wa kushoto alitoa vilinda mikono katika mfuko wake wa nyuma wa suruali na kuvivaa. Akainama taratibu na kumshika yule mtu, huku akiwa makini sana na mlango. Hisia zake zilimwambia kwamba ule ulikuwa mtego. Alifanikiwa kumgeuza yule mtu, sasa alikuwa anaitazama sura yake.

Kwa makadirio tu, alikuwa anatazamana na mzee wa zaidi ya miaka sitini. Ngozi ya sura yake, rangi ya nywele zake yalithibitisha makadirio ya umri ya Daniel Mwaseba. Wakati Daniel akitafakari cha kufanya, yule mzee alifumbua macho yake kwa shida sana, huku akijitahidi kusema maneno ambayo hayakueleweka na masikio ya Daniel, zaidi ya kushuhudia mabonge mazito ya damu yakimtoka mdomoni.

“Yanipasa kumpeleka hospitali huyu mzee” Daniel aliwaza kichwani kwake. Na kweli, hali ya yule mzee ilihitaji kitu kimoja tu, kupelekwa hospitali. Kwa maana sio tu hakuweza kusimama kwa miguu yake, bali pia hakuweza hata kuuinua ulimi wake mwenyewe na kuongea. Tatizo lilikuwa sasa, Daniel hakumjua yule mtu ni nani?

Hakujua kama yule mtu amekuja kwake kwa bahati mbaya au makusudi. Kama alifika pale kwa bahati mbaya hakukuwa na tatizo sana, lakini kama alifika pale kwa makusudi, basi kulikuwa na tatizo, na bila shaka ni tatizo lililoambatana na hatari kubwa sana.

Daniel alitoa simu yake mfukoni kwa mkono wa kushoto. Alibofyabofya kutafuta namba ya mtu, alipoipata, aliipiga.
“Hallo Dokta Tawakal?” Daniel aliita simuni.
“Hallo Daniel, habari za masiku?” Dokta Tawakal alijibu kwa kuchangamka na kuuliza swali.
“Salama Dokta Tawakal, nipo sehemu mbaya kidogo, ninaomba tukutane nyumbani kwangu baada ya nusu saa, nina dharura kubwa sana. Hakikisha hakuna anayejua kama unakuja kwangu” Daniel alisema harakaharaka.
“Kuna nini Daniel?” Dokta Tawakal aliuliza kwa sauti iliyoambatana na uwoga.
“Naomba tukutane nyumbani kwangu baada ya nusu saa, nitakueleza kila kitu, hapa nilipo sio sehemu sahihi kukueleza hayo maswali unayoniuliza” Daniel alisema tena kwa haraka.
“Ok sawa, tukutane nyumbani kwako baada ya hiyo nusu saa” Dokta Tawakal alikubali.
Simu ikakatwa.

“Sasa nitamtoaje nje huyu mtu?” Daniel alijiuliza mwenyewe. Ofisi ya Daniel Mwaseba ilikuwa maeneo ya Posta, katikati ya jiji la Dar es salaam. Katika jengo la Decade Tower, ghorofa ya kumi na nne, katika ofisi namba arobaini na tano. Haikuwa kazi ndogo hata kidogo kumtoa yule mtu akiwa katika hali ile, katika ghorofa namba kumi na nne hadi chini bila kuzua kasheshe!. Jengo la Decade Tower lilikuwa ulinzi mkali sana wa kutumia kamera za kisasa za CCTV, kamera zikizosaidiwa na walinzi wazoefu kutoka kampuni binafsi ya ulinzi, kwa idadi walikuwa zaidi ya hamsini, wao na kamera zao, kazi yao kuu ilikuwa ni kulinda usalama wa jengo la Decade tower.

“Yanipasa nimtoe huyu mtu bila mtu yeyote kujua” Daniel aliwaza huku akikuna kichwa kwa mkono wake wa kushoto. Alikuwa anawaza njia gani sahihi ya kumtoa yule mtu asiyemfahamu ndani ya ofisi yake na kwenda kumpatia matibabu. Baada kama dakika mbili za kuwaza mwenyewe, alipata jibu. Kwanza alianza kumpekua mifukoni yule mtu, hakuwa na kitu chochote kile katika mifuko yake. Alisogea hadi kabati lililokuwa limeegemezwa katika kona ya ofisi, akalifungua kwa kutumia funguo alioutoa mfukoni.

Akalitazama kabati kwa muda wa dakika tatu, akipiga mahesabu yake. Baada ya kuridhika, akarudi nyuma hadi katika meza yake, akafungua droo la upande wa kushoto, akatafutatafuta kwa sekunde kadhaa, lakini hakukiona kitu alichokuwa anakitafuta. Akarudi tena kwa yule mtu aliyekuwa bado amelala chini, akambeba huku akiruhusu damu nyingi zikichuruzikia sakafuni na kuchafua mandhari ya ofisi yake. Moja kwa moja akaelekea naye kwenye lile kabati lililokuwa wazi, akamkalisha hovyo ndani ya kabati, akalifunga kwa funguo kwa nje. Alielekea mlangoni na kutoka nje, akafunga mlango kwa kutumia kadi maalum.

Harakaharaka, alielekea katika chumba cha sita, ambacho kilikuwa ni stoo ndogo. Alichukua ndoo ya maji na skwiza. Alirejea navyo ofisini kwake. Alianza kusafisha ofisi yote, alihakikisha hayabaki mabaki ya damu hata kidogo. Akatoka tena nje akihakikisha amefunga mlango vizuri kwa kutumia ile kadi maalum, alienda kurudisha vile vifaa vya kudekia stoo, kisha alipanda lift na kumshusha hadi chini kabisa ya jengo. Moja kwa moja, alienda katika duka moja la zana za kilimo lilikuwa karibu na lile jengo la Decade Tower, akanunua mfuko mkubwa mweupe wa nailoni. Harakaharaka alirejea ofisini kwake kwa kutumia lift.

“Ili zile damu zake zisibubujike njiani lazima nimhifadhi kwenye huu mfuko” Daniel aliwaza wakati akiufungua mlango wa ofisi yake kwa ile kadi maalum. Akaingia ndani kuelekea katika kabati alilomweka yule mtu. Kwa kutumia mkono wa kushoto, alifungua mlango taratibu kwa kutumia funguo, wakati mkono wake wa kulia ukielekeza bastola kabatini.

Alichokutana nacho sasa….
Kwa mara ya kwanza tangu azaliwe Daniel Mwaseba hakuyaamini macho yake. Alibaki mdomo wazi, mkono wake wa kulia ulioshika bastola ulikuwa unatazamana na kabati tupu, amini usiamini, hakukuwa na mtu ndani ya lile kabati. Lilikuwa kabati tupu, tupu tupu tupu.

Haditi inaitwa Hatari, mwandishi wako anaitwa Halfani Sudy, tukutane tena kesho tuisome tena Hatari ndani ya riwaya hii ya aina yake.

Pia facebook tunapatikana kwa jina la Simulizi Za Gilbert. Tufollow
 
Cover
IMG-20220308-WA0000.jpg
 
HALFANI SUDY Anasimulia HATARI
Simu 0629 360357
Mahali: Getho

……..Kwa mara ya kwanza tangu azaliwe Daniel Mwaseba hakuyaamini macho yake. Alibaki mdomo wazi, mkono wake wa kulia ulioshika bastola ulikuwa unatazamana na kabati tupu, amini usiamini, hakukuwa na mtu ndani ya lile kabati. Lilikuwa kabati tupu, tupu tupu tupu…..

Na Hii ni Sehemu ya Pili
“Ameenda wapi yule mzee?” Daniel Mwaseba alijiuliza mwenyewe, awali hakukuwa na wa kumjibu maswali yake ingawa walikuwa walikuwa watu wawili mle ofisini. Tofauti na awali, sasa Daniel hakukuwa na wa kumjibu kwakuwa alikuwa mwenyewe ndani ya ofisi yake. Mzee aliyemuacha akiwa amemfungia ndani ya kabati hakuwepo. Ilikuwa ni ajabu la nane la Dunia.
Daniel alilifunga kabati taratibu huku akiwa makini kuliko wakati wowote ule katika maisha yake. Kwa kasi aligeuka nyuma huku bastola yake ikinesa huku na kule katika mtindo wa ajabu, bado, hakukuwa na mtu. Wakati mkono ulioshika bastola ukiwa umeelekea katika mlango wa maliwato, macho yake yalitua juu ya meza. Macho yake yaliona kitu kipya ambacho hakikuwepo awali. Juu ya meza yake, kulikuwa na mfuko mkubwa wa nailoni mweupe mithili ya ule alioenda kuununua katika duka la zana za kilimo.
“Nani kauweka huu mfuko hapa?” Daniel alijiuliza tena kwa sauti ndogo huku akiusogelea ule mfuko. Akatoa vilinda mkono vingine na kuvivua vile vya awali, akavivaa mikononi. Akaushika ule mfuko na kuanza kuufungua. Mfuko ukafunga bila ya shida yoyote. Macho hayana pazia, moja kwa moja yalienda kuona kile kilichokuwa ndani ya ule mfuko wa nailoni. Daniel Mwaseba hakuamini alichokutana nacho, ndani ya ule mfuko kulikuwa na vipande vidogovidogo sana vya nyama, amini usiamini vilikuwa vipande vya nyama ya binadamu!
Mapigo ya moyo wa Daniel ulipiga kwa nguvu, mwili ulimwingia ubaridi huku nywele zikimsisimka! Sasa hisia za kwamba yule mtu alikuwa ni mtego zilitamalaki kichwani mwake. Kichwa chake kilifanya kazi ya kufikiria harakaharaka mara tatu zaidi ya anavyofikiria sikuzote. Kichwa kilikuwa kinatafuta namna sahihi ya kujitoa ndani ya ule mtego.
“Nifanye nini?” Kichwani mwake hili ndilo swali lililokuwa linajirudiarudia mara kwa mara. Wakati akiwa katikati ya alichokuwa anakifikria, mlango wa ofisi yake uligongwa kwa nguvu!
“Polisi” Hili ndio neno pekee lililopita kichwani mwake.
Harakaharaka aliuchukua ule mfuko wa nailoni uliokuwa umelala juu ya meza, akaufunga fundo kwa juu na kuutupia kabatini ambalo bado lilikuwa wazi, akasogea kwa haraka na kulifunga kabati kwa kutumia funguo. Alipomaliza tu kulifunga kabati mlango wa ofisi yake uligongwa kwa mara ya pili. Sekunde thelethini zilizofuata, harakaharaka Daniel akimalizia kuweka sawa vitu ndani ya ofisi. Kisha akatoa mfukoni kadi maalum ya kufungulia mlango na kuelekea mlangoni. Akaigusisha sehemu maalum, mlango ukafunguka. Mlango ulipofunguka tu, moja kwa moja alikuwa anatazamana na mdomo mpana wa bastola nyeusi, huku bega liliungana na mkono ulioshika bastola hiyo ukiwa ni askari Polisi. Nyuma yake akiwa na askari Polisi wawili na wazee wengine watatu ambao yeye hakuwatambua.
“Naitwa Inspekta Hayman kutoka kituo kikuu cha Polisi, kuna taarifa zimetufikia ofisini kwetu, tumekuja kuthibitisha kwamba ni kweli?”
Daniel alikohoa kidogo kuuondoa uwoga uliokuwa unamnyemelea kwa kasi, kisha aliuliza
“Taarifa gani mlizozisikia?”
“Tumepigiwa simu na Msamaria mwema, ametuambia kwamba mzee Maloto ameonekana akiingia katika ofisi yako, tumekuja kupekua ndani ya ofisi yako kama taarifa hizo ni sahihi, mimi kama nilivyojitambulisha, ninaitwa Inspekta Hayman kutoka kituo cha kati cha Polisi, nimekuja na hawa askari wenzangu wawili, huyu mzee aliyevaa shati la kijani ni mwenyekiti wa mtaa huu, huyu mwengine ni mjumbe wa mtaa, na huyu mzee mfupi ndiye mmiliki wa jengo hili, hii mkononi ni hati ya kuturuhusu kuipekua ofisi yako na jengo zima kwa ujumla” Inspekta Hayman alisema huku akimwonesha ile hati kwa mkono wake wa kushoto akiwa kashika sambamba na kitambulisho chake cha kazi.
“Mmhhhhh…” Daniel alihema kwa nguvu, maelezo ya Inspekta Hayman yalikuwa yamejitosheleza. Hakuwa na namna yoyote ya kujitetea, lakini swali lililopita kwa haraka katika ubongo wake ni mzee Maloto ni nani? Ilikuwa ni mara yake ya kwanza kulisikia jina hilo hapa Duniani, lakini aliona pale sio mahala sahihi pa kuuliza swali hilo.
“Mnaweza kuingia ndani kufanya upekuzi wenu” Daniel alisema kwa sauti ya upole akiwapisha wapite mlangoni, hakutaka kuwazuia askari Polisi kufanya kazi yao.
Watu wote sita waliingia mle ndani bila ya kusema neno lolote. Ukaanza msako wa kumtafuta mzee Maloto ndani ya ofisi ya Daniel Mwaseba.Ilikuwa tafrani ndani ya ofisi ya Daniel. Huyu akifunua hapa, yule anafunika pale, huyu akifunika hapa, yule anafunua kule. Lakini katika funika funua hiyo hawakumuona mzee Maloto. Walipekua hadi sehemu ambapo kiuhalisia binadamu wa kawaida hawezi kujificha. Lakini katu, hawakumuona mzee Maloto.
“Tunaomba ufungue kabati tuangalie na humo” Inspekta Hayman alisema kwa sauti kavu huku akimwangalia kwa jicho la ‘Leo kwisha jeuri yako’.
Moyo wa Daniel Mwaseba ulimpiga kwa nguvu, kauli ya Inspekta Hayman iliondoka na ujasiri wake anaokuwa nao siku zote. Kufunguliwa kwa kabati lililokuwa mbele yake ilikuwa ni sawa na kuiitia shingo yake katikati ya kitanzi, na kumsubiri mnyongaji mzoefu atekeleze kazi yake.
“Fungua mlango wa kabati kijana” Yule mzee aliyetambulishwa kama Mwenyekiti wa mtaa alilirejea ombi la Inspekta Hayman akimtoa Daniel katikati ya mawazo.
Sasa, Daniel hakuwa na namna nyingine ya kufanya zaidi ya kufungua mlango wa kabati. Alitoa funguo aliokuwa ameuhifadhi katika mfuko wa kulia wa suruali yake. Aliushika kwa mkono wa kuume na kuelekeza katika kitasa cha kabati. Aliushuhudia mkono wake mwenyewe jinsi ukivyotetemeka wakati ukielekea kabatini. Mkono ulitetemeka, lakini ulifika, ukafungua kabati ambalo katu moyo wake haukutaka lifunguliwe. Sasa kabati lilikuwa wazi, ule mfuko wa mweupe wa nailoni ulikuwa umelazwa hovyo chini kabisa ya kabati.
“Toa huo mfuko!” Inspekta Hayman aliongea kwa sauti yenye mamlaka akimwangalia Daniel Mwaseba. Huku akisitasita Daniel aliutoa ule mfuko, ambao kwake ulikuwa sawa na bomu.
“Naomba ufungue huo mfuko tuone kuna nini ndani yake?” yule Mwenyekiti alisema huku akimwangalia Daniel kwa macho makali.
“ Mnafikiri binadamu mnayemtafuta anaweza kujificha ndani ya mfuko huu?” Daniel aliuliza swali huku akimwangalia yule Mwenyekiti.
“Tumesema fungua huo mfuko!” Inspekta Hayman alisema kwa nguvu huku akimwelekezea bastola yake Daniel Mwaseba.
Daniel hakuwa na namna yoyote ile zaidi ya kuufungua ule mfuko. Taratibu alianza kuufungua fundo la mfuko, huku moyoni akiomba dua kisionekane kitu kilichokuwa ndani ya ule mfuko.
Bila hiyana mfuko mweupe wa nailoni ukafunguka…..

Je nini kitatokea?
Njoo tena kesho saa nne asubuhi tuyasome maandishi ya Halfani Sudy, pia tufwate Facebook kwa jina la Simulizi Za Gilbert
 
Halfani Sudy anasimulia HATARI
Mawasiliano 0629 360357
Mahali; Getho

“Naomba ufungue huo mfuko tuone kuna nini ndani yake?” yule Mwenyekiti alisema huku akimwangalia Daniel kwa macho makali. Daniel hakuwa na namna yoyote ile zaidi ya kuufungua ule mfuko. Taratibu alianza kuufungua mfuko huku moyoni akiomba dua kisionekane kitu kilichokuwa ndani ya ule mfuko.
Mfuko mweupe wa nailoni ukafunguka…..

Na hii ni Sehemu ya Tatu….
Kila mmoja alibaki mdomo wazi! Hakuna macho yaliyoamini yanachokiona kati ya macho kumi na nne yaliyokuwemo mle ndani. Kwa maana yalishuhudia vitu vya kutisha sana ndani ya ule mfuko mweupe wa nailoni, vipande vidogovidogo vya mwili wa binadamu vilikuwa vimejazwa hovyo, huku mfuko ukiwa umejaa na damu mbichi! Ilikuwa ni hali ya kutisha sana!
“Ni nini hiki tunachokiona?” Yule mzee aliyetambulishwa kama mjumbe aliipata sauti yake na kuuliza swali.
“Ukatili mbaya sana ameufanya huyu kijana, amemuua mzee Maloto, kwa hakika atalipa kwa hiki alichokifanya, lazima nihakikishe anaozea jela maisha yake yote! Amefanya mauaji ya kutisha sana, kama kuna asichostahili kijana huyu basi ni kuishi!” Mwenyekiti alisema kwa hasira akimwangalia Daniel Mwaseba.
Daniel Mwaseba alibaki akiwaangalia kwa zamu watu wote waliokuwa mle ndani. Sasa mambo yalikuwa hadharani, hivyo hata uwoga aliokuwa nao awali ulianza kumtoka taratibu. Alirudi kuwa Daniel Mwaseba halisi, mpelelezi kutoka kikosi maalum ndani ya jeshi la Polisi. Daniel Mwaseba ambaye ni mpelelezi namba moja nchini Tanzania.
“Mfunge pingu!” Inspekta Hayman alimwamrisha mmoja kati ya wale Polisi aliokuja nao. Yule polisi aliyeambiwa akaichomoa pingu yake kiunoni. Na hiyo ndio nafasi adhimu aliyokuwa anaisubiri Daniel Mwaseba. Yeye, alikuwa tayari kwenda jela lakini si nyakati kama hii, nyakati ambayo alikuwa anauhitaji uhuru wake kuliko wakati wowote ule katika maisha yake. Alikuwa anauhitaji uhuru wake kwasababu kuna vitu alikuwa anahitaji kuvitafutia majibu, alikuwa anahitaji kujua mzee Maloto ni nani? Alikuwa anahitaji kujua kwanini aje auwawe ofisini kwake? Alikuwa anahitaji kumjua Msamaria mwema gani aliyewapigia simu askari Polisi? Akiamini kuwa bila shaka huyo Msamaria mwema kuna kitu anakijua kilichosababisha kifo cha mzee Maloto. Angepata majibu ya maswali hayo pengine angekuwa tayari kwenda jela kama ilivyohitajika na Mwenyekiti lakini si sasa…….
Wakati yule askari akimsogelea Daniel Mwaseba na pingu yake mkononi, kichwani kwa Daniel kulikuwa kumeshapanga vyema mashambulizi yake. Wakati mkono wa kushoto wa yule askari ukiushika mkono wa kulia wa Daniel Mwaseba kwa ajili ya kuanza kuufunga pingu.
Daniel Mwaseba alifanya kitu….
Alimkwepa kwa nguvu yule askari Polisi aliyekuwa anataka kumfunga pingu kwa mtindo wa ajabu huku kiganja chake cha mkono wa kulia kikiigusa kwa nguvu shingo yake, yule askari Polisi alidondoka chini taratibu huku macho yake yakiushangaa uwezo wa yule Binadamu. Macho ya Inspekta Hayman yalikishuhudia kile kitendo kilichofanywa na Daniel Mwaseba, kwa uharaka alimwelekeza bastola yake aliyokuwa ameishika kama kipande cha muwa.
“Usijari…..”Inspekta Hayman hakumaliza kusema alichotaka kusema, kwani Daniel alifanya kitu, kwa kasi ya ajabu alipiga hatua moja na kuikwapua ile bastola kwa teke la mguu wake wa kulia, kwa kasi ileile alimzungusha Inspekta Hayman kama wafanyavyo wacheza mziki wa R&B na kuwa nyuma yake. Shingo ya Inspekta Hayman iliguswa na ubaridi wa mdomo wa bastola ya Daniel Mwaseba, ilikuwa ni bastola yake mwenyewe iliyotua mikononi mwa Daniel baada ya kurejea kule juu iliporushwa na teke.
“Yeyote atakayejaribu kufanya chochote bila kumwambia neno lolote napasua mishipa ya shingo ya huyu mwenzenu!” Daniel alisema kwa ukali, huku toni ya sauti yake ikimaanisha alichokuwa anakisema.
Watu wote mle ndani walimwangalia Daniel kwa macho ya mshangao. Hakuna aliyekuwa anaamini kasi ya vitendo vilivyofanywa na Daniel Mwaseba. Ilikuwa ni kasi kubwa sana kufanywa na binadamu wa kawaida, ilikuwa ni kama kufumba na kufumbua.
“We Mwenyekiti, chukua pingu kwa yule askari aliyelala chini….” Daniel alisema huku akimwangalia Mwenyekiti kwa macho makali. Huku akitetemeka Mwenyekiti alimsogelea yule askari aliyekuwa hajitambui pale chini. Akaichukua ile pingu aliyokuwa bado ameishika mkononi mwake.
“Mfunge yule askari!” Daniel alisema huku akimwonesha yule askari mwengine kwa kutumia mdomo wa bastola. Mwenyekiti alifanya kama alivyoagizwa.
“Lete hiyo pingu yake!” Daniel alisema baada ya Mwenyekiti kumfunga pingu yule askari. Mwenyekiti akaichukua pingu ya yule askari iliyokuwa inaning’inia kiunoni na kumpelekea Daniel Mwaseba. Alipomkaribia Daniel alisema.
“Mfunge na huyu!” Mwenyekiti alimfunga ile pingu Inspekta Hayman. Sasa askari wale wawili walikuwa wamefungwa pingu. Huku akiwaelekeza bastola watu waliokuwa mle ndani Daniel alisogea katika meza yake, alitoa kamba katika droo ya upande wa kulia na kumfunga yule askari mwengine na Mjumbe, Mjumbe hakuweza kuuzuia mkojo wakati akifungwa kamba na Daniel Mwaseba.
“Ninaondoka na ninyi!” Daniel alisema akiwaangalia kwa zamu Mwenyeki na mmiliki wa ile hoteli. “Mtu atakayejaribu kufanya ujuaji wowote ule ndio utakuwa mwisho wa maisha yake. Niwaambie tu, mpo karibu na kifo kuliko wakati wowote ule katika maisha yenu!”
Mwenyekiti na yule mmiliki wa hoteli waliitikia kwa kichwa, huku uwoga wa kutupwa ukionekana hata katika mitikisiko ya vichwa vyao.
“Tangulieni mlangoni!” Daniel alisema kwa ukali, mithili ya ng’ombe waswagwao walielekea mlangoni. Daniel naye alisogea pale mlangoni na kuufungua ule mlango kwa kadi maalum. Mlango ukafunga, wote watatu wakatoka nje, huku Daniel akiwa kwa nyuma yao. Akihakikisha hawafanyi jambo lolote la ajabu.
“Elekea kwenye lift, tunaelekea chini kabisa, mdomo wa bastola yangu umeelekezwa kati migongo yenu….” Daniel alisema kwa sauti ya taratibu, kauli ambayo ilizidisha hofu kwa wale watu wawili.
Safari sasa ilikuwa ya kimyakimya, walipanda lift pamoja na kutokea katika floo ya chini kabisa. Chini ya jengo la Decade tower kulikuwa na ofisi ya mapokezi, pembeni uitazamayo pindi tu utakaposhuka katika lift, kwa upande wa kushoto kulikuwa na hoteli nzuri na ya kisasa huku upande wa kulia kulikuwa na masofa kadhaa kwa ajili ya kupumzika watu wajao katika ofisi mballimbali. Daniel Mwaseba na watu wake walielekea mapokezi.
“Ninatoka kidogo Tina” Daniel alisema akimwangalia msichana mzuri aliyekuwepo pale mapokezi. Msichana alinyanyua sura yake iliyokuwa inaangalia tarakilishi, alipomwona Daniel alitabasamu.
“Sawa kaka Daniel” Tina alijibu huku akimwangalia Daniel kwa jicho la ‘U mtanashati sana kijana wewe’.
Moja kwa moja walitoka nje, sehemu ambapo kulikuwa kumeegeshwa magari mengi sana. Daniel aliwaelekeza mahali lilipokuwa gari lake, nao bila kusita walifuata. Haikuwa mbali sana, dereva aliyekuwa ndani ya gari alishuka na kuwafungulia wageni. Daniel na watu wake walikaa katika siti za nyuma.
“Martin, tunaelekea nyumbani” Daniel alisema taratibu huku akiangalia mbele.
“Sio uwanja wa ndege tena? Usiniambie umeghairisha safari yako?” Martin aliuliza kwa mshangao.
“Ni kweli Martin, nimeghairisha safari yangu nitaenda wakati mwengine, nina jambo muhimu sana la kufanya na hawa watu nilioingia nao garini” Daniel alisema huku safari hii akiwaangalia kwa zamu Mwenyekiti na Mmiliki wa jengo la Decade tower.
Martin hakuuliza swali lengine tena, alielewa ni kitu gani Daniel alikuwa anamaanisha, aliwasha gari na kulitosa barabarani, safari ya kwendaMikocheni nyumbani kwa Daniel Mwaseba ilianza.
Ndani ya gari kukawa kimya, kila mmoja akiwaza lake.

****

Saa moja baadae.
KUTOKANA na foleni iliwachukua saa zima kina Daniel kufika Mikocheni, nyumbani kwa Daniel Mwaseba. Martin aliegesha gari katika uwanja mpana katika nyumba ya Daniel Mwaseba. Daniel na watu wake walishuka na kuelekea sebuleni, huku Martin akifuata kwa nyuma baada ya kuhakikisha amefunga geti vizuri. Walipofika tu sebuleni, simu ya Daniel Mwaseba iliita, ilikuwa ni namba ya simu ya Dokta Tawakal, sasa alikumbuka miadi yake na Dokta Tawakal ya kukutana nyumbani kwake baada ya nusu saa.
“Umefika wapi Dokta Tawakal?” Daniel alisema baada tu ya kupokea simu.
“Sikiliza Daniel Mwaseba, kama kuna kitendo cha hatari uliwahi kukifanya katika maisha yako basi kimefunikwa na hiki kitendo cha hatari ulichokifanya leo. Sisi hatuna shida na wewe, tunakuomba mwachie Babu Ogutu tukuachie Dokta wako, na kuanzia hapo kila mmoja ataishi maisha yake, ukifanya hivyo Daniel utakuwa umeiepusha hatari kubwa sana!” Sauti nzito ya kiume iliunguruma kwenye simu.
Daniel alikata ile simu bila kujibu kitu chochote, akaizima kabisa simu yake.
Je nini kitatokea?
Tuwe wote kesho saa nne asubuhi Mungu akipenda tukiendelea na mwendelezo wa hadithi hii kutoka kwa Mwandishi Halfani Sudy.

Maoni yanaleta hamasa kwa mwandishi, maoni yanatupa hari ya kuzidi kuendelea. Hakikisha unalike na kutoa maoni yako baada ya kusoma.
 
Hadithi nzuri sana tunasubiri muendelezo wake
 
Shukrani mkuu ila ongeza episode kidogo
 
Halfani Sudy anasimulia HATARI
Mawaliano 0629 360357
Mahali Getho

Na hii ni Sehemu ya Nne….
Daniel alikata ile simu bila kujibu kitu chochote, akaizima kabisa simu yake.
“Karibuni sana ndugu zangu………” Daniel alianza kusema huku akiwaangalia wale watu wawili, ambao kwa sasa alimtambua mmoja wao kwa jina la Babu Ogutu, kama alivyoambiwa na Sauti inayounguruma simuni.
“Daniel, usinambie kuwa haujasafiri?” Sauti ya mtoto wa kike ilisikika ikisema ikitokea mlango unaoelekea chumbani, huku mtoto wa kike mwenyewe akiwa anatembea kwa madaha akielekea sebuleni..
“Hannan, ni kweli nimeghairisha safari yangu kwa sababu ya huu ugeni uliopo mbele yake, nina kazi nao muhimu sana watu hawa. Martin wapeleke hawa watu katika chumba cha mateso, nitaonana nao baada ya nusu saa” Daniel alisema bila ya wasiwasi wowote ule.
Martin alinyanyuka na kuongozana na wale watu hadi katika chumba cha mateso, hakuna aliyeongea chochote wakiwa njiani kuelekea katika chumba cha mateso. Martin aliwaingiza ndani na kuwafunga vizuri kwa kamba vitini, kisha alihakikisha amewafungia mlango kwa nje.
“Mmmeingia choo cha kike….” Martin alisema peke yake kwa sauti ndogo wakati akirejea ukumbini mahali walipo wakina Daniel Mwaseba.
“Daniel, ni kina nani wale watu? “ Hannan aliuliza swali huku akimwangalia Daniel Mwaseba kwa macho ya udadisi.
Daniel alichukua nafasi ya kuwasimulia kina Hannan kila kitu kilichotokea asubuhi katika ofisi yake a;ipoenda kujiandaa kwa safari. Hannan na Martin mara kadhaa waliingiwa na uwoga juu ya simulizi ya kuogfya ya Daniel Mwaseba, lakini Daniel mwenyewe hakuonesha uwoga wowote ule wakati akisimulia.
“Pole sana Daniel, sikujua kama ulipitia katika mkasa mzito kama huo asubuhi hii, mimi nilijua sasahivi upo uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius K. Nyerere ukimalizia taratibu ili ukaianze likizo yako huko Dubai” Hannan alisema kwa sauti ya masikitiko.
“Kiukwe ilibidi iwe hivyo Hannan, ila kwa bahati mbaya haijawa hivyo. Ujio wa yule mzee ambaye hadi sasa ninamtambua kwa jina la mzee Maloto umebadilisha kila kitu. Sasa tuna kazi ya kufanya uchunguzi ili kujua dhima ya ujio wa yule mzee, nahisi ujio wa mzee Maloto ni ishara kwamba kuna jambo la hatari linapangwa sehemu Fulani. Kazi yetu kuu ni kuijua hatari hiyo kabla haijaleta madhara. Uchunguzi wetu safari hii utakuwa mgumu sana, kwakuwa najua dakika chache zijazo itatangazwa ninasakwa na jeshi la Polisi kwa nilichowafanyia Inspekta Hayman na wenzake, kwahiyo tutafanya uchunguzi wetu huku mimi nikiikimbia mikono yenye nguvu ya dola. Lakini pamoja na kusakwa, tuna faida moja kubwa, tunazo sehemu tatu za kuanza na uchunguzi wetu, kwanza tunao hawa watu wawili ndani ya chumba cha mateso, lazima tukapate baadhi ya majibu kutoka kwao, bila shaka watatupeleka katika chanzo, nitaifanya kazi hiyo ya kwenda kuwahoji kwa kushirikiana na Martin Hisia, pili, Inspekta Hayman alinambia kwamba walipigiwa simu na Msamaria mwema, lazima tuingie kwa siri kwenye kanzidata ya mawasiliano ya jeshi la Polisi na kumjua huyo Msamaria mwema huyo ni nani, kwasasa sitaki tuwashirikishe jeshi la Polisi kwakuwa ninajua watakuwa wana hasira sana na mimi kwa nilichowafanyia wenzao, Hannan, mchawi wa kompyuta najua utatupa majibu juu ya huyo Msamaria mwema. Mwisho kabisa, dakika chache zilizopita nikiwa hapa, nimepigiwa simu na mtu akidai amemteka Dokta Tawakal na kutaka tubadilishane na mtu wao aliyemtambulisha kwa jina la Babu Ogutu, lazima tumjue huyu mtu ni nani? Hannan utaifanya kazi hii pia” Daniel Mwaseba alisema kwa kirefu.
“Sawa Daniel. Ngoja nikachukue tarakilishi yangu nianze kazi, mkirudi kuwahoji wale watu tutakuwa na majibu juu ya Msamaria mwema na huyo mtu aliyekupigia simu na kukutisha dakika chache zilizopita” Hannan alisema kwa kujiamini.
“Nakuamini mchawi wangu wa kompyuta, bila shaka hakuna uzio wowote unaoweza kuwekwa kukuzuia kugundua juu ya watu hao wawili. Sisi tunaenda katika chumba cha mateso kupata majibu ya maswali yetu” Daniel alisema huku akinyanyuka sofani, Martin naye alifuata nyuma ya Daniel, moja kwa moja walielekea katika chumba cha mwisho, ambacho walikipachika jina la chumba cha mateso, wakati huo Hannan, alielekea chumbani mwake kuchukua tarakilishi mpakato yake. Tayari kwa kuanza kufanya kazi aipendayo, kazi ya kusaka taarifa za siri zilizofichwa kitaalam sirini.
“Naitwa Daniel, Daniel Mwaseba, ni askari mpelelezi kutoka katika kitengo maalum ndani ya jeshi la Polisi. Nje ya kazi hiyo, mimi pia ni mfanyabiashara wa kuuza magari yaliyotumika na spea za magari, ofisi yangu kwa shughuli hiyo ya pili ipo pale ofisini tulipokutana, katika jengo la Decade tower” Daniel alisema baada tu ya kuingia katika chumba cha mateso. Aliwaangalia wale watu wawili kuhakikisha maneno yake yawaingia wale watu wawili”
“Naitwa Martin, Martin Hisia. Mimi ni mpelelezi wa kujitegemea, mpelelezi niliyesajiliwa na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Mimi na Daniel jukumu letu siku zote ni kuhakikisha haki inafuatwa na dhulma inaachwa, kuhakikisha halali inafuatwa na haramu inaachwa, kuhakikisha thawabu inafuatwa na dhambi inaachwa, kuhakikisha hila zote mbaya na za hatari zinazopangwa juu ya raia na serikali yetu hazileti madhara na zinakuwa hadharani. Sisi ni wapole na wakarimu sana ukifanya tunachosema, lakini tu watu wakatili sana ukiwa mkaidi na kutofanya tunachosema” Martin alisema huku akimwangalia yule mtu waliyemtambua kama Mwenyekiti.
“Unaitwa nani mzee? “ Martin aliuliza swali moja kwa moja baada tu ya kujitambulisha.
Yule mzee aliwaangalia Daniel na Martin kwa zamu, pamoja na kujitahidi ili aonekane kuwa yupo sawa lakini hali ya uwoga iliionwa katika kiini chake na macho ya Daniel Mwaseba.
“Unaitwa nani?” Martin Hisia alirudia tena swali lake.
“Naitwa Babu Ogutu…” Yule mzee alijibu sauti yake ikiambatana na uwoga.
“Nafahamu wewe sio Mwenyekiti wa ule mtaa, nasema hivyo kwasababu namfahamu Mwenyekiti wa mtaa ule. Mkataba wa kupanga katika jengo lile ulifanyika ofisini mwake. Nawe, nafahamu pia kuwa wewe sio mmiliki wa jengo la Decade tower, namfahamu mmiliki wa jengo lile kwakuwa ni mimi ndiye niliyeingia naye mkataba wa kupanga ofisi yangu katika jengo lake. Hivyo sitegemei majibu hayo katika maswali yangu. Haya, niambieni ninyi ni kina nani na kwanini mlikuwa pale?” Daniel Mwaseba aliuliza huku akiwaangalia wale watu wawili kwa zamu.
Hakuna aliyejibu, wote wawili walikaa kimya kama kulikuwa hakuna walichoulizwa. Martin Hisia alimwangalia Daniel Mwaseba, Daniel alifinya kwa chini jicho lake la upande wa kushoto, Martin alimjibu kwa kufinya kwa juu jicho lake la upande wa kulia. Wale watu wawili hawakuelewa nini walikuwa wanamaanisha lakini wenyewe walielewana, ile ilikuwa alama maalum ya kutaarifiana kwamba muda wa kazi ulikuwa umefika.
Bila kusema kitu, Daniel Mwaseba alielekea kwenye kabati jeusi lililokuwa katika kona ya kile chumba, akatoa rundo la funguo lililokuwa juu ya kabati na kuchagua funguo mmoja, akauingiza funguo aliouchagua kitasani na kufungua kabati kiurahisi. Mbele yake alikuwa anatazamana na zana mbalimbali za kutesea binadamu. Akachukua chuma kirefu ambacho kilikuwa na mshikio mweusi wa plastiki wa rangi ya samawati.
Martin Hisia naye alielekea katika lile kabati, yeye alichukua kisu kidogo ambacho mpini wake wa plastiki ulikuwa na rangi ya kijani. Wakawa wanarudi pamoja, kila mmoja akielelekea kwa mtu wake.
“Hatupendi kuwafanyia hiki tunachoenda kuwafanyia, lakini hatuna namna nyingine sahihi ya kufanya zaidi ya kufanya hivi, mmejifanya wakaidi, na siku zote hivi ndivyo tuwafanyavyo wakaidi” Daniel alisema kwa sauti ndogo wakati akimfuata yule aliyejiita mwenyekiti.
Je nini kitatokea?

Tuwe wote katika sehemu ya tano.
Tuandikie maoni yako baada ya kuisoma
IMG-20220311-WA0000.jpg
 
Tuandikie maoni yako baada ya kuisomaView attachment 2156115
Ni nzuri sana mambo yanazidi kunoga
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom