RIWAYA: Tai kwenye mzoga

mkuu mbona namba uloyoweka haipatikani
0688058669/
0713419558/
0753382210

Umepiga zote hizi hujampata? Pia nimeweka namba za mawakala wanaouza vitabu dar na mikoani umewapigia?

VITABU vya TAI KWENYE MZOGA, MIFUPA 206 na UFUKWE WA MADAGASCAR sasa
vinapatikana sehemu zifuatazo hapa nchini.
DAR ES SALAAM
-Posta pembeni ya Mnara wa Askari, nje ya duka la madawa la JB Pharmacy.
-Namba za wakala; 0713454152
; 0755454152
Stendi Kuu ya Mabasi ya mkoani UBUNGO.
-Namba ya Wakala; 0715546000
Duka la Kona ya Riwaya, Kinondoni,
-Namba ya wakala; 0655428085
MOSHI TOWN
-Namba za Wakala; 0754963999
; 0654241700
ARUSHA
Chini ya Mti karibu ya Idara ya Maji
-Namba ya wakala : 0755366822
: 0655366822
Opposite/ Mkabala na Benki ya Stanbic
-Namba ya wakala ; 0715413369
; 0762413369
-Duka la Vitabu la Case Book Store, Naaz
-Duka la Vitabu la Y2K Booshop Ilipo stendi ya mabasi ya Dar Express
IRINGA
-Duka la Vitabu la LUTENGANO
Namba ya muuzaji; 0767361984
-Mnara wa saa kwa wauza magazeti
Namba za mawakala; 0755860480
; 0752518911
:0763500396
MWANZA
-Duka la Vitabu la Victoria Education Centre, Eneo la Kemondo;
-Namba za wakala : 0754057315
-Pembeni ya jengo la NSSF, Mtaa wa Kauma
Namba za wakala ;0755950328
;0685182331
Wakala Tobias Edwin: 0746101949
-Mtaa wa Liberty, pembeni ya jengo la SEMIRA
Namba ya wakala ;0762002992
KWA MAELEZO ZAIDI:
Tembelea Ukurasa wa facebook wa mwandishi; Riwaya za Mwandishi Kevin Mponda.
Namba za simu za mwandishi; 0688058669/0713419558/0753382210
 
ULIKUWA NI MUDA WA KATI YA SAA KUMI NA SAA KUMI NA MOJA
ALFAJIRI ya siku iliyofuata na nilikuwa sijatongoa hata lepe moja la usingizi
wakati niliposikia makelele ya makufuli ya ule mlango wa pango yakifun￾guliwa kwa nje. Ghafla moyo wangu ulianza kuingiwa na wasiwasi mwingi,
nikageuka kuwatazama wenzangu mle pangoni nikagundua kuwa nao wali￾kuwa wameshtuka na kuamka toka usingizini na sasa walikuwa wamegeuka
kuutazama ule mlango wa pango huku nyuso zao zikiwa na mashaka.
Mara baada ya Ikirezi kushtuka toka usingizini aligeuka kuutazama ule
mlango kisha akageuka kunitazama mimi na hapo niliusoma uso wake namna
alivyokata tamaa, nikamuonesha ishara ya kumtuliza huku nikimtaka kuwa
asiwe na wasiwasi ingawaje hata mimi binafsi nilifahamu kuwa ujio ule wa
alfajiri haukuwa ule wa kutuletea chakula bali kulikuwa na jambo fulani lisi￾lo la kawaida. Jérome Muganza aligeuka kunitazama na hapo nikayaona ma￾chozi yakianza taratibu kushuka mashavuni mwake.
“Wanakuja kutuchukua na kama siyo wewe basi nitakuwa mimi” Jérome
Muganza aliniambia huku sauti yake imejaa kitetemeshi cha hofu.
“Usijali wala hakuna baya lolote litakalotokea” niliongea kama mpumbavu
huku nikijitahidi kumfariji Jérome Muganza ingawaje kwa kiasi fulani nili￾fahamu kuwa alichokuwa akikizungumza kilikuwa kweli. Nilimuona Jérome
Muganza akiangua kicheko hafifu na nilipogeuka kumtazama nikagundua
kuwa kicheko chake hakikuwa cha furaha bali kicheko cha hofu na kukata
tamaa huku machozi yakimtoka.
“Usinifariji rafiki yangu kwani usiku wa leo sikutapa usingizi vizuri, nilifa￾hamu fika kuwa leo ni mwisho wangu na muda si mrefu ninaenda kufa na lab￾da huenda tutakufa pamoja, mimi na wewe” nilimuona Jérome Muganza kama
ambaye alikuwa akitapatapa kwa hofu, nikamvuta haraka na kumwambia
“Hautakufa rafiki jipe moyo na Mungu wako atakusaidia”
Muda si mrefu ule mlango ulifunguliwa na hapo tukawaona wale wanajeshi wawili waliotuletea chakula siku ya jana wakiwa wamesimama mlangoni
pale, hata hivyo wakati huu hawakuwa na sufuria ya ugali wala ndoo ya maji
na hapo nikahisi baridi kali ya hofu ikipita nyuma ya shingo yangu.
Niliwatazama usoni wanajeshi wale nikazidi kukata tamaa nilipoliona
lile tabasamu la kinyama likianza kuumbika nyusoni mwao na sasa waliku￾wa wamesimama pale mlangoni huku wakiyazungusha macho yao taratibu
kumtazama mtu mmoja baada ya mwingine mle pangoni. Watu wote waka￾wa wameinamisha vichwa vyao chini wakikwepa kuonesha sura zao siziwe
kivutio katika macho ya wanajeshi wale. Moyo wangu ukapigwa na taharuki
kwa sekunde chache pale nilipoyaona macho ya askari wale yakiweka kituo
kwa Jérome Muganza na hapo nikaliona tena lile tabasamu la kinyama likizidi
kuchanua kwenye nyuso zao.
“Wewe! simama juu” askari mmoja alifoka huku akimtazama Jérome
Muganza na hapo nilimuona Jérome Muganza akisita kusimama kama ambaye
amri ile haikumhusu.
“Unajifanya hukunisikia siyo? yule askari alifoka kwa hasira na kuanza kui￾andaa bunduki yake waziwazi na hapo nikawa napiga mahesabu ya haraka￾haraka ya namna ya kuweza kuwavamia kwa hila wanajeshi wale. Lakini ka￾tika mahesabu yangu niligundua kuwa namna yoyote ya hila katika mazingira
yale ingenipelekea karibu na kifo kwani hakukuwa na mwanya wa kutosha wa
kuweza kufanya hila yeyote kwa sababu wale wanajeshi walikuwa mbali sana
kutoka pale nilipokuwa nimeketi hivyo hadi kuwafikia risasi siyo chini ya sita
zingekuwa tayari zimepenya mwilini mwangu na kuniacha nikiwa marehemu.
Hivyo nilijionya na kutulia huku nikimuomba Mungu.
Nilipogeuka tena hapo nikakutana na macho yaliyokata tamaa ya Jérome
Muganza yakinitazama kana kwamba mimi ndiye niliyekuwa na mamlaka
ya kuwapa amri wanajeshi wale wamwache. Nikamuonea huruma sana hata
hivyo nilimfanyia ishara ya kichwa kuwa asimame juu maana nilijua endapo
angeendelea kukaa pale chini na kupuuza amri ya wanajeshi wale ingekuwa
ni sawa na kukigongea hodi kifo. Jérome Muganza akanielewa na kusimama
kama nilivyomtaka hata hivyo nilipomtazama niligundua kuwa alikuwa akite￾temeka sana kwa hofu.
“Sogea mbele!” yule mwanajeshi akafoka na hapo Jérome Muganza akaf￾anya kama alivyoambiwa, akaanza kusogea taratibu kuelekea ile sehemu ya
katikati ya pango. Tukio hili likanifanya niikumbuke siku ya jana ambayo Dr.
Francois Trezor alipigwa risasi humu pangoni baada ya kutimiza amri zin￾azofanana na hizi anazopewa Jérome Muganza. Ghafla koo langu likaanza
kukauka kwa hofu.
“Simama hapo hapo” yule mwanajeshi alifoka tena wakati Jérome Mugan￾za alipofika sehemu ya katikati ya pango, Jérome Muganza akasimama kama
alivyoamrishwa huku akigeuka tena kunitazama. Nilimuonea huruma sana
hata hivyo sikuwa na la kufanya nikabaki nikimtazama tu. Mara tu Jérome
Muganza aliposimama wale wanajeshi wakaanza kumsogelea taratibu na wa￾lipomfikia niliwaona wakitaka kumshika mikono na hapo nilimuona Jérome
Muganza akipingana na tukio lile kwa kuinyanyua mikono yake hewani ili isishikwe.
Wale wanajeshi wakajaribu kutaka kumdhibiti hata hivyo walionekana
kuelekea kushindwa ndipo mmoja wao akamuwahi kwa kumgonga na kitako
cha bunduki kichwani. Lilikuwa ni pigo moja la nguvu kiasi kwamba nili￾weza kusikia mngongano wa kitako cha bunduki ya askari yule na kichwa
cha Jérome Muganza na muda ule ule niliiona damu ikiruka hewani kutoka
kwenye jeraha kichwani mwa Jérome Muganza huku yeye akipiga yowe kali
la maumivu.
Hata hivyo sauti yake haikwenda mbali sana mle pangoni kwani taratibu il￾ififia na hapo nikamuona Jérome Muganza akianguka chini huku fahamu ziki￾wa zimemtoka, hata hivyo wale wanajeshi walimuwahi kabla hajafika chini
wakamdaka huku mmoja akiuweka mkono wake mmoja begani na yule askari
mwingine akafanya vivohivyo kwa ule mkono uliosalia hali iliyompelekea
Jérome Muganza abaki akibembea katikati yao kisha wakaanza kumburuta
wakielekea nje ya pango. Na mara tu baada ya kutoka nje ule mlango wa
pango ulifungwa hivyo wakawa wameendoka na Jérome Muganza, nikabaki
nimeduwaa nisijue la kufanya.
Kwa kweli nilijihisi kuchanganyikiwa kwani nilijua hata kama nafasi ya
kutoroka mle pangoni ingepatikana bado swala la kutoka salama nje mapango
haya lingebaki kuwa ni kitendawili pasipo uwepo wa Jérome Muganza, kwani
ni yeye ndiye aliyekuwa akivifahamu vizuri vichochoro vya mapango haya
na vinginevyo tungejikuta tukizunguka mle ndani na si ajabu sana tungejikuta
tunarudi kule kule tulipotoka.
Bila kujielewa nikajikuta nikigongesha kwa nguvu ngumi yangu ya mko￾no wa kulia kwenye kiganja changu cha mkono wa kushoto huku tusi zito
likiniponyoka mdomoni, nikainamisha kichwa chini huku nikijihisi kuishi￾wa nguvu na kukata tamaa. Nilipoinua kichwa nikashtuka kumuona Ikirezi
na Jean Pierre Umugwaneza wakiwa pembeni yangu hata hivyo hakuna ali￾yenisemesha ingawaje nilipowatazama niligundua kuwa walikuwa wamenuia
kunifariji hasa baada ya fahamu kuwa mtu ambaye angefuatia kuchukuliwa
mle pangoni nilikuwa mimi. Nikatabasamu kidogo kuwatia moyo huku niki￾waonesha kuwa sikuwa nimekata tamaa sana na hali ile.
__________
SIKU NZIMA ILIYOSALIA MLE PANGONI hali ilikuwa imebadilika
sana, yale maongezi ya kirafiki na hali ya matumaini niliyokuwa nimejita￾hidi kuirejesha ilikuwa imetoweka na wakati wote mle pangoni kulikuwa na
ukimya na vilio hafifu vya hapa na pale vilivyokuwa vikija na kuondoka kama
upepo. Hata hivyo nilishangazwa sana na Ikirezi kwani wakati huo wote haku￾wa akilia badala yake alionekana ni mtu mwenye mawazo sana. Mchana kut￾wa ulipita na hatimaye ukaingia usiku bila ule mlango wa pango kufunguliwa
tena na hivyo tulishinda siku nzima bila kuletewa chakula. Usiku ulipoingia
nikajua siku ile ndiyo ilikuwa imepita kimya kimya na suala la chakula lin￾gekuwa ni mpaka kesho.
Sikuwa na mashaka kuwa ningeweza kuvumilia njaa hata kwa muda wa siku tatu hadi nne kutokana na mazoezi ya kikomandoo na mafunzo ya kijeshi
ambayo yalikuwa yamenikolea vizuri mwilini isipokuwa nilikuwa nikiwaho￾fia wenzangu mle pangoni ambao afya zao zilikuwa zimedhoofika sana.
Usiku ule ulikuwa mgumu sana kwangu pengine katika kipindi chote cha
maisha yangu hapa duniani. Akili yangu haikuweza kutulia kabisa kwani mara
kwa mara nilijikuta nikizungumza peke yangu kama mwehu. Wakati wote
mle ndani ya pango nilikuwa nikimuwaza Jérome Muganza, nikawa kama
ninayemuona akiwa katika mateso makali ya kinyama mbele ya wanajeshi
wale katili waliomchukua, nikabaki nikimuombea kwa Mungu amukoe na
kadhia hiyo.
Niliyaona masaa yalikuwa yakienda haraka sana kupita kiasi na siku ya pili
ilikuwa ikikaribia sana. Nikaanza kuhisi kuwa wale wanajeshi ni kama walio￾kuwa wakiusogelea ule mlango wa pango taratibu kuja kunichukua. Sikuwa
nikiogopa kuja kuchukuliwa mle ndani ila kilichokuwa kikinitia hofu ni kuwa
kitu gani kingefuata baada ya kuchukuliwa mle pangoni. Ulipofika usiku wa
manane watu wote mle pangoni walilala nikabaki macho peke yangu nikien￾delea kutafakari juu ya hatima yangu.
__________
ALFAJIRI YA SIKU ILIYOFUATA iliingia katika utaratibu kama ule ulio￾zoeleka wa siku zote mle pangoni ingawaje mimi binafsi niliiona ile siku ili￾kuwa imewahi sana, hata hivyo nilikuwa na nguvu na tumaini jipya, tumaini
ambalo sikuweza kufahamu lilitokea wapi. Uso wangu ulijawa na furaha sana
hali aliyowafanya watu wote mle pangoni wanishangae. Watu wote mle pan￾goni walikuwa wakiniaga na kunitia moyo kwani walikuwa wakijua kuwa
muda wowote ningekuja kuchukuliwa na wale wanajeshi.
Nilizipokea faraja zao na kuwatia moyo kuwa wasiwe na wasiwasi na mimi
na kuwa hakuna baya lolote ambalo lingenitokea ingawaje moyoni nilikuwa
na hofu sana. Baadhi yao walilia sana hata hivyo nilijitahidi kuwatuliza in￾gawaje moyoni nilifahamu kuwa mwanzo wa safari yangu ya kifo ulikuwa
umewadia. Nilitarajia kuwaona wale wanajeshi wakija kunichukua mapema
mle pangoni lakini haikuwa hivyo kwani masaa yaliendelea kusonga na hapo
nikajikuta nikianza kuingiwa na wasiwasi.
Kitendo cha kutomuona Jérome Muganza akirudishwa tena mle pangoni
kikazidi kuniongezea hofu moyoni huku nikiwaza kuwa pengine angekuwa
ameuwawa na wale wanajeshi. Muda wote nikiwa ndani ya lile pango niliku￾wa nikiwafariji Ikirezi na Jean Pierre Umugwaneza kuwa wasiwe na wasiwasi
na badala yake waendelee kumuomba Mungu atuokoe na kadhia ile.
__________
HAIKUWA MPAKA ILIPOFIKA MCHANA ndipo nilipoyasikia makufuli
ya ule mlango wa pango lile yakifunguliwa kwa nje. Watu wote mle pangoni
wakawa wameshtuka na kugeuka wakinitazama katika namna ya kuniambia
buriani hata hivyo mimi nilibaki nikiutazama ule mlango wa pango. Baada ya
muda mfupi niliuona ule mlango ukifunguliwa na hapo niliwaona wanajeshi wanne wakiingia mle ndani, nikafahamu kuwa ulinzi ulikuwa umeongezwa
na hiyo ilitokana na kuwa walikuwa wakija kumchukua mtu hatari aliyekuwa
akizifahamu mbinu zote za kijeshi ambaye mtu huyo ni mimi.
Niliwatazama wale wanajeshi huku nikiwakumbuka wawili miongoni
mwao kuwa walikuwa ni wale waliomchukua Jérome Muganza siku ya jana.
Wale wengine sura zao zilikuwa ngeni machoni mwangu na wote walikuwa ni
wanajeshi wenye afya nzuri, warefu na wenye miili iliyojengeka vizuri kima￾zoezi na wote walikuwa na bunduki zao mikononi. Nilipowachunguza usoni
nikaziona nyuso zao kuwa hazikuwa na mzaha hata kidogo.
Mara baada ya mlango wa pango kufunguliwa wale wanajeshi wawili wa￾geni machoni mwangu waliingia ndani na kusogea mbele zaidi wakiwaacha
wale wenzao kiasi cha hatua kama nne nyuma yao kisha wakasimama na
kuanza kumtazama mtu mmoja baada ya mwingine mle pangoni. Mimi sikuifi￾cha sura yangu kwani nilifahamu kuwa kwa vyovyote walikuwa wamenifuata
mimi na hata kama ningejificha wangenipata tu.
Hivyo nilibaki nikiwatazama wale wanajeshi huku wenyewe wakiendelea
kuwachunguza watu mle pangoni, lakini hatimaye wakaweka kituo kunitaza￾ma mimi na hapo nikahisi kama niliyemwagiwa maji ya baridi.
“Luteni Venus Jaka wa jeshi la wananchi wa Tanzania leo ni zamu yako
kamanda” mwanajeshi mmoja kati ya wale wawili aliongea kwa dharau huku
akinitazama.
“Zamu yangu kufanya nini? niliwauliza na hapo wote wakaangua kicheko
“Kwa hiyo unataka kuendelea kukaa humu ndani uchi namna hiyo? mwen￾zake alidakia huku akiendelea kucheka.
“Kamanda wetu anataka kukuona na bila shaka utakuwa na majibu ya mas￾wali yake” yule mwanajeshi mwingine aliendelea
“Maswali gani? niliwauliza huku nikinuia kuwakoroga akili zao.
“Utajua kila kitu pale utakapoonana naye” mmoja alinijibu na hapo nika￾geuka kuwatazama wanajeshi wawili waliokuwa wamesimama pale mlangoni
ambao ndiyo wale waliomchukua Jérome Muganza siku ya jana.
“Jérome Muganza yuko wapi? niliwauliza wale wanajeshi kwa hasira.
“Huu ni wakati wa kuyawazia maisha yako Luteni na si maisha ya Jérome
Muganza” mmoja alinijibu kwa dharau.
“Mnafichaficha nini kwanini msizungumze kama wanaume waliotahiriwa
jandoni au mmemuua? niliwauliza na hapo nikajikuta nikitandikwa ngumi nne
tumboni hali iliyonipelekea nimtapikie usoni yule mwanajeshi aliyekuwa aki￾nipiga huku nikihisi maumivu makali sana tumboni.
Yule mwanajeshi alighadhibika sana kwa yale matapishi yangu akazidi kun￾ishushia kipigo cha nguvu lakini mwenzake aliwahi kumkataza kuwa aniache
kwani hali yangu ingezidi kuwa mbaya zaidi. Yule mwanajeshi alisitisha kuni￾piga huku akionekana kufura kwa hasira ya kukatishwa adhma yake na muda
uleule ikachukuliwa kamba kisha nikaanza kufungwa miguuni na mikononi
kama ng’ombe anayeandaliwa kuchinjwa.
Nilijaribu kufurukuta lakini haikunisaidia kitu kwani yule mwanajeshi
alinidhibiti kikamilifu nikabaki nikihema tu kwa hasira. Alipomaliza kunifunga ile kamba wale wanajeshi waliomchukua Jérome Muganza walikuja
na kunibeba begani kama gogo wakinitoa mle pangoni na wale wanajeshi
wengine wakatufuata kwa nyuma huku mitutu yao ya bunduki ikiwa tayari
muda wowote kufanya shambulizi pale ambapo ningejidai kuleta ujanja.
Mara baada ya kutoka nje ya lile pango ule mlango ukafungwa na wale wa￾najeshi walionibeba waliniweka chini na hapo mmoja alinimbia
“Hatuna utaratibu wa kumbeba mtu luteni utabidi utembee mwenyewe”
Niliitazama miguu na mikono yangu nakaiona kuwa ilikuwa bado imefung￾wa kamba kwa umadhubuti wa hali ya juu na hapo nikashindwa kumuelewa
yule mwanajeshi alimaanisha nini kuniambia nitembee mwenyewe waka￾ti mikono na miguu yangu ilikuwa bado imefungwa. Wakati nikiendelea
kushangaa nilishtukia nikipigwa mtama na hapo nikaanguka chini mzimamzi￾ma na kujipigiza bila mhimili wowote, nikasikia maumivu makali mno.
Mara nikamuona mwanajeshi mmoja akitoa ule mnyororo uliokuwa ukitu￾mika kuniburuta hapo awali wakati nilipokuwa nikiletwa mle pangoni na hapo
nikafahamu kuwa yule mwanajeshi alimaanisha nini wakati aliponiambia
kuwa “Hatuna utaratibu wa kumbeba mtu Luteni utabidi utembee mwenyewe”
Bila ya kufunguliwa zile kamba nilimuona mwanajeshi mmoja akiufunga
ule mnyororo miguuni kwangu na hapo hofu ikanishika kwani nilifahamu
kuwa kutembea kwenyewe kulikozungumziwa kulikuwa ni kule kuburutwa
kama ule utaratibu uliotumika wakati nilipokuwa nikiletwa mle pangoni.
Zoezi la kunifunga ule mnyororo lilipokamilika safari ilianza, mwanajeshi
mmoja alitangulia mbele yangu akiuvuta ule mnyororo niliofungwa miguuni
na mwingine alitembea sambamba na mimi pembeni yangu. Nyuma yangu
walinifuata wanajeshi wawili waliosalia na bunduki zao mikononi. Kwa kweli
nilisikia maumivu makali mno huku nikipiga mayowe bila msaada wowote
kwani wale wanajeshi walikuwa wakinicheka tu na wakati fuani niliwasikia
wakibadilishana maneno kwa lugha ya kinyarwanda ambayo mimi nilikuwa
siifahamu kabisa.
Wakati nikiendelea kuburutwa kwenye sakafu ile mbaya ya mapango yale
nilihisi vile vidonda vikubwa vya michubuko mgongoni mwangu vilivyokuwa
vimeanza kukauka vilikuwa vikitoneshwa upya huku nikiendelea kuchunika
vibaya sehemu za nyuma za mwili wangu. Nilisikia maumivu makali sana am￾bayo sikuwahi kuyapata katika maisha yangu hata hivyo sikuwa na jinsi nili￾baki kumwomba Mungu anisaidie na hapo nikaanza kupoteza fahamu taratibu
ingawaje niliweza kuzihisi njia tulizokuwa tukizipita mle pangoni japokuwa
kulikuwa na giza zito mno lisiloruhusu kumuona hata mtu wa pembeni yangu.
Wakati tukiendelea na safari yetu mle pangoni niligundua kuwa baadhi ya
sehemu za mapango yale zilikuwa na majimaji yaliyokuwa yakitiririka kwenye
mifereji hafifu ya mle ndani. Pia niliweza kuzisikia sauti za popo waliokuwa
wakipiga makelele sehemu fulani fulani na hapo nikayakumbuka maneno ya
Jérome Muganza juu ya popo na chatu wakali waliokuwa ndani ya mapan￾go haya. Nikajikuta nikimuomba Mungu atuepushe tusije tukakumbanana na
mashambulizi ya viumbe hao huku mimi nikiwa bado nimefungwa mikono na
miguu yangu. Tulisafiri kiasi cha umbali wa kama mita mia mbili hivi huku tukizipita kona
nane za mapango yale ambazo nilikuwa makini sana kuzihesabu huku nikijari￾bu kuyazoea mazingira yake. Baada ya kusafiri kwa umbali ule hatimaye sa￾fari yetu ilikuja kuhitimika mbele ya mlango mmoja uliokuwa sehemu fulani
katika mapango yake.
Tulipofika hapo wale wanajeshi walisimama na mmoja wapo akaenda ku￾gonga kwenye mlango ule, baada ya kugonga kidogo nilimuona mtu fulani
ndani ya chumba kile akifungua dirisha dogo lililokuwa juu ya mlango ule
na kuchungulia. Alipofungua akatazama tazama kisha sura yake ilitoweka na
lile dirisha kikafungwa halafu muda ule ule niliuona ule mlango wenye diri￾sha ukifunguliwa. Mlango ulipofunguliwa yule askari aliyekuwa mbele yangu
akaanza tena kuniburuta kuelekea ndani ya chumba kile cha pango huku wale
wenzake wakitufuata kwa nyuma.
Tulipoingia tu mle ndani ule mlango ulifungwa nyuma yetu na tukawa tu￾metokezea kwenye korido nyingine ya pango ambapo tuliendelea na safari
nyingine yenye urefu wa kama mita ishirini hivi. Tulipofika hapo tukakun￾ja kona upande wa kushoto na hapo mbele yetu niliuona mlango mwingine
mkumbwa zaidi ya ule wa awali na kulikuwa na miale hafifu ya mwanga iliy￾okuwa ukipenya kutoka ndani ya chumba kile. Tulipofika tulisimama na mwa￾najeshi mmoja alienda kugonga mlangoni pale kama alivyokuwa amefanya
kwenye ule mlango wa awali.
Kulikuwa na dirisha jingine dogo kama lile lililokuwa kwenye ule mlango
wa awali ambapo mara baada ya yule mwanajeshi kugonga lile dirisha lili￾funguliwa kisha mtu fulani alichungulia. Sikuweza kuiona vizuri sura ya mtu
yule na mara baada ya mtu yule kuchungulia lile dirisha lilifungwa kisha ule
mlango ukafunguliwa na yule mwanajeshi akaanza kuniburuta kuelekea ndani
ya chumba kile.
__________
TULIPOINGIA TU MLE NDANI ule mlango ulifungwa nyuma yetu na
hapo nikajua kuwa tulikuwa tumefika mwisho wa safari yetu. Tulipoingia tu
niliweza kumuoa yule mtu aliyetufungulia mlango akiwa amesimama pembe￾ni ya mlango ule. Niligeuka kutazamatazama upande huu na ule mle ndani na
hapo nikakikumbuka vizuri kile chumba kuwa kilikuwa ni kile chumba nili￾chokuwa nimeletwa siku ya kwanza baada ya kutekwa kule njiani.
Mbele ya chumba kile nyuma ya meza kubwa idadi ya watu ilikuwa ime￾ongezeka na kulikuwa na makamanda watano wa jeshi. Watatu walikuwa ni
wale niliowaona siku ile ya kwanza nilipofikishwa ndani ya mapango haya
yaani Kanali Bosco Rutaganda na wenzake wawili. Wengine walikuwa ni
makamanda na maafisa wa kizungu wa jeshi la umoja wa mataifa la kulinda
amani nchini Rwanda. Maafisa hao wawili wa kizungu walikuwa ni wa jeshi la
Ufaransa, niliweza kuwatambua kutokana na mavazi yao ya kijeshi hata hivyo
nilishindwa kuelewa ni kwanini maafisa wale wa jeshi la umoja wa mataifa
walikuwa mle ndani.
Wakati huo yule mwanajeshi aliyekuwa akiniburuta alikuja na kuniketisha kwenye kiti kilichokuwa kikitazamana na ile meza ya maafisa wa kijeshi
waliokuwa kiasi cha umbali wa hatua nne mbele yangu na hapo nilijikuta niki￾tazamana na meza ile huku Kanali Bosco Rutaganda akiwa katikati yao.
Nilijihisi mfadhaiko kwa kuketi uchi mbele ya wanaume wenzangu hata
hivyo sikuwa na namna nikabaki nikitazamana na Kanali Bosco Rutaganda
na hapo nikaliona tabasamu lake la dhihaka likichanua usoni mwake. Nili￾pokichunguza chumba kile cha pango nikagundua kuwa sehemu kubwa ya
chumba kile ilitawaliwa na giza zito. Mwanga mdogo wa taa ya kandili ili￾yokuwa juu ya meza ya maafisa wale ndiyo iliyoleta nuru kidogo mle ndani.
Baada ya kuketishwa vizuri na kufungwa kamba kwenye kiti kile wale wa￾najeshi wawili yaani yule aliyekuwa akiniburuta na yule mwenzake waliyeku￾wa wakiongozana kutuletea chakula kule pangoni walipiga saluti kwa pamoja
wakaaga na kuondoka hivyo mle ndani tulibaki jumla ya watu tisa. Yaani wale
maafisa wa jeshi watano waliokuwa wameketi nyuma ya ile meza, mimi na
wanajeshi wengine watatu, wawili wakiwa ni wale waliokuwa wakinilinda
kwa nyuma wakati nilipokuwa nikiburutwa kuja humu ndani na mmoja aliku￾wa ni yule aliyetufungulia mlango wa chumba hiki cha pango.
Wanajeshi wale wawili walikuwa wamesimama nyuma yangu na yule
mmoja alisimama pale mlangoni wote wakinitazama na sasa chumba kilikuwa
kimetulia na hakuna sauti yoyote iliyokuwa ikisikika mle pangoni. Niliyazun￾gusha macho yangu taratibu kukikagua vizuri kile chumba na watu wale, juu
ya ile meza ya maafisa wa kijeshi kulikuwa na bastola moja ambayo sikuelewa
nini hasa lilikuwa dhumuni la kuiweka bastola ile pale mezani. Wale wanajes￾hi wawili waliokuwa nyuma yangu sikuweza kugeuka na kuwatazama kutoka￾na na namna kamba zile nilizofungwa zilivyokuwa zimenikaba.
Nilipogeuka kumtazama yule mwanajeshi aliyesimama pale mlangoni
nikaiona kurunzi ndefu ikiwa imening’inia kiunoni mwake na bunduki yake
mkononi tayari kunishambulia pale ambapo ningethubutu kufurukuta. Nika￾yarudisha tena macho yangu kuwatazama wale maafisa wa kijeshi mbele yan￾gu.
“Habari yako Luteni” Kanali Bosco Rutaganda akaanza kwa kunisalimia
huku akitabasamu nikajua tu alikuwa akinisanifu hata hivyo nilimuitikia kwa
utulivu.
“Si nzuri”
“Kwa nini? aliniuliza huku akiiegemeza mikono yake mezani.
“Nina njaa kali naomba mnisaidie chakula kwanza” niliwaambia hapo wote
wakaangua kicheko.
“Mara hii tu unahitaji chakula wakati hata kazi yetu bado hujaifanya? Kana￾li Bosco Rutaganda akaniuliza huku akiendelea kuangua kicheko hafifu.
“Nahitaji chakula kwanza ndiyo nitaweza kuwafanyika hicho mnachokihi￾taji” nilisisitiza
“Usilete hila Luteni kwani huu si wakati wake” Kanali Bosco Rutaganda
alikatisha kicheko chake na kuniamba huku akinikazia macho.
“Hila gani nitakayoileta hapa katika hali ya kufungwa kama hii?, nina njaa
kali nahitaji chakula kwanza” nilimwambia huku nimeshikwa na hasira na hapo nikamwona Kanali Bosco Rutaganda akimfanyia ishara fulani yule mwa￾najeshi aliyesimama pale mlangoni na hapo nilimuona yule mwanajeshi aki￾fungua mlango na kutoka nje ya lile pango.
Ulipopita muda wa dakika kama kumi yule mwanajeshi alirudi akiwa na sa￾hani moja iliyojaa wali na nyama ya kuku, mkono mwingine alishika gudulia
la maji ya kunywa na kikombe. Nilistaajabu sana kukiona chakula cha nam￾na ile mle pangoni huku nikijiuliza kilikuwa kimeletwa au kulikuwa na watu
fulani mle pangoni waliokuwa wakipika, kwa kweli sikutapa majibu. Yule
mwanajeshi aliyerudi na chakula alikuja na kusimama pembeni yangu huku
akiitazama ile meza ya Kanali Bosco Rutaganda, nikajua alikuwa akisubiri
amri kutoka kwa bosi wake.
“Nifungue mikono wewe bwege sasa unadhani nitakulaje, vitu vingine siyo
mpaka usubiri maelekezo ya mumeo” nilimwambia yule mwanajeshi na hapo
nilimuona alivyobadilika na kufura kwa hasira ingawaje hakunifanya kitu cho￾chote mbele ya mabosi wake.
“Mfungue” Kanali Bosco Rutaganda akamwambia na hapo nikamuona yule
mwanajeshi akianza kunifungua zile kamba nilizofungwa kifuani na mikononi,
hata hivyo niligundua kuwa alikuwa akinifungua kwa jazba kwa vile nilikuwa
nimemtukana. Hali ile ikanifanya nianze kuwaza kuwa endapo wale maafisa
wa kijeshi wasingekuwepo mle ndani mwanajeshi yule angeweza kuitumia
nafasi hiyo kuzimalizia hasira zake zote kwangu, hata hivyo sikumuacha na
wakati alipokuwa akinifungua zile kamba nilimnong’oneza
“Mbona unakuwa na hasira hivyo utadhani mwanamke mwenye mimba
changa? nilimwambia na hapo akanitandika ngumi mbili mgongoni za kiujan￾jaujanja ambazo hakuna mtu yeyote aliyemuona mle ndani na hapo nikahisi
maumivu makali mgongoni.
“Leo ndiyo mwisho wako wewe mwanaharamu na usifikiri kwamba utapata
nafasi ya kuponyokwa tena na maneno yako machafu mdomoni” yule mwa￾najeshi alininong’oneza kwa hasira bila ya mtu yeyote mwingine kumsikia
mle ndani kwani wale maafisa wa kijeshi walikuwa wakiteta jambo fulani
hivyo hawakuwa wakitutazama kwa wakati ule.
Nilitabasamu kidogo huku nikiyatafakari maneno ya mwanajeshi yule, sasa
nilifahamu kuwa nilikuwa nikiandaliwa mazingira ili niuwawe. Nikaushuku￾ru uchokozi wangu kwani ulikuwa umenipelekea kuzisikia habari zile nyeti
ingawaje yule mwanajeshi yeye alidhani kuwa alikuwa akiniambia vile kwa
kunikomoa kumbe badala yake alikuwa amenipa habari za kunitahadharisha.
Niliwatazama tena wale maafisa wa kijeshi mbele yangu, upande wa kush￾oto wa Kanali Bosco Rutaganda alikaa mzungu mmoja ambaye nilimtambua
kwa cheo chake cha kijeshi cha Meja Theodole Nicholous na kulia kwake
alikaa Luteni Kanali Jean Petit wote wakiwa na beji maalum vifuani mwao
kwenye sare zao za kijeshi, beji hizo zikieleza majina na vyeo vyao.
“Hawa ni akina nani? nilimuuliza Kanali Bosco Rutaganda huku nikiwako￾dolea macho wale maafisa wa kijeshi wazungu
“Hawa ni marafiki zetu wanaotusaidia kulinda amani hapa nchini Rwanda”
Kanali Bosco Rutaganda alinijibu kwa utulivu
“Kwanini wako hapa?
“Wanataka kukusikia wewe”
“Wanisikie nini?
“Chochote unachokifahamu kuhusiana na hali ya usalama ya hapa Rwanda
kwani pengine taarifa zako zikawasaidia wazidi kudumisha usalama” Kanali
Bosco Rutaganda alinijibu huku akinitazama na hapo nikauona uso wake nam￾na ulivyobadilika na kuwa wa kinyama.
“Kitu gani?
“Usilete mchezo na mimi luteni, usidhani kuwa nimekuja hapa kufungisha
ndoa, kumbuka ulituambia kuwa una njaa kali na usingeweza kuifanya kazi
yetu hadi upewe chakula. Umepewa chakula sasa ni wakati wa kujibu maswali
yetu kwa unyoofu na si kutuletea ubabaishaji” Kanali Bosco Rutaganda alini￾fokea kwa hasira kisha akakohoa kidogo na kuendelea
“Tuambie, ulitumwa hapa Rwanda kufanya nini na kipi ulichokipata mpaka
sasa?
“Mimi sikutumwa na mtu bwana nani aliyekuambia mimi nimetumwa?
“Kama hujatumwa ni sawa, basi tueleze ni kipi kilichokuleta hapa Rwanda”
“Nilikuja kupumzika na kustarehe tu niifurahie likizo yangu”
“Na hili jina la Patrick Zambi umelipata wapi?
“Nimepewa na wazazi wangu”
“Kwa hiyo wewe una majina mawili?
“Matatu” nilimkatisha huku nikipandwa na hasira kwa kuulizwa maswali ya
kipuuzi na mwanafunzi wangu wa kijeshi.
“Majina matatu?
“Ndiyo, moja ni la kikabila” niliongea na hapo nikamuona Kanali Bosco
Rutaganda akicheka kwa dharau.
“Usitudanganye luteni mtu mmoja hawezi kuwa na majina matatu huo ni
utapeli, mara hii uitwe Venus Jaka mara hii uitwe Patrick Zambi na wakati
huohuo uitwe sijui nani huko, hebu kuwa mkweli na utuambie umefuata nini
hapa Rwanda”
“Si nimeishakueleza kuwa nimekuja hapa Rwanda kupumzika na kustarehe,
nipo likizo kwa kipindi cha mwezi mmoja”
“Usijifariji kuwa unaweza kutudanganya danganya kirahisi luteni”
“Sasa mnataka nisemeje? nilimuuliza.
“Sema ukweli wako kwani ni ukweli tu ndiyo utakaokusaidia vinginevyo
hatutoivumilia janja yako” Kanali Bosco Rutaganda aliniambia halafu akawe￾ka kituo kidogo kama anayefikiria jambo kabla ya kuendelea tena
“Bila shaka upo hapa nchini Rwanda kwa ajili ya uchunguzi wa kifo cha
mwandishi wa habari Tobias Moyo, hizo ndizo habari tulizonazo na wewe si
mwandishi wa habari wa kujitegemea uitwae Patrick Zambi kama unavyopen￾da watu wa hapa Rwanda wakufahamu. Wewe ni mpelelezi tena wa jeshi la
wananchi wa Tanzania mwenye cheo cha luteni. Tunachotaka kufahamu ni
yapi mafanikio ya kazi yako tangu ulipofika hapa Rwanda”
Niliinua macho yangu kumtazama Kanali Bosco Rutaganda huku nikiwa na
donge la chuki kooni baada ya kuifahamu vizuri hila yake. Yule mwanajeshi alimaliza kunifungua zile kamba katika muda mfupi tu na hapo nikahisi ahue￾ni, nikaipokea ile sahani ya wali na kuipakata mapajani kisha nikaanza kula
taratibu bila kujali kuwa wale watu mle ndani walikuwa wakinitazama.
Wakati nikiendelea kula nikajikuta nikimuwaza Jérome Muganza huku niki￾jiuliza kama alikuwa tayari amekwisha uwawa au bado alikuwa hai, na kama
alikuwa hai alikuwa wapi kwa wakati huu. Niliendelea kula taratibu huku niki￾tafakari ulinzi imara uliokuwa mle ndani, kwa kweli nilikata tamaa sana kwani
sikuona udhaifu wowote ambao ningeweza kuutumia katika kujiokoa. Wale
wanajeshi hawakuyaondoa macho yao kwangu kwani kila mmoja alionekana
kuzifuatilia vizuri nyendo zangu na hali hiyo ilinikatisha tamaa sana.
Nilikumbuka namna safari yangu ilivyokuwa nzuri wakati nilipokuwa niki￾toka jijini Dar es Salaam kuja hapa Rwanda na kwa kweli sikuwa nimetarajia
kukutana na kadhia hii tena mapema kiasi hiki. Sasa nilijiona kuwa nilikuwa
nikielekea kufa tena kifo cha aibu kisicholingana kabisa na hadhi yangu. Kufa
nikiwa uchi wa mnyama na pengine maiti yangu kutupwa sehemu fulani mle
pangoni na taarifa zangu kupotelea kusikojulikana.
Kwa mara nyingine nilijikuta nikimkumbuka Brigedia Masaki Kambona,
mratibu wa safari zangu za kijasusi na hapo nikaanza kumhisi ni kama ali￾yekuwa akiujua mwisho wa maisha yangu mahali pale, kwa kweli nilihisi
kuchanganyikiwa.
“Luteni fanya haraka utueleze mpaka sasa umefikia wapi katika harakati
zako hapa Rwanda kwani wageni wangu wanataka kuondoka na wanahitaji
kusikia toka kwako” Kanali Bosco Rutaganda aliyakatisha mawazo yangu na
kuyarudisha mle pangoni na hapo nikabaki nikimtazama tu.
“Tafadhali tueleze luteni hatuna muda wa kuendelea kukusubiri zaidi”
Kanali Bosco Rutaganda aliendelea na hapo nikamuona ni kama aliyekuwa
akiharakisha kifo changu huku nikiingiwa na hofu kwani sikujua ni kitu gani
kingetokea pale ambapo kile walichokitarajia kutoka kwangu wangekikosa.
Nilipokuwa nikimaliza tonge la mwisho la chakula kwa maana nyingine
nilijiona ni kama niliyekuwa nikigongelea msumari wa mwisho kwenye jene￾za langu mwenyewe, nikaiweka ile sahani chini kisha nikajimiminia maji na
kugida bilauri mbili za chapuchapu. Kilikuwa chakula kizuri na kitamu na
nilipomaliza kula nikahisi hali ya nguvu ya mwili wangu ilikuwa imerudi seh￾emu yake.
Nilikuwa nimeshiba vizuri hivyo nilitulia kwenye kile kiti nikisubiri ki￾fuatacho. Kanali Bosco Rutaganda alinitazama na kukenua meno yake meusi
yenye ukungu wa moshi wa sigara huku akitabasamu. Hata hivyo tabasamu
lake halikuwa na maana yoyote kwangu kwani nilibaki nikimtazama kwa ha￾sira.
“Bila shaka umeshiba vizuri luteni na sasa upo tayari kutueleza” Kanali Bo￾sco Rutaganda aliniambia huku akiendelea kutabasamu kwa dhihaka.
“Nilikuwa na njaa sana”
“Haya tueleze”
“Sasa mnataka niwaeleze nini ambacho hamkijui? nilimuuliza huku nikiji￾chokoa meno kutoa mabaki ya vipande vya nyama vilivyonasa.
“Tunachokijua sisi ni sehemu ndogo tu ya ulichonacho ndiyo maana upo
hapa utueleze hiyo sehemu iliyosalia”
“Mna hakika gani kwamba mimi nina hiyo sehemu iliyosalia? niliwaambia
na hapo nikawaona wakigeuka kutazamana huku kila mmoja akionesha kuka￾sirishwa na maneno yangu
“Luteni si unafahamu kuwa kufanya ujasusi kwenye nchi yoyote ni kosa
kubwa lisilostahili kusameheka, kwani hiyo ni sawa na kuzichunguza siri za
nchi husika na kuzitumia kwa maslahi ya nchi yako. Kosa hilo huwa halina
msamaha na msamaha pekee unaoweza kujitokeza ni kwa kushirikiana na sisi
vizuri kwa kutupatia taarifa tunazozihitaji”
“Mimi sina taarifa zozote vinginevyo si mngeziona katika ile kamera yangu
mliyoichukua”
“Usitufanye sisi ni watoto luteni! ile kamera ni mpya na wala haina kitu
chochote tumeisha ichunguza”
“Si ndiyo nilikuwa nataka nianze kazi yangu nyie mkanikamata”
“Ulikuwa ukitaka kuanzia wapi hiyo kazi yako?
“Bado nilikuwa sijaamua nianzie wapi ila mpaka kufikia usiku wa siku ile
ningepata wazo la wapi pa kuanzia. Hivi hufahamu kuwa kazi yangu nyingine
ni uandishi wa habari? nilimuuliza Kanali Bosco Rutaganda na hapo niliona
uso wa chuki kali ukiumbika taratibu usoni mwake.
“Tukitaka tunaweza kukulazimisha utuambie kila kitu lakini sidhani kama
utapenda tufike huko, hata hivyo uvumilivu wetu huwa una kikomo”
Kanali Bosco Rutaganda aliniambia huku uso wake umefura kwa hasira. Ni￾lipomtazama nikagundua kuwa alikuwa akimaanisha alichokuwa akikiongea
lakini hali hiyo haikunishawishi nitake kumueleza juu ya safari yangu ya kuja
hapa Rwanda. Nilimkumbuka mwalimu wangu wa mafunzo ya kijeshi wakati
nilipokuwa mafunzoni pale alipokuwa akisema “Unapokamatwa mateka ka￾tika uwanja wa kivita usidhani kuwa ukisema ukweli ndiyo utakuwa salama,
hiyo haitakusaidia kitu kwani hata kama ukizungumza ukweli adhabu yako
bado itabaki palepale kwani wewe bado ni mateka tu”. Na katika pango hili
nilifahamu kuwa nikiwa kama jasusi adhabu pakee niliyostahili ingekuwa ni
kifo tena bila shaka kifo cha kinyama chenye maumivu makali mno, hivyo
niliona ni bora nife na siri zangu moyoni kuliko kuwaambia kwani hiyo isin￾genifaa chochote.
Niliwatazama wale wazungu wawili wafaransa maafisa wa jeshi la umoja
wa mataifa (UN) ambao walikuwa hapa nchini Rwanda kama walinzi wa
amani huku nikishindwa kuwaelewa walikuwa ni walinzi wa amani wa namna
gani wanaoshirikiana na mtu muuaji kama Kanali Bosco Rutaganda, na wali￾kuwa wamekuja mle pangoni kusikia nini kutoka kwangu?.
Nilikumbuka kuwa Kanali Bosco Rutaganda alinitaka nimueleze nilipofikia
katika upelelezi wangu juu ya kifo cha mwandishi Tobias Moyo lakini nil￾ishindwa kuelewa ni kwanini alinitaka nimueleze mambo yangu mbele ya
maafisa wale. Nikabaki nimeinamisha kichwa changu chini huku nikimuomba
Mungu.
Nikiwa bado natafakari nilimsikia Kanali Bosco Rutaganda akiteta jambo fulani na wale maafisa wa jeshi wazungu katika lugha ya kifaransa kisha
nikamuona Kanali Bosco Rutaganda akigeuka kunitazama.
“Luteni!, au labda nikuoneshe ni kitu gani ninachomaanisha” Kanali Bosco
Rutaganda aliniambia na hapo nilimuona yule mwanajeshi aliyesimama pale
mlangoni akiiwasha ile kurunzi yake iliyokuwa ikining’inia kiunoni halafu
akamulika upande wa kushoto wa pango lile sehemu kulikokuwa na giza, ik￾abidi na mimi nigeuke kuutazama ule mwanga wa ile kurunzi mahali ulipoku￾wa ukimulika, loh! nilijikuta nikishikwa na taharuki.
Kulikuwa na miili ya watu wawili iliyokuwa imefungwa kamba miguu juu
kichwa chini huku ikining’inia toka sehemu ya juu ya pango lile, umbali mfupi
toka pale nilipoketi. Miili hiyo ilikuwa ikibembea taratibu juu ya paa la pan￾go lile na nilipoitazama nikajikuta nikikata tamaa sana ya maisha yangu. Ule
mwili wa mtu wa kwanza ulikuwa umetapakaa damu kila mahali na nilipouta￾zama vizuri nikaona kuwa ulikuwa na majeraha ya mapanga karibu kila eneo,
vilevile damu nyingi ilikuwa imejikusanya chini ya mwili ule na sikuwa na
shaka kuwa mtu yule alikwishakufa ingawaje matone ya damu yake yalikuwa
bado yakiendelea kuchuruzika taratibu pale chini sakafuni.
Ule mwili wa mtu wa pili ulionesha uhai hafifu kwa kiasi fulani ingawaje
nao ulikuwa na majeraha katika baadhi ya sehemu na ulikuwa ukiendelea ku￾churuzika damu taratibu. Niliutazama mwili wa mtu yule na hapo nikajikuta
nikimkumbuka Jérome Muganza na kwa kweli hofu ilinishika sana hasa pale
nilipowaza kuwa pengine angekuwa yupo miongoni mwa watu wale wawili.
Wakati nikiendelea kuwaza ghafla ile kurunzi ilizimwa na kunifanya nigeu￾ke kutazama kwenye ile meza ya maafisa wa kijeshi na hapo nikajikuta niki￾tazamana na Kanali Bosco Rutaganda huku lile tabasamu lake la kinyama li￾kichanua usoni mwake. Kisha nikamuona akifikicha macho kwa vidole vyake
na alipomaliza aliiweka tena mikono yake pale mezani.
“Tuambie luteni umefikia wapi katika upelelezi wako?
“Nikwambie nini tena?, na hawa maafisa wa jeshi la kulinda amani la umoja
wa mataifa wapo hapa kwa sababu gani?
“Hawa ni marafiki zetu wanaotusaidia sana kulinda amani hapa nchini na
wamekuja humu ndani kututembelea na kusikia kutoka kwako” Kanali Bosco
Rutaganda aliniambia huku akicheka kwa kebehi.
“Wanawasaidia nini?
“Hiyo si kazi uliyotumwa hapa Rwanda tafadhali tuambie umefikia wapi
kwenye huo uchunguzi wa kifo cha Tobias Moyo na usitupotezee muda wetu
luteni” Kanali Bosco Rutaganda alipiga mikono yake juu ya meza na kufoka.
“Mbona mnaning’ang’aniza niwape majibu kwa kazi ambayo hamjanituma?
niliwaambia lakini kabla sijaamaliza kuongea ghafla nilishangaa nikichotwa
pale nilipoketi kwa wepesi wa kushangaza na muda uleule nikapandishwa juu
na kugeuzwa kichwa chini miguu juu, nikawa nikining’inia hewani na kile kiti
nilichokuwa nimekikalia nikawa nakiona kwa chini yangu.
Nikagundua kuwa kile kiti kilikuwa kimewekewa mtego wa kamba un￾aoweza kumchukua hewani mtu yoyote pale anapokikalia baada ya kufyatuli￾wa kwa siri. Wale watu wote mle ndani wakaangua kicheko cha dhihaka. Kwa kweli nilijiona kama bwege kwa kuchezewa akili yangu bila kupenda na hapo
tusi zito likaniponyoka nikiwatukana watu wote mle ndani.
“Hakuna aliyewahi kuingia kwenye pango hili akabaki na siri zake moyoni
luteni, hivyo hata wewe tunaamini kuwa utatuambia tu” Kanali Bosco Ruta￾ganda aliniambia na muda huohuo nilimuona akiinama na kuvuta droo mo￾jawapo ya ile meza aliyoketi na mikono yake iliporudi mezani ilikuwa imeshi￾ka misumari na nyundo. Hofu ikazidi kunishika, nikajikuta nikifumba macho
na kumuomba Mungu kwani nilifahamu kitu gani kilichokuwa kikifuatia. Ni￾lipofumbua macho nikamuona yule mwanajeshi aliyekuwa amasimama pale
mlangoni akifungua mlango na kutoka, nikajua alikua ameagizwa kitu fulani.
Muda mfupi baadaye yule mwanajeshi alirudi huku akiwa amebeba jiko
la mkaa uliokolea vizuri, nilishtuka sana kuliona lile jiko na nilipotazama
vizuri nikaviona vipande vya nyaya ngumu kama zile zitumikazo kubanikia
mishikaki zikiwa zimepata moto kisawasawa na kuwa nyekundu na hapo ni￾kajua kuwa nilikuwa nikiandaliwa mimi, kwa kweli nilikata tamaa sana. Yule
mwanajeshi alitoka tena na aliporudi alikuwa na betri kubwa ya gari aina ya
Yuasa iliyokuwa imefungwa nyaya katika temino zake. Kisha vitu vyote vile
vikasogezwa karibu yangu na hapo nilimuona yule mwanajeshi akiijaribu ile
nguvu ya betri kwa kuzigusanisha zile nyaya mbili ambapo zilipiga shoti kub￾wa na kutoa cheche.
Nilimuona yule mwanajeshi akifurahi kisha akaenda kuichukua ile nyundo
na ile misumari iliyokuwa pale juu ya meza ya Kanali Bosco Rutaganda na
aliporudi wale wanajeshi wawili walinishika na kunidhibiti vizuri nikawa si￾wezi hata kujitikisa. Muda huo huo yule mwanajeshi wa mlangoni akazunguka
nyuma yangu na kunishika na mara nikaanza kuhisi maumivu makali huku
nikipiga mayowe lakini hakuna aliyeonekana kushtushwa na hali ile.
Walikuwa wakinigongelea msumari mgongoni mwangu na ule msumari
ulipoingia nusu ya sehemu yake wakaanza kugongelea msumari mwingine
kwenye paja langu la mguu wa kushoto na walipomaliza wakafanya hivyo￾hivyo kwenye paja la mguu wangu wa kulia. Walipomaliza wakahamia na
mikononi ambako walinigongelea misumari miwili mingine, mmoja mkono
wa kushoto na mwingine mkono wa kulia.
Nilihisi maumivu makali mno ambayo sikuwahi kuyapata tangu nizaliwe.
Damu nyingi ilikuwa ikinitoka toka katika majeraha yale ya misumari lakini
hakuna aliyeonekana kujali.
“Luteni! utatusamehe sana kwani hatukupenda tufikishane huku ila ni wewe
ndiye uliyetulazimisha kufanya hivi, hata hivyo muda wa kujiokoa bado
upo. Unaweza kujiokoa kwa kutuambia ukweli kuwa ulikuwa umefikia wapi
kwenye upelelezi wako hapa Rwanda na ulikuwa ukishirikiana na nani kwani
bado hujachelewa sana” Kanali Bosco Rutaganda aliniambia.
Sikumjibu neno kwani hasira ilikuwa imenishika mno na badala yake nika￾kusanya mate mdomoni na kumtemea usoni. Nilikuwa nimemlenga vizuri na
mate yale yalimpata vizuri usoni pale alipoketi na hapo akajipangusa kwa ki￾ganja chake huku akiwa amefura kwa hasira. Akanyanyuka na kunifuata pale
nilipoketi na hapo akaanza kunitandika ngumi mwilini. Aliendelea kunishushia kipigo hadi pale alipochoka huku wale wanajeshi
wengine wakiwa wakiwa wamenishikilia kikakamavu ili nisifurukute. Damu
ilianza kunitoka mdomoni na puani nikawa nikihema hovyo kuitafuta hewa ya
oksijeni iliyoonekana adimu sana kwa wakati ule.
“Wakati mwingine jifunze kuwa na adabu Luteni kwani jeuri haitakusaidia
kitu hapa” Kanali Bosco Rutaganda alifoka baada ya kusitisha kipigo kile ki￾sha nilimuona akigeuka kuwatazama wale wanajeshi.
“Endeleeni na kazi” hatimaye aliwaambia wale wanajeshi na muda huohuo
nikamuona mwanajeshi mmoja akizichukua zile nyaya za umeme zilizoungan￾ishwa kwenye ile betri ya gari na hapo nikajua kuwa walikuwa wamepanga
kunipa mateso kwa kunipiga shoti ya umeme kwani ulikuwa ni mtindo wa
mateso niliokua nikiufahamu vizuri.
Ulikua ni mtindo wa mateso wenye maumivu makali mno yasioelezeka.
Zile nyaya zilipounganishwa kwenye ile misumari iliyogongelewa mwilini
nikaanza kupigwa shoti kali nikitetemeshwa mwili mzima, nilihisi maumivu
makali sana nikapiga mayowe ya hofu huku nikitokwa na jasho jingi.
Hali yangu ilipoanza kuwa mbaya wakaondoa zile nyaya kwenye ile misu￾mari na hapo nikahisi auheni kidogo hata hivyo nilijihisi kizunguzungu huku
nikihisi kutaka kutapika.
“Mwacheni” Kanali Bosco Rutaganda aliwaambia wale wanajeshi “Bila ya
shaka sasa yupo tayari kutuambia”
Mimi nikabaki nikiwatumbulia macho.
“Luteni swali letu si unalifahamu, tunasubiri jibu lako”
“Mimi sifahamu chochote” niliwaabia huku nikiwatazama wale wazungu na
hapa nikawaona wakitabasamu.
“Endeleeni na kazi” Kanali Bosco Rutaganda akawaambia wale wanajeshi
na zile nyaya zikaunganishwa tena kwenye ile misumari. Nikapiga tena yowe
la maumivu huku nikiwasihi waniache kwani hali yangu ilikuwa mbaya sana
lakini hakuna aliyesikiliza ombi langu. Yale mateso yaliendelea zaidi hadi pale
nilipoonekana kuishiwa na nguvu ndipo waliponiacha. Kanali Bosco Rutagan￾da akasimama na kuja kuninong’oneza sikioni.
“Afadhali utuambie Luteni, tupo tayari kukubadilishia starehe endapo hii
itaonekana haikufai”
“Mimi sifahamu chochote” nilimwambia
“Unafahamu kila kitu Luteni usitudanganye”
“Ningekuwa nafahamu ningewaambia”
“Endeleeni na kazi” akawaambia wale wanajeshi baada ya kuona naendelea
kukaidi na safari hii Kanali Basco Rutaganda aliongea kwa hasira akiwaambia
wale wanajeshi, na zile nyaya zilipounganishwa kwenye ile misumari mwilini
ziliachwa kwa muda mrefu zaidi.
Nilihisi maumivu makali sana nikapiga mayowe nikiwasihi waniache na
wakati huo nikawa nikiisikia sauti yangu namna ilivyokuwa ikisafiri na kuten￾geneza mwangwi kwenye kona za pango lile. Niliendelea kupiga mayowe
huku kile kizunguzungu kichwani kikizidi kuongezeka na hatimaye nikaacha
kupiga mayowe kwani nilihisi kuishiwa nguvu.
“Tuambie Luteni” nilisikia tena sauti ya Kanali Bosco Rutaganda ikini￾nong’oneza tena sikioni
“Mimi sifahamu chochote mtaniua bure tu” nilimjibu huku nikifumbua ma￾cho kumtazama na hapo nilimuona akiwa ameshika waya uliokuwa kwenye
lile jiko la mkaa ambao wakati huu ulikuwa umepata moto kiasi cha kuwa
umebadilika rangi na kuwa mwekundu. Ule waya sasa ulikuwa sentimita
chache mbele ya macho yangu na nilipomtazama Kanali Bosco Rutaganda
nikamuona akitabasamu.
“Tunakubadilishia starehe Luteni utatusamehe kidogo” Kanali Bosco Ru￾taganda aliniambia huku akicheka na muda uleule wale wanajeshi wakanika￾mata vizuri kiasi kwamba sikupata nafasi ya kujitingisha na ule waya uliopata
moto vizuri ukawekwa juu ya jicho langu la kulia. Maumivu niliyoyasikia
hayaelezeki kwani nilikuwa nikiungua taratibu na nikawa nikinusa harufu ya
nyama mbichi iliyokuwa ikiungua pembeni ya jicho langu, harufu ya mchomo
wa nyama iliyoambatana na moshi hafifu. Maumivu niliyoyasikia niliomba
ardhi ipasuke nitumbukie ili niwe mbali na kadhia ile.
Nikaachama mdomo wangu ili nipige mayowe kuomba msaada lakini sauti
haikutoka. Kwa kweli nilijisikia vibaya sana kama niliyekuwa mbioni kukata
roho.
“Haya tuambie Luteni” Kanali Bosco Rutaganda alininong’oneza hata
hivyo sikuweza kumjibu kwani hali yangu ilikuwa mbaya sana.
“Endeleeni na kazi” nilimsikia akiwaambia tena wale wanajeshi na hapo
nilianza tena kuchomwa na zile nyaya kila sehemu mwilini nikilazimishwa
kuongea. Zoezi hili liliendelea huku nikihisi maumivu makali mno mwilini
hata hivyo niliendelea kushikilia msimamo wangu wa kutowaeleza chochote.
Waliendelea kunipa mateso yale na mengine zaidi kwa muda mrefu na wa￾lipoona sielekei kuwaambia chochote cha maana Kanali Bosco Rutaganda
akawaambia wale wanajeshi waniache.
“Naona umedhamiria kufa kiume Luteni, wala usijali tunayo njia nyingine
itakayokulazimisha kuongea” Kanali Bosco Rutaganda aliniambia na muda
huo nikamuona akichomoa kisu chake kiunoni.
“Mkamateni vizuri” akawaambia wale wanajeshi
“Unataka kunifanya nini? nilimuuliza kwa hofu
“Usiwe na haraka subiri utaona tu” Kanali Bosco Rutaganda aliniambia
na hapo nikawaona wale wanajeshi wakinishika vizuri, hofu ikaniingia sana
kwani sikujua ni nini walichotaka kunifanyia. Nilijitahidi kufurukuta hata
hivyo sikufanikiwa kwani nilikuwa nimeshikwa kisawasawa na hapo Kana￾li Bosco Rutaganda akaushika mkono wangu halafu kwa kutumia kile kisu
chake mkononi akaanza kunikata kidole changu cha mwisho kiganjani. Nili￾sikia maumivu makali sana huku damu nyingi ikinitoka kwenye lile jereha
mkononi, nilijitahidi kupiga mayowe lakini sikufanikiwa sana nikaambulia
kipigo.
Hatimaye kizunguzungu kilinizidi nikawa siwezi tena kuwaona watu walio￾kuwa mbele yangu mle ndani. Nikaanza kuhisi kuwa hali yangu ilikuwa
ikizidi kuwa mbaya zaidi mle pangoni, damu iliendelea kunitoka kwenye lile jeraha mkononi na nikahisi kuwa uzito wote wa mwili wangu ulikuwa ni kama
unaokielemea kichwa changu.
Nikiwa bado nimening’inia hewani nilijitahidi tena kufumbua macho yangu
bila mafanikio, nikawa nikiona giza tu mbele yangu na kwa mbali niliisikia
sauti ya Kanali Bosco Rutaganda ikiniambia.
“Tuambie Luteni vinginevyo tutaendelea na zoezi hili kwenye vidole
vingine vilivyosalia”
Nilijitahidi tena kufumbua mdomo wangu ili nimjibu hata hivyo sikufan￾ikiwa kwani fahamu zilikuwa mbioni kunitoka. Mwili wangu ulizidiwa na
maumivu makali yasiyoelezeka na sasa nikatambua kuwa mwisho wangu uli￾kuwa umefika.
Kwa mbali niliweza kuhisi kuwa ile mikono ya wale wanajeshi walionishika
ilikuwa ikiniachia taratibu na mwili wangu sasa ulianza kuwa mwepesi inga￾waje ule uzito wa kichwa na maumivu mwilini bado nilikuwa navyo. Halafu
ghafla nikawa siwezi tena kuhisi chochote mle pangoni. Fahamu zikawa zi￾menitoka.

*************


NILIJIHISI NI KAMA NILIYEKUWA umbali mrefu sana angani nikiangu￾ka kwa kasi sana kuelekea ardhini huku nikiwa nimetanguliza kichwa chini.
Picha kamili ya eneo lile nililokuwa nikielekea sikuweza kuiona na kichwa
changu kilikuwa kizito mno kama niliyefungiwa jiwe kubwa.
Mwanga hafifu uliokuwa ukipenya katikati ya kope za macho yangu nili￾yokuwa nimeyafumbua kidogo ndiyo ulionishawishi kufumbua macho yan￾gu taratibu nikiyazungusha huku na kule bila ya kufanya ishara ya mjongeo
wowote. Mbele yangu nikaona taa ya kandili iliyokuwa juu ya meza pana
yenye viti vitano vitupu nyuma yake ingawaje meza na viti hivyo niliviona ni
kama vilivyokuwa vimegeuzwa juu chini. Nikagundua kuwa fahamu zilikuwa
zikinirudia huku ile picha ya kabla sijapoteza fahamu ikianza taratibu kujik￾umbusha katika fikra zangu.
Nilikumbuka kuwa nyuma ya meza ile walikuwa wameketi maafisa wa jeshi
ambao wakati huu hawakuwepo mle ndani kwani vile viti vilikuwa wazi. Ni￾likumbuka pia juu ya meza ile kulikuwa na bastola ambayo nayo wakati huu
haikuwepo na badala yake kulikuwa na kisu kilichokuwa kimetapakaa damu.
Nikakitazama kile kisu na kukumbuka kuwa kilikuwa ni kile kisu cha Kanali
Bosco Rutaganda ambacho ndiyo kilichotumika katika kukikata kidole chan￾gu mkononi. Loh! nikahema taratibu huku nikijiuliza maafisa wale wa jeshi
pamoja na Kanali Bosco Rutaganda walikuwa wameenda wapi.
Nikiwa bado ninaendelea kuning’inia hewani huku miguu yangu na miko￾no ikiwa imefungwa kamba, nilibembea taratibu nikijizungusha nyuma yangu
ili kukagua kama kulikuwa na mtu yeyote aliyekuwa mle ndani lakini katika
mjongeo ambao usingeweza kumshtua mtu yeyote wa karibu. Ile kamba iliy￾okuwa imenining’iniza ilijizungusha taratibu kwa jitihada nilizozifanya kiasi
kwamba mtu yeyote ambaye angenitazama angeweza kudhani kuwa ulikuwa
ni mjongeo wa kawaida tu. Wakati nikijizunguka niliyatupa macho yangu
kukikagua vizuri kile chumba cha pango na hapo nikagundua kuwa kulikuwa na mwanajeshi mmoja tu mle pangoni ambaye ndiye yule aliyekuwa amesima￾ma katika ule mlango wa kuingilia mle pangoni.
Wale wanajeshi waliokuwa wakinilinda nyuma yangu hawakuwepo na hapo
nikajua kuwa hata wao walikuwa wametoka. Sasa nilibaki nikimtazama yule
mwanajeshi mmoja aliyebakia mle ndani ambaye wakati huu alikuwa ame￾zama katika kuvuta sigara kiasi cha umbali wa hatua zisizopungua tano toka
pale nilipokuwa. Bunduki yake alikuwa ameining’iniza begani huku akitem￾bea taratibu kulizunguka pango lile.
Nilifikiri na kuona kuwa hii ingekuwa nafasi pekee ninayoweza kuitumia ku￾jiokoa kabla ya wale wanajeshi wangine hawajarudi mle ndani au vinginevyo
isingejitokeza bahati nyingine kama hii. Nilijitahidi kuupima mwili wangu
kama ulikuwa na nguvu za kutosha na nikajiridhisha kuwa bado nilikuwa na
uwezo mzuri wa kupambana. Kitu pekee kilichonitia mashaka ni namna gani
ningeweza kupambana huku mikono na miguu yangu ikiwa bado imefungwa
namna ile hata hivyo sikukata tamaa.
Nikawa sasa napanga mahesabu yangu kichwani namna ya kuanza hata
hivyo nilifahamu fika kuwa kujiokoa kwangu kungetokana na kupungua kwa
umbali kati yangu na yule mwanajeshi aliyebaki mle ndani. Kilipita kitambo
kifupi mle pangoni huku nikimsubiri kwa hamu yule mwanajeshi anikaribie
pale nilipo lakini haikutokea hivyo kwani bado aliendelea kuvuta sigara yake
huku akizunguka mle pangoni taratibu katika umbali usiokuwa na msaada
wowote kwangu.
Nilipoona muda unazidi kusonga bila ya yeye kusogea karibu yangu
nikaamua nijitikise kidogo ili kumshtua. Jaribio langu likazaa matunda kwani
yule mwanajeshi akawa kama ameshtushwa na mtikisiko wangu hivyo alisi￾mama na kunitazama huku akiwa ameitoa sigara mdomoni na mimi nikatulia
bila kujitikisa tena. Yule mwanajeshi aliendelea kunitazama kwa udadisi kama
anayejishauri kitu halafu mara nikamuona akipiga hatua kuelekea mlangoni.
Nikajikuta nikikasirishwa na tukio lile kwani nilijua yule mwanajeshi aliku￾wa akienda kuwaita wenzake, niliaani sana tukio lile nikafura kwa hasira. Yule
mwanajeshi alipofika mlangoni akageuka tena kunitazama na hapo nikamuo￾na ni kama aliyejishauri kwamba aidha atoke akawaite wenzake au alitakiwa
athibitishe kwanza kuwa nimerudiwa na fahamu.
Nilimuona akiufungua ule mlango kidogo huku akinitazama halafu mara
nikamuona akiufunga tena ule mlango na kuanza kunifuata. Nikajikuta nikifu￾rahi kupata nafasi niliyokuwa nikiisubiri kwa hamu. Sasa nilikuwa na hakika
kuwa yule mwanajeshi alikuwa akija kunichuguza kwa ukaribu ili ajiridhishe
kabla ya kwenda kuwaita wenzake nami nikajiandaa kufanya shambulizi la
uhakika.
Alikuwa amebakisha umbali wa hatua moja tu kunifikia pale nilipojirusha
hewani kumrukia akawa kama aliyeshtushwa na tukio lile hivyo akataka
ageuke nyuma na kunikimbia. Chupuchupu nimkose lakini alikwisha chele￾wa kwani nilikilengesha kichwa chake vizuri ili kipite katikati ya mikono
yangu miwili iliyofungwa kwamba kwa pamoja. Mahesabu yangu yalifani￾kiwa kwani kichwa chake kiliingia katikati ya mikono yangu akataka akitoe kwa kutumia mikono yake lakini mbinu hiyo haikumsaidia kwani nilikuwa
nimefanikiwa kumbana vizuri kwa kubari moja timamu isiyoruhusu hata kasi
kidogo cha hewa kupenya kwenye kolomelo lake. Akajitahidi kufurukuta na
kutupatupa miguu huku na kule hata hivyo sikumuacha ingawaje alikuwa ni
mwenye nguvu mno.
Alipoona sina mpango wa kumuachia akaanza kunitupia ngumi usoni,
chache zikanipata nyingine nilifanikiwa kuzikwepa hata hivyo niliona endapo
hali ile ingeendelea pengine bahati ingeangukia upande wake na kufanikiwa
kuniponyoka hivyo nilikusanya nguvu tena na kujitupa naye upande mwingine
bila ya kuilegeza ile kabari na tulipojitupa upande ule nikafanikiwa kuivunja
shingo yake, kichwa chake kikalegea na hapo akaishusha chini mikono yake
taratibu huku nikiwa bado nimembana kikamilifu ili asipate nafasi ya kupiga
yowe la kuomba msaada na wakati huo nilikuwa namuomba Mungu kuwa
wale wenzake wasije wakarudi mapema mle ndani na kunikuta nikiwa bado
katika hali ile ya kuning’inia hewani kama nyama buchani.
Yule mwanajeshi alirusha miguu na mikono na hatimaye akatulia na hapo
nikajua nilikwisha maliza kazi, nikamuacha akijibwaga chini kama gunia na
mimi nikabaki nikibembea hewani taratibu. Sasa mawazo yangu yalihamia
kwenye kile kisu kilichokuwa pale juu mezani. Niliupima kwa macho urefu
wa ile kamba iliyokuwa imenining’iniza mle pangoni huku nikijiuliza kama
ingeweza kunifikisha pale juu ya meza kwenye kile kisu.
Sikuwa na uhakika sana na makadirio yangu hata hivyo sikuwa na njia
nyingine mbadala hivyo nikaanza kupunguza ule urefu kati yangu na ile meza
yenye kile kisu kwa kubembea taratibu kutoka upande huu kwenda ule. Mwen￾do ulipochanganya vizuri nikagundua kuwa ile kamba ilikuwa fupi kidogo
hivyo palihitajika jitihada nyingine kukifikia kile kisu juu ya meza. Niliende￾lea kuchochea mwendo kasi wa ile kamba na hatimaye nikawa nimekikaribia
kile kisu hivyo nikawa nikienda na kukigusagusa pasipo kupata nafasi nzuri
ya kukichukua. Zoezi hili likaanza kunikatisha tamaa kwani kile kisu nilikuwa
nikikigusa pasipo kupata nafasi nzuri ya kukichukua kiasi kwamba kilikuwa
kikisogea mbele zaidi. Nilirudiarudia zoezi lile bila ya mafanikio na hatimaye
nikapata wazo jipya.
Nilipoenda kwa mara nyingine sikujishughulisha na kile kisu badala yake
niliishika pembe ya meza ile na kuivuta kidogo ile meza hivyo nikawa nikien￾da kwa kupunguza umbali wakati huo huo nikiomba ile sauti hafifu ya mburu￾to wa meza isije ikasikika. Mwishowe nikafanikiwa kuisogeza ile meza karibu
na kukichukua kile kisu mezani, nikakishika kwa kiganja changu cha mkono
wa kulia na kuanza kuzikata haraka zile kamba za mikononi. Nilipomaliza ni￾kajipinda na kuishika ile kamba iliyoning’iniza miguu yangu na hapo nikaanza
kuikata kwa haraka huku mara kwa mara nikigeuka kuutazama ule mlango
wa pango ili kujua kama kulikuwa na mtu yeyote aliyekuwa akija. Hali bado
ilikuwa poa tu na hapakuwa na mtu yeyote.
Nyuzi ya mwisho ya kamba ile nilipoikata ilinifanya nianguke ardhini kama
fuko la maembe hata hivyo nilikuwa makini sana nikitua kama paka pasipo
kutoa sauti yoyote ya kishindo. Nilikuwa kama niliyepata nguvu na roho mpya huku nikiyapuuza yale maumivu makali mwilini mwangu. Niliichomoa ile
misumari niliyogongelewa mwilini na hapo nikasikia maumivu makali sana
huku damu nyingi ikinitoka kwenye majeraha yale.
Nilipojaribu kupiga hatua kutembea mara ya kwanza nilishindwa na kupiga
mweleka hata hivyo niliposimama tena nikahisi nguvu mpya mwilini na kile
kizunguzungu kilikuwa kimeanza kupungua ingawaje kichwa bado kilikuwa
kizito na kikiuma sana.
Nilimsogelea yule mwanajeshi kwa tahadhari na nilipomfikia nikajua
asingeweza kuamka tena hivyo nikaichukua ile bunduki yake na ile kurunzi
aliyokuwa akiibeba kiunoni mwake, nilipompekua nikazipata funguo za ule
mlango wa kutokea nje ya pango. Nilipata wazo kuwa isingefaa kuondoka
mle ndani pasipo kuzikagua zile droo za ile meza hivyo nilikatisha katikati ya
kile chumba kuiendea ile meza na nilipofika nikaanza kuzifungua zile droo na
kuanza kupekua, mara nikawa nimeipata ile bastola ambayo ilikuwa juu ya
meza pamoja na kitabu kidogo ndani ya droo zile.
Ni wakati huu nilipogutuka kuwa nilikuwa uchi nikawaza kuwa nisingeweza
kutoka mle ndani nikiwa katika hali ile hivyo nikamkumbuka yule mwanajeshi
niliyemuua mle ndani. Sikutaka kupoteza muda haraka nikamrudia na kumvua
nguo zake ambazo nilizivaa kwa haraka isiyoelezeka ili nisije nikachelewa
na kukutwa mle ndani. Urefu wake na wangu ulikuwa ukilingana hivyo mag￾wanda yake yalinienea vizuri na nilipomaliza nilimvua na buti zake miguuni
na kuzivaa. Sasa nilijihisi kuwa nilikuwa tayari kutoka mle pangoni ingawaje
wasiwasi bado nilikuwa nao juu ya zile njia za kutokea nje ya mapango haya
ambazo zilikuwa ni zenye kona na makutano mengi kiasi kwamba kwa mtu
yeyote mgeni angejikuta akizunguka na kurudi alipotoka bila kujijua.
Nilikuwa tayari nimekwishaufikia mlango wa kutoka nje ya chumba kile
cha pango wakati niliposikia sauti hafifu ikiita nyuma yangu.
“Patrick…Patrick, usiniache” ile sauti ilirudia tena kusisitiza nikatazama
nyuma na kugundua kuwa ilikuwa akitokea kwenye ile sehemu ya pango ili￾yokuwa na giza.
“Wewe ni nani? niliuliza kwa hofu huku nikiona kero kwa mtu yule kwani
ni kama aliyekuwa akinichelewesha kuondoka mle pangoni.
“Ni mimi Jérome,…Jérome Muganza tafadhali usiniache”. Ile sauti ilisisiti￾za na hapo nikajikuta nikiikumbuka ile miili ya wale watu wawili iliyokuwa
imening’inizwa kwenye lile eneo lenye giza mle pangoni. Nikaiwasha ile ku￾runzi kumulika na hapo nilikutana na sura ya mtu iliyotaabika ikinitazama kwa
matumaini. Kama si kuikumbuka vizuri ile sura yake nisingeweza kujiridhi￾sha kirahisi kuwa mtu yule alikuwa ndiye yule Jérome Muganza, mmiliki wa
magazeti la République na mateka mwenzangu niliyekuwa naye kule pangoni
kwani mwili wake wote ulikuwa umetapakaa damu.
“J’erome!, ni wewe? nilimuuliza kwa furaha huku nikishindwa kuamini ma￾cho yangu.
“Ni mimi Patrick njoo uniokoe haraka watarudi sasa hivi na kutukuta humu
ndani” yule mtu alinisisitiza na sikutaka kupoteza muda tena nikamfuata na
kuikata ile kamba iliyokuwa imemning’iniza juu kisha nikamshusha chini taratibu na kuzikata zile kamba nyingine alizofungwa miguuni na mikononi
kwa msaada wa kile kisu nilichokichukua juu ya ile meza iliyokuwa mle
ndani. Nilipomchunguza vizuri nikagundua kwa alikuwa na majeraha makub￾wa ya mapanga mwilini isipokuwa sehemu za kichwani tu na hilo likanitia
moyo kuwa angekuwa na unafuu kidogo ingawaje alikuwa amepoteza damu
nyingi sana.
“Utaweza kutembea? nilimuuliza.
“Ndiyo” alinijibu ingawaje nilipomchunguza vizuri nilifahamu kuwa
isingekuwa rahisi kwake kutembea kama alivyodhani.
“Nilidhani ungekuwa umeuwawa Jérome”
“Ndiyo bila shaka ningekuwa nimeuwawa kwani nilipowaona wanazidi
kunichabanga mapanga ikabidi nijidai nimekufa, nafikiri hicho ndicho kili￾chowafanya waniache”
“Kwa hiyo uliniona wakati nilipokuwa nikiletwa humu ndani na kuteswa?
“Nilikuona na kwa kweli nilikata tamaa sana kwani sote mle pangoni tuli￾kuwa na imani kuwa ni wewe tu ndiye ambaye ungeweza kutuokoa. Nilikuwa
nikiona kila kitu ulichokuwa unafanyiwa humu ndani hata hivyo sikutaka hata
kujitingisha kwani kwa kufanya hivyo wangenishtukia kuwa bado mzima na
hivyo wangenimalizia kabisa” Jérome Muganza alikuwa akiongea huku akit￾weta kwa hofu.
“Usijali rafiki yangu sasa upo salama Mungu wako amekuokoa. Na huyu ni
nani? nilimuuliza huku nikiumulika ule mwili wa yule mtu mwingine pembeni
yake.
“Simfahamu, nilimkuta humu ndani akiwa katika hali hiyohiyo bila shaka
atakuwa amekufa”
Nilimsogelea yule mtu na kumtingishatingisha hata hivyo hakuonesha is￾hara yoyote ya uhai, nikamchunguza vizuri na kugundua kuwa alikuwa tayari
amekufa.
“Tuondoke humu ndani Patrick wale watu watarudi sasa hivi” Jéremo
Muganza alinisisitiza
“Wameenda wapi? nilimuuliza
“Nilimsikia yule afisa aliyekuwa akikuhoji wewe akiwaaga wale wanajeshi
wengine kuwa alikuwa akiwasindikiza wale maafisa wa jeshi wa kizungu na
kuwa angerudi muda si mrefu ili aendelee kukuhoji wewe mpaka hapo utaka￾pozungumza kile anachokihitaji kwako”
Niligeuka kumtazama Jérome Muganza kisha nikatabasamu huku niki￾yaamini maneno yake kwani wakati wale maafisa walipokuwa wakiondoka
mimi nilikuwa bado nimepoteza fahamu. Muda uleule nikaunyanyua mkono
mmoja wa Jérome Muganza na kuuweka begani nikimsaidia kutembea, sasa
tukawa tukielekea kwenye ule mlango wa kutokea nje ya kile chumba cha
pango. Moyoni nilikuwa nimefurahi sana kukutana tena na Jérome Muganza
akiwa hai kwani bado angekuwa msaada mkubwa kwangu katika kutoroka
katika mapango haya kwa kuzingatia kuwa ni yeye tu ndiye aliyekuwa akizi￾fahamu vizuri njia zote za mle ndani.
“Nashukuru sana Patrick” aliniambia nami nikatikisa kichwa kukubali shukrani zake nikiendelea kumkokota huku mkono wangu wa kushoto am￾bao ndiyo niliokuwa nimemuegemeza Jérome Muganza ukiwa ameshika ile
kurunzi na mkono wangu wa kulia akiwa umeishika vema ile bunduki niliy￾opora kwa yule askari niliyemuua huku nikiwa tayari kufanya shambulizi lo￾lote mbele yangu. Tulipoufikia ule mlango wa kile chumba nilipachika funguo
kwenye kitasa na kuufungua na hapo niligeuka kumtazama Jérome Muganza,
nikamuona ni kama aliyekuwa akisita kuendelea na safari.
“Vipi? nilimuuliza
“Kuna watu wanakuja” aliniambia na hapo nikayatega masikio yangu
kusikiliza vizuri, kwa mbali nilisikia mwangwi hafifu wa sauti za watu walio￾kuwa wakija upande wetu, nikajua kwa vyovyote wangekuwa ni wale wanajes￾hi wakirudi mle ndani. Nikapiga mahesabu ya haraka haraka na kuona kuwa
tusingeweza kufika mbali kabla ya watu wale hawajatufikia endapo tungea￾mua kutoka mle ndani kwani zile njia za pango zilikuwa nyembamba sana
na ingekuwa rahisi sana kwetu kushambuliwa. Hivyo nikafanya maamuzi ya
haraka ya kurudi mle ndani ya pango ingawaje Jérome Muganza hakuonekana
kuafikiana haraka na wazo langu.
Tulirudi ndani ya pango lile haraka sana huku nikimkokota Jérome Mugan￾za na kwenda kumficha kule sehemu yenye giza mle pangoni. Sauti za wale
watu zilizidi kusikika na kabla hawajafika mle ndani nilikimbia haraka na
kwenda kuiburuta ile maiti ya yule mwanajeshi niliyemuua mle pangoni na
kwenda kuificha nyuma ya ile meza ya mle ndani kisha nikabanisha nikisubiri.
Zile sauti ya maongezi ya wale watu sasa ilikuwa imeongezeka ijapoku￾wa sikuweza kufahamu walikuwa wakizungumzia nini kutokana na lugha
yenyewe ya kinyarwanda waliyokuwa wakiizungumza ambayo mimi nilikuwa
siifahamu. Muda mfupi uliofuata niliuona ule mlango wa pango ukifunguliwa
kisha mwanajeshi mmoja mrefu mwenye mwili uliojengeka vizuri alisimama
pale mlangoni halafu akawa ni kama anayesita kuingia baada ya kushtukia
mabadiliko ya hali fulani ya mle ndani.
Toka kwenye maficho yangu mle ndani nilimchunguza vizuri mtu yule
nikamkumbuka kuwa alikuwa miongoni mwa wale wanajeshi wawili walio￾kuwa wakinilinda nyuma yangu kipindi kile nilipokuwa nikihojiwa na Kanali
Bosco Rutaganda.
“Vipi? mwenzake alimuuliza kwa nyuma alipomuona anasita kuingia mle
ndani
“Subiri kwanza”
“Kwani kuna nini? mwenzake aliuliza tena huku akijipenyeza pembeni yake
kutazama mle ndani.
“Wakati ulipokuwa ukitoka humu ndani ulimuacha Koplo Karazama? yule
mwanajeshi wa kwanza kuingia alimuuliza mwenzake huku akionesha masha￾ka.
“Ndiyo, niliwaacha yeye na yule mateka” mwenzake alijibu kwa wasiwasi
huku akikikagua vizuri kile chumba kwa taharuki.
“Sasa mbona hayupo na yule mateka mbona simuoni?, una hakika ulimua￾cha humu ndani wewe?
“Kwani si tuliondoka pamoja japokuwa mimi ndiye niliyefunga mlango”
“Acha upumbavu wewe sasa mbona watu wote hawapo? mwenzake alifoka
huku akiendelea kutazama mle ndani. Ukimya kidogo ukafuatia na hapo nikaf￾ahamu kuwa walikuwa wakifanya tathmini ya hali ya mle ndani huku macho
yao yakizunguka kutazama kila mahali
“Au pengine atakuwa amemhamishia kwenye kile chumba kingine”
“Labda lakini kwa sababu gani?
“Hebu nenda katazame” yule mwanajeshi mmoja alipoondoka nilimuona
yule mwanajeshi aliyebaki akinyata taratibu kuiendea ile kamba iliyokuwa iki￾ning’inia ambayo hapo awali nilikuwa nimening’inizwa mimi kwa juu. Wakati
akielekea ilipo ile kamba yule mwanajeshi akaichomoa bastola yake kiunoni.
Alipofika pale ilipokuwa ile kamba akaanza kuchunguzachunguza, namna ya
ile kamba kuonekana imekatwa kwa juu bila shaka ilimshtua sana kwani muda
uleule yule mwanajeshi akageuka kutazama juu ya ile meza ambayo mimi
nilikuwa nimejificha kwa nyuma na ile maiti ya yule kwa majeshi mwingine,
nikajua pengine alikuwa akikikumbuka kile kisu kilichokuwa juu ya meza ile.
Mimi sikumkawiza kwani alikuwa akija kwenye uelekeo mzuri nilioutaka, ni￾likuwa nimejiandaa vizuri na toka pale nilipojificha nilikichukua kile kisu am￾bacho wakati huu nilikuwa nimekichomeka katika mkanda wa suruali yangu.
Mchezo wa shabaha ya visu ulikuwa ni mchezo niliyoupenda na kuuche￾za vizuri wakati wote nilipokuwa jeshini hivyo ilikuwa ni kazi rahisi sana
kwangu. Nilikishika vizuri kile kisu upande wa makali kisha nikakizungusha
mkononi mara tatu kabla ya kukifyatua hewani. Ilikuwa ni shabaha nzuri sana
kwani kile kisu kilipenya na kuzama katikati ya shingo ya yule mwanajeshi na
sehemu ya mpini tu ikabaki kwa nje. Nikamuona namna alivyoshikwa na taha￾ruki na macho yamemtoka huku mkono wake wa kushoto ukiwa umeushika
ule mpini wa kisu ambao sasa ulikuwa umetapakaa damu kila mahali akijaribu
kukichomoa kisu kile bila mafanikio.
Alikuwa tayari ameniona hivyo ule mkono wake ulioshika bastola
akaunyanyua na kuulekezea kwangu hata hivyo hakufanikiwa kunilenga
kwani nilikuwa tayari nimekwishamfikia. Nikaupiga teke ule mkono wake
na ile bastola aliyoishika ikapaa hewani lakini kwa bahati mbaya sana ule
mtikisiko ukapelekea risasi kufyatuka na kuchimba ardhini hata hivyo niliwa￾hi kuidaka ile bastola kabla haijafika chini. Hata hivyo nilikuwa na wasiwasi
sana kwani ule mlio wa risasi ungeweza kumshtua mtu yeyote ambaye an￾gekuwa jirani na eneo lile na mimi sikupenda hilo litokee kwani siri yetu ya
kutoroka ingeweza kugundulika mapema. Wakati haya yakiendelea nilifaha￾mu fika kuwa macho ya Jérome Muganza yalikuwa kule gizani yakinitazama
na sikufahamu alikuwa akiichukuliaje hali ile.
Yule mwanajeshi alianguka chini kama gunia nikamuwahi kumziba mdomo
huku nikimkandamiza chini kwa mikono yangu na hapo akafurukuta kidogo
na kutulia. Muda uleule nikamburuta na kumficha kule nyuma ya ile meza ki￾sha nikabanisha gizani na kisikilizia. Sekunde chache baadaye yule mwenzake
alirudi na kuingia mle ndani huku akitweta kwa hofu, akaanza kuita
“Afande Nzeymana!”
Yule mtu aliendelea kuita kwa muda mrefu na alipoona kuwa haitikiwi aka￾simama na kuanza kutazama mle ndani na hapo niliweza kuusoma uso wake
namna ulivyokuwa umejawa na hofu na wasiwasi mwingi. Aliendelea kumuita
mwenzake kisha akaweka kituo kabla ya kuendelea “Afande Nzeymana!...”
aliendelea kuita halafu bila kusikiliza kuwa alikuwa akiitikiwa au lah! kisha
niliyaona macho yake yakitazama mle ndani sakafuni.
Niliyazungusha macho yangu kutazama pale alipokuwa akitazama nikagun￾dua kuwa alikuwa akiitazama ile damu ya mwenzake ambaye nilikuwa ni￾meishamalizanaye muda mfupi uliyopita. Ile damu kutoka kwenye lile jeraha
la kile kisu la yule mwenzake ilikuwa imesambaa kidogo pale chini hivyo
nilimuona akiikamata vizuri bunduki yake mkononi huku akinyata taratibu
kuisogolea vizuri ile damu. Alipoifikia karibu ile damu akaichunguza kidogo
na kuanza kuzitupa hatua zake hafifu kuifuatilia kule ilipoelekea hata hivyo
hakufika mbali pale alipoinua macho yake na kujikuta akitazamana na mtutu
wa bastola yangu, loh! niliweza kuiona taharuki usoni mwake.
“Weka chini bunduki yako” nilimwambia huku akiwa bado haamini macho
yake na kwa msisitizo zaidi nikavuta kilimi cha bastola yangu na kuiruhu￾su risasi moja kukaa kwenye foleni tayari kufyatuka. Kusikia vile tu jamaa
akaiangusha chini bunduki yake bila kupenda.
“Rudi nyuma hatua tatu” nilimwambia tena na bila ubishi akafanya kama
nilivyomuagiza. Sasa nikawa nimepata nafasi ya kuiokota ile bunduki yake
na kusimama
“Kanali Bosco Rutaganda yupo wapi? nilimuuliza kwa hasira
“Amewasindikiza wageni”
“Atarudi muda gani?
“Hakutuambia” alinijibu katika sauti iliyojaa hofu na kitetemeshi
“Mko wangapi humu ndani?
“Wengi tu ila hatuonani kwani kila mmoja anashughuli yake aliyopangiwa”
“Nani aliyetoa amri ya kukamatwa kwa watu na kuja kufichwa humu pan￾goni?
“Sijui ila sisi huwa tunapokea amri zote toka kwa Kanali Bosco Rutaganda”
“Wale wazungu wanamahusiano gani na Kanali Bosco Rutaganda?
“Ni marafiki zake” yule mwanajeshi alinijibu hata hivyo nilipomtazama
nilimshtukia kuwa alikuwa akiichomoa bastola yake aliyokuwa ameisunda
nyuma kiunoni na sikumpa nafasi kwani muda uleule nikabonyeza kilimi cha
bastola yangu na risasi moja iliyotoka ikamzoa na kukifumua vibaya kichwa
chake alipotua chini alitulia kimya na mimi nikageuka kule gizani na kuanza
kuita.
“Jerome…Jerome…!” muda uleule nikamuona Jérome Muganza akitoka
kule mafichoni huku akiwa anashindwa kuamini mambo yaliyotokea mle
ndani. Bila shaka alikuwa amepumbazika kwa kunishangaa mimi namna
nilivyokuwa nimeyasawazisha mambo kiulaini na kwa muda mfupi. Nilim￾wambia Jérome Muganza amvue maiti mmoja nguo zake na azivae naye akaf￾anya haraka kama nilivyomuagiza na wakati akivaa zile nguo mimi nilikuwa
nikizikusanya zile silaha zote mle ndani pamoja na kukichomoa kile kisu toka shingoni mwa yule mwanajeshi. Katika muda mfupi tu tukawa tupo tayari
kikitoroka chumba kile na zile silaha zote nilizibeba kwani sikuwa nafahamu
kuwa hali ya huko mbele ingekuwaje.
__________
TULITOKA NJE YA CHUMBA KILE NA KUKIFUNGA, niliutazama ule
uelekeo tuliokuja nao hapo awali na sikutaka turudi tena na njia ile kwani
tungeweza kukutana na hatari yoyote. Jérome Muganza alinionesha njia
nyingine ambayo tungeweza kuitumia ijapokuwa ilikuwa imeachwa kutumika
kwa muda mrefu kutokana na kujawa na majani mengi mle ndani, nikaafiki￾ananaye kwani yeye ndiye aliyekuwa akivielewa vizuri vichororo vya mle
ndani.
Tuliambaa na korido fupi ya pango lile na mbele kidogo tulikutana na njia
nyingine iliyokatisha mbele yetu, tukaifuata njia hiyo kwa upande wa kushoto
huku Jérome Muganza akiwa ametangulia mbele na mimi nyuma yake. Nilim￾uuliza kama alikuwa akifahamu kutumia silaha akaniambia kuwa alikuwa ha￾fahamu nikaona angekuwa mzigo kwangu kwani kwa rika lake vijana wengi
wa nchini Tanzania walikuwa wakifahamu kutumia silaha kutokana na kupi￾tia mafunzo ya mgambo ambayo yalikuwa ni lazima kwa mfanyakazi yeyote
kuyapitia kabla ya kuajiriwa hata hivyo sikuwa na jinsi.
Tuliendelea na safari yetu taratibu na kwa tahadhari huku mara kwa mara
nikigeuka nyuma kutazama kama tulikuwa tukifuatiliwa au lah!, wakati fu￾lani nilimsimamisha Jérome Muganza pale nilipohisi kuwa tulitapaswa kuli￾chunguza kwa tahadhari eneo tulilokuwa tukilipita. Tulikutana na kona nyingi
sana mle pangoni lakini nilishangaa kumuona Jérome Muganza akizifahamu
vizuri kona zote mle pangoni na mwishowe tukawa tumefika sehemu fulani
kulipokuwa na jabali kubwa. Tulipofika hapo niliweza kusikia sauti ya maji
yaliyokuwa yakipita sehemu ya chini ya eneo lile.
Tulikuwa ndiyo tunalikaribia vizuri lile jabali pale nilipoona kivuli cha
mtu kikitujia mbele yetu, nikawahi kuizima ile kurunzi na kumtaka Jérome
Muganza atulie. Mpaka wakati huu tulikuwa tumechoka sana kwani zile njia
za mle pangoni kwa sehemu kubwa zilikuwa nyembamba sana zinazoruhusu
mtu mmoja tu kupenya kwa kulalia tumbo katika umbali tofauti. Nilimuona
Jérome Mugaza kama aliyekuwa ameanza kubabaika baada ya kumuona yule
mtu mbele yetu akija nikawahi kumbana kwa nguvu mkono wake kuwa atulie.
Akanisikia na kubanisha pembeni yangu ingawaje niliyasikia mapigo ya moyo
wake namna yalivyokuwa yakihangaika hovyo na hapo nikamshika kifuani na
kumtuliza. Muda huohuo yule mtu alitupita karibu bila ya kutushtukia huku
akiwa na bunduki yake begani na ndoo ya maji mkononi nikajua kuwa alikuwa
akitoka kuteka maji kule chini ya jabali.
Tuliendelea kujibaza ile sehemu mpaka yule mtu alipopotea kwenye kona
nyingine iliyokuwa nyuma yetu upande wa kulia na hapo nikampa ishara
Jérome Muganza kuwa tuendelee na safari yetu. Sasa tulikuwa tukienda kwa
tahadhari kubwa sana kwani tulifahamu kuwa tulikuwa tupo karibu sana na makazi ya askari wa Kanali Bosco Rutaganda. Na wakati tukiendelea na safari
mimi bado akili yangu ilikuwa ikiwaza kule nyuma tulipotoka kuwa ungepita
muda gani mpaka kushtukiwa kutoroka kwetu, na Kanali Bosco Rutaganda
angetaharuki vipi pale ambapo angeambiwa kuwa mateka wake wametoroka.
Nilifahamu fika kuwa Kanali Bosco Rutaganda asingekubali kushind￾wa kirahisi hivyo kwa vyovyote angewapanga wanajeshi wake katika kila
kona ya mapango haya akihakikisha kuwa hatufanikiwi kutoroka na tunaka￾matwa mapema na kurudishwa tena kwenye himaya yake. Hata hivyo hilo
nisingekubaliana nalo asilani kwani nilifahamu kuwa endapo tungekamatwa
tena adhabu yetu ingekuwa kifo na kuliko kuuwawa kinyama na Kanali Bo￾sco Rutaganda ingekuwa ni afadhali nijiue mimi mwenyewe lakini pia kabla
ya kufikia hatua hiyo ningemuonesha Kanali Bosco Rutaganda kuwa mimi si
mwanafunzi bali bado nilikuwa mwalimu wake wa kijeshi tena niliyehitimu
vizuri katika medani za kijasusi, iwe porini au mjini, mapangoni au jangwani.
Kila mara Jérome Muganza alikuwa akigeuka nyuma kunitazama bila ya
kusema neno ingawaje tulikuwa hatuonani vizuri kutokana na giza zito la
mle pangoni. Zile kelele za maporomoko hafifu ya maji nilikuwa nikiende￾lea kuzisikia ingawaje bado sikuweza kujua kuwa yale maji yalikuwa eneo
gani katika ile sehemu. Tulifika mbele eneo fulani tukaingia katika uchochoro
mwembamba wenye mwamba wa chokaa, tukawa tukipita kiubavu ubavu na
pale tulipoona panatatiza niliwasha kurunzi kidogo kumulika na kisha kuizima
na safari ikaendelea, sikutaka kuitumia sana ile kurunzi japokuwa mle ndani
kulikuwa na giza zito.
Tulipoupita ule mwamba wa chokaa tukawa tumetokezea eneo lililokuwa na
makutano ya njia tatu za pango, njia moja upande wa kushoto ya pili upande
wa kulia na ya tatu mbele yetu. Tulipofika pale nilimuona Jérome Muganza
akisita kidogo na hapo nikajua kuwa kwa vyovyote alikuwa akijaribu kuzi￾kumbuka vizuri njia zile nami sikutaka kumuingilia kwenye maamuzi yake
hivyo nikamuacha aitulize vizuri akili yake na kufikiri vizuri ili aweze kui￾chagua njia iliyo sahihi. Baada ya muda mfupi akawa amekumbuka vizuri,
nikamuonna tena akigeuka kunitazama, safari hii alinitazama kwa muda kido￾go kisha akaanza kuifuata ile njia ya upande wa kulia nami ikabidi nimfuate
kwa nyuma ingawaje nilianza kupatwa na wasiwasi juu ya namna Jérome
Muganza alivyokuwa akigeukageuka nyuma kunitazama.
Tulitembea kidogo kwa kuinamainama na baada ya kitambo kirefu cha safa￾ri yetu tukatokezea kwenye njia pana zaidi lakini iliyokuwa na vipango vingi
vidogovidogo vyenye ncha kali lakini hatukupata shida sana kutokana na zile
buti ngumu za kijeshi tulizovaa miguuni. Tulipofika mbele kidogo tukatokezea
kwenye uchochoro mwingine mwembamba ulituhitaji kupita katika mtindo wa
kulala chini na kutambaa. Uchochoro huo ulikuwa unaelekea sehemu ya chini
zaidi ya mapango yale na kwa mbali niliweza kuyasikia tena yale makelele ya
maji yaliyokuwa yakitiririka sehemu fulani katika eneo lile.
Lakini kabla ya kuanza safari katika kichochoro kile nilimuona Jérome
Muganza akigeuka tena nyuma kunitazama kama alivyokuwa akifanya kule
nyuma. Kwa kweli nilishindwa kumuelewa kuwa alikuwa akimaanisha nini kufanya vile wakati mle ndani kulikuwa giza zito na tulikuwa hatuonani hata
hivyo nilipiga moyo konde na kumpuuza huku tukiendelea na safari yetu. Tu￾lishuka chini ya mapango yale kwa namna ileile ya kutambaa kisha tukapin￾da kona kushoto na hapo tukawa tumetokezea eneo kama lile lakini kwenye
pango jingine lililokuwa chini lakini fupi sana lisilomruhusu mtu kupita akiwa
anatembea na yenye matope mazito. Tuliserereka na kuingia kwenye lile tope
na kuzama nusu ya kiwiliwili na hapo niliyasikia vizuri yale makelele ya maji
kuwa yalikuwa karibu sana na pale tulipokuwa.
Na kwa mara ya kwanza nilimsikia Jérome Muganza akiniambia kuwa eneo
lile lilikuwa na popo wakubwa na wakali mno wajulikanao kwa lugha ya ki￾taalamu kama hysignathus Monstrosus hivyo alinitaka niwe makini sana nami
nikatingisha kichwa kumuonesha kuwa nilikuwa nimemuelewa na hapo aka￾geuka kunitazama tena kisha akageuka mbele na hapo tukaanza tena kuende￾lea na safari yetu. Nilikuwa nimemwambia Jérome Muganza kuwa tulitakiwa
kurudi kwanza kule pangoni walipofungwa wenzetu ili tukawaokoe halafu
baada ya hapo ndiyo tungetoroka kwa pamoja. Hivyo kwa mujibu wa maelezo
yake njia ile ndiyo iliyokuwa njia rahisi na ya kificho ya kuweza kutufikisha
kule pangoni walipofungwa wenzetu.
Ile sehemu ya chini ya pango tulikotokezea ilikuwa na matope mazito
yenye utelezi mkali ya udongo mfinyanzi na ilikuwa ni shida sana kutem￾bea hivyo mwendo wetu ulikuwa umepungua sana na kama ingetokea kuwa
Jérome Muganza angeniacha pale angekuwa ameniweza sana kwani nilikuwa
nimeshapoteza ramani yote ya kule tulipotoka na sikuwa na ramani ya kule
tunapokwenda na pale tulipokuwa sikufahamu tulikuwa eneo gani japokuwa
Jérome Muganza alikuwa ameniambia kuwa tulikuwa tumeukaribia mrefe￾ji mkubwa wa maji uliokuwa mle pangoni. Na kwa mujibu wa maelezo ya
Jérome Muganza ni kuwa kwa kuutumia mfereji huo ndiyo ambao ungetusa￾firisha moja kwa moja hadi karibu na lile pango walikofungwa wale wen￾zetu huku akidai kuwa mfereji huo ulikuwa ni miongoni mwa mifereji mingi
inayotoka kwenye chemi chemi za mapango haya kuelekea bonde la ufa la
Albertine.
Sikuwa na saa yangu ya mkononi lakini niliweza kukisia kuwa tulikuwa
tumetembea katika lile tope zito katika muda usiopungua nusu saa na wakati
huo miguu na viungo vyote mwilini vilikuwa vimeanza kuchoka kutokana na
kutumia nguvu nyingi katika kutembea katika matope yale mazito. Kona moja
tu ilikuwa imesalia mbele yetu kabla ya kuufikia ule mfereji mkubwa wa maji
pale nilipomuona Jérome Muganza mbele yangu akisita kuendelea na safari na
mara hii hakugeuka tena kunitazama kama alivyokuwa akifanya kule nyuma
isipokuwa nilimuona akisimama kwa ghafla sana huku akiangalia kule mbele.
Nikashikwa na wasiwasi na kumuuliza
“Mbona umesimama, kuna nini?
“Kuna kitu fulani pale mbele” alinong’ona na hapo nikasogea vizuri kutaza￾ma kule mbele hata hivyo sikuona chochote.
“Mbona sioni kitu”
“Tazama vizuri pale mbele upande wa kushoto” aliniambia kwa sauti ya kunong’ona na hapo nikayakaza vizuri macho yangu kutazama kwa makini
kule mbele hata hivyo bado sikuona chochote.
“Sioni chochote” nilimwambia Jérome Muganza huku nikigeuka kumtaza￾ma hata hivyo Jérome Muganza hakunijibu kitu badala yake aliendelea kusi￾mama huku akitazama kule mbele katika namna ya hofu na wasiwasi. Nili￾pomchunguza vizuri nikajua kuwa alikuwa ameanza kutetemeka kwa hofu na
hapo nikaanza kushikwa na wasiwasi. Niliacha kumtazama Jérome Muganza
nikageuka tena kutazama kule mbele alipokuwa akitazama na mara hii niliwe￾za kuona alichokuwa akikitazama.
Kiasi cha umbali mfupi tu toka pale tulipokuwa mbele yetu, kiumbe kikub￾wa cha ajabu chenye upana unaofanana na ule wa gogo la mti kubwa lenye
urefu usiojulikana kilikuwa kimegeuka kututazama au pengine kutushangaa
kama sisi tulivyokuwa tukikishangaa. Tofauti iliyokuwepo baina yetu na ki￾umbe kile ni kuwa sisi tulikuwa hatujiwezi kwa hofu wakati chenyewe ni
kama kilikuwa kikitabasamu lakini vilevile kikijuliza kama tulikuwa tumeko￾sea njia au tulikuwa tumedhamiria kupita pale alipokuwepo. Na hapo nikafa￾hamu nini kwani Jérome Muganza alikuwa akitetemeka vile.
Lilikuwa joka kubwa sana ambalo sikupata kuwahi kuliona sehemu yoy￾ote duniani wala kwenye picha yoyote. Katika muda wa sekunde moja tu
tangu nilione joka lile mbele yetu nilihisi damu yangu ilikuwa ikichemka
isivyokawaida mwilini, jasho nalo lilikuwa limeanza kunitoka kila sehemu
mwilini ingawaje mle ndani ya pango kulikuwa na baridi kali. Mate yalikuwa
yakinikauka haraka mdomoni na ni kama mapigo elfu moja ya moyo wangu
yaliyokuwa yamesafiri katika nukta moja tu ya sekunde.
Lile joka lilikuwa limetuona na lilikuwa likijizungusha taratibu kututaza￾ma vizuri, sikuweza kuliona vizuri lakini ukubwa wa kichwa chake ulikuwa
ukifanana na ukubwa wa kichwa cha simba dume na kichwa chake kiliku￾wa chenye umbo bapa na chenye mifupa imara ya taya lake. Nilikuwa niki￾wafahamu vizuri nyoka wengi jamii ya chatu kwani niliwahi kukutana nao
maporini katika harakati zangu lakini nilikataa kulifananisha joka lile na chatu
kutokana na umbo la kichwa chake lilivyokuwa kama jeneza, rangi ya ngozi,
umbo na macho yake.
Nyoka wote wasiokuwa na sumu nilikuwa nikiwafahamu vizuri kwa tabia
moja tu kubwa, macho yao yalikuwa na kiini chenye umbo la uviringo katikati
na wenye tabia ya kulizuia na kulirukia windo lao kwa kulibana mpaka pale
linapoishiwa pumzi ndiyo huanza kulimeza taratibu, lakini joka hili halikuwa
na tabia za awali zilizokuwa zikifanana na hizo. Nililitazama joka lile nikayao￾na macho yake makubwa na makali yalivyokuwa yakimeremeta katika namna
ya ajabu na hapo nikagundua kuwa lilikuwa ni aina ya joka lenye sumu kali
sana kwani macho yake hayakuwa na kiini chenye umbo la uviringo kama
wale nyoka wengine wasio na sumu bali macho yake katikati yalikuwa na kiini
chenye umbo linalofanana na ile alama ya kisu iliyopo kwenye karata.
Matundu ya pua yake yalikuwa makubwa kama matundu ya pua ya binada￾mu na sehemu ya mbele ya mdomo wake ilikuwa pana na iliyogawanyika
katika mafungu ya sehemu kuu nne. Rangi ya ngozi yake ilikuwa na mabakamabaka kama ya kombati ya jeshi na rangi hiyo ilikuwa na mstari mpana
wa rangi ya njano uliyoizunguka shingo yake kama ushanga. Sehemu ya kiwi￾liwili chake ilikuwa imebakia kwenye upande mwingine wa pango. Sasa joka
lile kubwa la ajabu linalotisha lilikuwa likijisogeza taratibu kututuzama huku
likifoka na kutoatoa nje ulimi wake mkubwa na mrefu uliotengeneza pacha
sehemu yake ya mbele.
Sikutaka kugeuka nyuma kwani nilifahamu fika kuwa kwa kufanya hivyo
kungeweza kulishawishi lile joka lifanye maamuzi ya haraka ya kutushambu￾lia hivyo niliyazungusha macho yangu taratibu na kumtazama Jérome Mugan￾za aliyekuwa pembeni yangu na hapo nikamuona kuwa alikuwa amefikia
kwenye kiwango chake cha mwisho cha hofu. Roho yake ni kama ilikuwa
tayari imekwishajitenga na mwili na hivyo alikuwa tayari chochote kitokee
kwani hakuwa na tumaini jengine la kutoka na ushindi mbele ya joka lile
lililoonekana kutokuwa na mazoea hata kidogo na binadamu.
Kwa sekunde chache ni kama akili yangu ilikuwa imepigwa na ugonjwa wa
kiharusi na kushidwa kufanya kazi yake kwa usahihi. Niliona ni kheri ninge￾pambana na Kanali Bosco Rutaganda ambaye ni binadamu kama mimi kuliko
kupambana na kiumbe kile. Nilikatishwa tamaa na mambo makubwa mawili
katika kutaka kupata ushindi kwa joka lile. Kwanza, tulikuwa tupo katikati ya
tope zito mno na linaloteleza hivyo kwa vyovyote isingekuwa rahisi kwetu
kukimbia. Pili, nilifahamu kuwa lile lilikuwa joka mkubwa tena lenye sumu
kali hivyo endapo tungelipa mwanya wa pigo moja tu la kutuuma na kutu￾kamulia sumu yake tusingefika mbali na sumu yake kali ingetukausha haraka
na hicho ndicho kilichonikatisha tamaa.
Lile joka sasa lilikuwa limetulia likitutazama kama linalotuvizia tujitikise tu
ili tuzijutie nafsi zetu. Nikazikumbuka zile bunduki nilizozichukua kule pan￾goni tulipotoroka kuwa bado nilikuwanazo mwilini hata hivyo kwa wakati huu
nilifahamu kuwa zisingetufaa kitu kwani toka kuzichukua hadi kujiweka sawa
lile joka lingekuwa tayari limekwishatushambulia.
Niliacha kumtazama Jérome Muganza ambaye alikuwa ameganda kama
sanamu pembeni yangu nikayapeleka macho yangu kulitazama tena lile joka
huku akili yangu ikionekana kuzidiwa uwezo wa kufanya kazi. Nilipoende￾lea kulitazama vizuri lile joka nikagundua kuwa lilikuwa likijiandaa taratibu
kutushambulia hivyo nikajua tusingekuwa na muda mrefu wa kuendelea ku￾jishauri nini cha kufanya. Nikaikamata vizuri ile kurunzi niliyoichukua kule
pangoni huku mkono wangu mwingine nikiuzungusha taratibu kiunoni mwan￾gu kukichukuwa kile kisu na wakati huo wote macho yangu hayakuhama kwa
lile joka.
Niliweza kuyasikia mapigo ya moyo wangu namna yalivyokuwa yakihan￾gaika ovyo hata hivyo niliyapuuza. Lile joka sasa lilikuwa likijigeuza tara￾tibu kunitazama na hapo nikajua kuwa lilikuwa limenishtukia nilichokuwa
nikikifanya, mara nikaanza kuliona likijiandaa kufanya shambulizi makini la
kushtukiza. Sasa nilifahamu kuwa nilipaswa kufanya maamuzi makini na ya
haraka bila ya kuchelewa zaidi vinginevyo lingeniwahi na kunifanya kafara.
Lile joka sasa nililiona kuwa lilikuwa tayari kunishambulia ikabidi niwahi kulipotezea shabaha yake hivyo haraka nikaiwasha ile kurunzi na hapo mwan￾ga mkali ukaangaza kisha nikamulika upande mwingine wa lile pango na hapo
lile joka likageuka haraka sana kuutazama ule mwanga kule ulipomulika.
Jaribio langu la kwanza likawa limefaulu vizuri na hapo nikajikuta nikimsifu
Mungu kwa kunipa binadamu akili nyingi kuliko viumbe vingine wote, lakini
kwa namna nyingine mambo yaliharibika.
Lile eneo lilikuwa na popo wakubwa wenye mbwawa pana kama Mwewe.
Popo hao wengi kumbe walikuwa wamening’inia juu ya paa la pango lile
hivyo ule mwanga wa kurunzi ukawa umewaharibia starehe yao na kuwafanya
wachanguke kila mahali na kuanza kuzungukazunguka hovyo mle ndani huku
wakitoa sauti mbaya zinayoumiza masikio.
Nilimuona Jérome Muganza akiwahi kujilaza chini na kujifunika kichwa
chake kwa mikono ili wale popo wasimuume hata hivyo mimi sikushughulika
nao sana kwani macho yangu bado yalikuwa kwa lile joka. Wale popo wali￾kuja na kuanza kunipiga usoni na kichwani kwa mbwawa zao ngumu kama
waliokuwa wakinitaka niizime ile kurunzi, nikawaputa kwa mkono wangu la￾kini wakati huohuo nikiendelea kulitazama vizuri lile joka mbele yangu amba￾lo wakati huu lilionekana kutusahau kwa muda likibabaishwa na ule mwanga
kurunzi ukutani, wale popo na makelele yao.
Niliuhamisha ule mwanga wa kurunzi na kumulika sehemu nyingine ili lile
joka ligeuke tena kuutazama ule mwanga na wakati huo niweze kuliona vizuri.
Lile joka likafanya kama nilivyotaka, likageuka na kuutazama ule mwanga na
hapo nikakibana vizuri kile kisu changu mkononi na kuanza kukizungusha na
kilipokoleavizuri nikakifyatua na kukirusha usawa wa kichwa cha lile joka.
Ilikuwa ni shabaha nzuri sana kwani kile kisu kilipenya vizuri katikati ya jicho
lake la upande wa kulia na kuiacha sehemu ya mpini tu kubaki kwa nje.
Muda uleule lile joka likaanza kuyumbayumba likijipigizapigiza kichwa
chake ukutani huku likitoa sauti kali na mbaya ambayo iliniogopesha sana
kiasi kwamba hata wale popo walihofia usalama wao wakatoka mle pangoni
na kukimbia. Lile joka liliendelea kujipigiza pigiza ukutani kwa hasira huku
likijinyonganyonga hivyo likawa linapasua kuta za lile pango kama mchezo.
Vumbi kali likatimka mle ndani na baadhi ya udongo ukawa ukiporomoka
toka juu ya lile pango. Nikaanza kuhisi kuwa mwangwi wa sauti kali ya lile
joka ulikuwa ukisafiri na kupenya katika kila kona ya mapango yale.
Wakati likiendelea kujipigiza na kujinyonganyonga ndiyo nikakiona kile
kiwiliwili chake kwa sehemu tu, urefu wa kiwiliwili chake ulikuwa sawa na
urefu wa mti mrefu wa mnazi. Mkia wake ulikuwa una nguvu sana, ulinipiga
nikaukwepa hivyo ukaenda kupasua sehemu ya ukuta wa pango lile hata hivyo
upepo wake tu ulifanikiwa kuniyumbisha. Ile sehemu ya ukuta wa pango iliy￾ovunjika chini yake ndiyo kulikuwa na ule mfereji mkubwa wa maji tulioku￾wa tukiufuata hivyo lile joka likawa limeturahisishia kazi. Sikuona sababu ya
kuendelea kupambana tena na lile joka kubwa lenye hasira kwani nilifahamu
hatari ambayo ingenikabili hasa ukichukulia kuwa nilikuwa tayari nimelije￾ruhi jicho moja. Nililicha liendelee kujipigizapigiza hovyo kisha nikamshika
Jérome Muganza mkono na kuanza kumvuta kuwa tuondoke. Jérome Muganza hakuweza hata kuongea kwani hofu ilikuwa bado imem￾shika na alikuwaakiyaona mambo yote yaliyokuwa yakitokea mle pangoni ni
kama ilivyokuwa sinema ya kutengeneza.
Tulisota juu ya tope lile mpaka tukafika ukingoni kwenye ule ukuta wa pan￾go uliovunjika ambako chini yake kulikuwa na ule mrefeji wa maji na hapo
nikamshika mkono Jérome Muganza na kijirusha naye kwenye ule mfereji.
Ulikuwa ni mfereji mkubwa kiasi na wenye maji baridi sana. Nilimuuliza
Jérome Muganza kama alikuwa fundi wa kuogelea akaniambia kuwa nisiwe
na wasiwasi huku akiwa bado haamini macho yake.
Safari nyingine ikaanza tena yeye akitangulia mbele na mimi nikimfuata
kwa nyuma huku silaha zangu nikizinyanyua juu kwa mkono mmoja ili zisi￾loane kwenye yale maji wakati tukiogelea. Tukaanza kuogelea taratibu kuu￾fuata uelekeo wa ule mfereji. Yale maji ya ule mfereji yalikuwa ya baridi mno
na yalikuwa yakiendelea kutusafisha yale matope yaliyokuwa yametuganda
mwilini. Kwa kweli hata mimi nilikuwa siamini kuwa tulikuwa tumeponyoka
toka katika domo la lile joka kali na la kutisha tena muda mfupi tu uliyopita.
__________
TULIENDELEA KUOGELEA TARATIBU NA KWA UTULIVU huku
tukiwa tumeongozana kuufuata uelekeo wa ule mfereji. Ile kurunzi nilikuwa
nimeizima na kuishikilia mkononi na macho yangu yote yalikuwa kwa Jérome
Muganza nikizifuatilia kwa ukaribu nyendo zake. Nilimshangaa sana Jérome
Muganza kuwa alikuwa ni mwogeleaji stadi mno akiyakata maji kama samaki,
ule mfereji ulitusafirisha na tukawa tukikunja kona moja na kuingia nyingine.
Nilikuwa nikizihesabu vizuri zile kona na hadi wakati huu tulikuwa tumezia￾cha kona nane nyuma yetu na bado tulikuwa tukiendelea kuogelea katikati ya
giza zito.
Tulifika sehemu moja kwenye kona fulani ambako ule mfereji ulikuwa
umekunja kona kuelekea sehemu ya chini zaidi ya pango lile. Tukaogelea na
kwenda kusimama kwenye ile kona sehemu iliyokuwa na mchanga mwepesi
na laini kama wa ufukweni na safari yetu ikaishia hapo.
Tulitoka mle mferejini na kuketi kwenye ufukwe ule mdogo uliojaa mchanga
huku kila mmoja akionekana kuzama katika fikra zake. Nilimtazama Jérome
Muganza na kumuona kuwa alikuwa bado akitweta kwa hofu na hakuna ali￾yemsemesha mwenzake ingawaje niligundua kuwa Jérome Muganza alikuwa
akinitazama kwa jicho la wiziwizi tukio ambalo liliendelea kunipa wasiwasi.
Wakati Jérome Muganza akipumzika mimi nilikuwa nikizikagua vizuri zile
silaha nilizoziiba kwa wale askari wa Kanali Bosco Rutaganda na kuziweka
sawa kukabiliana na chochote ambacho kingetokea mbele ya safari yetu. Nili￾pomaliza kuziweka vizuri zile silaha nilijilaza pale mchangani kuupa mwili na
akili yangu utulivu kidogo na hapo nikajihisi ni kama niliyeutua mzigo mzito
mno ulikuwa ukinielemea kwa kipindi kirefu mwilini kwani nilikuwa sijapata
nafasi ya kupumzika tangu nilipotekwa na kuletwa mle pangoni hata hivyo
yale maumivu ya majeraha mwilini nilikuwa bado nikiyasikia.
Nikiwa bado nimelala pale mchangani huku nikitazama sehemu ya juu ya pango lile niligundua kuwa Jérome Muganza alikuwa amegeuka kwa siri
kunitazama tena na alikuwa akinipiga jicho la wizi taratibu katika mtazamo
usioeleweka kana kwamba mimi nilikuwa kiumbe cha ajabu mbele yake. Kwa
kweli moyo wangu ulianza kushikwa na wasiwasi sana juu ya tabia yake ile
na sikufahamu ni kwanini alikuwa akinitazama namna ile kila mara, vilevile
sikufahamu alikuwa akiniwazia nini kichwani.
Nilianza kuhisi kama kengele ya tahadhari ilikuwa ikianza kugonga
kichwani mwangu ikinitahadharisha kuwa niwe makini na mtu ninayeongo￾zana naye hata hivyo nilijikuta nikiyapuuza mawazo yangu kwani sikuona
dalili yoyote ya hatari kwa wakati ule. Sikutana Jérome Muganza aendelee
kunitazama vile hivyo niligeuka na kumuuliza
“Bado tupo mbali sana na lile pango? nilimuuliza na hapo akaacha kunita￾zama na kutazama pembeni.
“Siyo mbali sana kutoka hapa” alinijibu kivivuvivu huku akiendelea kuta￾zama pembeni.
“Inaweza ikatuchukua muda gani?
“Muda wa kama dakika kumi na tano unaweza kututosha” Jérome Muganza
aliniambia na nilipogeuka vizuri kumtazama nikamuona ni kama aliyekuwa
amezama katika fikra fulani hali iliyompeleka mawazo yake yasiwe pale.
“Vipi kuhusu gazeti lako?, utaendelea na kazi yako endapo tutafanikiwa ku￾toka humu pangoni salama?
“Kwa sasa siwezi kufahamu kwani bado hatujatoka”
“Gazeti lako bado ni muhimu sana katika kuieleza dunia juu ya unyama
unaofanyika humu ndani” nilimchombeza kidogo Jérome Muganza huku uso
wangu ukiumba tabasamu hafifu na hapo nikamuona akigeuka kunitazama
hata hivyo nilishangazwa kidogo na uso wake kwani haukuonesha tashwishwi
yoyote. Baadaye nilimuona akitabasamu kidogo kabla ya tabasamu lake kufi￾fia taratibu na hatimaye kukoma.
__________
NILIHISI KUWA TULIKUWA TUMEPUMZIKA kwa muda wa kutosha
pale ufukweni kiasi cha kuipa utulivu wa kiasi miili na akili zetu hivyo toka
pale nilipolala nilisimama taratibu na hapo nikajihisi kama niliyekuwa nime￾pata nguvu mpya.
“Simama twende hatuna muda zaidi wa kuendelea kukaa hapa” nilimwam￾bia Jérome Muganza huku nikimtazama usoni na hapo nilimuona ni kama
anayesita kuendelea na safari lakini hatimaye alisimama kivivuvivu na hapo
safari yetu ilianza tena. Kama ilivyokuwa kawaida yetu Jérome Muganza al￾itangulia mbele kwa kuwa yeye ndiye aliyekuwa akizifahamu vizuri njia za
mapango yale.
Wakati tukiondoka eneo lile nyuma yetu nilikuwa nikiyasikia yale makelele
ya maji yaliyokuwa yakisafiri mferejini. Tuliingia kwenye uchochoro
mwingine wa pango lile ambao ulikuwa mwembamba na mfupi kwa kwenda
juu hivyo tukawa tunatembea kwa kuinama inama. Nilipotaka kuwasha ile
kurunzi Jérome Muganza alinitahadharisha kuwa nisiiwashe kwani eneo lile lilikuwa na popo wengi ambao wangeweza kutushambulia endapo wangeuona
mwanga wa ile kurunzi, hivyo tuliendelea kutembea gizani. Kiasi cha umbali
wa mita kama thelathini mbele yetu tulifika katika eneo lilioonekana kama njia
panda yenye makutano ya vichochoro vinne.
Tulipofika pale Jérome Muganza alisita kidogo na hapo nikajua kuwa ali￾kuwa akijaribu kuyakumbuka vizuri mazingira yale. Baada ya muda mfupi
nilimuona Jérome Muganza ikipinda kona kuingia uchochoro wa upande wa
kulia nami nikamfuata kwa nyuma. Tukawa tumeingia kwenye uchochoro
mwingine ulioonekana kama uliokuwa ukiturudisha kule tulipokuwa tukitoka
lakini tulipofika mbele kidogo tulichepuka na kuingia upande wa kushoto. Uli￾kuwa ni uchochoro mwembamba sana uliofanana na tundu dogo linaloelekea
mgodini hivyo tulijongea kwa kulalia tumbo.
Ulikuwa ni uchochoro wenye joto kali hivyo nilihisi zile gwanda za jeshi
nilizozivaa zilikuwa mbioni kulowana kwa jasho. Tulipovuka uchochoro ule
tukatokezea kwenye pango jingine lililokuwa likielekea sehemu ya chini zaidi.
Lilikuwa ni pango lililokuwa linafanana na lile pango tulilokutana na lile joka
hatari hivyo nilihisi damu yangu ikianza kuchemka taratibu kwenye pango
lile. Wakati tukishuka kule chini ile hali ya joto ilikuwa ikipungua taratibu na
sehemu yake kuchukuliwa na baridi kali, Jérome Muganza akaniambia kuwa
tulikuwa tumelikaribia lile pango walilofungwa wenzetu.
Sasa tulikuwa tukitembea kwa tahadhari sana katikati ya pango lile lenye
giza kote. Tukawa tunatembea kwa kupapasapapasa. Sehemu ya chini ya pan￾go lile kulikuwa na mawe yaliyochongoka sana hata hivyo kwa kuwa tulikuwa
tumevaa zile buti za kijeshi hatukuweza kupata adha yoyote. Tulitembea kwa
tahadhari sana na wakati huu niliyasikia tena yale makelele ya maji, nikajua
kuwa hatukuwa mbali sana ule mfereji. Tulifika sehemu fulani katikati ya lile
pango kulikokuwa na uchochoro na hapo tukaanza kupanda juu kwa kushikilia
mawe yaliyochongoka yaliyokuwa pembeni ya kuta za uchororo ule.
 
Jérome Muganza aliniambia kuwa mara baada ya kumaliza kupanda juu ya
uchochoro ule tungetokezea kwenye njia nyingine ya pango yenye nafasi nzuri
inayomruhusu mtu kutembea bila shida. Na mara baada ya kuingia kwenye
njia hiyo ya pango tungetembea umbali mfupi upande wa kushoto na hapo
ndiyo tungekuwa tumefika kwenye lile pango walikofungwa wenzetu. Kufikia
hapo nilimwambia Jérome Muganza arudi na kukaa nyuma yangu na mimi
ndiye ningekuwa nikiongoza msafara kwani tulikuwa tumefika kwenye eneo
lililokuwa likihitaji umakini wa hali ya juu na kosa lolote dogo ambalo tunge￾liruhusu lingeweza kuyagharimu maisha yetu sote.
Jérome Muganza akakubaliana na wazo langu hivyo akarudi nyuma na
mimi ndiye nikawa naongoza masafara hata hivyo bado nilikuwa na masha￾ka kuwa huenda wale wanajeshi wa Kanali Bosco Rutaganda mpaka wakati
huu wangekuwa wamekwishashtukia mpango wa kutoroka kwetu na hivyo
wengekuwa wameanza harakati za kututafuta, na sehemu ya kwanza ambayo
kwa vyovyote wangekimbilia ingekuwa ni katika lile pango walikofungwa
wenzetu, na kama walikuwa wamewahi kufika na kutukosa kwa vyovyote
wangeweka mtego wa kutusubiri. Haya ndiyo yalikuwa mawazo yangu mpaka wakati huu hivyo nilijua kuwa tulipaswa kuwa makini kwani tulikuwa
tukielekea kukabiliana na hatari kubwa zaidi mbele yetu.
Wakati tukiendelea na safari yetu nikapata wazo jingine jipya, wazo la kumpa
bastola Jérome Muganza kwa ajili ya kujihami pale ambapo ingehitajika kufa￾nya hivyo kwani nilifahamu japokuwa mimi nilikuwa komandoo niliyehitimu
vizuri katika mapambano lakini ningekuwa nafanya makosa makubwa kwa
kujiamini sana kwani endapo ingetokea nimezidiwa hakuna mtu mwingine
ambaye angenipa msaada. Jérome Muganza alikuwa ameniambia hapo awali
kuwa yeye hakuwa fundi wa kutumia silaha lakini nilifahmu kuwa asingesh￾indwa kutumia bastola kwa maelekezo machache ambayo ningempa. Hivyo
tulisimama kisha nikageuka na kumpa bastola na hapo nilistaajabu kidogo ku￾muona akiipokea vizuri bila ya kusita, nikampa maelekezo machache ya nam￾na ya kuitumia na akaonekana kuyaelewa vizuri hivyo safari yetu ikaendelea.
Mwisho wa uchochoro ule tukawa tumetokezea kwenye tundu dogo lili￾lojitokeza kwenye ile njia pana ya pango ambayo Jérome Muganza alikuwa
amenigusia kuwa ilikuwa ni njia ya kuelekea kwenye lile pango walikofungwa
wenzetu. Nilitanguliza kichwa taratibu huku masikio yangu yakiwa makini
kunasa chochote eneo lile wakati huo Jérome Muganza akinifuata kwa nyuma.
Hata hivyo sikusikia sauti ya kitu chochote zaidi ya zile kelele hafifu za maji
yaliyokuwa yakitiririka kwenye maeneo fulani fulani ya pango lile.
Nilipotanguliza kichwa changu vizuri kwenye ile njia pana ya pango nilitu￾lia nikitazama huku na kule huku nikijitahidi kuhisi kama kulikuwa na uwepo
wowote wa kiumbe hai eneo lile. Sikuhisi chochote na bado hali iliendelea
kuwa tulivu, sikuhisi chochote na bado hali iliendelea kuwa tulivu. Niliende￾lea kutazama tazama eneo lile na hatimaye umbali mfupi upande wa kushoto
nikauona mwanga hafifu uliopenya kwenye mlango wa lile pango tulilokuwa
tukilifuata na hapo nikaikumbuka ile taa ya kandili iliyokuwa katikati mle
ndani ya lile pango. Tabasamu langu hafifu likamea gizani kuwa tulikuwa tu￾metokezea sehemu sahihi na nilipogeuka nyuma nikamuona Jérome Muganza
kuwa alikuwa akinitazama kama mtu aliyekuwa akitarajia nimwambie cho￾chote. Hata hivyo bado ilikuwa mapema sana.
Nilitoa tena kichwa na kuyazungusha macho yangu taratibu eneo lile niki￾tarajia kuona au kuhisi chochote lakini hali bado ilikuwa tulivu. Sasa ulikuwa
ni muda mwafaka wa kuendelea mbele lakini kabla ya kuendelea mbele nili￾geuka nyuma na kumwambia Jérome Muganza
“Wewe utabaki hapa ukinilinda na hatari wakati mimi nitakapokuwa nikil￾iendea lile pango” na hapo nilimuona Jérome Muganza akitikisa kichwa aki￾onesha kunielewa.
“Unayo bastola mkononi chochote tofauti utakachokiona usisite kuitumia”
nilimsisitiza kisha nikageuka na kuanza safari. Nilipomaliza kutoka kwenye
ule uchochoro mwembamba wa pango nikajikuta nimetokezea katikati ya pan￾go jingine lenye nafasi na ukubwa wa kutosha unaoniwezesha kutembea bila
ya shida. Niliikamata vizuri bunduki yangu mkononi huku nikianza kutembea
kwa kunyata taratibu na katika utulivu usioweza kumshtua kiumbe hai yeyote
ambaye angekuwepo eneo lile. Kwa kila hatua mbili au tatu nilizozitupa nililazimika kusimama na kugeuka
nyuma kusikiliza kama kulikuwa na kiumbe chochote nyuma yangu na nili￾poona kuwa hali bado ilikuwa tulivu niliendelea mbele na safari yangu. Baada
ya muda mfupi nikawa nimeufikia ule mlango wa lile pango walimofungwa
wenzetu. Nilisimama na kuutathmini vizuri ule mlango kupitia ule mwanga
wa taa ya kandili uliokuwa ukipenya kwa chini.
Mapigo ya moyo wangu yakiwa yameanza kuniendea mbio niliyaona maku￾fuli mawili makubwa yakiwa yamefungwa vizuri kwenye komeo za mlan￾go ule juu na chini. Nilijaribu kufikiria haraka bila ya kupata majibu kuwa
ningewezaje kuzifungua zile kufuli mbili imara zilizokuwa zikinitazama pale
mlangoni. Kwa kweli sikupata majibu huku nikiwaza kuwa pengine kama
ningekuwa na zile zana zangu za kijasusi ningeweza kuyafungua lakini kwa
hapa sikuwanazo hivyo mawazo yangu yakajikuta yakiifikiria bunduki nili￾yokuwa nayo mikononi mwangu kwani kupitia bunduki hiyo ningeweza
kuyafungua yale makufuli kwa kuyafyatulia risasi. Hata hivyo baadaye nil￾iliona wazo hilo kuwa lilikuwa na walakini kidogo kwani milio hiyo ya ri￾sasi pengine ingeweza kuwashtua askari wa Kanali Bosco Rutaganda ambao
pengine wangekuwa jirani na eneo lile. Kufikia hapa nilihisi akili yangu kuwa
ilikuwa ikifanya kazi ya ziada katika kufikiria namna ya kuyafungua makufuli
yale.
Hata hivyo, nilifahamu kuwa ingekuwa hatari zaidi endapo ningeendelea
kusubiri eneo lile bila ya kutoa maamuzi ya haraka. Wakati nikiendelea ku￾fikiri mara nikapata wazo jipya ambalo lilifufua upya tumaini langu. Ni waka￾ti nilipokumbuka kuwa zile funguo za ule mlango wa lile pango nililokuwa
nikihojiwa na kanali Bosco Rutaganda sasa zilikuwa ndani ya mfuko wa lile
gwanda la kijeshi nililolivaa.
Nilikuwa nimesahau kuwa mara baada ya kukitoroka kile chumba cha lile
pango nikiwa na Jérome Muganza ni mimi ndiye niliyeufunga ule mlango
wa kile chumba na kuzichukua zile funguo za mlango. Kumbukumbu hizo
zikanifanya nianze kujipapasa haraka mifukoni na muda si mrefu nilijikuta
nikifurahi baada ya kuzipata zile funguo. Ulikuwa ni mkungu wenye funguo
nyingi hivyo nikawaza kuwa miongoni mwazo pengine zingekuwepo funguo
za makufuli ya huu mlango mbele yangu.
Nilizichukua funguo zile na kuanza kuusogelea ule mlango, ilikuwa ni
wakati nilipokuwa nikitaka kuyashika yale makufuli ili nianze kuyajaribu
kuyafungua wakati niliposhtushwa na nyaya fulani nyembamba zilizokuwa
zimefungwa kuyazunguka yale makufuli na hapo nikasita kuzipachika zile
funguo kwenye kufuli na badala yake nikainama na kuanza kuzitazama vizuri
zile nyaya kwa msaada wa mwanga hafifu toka katika ile kurunzi niliyokuwa
nayo mkononi.
Koo langu likaanza kukauka kwa hofu. Zilikuwa ni nyaya nyembamba za
madini ya shaba, nyaya hizo zilikuwa zimefumwa katika mtindo fulani wa
kuyazunguka yale makufuli na baada ya kutoka katika makufuli yale mbele
kidogo nyaya hizo zilikuwa zimeungana na kushuka chini ya mlango. kupitia
ule mwanga wa kurunzi niliweza kukiona kiboksi kidogo ambacho zile nyaya zilipotelea ndani yake.
Nilipozidi kukichunguza vizuri kile kiboksi nikajikuta nikishikwa na hofu
baada ya kugundua kuwa lilikuwa ni bomu la kutega, bomu ambalo enda￾po lingelipuka lingeweza kusambaratisha eneo kubwa la pango lile. Nilien￾delea kuchunguza vizuri na baadaye nikagundua kuwa zile nyaya zilikuwa
zimechomekwa kwenye matundu ya funguo kwenye yale makufuli ili endapo
mtu yeyote angeyashika yale makufuli na kupachika funguo angesababisha
mtikisiko kidogo wa zile nyaya, mtikisiko huo ungesababisha shoti kutokana
na mtego wenyewe ulivyokuwa umetegwa na hivyo shoti hiyo ingesababisha
mlipuko wa lile bomu na hatimaye kusambaratisha eneo lile na viumbe vyote
vilivyokuwa eneo lile.
Wakati nikiendelea na uchunguzi wangu bado nilikuwa na wasiwasi kama
kulikuwa na mtu yoyote aliyekuwa akinitazama eneo lile, nilimkumbuka
Jérome Muganza kule nilikomuacha na kujaribu kuwaza kama alikuwa aki￾nitazama au lah!.
Nilihisi muda ulikuwa ukienda haraka sana na endapo ningeendelea
kuchelewa ningekuwa naisubiri hatari. Nikiwa kama mwalimu mzuri wa
mafunzo ya kijeshi na komandoo niliyebobea vizuri katika medani za kivita,
mabomu ya kutegwa kama hili hayakuwahi kuwa kikwazo cha namna yoyote
katika harakati zangu. Kumbukumbu ya Operesheni Chakaza dhidi ya vikosi
vya majeshi ya Dikteta Iddi Amini Dada wa Uganda kwenye vita ya Kagera
ilikuwa bado ipo hai katika fikra zangu.
Katika Operesheni hiyo ya kuyaondoa majeshi ya wavamizi zaidi ya miaka
kumi na sita iliyopita mimi nikiwa mmoja wa makamanda wa jeshi la wanan￾chi wa Tanzania niliyekuwa nikiongoza platoon ya kikosi maalum cha kutegua
mabomu yaliyotegwa ardhini na adui. Tulifanikiwa kupata ushindi mkubwa
ambao ulikiletea heshima kubwa kikosi changu na kuwaacha askari wa Iddi
Amini Dada waliosalia kutupa bunduki zao chini na kunyanyua mikono yao
juu kusalimu amri. Hivyo nilipolitazama bomu hili haraka niligundua kuwa
lilikuwa ni bomu la namna gani na hapo nikainama na kuanza utundu wangu.
Pasipo kuzitikisa zile nyaya niliweza kuzifuatilia na kuielewa haraka sistimu
yake ya mlipuko kisha nikaufyatua mtego uliokuwa umeunganishwa na seh￾emu ya chanzo cha shoti inayoweza kulifanya bomu lile lilipuke. Nilipomaliza
nikazikata nyaya nyingine zilizokuwa na mahusiano na baruti ya bomu. Kwa
muda mfupi tu nikawa nimefanikiwa kulitegua lile bomu na kuzitenganisha
zile nyaya pasipo adha yoyote. Hatua iliyofuatia ilikuwa ni kuzichukua zile
funguo mfukoni na kuanza kuyafungua yale makufuli. Nikafanikiwa kuufun￾gua ule mlango wa pango mapema sana kuliko nilivyokuwa nikitarajia.
Nilipomaliza kuufungua ule mlango wa pango nikasimama mlangoni na
hapo nilijikuta nikitazamana na sura zenye mashaka, hata hivyo kulikuwa na
sura moja ngeni iliyokuwa imeongezeka mle ndani. Sura ya kijana mwenye
umri wa kati ya miaka ishirini na nne hadi ishirini na nane. Hata hivyo nili￾gundua pia kuwa watu watano walikuwa wemepungua mle ndani tangu mimi
nilipochukuliwa na wale askari wa Kanali Bosco Rutaganda.
Sikuwa nimemuona Ikirezi hivyo niliyazungusha macho yangu taratibu kuzitazama vizuri nyuso za watu waliokuwa mle ndani na hatimaye nilimuona
Ikirezi akiwa ameketi kwenye pembe ya pango lile huku pembeni yake akiwa
na Jean Pierre Umugwaneza. Wote walikuwa wameshikwa na mshangao kwa
kuniona pale mlangoni tena nikiwa huru. Bila kupoteza muda nikawaambia
wale watu wote mle ndani kuwa nilikuwa nimefika pale kuwaokoa hivyo wasi￾we na hofu.
Wakawa kama hawaniamini hata hivyo nilipozidi kuwaeleza namna ya
mambo yalivyokuwa niliziona nyuso zao zikianza kupata tumaini. Muda
uleule nikawaambia kuwa wasimame na kunifuata kwani safari yetu ya ku￾toroka mle pangoni ilipaswa kuanza haraka bila ya kuchelewa. Ikirezi na Jean
Pierre Umugwaneza wakawa wa kwanza kunielewa na kunifuata na watu
wengine mle ndani wakafuatia huku wengine wakimshukuru Mungu.
Wakati wale mateka wenzangu wakitoka mle ndani ya pango mimi niliwap￾isha pembeni huku nikiwahesabu na jumla yao ilikuwa watu ishirini na moja,
miongoni mwao walikuwepo wachache dhaifu walionekana kupata shida hata
ya kutembea lakini walijitahidi hivyo hivyo.
Watu wote walipotoka mle ndani niligeuka na hapo nikaiwasha kurunzi
yangu kumulika sehemu ya giza ya lile pango, nikaiona miili mitatu ya watu
imelala sakafuni na hapo nikatambua kuwa mtu mmoja zaidi alikuwa amek￾ufa tungu mimi nilipochukuliwa mle pangoni kwani hapo mwanzo nilikuwa
nimeiacha miili miwili tu yaani mwili wa Dr. Francois Trezor na ule wa mtu
mwingine ambaye sikumfahamu.
Watu wote walipomaliza kutoka mimi nikawa wa mwisho kufunga ule
mlango huku nikiwataka wakae kimya. Nilipomaliza kufunga ule mlango nil￾ilichukua lile bomu nililolitegua na kulitega kwa namna yangu huku nikizun￾gusha mtego wa waya sehemu ya chini ya eneo lile ambao ungempelekea mtu
yeyote asiye makini kujikwaa na hivyo kupelekea lile bomu kulipuka.
Mambo yote nilikuwa nikiyafanya kwa haraka na kwa umakini wa hali
ya juu na nilipomaliza nilitangulia mbele na kuwataka wale watu wanifuate.
Ikirezi na Jean Piere Umugwaneza wao walikuwa karibu yangu zaidi. Wakati
tukiendelea na safari niliwatahadharisha wale watu kuwa wakati wote wawe
kimya na kufuata maelekezo yangu, wakawa wamenielewa huku wakionekana
kushikwa na kihoro cha furaha. Tulitembea kwa tahadhari hadi tulipolifikia
lile tundu la pango sehemu nilipomuacha Jérome Muganza huku nikiwa na
tumaini kubwa la ushindi wa kutoka katika mapango yale tukiwa salama.
Nilifahamu fika kuwa Jérome Muganza bado angeendelea kuwa msaada
mkubwa katika kuufanikisha mpango wa kutoroka kwetu kwani ni yeye ndiye
aliyekuwa ikizifahamu vizuri njia za mapango haya.
Lakini furaha na matumaini makubwa niliyokuwa nayo yalibidilika ghafla
na sehemu yake kuchukuliwa na hofu na wasiwasi pale nilipofika kwenye lile
tundu na kutomkuta Jérome Muganza. Nikiwa nashindwa kukubaliana haraka
na hali hiyo sikutaka kuamini mapema kuwa Jéremo Muganza hakuwepo eneo
lile. Mwanzoni nilifikiri kuwa Jérome Muganza alikuwa amejibanza eneo fu￾lani mafichoni kwa ajili ya kujihakikishia usalama wake wakati akitusubiri
lakini nilianza kukata tamaa na kujihisi kuchanganyikiwa pale nilipoona muda unazidi kwenda bila ya yeye kujitokeza. Kwa mara ya kwanza hofu kubwa
ilianza kuutafuna mtima wangu, wasiwasi ukaanza kunishika huku nikiwaza
kuwa huenda kitu fulani kisicho cha kawaida kingekuwa kimemtokea Jérome
Muganza.
Niligeuka na kuutazama ule msafara wa watu nyuma yangu ambao bila ya
shaka kwa wakati huu walikuwa wakinifananisha na kijito cha maji katikati
ya jangwa kame kwa kuwa mkombozi wao, na hapo nikaanza kuona dalili za
uzito wa kuikamilisha furaha yao ya kuwatoa mle pangoni wakiwa salama
pasipo uwepo wa Jérome Muganza. Ikirenzi na Jean Pierre Umugwaneza bila
shaka waliniona namna nilivyosita ghafla baada ya kufika pale na kutumuona
Jérome Muganza hata hivyo nilijitahidi sana kuuficha mshtuko wangu mbele
yao kwani sikutaka kuwajengea mazingira yoyote ya wasiwasi ingawaje moy￾oni sikuwa na amani tena na safari yetu.
Ule msafara wa watu wote ulipofika kwenye lile tundu la pango niliupanga
vizuri nikimruhusu mtu mmoja baada ya mwingine kupita kwenye lile tundu
kuelekea sehemu ya chini ya lile pango huku nikiwa macho kutazama huku na
kule kama kungekuwa na kiumbe chochote ambacho kingekuwa kikikaribia
eneo lile lakini vilevile nikitarajia kumwona tena Jérome Muganza akijitokeza
lakini haikuwa hivyo. Jérome Muganza alikuwa ametoweka katika mazingira
ya kutatanisha.
Utaratibu wote ulikuwa ukifanyika kwa umakini na ukimya wa hali ya juu
ili kukwepa kukishtua kiumbe chochote ambacho kingekuwa karibu na eneo
lile. Baada ya muda mfupi lile zoezi likawa limemalizika na watu wote waka￾wa wamepita kwenye lile tundu la pango na mimi nikawa wa mwisho nyuma
yao.
Muda mfupi baadaye wote tukawa tumetokeza kwenye lile pango la chini.
Kabla ya kuanza safari yetu kule chini niliusimamisha kwanza ule msafara
kisha nikaanza kuzunguka eneo lile la jirani kumtafuta Jérome Muganza huku
nikimuita kwa sauti ya chini pale ambapo nilihisi huenda angekuwepo eneo
fulani mle ndani lakini niliishilia kukata tamaa tu kwani sikumuona Jérome
Muganza wala dalili zozote za uwepo wake na hapo nikahisi kuwa niliku￾wa nikipoteza muda wangu tu hivyo nilirudi kule ulipokuwa ule msafara wa
wenzangu na hapo safari yetu ya kuyatoroka yale mapango ilianza tena huku
mimi ndiye nikiuongoza ule msafara.
Kipindi chote cha safari yetu kichwani nilihisi kulemewa na mawazo juu ya
Jérome Muganza huku nikijiuliza maswali mengi bila ya kupata majibu.
Wasiwasi wangu mkubwa ulikuwa ni juu ya kufahamu kuwa ni njia ipi
ambayo ingekuwa sahihi kututoa salama nje ya mapango haya huku nikim￾kumbuka Jérome Muganza na kushindwa kuelewa ni yapi yaliyomsibu hata
nisimkute pale nilipomuacha. Wakati nikiendelea kuwaza dhana ya kuwa hu￾enda Jérome Muganza alikuwa ameamua kunitoroka ilianza kuumbika tarati￾bu katika fikra zangu kila nilipoendelea kumuwaza ingawaje sikuwa na hakika
sana na suala hilo. Nilikumbuka namna alivyokuwa akinitazama kila mara
wakati tulipokuwa tukiongozana tangu tulipotoroka kule pangoni baada ya
kuwavamia askari wa Kanali Bosco Rutaganda na hapo hisia tofauti zilianza kujengeka kichwani mwangu.
Jérome Muganza akiwa amekwishatoweka kusikojulikana bila ya kufahamu
masaibu yaliyomkuta sikuona sababu ya kuendelea kujishughulisha kumtafu￾ta kwani nilifahamu kuendelea kumsubiri eneo lile hatimaye tungekutwa na
wale askari wa Kanali Bosco Rutaganda ambao bado hisia zangu zilinieleza
kuwa walikuwa wakitutafuta kwa udi na uvumba. Nikapiga moyo konde na
kuendelea na safari huku wakati huu mimi nikiwa ndiyo kiongozi wa msafara
ingawaje sikuweza kuelewa kuwa ni njia ipi miongoni mwa zile njia nyingi za
mle pangoni ingekuwa sahihi kutufikisha mahali tunapotaka.
Tuliendelea na safari yetu mle pangoni huku wote tukiwa kimya katikati ya
giza nene lisilo na mfano. Sikutaka kuiwasha ile kurunzi kwa kuhofia huenda
ingetufanya tuonekane na adui kwa wepesi vilevile tukijiweka mbali na ile
adha ya popo wakali na wakubwa waliokuwa katika kila kona ya mapango
yale.
__________
WAKATI ULE KABLA YA KUJA NCHINI RWANDA nilikuwa nimeu￾tumia muda wangu mfupi kujifunza mambo mbalimbali juu ya nchi hii kupitia
vitabu na ramani mbalimbali ambazo nilipewa na kiongozi wangu na mratibu
wangu wa safari za kijasusi Brigedia Masaki Kambona, mara baada ya kuni￾taka nije hapa Rwanda kufuatilia juu ya kifo cha mwandishi wa habari wa
ubalozi wa Tanzania ndugu Tobias Moyo.
Kumbukumbu niliyokuwa nayo kichwani ni kuwa mifereji yote iliyokuwa
ikitoka kwenye mapango haya ilikuwa imeunganika na kuingia kwenye bonde
la ufa la Albertine. Bonde la ufa la Albertine ni bonde kubwa la ufa katika
ukanda wa nchi za Afrika Mashariki na ndani ya bonde hilo kukiwa na maziwa
makuu kama Ziwa Albert na Ziwa Edward au vilevile ziwa hili likiitwa Ziwa
Rutanzige na wenyeji kwa upande wa kaskazini mashariki mwa nchi ya Ugan￾da, na milima ya Virunga iliyopo katikati ya Ziwa Rutanzige na ziwa Kivu kwa
nchi hii ya Rwanda. Baada ya hapo Ziwa Kivu humwaga maji yake katika
Ziwa Tanganyika kupitia mto uitwao Ruzizi. Hivyo kwa upande wa nchi ya
Tanzania maziwa yaliyopo katika bonde la Albetine ni Ziwa Tanganyika, Ziwa
Rukwa na Ziwa Nyasa wakati kwa nchi ya Kenya ni Ziwa Turkana.
Mbali na mito na maziwa haya makubwa mapango haya yalikuwa yakipa￾kana na misitu mikubwa ya bonde la ufa la Albertine ambapo kwa kumbu￾kumbu zangu misitu hiyo haikuwa mbali sana na mapango haya na endapo
tungefanikiwa kutoka humu ndani salama sehemu nzuri ya kukimbilia kwanza
ingekuwa ni katika misitu hiyo.
Jérome Muganza akiwa tayari ametoweka kusikojulikana sasa nilifahamu
kuwa ni mimi ndiye ningetakiwa kuuongoza msafara huu. Nikiwa nimetan￾gulia mbele tulimaliza kulivuka pango lile la chini na tulipofika mbele ku￾likuwa na njia panda. Kwa kuwa nilikuwa sizifahamu njia za mapango yale
tulipofika sehemu ile nilifanya maamuzi ya kuifuata njia fulani bila kufahamu
kuwa njia hiyo ingetufanya tutokezee wapi hivyo ni kama tuliokuwa tukiba￾hatisha tu. Niliuongoza msafara ule tukaingia uchororo wa upande wa kulia. Ulikuwa ni uchochoro mwembamba kiasi na wenye mawe yenye ncha kali
na kona nyingi. Sikufahamu kuwa uchororo ule ungetufikisha wapi hata hivyo
nilijiridhisha moyoni kuwa tulikuwa tunaendelea na safari yetu. Ilikuwa ni njia
yenye joto kali na hewa nzito sana hata hivyo hatukuwa na uchaguzi wa kurudi
nyuma na wakati wote Ikirezi alikuwa pembeni yangu na niliweza kuisoma
hofu aliyokuwa nayo kutokana na uharaka wa mapigo ya moyo wake. Wakati
huu wote nilikuwa namuomba tukutane na mfereji wa maji kati ya ile mifereji
mingi iliyokuwa ikipita ndani ya mapango haya kwani niliamini kwa kuufuata
mfereji huo hatimaye ungetuongoza hadi nje ya mapango haya.
Tulimaliza kupita uchororo ule tukaingia kwenye njia nyingine ya pango
ambayo tuliweza kutembea bila shida na wakati tukipita sehemu hiyo nilish￾tuka kuwaona wenzangu wakisita kuendelea na safari hivyo ikanibidi na mimi
nisimame na nilipogeuka nyuma nilimuona mwenzetu mmoja akiwa amekaa
chini. Nilipomsogelea na kumchunguza vizuri nikagundua kuwa alikuwa ni
mwanamke wa makamo na alikuwa miongoni mwa watu waliokuwa dhaifu
mle pangoni.
Nilimuuliza mama yule kama angeweza kuendelea na safari akaniambia
tusipoteze muda wetu kumuhangaikia yeye kwani alikuwa mbioni kufa kuto￾kana na udhaifu wa mwili wake huku akisisitiza kuwa tumuache palepale na
sisi tuendelee na safari yetu. Kwa kweli sikuafikiana na wazo lake ingawaje
kwa namna nyingine nilifahamu kuwa alikuwa akizungumza ukweli kwani
alikuwa amedhoofika sana kutokana na mateso ya kule pangoni. Tulisimama
kidogo huku nikifikiria namna ya kumsaidia, nilipowatazama wenzangu nili￾waona wote nao walikuwa hoi na wasingeweza kutoa msaada wowote hivyo
nikaamua kumbeba begani mama yule na safari yetu ikaanza tena kwani nili￾fahamu kuwa roho yangu isingeridhika endapo tungemuacha yule mwenzetu
peke yake.
Tuliendelea na safari yetu yule mama akiwa begani kwangu huku mimi niki￾ongoza msafara. Yule mama alikuwa amekonda na kudhoofika sana hivyo si￾kuhisi uzito mkubwa sana hata hivyo nilijua kuwa kama endapo tungetembea
umbali mrefu kwa vyovyote ningechoka. Wakati wote tulipokuwa tukiendelea
na safari yule mama alikuwa akinisihi kuwa nisijisumbue kumbeba kwani an￾genifia tu mikononi hata kabla hatujafanikiwa kufika mbali lakini mimi sikum￾sikiliza hivyo tuliendelea tu na safari yetu.
Kule chini ya pango fukuto lilikuwa likiongezeka na hali ile ilinifanya nihisi
kuwa huenda mvua kubwa ilikuwa mbioni kunyesha. Giza zito lililokuwa mle
pangoni halikutoa mwanya wa kuweza kukisia kuwa muda ule ungekuwa saa
ngapi. Tuliifuata ile njia na mbele kidogo njia ile ilikunja kona upande wa
kulia ambako ilizidi kuwa nyembamba zaidi ingawaje tulipoingia uchororo ule
hali ya hewa ilibadilika na kuwa nafuu kidogo. Wakati tukiendelea na msafara
mara kwa mara nilijikuta nikihisi kuwa wale askari wa Kanali Bosco Rutagan￾da walikuwa wakitufuatilia kwa nyuma hata hivyo sikupenda kujikita katika
mawazo hayo.
Tulikuwa tumekwishatembea umbali mrefu pengine katika muda wa dakika
zaidi ya arobaini tukiingia pango hili na kutokezea pango jingine huku tukishuka na kupandisha katikati ya giza zito la mle ndani bila ya kuiwasha ile
kurunzi pale nilipoanza kuhisi kuwa tulikuwa tukizunguka sehemu moja na
hatukuwa tumepiga hatua katika safari yetu. Nilianza kuhisi kichwa kilikuwa
kikiniuma na mwili wangu ulikuwa mbioni kuelemewa na uchovu, yale majer￾aha ya mgongoni nayo niliyahisi kuwa yalikuwa yameanza tena kuvuja damu.
Hali hiyo ikanitia wasiwasi na hapo nikaona kuwa ingekuwa vema endapo
tungeamua kupumzika kidogo hivyo niliusimamisha ule msafara katikati ya
pango moja lililoonekana kuwa na nafasi ya kutosha kuketi kwa ile idadi yetu.
Hakuna aliyejaribu kupingana na wazo langu kwani watu wote mle ndani
walikuwa hoi kwa uchovu. Hivyo wote tuliketi chini na kupumzika na hapo
watu wakapata nafasi ya kuzungumza hili na lile lakini kwa sauti ya chini
kwani nilikuwa tayari nimewatahadharisha kuwa sauti ya namna yoyote in￾geweza kutufichua kwa adui.
Wakati wale watu wakiendelea kupumzika mimi mawazo yangu yalikuwa
yakifikiria juu ya njia ipi ambayo ingetusaidia kutoka mle pangoni na kwa
kweli nilihisi kuanza kuchanganyikiwa huku kichwa kikizidi kuniuma. Nili￾waona Ikirezi na Jean Pierre Umugwaneza wakiwa wamesogea karibu yan￾gu na ingawa tulikuwa gizani Ikirezi alinishika mkono na kuvitekenya vidole
vyangu taratibu na hapo nikafahamu kuwa kwa kiasi fulani alikuwa amekata
tamaa ingawaje hisia zake za mapenzi kwangu ndiyo tumaini pekee lililokuwa
limebakia moyoni mwake.
Nilihisi kuwa alikuwa akilia hivyo nikanyanyua mkono wangu na kuyapan￾gusa machozi yake ingawaje akili yangu kwa kweli haikuwa pale. Jean Pierre
Umugwaneza yeye alikuwa amezama katika fikra zake na kwa kweli nilim￾uonea huruma kwa kupoteza mke na mtoto wake kwa ajili yangu. Yule mama
niliyekuwa nimembeba sasa nilikuwa nimemlaza chini huku akiwa amelalia
mapaja yangu na mikono. Wakati tukiendelea kupumzika nilimuona akiusoge￾za mkono wake taratibu na kuushika mkono wangu wa kushoto na hapo aka￾jikaza na kuanza kuongea kwa shida
“Jina lako nani? aliniuliza
“Patrick Zambi” nilimtajia jina langu la bandia
“Mimi ni Madame Maria Grace” aliniambia kwa sauti hafifu iliyonifanya
niyatege vizuri masikio yangu ili nimsikie na hapo akakohoa kidogo na kuen￾delea “Mimi ni mfanyakazi wa benki ya taifa ya Rwanda na mume wangu ni
afisa wa ngazi ya juu wa jeshi la RPF”. Nilishtuka na kumtazama mama yule
ingawaje sikuweza kumuona vizuri kutokana na giza hafifu lililotanda mle
ndani, kilichonishtua zaidi ni juu ya kutamkwa kwa jeshi la RPF. Halikuwa
jina geni masikioni mwangu kwani niliwahi kulisikia mara nyingi jeshi hilo
lisilo rasmi lililokuwa likisemekana kuendesha harakati zake msituni za ku￾taka kuiondoa madarakani serikali ya rais Jevenal Habyarimana, rais wa nchi
ya Rwanda.
“Umesema mumeo ni afisa ngazi ya juu katika jeshi la RPF? nilimuuliza
kama ambaye sikusikia vizuri.
“Ndiyo! yeye ni afisa wa jeshi la Rwandese Patriotic Front, (RPF)” aliongea
kwa msisitizo
“Yupo wapi sasa?
“Sifahamu kwani hakuwahi kuniambia, labda yuko DRC Congo au Uganda,
mimi sifahamu”
“Jina lake?
“Meja Ciprian Ndikumana”
Nilimsikiliza vizuri mama yule huku nikijaribu kulihifadhi jina la mumewe
kichwani mwangu ingawaje sikuona kama lingekuwa na umuhimu wowote
katika harakati zangu, nikabaki nikimtazama tu mama yule.
“Ilikuwaje ukafika humu pangoni? nilimuuliza.
“Walitaka niwaoneshe mahali alipo mume wangu nilipowaambia kuwa si￾fahamu mahali alipo ndiyo wakanishushia kipigo na kunibaka kabla hawaja￾nileta humu pangoni”
“Unadhani ni kwanini walimhitaji mmeo?
“Walitaka kumuua wakidai kuwa ni mmoja wa watu hatari anayestahili kuu￾wawa kwani alikuwa akiharibu mipango yao”
Wakati yule mama akiendelea kuongea mimi akili yangu ilikuwa ikiwaza
juu ya Rwandese Patriotic Front (RPF), kikundi cha kijeshi hatari kilichoku￾wa kikiendesha harakati za kuing’oa madarakani serikali ya Rwanda.
Kumbukumbu zangu ziliendelea kunieleza kuwa ilikuwa ni mwaka jana tu
mwezi Agosti wakati kikundi hicho cha kijeshi kinachoongozwa na Meja Paul
Kagame kilipokubali kuwekeana sahihi na serikali ya Rwanda chini ya Rais
Jùvenal Habyarimana juu ya kusitisha mapigano huko mkoani Arusha nchini
Tanzania. Nilikuwa mbioni kuzama katika fikra hizo pale sauti ya yule mama
iliponikatisha fikra zangu
“Ninaye mtoto mmoja, binti yangu anaitwa Diane Ndikumana, tafadhali
ukifanikiwa kutoka humu mapangoni naomba ukamtafute, anasoma shule ya
wasichana ya Sainte Anne Marie ipo jijini Kigali. Utakaporudi nchini Tan￾zania nakuomba uende naye bila shaka atakuwa salama zaidi akiwa huko.
Nakuomba ukamueleze yaliyonisibu kwani yeye ndiye mwanangu pekee na
sidhani kama nitabahatika kuonana naye tena katika uso wa dunia hii” yule
mama aliendelea kuongea huku akilia na machozi yake yalikuwa yakidon￾dokea mkononi mwangu ingawaje kutokana na afya yake kudhoofika sana
hakuweza kutoa sauti. Uchungu ulinishika sana hadi nikajikuta nikijuta kuja
katika nchi hii ingawaje hata hivyo safari yangu ilikuwa ndani ya majukumu
ya kazi yangu. Ukweli ni kwamba yule mama alikuwa amefikia kwenye ki￾wango chake cha mwisho kabisa cha kukata tamaa na hakukuwa na neno lo￾lote la faraja ambalo lingeweza kumpa tumaini moyoni mwake, hivyo nilibaki
nikihema kwa hasira. Yule mama aliendelea
“Patrick!” yule mama aliniita
“Naam!”
“Wewe ni mwanaume mwenye moyo wa kipekee ambaye sijawahi kumuo￾na katika maisha yangu, angalia hata sasa hutaki kuniacha na unaamini kuwa
utaniokoa tu. Mungu akubariki sana lakini mimi sina muda mrefu tangu sasa
nitakufa”
Kwa kweli uchungu ulinishika sana hivyo nikaishika mikono ya yule mama na kuiminyaminya nikimtia moyo na hapo yule mama akaendelea kuongea
“Ninapesa nyingi sana kwenye akaunti yangu, zinaweza kutosha kumsome￾sha binti yangu hadi chuo kikuu, nenda ukazichukue umsaidie mwanangu na
zitakazobaki chukua. Ukifanikiwa kutoka humu ndani nenda ukaitafute nyum￾ba namba 16Masaka Avenue jijini Kigali, ndani ya chumba changu utapata
kila kitu cha kukusaidia” yule mama aliniambia kwa msisitizo nikawa nam￾sikiliza vizuri na kumuelewa.
“Usijali hutokufa mama, muombe Mungu wako akuokoe” nilimfariji hata
hivyo safari hii yule mama hakuniitikia wala kuung’ang’ania tena mkono
wangu badala yake niliihisi mikono yake ilikuwa ikiiachia taratibu mikono
yangu kama iliyoishiwa nguvu. Nikawahi kuishika ile mikono yake bila tu￾maini lolote la upande wa pili na hapo nikafahamu ni kipi kilichokuwa kik￾iendelea, huzuni ilinishika sana. Nilimtazama yule mama kwa kitambo kisha
nikashusha pumzi ndefu katika hali ya kukata tamaa huku nikiiachia mikono
yake na kujifuta machozi kwa viganja vyangu, yule mama alikwisha kata roho.
Loh! nafsi yangu iliumia sana kwa kuyasikia maelezo yale. Sikuwa niki￾umia na kuhuzunika kwa sababu ya kumuona mtu akikata roho la hasha!, hilo
kamwe lisingenihuzunisha kwani mpaka sasa nilikuwa tayari nimekwisha￾waona watu wengi sana wakikata roho tena katika mazingira yenye mateso
makali kushinda ya huyu mama. Kilichonihuzunisha ni namna watu wale wa
mle pangoni walivyotekwa kibabe na kuteswa bila sababu zozote za msingi.
Nilipogeuka kuwatazama Ikirezi na Jean Pierre Umugwaneza nikagundua
kuwa hata wao pia walikuwa wameshuhudia tukio lile la yule mama kukata
roho pamoja na watu wachache waliokuwa pale jirani yangu. Sikuzungumza
neno lolote kwani sikuona kipi ningepaswa kuongea kwa wakati ule bada￾la yake nilimtengeneza vizuri yule mama, nikatoa heshima zangu za mwisho
nikiwa kama binadamu wa karibu niliyeguswa na kifo cha yule mama na nili￾pomaliza nikamlaza vizuri kando ya ukuta wa lile pango huku moyoni nikiwa
nimeshikwa na huzuni sana.
__________
NILIHISI KUWA TULIKUWA TAYARI TUMEPUMZIKA kwa muda wa
kutosha na tulikuwa tumepata nguvu mpya hivyo niliona ni bora tuendelee na
safari yetu bila kupoteza muda nikawaambia wenzangu na hapo safari ikaan￾za tena huku mimi nikiwa kiongozi wa msafara lakini tukiwa tumempoteza
mwenzetu mmoja. Nikiwa nafahamu kuwa kulikuwa na hatari kubwa ya ku￾endelea kuzunguka mle pangoni bila ya sisi wenyewe kujijua niliamua kuba￾dilisha uelekeo nikiziacha zile njia za pango zilizoonekana kutokuwa na dalili
zozote za kupitwa na viumbe hai na badala yake tukawa tukiufuata uelekeo wa
njia za pango zilizoonesha matumaini ya kutumika na watu. Utaratibu wetu wa
safari bado ulikuwa ni uleule wa kutembea gizani bila ya kuruhusu maongezi
yoyote baina yetu.
Tulimaliza kulivuka pango lile na kuingia kwenye uchororo wa pango
jingine lililoonekana kuwa jembamba kiasi lakini lenye kuturuhusu kupita bila
usumbufu wa aina yoyote, hata hivyo tulijikuta tukikabiliana na utandu mkubwa wa Buibui. Tulipomaliza tu kulivuka pango lile mbele yetu kulikuwa na
njia mbili, moja upande wa kushoto na nyingine inayoenda upande wa kulia.
Tulipofika pale mimi nikawaongoza wenzangu kuifuata ile njia ya upande wa
kushoto.
Ilikuwa ni njia ya pango isiyoeleweka yenye sehemu fulani pana zenye mii￾nuko na miteremko ya hapa na pale. Mwisho wa njia ile tulikutana na mterem￾ko mkali hivyo tukawa tukishuka chini taratibu. Tulipomaliza kushuka chini
tulijikuta tumetokezea kwenye eneo jingine la pango lenye matope mazito la￾kini si mengi sana kama yale tuliyokabiliana nayo kwenye lile pango wakati
nilipokuwa na Jérome Muganza.
Wakati tukiingia kwenye pango lile mimi nikiwa nimetangulia mbele ni￾likuwa wa kwanza kukabiliana na harufu kali ya uvundo iliyopenya puani,
harufu ile mbaya isiyovumilika ilikuwa ikizidi kutufikia taratibu kwa namna
tulivyokuwa tukilifikia lile pango. Kwa kweli nilianza kujisikia kutaka kutapi￾ka na kuna wakati niliwaona wenzangu wakisita kuendelea na safari. Ilikuwa
harufu kali sana ya uvundo iliyotokana pengine na vitu fulani vilivyooza vi￾sivyoeleweka. Nilishtuka na kusita kuendelea na safari huku wenzangu wote
wakiwa nyuma yangu na ile harufu ilizidi kuwa kali mno.
Tulisimama mle pangoni gizani huku kila mmoja akionekana kuzama ka￾tika fikra zake kwa utulivu, pia niliweza kuhisi namna wenzangu walinyoku￾wa na hofu na kwa mara ya kwanza nilijikuta katikati ya maamuzi magumu,
maamuzi ya aidha tuendelee na safari yetu au tugeuze nyuma na kurudi tulipo￾toka. Lakini hata hivyo suala la kurudi nyuma sikutaka kukubaliana nalo huku
nikijiuliza kuwa hata kama tungeamua kurudi nyuma tungekuwa tukielekea
wapi na vilevile sikuona kama ilikuwa ni busara kuikimbia ile harufu mbaya
mle ndani bali tulipaswa kuichunguza na kujiridhisha kuwa ilikuwa ikitokea
wapi na baada ya hapo tungeendelea na safari yetu.
Wakati tukiwa katika hali ile ya sintofahamu ghafla tulianza kusikia makelele
ya popo walioanza kutimka ghafla na kuanza kuzungukazunguka ovyo mle
pangoni bila ya uelekeo maalumu kama waliochanganyikiwa. Nilishtuka na
kushikwa na butwaa huku hofu ikiwa imeanza kunisakama, nikageuka nyuma
na kuwaona wenzangu wakirudi nyuma taratibu na hapo wasiwasi ukanishika.
Hata hivyo sikushawishika kurudi hata hatua moja nyuma, nikasimama pale￾pale na kuyatega vizuri masikio yangu huku bunduki yangu ikiwa imetulia
vema mkononi tayari kuanzisha shambulizi. Wakati nikiendelea kutega ma￾sikio niligundua kuwa zile sauti za wale popo zilikuwa zimeingiliana na sauti
nyingine tofauti za kitu nisichokifahamu na mchanganyiko wa sauti hizo uli￾kuwa ukiongezeka.
Nilishindwa kuendelea kuvumilia nikabonyeza batani ya mwanga mkali
kwenye ile kurunzi niliyokuwa nimeishika mkononi kisha nikamulika mbele
yangu. Nilichokiona kilinifanya nitaharuki, nilipoyatuliza mawazo yangu
vizuri niligundua kuwa nilikuwa nimeanza kutetemeka mwili mzima, ule
mwanga wa ile kurunzi ulikuwa ukichezacheza sambamba na mitetemo ya
mkono wangu.
Mbele yangu lilikuwa limesimama joka kubwa ambalo sikuwahi kuwaza hata siku moja kuwa dunia ingekuwa na joka kubwa kiasi kile, kichwa na
sehemu ya shingo yake ilikuwa imeenea kwenye njia yote ya lile pango. Tu￾likuwa kama wote tumeshtukizana kwani lile joka nalo ni kama lililokuwa
limeshikwa na mshangao kuniona mimi mbele yake. Nilipolichunguza vizuri
nikagundua kuwa joka lile lilikuwa likimalizia kummeza mtu fulani ambaye
mimi sikumfahamu na lilikuwa tayari limemmeza mtu huyo kuanzia sehemu
ya miguu mpaka kiunoni.
Bila shaka mtu yule aliyekuwa akimezwa alikuwa amesumbuana sana na
lile joka hadi kufikia hatua ya lile joka kufanikiwa kummeza kuanzia miguu
na si kichwani kama reptilia wengi wanavyomeza mawindo yao. Yule mtu
alikuwa ameenea vizuri kwenye kinywa cha joka lile kama kijiti kidogo cha
kuchokoa meno kwenye kinywa cha binadamu. Domo lake pana lilikuwa lik￾ijitahidi kumsogeza vizuri yule mtu ili lifanikwe kummeza kwa urahisi zaidi
ingawaje yule jamaa alikuwa akiendelea kupambana nalo kwa kushika huku
na kule akijizuia ili asimezwe.
Lile joka sasa lilikuwa likinitazama kwa uchu katika namna ya kama lile
joka nililopambana nalo kule pangoni wakati nilipokuwa na Jérome Muganza.
Niliyazungusha macho yangu kutazama pale pembeni yake na hapo nikaona
kitu kilichokuwa kikitoa harufu ile mbaya. Lile joka lilikuwa limetapika na
matapisha yake yalikuwa yamesambaa ovyo mle ndani, nilipoyatazama vizuri
matapishi yale nikaona baadhi ya mifupa na mafuvu ya watu. Kulikuwa na
mafuvu matatu ya watu na hapo nikajua kuwa lilikuwa limetapika muda mfupi
uliopita.
Nikiwa nimetaharuki nilijaribu kuituliza akili yangu huku nikifikiria namna
ya kumuokoa yule jamaa aliyekuwa akiendelea kumezwa na lile joka, mara
nikajikuta nikishawishika kutaka kilifyatua risasi ili limuachie yule jamaa hata
hivyo nilipokuwa nikiendelea kutafakari niligundua kuwa risasi zisingeweza
kuleta ukombozi kwani lile joka lilikuwa kubwa sana kiasi kwamba kwa risasi
za bunduki niliyokuwa nayo zingemkuna tu kidogo kama mwiba wa mchon￾goma kwenye ngozi ya Tembo.
Nilipomtazama yule mtu aliyekuwa akimezwa na lile joka nilimuona aki￾jitahidi kuniongelesha maneno fulani ambayo sikuweza kuyasikia vizuri in￾gawaje yule mtu alikuwa akinitazama na wakati huohuo lile joka lilikuwa li￾membakiza kummeza sehemu ya kifua hadi kichwa kwani nusu ya kiwiliwili
chake ilikuwa tayari imeshaingia kinywani mwa yule joka.
“Sikusikii vizuri” nilimwambia yule jamaa kwa lugha ya kiswahili pasipo
kujua kama alikuwa akinielewa au lah! pale nilipoona hatuelewani kutokana
na suati yake kuwa hafifu.
“Wanakuja na muda si mrefu watafika hapa na kuwakamata” yule mtu
aliongea kwa sauti huku akionekana kibanwa na akiitumia nguvu yake ya
mwisho iliyosalia mwilini
“Akina nani? nilimuuliza huku nikishindwa kumuelewa
“Askari wa Bosco Rutaganda mliowatoroka, mimi pia nilikuwa nikiwatoro￾ka wao bahati mbaya ndiyo nikakamatwa na hili dubwana” yule mtu aliende￾lea kuongea huku akimezwa taratibu na lile joka na mimi nikabaki nimeduwaa kama niliyepigwa na shoti ya umeme.
“Wako wapi hao askari?
“Nimewaacha nyuma wananifukuza nyie kimbieni mkichelewa watawakuta
hapa”
“Unaifahamu njia ya kutokea humu ndani? nilimuuliza tena yule mtu hata
hivyo nilikuwa nimeisha chelewa kwani yule jamaa alikuwa tayari amekwis￾hapotelea kwenye lile domo la lile joka. Lile joka lilimalizia kummeza yule
jamaa likiwa kama lililosukutua kidogo huku likiutoa ulimi wake nje na ku￾jipangusa vizuri kwenye kingo za domo lake kisha lilipomaliza likayasima￾misha macho yake kunitazama kama linalonipigia mahesabu ya kunikamata.
Kwa kweli hofu ilinishika sana, nikaanza kurudi kinyumenyume taratibu ni￾kikwepa kulipa mgongo na hapo nikaliona nalo pia likijisogeza kwa hila kuni￾fuata. Mpaka wakati huu sikufahamu kama wale wenzangu walikuwa bado
wapo nyuma yangu au walikwishakimbia na kuniacha pale peke yangu, kwani
sikuweza kugeuka nyuma kuwatazama. Nikawambia wale watu nyuma yangu
wakimbie kurudi kule tulipotoka hata hivyo hakuna aliyenijibu hivyo nikajua
wenzangu tayari walikwishakimbia.
Mpaka hapa nilijiona sina ujanja tena wa kulitoroka lile joka kwani lilioneka￾na kuwa makini kunitazama nyendo zangu bila ya kutoa mwanya wowote wa
kilihadaa. Lilikuwa ni joka aina ya chatu mkubwa mwenye mchanganyiko wa
ngozi yenye mabakamabaka ya rangi nyeusi, njano na kahawia na angalau hili
lilinipa faraja kidogo kuwa nilikuwa nikikabiliana na joka kubwa lakini lisilo
na sumu.
Wakati nikirudi kinyumenyume taratibu na kwa tahadhari ya hali ya juu
mara nilishtushwa na sauti ikiniita nyuma yangu kwani mpaka wakati huu
nilikuwa nikijua kuwa nilikuwa peke yangu eneo lile na wale wenzangu walio￾kuwa nyuma yangu niliamini kuwa walikwishakimbia. Hivyo sauti ile nyuma
yangu ilinishtua sana na bila kujishauri nikageuka nyuma kutazama na hapo
nikawa nimefanya kosa kubwa sana ambalo sikulitegemea. Kumbe ile sauti
iliyoniita ilikuwa ni ya Ikirezi na alikuwa akiniita kunitahadharisha kuwa ni￾kimbie, niligundua hivyo baada ya kugeuka nyuma na kumtazama.
Ikirezi alikuwa hatua chache nyuma yangu lakini nilikuwa nimefanya kosa
kubwa kugeuka kwani nilikuwa nimetoa mwanya kwa lile joka kunishambu￾lia. Kwa kasi ya ajabu nilishangaa nikichotwa hewani, nikajaribu kufurukuta
bila ya mafanikio na hapo nikamsikia Ikirezi akipiga yowe la hofu huku aki￾kimbia. Lile joka lilikuwa limenikamata mdomoni kisha likanipindua hewani
kichwa chini miguu juu hata hivyo sikuiachia ile kurunzi mkononi wala zile
bunduki. Lile joka lilinigeuzageuza zaidi ya mara nne likinivuruga akili yangu
kisha likanirudisha katika hali ya kawaida kichwa kikiangalia juu hata hivyo
nilijihisi kizunguzungu na ile harufu mbaya iliyokuwa ikitoka kinywani mwa
lile joka ilizidi kunifanya nitake kutapika.
Lile joka lilijitahidi sana kuibana mikono yangu niliyoinyanyua juu bila ma￾fanikio na kuona hivyo likaamua kujiviringisha mwilini mwangu na kuniweka
kati, likawa limenibakisha sehemu ya kichwa na kifua tu, nywele zilinisimama
mwilini kwa hofu ya kuzungukwa na joka lile. Nilipojitahidi kufurukuta ili nijinasue nililiona likiukaza vizuri mwili wake
na kunibana kisawasawa na hapo nikaanza kuhema kwa shida kwani sehemu
ya tumbo langu ilikuwa imebanwa vibaya na lile joka na hapo nikajua kama
ningeendelea kufurukuta lile joka lingezidi kunibana na hata ile nafasi ndogo
ya kuvuta pumzi niliyobakiwa nayo nisingeipata tena hivyo nikaamua kuji￾legeza kama mfu na hapo nikaliona lile joka likitulia. Liliendelea kunitazama
kwa karibu na hapo nilijikuta nikikabiliana na harufu mbaya ya pumzi iliyoku￾wa ikipenya kinywani mwake hata hivyo sikudanganyika kuiachia ile kurunzi
wala ile bunduki mkononi mwangu.
Ulipita kama muda wa dakika tano hivi lile joka likiendelea kunitazama na
huku mimi nikiwa nimejikausha kama niliyekufa ingawaje nilikuwa nimeka￾ta tamaa sana na hofu ilikuwa imenishika sana. Wakati huo mawazo mengi
yalikuwa yakipita kichwani mwangu huku nikiiona dunia kama iliyokuwa
ikinielemea, nikajikuta nikiwawaza wale askari wa Kanali Bosco Rutaganda
ambao walikuwa wakimfukuza kwa nyuma yule mtu aliyetangulia kumezwa
na hili joka.
Niliwakumbuka Ikirezi, Jean Pierre Umugwaneza na wale watu wengine
niliyokuwa nimeongozana nao na hapo nilihisi kuwa wasingeweza kufika
mbali endapo wangeamua kukimbia kwani walikuwa hawazifahamu zile njia
za pango hivyo wale askari wa Kanali Bosco Rutaganda hatimaye wange￾wakamata hata kabla hawajafika kokote. Hata hivyo nilijihisi nilikuwa mzem￾be sana kwa kumkimbia binadamu mwenzangu na kuja kukamatwa na kumez￾wa na joka kama hili lisilokuwa na akili hata moja kichwani.
Niliisikia sauti ya Ikirezi ikiendelea kupiga mayowe hata hivyo kadiri muda
ulivyokuwa ukizidi kwenda ile sauti ilianza kupotea masikioni mwangu na
hatimaye kukoma kabisa na hapo hofu ilianza kuniingia kwa kuona kuwa nili￾kuwa nimetelekezwa peke yangu.
Nilifahamu kuwa sasa nilikuwa sina ujanja tena na mwisho wangu ulikuwa
umewadia. Kwa kweli nilijihisi kuchanganyikiwa kwani mawanzo mengi ya￾kawa yakipita kichwani mwangu kama ninayeona mauzauza mbele yangu. Ni￾kiwa katika hali ile niliyafumbua macho yangu taratibu na kwa siri kulitazama
tena lile joka na hapo nikaliona kuwa lilikuwa bado likiendelea kunitazama.
Wale popo waliokuwa mle pangoni walikuwa wakiendelea kuzungukazungu￾ka na baadhi walikuja na kulipiga lile joka kwa mbawa zao kichwani. Nilifu￾rahi sana kuwaona wale popo wakilisumbua lile joka huku nikijua kuwa kama
ile hali ingeendelea vile lile joka lingeendelea kupoteza umakini kwangu.
Muda uliendelea kusonga bila kuona dalili zozote za lile joka kuniachia
ingawa nilianza kuliona kuwa lilikuwa limeanza kupoteza umakini kwangu.
Mbinu yangu ya kujilegeza na kujidai mfu baada ya muda mrefu kidogo kupita
nikaanza kuiona ikianza kuzaa matunda kwani lile joka lilianza kujifungua
taratibu huku likiweka kituo kila mara na kunitazama kama ningeanza tena
kufurukuta.
Mimi niliendelea kujikausha huku nikiliona lile joka likitoa ulimi wake
wenye pacha na kuurudisha ndani kwa nyakati tofauti. Hata hivyo furaha yan￾gu ilitoweka ghafla muda mfupi baada ya lile joka kumaliza kujifungua toka mwilini mwangu pale nilipoliona likianza kujinyonganyonga taratibu huku
likijisogeza karibu yangu na hapo nikaanza kupatwa na wasiwasi kuwa huenda
lilikuwa likitengeneza mkakati wa kunimeza mzimamzima. Nikiwa nafahamu
kuwa hii ingekuwa nafasi yangu ya mwisho ya kujitetea sikutaka kuendelea
kuigiza kuwa mimi ni mfu hivyo nikaikamata vizuri bunduki yangu mkononi
huku macho yangu sasa yakiwa makini kulifuatilia kwa ukaribu nyendo zake.
Wakati nikiwa najiandaa mara nilisikia kelele za watu waliokuwa wakikim￾bia kuja upande ule wa pango tuliokuwa mimi na lile joka hata hivyo sikutaka
kufanya tena yale makosa kama ya wakati ule ya kushawishika kugeuka na ku￾watazama watu wale kuwa wangekuwa ni akina nani, kwani nilifahamu kuwa
kosa hilo lingeweza kutoa mwanya na nafasi nzuri kwa lile joka kunimeza
mzimamzima. Hivyo sikugeuka kuwatazama wale watu na badala yake macho
yangu yakawa makini kulitazama lile joka kila tukio lililokuwa likifanya.
Nikaliona lile joka kuwa lilikuwa limeanza kukusanya nguvu ya kunimeza
nami macho yangu yakawa yameweka kituo kukitazama kichwa chake kwani
hicho ndiyo nilifahamu kuwa ningepaswa kushughulika nacho ingawaje ukub￾wa wake ulikuwa ukinitisha.
Wakati haya yakiendelea zile sauti za wale watu waliokuwa wakikimbia
kuja ule upande wa pango tuliokuwa mimi na lile joka sasa zilikuwa zime￾karibia sana na zilikuwa zimelishtua hata lile joka, likawa kama linalotaka
ligeuke kisha litazame upande ule zile sauti zilipokuwa zikitokea lakini wakati
huohuo likinichunga nisilitoroke.
Lakini hatimaye liliamua limalizane kwanza na mimi harakaharaka kabla
halijaendelea kushangaa upande ule wa wale watu hivyo liliniwahi kwa kuzu￾ngusha kichwa chake kwa wepesi wa hali ya juu ili linikamate hata hivyo
halikufanikiwa kwani niliinama chini nikalikwepa na kichwa chake kikapita
kwa kasi ya ajabu na kusababisha upepo mkali mithili ya kimbunga kilichoni￾yumbisha vibaya sana hata hivyo sikutaka kuzubaa na muda uleule nikayatupa
macho yangu kuutazama ule uchochoro mdogo wa njia ya pango tuliokuja na
wenzangu ambao hawakuwa mbali na pale nilipokuwa nimesimama na wakati
huohuo niligeuka kulitazama tena lile joka na hapo nikakutana na shambulizi
la pili.
Lile joka likawa kama lililoshikwa na hasira baada ya pigo lake kuniko￾sa hivyo lilikivurumisha kichwa chake na kunipiganacho likanitupa hewani
huku nikilisikia likitoa mlio fulani wa hasira. Kwa ile kasi nikaenda kujipigiza
kwenye ukuta wa pango ambako nilipiga yowe kali la maumivu nikaanguka
chini huku nikisikia maumivu makali mno hata hivyo sikuiachia ile kuruzi
wala ile bunduki mkononi.
Vumbi kali likawa limetimka mle ndani, nikaaza kukohoa ovyo hata lile
joka nikawa silioni vizuri mbele yangu hata hivyo nilijitahidi kusimama hara￾ka nikitazama huku na kule. Zile vurugu zikawa zimewashtua tena wale popo
hivyo wakaanza kunifuata na kunizunguka wakinipiga kwa mbawa zao ngu￾mu kichwani. Nikajitahidi sana kuwafukuza bila mafanikio huku nikijitahidi
kuufunika uso wangu. Nilipoona wanazidi kuongezaka na kuniuma nikaamua
kuizima ile kurunzi mkononi na hapo giza zito likatanda mle pangoni hata hivyo niliendelea kukohohoa sana kutokana na lile vumbi kali la mle ndani.
Nilikohohoa sana na hatimaye nikapunguza kukohoa na kuacha kabisa huku
nikihema ovyo na hapo nikawa nasikia maumivu makali kwenye bega langu
la kushoto, wale popo wakawa wameacha kunishambulia wakaondoka, nika￾baki nikitweta kwa hofu. Kwa mbali nililisikia lile joka likijisogeza taratibu
kuja ule upande wangu nikajua kuwa lilikuwa limenisikia wakati nilipokuwa
nikikohoa.
Sikutaka kuendelea kukaa sehemu ile hivyo nikaanza kutembea taratibu
kwa kupapasa ukuta wa pango wakati huohuo nikiomba kimoyomoyo kuwa
nisije nikangogana nalo. Hata hivyo nilifika eneo fulani ikanibidi nisimame
kwani ni kama lile joka lilikuwa mbele yangu likinitazama kwa namna macho
yake makubwa yaliyokuwa yakimeremeta, nikajua lilikuwa likiniona gizani.
Sikutaka kuendelea kusubiri zaidi kwani ujasiri mpya ni kama ulikuwa
umeniingia hivyo nikaikamata kurunzi yangu vyema na kuiwasha kisha ni￾kalimulika lile joka usoni na hapo nikajikuta nikitazamana nalo ana kwa ana.
Bila ya kupoteza muda nikaizugusha bunduki yangu toka begani na kuibana
vizuri kwapani na hapo sikulipata lile joka hata sekunde moja ya kutafakari
nikalifyatulia risasi mfululizo bila ya kujali milio ya risasi zile ingesikika na
wale askari wa Kanali Bosco Rutaganda au lah!.
Ukweli ni kwamba sikutarajia kuwa risasi zile zingeliua lile joka kwani lil￾ikuwa kubwa mno lakini angalau zilifanya kazi. Zile risasi zikafanikiwa kuli￾vuruga sehemu ya mbele ya domo lake na nyingine zikalijeruhi jicho lake la
kushoto, lile joka likakasirika na kunirukia hata hivyo nilikwisha liona hivyo
nikalikwepa na hapo likajibamiza kwenye ukuta wa pango lile na kuubomoa.
Vumbi jingi likatimka mle ndani na muda uleule nikaizima ile kurunzi na ku￾jirusha upande mwingine uliokuwa salama. Sasa nikawa nauwazia ule ucho￾choro tuliokujia ambao toka pale nilipokuwa ulikuwa kiasi cha umbali usio￾pungua hatua kama sita.
Kitendo cha kuizima ile kurunzi nikawa nimelipotezea shabaha lile joka
hivyo likawa likijipigiza huku na kule ukutani na sehemu ya dari ya lile pango
na hapo mabonge makubwa ya udongo wa pango lile yakawa yakimegeka
na kuangukia mle pangoni. Vumbi likaongezeka na muda uleule nikawasikia
wale popo wakianza tena kuzunguka ovyo mle pangoni hata hivyo kwa kuwa
nilikuwa nimeizima ile kurunzi hawakunifuata. Wakati lile joka likiendelea
kujipigizapigiza ukutani kwa hasira mara nilizisikia zile kelele za watu walio￾kuwa wakikimbia wakiingia mle pangoni tulipokuwa mimi na lile joka halafu
muda huohuo kurunzi yenye mwanga mkali ikawashwa ikimulikamulika mle
pangoni.
Nilitupa macho yangu kutazama ule mwanga ulipotokea na hapo nikawao￾na wanajeshi sita na bunduki zao mkononi nao wakawa wameniona kwenye
ile pembe niliyojibanza. Haraka wakazielekeza bunduki zao kwangu ili wani￾lenge hata hivyo hawakufanikiwa kwani muda uleule nililiona kundi kubwa la
popo likiwavamia na kuanza kuwashambulia, wakawa wakijitahidi kupamba￾na nao hata hivyo hawakuonekana kufanikiwa kwani lile joka lilikuwa tayari
limeshageuka na kuwaona. Kwa kasi ya ajabu na wapesi usioelezeka lile joka likajirusha na kumchota
yule mwanajeshi aliyekuwa ameshika ile kurunzi, kwa hofu yule mwanajeshi
akaiachia ile kurunzi aliyoshika pamoja na bunduki yake vyote vikaanguka
chini lakini ile kurunzi ilikuwa imeangukia juu ya jiwe dogo lililokuwepo pale
chini na kugeuka ikiwamulika wale wanajeshi waliobaki. Ilikuwa ni nafasi
nzuri ambayo sikuwahi kuifikiria, nikaikamata vizuri bunduki yangu na ku￾wafyatulia risasi zisizo na idadi wale wanajeshi na hapo nikasika vilio vya
mayowe na maumivu, wote nikawa nimewapata.
Niligeuka nyuma kulitazama tena lile joka nikaliona lilikuwa limeshaanza
kunisahau na sasa lilikuwa likijishughulisha kummeza yule mwanajeshi lil￾ilomkamata na hiyo ilikuwa ni nafasi nzuri kwa mimi kulitoroka lile eneo.
Nikaipiga risasi moja ile kurunzi ya yule mwanajeshi iliyokuwa pale chini
juu ya lile jiwe ikiendelea kumulika na hapo ikachanguka vipandevipande na
kuzimika sasa mle ndani kukawa na giza zito.
Nikaaanza kuambaa ambaa na ule ukuta wa pango taratibu hadi nilipoufikia
ule uchochoro tuliokujia na wenzangu nikauingia hata hivyo lile joka lilikuwa
limeniona likaniwahi lakini halikuweza kunipata kwani liliishilia kunipangusa
tu buti zangu miguuni na kupasua sehemu ya mdomo wa pango lile. Chupu￾chupu linikamate hata hivyo niliwahi kugeuka na kulishambulia kwa risasi na
hapo likarudi nyuma na kuanza tena kujipigiza ukutani na kwa kuwa nilikuwa
na hakika kuwa lisingeweza kupenya kwenye uchororo ule mdogo niliouingia
sikuwa na shaka yoyote hivyo kwa mara ya pili nikawa nimefanikiwa kupon￾yoka kwenye mdomo wa kifo.
Niliuparamia ule uchochoro wa pango niliouingia nikapenyapenya na ku￾tokezea upande wa pili huku nikiwa natweta isivyokawaida. Hata hivyo nili￾jua kuwa wale askari wa Kanali Bosco Rutaganda pamoja na lile shambu￾lizi nililowafanyia bado lisingekuwa ndiyo mwisho wao hivyo kwa vyovyote
wengine wangekuwa nyuma yao wakiendelea na msako wa kututafuta hivyo
endapo ningeendelea kuzubaa eneo lile hatimaye wangenifikia na sikupenda
kuitegemea tena bahati.
Nilifika mwisho wa uchochoro ule na kusimama huku nikiwa nimechoka
sana, giza lilikuwa zito mno mbele yangu na sikuweza kuona kitu chochote
wala kuweza kuhisi kuwa pale nilikuwa wapi. Akili yangu yote ilikuwa iki￾wawaza Ikirezi, Jean Pierre Umugwaneza na wale watu wengine niliyokuwa￾nao kwenye ule msafara wa kutoroka mle pangoni hapo awali. Niliikumbuka
ile sauti ya Ikirezi alipokuwa akipiga kelele za hofu wakati nilipokuwa niki￾kamatwa na lile joka na sikuweza kufahamu kuwa ilikuwa imepotelea wapi.
Pango zima lilikuwa limetawaliwa na ukimya usio wa kawaida ingawaje may￾oni sikukubali kuwa ule ungekuwa ukimya salama.
Nikiwa bado nimesimama lile eneo nilianza kuwaita Ikirezi na Jean Pierre
Umugwaneza bila mafanikio wala dalili zozote za kuzisikia sauti zao zikii￾tikia, moyo wangu ukazizima kwa hofu na wasiwasi nikaanza kuhisi kuishiwa
nguvu na kuanza kukata tamaa. Nilifahamu fika kuwa ningeweza kujichagulia
njia yangu na kutoroka mle pangoni peke yangu lakini sikupenda nitoroke
peke yangu mle pangoni bila ya kuwasaidia wale wenzangu kwani hivyo ndivyo nafsi yangu ilivyokuwa imedhamiria kufanya lakini sasa hilo nilili￾fahamu kuwa lisingewezekana tena kutekelezeka kwani sikufahamu kuwa
wale wenzangu walikuwa wameelekea wapi na kutokana na yale mapango
yalivyokuwa isingekuwa rahisi kwangu kuwatafuta.
Niliendelea kuita huku nikimulikamulika kwa ile kurunzi yangu mkononi,
sikufanikiwa kumuona mtu yeyote eneo lile badala yake nilijikuta nikikabi￾liwa na ghasia za popo wengi waliokuwa eneo lile hivyo ikabidi niizime ile
kurunzi huku nikijihisi kukata sana tamaa sana. Nilisimama huku nikiwa
nimekata tamaa sana nikawa najishauri niufuate uelekeo gani katika pango lile
lililokuwa mbele yangu.
Kadiri muda ulivyokuwa ukizidi kusonga nikaanza kuhisi kuzidi kuchan￾ganyikiwa na baada ya kujishauri sana hatimaye nikaamua kuushika uelekeo
wa upande wa kulia wa lile pango huku nikitembea kama niliyeishiwa nguvu.
Wakati nikiendelea na safari yangu nilihisi maumivu makali sana kwenye bega
langu la kushoto, maumivu ambayo niliyahisi kuwa yalikuwa yakiongezeka
taratibu kwa kadiri muda ulivyokuwa ukienda hata hivyo sikusimama.
Nilifika mwisho wa pango lile na kwa upande wa kulia nilikutana na njia
mbili pacha mbele yangu, nikasimama na kuanza kujishauri kuwa nichukuwe
uelekeo upi kati ya njia zile mbili. Nilipoona kuwa muda unazidi kusonga
hatimaye nikawa nimepata wazo ambalo nililiona kuwa lingenisaidia. Nikai￾washa ile kurunzi yangu mkononi na kuanza kumulika sehemu ya chini ya
eneo lile huku nikifahamu kuwa kwa vyovyote wale popo waliokuwa eneo
lile wangekuja na kunishambulia baada ya kuuona ule mwanga wa kurunzi,
hata hivyo niliwapuuza wale popo na badala yake macho yangu yaliendelea
kutazama pale chini kwa umakini.
Hatimaye nilifurahi kuziona alama za nyayo za miguu ya watu katika
mchanga laini uliokuwa eneo lile, alama hizo nyingi zilikuwa zimepita na
kuushika uelekeo wa upande wa kushoto kati ya vile vichochoro viwili pacha
vilivyokuwa mbele yangu na hapo nikajua kuwa kwa vyovyote watu wale
wangekuwa ni wale wenzangu. Nikazima ile kurunzi na kuanza kuzifuatilia
zile nyayo nikiingia katika ule uchochoro wa upande wa kushoto na kila nili￾pohisi kuwa nyayo zile zilikuwa mbioni kunipotea niliiwasha tena ile kurunzi
na kumulika chini kisha nikazima na kuendelea na safari yangu. Sasa zile ala￾ma za nyayo za watu ndiyo zikawa mwongozo wangu.
Bado niliendelea kuzifuatilia zile nyayo katika ule uchochoro. Ulikuwa
ni uchochoro mrefu na mpana wenye mchanga mwingi kwa chini. Tumaini
jipya la kuweza kukutanana wale wenzangu mbele ya safari likawa limeanza
kuchipua upya kadiri zile alama za nyayo za watu zilivyokuwa zikiniongoza
mbele yangu hata hivyo furaha yangu ilikuwa haijakamilika kila nilipokuwa
nikifikiria uwezekano wa kukutana na joka lingine mbele ya safari. Kwa kweli
nilikuwa nimeanza kuchoka kupambana na majoka yale hatari na makubwa
yaliyokuwa ndani ya mapango haya na nilianza kuona kuwa kungekuwa na
uwezekano mkubwa wa kupoteza mapambano hayo pale endapo ingetokea
kukutana tena na joka kubwa kama lile lililonikosakosa muda mfupi uliopita.
Nilifika mwisho wa uchochoro ule nikakutana na makutano ya njia nne za pango mbele yangu, njia moja ikiendelea mbele yangu, nyingine kushoto na
nyingine kulia kwangu. Kufikia pale nilishindwa tena nichague uelekeo upi
hivyo niliiwasha tena ile kurunzi kumulika chini na hapo furaha yangu ika￾toweka ghafla nilipoona kuwa zile alama za nyayo za ile miguu ya wale watu
zilikuwa zimeishia pale na kutoweka kusikojulikana na badala yake niliio￾na alama kubwa ya mburuto uliotoka kwenye ule uchochoro wa kushoto na
kuingia ule uchochoro wa kulia.
Alama hiyo ya mburuto ule mkubwa ilizidi kunitia mashaka, hisia zangu
zikaanza kuniambia kuwa mburuto ule ungekuwa wa moja ya majoka makub￾wa yaliyokuwa mle ndani ya mapango. Niliendelea kuchunguza kwa makini
pale chini na sikuweza tena kuziona zile alama za nyayo za wale watu kati￾ka uelekeo wa ile njia ya ule mburuto mkubwa ulikopotelea. Nilitembea kwa
tahadhari nikiwa na wasiwasi mwingi sana kwa kadiri nilivyokuwa nikizitupa
hatua zangu kuufuata ule mburuto. Nilipofika mbele niliuona ule mburuto uki￾wa umechepuka na kuingia kwenye uchochoro wa upande wa kushoto na ku￾likuwa na sehemu iliyobomoka katika ukuta wa uchochoro ule kiasi kwamba
nikaanza kuhisi kuwa huenda kulikuwa na purukushani zilizokuwa zimetokea
eneo lile.
Niliingia kwenye uchochoro ule na kuendelea kutembea kwa tahadhari zote
huku kila mara nikiiwasha ile kurunzi kumulika mbele yangu kabla ya kuizima.
Ule uchochoro ulikuwa mwembamba sana na uliokuwa ukishuka sehemu ya
chini ya lile pango hata hivyo kwa wakati huu uchochoro ule ulionekana kuta￾nuliwa kidogo na baadhi ya kuta zake zilikuwa zimevunjikavunjika bila shaka
kutokana na jitihada za kiumbe kilichopita eneo lile kuonekana kulazimisha
kupita.
Niliendelea kushuka na uchochoro ule na mbele kidogo ule uchochoro uli￾chepuka upande wa kulia, niliendelea kuuona ule mburuto ukiendelea kushuka
kwenye ule uchochoro. Baada ya kutembea umbali mfupi niliuona tena ule
uchochoro ukikunja kona upande wa kushoto na kuteremka sehemu ya chini
ya lile pango. Niliendelea kuufuata ule uchochoro huku nikiwa bado naende￾lea kuuona ule mburuto mbele yangu, ule mburuto uliishia kwenye pango pana
na kubwa lililokuwa kule chini. Wasiwasi mwingi ukiwa umenishika nilite￾remka kule chini ya pango taratibu na wakati huo nikaanza kuhisi vumbi kali
eneo lile na ukingo wa uchochoro ule ulionekana kubomoka.
Giza lilikuwa zito mno kule chini na sikuweza kuhisi chochote hivyo hati￾maye nilitoa kichwa na kuchungulia kwenye lile pango kule chini huku nikii￾washa ile kurunzi. Kwa mara nyingine nikajikuta nikitaharuki kwa hofu, lile
pango lilikuwa kubwa mno na chini yake kulikuwa na tope zito lililochang￾anyikana na majimaji kila mahali. Nilipomulika kule chini nikaziona maiti za
watu watano zikiwa zimelala juu ya tope lile na nilipowatazama vizuri wale
watu nikangudua kuwa miongoni mwao watu watatu walikuwa wanawake na
wawili walikuwa wanaume na wote walikuwa uchi wa mnyama, hapo nikaf￾ahamu kuwa watu wale walikuwa miongoni mwa wale watu niliokuwa nime￾ongozana nao katika ule msafara wa kutoroka.
Nilianza kuwaita wale watu bila yoyote kati yao kuitikia wala kuonesha dalili zozote za kushtuka, nikaizunguka kurunzi yangu kumulika upande wa
kulia wa pango lile na hapo nilishtuka kwani nilijikuta nikitazamana na joka
lingine lakini halikuwa kubwa kama lile la awali.
Nililitazama kwa udadisi joka lile nalo likageuka kunitazama, lilikuwa liki￾fanana na lile joka la mwanzo lenye mstari wa njano shingoni, joka lile liliku￾wa kwenye ile jamii ya wale nyoka wenye sumu kali kutokana na mwonekano
wake na hapo nikatambua kuwa ndiyo lililokuwa likiwafukuza wale watu na
hatimaye kuwauma hadi kufa kwa sumu yake kali. Sasa joka lile lilikuwa li￾megeuka kwa hasira kunitazama, hofu ikanishika hata hivyo sikushawishika
kutaka kutimua mbio kwani nilifahamu kuwa nisingefika mbali kabla ya lile
joka kunifikia na hatimaye kuniuma.
Wakati nikiendelea kufikiria kitu cha kufanya nililiona lile joka likijisoge￾za taratibu karibu yangu na hapo nikajua kuwa lilikuwa likinipigia mahesabu
ya kunishambulia. Sikuona sababu ya kuendelea kusubiri nikaikamata vizuri
bunduki yangu huku mahesabu yangu yote yakiwa kwenye kichwa chake hata
hivyo sikufanikiwa kupata muda wa ziada wa kuendelea kujiandaa kwani ni
kama lile joka lilikuwa limeyashtukia maandalizi yangu na hivyo kufumba na
kufumbua lile joka lilikuwa tayari limekwisha nifikia pale nilipo.
Likaanza kujiandaa kunifanyia shambulizi moja la kutaka kuniuma huku
likiwa tayari limefura kwa hasira, kufumba na kufumbua kwa kasi ya ajabu
joka lile likajirusha kuniuma lakini ikawa kama bahati nikawahi kulikwepa
nikijirusha pembeni na hapo likaenda kujipigiza kichwa chake kwenye ule
ukuta wa pango umbali mfupi toka pale nilipokuwa na kuacha alama kub￾wa ya tundu ukutani. Kichwa chake kilikuwa kimetokezea upande wa pili wa
ukuta ule lakini huku nyuma lile joka lilinichapa kwa mkia wake na kunitupa
upande mwingine wa lile pango. Nikajibamiza kwenye ukuta wa pango lile na
kuanguka chini huku nikisikia maumivu makali mno hata hivyo sikuiachia ile
kurunzi wala ile bunduki yangu mkononi.
Lile joka lilifurukuta na kufanikiwa kujitoa toka kwenye lile tundu lililoin￾giza kichwa chake huku ule mkia wake ukiendelea kujipigapiga huku na kule
hata hivyo nilifanikiwa kuyakwepa mapigo yake yote. Lilimaliza kujichomoa
toka kwenye lile tundu kisha likageuka na kusimama huku likiwa limefura
kwa hasira.
Sikutaka kupoteza muda tena kwani nilifahamu kuwa hii ndiyo ingekuwa
nafasi yangu ya kipekee ya kuliwahi na muda uleule nikaanza kulifyatulia
risasi mfululizo kuelekea usawa wa kichwa chake. Hakika risasi zile zililipata
kisawasawa joka lile na kufanikiwa kuifumua vibaya sehemu ya kushoto ya
kichwa chake na hapo likatoa mlio wa ajabu ulioyaumiza masikio yangu mlio
huo ukisambaa pengine katika sehemu kubwa ya pango lile huku lenyewe
likijipiga kichwa na kuutupa mkia wake huku na kule na hapo vumbi kali
likatimka mle ndani. Hata hivyo mimi sikusitisha mashambulizi yangu, nilien￾delea kulimiminia risasi kukilenga kichwa chake na hapo likawa likijitahidi
kuzikwepa bila mafanikio.
Niliendelea kulifyatulia risasi mpaka hadi pale risasi ziliponiishia na hapo
nikaitupa ile bunduki ili niichukuwe bunduki nyingine lakini ilikuwa ni muda huohuo pale nilipoliona lile joka likiangukia usawa wangu, nikawahi kulikwe￾pa. Lilipoanguka chini nikaiwasha ile kurunzi yangu na kulimulika lile joka
na hapo nikagundua kuwa nilikuwa nimekisambaratisha vibaya kichwa chake
kwa zile risasi.
Pale chini lilipoangukia lile joka liliendelea kujinyonganyonga kiwiliwili
chake na kwa kweli nilikuwa nimefikia kikomo cha hofu yangu. Nilihisi kuwa
jasho lilikuwa likinitoka kila mahali mwilini mwangu na mapigo ya moyo ya￾likuwa yakinienda mbio isivyo kawaida, nikabaki nimesimama kama sanamu.
Hofu ikiwa imenishika sikuona sababu ya kuendelea kusubiri mle ndani
hivyo nikaanza kunyata kuelekea kwenye ule uchochoro niliyokujia na akili
yangu sasa ilikuwa ni kuondoka haraka eneo lile kabla hatari nyingine hai￾janifikia. Nilifanikiwa kuufikia uchochoro ule na kabla ya kuuingia ikanibidi
nigeuke nyuma kumulika baada ya sauti nyingine ya mburuto kuanza kusikika
mle pangoni.
Nilichokiona kilinifanya nitake kuzimia, kumbe ile sauti ya mburuto iliy￾okuwa ikivuma mle pangoni ilikuwa ni ya joka lingine kama lile nililopambana
nalo mle ndani na lilikuwa likija mle pangoni bila shaka kumtafuta mwezake.
Joka lile lilikuwa limechungulia kupitia tundu moja lililokuwa kwenye kona
ya ukuta wa pango lile na muda mfupi uliofuata nililiona lile joka taratibu
likianza kujipenyeza kwenye lile tundu kuingia mle pangoni.
Nilihisi kutaka kuchanganyikiwa kwani nilikuwa nimechoka sana na hivyo
nisingekuwa na uwezo wa kupambana tena na joka lingine kubwa kama lile
kwani nilihisi kuwa ule ushindi niliokuwa nikiupata ni kama ulikuwa wa baha￾ti tu na nijuavyo mimi bahati haikuwa na mazoea kwa mtu mmoja.
Sikutaka kupoteza muda nikaingia kwenye ule uchochoro cha pango na
kuanza kutimua mbio bila ya kugeuka nyuma na moyo wangu ulikuwa ukien￾da mbio sana. Nilipofika mwisho wa ule uchochoro nikaingia upande wa kulia
kushika njia nyingine ya pango, niliendelea kutimua mbio bila ya kuelewa
kuwa nilikuwa nikielekea wapi. Niliingia kona hii na kutokezea ile nikaiacha
njia moja na kuingia nyingine ilimradi sikutaka tena kusimama huku nikihofia
kuwa lile joka lingekuwa nyuma yangu likinifukuza.
Kwa kweli nilijihisi kichanganyikiwa na damu yote mwilini mwangu ni
kama ilikuwa imehamia usoni mwangu huku kichwa kikinigonga sana hivyo
nilihisi nguvu zilikuwa zikiniishia na bega langu la kushoto lilikuwa likiniuma
sana. Niliendelea kukimbia mpaka nilipofika eneo fulani mle pangoni, eneo
pana ambalo nilihisi kuwa huenda lingekuwa na usalama kidogo kwa mimi
kupumzika huku nikiendelea kutweta. Nikageuka nyuma kutazama hata hivyo
sikuliona tena lile joka wala kusikia sauti ya ule mburuto. Nikajisongeza na
kujiegemeza kwenye ukuta wa pango huku mapigo ya moyo wangu yakien￾delea kuvurugika.
Nikiwa nimeendelea kusimama lile eneo nikaanza kuhisi miguu yangu ili￾kuwa mbioni kuishiwa nguvu hivyo nikasota ukutani taratibu na kuketi chi￾ni. Kwa kweli nilihisi ni kama niliyepotea njia kwenye jangwa lisilokuwa na
mwisho. Ikirezi, Jean Pierre Umugwaneza na wale watu wengine sikuweza
kuhisi kuwa walikuwa wapi wakati huu hata hivyo uzima wangu lilikuwa suala la muhimu zaidi ITAENDELEA
 
MUDA MFUPI SANA ULIKUWA UMEPITA nikiwa pale chini nime￾pumzika wakati niliposhtushwa na sauti ya milio ya risasi iliyokuwa ikivu￾ma ndani pango lile. Nilishtuka na kusimama huku nikisikiliza kwa makini
milio ile ya risasi bila ya kufahamu ilikuwa ikitokea upande gani, moyo wangu
ulianza kwenda mbio na miguu yangu ilikuwa ikinishawishi nianze kitimua
mbio ingawaje akili yangu haikukubaliana haraka na suala hilo.
Nikiwa bado nimesimama ile sehemu nilingudua kuwa ile milio ya risa￾si iliyokuwa ikirindima mle pangoni sasa ilikuwa ikiongezeka sambamba na
sauti ya vishindo vya hatua za watu, nikaikamata bunduki yangu mkononi
na kujiweka tayari. Muda mfupi uliofuata niliiona taswira ya mwanamke an￾ayekimbia ikijitokeza upande wa kushoto wa pango lile, nilipomtazama vizuri
mwanamke yule nikaona kuwa alikuwa ameongozana na wanaume wengine
wanne nyuma yake na wote walikuwa uchi kama walivyozaliwa na waliku￾wa wakitimua mbio. Japokuwa nilikuwa sijawaona vizuri kutokana na giza la
mle ndani lakini haraka hisia zangu zilinieleza kuwa mwanamke yule huenda
alikuwa Ikirezi na wale wanaume wengine walikuwa ni miongoni mwa wale
watu waliokuwa kwenye ule msafara wakati tulipokuwa tukitoroka kule pan￾goni.
Nikawaacha wanipite mbele yangu bila ya wao kuniona huku nikiendelea
kubanisha ile sehemu, moyoni nilifurahi sana kuwa nilikuwa nimekutana tena
na wenzangu japokuwa bado walikuwa hawajaniona hata hivyo idadi yao ilin￾ishtua sana kwani idadi yao ilikuwa imepungua.
Wale watu walinipita na kuendelea na mbio zao nikawaacha wafike mbele
kidogo kisha na mimi nikaunga msafara ule kwa nyuma yao nikikimbia ku￾wafuata. Ile milio ya risasi sasa niliisikia kuwa ilikuwa ikiongezeka nyuma
yangu na hapo nikajua kuwa wale watu mbele yangu walikuwa wakifukuzwa
na mtu au watu waliokuwa nyuma yao na bila ya shaka nilijua tu kuwa watu
hao nyuma yangu wangekuwa ni wale askari wa Kanali Bosco Rutaganda.
Tulipofika mbele tukaingia kwenye njia nyingine ya pango iliyokuwa upa￾nde wa kulia kwetu, ilikuwa ni njia nyembamba kiasi na yenye hewa nzito na
hapo niliwasikia wale wenzangu wakihema ovyo mara tu tulipoingia kwenye
uchochoro ule lakini hawakuonesha dalili zozote za kusimama na hakuna ali￾yeshtukia uwepo wangu nyuma yao.
Ile milio ya rasasi nyuma yetu ilikuwa imetukaribia sana na nilihisi kuwa
pengine ilikuwa umbali mfupi sana nyuma yetu na nilianza kuiona hatari kuwa
endapo ingezidi kutukaribia basi baadhi ya rasasi zingeweza kutulenga. Tu￾livuka uchochoro ile wa pango na kuingia uchochoro mwingine upande wa ku￾shoto uliyokuwa mpana kiasi lakini wenye mawe makubwa yaliyochongoka.
Kufikia pale niliwaona wale wenzangu wakipunguza mwendo ingawaje
niligundua kuwa walikuwa wakifanya vile bila yao wao wenyewe kupenda,
nikajua kuwa huenda walikuwa wameanza kuchoka. Zile risasi sasa zilikuwa
zimetufikia karibu na zilikuwa zikitukosakosa huku nyingine zikipita juu ya vichwa vyetu. Tuliharakisha kuivuka njia ile ya pango kisha tukaingia kwenye
njia nyingine iliyokuwa upande wa kulia kwetu. Zile risasi zilikuwa zikitukosa
na hali hiyo ilikuwa imewapelekea wale wenzangu kule mbele waanze kupiga
mayowe ya hofu.
Njia ile ya pango tuliyoingia ilikuwa ikielekea sehemu ya chini ya pango lile
na nilianza kushikwa na hofu nilipoyakumbuka yale majoka makubwa niliy￾okuwa nimepambana nayo ambayo mpaka sasa nilikuwa nimegundua kuwa
yalikuwa yakipendelea kuishi sehemu za chini zaidi za mapango yale mahali
penye matope yenye majimaji na popo ambao bila shaka ndiyo walikuwa ki￾toweo chao kikubwa.
Kwa kweli ilikuwa ni hali ya mikikimikiki na kila mmoja alipambana kuio￾koa nafsi yake. Bado tuliendelea kutimua mbio huku tukiendelea kukoswa￾koswa na zile risasi zilizokuwa zikifyatuliwa nyuma bila shabaha ya maalum.
Wakati tukiendelea kukimbia nilihisi kuwa ile milio ya risasi ilikuwa imetu￾karibia sana nyuma yetu na kama tungeendelea tu kukimbia vile wale watu
wangeweza kutupata kwa urahisi. Hivyo nilisimama na kugeuka na hapo
nikaanza kujibu mashambulizi na bila ya shaka nilimshtukiza sana yule mlen￾gaji nyuma yetu kwani hakudhani kabisa kuwa mmoja wetu angekuwa na si￾laha.
Majibishano ya risasi baina yangu na yule mlengaji aliyekuwa nyuma yetu
yalifanyika kwa umakini wa hali ya juu huku kila mmoja akionekana kumvizia
mwenzake, risasi zilizokuwa zikitupwa upande wangu zilinihangaisha sana
katika kuzikwepa nikilala chini nikijiviringisha huku na kule na kujibanza
kwenye baadhi ya kona lakini hatimaye nilifanikiwa kumpata mlengaji Yule
inagawaje sikuweza kufahamu kuwa nilimlenga eneo gani mwilini mwake la￾kini kukoma kwa ile mirindimo ya risasi na sauti kubwa ya mayowe aliyopiga
yule mtu baada ya kufanikiwa kuzipenyeza risasi zangu kwenye mwili wake
hiyo ilinihakikishia kuwa tayari nilikuwa nimemlenga yule mlengaji nyuma
yetu.
Niligeuka mbele na kuanza kukimbia tena nikiwafuata wale wenzangu lak￾ini wakati huo nikiwa nawaza kichwani kuwa wale watu mbele yangu huenda
wangekuwa wakijiuliza kuwa yale majibishano ya risasi yalikuwa baina ya
nani na nani. Wakati nikiendelea kukimbia nilikuwa nikimuomba Mungu kuwa
mbele yangu nisikutane na njia nyingine za pango kwani zingeweza kunichan￾ganya na hatimaye kushindwa kuelewa wenzangu wameelekea uelekeo upi.
Ile njia ya pango nilishukuru kuwa haikuwa na kona nyingine hivyo nilien￾delea kuifuata ikishuka sehemu ya chini ya lile pango. Wakati nikishuka chini
ya pango lile niligundua kuwa hewa ya mle ndani ilikuwa ikibadilika taratibu
kwa kutoka katika hali ya hewa nzito kwenda kwenye hali ya hewa safi na
nyepesi. Ile njia ilikuwa na utelezi mkali hivyo nilijikuta nikiteleza kuelekea
kule chini bila ya kupata nafasi ya kujitetea na hatimaye nilijikuta nimean￾gukia kwenye tope zito la udongo mfanyanzi lililofanikiwa kunimeza kuanzia
miguuni hadi sehemu ya kiuno.
Nilikuwa nimetokezea kwenye pango kubwa na pana lakini lenye mwanga
wa kutosha, mwanga ule ulikuwa ukipenya kutoka juu kupitia kwenye tundu kubwa lililokuwa juu ya pango lile. Kwa kweli nilijisikia furaha sana kwani
nilikuwa na hakika kuwa sasa nilikuwa nimekaribia kutoka nje ya mapango
yale.
Japokuwa nilikuwa nimezama kwenye lile tope lakini sikuwa nimeanza ji￾tihada za kujinasua badala yake nikiwa pale niliendelea kulitazama lile tundu
la juu ya pango kwa furaha sana huku nikiwa siyaamini macho yangu kuwa
nilikuwa nimefika sehemu nzuri yenye matumaini makubwa katika safari yan￾gu ya kukitoroka kifo katika mpango yale. Nikiwa bado nimezama kwenye lile
tope huku nikiwa furaha ya kupita kiasi ghafla nilishtushwa kwa sauti ya kike
ikiita jina langu na hapo nikageuka kutazama upande ule ile sauti ilikotokea
na hapo furaha yangu ikaongezeka zaidi pale nilipomuona Ikirezi kwenye
kona ya pango lile akiwa na wenzake mbioni kulivuka lile tope, nyuma yake
akifuatiwa na Jean Pierre Umugwaneza na wanaume wengine wawili ambao
nilizikumbuka haraka sura zao kuwa walikuwa miongoni mwa wale mateka.
Wote waligeuka kunitazama wakionesha sura za furaha nami nikafurahi
sana huku nikianza kujinasua toka kwenye lile tope kuwafuata kwani wao
walikuwa wanakaribia ukingoni kulivuka lile tope.
__________
NILIKUWA NDIYO KWANZA NIMEFIKA NUSU TU YA SAFARI YAN￾GU ya kulivuka lile tope la mle ndani ya pango nikiwafuata wale wenzangu
wakati ghafla niliposhtushwa na sauti za milio ya risasi iliyoanza kurindima
kupita lile tundu la juu ya pango na hapo nikayatupa haraka macho yangu ku￾tazama kule juu ya lile tundu. Niliwaona wanajeshi watatu wakiwa wanachun￾gulia kwenye lile tundu huku wote wakiwa wameielekeza mitutu ya bunduki
zao kule walipo akina Ikirezi na hapo haraka nikajua kuwa wale walikuwa ni
askari wa Kanali Bosco Rutaganda na kwa bahati nzuri walikuwa hawajanio￾na.
Sikutaka kusubiri nikapiga yowe kali kuwashtua wale wenzangu mbele yan￾gu nikiwataka walale chini haraka kwani walikuwa mbioni kushambuliwa.
Ikirezi, Jean Pierre Umugwaneza na yule mtu wa nyuma yake bila shaka wali￾nisikia na kunielewa haraka kwani kufumba na kufumbua wakawa wamejitu￾pa chini kwa wepesi wa hali ya juu. Bahati mbaya sana yule mtu wa mwisho
alikuwa amekwishachelewa kwani muda uleule nilimuona akitupwa hewani
huku akipiga yowe la maumivu, na akiwa bado yupo kule juu niliuona ubon￾go wake ukisambaratika hewani kama tope jepesi lililorushwa huku kichwa
chake kikirushwa upande mwingine. Kwa kweli sikuwahi kuliona tukio baya
la kifo kama kile na bila shaka silaha kali sana ya kivita ilikuwa ikitumika na
wale wanajeshi. Risasi bado ziliendelea kurindima mle ndani.
Bila ya kupoteza muda nilianza kujibu mashambulizi toka kule chini ni￾kiwashambulia wale wanajeshi waliokuwa wakichungulia kwenye lile tundu
kule juu. Shabaha ilikuwa ni miongoni mwa kigezo kilichotumika kuniingiza
kwenye mafunzo ya wanajeshi makomandoo muda mfupi baada ya kujiunga
na jeshi la wananchi wa Tanzania hivyo sikuwa na mashaka kabisa na kipaji
changu. Niliishika bunduki yangu kwa mkono wa kulia nikawa nakimbia huku niki￾washambulia wale wanajeshi kule juu nikiitumia njia ile kujikinga, kusham￾bulia na vilevile kulivuka lile tope lakini wakati huohuo macho yangu yak￾iendelea kutazama kule juu ili nisipoteze shabaha. Mkakati wangu ukaanza
kuzaa matunda kwani risasi chache tu nilizozifyatua ziliwapata vizuri wale
wanajeshi waliokuwa wakiendelea kutushambulia kwenye lile tundu la pango
kule juu na hapo nikawaona wanajeshi wawili wakianguka kutoa kule juu hadi
chini kwenye lile tope mle ndani.
Sikuwaacha watue kwa sterehe juu lile tope hivyo nikawa nikiendelea
kuwafyatulia risasi katika namna ya kuwasindikiza hadi mwisho wa safari
yao kwenye lile tope na walipofika chini walikuwa wafu. Pamoja na hayo
mashambulizi ya risasi kutoka kule juu bado yaliendelea na safari hii rasasi
zilikuwa zikichimba umbali mfupi sana pembeni yangu. Hofu ilinishika hata
hivyo sikusimama ingawaje kukimbia juu ya tope lile jingi kulinifanya nihisi
kuwa nilikuwa nikitembea badala ya kukimbia kama nilivyokuwa nikitaka.
Zile risasi zilizokuwa zikitushambulia nilihisi ni kama zilizokuwa zikinikosa￾kosa kwa bahati sana au pengine mlengaji hakuwa makini kwa shabaha.
Niliendelea kukimbia kulivuka lile tope zito huku zile risasi zikinikosakosa
na mashambulizi yale yalipozidi nilifahamu kuwa nisingeweza kufika mba￾li kabla ya yule mlengaji kufanikiwa kunipata hivyo nikawa nakimbia huku
moyoni nikimuomba Mungu kuwa niponyoke kwenye kadhia ile lakini wakati
huohuo akili yangu ikiendelea kupiga mahesabu ya nini kifanyike kwa wakati
ule.
Mara nikawa nimepata wazo jipya na hapo nikasimama na kuinyanyua ile
kurunzi yangu mkononi kisha nikawasha batani ya mwanga mkali na kummu￾lika yule mtu aliyekuwa akitushambulia kule juu. Mahesabu yangu yakazaa
matunda haraka kwani ule mwanga mkali wa ile kurunzi yangu ukamchang￾anya yule mtu kule juu hivyo akawa amesitisha kufyatua risasi na badala yake
akawa akijikinga usoni kwa kiganja chake ili kuuzuia ule mwanga wa kurunzi
ili aweze kuniona vizuri ingawaje mimi huku chini nilikuwa nikimwona vizuri
sana na sura yake mbaya kama panya ilikuwa imejianika vizuri kwenye ule
mwanga wa kurunzi yangu.
Ilikuwa nafasi nzuri na sikutaka kuipoteza hivyo niliikamata vizuri bunduki
yangu mkononi kisha nikaiweka kwenye shabaha nzuri na nilipovuta kilimi
cha bunduki ile risasi tatu za mwisho toka kwenye mtutu wa bunduki yangu
zilifanya kile nilichokitaka. Kwanza nilimuona yule mtu akitupwa hewani juu
ya lile tundu huku akinipiga yowe kali la maumivu na yowe hilo lilipokoma
nilimuona yule mtu akianguka mle ndani mzimamzima huku kichwa chake
kikiwa kimeharibiwa vibaya na risasi zangu.
Yule mtu nilikuwa nimempata na bila ya shaka umauti ulikuwa umemfika
na wakati huohuo bunduki yangu ikiwa imeishiwa risasi hivyo niliitupa na
kuendelea kulivuka ile tope kwa haraka huku nikiwa na hakika kuwa nilikuwa
nimewaua wale wanajeshi wote waliokuwa juu ya lile tundu. Ikirenzi, Jean
Pierre Umugwaneza na yule mtu mwingine walipoona yale mashambulizi ya
risasi yamekoma wakasimama na kuanza kukimbia wakimaliza kulivuka lile tope huku mimi nikiwa nyuma yao.
Nilikuwa ndiyo namalizia kulivuka lile tope wakati Ikirezi aliponishtua kwa
sauti ya yowe kali la tahadhari na bila ya kuchelewa nikafahamu lile yowe
lilikuwa likimaanisha nini kwani kwa haraka nilihisi kuwa alikuwa akiiona
hatari fulani nyuma yangu hivyo nikajitupa kando lakini nilikuwa nimech￾elewa kidogo kwani muda uleule nilihisi kitu fulani kikipenya ghafla kwenye
bega langu la kushoto huku kikiniachia maumivu makali mno yasiyoelezeka
halafu nikasombwa na katupwa hewani na hapo niliwasikia Ikirezi, Jean Pierre
Umugwaneza na yule mtu mwingine waliyeongozana naye wote wakipiga
mayowe ya hofu.
“Laleni chini tunashambuliwa” niliwaambia huku nikipiga makelele hata
hivyo walinielewa wakawahi kalala chini. Loh! nilisikia maumivu makali
sana begani, risasi moja ilikuwa imenipata na lile jeraha lake lilikuwa likivuja
damu. Zile risasi ziliendelea kurindima mle pangoni na pale nilipotupwa si￾kushawishika kujitingisha kwani kufanya hivyo kungemfanya yule mlengaji
aweze kuniona kwa urahisi ingawaje mwili wangu wote ulikuwa umetapakaa
matope hivyo nilifahamu kuwa yule mlengaji kule juu asingeweza kuniona
kwa wepesi.
Wakati huu sikuwa na silaha yoyote nyingine zaidi ya bastola moja niliy￾okuwa nimeisunda kiunoni mwangu hata hivyo sikuona kama ingekuwa ni
jambo la busara kuitumia bastola hiyo katika kuyajibu yale mashambulizi kule
juu kwani ilikuwa ni silaha ndogo sana ukiilinganisha na ile ya yule adui hivyo
ni kama ningekuwa napoteza risasi zangu bure. Zile risasi bado ziliendelea
kirindima mle ndani na pango lote lilitawaliwa na harufu ya moshi wa risasi.
Toka pale nilipokuwa nimetupwa nilianza kujivuta juu ya tope lile taratibu
kwa kutambaa huku nimelilalia tumbo langu katika mtindo wa kijeshi uitwao
crawling. Mirindimo ya zile risasi iliendelea hata hivyo mlengaji bila shaka
hakuwa fundi wa shabaha maana risasi zake zote zilikuwa zikiishilia kwenye
lile tope tu. Niliendelea kujivuta juu ya lile tope hadi nilipofika ukingoni na
hapo niligeuka kutazama kule juu, nikawaona wanajeshi wengine wanne
wakiwa wameongezeka kwenye lile tundu na wote walikuwa wakichungulia
ndani ya pango.
Wale wanajeshi wengine ni kama walifika pale juu kuongeza nguvu baada
ya kuona nimewadungua wenzao kwani haukupita muda mrefu mvua ya risasi
ilianza kushuka mle ndani ikielekezwa upande wangu na hapo nikajua kuwa
walikuwa wameniona. Niliona hatari ilikuwa ikinikaribia kwa haraka sana,
Ikirezi, Jean Pierre Umugwaneza na yule mtu mwingine walikuwa wame￾shamaliza kulipata lile tope na kulivuka kabisa baada ya kuona yale masham￾bulizi mengine ya risasi yakielekezwa kwao. Walipomaliza kulivuka lile tope
wakawa wamesimama wakinisubiri kwenye kona ya lile pango.
Nilijitahidi kukimbia ingawa lile tope liliendelea kunipunguza kasi wakati
huo zile risasi zikinisindikiza kwa nyuma na kunikosakosa lakini hatimaye
nilifanikiwa kulivuka lile tope na hapo safari ikaanza. Safari hii niliwataka
Ikirezi na wenzake wakae nyuma yangu na mimi ndiyo nikawa tena kiongozi
wa ule msafara huku ile kurunzi nikiwa nimeishika mkononi pamoja na ile bastola. Kulikuwa na njia nyembamba ya pango hivyo niliwaongoza wenzangu kuingia kwenye njia hiyo iliyokuwa na tope la kiasi lenye majimaji kwa chi￾ni. Akili yangu yote sasa ilikuwa kuutafuta mfereji wa maji wowote ndani ya pango lile kwani nilifahamu kuwa mfereji huo ndiyo ungekuwa njia ya
kutorokea nje ya mapango haya. Tulipomaliza kuipita ile njia tukaingia kicho￾choro kingine kilichokuwa mwisho wa njia ile ya pango kwa upande wa kulia,
tulipofika kwenye uchochoro ule matumaini yalianza kifufuka kwani chini
yake nilikuwa nikisikia kelele za maporomoka ya maji.
Nikasimama na kuwauliza wenzangu kama walikuwa wakijua namna ya
kuogelea, Jean Pierre Umugwaneza na yule mtu mwingine wakaniambia kuwa
wao walikuwa wakijua kuogelea lakini Ikirezi alikataa. Nikamwambia Ikirezi
asiwe na wasiwasi kwani itakapofika wakati wa kuogelea mimi ningemsaidia
wakati wale wengine wangekuwa wakiogelea wenyewe.
Tulikubaliana na hapo safari ikaendelea tukishuka chini kwenye ule ucho￾choro wa pango, baada ya kukata kona mbili kwenda kule chini tukawa tu￾mefika kwenye ule mfereji ambao hapo mwanzo nilikuwa nikiyasikia yale
maji yake yakiporomoka, ulikuwa mfereji mkubwa na wenye kina pia wenye
maji yanayosafiri kwa kasi. Nikamchukua Ikirezi na kumbeba begani huku
mikono yake akiwa ameipitisha shingoni mwangu kisha sote tukajitosa ndani
ya ule mfereji na muda huohuo Jean Pierre Umugwaneza na yule mwenzake
nao wakajitosa mferejini wakinifuata kwa nyuma.
Tofauti na ile mifereji ya maji ya hapo awali mara baada ya kujitosa kwenye
maji ya mfereji ule nilihisi kuwa maji yake yalikuwa mengi zaidi, ya baridi na
yanayosafiri kwa kasi kubwa sana. Ikirezi akiwa amenishika vizuri mgongoni
niliendelea kuyakata maji taratibu na kwa umakini huku yeye akiwa ameishi￾ka ile bastola yangu na ile kurunzi akimulika mbele kwani mle ndani ya ule
mfereji bado kulikuwa na giza.
Ule mfereji wa maji ulikuwa na kona nyingi sana, tuliogelea na kuzipita
kona saba za mfereji ule na kuna baadhi ya sehemu za mfereji ule zilikuwa
nyembamba sana hivyo yale maji yalikuwa mengi na yanayosafiri kwa kasi na
kuna baadhi ya sehemu za ule mfereji zilikuwa pana na hivyo kina chake cha
maji nacho kilipungua. Lakini kwa kadiri tulivyokuwa tukiendelea na safari
yale maji ya mfereji yalikuwa yakiongezeka taratibu na yalikuwa yakianza
kubadilika rangi na kuanza kuwa mekundu, wasiwasi ulianza kunishika kuwa
huenda mvua kubwa ilikuwa ikinyesha na yale maji yalikuwa yakiongezeka
kutokana na mvua hiyo.
Wakati fulani niligeuka nyuma kuwatazama wenzangu na hapo nikawaona
kuwa walikuwa makini sana kunifuatilia, kwa kweli sikuwa nikifahamu hasa
ule mfereji ungetufikisha wapi lakini bado nilikuwa na matumaini nao hata
hivyo sikupenda safari yetu iwe ndefu sana kwani nilifahamu kuwa ningecho￾ka kutokana na uzito wa Ikirezi mgongoni mwangu. Mle ndani ya pango la ule
mfereji kulikuwa na popo wengi wakubwa waliokuwa wakining’inia juu ya
dari la ule mfereji, popo hao walitushambulia kila tulipokutana nao hata hivyo
waliwahi kukata tamaa na kutuacha pale walipotuona tukizidi kusonga mbele. Ulipita muda mrefu tukiendelea kuogelea bila ya kuona tumaini lolote la
kutoka nje ya mapango yale na mimi nilianza kuhisi kuchoka kutokana na uzi￾to wa Ikerezi mgongoni mwangu hata hivyo sikutaka kukata tamaa japokuwa
lile bega langu lililojeruhiwa kwa risasi lilikuwa likiniuma sana huku likien￾delea kuvuja damu taratibu. Muda wote huo Ikirezi ilikuwa kimya mgongoni
mwangu na nilikuwa nikiyasikia mapigo ya moyo wake namna yalivyokuwa
yakienda mbio kwa hofu.
Baada ya safari ndefu ya kuogelea hatimaye tukatokezea kwenye sehemu
pana ya pango lile yenye kutisha, sehemu hiyo ilikuwa na maji mengi yaliyo￾sambaa na yenye kina kirefu, niliweza kuyahisi kutokana na nguvu ya uvutano
iliyokuwa eneo lile. Maji ya eneo lile yalikuwa yamebadilika rangi na kuwa
meusi na yanayozizima kwa wingi wake na yalikuwa yakienda kasi mno kuzu￾nguka eneo lile kabla ya kuendelea na safari yake kwa mbele yetu.
Nilimkumbuka mwalimu wangu wa somo la jiografia wakati alipokuwa
akitufundisha mada ya maumbo mbalimbali yatokanayo na mito ya maji
wakati nilipokuwa mwanafunzi wa sekondari na hapo nikaitambua sehemu
ile kama ielekeayo kutengeneza moja ya umbo la mto liitwalo Ox-bow lake
ingawaje katikati kulikuwa na shimo kubwa na maji yale yalikuwa yakizungu￾ka shimo lile kwa kasi kabla ya kuendelea na safari. Tulipofika eneo lile mimi
hofu ilinizidi kwani nilianza kuona hatari ya kuweza kutumbukia kwenye shi￾mo lile endapo tusingekuwa makini na sikufahamu shimo lile lililokuwa na
nguvu za ajabu za uvutano lilikuwa likielekea wapi.
Nilijitahidi kujizuia na bila ya mafanikio tukajikuta tumeingia kwenye ule
mzunguko wa maji na hapo nilimsikia Ikirezi akipiga mayowe ya hofu mgon￾goni mwangu hata hivyo nilimsihi aendelee kunishika. Sasa yale maji yalianza
kutuzungusha kwa kasi ya ajabu kando ya lile shimo na nilipogeuka nyuma
nikawaona Jean Pierre Umugwaneza na yule jamaa mwingine nao wakiwa
wameingia kwenye ule mzunguko wa maji.
Tuliendelea kuzungushwa na yale maji kandokando ya lile shimo kwa mara
kadhaa na kila nilipojitahidi kijinasua sikufanikiwa na hapo kizunguzungu kil￾ianza kunishika na kusababisha kichwa kuniuma kwa ghafla huku nikijisikia
kutaka kutapika.
Wakati nikielekea kukata tamaa mara ghafla nikaona wimbi kubwa la maji
likija kutokea kule tulipotokea, nikalitazama wimbi lile na kugundua kuwa
kwa vyovyote lingeweza kuleta namna ya ukinzani na ule mkondo wa mzu￾ngoko wa yale maji. Hivyo nikalitegea lile wimbi wakati linakutana na ule
mkondo wa maji na mimi muda huohuo nikawa nimezama kuingia katikati ya
lile wimbi na ule mkondo wa maji na tulipoibuka juu tukatupwa mbali kando
ya lile shimo na muda huohuo nikamuona na yule jamaa tuliyeongozana naye
akitupwa na yale maji kuja upande wetu lakini sikufanikiwa kumuona Jean
Pierre Umugwaneza na hapo wasiwasi ukanishika.
Nilipogeuka kumtazama yule jamaa ambaye sasa alikuwa pembeni yangu
uso wake ulitosha kabisa kunieleza juu ya tukio lililokuwa limetokea kwani
alikuwa amegeuka na kutazama ule upande lilipokuwa lile shimo na mimi
nilipotazama kule sikuona dalili yoyote ya kuwepo kwa mtu eneo lile na hapo nikajua kuwa Jean Pierre Umugwaneza alikwisha tumbukia kwenye lile shi￾mo. Loh! huzuni ilinishika sana nikajihisi kukata tamaa kwa kumpoteza mtu
muhimu sana aliyepoteza familia yake kwa kuyaokoa maisha yangu.
Wazimu ukanishika nikakosa uvumilifu na hapo nikaanza kuogelea kuli￾fuata lile shimo lakini Ikirezi akatambua haraka nilichokuwa nataka kuki￾fanya hivyo akaanza kupiga makelele ya kunionya kuwa nisiende hata hivyo
nilimpuuza lakini sikufika mbali yule jamaa tuliyeongozana naye akawahi
kunishika mguu na kunisihi nisiende. Baada ya hangaika hangaika ya hapa
na pale hatimaye niliamua kumsikiliza yule jamaa hivyo nikageuka na kuanza
kuogelea taratibu nikienda pembeni ya lile shimo huku nikiwa nimejawa na
huzuni sana.
Tulipofika kule kando ya lile shimo tulitulia kidogo tukiyatazama yale maji
yaliyokuwa yakizunguka lile shimo kwa kasi huku tukitarajia kumuona tena
Jean Pierre Umugwaneza lakini haikuwa hivyo kwani hapakuwa na dalili yoy￾ote ya kuonekana kwa binadamu eneo lile wakati huo yale maji ya mle pan￾goni yakiendelea kuongezeka taratibu mwishowe tukaamua kuendelea mbele
za safari yetu.
Tuliendelea kuogelea mpaka tulipofika mbele mahali ambapo ule mfereji
tuliokuwa tukiogelea ulikutana na mfereji mwingine na kuunganika na hivyo
kutengeneza mfereji mmoja mkubwa kama mto wenye maji mengi yanayosa￾firi kwenda mbele yetu. Tukazidi kuogelea huku tukiwa na hofu kuwa huenda
ule mto ungekuwa na maji mengi sana ambayo si ajabu sana yangetushinda
nguvu hata hivyo niliutambua haraka kuwa mto ule ulikua ni wa kipindi cha
masika tu na bila shaka kipindi cha kiangazi haukuwa na maji hata tone. Tu￾lipofika mbele kidogo mara tukaanza kuona mwanga wa asili wa mawingu
ukitufikia taratibu na hapo nikajua kuwa sasa tulikuwa tumefika sehemu ya
nje ya yale mapango kwa kweli nilihisi kama nguvu mpya ikinirudia mwili
mwangu huku moyo wangu ikigubikwa na furaha isiyo na kifani.
Eneo lile lote lilikuwa limetawaliwa na sauti ya maporomoko ya maji ya
ule mto wa masika, tulipofika nje kabisa ya yale mapango nikagundua kuwa
mvua kubwa ilikuwa ikiendelea kunyesha na hapo nikakumbuka lile fukuto la
joto kali lililokuwa mle pangoni. Yale maji ya mto yalikuwa mengi na wakati
huu yalikuwa yakisafiri kwa kiasi na yalikuwa yakiendelea kubadilika rangi na
kuzidi kuwa mekundu kutokana na mchanganyiko wa udongo wa eneo lile na
takataka zilizokuwa zikiendelea kukokotwa na yale maji.
Mara kwa mara tulilazimika kuyakwepa mabonge makubwa ya udongo,
mawe na magogo ya miti yaliyokuwa yakikokotwa na yale maji. Ikirezi akiwa
mgongoni mwangu niliendelea kuogelea taratibu mpaka pale nilipohisi kuan￾za kuchoka nikapata gogo moja kubwa lililokuwa likikokotwa na maji na hapo
nikalidandia hivyo likawa likitukokota taratibu kuufuata ule mto.
Wakati tukiendelea kuelea juu ya lile gogo niligeuka kuyatazama yale mapan￾go ya Musanze ambayo sasa yalikuwa nyuma yetu nikawa kama siyaamini
macho yangu kuwa hatimaye tulikuwa nimefanikiwa kumtoroka Kanali Bosco
Rutaganda na askari wake. Niligeuka kumtazama Ikirezi nikamuona aliku￾wa akitabasamu ingawaje uso wake bado ulikuwa umejawa na mashaka nami nikabaki nikitabasamu tu huku tukiendelea kuelea kwenye lile gogo taratibu
tukiyaacha yale mapango nyuma yetu. Yule jamaa tuliyeongozana naye akawa
amejilaza juu ya gogo lile huku naye akiendelea kuyatazama yale mapango
nyuma yetu huku akionekana kuzama kwenye fikra zake.
Mto ule wa masika ulikuwa ukikatisha kwenye eneo lenye miti mingi mi￾kubwa na misitu mizito isiyokuwa na dalili zozote za kuishi binadamu. Ni￾liitazama miti ile na kuiona kama moja ya mashihidi wangu katika safari hii
ya kukiponyoka kifo. Mvua kubwa ilikuwa ikiendelea kunyesha eneo lile na
usiku nao ulikuwa ukianza kuingia kwani japokuwa sikuwa na saa yangu
mkononi lakini nilihisi tu kuwa muda ule ungekuwa ni kwenye nyakati za saa
kumi na mbili jioni.
__________
MVUA KUBWA ILIKUWA IKIENDELEA KUNYESHA eneo lile na
mifereji midogomidogo ya maji iliyokuwa ikitokea sehemu za juu za milimani
ilikuwa ikitiririsha maji yake katika mto ule wa msimu na hivyo kupelekea
ongezeko kubwa la maji yenye kasi ya ajabu na sasa tulikuwa tukisukwasukwa
na maji yale yaliyokuwa yakiendelea kulikokota lile gogo tulilolidandia. Tu￾lipelekwa upande huu na ule wa ule mto bila ya pingamizi lolote. Sikuwa na
shaka kuwa tulikuwa tukisafiri kwenye kina kirefu sana cha maji kutokana na
namna gogo lile kubwa tulilolidandia lilivyokuwa likielea kama bua.
Nilipoyazungusha macho yangu kutazama eneo lile nikagundua mto ule uli￾kuwa umepita kwenye korongo pana na refu. Tulipokuwa katikati ya misitu ile
huku tukiendelea kusafiri taratibu niligeuka kumtazama tena Ikirezi pembeni
yangu nikamuona kuwa alikuwa ameanza kuishiwa na nguvu ya kuendelea
kulikumbatia lile gogo hivyo nikamsogelea na kumshika vizuri mkono wake
na hapo akageuka kunitazama bila ya kusema kitu. Uso wake ukawa ni kama
mtu anayetaka kucheka na kulia kwa wakati mmoja huku nikiiona hofu iliyo￾fichika usoni mwake.
Yule jamaa mwingine tuliyetoroka naye yeye alikuwa amelikumbatia vizuri
lile gogo huku akitutazama. Giza la jioni lilikuwa likipiga hodi taratibu na sau￾ti pekee iliyokuwa ikipenya masikioni mwangu ilikuwa ni ile sauti ya mzizimo
wa yale maji ya mto.
Tukiwa tunaendelea kusafiri juu ya lile gogo ghafla nilianza kuhisi kichwa
changu kilikuwa kizito sana nikaanza pia kuhisi kizunguzungu na wakati huo￾huo nikawa nahisi kama ninayetaka kutapika. Niligeuka kulitazama lile jeraha
la risasi begani mwangu na hapo nikaona kuwa nilikuwa nimepoteza damu
nyingi sana na bila shaka kile kizunguzungu kilitokana na upotevu wa damu
hiyo.
Taratibu hofu ilianza kuniingia nikawa naanza kuiona hatari mbele yangu ya
kupoteza nguvu na hatimaye kumezwa kabisa na maji ya ule mto endapo nin￾geendelea kuelea juu ya gogo lile kwa muda mrefu. Ule mto ulikuwa una kona
nyingi sana kwa kule mbele yetu na hali hiyo ilinifurahisha sana kwani zile
kona zilikuwa zikipunguza ile kasi ya maji. Hata hivyo hofu ilikuwa ikizidi
kuniingia kwani uwezo wa macho yangu kuona ulikuwa ukipungua kwa haraka sana kadiri muda ulivyokuwa ukizidi kwenda.
Niligeuka tena kumtazama Ikirezi nikawa namuona kwa mbali kama anay￾enishangaa ingawaje sikufahamu kwa haraka kuwa alikuwa akinishangaa nini.
Niligeuka tena kumtazama yule jamaa tuliyeongozana naye nikamuona kuwa
naye alikuwa akinishangaa sasa nikawa kama na mimi nataka kujishangaa
mwenyewe lakini sikufahamu ningejishangaa kwa sababu zipi. Mara muda
uleule nikawa nimeanza kupoteza taswira iliyokuwa mbele yangu na hapo
nikawa naona kama ile miti ya ile misitu iliyokuwa kando ya ule mto ilikuwa
ikiongezeka urefu na ilikuwa ikinipita kwa kasi sana kurudi nyuma yangu.
Muda huohuo nikawa nikihisi kuwa nguvu zilikuwa zikianza kuniishia
mwilini na kwa mbali nilianza kuhisi pia kuwa nilikuwa nikididimia kwenye shimo kubwa na refu lenye giza zito. Hofu ikiwa imenishika nikaanza ku￾fumbua mdomo ili nipige mayowe ya kuomba msaada lakini hata ile sauti ya mayowe niliyokuwa nikiipiga sikuweza kuisikia masikioni mwangu.
Mara nikawa siwezi kuona tena mbele yangu na sauti pekee niliyokuwa ni￾kiisikia ni ile sauti ya mzizimo wa yale maji mengi ya mtoni na wakati nikien￾delea kuwa katika hali hii ghafla nikasikia nikipigwa na kitu kizito kichwani
na baada ya hapo sikufahamu kilichoendelea.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom