Kudo
JF-Expert Member
- Nov 2, 2017
- 1,821
- 6,122
Sehemu ya 1*
Dar es laam saa 1:30am
Tarehe 20/07/2017
Doka Joker au maarufu kwa jina Dj alikuwa anawapa tabu ya kucheza wapenzi wa muziki,mara apige nyimbo za Diamond,haijaisha utasikia wimbo wa Alikiba,kila alipopiga wimbo basi watu walilipuka kwa mayowe kuonesha wamekunwa na utalaamu wa Dj kusugua mashine.
Watu wawili walikuwa wamekumbatiana muda wote,huku wakiwa wapo bize na wayazungumzayo,muziki ulipigwa ila hawakuwa na kushangilia au kucheza kulingana midundo ya mziki wao walikutanisha vichwa vyao huku mikono yao ikipita kiunoni mwa kila mmoja,maumbo yao yalikuwa na kazi ya kwenda kushoto na kulia kila mara na kwa mwendo wa taratibu sana.
Mbena alimuuliza Maiga
"Ni lini utakuja nyumbani?"
"Aah nitakuja baada ya mitihani ya kuhitimu chuo kwani umechoka kukaa kwenu?"
"Sio kama nimechoka ila naogopa kuishi mbali na ww Maiga nataka uwe wangu peke yangu,vile visichana vyako visije kunipokonya bwana"
"Mbena mpenzi acha wivu nishakupeleka nyumbani,bado Mimi kwenda kwenu,lakini si unajua wazazi wetu wote wanajua uhusiano wetu afu...."
Maiga hakumalizia kauli yake kuna mtu alipita karibu yake akampiga kikumbo akageuka kutazama hakuona mtu,akayarudisha macho kwa mpenzi wake Mbena aliekuwa akimtizama kwa swali la kulikoni nae pasipo kutoa sauti akanyanyua mabega kwenda juu kuashiria hajui kitu wakaendelea na maongezi yao.
Saa 2:05
Mziki bado ulikuwa umepamba moto huku sasa hali ya hewa mule ukumbini ikianza kuwa na harufu kali ya jasho,.
Maiga alimuaga mpenzi wake Mbena akaelekea vyooni kujisaidia,.
Akapiga hatua mbili na kumgeukia mpenzi wake Mbena akamtazama tena kisha akamkonyeza na kugeuka kuelekea vilipo vyoo vya ukumbi ule wa kuchezea muziki.
Saa 2:20
Alitizama saa yake ikamthibitishia ni zaidi ya dakika kumi na tano tangu Maiga amuage ya kuwa anaelekea chooni na hajarudi,kichwani mwake alihisi ni pengine Maiga anamtu mwingine huko vyooni au atakuwa upande mwingine tofauti na huo akimsaliti,akajenga picha vile usaliti ule unavyoendelea,akajikuta anakabwa koo kwa uchungu na hasira, akaona kukaa bila kufanya kitu ni kujisumbua ngoja amfuate hukohuko akawaadabishe yeye mwenyewe,akasimama kwa hatua za shari akauendea mlango wa kuingilia vyooni kule.
Kwa hatua za kujiamini akaucha mlango wa kuingilia vyoo vya kike na kuingia vyoo vya kiume,akakuta kuko kimya na kumetulia huku kwa mbali,ukisikika mziki ukitoka kwenye sipika za ule ukumbi wa mziki,akaanza kufungua mlango mmoja mmoja na kuangalia,lakini kila alivyokuwa akikagua na ukimya ule akaanza kuogopa lakini kwa nguvu ya wivu akazidi kupiga moyo konde na kuvikagua vyumba vyote ila hakumkuta Maiga.
Milango ya vyoo ilikuwa imepangana na kuacha upande mmoja kama korido ndefu na mwishoni mwa korido ile kulikuwa na uwazi ulioelekea upande wa kulia wa vyoo vile,Mbena akafuata usawa huo na kujikuta sehemu ya kushushia haja ndogo,akaanza kuambaa na uwazi huo,
Hakufika mbali akakutana na damu iliokuwa ikielea ndani ya eneo lilotengenezwa kwa ajili ya kusafirisha mkojo,hofu ikatanda moyoni mwa Mbena lakini akapiga moyo konde na kusogea upande huo hapo hakuamini macho yake alichokiona
Maiga alikuwa amesimama huku mkono mmoja akiwa ameugemeza ukutani na mgongoni mwake kulisimama mpini wa kisu huku damu zikimtililika,Mbena hakuamini macho yake akapiga kelele kubwa na kwa haraka akamkimbilia Maiga na kumvuta akamweka kando huku akilia,akaushika mpini ule wa kisu na kujaribu kuuchomoa,matendo yote aliyafanya huku akiwa hajielewi akipiga kelele na akiliita jina la Maiga.
Wakati akihangaika kumsaidia Maiga punde akaingia mtu mle chooni huku akiwa amejiziba sura yake kwa kofia,alikuwa kashika kamera akampiga picha kadhaa Mbena kisha kwa kasi ya umeme akapotea mle chooni,wakati yeye akiwa akitoka wakaingia watu wanne wakamkamata Mbena,mmoja kati yao akampiga na kitu kizito kisogoni pake kisha wakamchukua na kutokomea nae wanakokujua,
Haikuchukua muda ukumbi wa burudani ukageuka vilio na mikimbio ya huku na huko.....
Asalaam Kudo (Bahati Mwamba)