Abdallahking
JF-Expert Member
- Mar 19, 2018
- 3,983
- 10,804
Riwaya ya Kijasusi: SAUTI YAKE MASIKIONI MWANGU
Mwandishi: KELVIN KAGAMBO
Imeletwa Kwenu na: BURE SERIES
SEHEMU YA 1
“..... na sasa ni zamu yako. Sali sala za mwisho tufunge mkataba.”
“Lakini braza Jisu haya yote yanatoka wapi? Kosa langu nini?”
“Unaleta dharau sio? Hujui kosa lako au unauliza kutafuta faida? Sikia Mkuki, mimi sio Jisu yule unayemfahamu, halafu hii kazi ni lazima itimie, lazima nikuue.” Akazungumza kwa msisitizo mwanaume huyo aitwaye Jisu; mrefu, mweusi mwenye mwili wa mazoezi; upara kichwani na sharafa nene zilizoungana kidevuni kutokea chini ya kila sikio lake.
Kisha akaikamata barabara bastola iliyokuwa mkononi mwake, akamuelekezea Mkuki ambaye kwa muda huo alikuwa amepiga magoti mbele ya Jisu. Akavuta pumzi zake kwa kuhesabu moja mpaka tatu ili kujiongezea ujasiri. Akatumbukiza kidole cha shahada cha mkono wake kwenye ‘trigga’ ya bastola kisha akaanza kubofya taratibu.
“Paaaaa!” Mlio mkubwa wa risasi ulisikika nama hiyo, lakini kabla hata shambulio hilo halijafanikiwa Mkuki alikurupuka kutoka usingizini na kuikata ndoto ile mbaya yenye kutisha.
Akaketi kitandani huku akitweta na kutokwa jasho mithili ya mtu aliyelowa mvua ya manyunyu. Akajipa sekunde kadhaa kuirejesha akili yake duniani na alipofanikiwa katika hilo alishusha pumzi ndefu ya kushukuru kwamba lile halikuwa tukio halisi.
Ghafla akashituka; aligundua kitu kipya ambacho hakikuwa cha kawaida—aling’amua kwamba alikuwa kwenye chumba asichokifahamu kabisa, yaani hakuwahi kuwa hapo kabla.
Kilikuwa ni chumba chenye ukubwa wa chumba cha kawaida cha kulala, kuta zote za chumba hicho zilipakwa chokaa huku kitanda na meza ndogo vikiwa ni vitu pekee vilivyomo ndani.
‘Niko wapi?’ Likawa ni swali la kwanza kugonga kichwani mwa Mkuki. Hapo akajipa muda kuvuta kumbukumbu ya kila alichopitia kabla ya kuwa pale chumbani na hakika ubongo wake ulimsitiri, alikumbuka kila kitu.
Alikumbuka watu wawili aliokuwa nao mara ya mwisho, akakumbuka ajali mbaya aliyoipata akiwa na watu hao, pia alikumbuka kwamba ajali ile ilisababishwa na mlipuko mkubwa wa bomu.
‘Au nimesaidiwa?’ akajiuliza Mkuki ‘Lakini ngonja, ngoja nione.’ Akajipa moyo wa kusubiri na hamasa ya kufanya udadisi.
Basi akateremka kutoka pale kitandani; alihisi maumivu mwilini lakini hayakumzuia kutembea kuelekea mlangoni. Lakini kabla hata hajafikia lengo mlango ulifunguliwa, akaingia mwanamke mmoja aliyekuwa akiimba kwa sauti ya juu iliyoashiria uhuru mkubwa alionao, lakini ghafla mwanamke huyo aliacha kuimba mara tu alipomuona Mkuki.
Alikuwa ni mwanamke wa ki-Asia, msichana mfupi, mwembamba, mweupe mwenye nyelwe ndefu na nyingi zilizoficha uso wake wote ingawa hilo halikumzuia kuona mbele.
“Umeamka?” Akauliza mwanamke huyo, lakini kwa lugha ambayo Mkuki hakuilewa, lugha yenye kufanana kabisa na Kichina.
“We ni nani?” Mkuki naye akamtupia swali kwa lugha adhimu ya Kiswahili huku akirudi nyuma taratibu.
“Tulia. Kaa kitandani.” Yakamtoka kwa upole yule msichana, tena kwa lugha ile ile yenye kukanganya masikioni mwa Mkuki.
“Wewe nani na niko wapi hapa?”
“Tulia. Rudi kitandani. Bado hujapona, utajitonesha.” Akasema msichana huyo lakini kwa sababu ya mgongano wa lugha kati yao ilikuwa ni kama anatwanga maji kwenye kinu.
Akanyamaza kidogo yule msichana, akamtazama Mkuki kana kwamba kuna kitu alikuwa akifikiria juu yake kisha akapaza sauti kumuita mtu ambaye bila shaka hakuwa mbali na chumba kile.
“Babaaaa....” Aliita hivyo na sauti ya kiume kutoka nje ikamuitikia.
“Njoo. Amaeamka.” Akasema binti.
Punde mlango ukafunguliwa, akaingia mzee ambaye kwa mtazamo wa haraka Mkuki alijiridhisha kwamba babu huyo alikuwa ni Mchina. Alikuwa ni mzee wa kati ya miaka 60 na 70; mfupi, mwembamba, mweupe, mwenye mvi kichwa kizima na macho madogodogo ya kuvimba.
“Umeamka?” Akauliza mzee huyo kwa lugha ile ile iliyokuwa ikitumiwa na yule msichana, kisha kabla ya kupewa jibu alimfuata Mkuki, akamshika mkono na kumchukua hadi kitandani, akamkalisha.
“Unajisikiaje?” Akauliza yule mzee lakini kwa jinsi ambavyo Mkuki alikuwa akimtazama akagundua fika kwamba kulikuwa na kikwazo cha lugha kati yao.
“Hunielewi? Huzungumzi Kithaiwan?” Akamuuliza lakini bado aliambulia jibu la ukimya.
Akamgeukia yule msichana. “Haelewi.” Akamwambia. Kisha akamgeukia tena Mkuki. “Unaitwa nani?” Akamuuliza; hapa akijitahidi kutumia na vitendo kutafsiri swali lake.
Mkuki akamuelewa lakini pia tayari alishagundua kwamba watu wale hawakuwa na lengo baya juu yake.
“Mkuki. Naitwa Mkuki.” Akajibu.
“Nani?.”
“Mkuki.” Akajibu kwa msisitizo.
“Mkuki?” Akauliza yule mzee kuthibitisha.
“Ndiyo.” Akajibu huku akitingisha kichwa kukubali.
“Ooooh! Mimi ni Wong,” akajitambulisha yule mzee na kuongozea. “Na yule ni Mei Lee.” Akamtambulisha na yule msichana.
“Sisi tumekuokota ufukweni. Tumekusaidia. Unaweza kutuambia unatokea wapi?” Akahoji yule mzee lakini Mkuki alibaki akitumbua macho tu kama ishara ya kwamba hakuwa akimulewa, labda tu pale alipojitambulisha yeye pamoja na yule msichana.
“Baba? Hakuelewi. Tumpe muda.” Akazungumza yule msichana ambaye muda wote sura yake ilikuwa imefunikwa kwa nywele zake ngingi na ndefu.
“Sawa. Simama. Twende.” Akasema yule mzee aliyejitambulisha kwa jina moja la Wong huku akisindikiza sentesi yake kwa vitendo, Mkuki akamuelewa, akasimama na kuanza kumfuata kuelekea nje.
**************************************
Mkuki Salum Goigoi ndilo jina lake halisi, kijana aliyezaliwa na kukulia nchini Tanzania. Hadi mwaka huo 1998 alikuwa na umri wa miaka 23 duniani ingawa haikuwa rahisi kugundua hilo kwa kumtazama; alikuwa akionekana mkubwa zaidi na amekomaa kwelikweli.
Ni mwembamba wa kukonda, mrefu, mweusi mwenye uso wa duara wenye kufanyiza upole fulani unapomtazama; ingawa si kweli kwamba amejaaliwa haiba hiyo.
Kichwa chake kilibeba kumbukumbu za yote yanayomuhusu; yaani alipotoka; kilichotokea; yeye ni nani na mengineyo lakini juu ya yote hayo alinuwia kutowaambia wenyeji wake ukweli wowote na hii ni kwa sababu alikuwa anataka kukwepa kurejeshwa nchini Tanzania.
Hapo alikuwa nchini Thaiwan; taifa dogo ambalo ardhi yake yote ni kisiwa. Nchi ambayo ipo barani Asia, katikati ya China na taifa la Taiwan.
Wathaiwan walikuwa wakifanana kwa kiasi kikubwa sana na Wachina; kimuenekano, kitamaduni na hata itikadi. Wenyeji wa Mkuki walikuwa wakiishi Mkoa wa Shenghei katika kijiji kiitwacho Chensuua; kijiji ambacho wakazi wake walikuwa wakiishi kwa kutegemea shughuli za uvuvi kwa kiasi kikubwa.
Basi kwa siku chache za awali Mkuki aliishi na wenyeji wake kama mtu asiyekumbuka lolote; alijitengenezea mazingira hayo ili wenyeji wake wasipate sababu ya kumrejesha alipotoka; lengo lake ilikuwa ni kulowea palepale.
Kwa siku tano tu za awali alitambulishwa kwa vijana wenzake; kazi hiyo aliifanywa na mzee Wong ili kumsaidia Mkuki kujifunza jinsi ya kuishi kwa kuendana na taratibu zao za maisha ikiwemo kuifahamu lugha kwa urahisi na mambo mengine.
Katika hilo Mkuki alipata changamoto kubwa ya ubaguzi; yaani ingawa vijana walimkubali wakati anatambulishwa kwao lakini hawakutaka kuwa karibu naye—hilo lilifanywa nyuma ya mzee Wong, walimbagua Mkuki kwa sababu ya rangi.
Lakini Maufeng aliamua kuwa tofauti ya vijana wote wa kijijini Chensua—huyu yeye alikuwa ni mvualana wa Kithaiwan ambaye ni pekee aliyekubali kujenga ukaribu na Mkuki ingawa pia kulikuwa na sababu iliyomsukuma kufanya hivyo.
Maufeng yeye alikuwa na matatizo ya akili yanayompelekea kuwa mwendawazimu kabisa kwa kipindi fulani, hivyo vijana wengi walimtenga pia ingawa tatizo lake halikuwa likitokea mara kwa mara.
Maufeng akawa ni mtu wa tatu muhimu kwa ajili ya maisha ya mkuki pale ugenini, yaani ukiwajumuisha mzee Wong na binti yake Mei Lee.
******************************
Wiki mbili za Mkuki ndani ya Thaiwan zilikatika. Sasa taratibu alionekana kuanza kuifahamu lugha ingawa si kwa kiasi kikubwa, na msaada wa nguvu aliupata kutoka kwa Maufeng na mzee Wong, lakini Mei Lee—yule binti wa mzee Wong hakuwa katika orodha hiyo.
Ukweli ni kwamba Mei Lee hakuwa ni msichana wa kawaida; alikuwa ni mpole na kimya kupita maelezo na ili kuthubitisha hiko fikiria suala hili, kwamba tangu Mkuki aanze kuishi kwao hawajawahi kukaa pamoja na kupiga soga ingawa wote walikuwa ni vijana wanaorandana umri. Wala Mei Lee hakuwa na rafiki, jambo pekee alilokuwa akilifanya muda mwingi ni kuimba nyimbo zake mwenyewe na hakika alikukuwa ni mwanamuziki mzuri aliyejaaliwa sauti murua.
Yote tisa; kubwa zaidi ni kwamba kwa kipindi chote hicho cha wiki mbili cha Mkuki kuwa pale hakuwahi kuona sura ya binti huyo, muda wote aliifunika kwa nywele zake kama mtu anayeficha kitu fulani.