Riwaya: Saa za Giza Totoro

Riwaya: Saa za Giza Totoro

SEHEMU YA 39



Nilipiga magoti kwa heshima pembeni ya kaburi lake, machozi yakawa yananitoka kwa wingi. Bado sikuwa na majibu kama ile bastola niliyoificha kwenye sanda yake pamoja na fedha alikuwa amezikwa nazo au la!
SASA ENDELEA...
“Pole sana mdogo wangu, naujua uchungu wa kuondokewa na baba, afadhali wewe ameondoka ukiwa umeshakuwa mkubwa, mimi baba yangu alifariki nikiwa bado mdogo sana,” alisema Bonta huku akinipigapiga begani, akawa ananifariji kwa upole na kunitaka nijikaze.
Nilikaa pale kaburini kwa zaidi ya nusu saa, ndugu zangu wengine wote wakaondoka na kuniacha mimi na Bonta, baadaye niliinuka pale nilipokuwa nimepiga magoti na kusogea pale chini ya mkorosho alipokuwa amekaa Bonta, tukakumbatiana huku nikiwa bado naendelea kulia.
“Nilificha mashine na fedha kidogo kwenye sanda ya baba wale polisi walipokuja kunikamata.”
“Najua! Nimekuhifadhia,” alinijibu Bonta na kunifanya nipigwe na butwaa.
“Kwani ilikuwaje, mbona walipofika sikukuona, uliyeyukia wapi?” nilimuuliza Bonta, hakunijibu chochote badala yake, alipandisha mkono wa fulana yake na kunionesha hirizi kubwa aliyokuwa ameivaa.
“Nilikwambia kuhusu hili suala naona mpaka leo hujanipa majibu,” aliniambia, nikashusha pumzi ndefu na kumtazama. Hakuwa amenijibu swali langu, nikamuuliza tena. Aliniambia kwamba akiwa amekaa pale nje, alianza kuhisi hirizi hiyo ikimbana, akalazimika kuondoka haraka na muda mfupi baadaye ndipo askari walipowasili.
“Pombe huziwezi mdogo wangu, siku nyingine utakuja kusababisha matatizo makubwa sana, unatakiwa kuwa makini,” aliniambia na kuanza kunipa somo la jinsi ninavyotakiwa ‘ku-behave’ ninapokuwa mbele ya macho ya watu.
Nilichokuwa nampendea Bonta ni kwamba alikuwa akizungumza na mimi kwa busara sana, alikuwa ananijenga sana kiakili. Aliniambia kama najijua nina kichwa cha panzi, basi nisilewe mbele za watu, nikitaka kunywa bora ninywe kiasi kidogo au kama nataka kulewa basi nijifungie ndani. Nilimuahidi kwamba suala kama hilo haliwezi kujirudia tena na nitakuwa makini zaidi.
“Jioni tunatakiwa kurudi kambini, huku hakufai tena,” aliniambia Bonta, nikatingisha kichwa kuonesha kukubaliana naye. Tuliondoka pale kaburini na kurudi kule nyumbani, tukakaa pale chini ya mti wa mkorosho huku kila mmoja akitafakari mambo yake.
Bado moyo wangu ulikuwa na chuki kubwa kwa wote waliosababisha nishindwe kumzika baba na nilijiapiza kwamba lazima siku moja walipie kwa walichokifanya. Muda uliyoyoma kwa kasi na hatimaye kigiza kikaanza kuingia, nilienda ndani na kukaa na mama, nikawa namfariji kwa sababu bado alikuwa na uchungu mkali ndani ya moyo wake.
“Kuwa makini mwanangu, naomba utafute fedha kwa njia za halali, ukifanya kazi halali utakuwa na maisha mazuri sana kwa sababu inaonekana una nyota inayowaka sana. Ila usipende njia za mkato,” mama aliniambia kwa upole baada ya kumwambia kwamba jioni hiyo natakiwa kurudi Dar es Salaam kwa sababu kesho yake asubuhi natakiwa kazini.
Mama aliongea mambo mengi sana, kwa jinsi ilivyoonesha na yeye alishaanza kuwa na wasiwasi juu ya mwenendo wangu. Alinisihi sana kuachana na ulevi na kunitaka nisimame imara kama kiongozi wa familia.
“Baba yako hatunaye tena, wewe ndiyo unatakiwa kuwa kiongozi wa hii familia, ukifanya uzembe ujue kwamba tutakaoumia ni sisi, nakupenda sana mwanangu. Pia baba yako ameondoka lakini tumebaki na madeni mengi makubwa, kama unavyojua kipindi cha mwanzo fedha zote za matibabu tulikuwa tunaazima kwa watu,” alisema mama.
Kuhusu hilo la madeni, nilimwambia nitalimaliza na hakuna tatizo na ili kumfanya awe na amani, palepale tulianza kuorodhesha watu wote waliokuwa wanatudai na viwango vya fedha, tukajumlisha fedha zote kisha nikamhakikishia mama kwamba kabla sijaondoka nitampa akawalipe.
“Unazo hela zote?”
“Ndiyo mama!” nilimjibu kwa kujiamini, basi akashindwa kujizuia, akanikumbatia huku akianza tena kulia. Sijui kwa nini alikuwa akinikumbatia analia sana kwa sababu hiyo haikuwa mara ya kwanza.
Basi nilimhakikishia kwamba nimemuelewa na nitayafanyia kazi mambo yote aliyoniambia, nikainuka na kuelekea kule chumbani nilikokuwa nimehifadhi ule mzigo wa fedha niliokuja nao, nikahesabu kiasi cha madeni yanayotakiwa kulipwa, nikaziweka pembeni kisha zile nyingine nikazifunga vizuri kwenye mfuko, nikarudi kule nilikomuacha mama.
Nilimkabidhi burungutu la hela za madeni, kisha nikampa ulemfuko mwingine uliokuwa na mabunda kadhaa ya fedha, nikamwambia anihifadhie lakini kama kutakuwa na mahitaji yoyote pale nyumbani, asisite kutumia.
“Umepata wapi mihela yote hii mwanangu?” aliniuliza huku akiwa ni kama haamini.
“Nafanya kazi mama, na bosi wangu aliposikia nimefiwa, ameguswa sana na kunipa fedha kwa ajili ya kunisaidia masuala yote ya msiba,” nilimwambia, akanikumbatia tena na kuanza kuzihesabu zile fedha.
Niliona kabisa mikono yake ikiwa inatetemeka kwa sababu fedha zina tabia moja, ukipewa kiwango kikubwa ambacho hujawahi kukishika katika maisha yako, lazima utetemeke. Tena ukiambiwa kwa mfano uzitoe sehemu moja kwenye nyingine ndiyo kabisaa! Fedha nyingi zinaogopesha sana.
Basi baada ya muda, tuliaga, ikiwa ni takribani saa mbili za usiku, kabla sijaondoka niliwagawia fedha ndugu zangu wote, kila mmoja kwa ajili ya mahitaji yake madogomadogo, wakanishukuru sana na kuniona kama mkombozi wao.
Tulitoka na Bonta mpaka kituoni, kwa muda ule, magari yalikuwa ni ya kuvizia kwa sababu muda ulikuwa umeenda sana. Tukiwa pale kituoni tukisubiri gari, Bonta alinipa ile bastola yangu pamoja na zile fedha.
Nilijaribu sana kumdadisi kwamba yeye aliionaje bastola hiyo wakati nilikuwa nimeificha kwenye sanda? Akaniambia kwa watu wanaopata mafunzo kila siku kama mimi na yeye, ni rahisi kwa mmoja kugundua mwenzake anawaza nini haraka.
“Nilijua hawawezi kukukamata na bunduki kwa sababu hata kama ulikuwa umelewa, wewe siyo mjinga kiasi hicho. Walivyoondoka na wewe, mimi nilikuwa mtu wa kwanza kuingia kule chumbani, nikatafuta kila sehemu lakini sikuiona, nikajua lazima itakuwa pale kitandani, na kweli niliiona kwenye sanda,” alisema Bonta na kunifanya niishiwe na maneno.
Tuliendelea kusubiri usafiri na kwa bahati nzuri, tulipata lifti kwenye gari lililokuwa limebeba mananasi. Bonta aliniambia kwamba usafiri huo ni mzuri zaidi kwetu kwa sababu hakuna anayeweza kutushtukia, hasa ukizingatia kwamba ilikuwa ni usiku. Basi tuliianza safari, tukiwa tumebanana kule mbele kwa dereva.
Njiani tulisimamishwa na trafiki mara moja tu na wala hakuwa na shida na sisi bali dereva ambaye naye alipompa ‘kitu kidogo’, alituruhusu.
Hatimaye tuliwasili Gongo la Mboto, ikiwa ni karibu saa nne za usiku. Bonta akaniambia kwamba muda huo haukuwa mzuri kwetu kutembea, tukaingia kwenye baa moja iliyopo karibu na barabarani, tukala chakula na kunywa kidogo wakati tukivutavuta muda.
Kwenye kama saa sita kasoro hivi, tuliondoka kwa kutumia bodaboda mbili, tukaenda mpaka nyumbani kwangu, Sinza. Kwa jinsi tulivyokuwa tumechoka, ilibidi tupumzike kidogo, mimi nikaoga na kubadilisha nguo, kwenye kama saa tisa kasoro za usiku, tulitoka na safari ya kuelekea kambini kwa kutumia pikipiki ya Bonta ilianza. Kila kitu kilikuwa kikifanyika usiku kwa usiku.
Saa kumi na moja alfajiri, tayari tulikuwa tumeshawasili kambini Kibaha, tukakuta wenzetu ndiyo wanamalizia kufanya mazoezi. Kama zilivyokuwa taratibu za pale, tulisaini karibu sehemu tatu, kuanzia kule getini, mapokezi na kwa matron kuonesha kwamba tulikuwa tumerudi salama.
Kutokana na uchovu niliokuwa nao, nilienda moja kwa moja chumbani kwangu, nikavua nguo zote na kuzitupa pembeni, nikapanda kitandani na kujilaza na haukupita muda mrefu, nikapitiwa na usingizi mzito.
Nilipokuja kuzinduka, tayari jua lilikuwa kali na kilichonishtua, ni baada ya kuhisi kuna mtu alikuwa amelala pembeni yangu. Niliamka kichovu, kuangalia pembeni nikamuona Kezia akiwa amejilaza pembeni yangu, akiwa amejitanda na mtandio mwepesi bila kuwa na kitu kingine chochote.
“Pole na msiba mume wangu na pole na safari,” aliniambia huku akinikumbatia kwa mahaba na kuanza kunibusu sehemu mbalimbali za mwili wangu.
“Ahsante Kezia, asa...nte sa...na,” nilisema huku nikijaribu kujitoa kwenye mwili wake kwa sababu alikuwa akinifanyia uchokozi wa hali ya juu na kwa wakati huo sikuwa kwenye ‘mood’ ya kile alichokuwa anakitaka.
Nilifanikiwa kumtoa, akawa ananitazama usoni kwa mshangao.
“Umepatwa na nini tena, mbona umeumia hivyo?” alisema kwa upole. Kumbe muda wote hakuwa amenitazama vizuri, nikashusha pumzi ndefu na kumjibu kwa kifupi kwamba asiwe na wasiwasi mimi niko sawa.
“Uko sawa kivipi? Angalia jicho moja limevilia damu, usoni una alama nyingi, nani amekufanyia hivi?” Kezia alizidi kunidadisi huku akiendelea kunikagua mwili mzima.
Kiukweli kipigo cha wale askari kilikuwa kimenisababishia maumivu makali sana mwilini, kama isingekuwa uwezo wangu wa kuhimili maumivu, pengine nisingeweza hata kuinuka kitandani.
“Pole sana mume wangu,” alisema Kezia huku akiinuka, akavaa nguo zake harakaharaka na kuniambia nimsubiri. Alitoka na aliporudi, alikuwa na kiboksi cha huduma ya kwanza mkononi huku mkono mwingine akiwa ameshika birika la ‘heater’.
Akafungulia maji kwenye bomba la mle ndani na kujaza kwenye birika, akalichomeka kwenye umeme na kuanza kuchemsha maji. Maji yalipochemka, aliniandaa vizuri kisha akaanza kunichua maeneo yote yaliyokuwa na maumivu. Kiukweli alinisaidia sana kwa sababu nilikuwa na maumivu karibu mwili mzima.
Je, nini kitafuatia?
 
Duuuh..
SEHEMU YA 03

“Inuka na ufanye ninachokueleza, ukizingua unajua nini kitatokea,” nilisema kwa sauti ya chini lakini yenye mamlaka, yule mwanamke akakurupuka akiwa ni kama haamini kilichotokea, Suma naye akawa anatetemeka akiwa haelewi nimeingiaje pale

SASA ENDELEA...

“Snox! Nakuomba mdogo wangu, please show me some mercy!” (Nionee huruma tafadhali) alisema Suma huku akiwa anatetemeka kuliko kawaida lakini sikumjali.
“Look at my face!” (Nitazame usoni), nilimwambia kwa Kiingereza kilichonyooka, akanitazama usoni halafu akawa ni kama ameshtuka kidogo.

“Mlikuja mkanipiga na kunijeruhi kiasi hiki, mkamteka Saima wangu na kama hiyo haitoshi, mmekuja kuchoma moto nyumba yetu. Bado unategemea kwamba nitakuonea huruma?” nilisema huku na mimi nikitetemeka kwa hasira.
”No! Nisikilize kwanza Snox,” alisema huku akiniita kwa jina langu la kazi. Watu wengi mitaani huwa wanaamini Snox ni jina langu halisi kwa sababu kila ninakoenda ndilo linalotumika lakini ukweli ni kwamba halikuwa jina langu halisi wala halikuwa na uhusiano wowote na jina langu halisi.

Kiuhalisia jina langu naitwa Keneth au Kenny lakini kama nilivyosema, waliokuwa wakinijua kwa jina hilo, walikuwa wachache mno, tena wale wanaonijua tangu nikiwa mdogo lakini wengine wote walikuwa wakiniita Snox.
“Najua mlitumwa, nataka kujua mhusika ni nani,” nilisema huku nikimkokota taratibu kuelekea kule uani. Yaani ungeshuhudia kilichokuwa kinaendelea, pengine ungepata picha halisi ya kile wanachosema ‘sungura kamkaba tembo’.
Suma alikuwa na mwili mkubwa uliojengeka kimazoezi lakini licha ya ukweli kwamba mimi nilikuwa na kamwili kadogo ka wastani, nilikuwa namkokota kama ng’ombe anayepelekwa machinjioni.

Kwa jinsi nilivyoingia eneo lile mpaka kumpata, bado alikuwa amepigwa na butwaa na hiyo pekee ilitosha kumchanganya kichwa na kibaya alikuwa anafahamu akili zangu nikishika ‘mashine’ zinakuwaje kwani tumewahi kufanya ‘kazi’ pamoja.
“Nataka jibu, sitaki blaah! Blaah!” nilisema huku nikizidi kulikandamiza bomba la AK47 kwenye ubavu wake, nikaikoki na kumfanya ashtuke.
“Nitakwambia Snox, mimi na wewe tumeshakuwa kama ndugu, huna haja ya kutumia nguvu kwangu,” alisema Suma kwa upole, nikatega masikio kwa makini kumsikiliza.
“Mzee anasema umemsaliti, anataka kuhakikisha unapata taabu mpaka mwenyewe ukome.”
“Mzee gani?”
“Aah Snox, kwani nikisema mzee wewe unaelewaje? Kuna mwingine tena zaidi ya bosi?”
“Nimemsaliti kivipi?”
“Kitendo cha kukataa kazi bila sababu za msingi, kimemkasirisha sana na anasema atahakikisha anakomaa na wewe mpaka aone mwisho wako,” alisema Suma lakini maneno yake hayakuniingia akilini. Nilijua kabisa kwamba ananidanganya kwa sababu alichokisema hakikuwa na uzito wowote wa kumfanya mtu aniwinde kwa kiasi kile.
“Saima yuko wapi?”
“Sijui chochote kuhusu Saima, sikuhusika kwenye hiyo kazi.”
“Unanificha si ndiyo?”
“Snox, sina sababu ya kukuficha chochote ndugu yangu, ila labda Seba anaweza kuwa anajua chochote maana siku hizi ndiyo mtu wa karibu zaidi na mzee.”
“Nitampata wapi?”
“Lazima muda huu atakuwa anakula bata Trace Element, kule Masaki,” alisema Suma akitegemea kwamba baada ya maelezo hayo nitamuachia.
Kwa walichonifanyia, japokuwa sikuwa na nia ya kukatisha maisha ya mtu yeyote, lakini ilikuwa ni lazima niwashikishe adabu wote waliohusika halafu mwisho nitamalizia na huyo aliyewatuma, ambaye nilikuwa na hasira kali sana juu yake kwa alichonifanyia maishani mwangu.

Nilimsukuma Suma kwa nguvu, akakimbia na kusimama mbele hatua kadhaa mbele, akanigeukia haraka huku akiwa ameinua mikono juu maana alikuwa anajua ni nini ninachotaka kukifanya. Mara nyingi kama mtu amekuteka na mkononi ana silaha ya moto, anapokwambia ukimbie, au anapokusukumia mbali na yeye, usidhani anafanya hivyo kwa sababu kweli amekusamehe, mara nyingi ni kwa sabahu anataka apate nafasi ya kukulenga vizuri ili akupige risasi. Suma alilijua hilo na ndiyo maana alifikia hata hatua ya kunipigia magoti akiomba nisimfanyie chochote.

Sikutaka kusikiliza la muadhini wala mchota maji, nilifanya kile nilichoona kinafaa, mlio mkali wa bunduki ulisikika, na hasa ukizingatia kwamba ilikuwa imekatwa mtutu, mlio wake ulikuwa mkubwa na wa kutisha sana.
Sikupoteza muda, nilimruka pale chini alipokuwa ameangukia akitokwa na damu nyingi, nikachumpa kwenye ukuta na muda mfupi baadaye, nilikuwa nikiteremka upande wa pili wa ukuta. Nilijua kwa vyovyote lazima mlio huo urtasikika kwa polisi waliokuwa doria ambao lazima watakuja eneo hilo kwa hiyo nilipita njia tofauti na niliyojia.

Wateja waliokuwa wakiendelea kuburudika mle ndani kwa vinywaji na muziki, walishtuka mno kusikia mlio wa bunduki, tena kutokea ndani kabisa ya ‘chimbo’ lao, kila mmoja akaanza kutimua mbio kuokoa maisha yake, wengine wakikanyagana hovyo na kusababisha madhara yawe makubwa.

Zile purukushani zilinisaidia hata mimi kuondoka eneo hilo kwa urahisi zaidi kwani nilijichanganya na kujifanya na mimi naogopa mlio wa risasi, nikawa nakimbia ‘mdogo-mdogo’. Ungeniona wala usingeweza kuhisi kwamba mimi ndiyo nilikuwa chanzo cha mshike-mshike uliokuwa unaendelea.
Nilitokezea Sinza ya Mugabe baada ya kuwa nimekatiza sana vichochoro ili nisionekane na mtu yeyote. Nilisimama kando ya barabara na muda mfupi baadaye, bodaboda moja ilikuja, nikaipungia mkono na hatimaye ikasimama.
‘Duh, baba umepiga pigo za kijambazi kabisa! Niuzie hilo koti,” alisema dereva wa bodaboda huku akichekacheka, nikanyamaza tu kwani ninapokuwa nimeivaa sura ya kazi huwa sipendi kucheka kwa sababu nimewahi kufundishwa kwamba unapocheka, unaondoa uzingativu wa akili.

“Nipeleke Trace Element.”
“Trace Element au Element?”
“Nimekwambia Trace Element,” nilisema kwa msisitizo, yule dereva wa bodaboda akanywea na nikamuona kama ananitazama kwa macho ya kuibia hivi. Basi aliwasha pikipiki na tukaondoka huku kila mtu akiwa kimya kabisa. Njia nzima nilikuwa namsisitiza kuongeza kasi nadhani mpaka mwenyewe baadaye alikoma.

Basi baada ya kama dakika thelathini, tayari tulikuwa tumewasili Masaki, nikateremka kwenye bodaboda na kumlipa fedha zake kisha harakaharaka nikajichanganya na kuelekea kwenye chimbo lingine liitwalo Trace Element.
Unajua watu wengi wanapajua Club Element lakini hawajui kwamba kuna chimbo lingine la kijanja liitwalo Trace Element, ambalo ndani yake kuna watu wabaya wa kila aina.

Mara nyingi, wau wabaya huwa hawachangamani na watu wazuri mara kwa mara, hata wanapokunywa pombe, huwa wanatenga kujificha kwenye machimbo yao ambayo wanakutana wenyewe kwa wenyewe, hapo ndipo wanapokuwa na amani ndani ya mioyo yao kwani wakijichanganya na watu wasiowajua, kila anayemuona anahisi ni polisi au mpelelezi.
Kwa sababu mara kwa mara nilikuwa nakuja eneo hilo na wenzangu wakati nikiwa mwanachama kamili, nilikuwa nazijua njia nyepesi za kutoroka, hasa polisi wanapokuja kwa lengo al kufanya ukaguzi, niliamua kutumia njia hizohizo kuingilia kwa sababu nilikuwana uhakika pale getini nisingeruhusiwa kuingia.

Basi nilizunguka upande wa pili na kukwea juu ya mti uliokuwa jirani na fensi, nikatambaa na kujivuta juu kwa juu mpaka nilipopanda juu kabisa ya fensi, nikatafuta sehemu nzuri ya kurukia, nikadondokea ndani kimyakimya bila mtu yeyote kujua.

Unaweza kushangaa huu umahiri wa kuparamia kuta za watu, taha ndefu kiasi gani bila kushtukiwa na mtu yeyote nimeupata wapi? Katika kipindi chote nilichokuwa nafanya kazi za uhalifu, mimi ndiyo nilikuwa nategemewa zaidi kwenye masuala ya kuruka fensi na kwenda kufungua mageti kwa ndani.

Mara nyingi ili majambazi waingie ndani kwa urahisi, lazima mmoja atangulie ndani kupitia ukuta na akiingia, anaenda kufungua geti kwa ndani ili wote waliopo nje waingie na huko ndiko nilikopata ujuzi huo.

“Kumbe wakati napanda kwenye ule mti, mmoja kati ya walinzi wa eneo hilo, alikuwa ameshaniona na akawa anasubiri aone mwisho wangu. Nikiwa pale chini, nilishtukia bomba la baridi likinigusa shingoni, likifuatiwa na sauti ya ‘tulia hivyohivyo kwa usalama wako)’, nikajua nimepatikana.

Je, nini kitafuatia?

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
SEHEMU YA 40


ILIPOISHIA:
Akafungulia maji kwenye bomba la mle ndani na kujaza kwenye birika, akalichomeka kwenye umeme na kuanza kuchemsha maji. Maji yalipochemka, aliniandaa vizuri kisha akaanza kunichua maeneo yote yaliyokuwa na maumivu. Kiukweli alinisaidia sana kwa sababu nilikuwa na maumivu karibu mwili mzima.
SASA ENDELEA...

Maji ya moto ni dawa nzuri sana ya maumivu kwa sababu baada ya kumaliza kunichua, nilijisikia viungo vyote vikiachia, angalau sasa nikawa najisikia vizuri. Alihamia kwenye kile kiboksi, mle mlikuwa na vifaa vyote muhimu kwa ajili ya huduma ya kwanza.
Akaanza kwa kunisafisha lile jeraha langu la mguuni nililolipata baada ya kuruka ukuta kisha nikaenda kulitonesha kule msibani. Alinisafisha vizuri na kunifunga ‘plasta’, akaendelea kunisafisha maeneo yote niliyokuwa na michubuko ya hapa na pale, kisha akanipa dawa za kutuliza maumivu.
“Hapana! Nimekunywa pombe.”
“Hizi hazina tatizo, hata kama umekunywa,” alisema, basi nilipokunywa, nilizidi kujisikia vizuri, yale maeneo yaliyokuwa yamevimba kwa kipigo yakaanza kupungua na hata tabasamu kwenye uso wangu likarejea.
“Ni nani aliyekufanyia hivi?” Kezia aliendelea kuhoji, kwa sababu ya wema alionifanyia, sikuona kama kuna sababu ya kuendelea kumficha. Nilimsimulia kila kitu kilichotokea kwenye safari yetu, wakati mwingine akawa anasikitika, wakati mwingine anacheka.
“Napenda sana kuolewa na mwanaume wa aina yako, yaani una sifa zote ninazozitaka! Mwanaume unatakiwa kuwa mgumu kama wewe,” alisema Kezia huku akinikumbatia na kunibusu. Tuliendelea kupiga stori za hapa na pale na baadaye, tulijikuta tukiwa kama tulivyoletwa duniani.
Kwa mara nyingine tukaangukia dhambini huku Kezia akionesha kufurahishwa sana na kiwango changu ambacho kila siku kilikuwa kikiendelea kukua. Baada ya hapo, tulipata muda wa kutosha wa kupumzika na siku hiyo sikutoka kabisa nje, Kezia alikuwa akinihudumia kwa kila kitu.
Kutokana na hali yangu, nilipewa mapumziko ya siku tatu kutohudhuria mazoezini wala kupangwa kazi yoyote ya kutoka ili nipate muda wa kuomboleza kifo cha baba lakini pia ili mwili wangu ukae sawa.
Kwa hiyo Kezia alikuwa anakaa na mimi muda wote isipokuwa ule muda wa kwenda mazoezini tu ndiyo anatoka lakini akimaliza, anarudi tena mle ndani kwangu.
Lile angalizo nililopewa na Bonta kuhusu Gamutu wala sikuendelea kulijali kwa sababu huyo Gamutu mwenyewe kumbe alikuwa akiondoka mara kwa mara kwa hiyo muda mwingi hakuwepo pale kambini.
Kitu ambacho huwa kinaniumiza sana moyo wangu, ni kwamba Kezia alionesha mapenzi mazito sana juu yangu, alifanya kilakitu ambacho mwanamke anatakiwa kumfanyia mwanaume anayempenda lakini sijui ni akili za kitoto, kutoelewa maana ya upendo au ni moyo tu kushindwa kumchagua mtu, kiukweli nilikuwa namtumia kama chombo cha starehe tu lakini sikuwa na malengo yoyote juu yake.
Nitakuja kufafanua nini hasa ambacho kilitokea lakini kila nikikaa na kukumbuka mambo ambayo Kezia alinifanyia, moyoni nakiri kabisa kwamba hakustahili kulipwa mabaya na mimi.
Basi kwa kifupi ni kwamba kwa siku zote tatu, Kezia alikuwa akinihudumia kwa karibu kabisa, akinipa penzi zito ambalo lilinisahaulisha mambo yote yaliyotokea. Ile huzuni ya kumpoteza baba ilipungua sana, yale maumivu ya kuonewa na polisi nayo yalipungua sana na kiukweli, nilipata nguvu mpya.
Kitu kingine ambacho Kezia alikuwa akinisisitiza sana, ni kwamba kichwa changu hakikuwa kimezoea mambo ya mipombe mikali na mibange, akawa ananiambia kwamba kama nataka kunywa, basi ni bora ninywe bia, tena kwa kipimo lakini siyo kuparamia pombe kali kama alivyokuwa anafanya Bonta na wenzake.
Aliniambia kwamba wao walianza kunywa pombe muda mrefu uliopita, na hata umri wao ulikuwa ukiwaruhusu kulewa sana lakini kwangu mimi bado nina safari ndefu maishani kwa hiyo nikiendekeza pombe naweza kupoteza mwelekeo.
Ilivyoonesha ni kwamba Kezia alikuwa akiniandaa kuwa mwanaume anayemtaka, anayeweza kusimama imara kama mumewe. Hali hiyo ilinisaidia sana na kweli ndani ya kipindi kifupi tu, nikawa nimeshaweza kujidhibiti kwenye suala zima la ulevi.
Kazi zilikuwa zikiendelea, kila baada ya siku mbili au tatu, wanaume walikuwa wakitoka usiku wa manane kuelekea kazini na kurejea alfajiri kabla ya mapambazuko lakini kama nilivyosema, mimi sikupangwa, nilipewa muda wa kupumzika.
Tukio langu la kwanza kufanya, lilikuwa ni takribani siku kumi tangu kurejea kutoka msibani na siku hiyo nakumbuka alikuja bosi Mute mwenyewe kuzungumza na mimi. Ilikuwa ni ishu ya kwenda kuvamia benki moja pale Ubungo, sitapenda kuitaja jina kwa sababu maalum lakini naamini wengi watakuwa wanalikumbuka kwa sababu lilitingisha sana Jiji la Dar es Salaam.
Ishu ilikuwa hivi, bosi Mute aliniambia kwamba kuna wafanyabiashara wakubwa kutoka mkoani Arusha walikuwa wanakuja kuuza madini na wamepanga wakishamaliza biashara, waende kuweka fedha kwenye benki hiyo.
Hata sijui taarifa hizi za ndani alikuwa amezipata wapi lakini baadaye nilichokuja kujifunza, ukisikia ujambazi mkubwa umetokea benki, basi lazima wafanyakazi wa benki husika, iwe ni wale wa ndani au walinzi wa nje, wanakuwa wamehusika kwa namna moja au nyingine.
Sasa kilichotakiwa kufanyika, ni kwamba bosi Mute aliniambia kwamba mimi lazima niende kusoma mazingira ya eneo lenyewe, kuanzia jengo la benki lilivyokuwa, walinzi wanavyokaa, aina ya walinzi wanaolinda, ndani ya benki kukoje, barabarani kukoje na kila kitu.
Hiyo ndiyo ilikuwa kazi yangu ya kwanza kufanya nikiwa kama ‘master-mind’ na kiukweli bosi Mute alionesha kuniamini sana. Aliniambia kwamba kwa sababu hatuna uhakika kama katika matukio yote yaliyofanyika kuna mahali sura yangu imenaswa, ni vizuri nikabadili mwonekano.
“Ukivaa kisharobaro ni nadra sana mtu kukutilia mashaka, utaonekana kama mtoto wa mama ambaye huwezi kuwa na madhara yoyote,” alisema bosi Mute, akaendelea kunipa maelekezo yote muhimu na gia ambayo nilitakiwa kuingia nayo, ni kwenda kufungua akaunti nikitumia vielelezo bandia.
Baada ya mchongo mzima kukamilika, nilikaa kusubiri siku ambayo natakiwa kwenda kuanza kazi. Nakumbuka siku hiyo ilikuwa ni Jumatatu, niliondoka kambini Jumapili usiku na aliyenipeleka mjini alikuwa ni Bonta.
Aliniacha kwenye Hoteli ya Red Crescent iliyopo mkabala ya Stendi ya Ubungo kisha yeye akarudi kambini usiku huohuo, nikabaki peke yangu. Usiku huo ulikuwa mrefu sana kwangu, basi kesho yake asubuhi niliwahi kuamka kuliko kawaida na kujiandaa. Nikavaa nguo mpya nilizokuwa nimenunuliwa na bosi Mute kisha nikatoka na kuelekea kwenye benki hiyo.
Nilikuwa miongoni mwa wateja wa mwanzomwanzo asubuhi hiyo lakini kwa sababu nilikuw akwenye kazi maalum, sikutaka kuhudumiwa haraka. Niliifanya kazi yangu kwa umakini mkubwa kwa sababu bosi Mute alinisisitiza kwamba ndani na nje ya benki hiyo kuna kamera za CCTV zinazofuatiliwa kwa saa ishirini na nne kwa hiyo isipokuwa makini naweza kuishia pabaya. Baada ya kusoma ramani nzima ya mle ndani, ilifika zamu yangu ya kwenda kuhudumiwa.
“Karibu kaka, naomba nikuhudumie,” alisema msichana mmoja kwa uchangamfu, macho yangu yalipotua kwenye uso wake, nilijikuta nikitokewa na hali ambayo kiukweli haijawahi kunitokea maishani mwangu, nilihisi kama nimepigwa na radi hivi, mwili wote ukasisimka na kubaki nikimtumbulia macho msichana huyo.
“Vipi, mbona umeduwaa,” alisema, kauli ambayo ilinizindua kutoka kwenye ile hali niliyokuwa nayo.
“Mh! We dada ngoja tu nikupe sifa zako, wewe ni mzuri sana, yaani moyo wangu umelipuka kweli baada ya kukuona ndiyo maana unaniona kama nimezubaa,” nilisema huku nikiwa naendelea kumtazama.
Kiuhalisia huwa nina aibu sana hasa ninapokuwa jirani na hawa viumbe wa jinsia ya kike na angalau kidogo kukaa karibu na Kezia muda mrefu kulinifanya nianze kuwazoea lakini sijui ujasiri wa kumtamkia maneno hayo niliupata wapi.
Kitendo cha kufunguka, kilimfanya yule dada acheke sana kwa furaha, basi wakati akicheka mimi nikawa namtazama jinsi meno yake yalivyopangika vizuri mdomoni mwake. Kiukweli nilikuwa nimepatikana.
“Na wewe mbona mzuri kakaangu, kifua cha mazoezi kimefanya upendeze sana, unaitwa nani kwani?”
“Snox! Naitwa Snox,” nilisema kwa sauti ya kukauka kwani mate yalikuwa yamenikauka mdomoni. Licha ya uzuri wa sura yake, msichana huyo alikuwa mchangamfu kwelikweli, tofauti na wasichana wengi ambao wakishajijua kwamba wana sura nzuri, wanakuwa na nyodo kwa kila mtu.
“Nataka kufungua akaunti dadaangu, nimeuza shamba langu huko kijijini nimeona nije niweke akiba benki, hebu nipe utaratibu,” nilimuuliza, huku nikiwa makini kufautisha maelezo ya bosi Mute kama alivyoniambia.
Alinieleza mahitaji yote ya muhimu niliyokuwa natakiwa kuwa nayo, maelekezo ilikuwa nikwamba akishaniambia mahitaji hayo, nitoke na kujifanya naenda kufuatilia kisha nirudi baadaye ili nilizoee vizuri eneo la benki.
“Naomba namba yako ya simu tafadhali!” nilijikuta nikikiuka maelekezo ya bosi Mute kwa sababu alinisisitiza sana kwamba sitakiwi kuacha alama yoyote eneo hilo.
Aliniambia hata kama nitanunua vocha, sitakiwi kuikwangulia eneo hilo kwani polisi watakapokuja kufanya uchunguzi baada ya tukio, wanaweza kutumia ganda la vocha kuangalia namba iliyotumika kuingiza vocha hiyo, kisha wakaangalia nani anayemiliki hiyo namba ya simu na mwisho kunifikia.
“Mh! Na wewe handsome boy una haraka! Mara hii unataka namba ya simu, hebu ninunulie kwanza supu, mi sijanywa hata chai, ukishaleta hizo fomu nitakupa namba ya simu,” aliniambia huku akiwa amechangamka kwelikweli.
Basi niliingiza mkono mfukoni na kutoa burungutu la noti za shilingi elfu kumikumi, nikachomoa mbili na kumuwekea mezani. Kumbe kitendo cha mimi kutoa fedha pale, kwanza kilimzubaisha kwa sababu kwa mtu kama mimi kumiliki kiasi kikubwa cha fedha kama kile, ilikuwa ni maajabu.
Lakini jambo la pili, kumbe kwa sheria za benki, fedha zinatakiwa kutolewa kaunta tu na siyo pale mapokezi kwani kamera zilikuwa zinanasa tukio hilo na viongozi wake wangeweza kuhisi kwamba nampa rushwa.
“Nenda kampe yule dada wa pale dirishani, nitaifuata palepale,” alisema kwa uchangamfu, huku safari hii akinitazama kwa macho ya tofauti, nadhani fedha zilimtisha! Ama kwa hakika fedha ni uchawi wa Kizungu.
“Ahsante handsome boy!” aliniambia huku akicheka halafu kwa makusudi, akainuka harakaharaka na kujifanya kama anachukua faili pale nyuma kwenye kaunta, macho yangu yakatua kwenye mgongo wake, nikajikuta tu mapigo ya moyo yakinienda mbio kisha nikameza mate kama fisi aliyeona mfupa. Ama kwa hakika alikuwa ameumbika!
Basi nilifanya viol alivyonieleza huku nikiendelea kugeukageuka kumtazama, bado kidogo nijigonge kwenye kaunta kwa sababu ya kugeuka kumtazama, nikamuona akiwa anacheka kwelikweli, nikajua lazima na yeye amenielewa. Nilienda mpaka pale kaunta, nikampa yule dada zile fedha huku nikipitisha macho huku na kule kusoma ramani.

Itaendelea
 
SEHEMU YA 41




ILIPOISHIA:
Basi nilifanya viol alivyonieleza huku nikiendelea kugeukageuka kumtazama, bado kidogo nijigonge kwenye kaunta kwa sababu ya kugeuka kumtazama, nikamuona akiwa anacheka kwelikweli, nikajua lazima na yeye amenielewa. Nilienda mpaka pale kaunta, nikampa yule dada zile fedha huku nikipitisha macho huku na kule kusoma ramani.
SASA ENDELEA...

“Hizi za nini?”
“Yule dada pale amenipa nikuletee, anasema mhifadhie.”
“Nani, Saima?” aliuliza yule dada wa mapokezi huku akinitazama lakini pia akimtazama Saima pale alipokuwa amekaa, akampungia mkono na kumpa ishara fulani, basi yule dada akazipokea na kuziweka upande wa ndani wa ile ‘teller’ aliyokuwa amekaa.
“Kuna kingine nikusaidie kakaangu,” aliniuliza yule dada baada ya kuona macho yangu hayatulii, nikatingisha kichwa na kuachia tabasamu la uongo, nikageuka na kuanza kutoka huku macho yangu yakiendelea kusoma ramani ya jinsi jengo zima la benki lilivyokuwa.
“Bye!” alisema Saima huku tabasamu pana likiwa limechanua kwenye uso wake, nikampungia mkono huku na mimi nikitabasamu. Kwa uchangamfu alionionesha, nilijua hata iweje hawezi kuruka nitakapomtamkia kwamba nampenda na nataka tuingie kwenye uhusiano ‘siriasi’.
Nilitoka mpaka nje huku nikiendelea na kazi, nikawatazama walinzi waliokuwa kando kidogo ya mlango mkubwa wa kuingilia, nikatazama na upande wa pili ambako pia kulikuwa na walinzi wa kampuni binafsi ya ulinzi, wote wakiwa na silaha.
Nilitazama pia jinsi kamera za ulinzi (CCTV) zilivyokuwa zimefungwa, nikatoka mpaka barabarani na kusimama kwa sekunde kadhaa. Nikawa natazama jinsi magari yanavyoingia na kutoka kwenye eneo hilo la benki na jinsi magari ya kwenye Barabara ya Morogoro yalivyokuwa yakipishana.
Kwa jinsi eneo hilo lilivyokuwa, ili kufanikisha zoezi la kuondoka na fedha kwenye benki hiyo, ilikuwa ni lazima wawepo watu wa kuzuia magari barabarani kwa sababu eneo hilo magari yalikuwa yakipita kwa kasi sana.
Baada ya kuzugazuga kwa muda pale nje, nilivuka hadi upande wa pili wa barabara, nikatafuta sehemu na kukaa huku nikiwa naitazama ile benki vizuri. Baadaye nilitoka na kuelekea upande wa stendi ya mabasi yaendayo mikoani ya Ubungo, napo nilipasoma vizuri na kuona mwingiliano uliokuwepo kati ya pale stendi na ile benki.
Baada ya muda, nilitafuta sehemu na kukaa, nikaagiza soda na biskuti, nikawa navutavuta muda ili nirudi tena pale benki kwenda kukamilisha kazi niliyotumwa. Basi ilipofika mishale ya kama saa sita hivi, muda ambao hata nikimwambia yule dada kwamba nimetoka kufuatilia vielelezo alivyoniagiza hawezi kushtuka, niliinuka pale nilipokuwa nimekaa na kuanza kujisogeza kule benki.
Kila hatua niliyokuwa napiga ilikuwa na maana kubwa sana, nilikuwa nikifuatilia taarifa zote kuhusu benki hiyo, nikaingia mpaka ndani ambapo nikiwa pale mlangoni wakati naingia, kumbe tayari yule dada ambaye sasa nilikuwa najua kwamba anaitwa Saima baada ya kumsikia rafiki yake akilitaja jina hilo, alikuwa ameshaniona.
“Handsome boy!” aliniita huku akichekacheka baada ya kuniona, nikaingia na kwenda kukaa pale kwenye kiti cha wateja, yeye akiwa amekaa nyuma ya meza, tukawa tunatazamana huku tabasamu pana likiwa limechanua kwenye uso wake.
“Umechelewa! Sikuhudumii mpaka nikale lunch kwanza, upoo!” alisema huku akisimama na kujifanya anaweka faili kwenye kabati lililokuwa na mafaili nyuma ya pale alipokuwa amekaa, kwa mara nyingine nikawa nautazama mgongo wake, safari hii kwa karibu kabisa.
Pia kitendo cha yeye kusimama, kilifanya pafyumu nzuri aliyokuwa amejipulizia, isikike vizuri kwenye pua zangu, nikajikuta nikiwa kwenye hali mbaya zaidi.
“Twende nikakununulie lunch, tukija ndiyo nitakufungulia akaunti, umeshakamilisha kila kitu,” alisema huku akinyoosha mkono akitaka nimpe ile bahasha niliyokuwa nimeishika. Akatoa zile nyaraka zilizokuwemo mle ndani na kuanza kukagua moja baada ya nyingine.
“James Mwihava! Kumbe unaitwa James, handsome boy!”
“Saima bwana! Kwa nini unapenda sana masihara, ntakuchapaa,” nilimtania, akashtuka sana kusikia nimelitaja jina lake, akawa ananitazama kwa mshangao.
“Umelijuaje jina langu?”
“Nimelijua, kwani kuna ubaya wowote?” nilimwambia, nikaona aibu za kikekike zimemjaa usoni.
“Twende huku utanieleza vizuri,” alisema huku akizunguka kwenye ile meza na kutokea upande wa pili, akaenda kwa yule rafiki yake pale kaunta, wakawa wanazungumza huku wakinigeukia, kisha akaja pale alipokuwa ameniacha, tukaongozana na kutoka.
“Umependeza mama!” nilimwambia huku nikiendelea kumtazama kwa matamanio ya hali ya juu.
“Mh! Nimependeza wakati nimevaa sare, labda useme sare zetu nzuri,” alisema Saima huku akipunga mkono na kuita Bajaj, ikaja na kusimama pale nje, watu wakawa wanatutazama, nadhani ni kwa sababu ya uzuri wa Saima.
“Ujue mimi huwa ni mgumu sana kumzoea mtu ghaflaghafla, sijui kwa nini wewe nimekuzoea ghafla kiasi hiki handsome boy!” alisema Saima tukiwa kwenye Bajaj, nikaishia kucheka tu.
“Mchumba wako anaitwa nani?” aliniuliza wakati tukiteremka pale Blue Pearl.
“Ninao wengi, sasa sijui wewe unamzungumzia yupi,” nilimwambia huku nikicheka, naye akacheka na kuniambia eti naonekana mimi ni ‘kivuruge’. Sikutaka kuwa siriasi sana kwa sababu ukweli ni kwamba nilikuwa nimetokea kumpenda sana huyu msichana na Bonta amewahi kunifundisha kwamba wanawake wengi huwa hawapendi wanaume ambao wako ‘siriasi’ sana.
“Mwanamke hata kama ni mzuri vipi, ukimuingia kwa gia ya masihara ni rahisi kumteka, mfanye afurahi tu na onesha kumjali,” mafunzo aliyokuwa ananipa Bonta yalikuwa yakipita ndani ya kichwa changu wakati tukiendelea kupiga stori za hapa na pale na Saima.
Tuliingia kwenye hoteli hiyo na kukaa kwenye cafe ya kisasa, wahudumu ambao ilionesha wanamfahamu Saima, wakatuchangamkia na kutuhudumia. Kwa hesabu za harakaharaka, chakula kilicholetwa pale mezani, kilikuwa na thamani kama ya shilingi elfu kumi na tano kwa kila mmoja, kwa hiyo jumla ilikuwa ni shilingi elfu thelathini.
Ujue kama umezoea kula msosi wa shilingi elfu mbili kwa mama ntilie, usije ukarogwa ukaingia kichwakichwa kwenye hizi hoteli kubwakubwa kwa sababu chakula kilekile unacholipia shilingi elfu mbili, usishangae ukaambiwa shilingi elfu kumi.
Hata hivyo kwa sababu fedha hazikuwa tatizo kwangu, sikuwa na wasiwasi, tukaanza kula huku mara kwa mara nikimtazama Saima usoni.
“Usiniangalie sana bwana mi najisikia aibu,” alisema Saima baada ya kuona nazidi kumkazia macho. Hii ni siri nyingine aliyonifundisha Bonta kwamba kama unampenda msichana au mwanamke, jitahidi kumtazama machoni anapozungumza.
“Sasa unanionea aibu ya nini jamani!”
“Mh! We hujui kwa nini?”
“Ndiyo sijui! Basi ngoja nikulishe kabisa ili kama ni aibu uone vizuri,” nilimwambia huku nikikata kipande cha kuku na kumlisha, basi akacheka sana kwa furaha.
“You know how to behave like a real gentleman! I feel good how you treat me like a queen!” (Unajua namna ya kusimama kama mwanaume wa kweli! Najisikia vizuri jinsi unavyonijali kama malkia!) alisema Saima, safari hii na yeye akiwa ananitazama machoni, tukawa tunatazamana.
“Ooh! Im sorry! Aaah!” alisema huku akikwepesha macho yake harakaharaka baada ya kuwa tumetazamana kwa sekunde kadhaa. Sijui nini kilimtokea nilichogundua ni kwamba baada ya kutazamana naye kwa sekunde kadhaa, kila mmoja alimtazama mwenzake ndani kabisa ya macho, Saima alipoteza kabisa utulivu.
“Muda wa lunch umeisha, tuondoke!” alisema Saima huku akikusanya vitu vyake pale mezani na kutaka kuinuka.
“Subiri kidogo!” nilimwambia huku nikisimama, akakaa huku akigeukia upande wa pili, akiwa hataki kabisa kutazamana tena na mimi. Basi nilimfuata yule mhudumu aliyetuhudumia, nikatoa noti tatu za shilingi elfu kumikumi na kumkabidhi, sikusubiri sijui alete bili kisha nisaini, mambo ya Kizungu hayo mimi sijayazoea.
Harakaharaka nilirudi pale nilipomuacha Saima, nikampa ishara kwamba tuondoke, akafungua pochi yake na kutoa noti tatu za shilingi elfu kumikumi kwa ajili ya kulipia, nikamwambia asiwe na wasiwasi nimeshalipa.
“Lakini mimi ndiyo niliyekutoa lunch, ulipaswa uniache nikulipie.”
“Usijali, utanilipia siku nyingine, ahsante sana kwa ukarimu wako,” nilisema huku nikimshika mkono kwa lengo la kumuongoza ili tutoke. Kumbe kitendo cha mimi kumshika mkono kikawa kimeenda kuamsha mambo mengine, tukajikuta tumetazamana tena, safari hii tukiwa karibu kabisa.
Ama kwa hakika Saima alikuwa ameumbika, uso wake haukuwa na kovu hata moja, alikuwa na rangi fulani hivi ya kuvutia sana, meno yake yalikuwa meupe na yaliyopangika vizuri, mdomo wake sasa! Alikuwa na lips fulani hivi nzuri sana, nikajikuta navutiwa kuendelea kumtazama tu.
“Ooh! Stop it, James stop it!” alisema huku akijitoa kwenye mikono yangu, akaanza kutembea harakaharaka kuelekea nje, kumbe watu wote waliokuwa mle cafe, walikuwa wakitutazama, huku nyuma tukaacha minong’ono mingi ikiendelea huku wengine wakicheka.
Hakunisemesha chochote, tukatoka mpaka nje na japokuwa palikuwa jirani na pale benki, tulipanda tena Bajaj, ikaenda kutushusha pale nje, tukaingia ndani na moja kwa moja akaenda kwenye meza yake, wateja kadhaa wakawa wanamsubiri. Alishindwa kuanza kunihudumia mimi, ikabidi nikae kwenye foleni na hiyo ilikuwa nafasi nzuri sana kwangu ya kuendelea kuusoma mchezo mzima.
Mara kwa mara nilikuwa nikimtazama Saima kwa macho ya kuibia lakini yeye wala hakuwa na ujasiri wa kunitazama tena, akawa bize na wateja mpaka ilipofika zamu yangu. Akainua uso wake na kunitazama, na mimi nikamtazama, tukawa tunatazamana.
“Mh!” aliguna Saima kisha akakwepesha macho yake, alionesha kukosa kabisa utulivu. Ikabidi nimsaidie kumrudisha kwenye ‘mudi’ ya kazi.
“Uliiweka pale bahasha yangu,” nilimwambia, kweli alipotazama juu ya ‘printer’, aliiona, akatoa nyaraka zote zilizokuwa mle ndani, akachukua fomu fulani na kuanza kujaza taarifa zote za muhimu. Hakunisemesha chochote, kwa hiyo na mimi hiyo ikawa nafasi nzuri ya kuendelea na kazi yangu.
Nilikuwa makini sana asije akagundua chochote, alipomaliza aliinuka na kuniambia nimfuate, kweli nikamfuata. Akanipeleka kwa mhudumu mwingine na kumpa maelekezo huku akimkabidhi zile fomu zangu.
“Ukimaliza uje pale kwangu, nakusubiri,” alisema huku akiondoka, nikatabasamu. Yulemhumudu mwingine aliichukua ile fomu yangu na kuanza kujaza taarifa zangu kwenye kompyuta, akanielekeza nini cha kufanya, ikiwa ni pamoja na kuweka saini ya dole gumba. Dakika chache baadaye, akawa ameshamaliza.
Nililipia gharama za kufungua akaunti, na nikaweka shilingi laki moja kama kianzio kwenye akaunti hiyo, akaniambia kwamba nitapigiwa simu kadi yangu itakapokuwa tayari, nikajaza fomu nyingine pale kisha nikawa nimeshamalizana naye.
Muda huo ulikuwa umetosha kabisa kwa mimi kufanya kazi yangu, nikatoka na kumfuata Saima ambaye safari hii nilimkuta akiwa hana mteja, isipokuwa yuko bize na kompyuta yake.
“Hicho kidani chako ulichovaa mkononi kizuri,” nilimchokoza, akaniangaliakwa macho yaliyojaa ujumbe mzito, kisha akanionesha ishara kwamba nikae.
“Hii itakuwa kumbukumbu yangu kwako, ukinimiss kitazame, sawa eeh!” alisema huku akivua kile kidani chake kilichokuwa kinang’ara, akanivalisha mkononi huku akiwa makini kuhakikisha hakuna mtu mwingine yeyote anayeona kinachoendelea kwa sababu hakikuwa kikihusiana na kazi. Kilikuwa kidani kizuri kwelikweli, basi nikamshukuru pale na mwisho nikamkumbushia ombi langu la namba yake ya simu.
Alichukua kikaratasi, akaandika namba zake kisha akakikunja na kusimama, akanipa ishara kwamba tutoke, nikatangulia mbele na yeye akawa ananifuata. Tulitoka mpaka nje, akanisindikiza mpaka pale kwenye Bajaj.
“Kwani unaelekea wapi?”
“Sinza!” nilimjibu kwa sababu licha ya kwamba usiku uliopita nililala kwenye Hoteli ya Red Crescent hapohapo Ubungo, maelekezo niliyopewa na bosi Mute, asubuhi nitakapotoka hotelini hapo, sikutakiwa kurudi tena kwa sababu za kiusalama.
“Naomba nikulipie Bajaj mpaka Sinza,” aliniambia huku akinioneshea Bajaj ya kuingia, nilifanya hivyo. Cha ajabu, na yeye alipanda na kitu cha kwanza alichokifanya, ilikuwa ni kunikumbatia kwa nguvu, sikujivunga kabisa, na mimi nikamkumbatia kisha nikambusu, kitendo ambacho kilionesha kumsisimua mno kwani muda huohuo mapigo ya moyo wake yalianza kumuenda mbio.
“Mimi huwa nina dharau sana kwa wanaume, sijui wewe umenipa nini yaani, nimetokea kukupenda ghafla halafu sitamani uondoke James, nakuomba usinielewe vibaya, I love you so much!” alisema Saima kwa sauti iliyoonesha kumaanisha kile alichokuwa anakisema.
Kufumba na kufumbua tukagusanisha ndimi zetu, mikono yangu ikawa inapita taratibu kwenye mwili wake. Kila kitu kilikuwa kimetokea kwa haraka mno, yaani ungeweza kufananisha na ajali.

Je, nini kitafuatia?
 
SEHEMU YA 42



ILIPOISHIA:
Mimi huwa nina dharau sana kwa wanaume, sijui wewe umenipa nini yaani, nimetokea kukupenda ghafla halafu sitamani uondoke James, nakuomba usinielewe vibaya, I love you so much!” alisema Saima kwa sauti iliyoonesha kumaanisha kile alichokuwa anakisema.

SASA ENDELEA...
Kufumba na kufumbua tukagusanisha ndimi zetu, mikono yangu ikawa inapita taratibu kwenye mwili wake. Kila kitu kilikuwa kimetokea kwa haraka mno, yaani ungeweza kufananisha na ajali.
“Nipigie simu, namba yangu hiyo hapo! Nataka jioni nikitoka kazini tuonane,” aliniambia, akanibusu tena na kuteremka kwenye Bajaj, akawa anatembea harakaharaka kurudi kule benki.
“Daa! We jamaa unafaidi sana! Umempa nini huyu dada? Yaani anaringa sijapata kuona, nashangaa kwako amekuwa mlaini kabisa,” alisema dereva wa Bajaj ambaye kumbe alikuwa akitutazama kwa macho ya kuibia, nikaishia kucheka tu.
Nilimuelekeza sehemu ya kunipeleka, akaondoa Bajaj na muda mfupi baadaye, tulikuwa barabarani tukielekea Sinza. Basi njia nzima yule dereva wa Bajaj alikuwa ananipa stori za Saima na jinsi alivyokuwa akiwatoa nishai wanaume waliokuwa ‘wakimshobokea’ kutokana na uzuri wake.
Kwa sifa zile alizonipa, moyoni nilijiapiza kwamba kama Saima atanikubalia ombi langu, nipo tayari hata kumuoa. Basi alinifikisha mpaka Sinza, nikataka kumlipa lakini akaniambia tayari nilishalipiwa, eti Saima alikuwa ameshamlipa, nikatabasamu huku yule dereva wa Bajaj naye akitabasamu, harakaharaka nikateremka kwenye Bajaj na kuanza kuelekea pale kwangu.
Maelekezo niliyopewa na Bosi Mute ilikuwa ni kwamba nikimaliza kazi nirudi kambini moja kwa moja, lakini niliona nitakuwa sijautendea moyo wangu haki kama nitaondoka bila kufika kwangu, lakini kubwa zaidi kama sitapata nafasi ya kuonana na Saima jioni kama mwenyewe alivyoniambia.
Niliingia ndani kimyakimya na kwenda kwenye kioo, jinsi nilivyokuwa nimevaa siku hiyo, ilikuwa vigumu sana kunigundua kwamba ni mimi kwa sababu kiukweli nilikuwa na mwonekano mwingine tofauti kabisa.
Nilijicheka sana baada ya kugundua kwamba kumbe pale wakati Saina ananibusu, aliniachia lipstick kwenye mdomo wangu, nikaanza kujifuta huku nikiendelea kucheka.
Niliingia chumbani kwangu, nikavua nguo na kuingia bafuni, nikajimwagia maji kisha nikarudi chumbani na kujilaza kitandani, mawazo juu ya Saima yakiwa yanapita ndani ya kichwa changu. Kiukweli nilijiona kuwa mwenye bahati kubwa sana siku hiyo.
Nilichukua kile kikaratasi alichoniwekea Saima kwenye mfuko wa shati langu, nikakifungua na kuitazama namba aliyokuwa ameniandikia kwa mwandiko mzuri. Nilikitazama na kile kidani cha mkononi alichonipa, moyo wangu ukajawa na hisia tamu za mapenzi huku nikijiapiza kwamba endapo nitaonana na Saima jioni hiyo, lazima ‘nifanye kweli’.
Nilipomaliza kuisevu ile namba, wakati najiandaa kumpigia Saima, mara simu yangu ilianza kuita.
Ilikuwa ni namba ngeni, harakaharaka nikapokea kwa sababu miongoni mwa masharti ya kazi zetu, ilikuwa ni kupokea simu haraka hata kama namba huijui kwani wengi wetu walikuwa na kawaida ya kubadilisha namba mara kwa mara ili iwe vigumu kwa askari kuwashtukia hata kama wakiamua kufuatilia mawasiliano ya simu.
Nilipoiweka tu simu sikioni, niligundua kwamba kumbe aliyekuwa amenipigia alikuwa ni Bosi Mute, swali la kwanza akaniuliza mahali nilipo.
“Nipo Sinza bosi.”
“Aliyekwambia uende Sinza ni nani?” aliniuliza, nikakosa majibu na kuanza kujiumauma. Alipoona sina majibu, aliniuliza kuhusu kazi ambayo kimsingi ndiyo iliyonitoa Kibaha, nikamwambia nimeikamilisha kwa asilimia mia moja.
“Nakuhitaji huku kambini haraka iwezekanavyo, chukua bodaboda mpaka Bunju, Bonta yupo pale anakusubiri,” aliniambia kisha simu ikakatwa.
“Daaah!” nilijisemea huku nikiinuka harakaharaka na kwenda kuvaa nguo zangu. Kwanza nilikuwa nimechoka na nahitaji kupumzika, lakini pia nilikuwa na shauku kubwa ya kuonana na Saima lakini kwa simu ile, maana yake ni kwamba ratiba zote zilikuwa zimevurugika.
Sikutaka kabisa kumuudhi Bosi Mute, ndani ya dakika tatu nikawa nimeshamaliza kila kitu, nikafunga milango na kutoka hadi barabarani ambako nilisimamisha bodaboda na kumuelekeza kunipeleka Bunju.
Japo palikuwa ni mbali, bodaboda yule alikubali, akanitajia dau lake na bila hata kuomba kupunguziwa, nilikubaliana naye, nikapanda kwenye bodaboda na safari ya kuelekea Bunju ikaanza.
Baada ya kama dakika arobaini na tano baadaye, tayari nilikuwa nimeshafika Bunju, nikateremka na kumlipa bodaboda hela yake, nikatoa simu yangu mfukoni na kuanza kutafuta namba ya Bonta. Kabla hata sijampigia, nilisikia nikiguswa begani, kugeuka nyuma alikuwa ni Bonta, akiwa amevalia mavazi ambayo yalifanya iwe vigumu kumtambua.
“Twen’zetu,” aliniambia. Nilijiona mzembe sana kwa sababu katika kanuni tulizokuwa tunafundishwa kule kambini, ni makosa makubwa mtu anayekujua akatangulia yeye kukuona kabla wewe hujamuona. Tulikuwa tukifundishwa kuzitumia sana akili zetu mahali popote tulipo.
Alikuwa amepaki pikipiki yake pembeni, tukaongozana mpaka pale, akapanda kisha na mimi nikapanda, akaiondoa kwa kasi kubwa na kuwaacha madereva wa bodaboda wakipiga mbinja kwani muungurumo wake ulikuwa mithili ya ndege.
Hatukuongeleshana chochote mpaka tulipofika kambini, ambako Bonta alinipeleka moja kwa moja hadi kwa bosi Mute aliyekuwa ndani ya ofisi yake ya hapo kambini.
“Nipe ripoti,” alisema baada tu ya mimi kufika, nikashusha pumzi ndefu na kumsalimu kwa adabu kwanza, kisha nikaanza kumsimulia kila kitu kama alivyokuwa ameniagiza.
Nilimueleza mambo yote aliyohitaji kuyajua, nikamuona akitingisha kichwa chake kama ishara ya kukubaliana na mimi, akaniambia mimi ndiye nitakayekuwa kiongozi wa kazi hiyo kwa sababu tayari nimeshayasoma mazingira ya benki hiyo.
“Sawa mkuu,” niliitikia kwa adabu, akaniruhusu nikapumzike. Nilitoka ofisini kwake na kwenda mpaka chumbani kwangu, nikaingia na kujilaza. Bado kumbukumbu za Saima zilikuwa zikipita ndani ya kichwa changu, nikawa najilaumu kwa jinsi nilivyokosa nafasi ya kukutana naye jioni hiyo.
Nilichukua simu yangu na kutafuta namba yake, nikampigia. Simu iliita mpaka ikakata bila majibu, nikapiga tena lakini bado hakukuwa na majibu yoyote. Nilihisi huenda hapokei kwa sababu namba haijui, nikaamua kumtumia meseji, nikamwambia mimi ni James, jina la bandia nililolitumia kufungulia akaunti pale benki.
Basi nilipotuma tu meseji hiyo, ndani ya muda mfupi sana simu yangu ilianza kuita, kutazama namba ya mpigaji, alikuwa ni Saima, nikajua kweli nilichokihisi ndiyo ukweli, moyoni nikaanza kuamini maneno ya yule dereva Bajaj kwamba Saima alikuwa na msichana anayeringa sana, nikatabasamu na harakaharaka nikaipokea.
“Handsome boy!” aliita Saima kwa sauti iliyochangamka kwelikweli, basi na mimi nikamchomekea: “Nambie cute baby!”
Akacheka sana na kuniuliza mbona nimechelewa kumpigia? Nikamjibu kwamba nilikuwa nimepata dharura kidogo na muda huo ndiyo nimetulia.
“Mimi nimeshatoka kazini, niko Mlimani City hapa nazugazuga, nilikuwa nasubiri simu yako ujue, haya niambie nije mpaka wapi,” alisema na kunifanya nipate wakati mgumu kwelikweli.
“Nimetoka kidogo niko Kigamboni, kuna dharura ilitokea,” nilimjibu, akaonesha kukwazika sana na majibu yangu. Ilibidi nianze kutumia usanii kumtuliza, nikamwambia aendelee tu na ratiba zake tutaonana kesho yake.
“Kwa nini lakini unanifanyia hivyo James jamani?” alisema kisha simu ikakatwa. Nilimtumia meseji ndefu ya kumuomba radhi, nikatumia uongo wa hali ya juu kumfanya anielewe, akanijibu tu kwa kifupi ‘poa’.
Nilijisikia vibaya sana, nikajua kwa jinsi msichana mwenyewe jinsi alivyokuwa mzuri, na sifa zake nilizopewa, anaweza kuamua kubadilisha maamuzi na kunichinjia baharini. Nikiwa bado naendelea kumtafakari, mara mlango ulifunguliwa, akaingia Kezia huku akiwa na bashasha za hali ya juu.
“Umeniletea zawadi gani,” aliniuliza na kabla sijamjibu, akakiona kile kidani nilichokuwa nimevaa mkononi, alichonipa Saima.
“Whaooo! Kizuriii, umejuaje kwamba huwa napenda sana ‘bracelets’ alisema huku akinivua, nilishindwa kumzuia, akakivaa kwenye mkono wake wa kushoto na kuanza kujiangalia.
“Ahsante sana mpenzi wangu, kumbe unanipenda eeh,” alisema Kezia, ikabidi tu nitabasamu kwa sababu kama ni kufosi kingi, Kezia alikuwa fundi kwelikweli. Tuliendelea na stori za hapana pale lakini akili zangu zote zilikuwa kwa Saima.
Unapozungumzia tafsiri ya msichana mrembo, basi Saima alikuwa mzuri kwelikweli, yaani hata sijui niuelezee vipi uzuri wake, itoshe tu kusema kwamba alikuwa ameumbwa akaumbika haswaa.
Tukiwa tunaendelea na stori za hapa na pale, Bonta alikuja kunigongea mlango, nikatoka ambapo aliniambia kwamba Bosi Mute amesema nikawaelekeze jinsi mpango mzima ulivyo kwa sababu kesho yake ndiyo siku tunayotakiwa kwenda kufanya kazi, kwa hiyo lazima wauelewe mchongo mzima vizuri kisha tufanye mazoezi.
Nilirudi ndani na kuvaa, harakaharaka nikatoka na kumuacha Kezia mle ndani. Kwa kawaida tunapoenda kwenye kazi kama hizo, huwa haturuhusiwi kuwa na simu, kwa hiyo simu yangu niliiacha mlemle ndani.
Tulienda mpaka kwenye chumba cha mikutano cha siri, ambapo niliwakuta wanaume wa kazi wakiwa wamekaa mkao wa kunisubiri, basi bila kupoteza muda, nilianza kuwaeleza jinsi mchongo mzima ulivyo, nikawaelekeza kwa mchoro jinsi jengo la benki lilivyokuwa, mahali fedha zilipokuwa zinahifadhiwa na mambo mengine yote, ikiwemo jinsi walinzi wanavyokaa.
Usikose next issue...
 
SEHEMU YA 43





ILIPOISHIA:
Tulienda mpaka kwenye chumba cha mikutano cha siri, ambapo niliwakuta wanaume wa kazi wakiwa wamekaa mkao wa kunisubiri, basi bila kupoteza muda, nilianza kuwaeleza jinsi mchongo mzima ulivyo, nikawaelekeza kwa mchoro jinsi jengo la benki lilivyokuwa, mahali fedha zilipokuwa zinahifadhiwa na mambo mengine yote, ikiwemo jinsi walinzi wanavyokaa.
SASA ENDELEA...

Baada ya hapo, tulitoka na kwenda mazoezini, ilikuwa ni kawaida kwamba kablaya kwenda eneo la tukio, watu wote mliopangwa lazima mkutane na kufanya mazoezi pamoja. Kezia naye alienda kuitwa, nikashangaa kusikia kwamba na yeye anatakiwa kuwepo kwenye kazi hiyo.
Tofauti na siku zote, Kezia alipofika alinitazama kwa jicho baya kwelikweli, nikajua mambo yameshaharibika. Nilijua lazima atakuwa ameshika simu yangu na ndiyo maana alikuwa na hasira na mimi kiasi hicho. Sikutaka kuruhusu mawazo juu yake yatawale sana kichwa changu, tukaanza kufanya mazoezi ya nguvu.
Mazoezi ya siku hiyo yalikuwa mazito na magumu kuliko kawaida, Gamutu ambaye alikuwa amerejea siku hiyohiyo, nadhani maalum kabisa kwa kazi hiyo, ndiye aliyekuwa anatuongoza na kama kawaida yake, huwa hana mchezo hata kidogo.
Tulifanya mazoezi ya nguvu kwa muda mrefu, kwenye kama saa saba hivi za usiku tukawa tumeshamaliza, kila mmoja akiwa hoi. Akatutaka tukapumzike mpaka saa kumi alfajiri ambapo tutakutana tena kwa ajili ya kupeana maelekezo ya mwishomwisho, tukatawanyika.
“Saima ni nani?” Kezia aliniuliza swali ambalo liliufanya moyo wangu ulipuke na mapigo ya moyo kuanza kunienda mbio.
“Ni rafiki yangu, nimekutana naye nilivyoenda mjini kwenye misheni.”
“Unanidanganya si ndiyo?”
“Sikudanganyi chochote Kezia, vipi kwani?” nilimuuliza huku nikimtazama usoni, nikakutana na uso wa mbuzi, akiwa amefura kwelikweli.
‘Kwa hiyo kumbe mimi unanitumia tu lakini wapo wanawake zako wengine ambao unawapenda si ndiyo?”
“Jamani Kezia, mbona unakuwa hivyo? Nieleze nini ulichokiona na nitakujibu maswali yako yote.”
“Ujue nakupenda sana Snox lakini naona unataka kucheza na moyo wangu. Mimi huwa sichezewi kiboyaboya kama unavyofikiria. Tangu nimekuja hapa wanaume kibao wananitongoza, wenye vifua vikubwa na mwonekano mzuri kuliko wewe lakini sina taimu nao, nimekuchagua wewe halafu unaanza kuniletea mambo ya kifala si ndiyo,” Kezia alizidi kutema nyongo, hali iliyonipa wakati mgumu sana kumtuliza.
“Sikia mama, twende ndani tukajadiliane, haya mambo mengine ni ya kuelewana tu, huna sababu ya kunikasirikia kiasi hicho,” ilibidi tu niwe mpole, akashusha pumzi ndefu na kunichimba mkwara kwamba anataka nikamueleze ukweli vinginevyo anauwasha moto usiku huohuo.
Basi tulienda naye mpaka kule kwenye chumba changu, usichokijua kuhusu Kezia ni kwamba anapokasirika, ule ‘usista duu’ anauweka pembeni na kuvaa uso wa mbuzi, huku akiwa anazungumza kihuni kwelikweli.
Ilibidi nitumie uongo wa hali ya juu, nikamueleza kwamba Bosi Mute wakati ananipa kazi, alinielekeza pia kutumia uwezo wangu binafsi wa kumtafuta msichana mrembo kwenye benki hiyo na kujifanya namtongoza ili kazi yetu iwe rahisi.
“Nimemuweka huyo kama chambo lakini siyo kweli kwamba nampenda, nawezaje kumpenda mtu mwingine ghafla wakati niko na wewe? Niamini mpenzi wangu,” nilisema kwa upole, Kezia akashusha pumzi ndefu na kidogo akaanza kuonekana kulegeza msimamo wake.
“Anaonekana amekupenda kwelikweli, cheki picha alizokutumia WhatsApp alisema Kezia, nikashtuka kwa sababu sikuwa na kawaida ya kutumia WhatsApp kwenye simu yangu japo nilikuwa nayo. Kumbe Saima alikuwa amenitumia picha zake nyingi, nyingine akiwa amejirekodi video eti akilia kwa nini nimekataa kuonana naye jioni hiyo.
“Mwambie kwamba una mke, tena mke mwenyewe mafia, nilitaka kumjibu bahati yake nikaja kuitwa kwenda kwenye mazoezi, namba yake nimeichukua, akiendelea atakutana na moto wangu,” alisema Kezia, nikashusha pumzi ndefu hasa baada ya kugundua kwamba hakuwa amezungumza naye chochote.
Basi ili kumtuliza Kezia, japokuwa wote tulikuwa tumechoka, nilimpa kile moyo wake ulichokuwa unahitaji, nikawa nimefanikiwa kumtuliza kabisa. Kwa kuwa alfajiri tulikuwa na mazoezi na aliyekuwa anasimamia alikuwa ni Gamutu, ilibidi atoke na kwenda kwenye chumba chake. Kile kidani aliondoka nacho, nikaamua kumuachia japo kwa shingo upande.
Alipotoka tu, harakaharaka nilichukua simu yangu na kufungua WhatsApp, nikaanza kuzitazama upya zile picha alizonitumia pamoja na video. Moto wa mapenzi ukazidi kukolea kwenye moyo wangu kwa sababu kama nilivyosema, Saima alikuwa mzuri kwelikweli na ilionesha kwamba alikuwa anaishi maisha fulani mazuri sana kwani video na picha alizonitumia, ilionesha kwamba amezipiga usiku huohuo akiwa chumbani kwake.
Ndani kwake kulikuwa kuzuri kwelikweli, kukiwa na vitu vingi vya thamani, nikazidi kupata picha kwa nini alikuwa anaringa kiasi kile kwa sababu ilionesha kwamba licha ya uzuri wake, lakini pia alikuwa ‘njema’ kiuchumi.
Hata sijui usingizi ulinipitia saa ngapi, nilikuja kuzinduka baada ya kusikia mlango ukigongwa kwa nguvu, nikakurupuka na kwenda kufungua mlango, alikuwa ni Gamutu.
“Umelala na nani humo ndani mbona nimegonga mlango muda mrefu hufungui,” alisema kibabe huku akinisukuma na kuingia ndani, akaangaza macho huku na kule lakini hakumuona mtu, akaniambia natakiwa kujiandaa haraka kwa sababu muda wa mazoezi umefika, nikamuitikia kwa heshima.
Sikutaka tena kuingia kwenye mgogoro wowote na Gamutu kwa sababu licha ya ukweli kwamba nilikuwa nimeokoa maisha yake, bado hilo halikuondoa ukweli kwamba alikuwa kiongozi wangu, tena mwenye hulka ya kibabe kwelikweli.
Ni hapo ndipo nilipokumbuka ushauri wa Bonta kwamba natakiwa kuwa makini sana na Kezia kwa sababu Gamutu alikuwa akimpenda sana na aliniona mimi kama ndiyo kikwazo cha yeye kumpata kirahisi.
Basi nilijiandaa harakaharaka na kuelekea kwenye uwanja wa mazoezi, muda mfupi baadaye wote tulikuwa tumeshakamilika, tukafanya mazoezi kwa mara nyingine, safari hii yakiwa ni yale ya kutumia zaidi silaha na kujihami, ilipofika saa kumi na mbili tulitawanyika kwa maelezo kwamba kila mmoja akajiandae kwani tunatakiwa kuondoka asubuhi hiyohiyo kuelekea eneo la tukio.
Tulipewa vifaa vyote muhimu kwa ajili ya kazi, ikiwa ni pamoja na silaha na nguo za kuvaa, kisha tukatawanyika. Hakukuwa na muda wa kupoteza, tulipata vifungua kinywa na ilipofika saa moja kamili, wote tuliokuwa tumepangwa kwenye kazi hiyo, tulianza kukusanyika kwenye ukumbi wa siri wa mikutano.
Tayari magari mawili, Toyota Alphard ya rangi nyeusi, tena mapya kabisa yalikuwa yamepaki pale nje. Kwa wasioyafahamu magari haya, yanafanana na Noah lakini yenyewe ni makubwa na ya kisasa zaidi, hata sijui bosi Mute alikuwa anayapata wapi magari mazuri kiasi hicho.
Tofauti na siku zote, asubuhi hiyo bosi Mute alikuwepo kuonesha kwamba alikuwa amelala palepale kambini, akatupa maelekezo ya mwisho na kuwatangazia wote kwamba mimi ndiye nitakayekuwa kiongozi wa msafara nikisaidiana na Gamutu.
Yalikuwa ni majukumu makubwa sana kuliko uwezo wangu lakini moyoni nikawa najiapiza kwamba nitaweza, hasa kutokana na ukweli kwamba nilikua nayajua vizuri mazingira ya mahali tulipokuwa tunaenda kufanyia kazi.
Nilipewa nafasi ya kutoa darasa la mwisho la jinsi mazingira tunayoenda kufanya tukio yalivyokuwa, nikaitumianafasi hiyo kueleza kwa ufasaha kiasi cha kila mmoja kuafiki niwe kiongozi wa msafara kwa sababu nilikuwa nayajua vizuri kwelikweli mazingira hayo.
Baada ya mimi kumaliza, bosi Mute alianza kugawa majukumu, akasema Kezia na jamaa mwingine aitwaye Suma, wenyewe kazi yao itakuwa ni kufunga barabara ili tutoke kwa urahisi baada ya kazi kukamilika, Bonta, Gamutu na wanaume wengine wanne, wao walipewa kazi ya kuingia kwenye vyumba kunakohifadhiwa fedha.
Mimi na wenzangu watatu, tuliambiwa kazi yetu itakuwa ni kupambana na walinzi pamoja na askari pamoja na kuwatuliza wateja wote tutakaowakuta pale benki. Bosi Mute akanigeukia tena na kusisitiza kwamba mimi ndiye nitakayekuwa na kazi kubwa zaidi kwa sababu kama nitashindwa kuwadhibiti askari na wateja, wenzangu wote hawawezi kufanya kazi yao kwa ufasaha.
Nikawa natingisha kichwa kuonesha kwamba namuelewa. Baada ya hapo, tulitoka na kuelekea kwenye magari, tukiwa jumla ya watu kumi na mbili. Tukaingia kwenye magari tukiwa tumegawanyika sitasita, ukijumlisha na madereva, jumla tulikuwa watu kumi na nne, jeshi kamili.
Saa mbili kamili tuliianza safari ya kuelekea jijini Dar es Salaam. Ndani ya magari, watu wote tulikuwa kimya kabisa, kila mmoja akitafakari ya kwake. Tulipitia njia ya Bagamoyo, tukapasua lami mpaka tulipofika Mwenge, tukakunja na kuingia Barabara ya kuelekea Ubungo.
Mpaka inafika saa tatu kama na dakika ishirini hivi, tayari tulikuwa tumeshafika Ubungo, tukagawanyika, gari moja likaingia sheli kuongeza mafuta, sisi la kwetu likapitiliza mpaka kwenye Hoteli ya Blue Pearl na kupaki pembeni.
Tukawa tunayasoma mazingira kutokea ndani ya magari huku madereva wote wakiwa wanawasiliana, tulichokuwa tunasubiri ilikuwa ni amri tu ambayo ilitakiwa itoke kwa Gamutu. Baada ya kujiridhisha kwamba kila kitu kipo sawa, tuligeuza gari na kuanza kuelekea pale benki tukipita ‘service road’ huku dereva akiendesha kwa kasi kubwa, tulipofika ile barabara ya kuingilia benki lile gari jingine nalo lilikuwa limeshafika.
Kezia na Suma ndiyo waliokuwa wa kwanza kuteremka, bunduki zikiwa mikononi, wote wakiwa wamevaa makoti marefu meusi na vitambaa vya kuziba nyuso zao, wakati watu wakiwashangaa, harakaharaka wote tulikokuwa ndani ya magari tukaruka na kuanza kufatua risasi kuwashambulia walinzi wa benki waliokuwa wamezubaa pale nje.
Gari letu likaingia barabarani na kufunga barabara, Kezia na Suma nao wakaanza kufyatua risasi, lile gari jingine likageuza na kuanza kurudi kinyumenyume kuingia pale benki. Lilikuwa ni tukio la kushtukiza kiasi kwamba hata wale walinzi, wakiwemo askari na walinzi wa kampuni binafsi, walishindwa kabisa kutuzuia.
Sekunde chache baadaye, tayari tulikuwa tumeshaingia ndani ya benki, tukafyatua risasi nyingi hewani na kutoa amri ya watu wote kulala chini, Gamutu, Bonta na wenzao wakaelekea kule kwenye vyumba vya kuhifadhia fedha.
“Atakayethubutu kunyanyuka namfumua ubongo, lala hivyohivyo,” nilipaza sauti kwa nguvu huku nikijaribu kuibadilisha ili hata kama kuna mtu ananijua, asitambue kama ni mimi. Wakati nayasema hayo, nilikuwa nikizunguka huku na kule, bunduki ikiwa mkononi, kidole kwenye ‘trigger’, tayari kwa chochote.
Mara macho yangu yalitua kwenye meza ya Saima, nilipotazama vizuri niligundua kwamba na yeye alikuwa ametii amri kwa kulala sakafuni. Kitendo cha mimi kuzungumza, alipatwa kama na mshtuko fulani hivi, akawa anageuka kwa kuibia huku akitaka kunitazama vizuri.
Usikose next issue...
 
SEHEMU YA 44



ILIPOISHIA:
Mara macho yangu yalitua kwenye meza ya Saima, nilipotazama vizuri niligundua kwamba na yeye alikuwa ametii amri kwa kulala sakafuni. Kitendo cha mimi kuzungumza, alipatwa kama na mshtuko fulani hivi, akawa anageuka kwa kuibia huku akitaka kunitazama vizuri.
SASA ENDELEA...
Mara macho yangu na yake yaligongana, kwa kuwa nilikuwa nimevaa ‘mask’ nilikuwa na uhakika kwamba hawezi kunitambua lakini cha kushangaza, tulipotazamana tu, harakaharaka alirudisha kichwa chake kule chini, akiwa ni kama hataki nigundue kama ameniona.
Nilibaki kama nimezubaa hivi kwa sekunde fulani, nilipokuja kugeuka, nilimuona mfanyakazi mwingine akijivuta sakafuni kusogea ukutani. Kwa kawaida, ndani ya mabenki huwa kunakuwa na vifaa fulani vya mawasiliano ya dharura ambavyo huwa vinafungwa maeneo ambayo kwa mtu mwingine ni vigumu kuviona, kama chini ya meza au jirani na anapokaa mfanyakazi yeyote wa benki.
Kunapotokea dharura yoyote, huwa wanafundishwa kubonyeza vifaa hivyo na kitendo cha kukibonyeza tu, kuna ishara zinatumwa moja kwa moja kwa makampuni ya ulinzi yanayohusika au kwenye vituo vya polisi.
Sasa alichokuwa anakifanya mfanyakazi huyu wa kiume, alikuwa anajiona kama yeye ndiyo mjanja kuliko sisi wote mle ndani, wakati wenzake tulikuwa tumekuja kwa ajili ya kazi na huko tulikotoka tumefundishwa kuua.
Nilimuelekezea bunduki yangu kisha nikavuta ‘trigger’, risasi tatu zikatoka mfululizo na kupiga ukutani, jirani kabisa na pale alipokuwa amelala. Japo nilikuwa na uwezo wa kumlenga kichwani, sikutaka kufanya hivyokwa sababu naye alikuwa ni kijana mdogo tu, ambaye ilionesha ndiyo kwanza alikuwa ameanza kazi. Mshtuko alioupata pale chini, mpaka nilimuonea huruma.
Nilichoweza kukiona ni majimaji yakichuruzika sakafuni na kulowanisha nguo zake, alishindwa kabisa kuzuia haja ndogo, cheza na mambo mengine lakini siyo manati ya mzungu.
“Mara ya pili nitapiga kwenye kichwa chako,” nilimshimba mkwara, akawa anatetemeka mithili ya mtu aliyetolewa kwenye pipa la barafu, nikawa naendelea na doria mle ndani, nikizunguka huku na kule, wakati mwingine nikipanda juu ya meza ili kuhakikisha hakuna yeyote anayekiuka amri ya kulala chini na kutulia.
Ndani ya dakika zisizozidi tatu, tayari Bonta, Gamutu na wenzao walikuwa wameshamaliza kazi kule ndani, kwa kutuia baruti za kupasulia miamba waliweza kuvunja ‘strong room’ na kutoka na sanduku kubwa la chuma, wakawa wanasaidiana kuliburuza kuelekea nje.
Niligeuka tena kumtazama Saima, macho yangu na yake yakagongana tena kisha harakaharaka akajilaza kama alivyofanya mwanzo. Mpaka hapo nilishahisi kwamba kuna kitu Saima atakuwa amekigundua, sikujali sana. Niliendelea na kazi yangu kuhakikisha hakuna anayeleta upinzani wa aina yoyote.
Bonta na wenzake wakalibeba lile sanduku la chumba ambalo lilionekana kuwa zito kwelikweli, tayari gari lilikuwa limeshasogezwa mpaka kwenye mlango wa benki, wakalipandisha na kutokana na uzito wake, gari lilididimia upande wa nyuma, wakaingia na gari likaondolewa kwa kasi ya kimbunga.
Nilitoa ishara kwa wenzangu kwamba tuondoke na ili kuwatuliza watu, ilibidi tufyatue risasi nyingi juu, zilizovunjavunja taa na kutoboa paa, kisha tukatoka kwa staili ya kupeana migongo, yaani huyu anatazama kule, huyu anatazama huku na mwingine anatazama upande mwingine, tukatoka mpaka nje.
Baada ya kufika nje, ilibidi tukimbie kwa sababu gari la akina Bonta lilikuwa limekwama kuingia kwenye barabara kuu, inaonesha Kezia na mwenzake walikuwa wamezidiwa nguvu. Kishindo tulichotoka nacho kilikua kikubwa kwelikweli, risasi zilipigwa utafikiri tupo vitani.
Madereva waoga wakawa wanayaacha magari yao na kukimbia kwa miguu, tukafanikiwa kuzuia magari ya pande zote na kipindi hicho bado barabara ya mabasi ya mwendo kasi haikuwa imejengwa kwa hiyo pale kulikuwa na barabara moja tu, mimi nikapita mbele na kuanza kuliongoza gari lililokuwa na mzigo kwa kupunga mkono na kumuelekeza dereva sehemu ya kupita.
Kabla hata sijafanikiwa kulitoa pale lilipokuwa limekwama, tulianza kusikia ving’ora vya magari ya polisi yakija kwa kasi eneo la tukio, ili kuwapunguza kasi, kwa pamoja tukawa tunafyatua risasi angani. Dereva alitumia akili ya ziada, akafuatisha nilichomuelekeza na kulitoa gari kwa kasi kubwa.
“Twende Snox!” alisema Bonta huku akifungua mlango, lengo langu mimi lilikuwa ni kurudi kwenye lile gari jingine tulilokuja nalo ambalo nalo dereva alikuwa akihaha namna ya kulitoa, kama unavyojua tena Ubungo kunavyokuwa na magari mengi.
Kauli ya Bonta ilinifanya nibadili mawazo, gari tayari lilishakolea mwendo, ikabidi nikimbie kwa kasi kubwa kulifuata huku nikiendelea kufyatua risasi, dereva akapunguza kidogo mwendo, nikawa nimeshafika, ‘nikachumpa’ kama mwanasarakasi na kuangukia ndani huku Bonta na wenzake wakinishikilia ili nisije nikaanguka, mlango ukafungwa na dereva akakanyaga mafuta kwa nguvu zake zote.
Gari likatoa mlio kama helikopta na kuanza kukimbia kwa kasi kubwa mno. Kumbe ile taharuki ya risasi tulizokuwa tunafyatua, ilisababisha madereva wapatwe na mchecheto, wakawa wanagongana hovyo pale kwenye taa za Ubungo na kusababisha barabara ijifunge kwa foleni.
“Shuka mdogo wangu katufungulie barabara,” alisema Bonta, nikaona kama wananitafutia kifo, yaani nishuke kwenye umati wote ule wakati huku nyuma tayari polisi wanakuja? Hata hivyo, niliwaza tena kwamba kama wote tutabaki kwenye gari, maana yake tutakamatwa kama kuku tukiwa hapohapo, nikaona potelea mbali, liwalo na liwe.
Nilifungua mlango wa lile gari kwa nguvu, nikashuka huku bunduki ikiwa mkononi, nikafyatua risasi kadhaa hewani kisha nikaanza kupaza sauti huku nikiwaelekeza madereva waliokuwa wanagombaniana kupita kuachia njia.
Ulikuwa ni uamuzi wa kishujaa sana kwa sababu kama miongoni mwa watu waliokuwa kwenye magari angekuwa na bunduki, angeweza kuniangusha kirahisi sana. Ujasiri wangu uliwapa nguvu sana akina Bonta, nao wakateremka, kila mmoja akiwa na bunduki mkononi, tukakiwasha pale kwenye mataa na ndani ya sekunde chache, tayari njia ilishafunguliwa.
Kwa bahati nzuri sana, lile gari la pili nalo lilikuwa limeshafika kwa hiyo alipopita dereva wa kwanza, alipita hapohapo dereva wa pili, tulipovuka tukafyatua tena risasi na kusababisha madereva waanze kuhaha tena, kila mmoja akitaka kukimbia na gari lake, barabara ikajifunga tena. Tukarukia kwenye magari na kuondoka kwa kasi ya kimbunga.
Hiyo ilikuwa na faida kubwa kwetu kwani polisi wasingeweza tena kuwahi kutufukuzia, magari yote mawili yakawa yanakimbia kwa kasi kubwa utafikiri yapo kwenye mashindano.
Basi tukawa tunagongesheana ngumi kama ishara ya kupongezana, Bonta akanikumbatia kwa nguvu, Gamutu naye akafanya hivyohivyo kwani nilikuwa nimeibuka nyota wa mchezo.
Tukiwa tumekaribia Mwenge, tulishtukia tukianza kushambuliwa kwa risasi kutokea nyuma, wote tukalala kwenye siti na kuanza kuangalia ni nini kilichokuwa kinaendelea.
Kumbe askari kama sita hivi waliokuwa wamepakizana kwenye pikipiki tatu, walikuwa wakitufukuza kwa kasi kubwa, basi Gamutu aliinuka kwa jazba na kumlenga dereva mmoja, akamimina risasi kama saba hivi, tukashuhudia pikipiki moja ikiruka kwa nguvu na kudondokea mtaroni huku askari wote wawili wakiangukia katikati ya barabara.
Wale wengine kuona vile, walifunga breki za ghafla, wote tukainuka na kuwapiga pigo takatifu, wote wakadondoka kwenye lami, lilikuwa ni tukio la sekunde chache sana, nikawa nayakumbuka mafunzo tuliyokuwa tunapewa kule Kazimzumbwi na yule mwalimu wetu, ambaye alisema kwa mtu mwenye silaha, sekunde moja inatosha kabisa kubadilisha stori yote.
Tayari tulishafika Mwenge, madereva wote wawili wakaingia kwa kasi kubwa kwenye barabara ya bagamoyo na kusababisha taharuki kubwa kwa watu mbalimbali, wakiwemo wafanyabiashara eneo hilo kwa sababu magari yalikuwa yakienda kwa kasi kubwa mno huku yakiwa yanaenda sambamba, yaani hakuna aliyepo nyuma wala mbele, yote yapo kwa usawa. Vuta picha magari mawili kwa pamoja yanakunja kwenye makutano ya Mwenge likiwa na kasi ya zaidi ya kilometa 120, tena taa zikiwa hazijaruhusu! Ilikuwa inatisha.
Mbele kidogo ilibidi dereva wetu aongeze kasi zaidi na kumpita mwenzake kwa sababu barabara ilikuwa nyembamba, upande wa pembeni kulikuwa na daladala zinapakia abiria, tukapita kama kimbunga na kuwaacha watu wote wakiwa wamepigwa na butwaa.
Hali ilikuwa inatisha mno, yaani kama kuna mtu angekuwa anavuka barabara kwa kasi ile, alikuwa anageuzwa na kuwa chapati ndani ya sekunde chache sana. Tuliendelea kupasua lami kwa kasi kubwa huku tukipiga kelele kwenye magari, kwani tayari tulishakuwa na uhakika na ushindi katika kazi ile ngumu na ya kutisha.
Je, nini kitafuatia?
 
Baharia Wa Buza

Shukrani kwa muendelezo.

USHAURI WANGU.

Unaweza ukaendelea kui post hapa hii hadithi,jamii forums haibebi watanzania wote wapenda riwaya kama hizi.
Sisi wachache tunaweza kuwa wapiga debe wako kwa watanzania wengine wasiokuwepo jamii forums ambao kimsingi ndio wengi katika kukinunua kitabu hiki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
SEHEMU YA 45








ILIPOISHIA:
Hali ilikuwa inatisha mno, yaani kama kuna mtu angekuwa anavuka barabara kwa kasi ile, alikuwa anageuzwa na kuwa chapati ndani ya sekunde chache sana. Tuliendelea kupasua lami kwa kasi kubwa huku tukipiga kelele kwenye magari, kwani tayari tulishakuwa na uhakika na ushindi katika kazi ile ngumu na ya kutisha.
SASA ENDELEA...
Kilichotufurahisha wengi, ni kwamba licha ya ugumu wa kazi yenyewe na mazingira yake, hakuna aliyekuwa amepigwa risasi kati yetu hata mmoja, na hilo ni miongoni mwa mambo yaliyofanya mimi nionekane kuwa shujaa wa nguvu kwa sababu ilikuwa nadra sana kwa ‘misheni’ za hatari kama zile, muwaangushe askari pamoja na walinzi binafsi, halafu nyie asiguswe yeyote kati yenu.
Mwendo tuliotoka nao ndiyo huohuo, hakuna sehemu dereva wetu alipunguza, yule wa nyuma naye akawa anakuja na moto uleule, yaani hata ingetokea kwamba tairi moja likapasuka, huo mzinga wake ulikuwa hauelezeki. Nadhani hiyo ndiyo sababu iliyomfanya bosi atupe yale magari, Toyota Alphard, tena mapya kabisa.
Tulipofika Bunju, ilibidi tuiache barabara ya lami na kuingia kwenye barabara za vumbi ambazo hata leo ukiniuliza ni zipi, sijui.
Lengo la kuingia kwenye barabara ya vumbi, tulijua lazima polisi watakuwa wanatufuatilia kwa hiyo kama tungeendelea kwenda na barabara ya lami, lazima wangepeana taarifa na kutuwekea kizuizi cha barabarani, au hata wangeweza kutufukuza na yale magari yao madogo, Golf ambayo yana uwezo wa kukimbia kwa kasi kubwa mno licha ya udogo wake.
Safari iliendelea kwa kasi, tukipita barabara za vichochoroni na hatimaye, tuliwasili kambini. Huwezi kuamini, tulimkuta bosi Mute akiwa anatusubiri kwa shauku kubwa, akizunguka huku na kule, huku akivuta ‘ciger’ kama hana akili nzuri. Aliposikia geti linafunguliwa, alitoka mbiombio na kuja pale magari yalipopaki, akiwa na ‘wenge’ la kufa mtu.
“Vipi za huko?”
“Safi! Tumekamilisha kama ulivyotuagiza,” nilimjibu kwa sababu hata alipouliza, alikuwa akinitazama mimi moja kwa moja, nadhani ni kwa sababu wakati tunaondoka alinieleza wazi kwamba mimi ndiyo nitakuwa kiongozi wa msafara pamoja na Gamutu na kwa kawaida, mnaporejea kazini lazima kiongozi wa msafara ndiyo atoe ripoti ya kilichotokea.
“Tumewapoteza wangapi?”
“Hakuna.”
“Majeruhi?”
“Hakuna!”
“Come oooon Snox!” alisema Bosi Mute huku akitanua mikono yake na kunikumbatia kwa nguvu, tayari akina Bonta nao walishateremka kwenye magari na kujipanga, akawa anapita kwa mmojammoja na kumkumbatia kwa furaha.
Aliwaita wengine ambao hawakwenda kwenye kazi na kuwaagiza waliteremshe lile sanduku kubwa tulilotoka nalo Ubungo. Lilikuwa zito kwelikweli, hata sijui Bonta na wenzake waliwezaje kulitoa kirahisi namna ile kule benki kwa sababu ‘vidume’ vilivyoshiba kama saba hivi, vilikuwa vikihaha kuliteremsha kwenye gari.
Likateremshwa na kufungwa na ‘crane’ maalum ya kunyanyulia vitu vizito, likaingizwa kule ndani kwenye karakana, wote tukaelekea kule karakana kwa lengo la kushuhudia likifunguliwa na mafundi vyuma ambao kazi yao ilikuwa ni hiyo tu. Mashine za kukatia vyuma ziliwashwa, mafundi wakaanza kulikata na muda mfupi baadaye, walifanikiwa kuukata mlango na ‘kuupachua’, wote tukakazia macho kutaka kujua kama je, yaliyomo yamo?
Mzigo uliokuwemo mle ndani, ulikuwa mkubwa mno kiasi kwamba hata bosi Mute mwenyewe, alipiga kelele na kushangilia kwa nguvu, akaja na kuanza kutukumbatia mmoja baada ya mwingine kwa furaha.
Taarifa zilizokuwepo ni kwamba tangu bosi Mute aanze kufanya kazi na vijana wake, hakuna siku ambayo wamewahi kufanya kazi kubwa iliyoingiza mzigo mkubwa kiasi hicho, ilikuwa imevunja rekodi.
Furaha aliyokuwa nayo bosi Mute ilikuwa haielezeki, kwa sababu kimsingi fedha zilikuwa nyingi kwelikweli.
Ilibidi zitolewe mle kwenye lile sanduku na kuwekwa pale mezani, pakajaa na kuweka mlima mkubwa kiasi cha kufanya maburungutu mengine yawe yanadondoka, ikabidi nyingine zijazwe kwenye mfuko wa sandarusi, ile inayotumika kuwekea mazao kama mahindi.
Hebu vuta picha, gunia la mahindi linafika nusu, hizo zote zikiwa ni fedha tu, unaweza kufanya makadirio mwenyewe zinaweza kuwa ni fedha nyingi kiasi gani. Basi mzigo uliingizwa stoo, kule kwenye vyumba cha chini ya ardhi, bosi Mute akasema hawezi kufanya chochote kwa muda huo kwa sababu amefurahi sana ndani ya moyo wake.
“Nataka tunywe, tulewe na kufurahi kwa kazi kubwa iliyofanyika, leo ni mwendo wa bata tu,” alisema bosi Mute kwa furaha, akashangiliwa kwa nguvu na muda huohuo tulielekezwa kuelekea kwenye bwalo la chini ambako tayari maandalizi ya ‘kula bata’ yalishaanza kufanyika.
Kreti nyingi za bia zilikuwa zimeshatolewa stoo pamoja na pombe nyingine kali, pakti nyingi za sigara na nilisikia kwamba eti ng’ombe mzima alikuwa ameangushwa siku hiyo kwa ajili ya kujipongeza. Nilichokuwa nampendea bosi Mute, alikuwa hana hiyana linapokuja suala la kutuburudisha.
“Leo nakuomba usinywe pombe,” Kezia alisema huku akiwa amenikumbatia, tukawa tunatembea taratibu kuelekea kule ukumbini.
Sikumjibu zaidi ya kucheka, nadhani kumbukumbu za vituko nilivyovifanya siku ile tuliporudi kutoka kwenye tukio la Kunduchi bado ilikuwa ikizunguka ndani ya kichwa chake.
Hata kabla Kezia hajazungumza chochote, mwenyewe nilishakuwa nimeamua kwamba sitaki kulewa, nilitaka kuwa na akili zangu timamu ili kuchanganua mambo kadhaa yaliyokuwa yanakisumbua kichwa changu.
“Nilikuwa sijui kwa nini watu wanakupenda sana na kukuheshimu, leo nimejionea mwenyewe.”
“Umeona nini?”
“Mh! Acha tu ninyamaze, elewa kwamba unastahili saluti yangu,” alisema Kezia huku akinipigia saluti, nikacheka kidogo na kurudisha uso wa mbuzi. Kuna kitu hakikuwa sawa ndani ya kichwa changu na hakika nilikuwa nahitaji sana kutuliza kichwa changu.
“Mdogo wangu, baadaye ukitulia naomba tuonane kwa hiyo hakikisha hulewi kwa sababu ninamazungumzo muhimu na wewe,” Bonta aliniambia wakati tukiingia ukumbini, akaniuliza swali lingine ambalo lilinifanya nicheke sana.
“Au umepanga kulewa kama siku ile?”
Nilijua tu kwamba angalizo alilonipa Kezia na hata hicho alichokisema Bonta, kilikuwa na lengo la kunikumbusha kwamba sitakiwi kulewa na kupitiliza, jambo ambalo hata mimi kuanzia mwanzo nilikuwa nimeshaliona.
Basi siku hiyo ilikuwa ni shangwe kwa kwenda mbele, watu walikunywa, wakala na kusaza, wakacheza muziki mpaka ikafika mahali, karibu asilimia tisini ya watu wote, wapo hoi kwa kulewa. Siku hiyo sikunywa pombe kabisa, kwa hiyo na mimi ikawa zamu yangu ya kuwasanifu wenzangu waliokuwa wamelewa.
“Mbona leo hujatupia vitu vyako? Unaumwa?”
“Hapana, nimeamua tu kupumzika.”
“Safi sana, unatakiwa kuwa unajitambua kama hivi, siyo watu wakukariri kwamba kila siku lazima ulewe. Nilitaka kukushukuru sana kwa kazi kubwa uliyoifanya na nimeamua kukupa ofa maalum,” alisema Bosi Mute aliyekuwa amenifuata pale kwenye kona nilipokuwa nimekaa nikiwa nimetulia.
“Nashukuru sana bosi.”
“Nitakupa mara tatu ya mgao watakaopata wenzako wote, bila wewe huu mpango usingekamilika kirahisi namna hii, najivunia sana kuwa na wewe kwenye himaya yangu,” alisema bosi Mute, kauli ambayo ilinifurahisha sana, tukakumbatiana kwa furaha huku akiniendelea kunishukuru sana.
Kiukweli nilifurahi sana kwa jinsi bosi alivyoonesha kunikubali, ujue hakuna kitu kizuri kama ufanye kazi mahali halafu uwe unajua kabisa kwamba bosi anakukubali!
Kazi tuliyokuwa tunafanya ilikuwa ni ya hatari sana lakini niseme tu kwamba namna tulivyokuwa tunaishi kwa upendo na mshikamano mkubwa, kuna wakati tulikuwa tukijisahaulisha kama ile ilikuwa ni kazi haramu.
Baada ya kumaliza kuzungumza na bosi Mute, nilitafuta upenyo wa kumkimbia Kezia ambaye alikuwa amelewa sana na sasa alikuwa akifanya mambo ya aibu hadharani, mara anikumbatie, mara anibusu, ilimradi shida tupu.
Nilipotoka, nilienda moja kwa moja chumbani kwangu na kwa sababu sikutaka usumbufu, nilijifungia mlango kwa ndani. Harakaharaka nikachukua simu yangu huku nikiwa na shauku kubwa ya kuwasiliana na Saima.
Niliposhika simu yangu tu, nilikuta ikiwa na missed calls za kutosha pamoja na meseji kibao. Namba yangu haikuwa ikifahamika na watu wengi, ikabidi nijiulize kulikoni mpaka iwe bize kiasi hicho? Ilibidi nianze kuangalia namba moja baada ya nyingine.
Nilichokigundua ni kwamba missed calls zote zilikuwa zimetoka kwa Saima, na hata meseji zote zilikuwa zimetoka kwake. Nilianza kusoma meseji moja baada ya nyingine harakaharaka, akaniambia kwamba eti wamepatwa na matatizo makubwa kazini kwao.
“Tumevamiwa na majambazi, wamevunja strong room na kuchukua hela kibao,” ilisomeka moja ya meseji yake, moyo wangu ukawapigwa na mshtuko mkubwa kwa sababu nilichokuwa nakijua ni kwamba wakati wa tukio lile, macho yangu na yake yalikutana, alinitazama machoni na mimi nilimtazama machoni, swali likabaki kuwa ni je, aliweza kunitambua? Kwa sababu nilikuwa nimevaa ‘mask’ iliyoziba sehemu kubwa ya uso wangu lakini kwa mtu mnayefahamiana, unaweza kujiziba uso mzima lakini akikutazama machoni tu, anaweza kukutambua vizuri kabisa.
Ilibidi nimuendee hewani kwa lengo la kutaka kujiosha, nilipuuza lile agizo la bosi Mute kwamba hakuna anayetakiwa kuwasiliana na simu kwa wakati huo kwa sababu inawezekana polisi wako bize wakijaribu kufuatilia kila taarifa ndogo waliyoipata kwa hiyo unaweza kujikuta ukiingia kwenye mtego.
“Haloo!”
“Haloo James! Ulikuwa wapi jamani nimekupigia simu muda wote huo inaita tu au ungesikia nimekufa ungefurahi? Wenzako tumevamiwa na majambazi leo asubuhi, watu wamepigwa risasi vibaya, walinzi wote wamekufa, hapa nilipo imebidi nirudi kwa mama maana najihisi kuchanganyikiwa mno,” alisema Saima kwa maneno mfululizo, huku akionesha kuwa na hofu kubwa ndani ya moyo wake.
“Mmevamiwa na majambazi? Wapi?”
Je, nini kitafuatia?
 
SEHEMU YA 46




ILIPOISHIA:
“Haloo!”
“Haloo James! Ulikuwa wapi jamani nimekupigia simu muda wote huo inaita tu au ungesikia nimekufa ungefurahi? Wenzako tumevamiwa na majambazi leo asubuhi, watu wamepigwa risasi vibaya, walinzi wote wamekufa, hapa nilipo imebidi nirudi kwa mama maana najihisi kuchanganyikiwa mno,” alisema Saima kwa maneno mfululizo, huku akionesha kuwa na hofu kubwa ndani ya moyo wake.
“Mmevamiwa na majambazi? Wapi?”
“Eeh! We unaishi dunia gani, hebu washa TV sasa hivi uangalie wanaonesha kwenye taarifa ya habari,” alisema kisha simu ikakatwa. Nilijifanyisha kama hakuna kitu chochote ninachokielewa kwa lengo la kuondoa ushahidi, kweli nikawasha TV na kukutana na taarifa ya tukio hilo.
SASA ENDELEA...
Ujue tatizo moja la haya matukio ya kihalifu, wewe uliyefanya unaweza kuona kama ni kitu cha kawaida sana, si ushazoea kufanya uhalifu? Lakini kwa wananchi wengine likawa ni tukio la kutisha kwelikweli.
Eti japokuwa mimi ndiye niliyekuwa ‘mastermind’ wa tukio lile lililofanikiwa kwa asilimia 100, nilikuwa naona kama kilichotokea ni kitu cha kawaida sana lakini nilipomsikiliza Saima presha aliyokuwa nayo, na kilichokuwa kinaoneshwa kwenye runinga, niligundua kwamba halikuwa tukio la kawaida kama mwenyewe nilivyokuwa nafikiria.
Lilikuwa ni tukio la kutisha kwelikweli, kwa sababu kwanza pale nje kwenye eneo walilokuwa wanakaa walinzi, wakiwemo askari na wale walinzi wa kampuni binafsi, palikuwa na madoa makubwa ya damu ukutani na sakafuni kwa sababu ndiyo mashambulizi ya nguvu yalipoanzia lakini pia, jengo lote la benki lilikuwa limeharibika vibaya utasema limepigwa na mabomu.
Lakini walipoanza kuoneshwa majeruhi waliokuwa wakiendelea na matibabu, nilishindwa kuendelea kutazama na kugeuzia uso wangu pembeni. Watu wengi walikuwa wamejeruhiwa, achana na wale askari waliopoteza maisha na miongoni mwa waliojeruhiwa, wengine maskini walikuwa ni wapita njia tu ambao hawakuwa na hili wala lile.
Nilijisikia vibaya sana kuwa sehemu ya watu wanaokatisha maisha ya watu wengine, na kuwajeruhi wengine wasio na hatia kwa sababu tu ya fedha. Nikiwa nimezama kwenye hali hiyo, simu yangu ilianza kuita, kutazama mpigaji alikuwa ni Saima, akaniuliza kama nilikuwa nimewasha TV?
“Dah! Inasikitisha sana Saima, kwa nini binadamu wengine wanakuwa wakatili kiasi hiki? Umepona lakini?”
“Namshukuru Mungu mimi sijaumia kabisa lakini kuna yule mkaka aliyekubeba kwenye Bajaj, amepigwa risasi ya mguu, wale walinzi pale nje wamekufa wote, yaani we acha tu, ni Mungu tu ametenda miujiza yake, ungeweza kusikia hata mimi nimekufa,” alisema Saima, moyoni nikawa najiambia kwamba ‘usingeweza kufa kwa sababu nilikuwa nakulinda’.
“Uko wapi kwani, yaani natamani sana nikuone labda moyo wangu utatulia,”alisema Saima, kengele ya hatari ikalia ndani ya kichwa changu. Kwa sheria zetu, kwa muda huo isingekuwa rahisi kuonana na mtu yeyote ana kwa ana, kwani ungeweza kuwa ni mtego wa polisi. Lakini pia hata kama isingekuwa mtego wa polisi, nilikuwa mbali sana na hakukuwa na uwezekano wowote wa mimi na yeye kuonana jioni hiyo.
“Niko huku Kigamboni,” nilimdanganya, ukimya ukapita kati yetu.
“Nikuulize kitu.”
“Niulize tu Saima,” nilisema huku mapigo ya moyo yakianza kunienda mbio kwelikweli.
“Kile kidani changu nilichokupa unacho?”
“Ninacho ndiyo, vipi kwani?”
“Kuna msala unataka kuniangukia huku, eti polisi wanasema wameokota kidani eneo la tukio lakini nilipokiangalia kinafanana sana na kile changu nilichokupa,” alisema Saima, kauli iliyofanya mapigo ya moyo wangu yalipuke na kuanza kunienda mbio kwelikweli. Ilibidi nimzugezuge kisha nikakata simu.
Nikatoka haraka na kumfuata Kezia ambaye bado alikuwa akiendelea kulewa kule ukumbini, akashtuka kuniona nakuja ‘mkuku’.
“Kile kidani kiko wapi?”
“Kidani gani?”
“Kile nilichokupa,” nilimwambia, naye akawa ni kama ndiyo anashtuka, akajishika mkononi, kidani hakikuwepo!
“Nilikivaa asubuhi wakati tunaenda kwenye kazi,” alisema, kauli iliyonichosha kabisa, nikajua siri inaenda kufichuka.
“Kwa nini unakuwa mzembe kiasi hicho Kezia? Angalia sasa tumeacha alama kwenye eneo la tukio.”
“Sikuelewi!”
“Hunielewi nini?”
“Kinachokupanikisha wewe ni nini?”
“Kidani kimeokotwa eneo la tukio.”
“Sasa wewe wasiwasi wako ni nini? Kwani kuna vidani vingapi vinavyofanana na kile?”
“Kina alama kile, lazima watatupata,” nilisema huku nikiwa nimechanganyikiwa kwelikweli lakini mwenzangu wala hata hakuonesha kujali, nadhani pombe alizokuwa amekunywa kuanzia mchana, ziliifanya hata akili yake isifanye kazi vizuri.
Niliachana naye na kurudi chumbani kwangu haraka, nikajifungia na kuanza kutafakari nini cha kumjibu Saima. Akili ilicheza kwa kasi kubwa, nikashusha pumzi ndefu na kabla sijaamua nini cha kufanya, simu yangu ilianza tena kuita, kutazama namba ya mpigaji alikuwa ni Saima.
Nilifikiria kama niipokee au la kwa sababu ukweli ni kwamba sikuwa na majibu. Nilipiga moyo konde na kupokea na ili kumpoteza maboya Saima, mimi ndiyo nilikuwa mzungumzaji mkuu.
“Unasema kwamba polisi wameokota kidani chako? Sasa kwani wao walijuaje kama ni chako?”
“Unajua kile kidani ni cha kipekee sana, kimetengenezwa kwa madini ya Tanzanite na ukikiangalia vizuri kina jina langu, sasa wakati polisi wanakiokota kuna mmoja kati ya walinzi wa hapo benki alikiona na kwa sababu amewahi kuniona nacho na akakisifia, akawaambia wenzake kwamba anahisi anamfahamu mwenye nacho,” alisema Saima na kuongeza:
“Nikaja kuitwa na kweli nilipofika, nilishindwa kukataa kwamba ni cha kwangu kwa sababu karibu watu wote pale kazini wanakifahamu na huwa wananisifia sana nikikivaa kwa jinsi kinavyong’ara.”
“Nahisi nitakuwa nilikidondosha jana pale wakati naondoka na Bajaj baada ya wewe kuwa umenipa.”
“Mh! Kama ni jana lazima watu wangekiona James, kwa jinsi kinavyong’aa isingekuwa rahisi watu kukipita bila kukiona tangu jana mpaka leo,” alisema Saima na kunifanya nizidi kuchanganyikiwa. Ilibidi tu niwe mpole na kuanza kumshawishi Saima asije akawaambia polisi kwamba alinipa mimi kwa sababu angeniingiza kwenye matatizo makubwa.
“Niachie mwenyewe nitajua namna ya kuzungumza nao,” alisema Saima kisha akakata simu. Moyoni nikawa najilaumu sana kwa sababu kilichofanyika kilikuwa ni uzembe wa hali ya juu.
Wasichokijua wengi ni kwamba askari wa upelelezi, hasa wale wa kikosi cha Crime Scene Investigation (CSI), huwa wana mafunzo maalum ya namna ya kuchunguza vidhibiti vyote vinavyookotwa kwenye eneo la tukio kisha kuunganisha nukta mpaka kupata picha kamili ya wahusika wa tukio.
Tulishafundishwa sana kuhusu kuwa makini tunapokwenda kwenye eneo la tukio na sijui kwa nini Kezia alifanya uzembe mkubwa kiasi hicho kwa sababu nakumbuka siku wakati Gamutu anatufundisha jinsi polisi wanavyoweza kutumia hata vocha iliyokwanguliwa na kutumika kisha ikatupwa eneo la tukio, kumpata mhusika.
Alitueleza kwamba wanao uwezo wa kuwasiliana na mamlaka ya mawasiliano au kampuni husika ya mtandao wa simu, kisha wakajua vocha hiyo imeingizwa kwenye simu gani na anayeitumia ni nani na huwa anawasiliana na nani mara kwa mara, kwa hiyo wanaanza kuwafuatilia watu wote na mwisho wanampata mhusika na kumkamata kisha kuanza kumhoji kwa kina mpaka wapate ukweli.
Lakini pia wanakuwana uwezo wa kufuatilia alama za vidole kwenye vocha iliyotumika na kumpata mhusika kwa kutumia vipimo vya kisasa vya DNA.
Unajua watu wengi wanaweza kudhani kwamba yale yanayoonyeshwa kwenye filamu za Hollywood, kwa mfano jinsi CIA na FBI wanavyofanya kazi zao wakadhani kwamba teknolojia hiyo bado haijafika hapa nchini lakini ukweli ni kwamba ipo na inafanya kazi viozuri kabisa.
Nikiwa bado natafakari, moyo wangu ukiwa na wasiwasi mkubwa, Saima alinipigia tena simu, nikasita kuipokea lakini nikaona hiyo inaweza kumpa wasiwasi zaidi, nikapokea lakini safari hii, wala hakutaka kabisa kuzungumzia kuhusu suala hilo, tukawa tunazungumza mambo mengine tofauti kabisa.
“Kwa hiyo leo pia siwezi kukuona?”
“Hatutaweza kuonana Saima, unaweza kudhani kwamba nafanya makusudi lakini ukweli ni kwamba ratiba yangu inanibana sana, tutaonana tu wala usijali,” nilimwambia Saima kwa lugha ya kubembeleza sana huku nikiwa makini nisije nikajikanyaga kwenye maelezo yangu, akakubaliana na mimi kwa shingo upande.
Akakubaliana na mimi kwa shingo upande kisha akaniambia kama nina salio, tuchati kwa meseji kisha akakata simu. Tukaanza kuchati, akawa ananieleza mambo mengi kuhusu maisha yake na familia yake, historia yake na mambo mengine mengi ambayo hata sikuwa namuuliza.
“Niambie kwa kifupi na wewe kuhusu historia ya maisha yako,” aliniambiakwenye meseji, huo ukawa mtihani mwingine kwangu kwa sababu ilikuwa ni kosa kubwa kujieleza kwa mtu yeyote kutokana na kazi zetu, kwa hiyo nikalazimika kubadilisha kabisa historia yangu, nikawa namwambia mambo ya uongo mtupu.
Japokuwa kuanzia mwanzo alishaniambia kwamba hakuna kitu asichokipenda kama uongo, sikuwa na namna zaidi ya kuendelea kumpanga kwa ‘uongo mtakatifu’. Tulichati mpaka usiku sana, tukaagana na kutakiana usiku mwema.
Tangu nionane na Saima ulikuwa ni muda mfupi sana umepita lakini kwa jinsi alivyokuwa amenizoea na kuniamini, ungeweza kudhani labda tumefahamiana hata miaka kumi iliyopita.
Sikupata usingizi mapema, bado kumbukumbu za tukio lile zilikuwa zikijirudia ndani ya kichwa changu na kama wahenga wanavyosemaga kwamba damu ya mtu ni nzito, hata usingizi ulipokuwa ukinipitia nilikuwa naweweseka sana na kuota ndoto za ajabuajabu.
Mwisho nikaamua kuamka na kwenda kufungua friji, nikatoa chupa ya pombe kali na kuanza kujimiminia kwa kasi. Ndani ya muda mfupi nikawa nimeshalewa, angalau sasa nilipojilaza nilipata usingizi. Yawezekana hii ndiyo sababu kubwa inayofanya wahalifu wengi wawe wanalewa sana, wanavuta bangi na wengine kujidunga madawa ya kulevya.
Katika hali ya kawaida, jinsi binadamutulivyoumbwa huwezi kufanya uhalifu mkubwa, hasa unaohusu kumwaga damu za watu wasio na hatia halafu moyo wako ukawa na amani. Kuna ile hali ya kuijutia nafsi, kujilaumu na kuwa na hofu kubwa huwa inatesa sana moyoni kiasi kwamba unaweza hata kuchanganyikiwa.
Besi kesho yake asubuhi, ratiba za pale kambini ziliendelea kama kawaida na kwa sababu bosi Mute aliahidi kukutana na sisi wote kwa ajili ya kila mmoja kupata mgao wake kulingana na kazi tuliyofanya, ilipofika saa mbili, watu wote walikuwa wameshaingia kwenye ukumbi wa siri wa mikutano.
Bosi Mute akaingia akiwa na brifkesi kubwa iliyobebwa na mmoja kati ya wapambe wake, akatusalimia kisha akaanza kumuita mmojammoja na kumpa bunda la hela, alianza na wale ambao hawakwenda eneo la tukio kwa sababu kwa kawaida ufanye kazi au usifanye, linapokuja suala la mgao lazima kila mtu apate chake, ingawa huwa viwango vinatofautiana.
Je, nini kitafuatia?
 
SEHEMU YA 47



ILIPOISHIA:
Bosi Mute akaingia akiwa na brifkesi kubwa iliyobebwa na mmoja kati ya wapambe wake, akatusalimia kisha akaanza kumuita mmojammoja na kumpa bunda la hela, alianza na wale ambao hawakwenda eneo la tukio kwa sababu kwa kawaida ufanye kazi au usifanye, linapokuja suala la mgao lazima kila mtu apate chake, ingawa huwa viwango vinatofautiana.
SASA ENDELEA...
Baada ya kugawa hela kwa wale wote, ilifika zamu ya sisi tulioenda eneo la tukio ambapo kila aliyekuwa akiitwa, alikuwa anapewa bahasha kubwa, zile zinazotosha kuingiza karatasi bila kulikunja ikiwa imejaa fedha ambazo zilikuwa zimepangwa vizuri.
Wa mwisho nilikuwa mimi, ambapo nilipofika pale mbele kwa bosi Mute, alinikabidhi bahasha kisha akanikumbatia na kuninong’oneza kwamba kama alivyoniahidi, atanipa mara tatu zaidi ya wenzangu lakini hataki wenzangu wajue kwa sababu wanaweza kujenga chuki.
“Bahasha zako mbili utazipitia kwa matroni, lakini hakikisha hakuna anayekuona,” aliniambia kisha akanishika mkono na kuanza kuzungumza kwa sauti iliyosikika na kila mmoja mle ukumbini.
“Huyu ndiyo ‘man of the match’, ni kijana mdogo sana kama mnavyomuona lakini nilichokitabiri kuanzia siku ya kwanza ndicho kinachoendelea kutokea, mliokuwa eneo la tukio jana mnajua ni kwa kiasi gani huyu chalii alifanya kazi kubwa, hebu mpigieni makofi tafadhali,” alisema bosi Mute, basi watu wote wakapiga makofi kwa nguvu huku wengine wakipiga miluzi kwa sauti ya juu.
“Snox, najivunia sana kuwa na wewe, nataka uendelee kujifunza kila siku ili uwe bora zaidi ya hapa, na nyie wengine naomba mumtazame jinsi Snox anavyojituma katika kazi na muige mfano kwake. Kuna wengi tu ambao tumekuwepo pamoja kwa kipindi kirefu lakini uwezo wenu ni wa kawaida sana.
“Hapa wote tunafuraha kubwa na kila mtu ana bahasha iliyojaa kwa sababu ya kazi nzuri ya Snox, yeye ndiye ‘aliyechora raketi’ na yeye ndiye aliyeongoza kazi kwa kusaidiana na gamutu, bila umakini na ushujaa wake leo tungekuwa tunatazamana tu hapa, au wengi mlioenda kwenye kazi msingerudi, huyu ni hazina yetu, tumpende, tumsaidie na tumuunge mkono,” alisema bosi Mute na kunikumbatia tena, watu wote wakashangilia sana.
Yaani zile sifa alizokuwa ananimwagia, zilikuwa ni nyingi mno mpaka ikafika mahali mwenyewe nikawa najishtukia kwamba huenda zikasababisha baadhi ya watu waanze kunichukia.
Basi baada ya hapom bosi Mute alitangaza kwamba kwa sababu za kiusalama, wote tulioenda kwenye kazi, hatutakiwi kuendelea kuwepo kambini hapo kwa sababu kama polisi wakigundua mahali tulipo, wanaweza kutuvamia na kusababisha matatizo makubwa.
Akasema tunatakiwa kujichanganya na kurudi uraiani lakini akasisitiza kwamba kila mmoja anatakiwa kuwa makini kujilinda yeye mwenyewe na kujiepusha na matukio yanayoweza kusababisha tukaingia matatizoni. Alitoa ratiba ya namna ya kuondoka kambini hapo akisisitiza kwamba kila mmoja anatakiwa kuondoka kivyake na kwenda kwenye makazi yake na kusubiri maelekezo mengine.
Msisitizo ulikuwa kwamba ni lazima kila mtu aende kwenye makazi yake na kutulia na pia akasisitiza kwamba hatutakiwi kuongozana au kukutana kwa namna yoyote mpaka atakapotoa maelekezo.
Baada ya hapo, watu wote walipiga makofi kisha tukatawanyika, akili zangu zote zikawa zinamuwaza Saima kwa sababu sasa ule muda niliokuwa nausubiri, ulikuwa umewadia.
“Tunafanyaje mshkaji wangu!” Kezia alisema baada ya kunifuata chumbani kwangu na kunikuta nikiwa napangapanga vitu vyangu kwenye begi dogo la mgongoni, tayari kwa safari ya kuondoka.
“Kuhusu nini?”
“Si tunaondoka wote?”
“Kwenda wapi?”
“Eeeh! Mbona unanijibu kavu hivyo!” Kezia alisema, nikashusha pumzi ndefu na kumtazama.
“Umefanya kosa kubwa sana la kutupa kidani changu eneo la tukio halafu mwenyewe unaonesha kuchukulia poa tu, kwa hiyo unataka nikuchekee?”
“Lakini kwani ni chako au changu? SI ulininulia mimi jamani?” alisema Kezia na kusababisha nipandwe na jazba, ilibaki kidogo niropoke kwamba sikuwa nimemnunulia yeye bali nilipewa na mwanamke ninayempenda kwa moyo wangu wote, lakini nilijitahidi kujizuia, nikawa naendelea kupanga vitu vyangu.
“Nisamehe mpenzi wangu, nilikivaa ili hata nikipigwa risasi nife nikiwa na kitu cha kumbukumbu kutoka kwako, nilifanya kwa mapenzi tu wala sikuwa na lengo lolote baya,” alisema Kezia huku akipitisha mikono yake kutoka nyuma na kunishika kiunoni.
“Tufanye yameisha,” nilimjibu kwa mkato, akanigeuza na kunikumbatia kwa nguvu, tukawa tunatazamana.
“Najisikia vibaya kukuudhi, tumekaa vizuri siku zote hizo tukiwa kwenye mazingira magumu kiasi hiki, leo nafasi ya sisi kwenda kuwa huru imepatikana unataka tuondoke tukiwa tumenuniana, nisamehe baba, nakiri makosa,” alisema Kezia kwa upole huku machozi yakiwa yanamlengalenga, nikashusha pumzi ndefu huku tukiwa bado tunatazamana.
“Nakupenda mwenzio, nataka tuondoke pamoja.”
“Lakini si umesikia maagizo ya bosi Mute kwamba hatutakiwi kuongozana sehemu yoyote?”
“Ni sawa lakini tunaweza kufanya ujanja tukawa pamoja bila ya mtu yeyote kugundua, nakuhitaji baba,” Kezia alizidi kunibembeleza, nikawa nauona ugumu nitakaokumbana nao kumchenga.
“Sawa Kezia, mimi pia nahitaji sana kuwa na wewe lakini hatutakiwi kufanya jambo lolote ambalo litafanya watu wagundue kwamba tuko pamoja. Nakuomba kila mtu aondoke kivyake halafu tupeane siku mbili tatu, mambo yakitulia tutakuwa pamoja, wala usijali,” nilimdanganya kisha nikambusu kwenye paji lake la uso.
“Unanidanganya!”
“Sikudanganyi, kweli tena,” nilisema huku nikipitisha mikono yangu kwenye kiuno chake, akawa anajinyonganyonga huku pumzi zake zikianza kubadilika.
“Unaniachaje sasa,” alisema huku akinisukumia kwenye kitanda, nikatii sheria bila shuruti na kuangukia juu ya kitanda, naye akaja juu yangu na kunilalia, tukagusanisha ndimi zetu huku mikono ya kila mmoja ikifanya utalii wa ndani kwenye mwili wa mwenzake.
Tukiwa kwenye hali hiyo, nilimuona akiinuka kidogo kisha akaanza kunifungua vifungo vya shati langu, nikajua kazi ipo. Sikutaka kumzuia chochote kwa sababu nilichokuwa nakitaka kwa wakati huo, ni kumfurahisha ili asiendelee kuniganda kwani kwa jinsi ninavyomjua, angeweza hata kuniharibia kwa Saima wangu.
Alipomaliza kwenye shati, alihamia chini, akanitoa magwanda yote kisha akahamia kwake. Muda mfupi baadaye, tulikuwa kama tulivyotoka kwenye matumbo ya mama zetu. Sijakaa sawa akakidaka kipaza sauti na kuanza kuimba nyimbo tamu, nikajikuta nikisisimka mno.
Muda mfupi baadaye, tayari ‘mkuu wa kaya’ alikuwa tayari ameshafura kwa hasira kali, akamshika na kumsukumizia sehemu anayotakiwa kuwepo kwa wakati huo, ikawa ni fujo mtindo mmoja. Safari hii yeye ndiye aliyekuwa nyota wa mchezo, alionesha kiwango cha hali ya juu dimbani kilichonifanya niwe nababaika mithili ya mtu anayetafuna bisi ngumu.
Mpaka kipyenga cha mapumziko kinapulizwa, alitoka kifua mbele akiwa na ushindi mnono mkononi. Tukapumzika kidogo na tulipoingia kwenye ngwe ya pili, sikukubali awe nyota wa mchezo tena, na mimi nikafanya kile nilichotakiwa kukifanya, akawa analalama tu.
“Nakupenda sana mwenzio, naomba usifikirie kuniacha,” alisema kwa hisia za hali ya juu, nikazidisha mashambulizi na muda mfupi baadaye, alitangaza kuiona theluji iliyopo juu ya Mlima Kilimanjaro, akanikamata kwa nguvu utafikiri tunacheza mieleka kisha akaangukia upande wa pili akiwa hoi.
Harakaharaka niliinuka na kwenda bafuni, nikajimwagia maji harakaharaka kisha nikarudi na kuendelea na maandalizi, yeye akiwa bado amelala, akionesha kuwa na uchovu wa hali ya juu.
“Kadiri siku zinavyozidi kusonga mbele ndiyo unavyozidi kuwa ‘mcharo’, nikigundua kama unanisaliti nitaku...” alisema huku akionesha ishara kwamba eti atanipiga risasi, nikacheka na kumuinamia pale alipokuwa amelala, nikambusu kisha nikaendelea kujiandaa.
“Kwani wewe unaondoka muda huu?”
“Ndiyo, kuna ishu nataka nikaifanye town.”
“Basi safari njema, take care na usisahau ahadi yetu,” alisema huku akiinuka kichovu, akanikumbatia tena na kunibusu kisha akaanza kuokota magwanda yake na kuyarudisha mwilini mwake, moja baada ya jingine.
Alipomaliza na mimi tayari nilikuwa nimemaliza, tukatoka pamoja na yeye akaelekea kwenye chumba chake wakati na mimi nikitoka kuelekea kwa matron ambako bosi Mute aliniambia kuna mzigo wangu mwingine nikauchukue lakini pia kukabidhi funguo kwa sababu hatukutakiwa kuondoka na funguo za vyumba vyetu.
Nilipofika, matron alinichangamkia sana, nadhani na yeye alikuwa ameshasikia taarifa zangu, akanipa daftari maalum la kusaini kisha akaingia ndani na alipotoka, alikuwa na bahasha kubwa mbili kama ile niliyopewa jana yake, akanikabidhi na kunitakia safari njema.
Ilibidi nifungue begi langu la mgongoni na kuziweka zile bahasha, mzigo ukaongezeka uzito. Ndani ya begi kulikuwa na nguo mbili tu za kubadilisha pamoja na viatu lakini sehemu kubwa ilikuwa imejaa maburungutu ya fedha, nikamshukuru na kuanza kutoka kuelekea kule kwenye geti la kutokea.
Kulikuwa na magari kadhaa pamoja na pikipiki na kila aliyekuwa anaondoka, alitakiwa kuchagua mwenyewe anaondoka na usafiri gani, mimi nikaona pikipiki ndiyo itakuwa rahisi zaidi.
Kitu ambacho namkubali bosi Mute, ni kwamba alikuwa na mipango mikali kwelikweli, magari yote na pikipiki, zilikuwa zimebandikwa matangazo huku madereva wakiwa wamevalia sare, kiasi kwamba mtu angeweza kudhani kwamba wanafanya kazi kwenye kampuni fulani inayotoa huduma kwa jamii.
Hali hiyoilifanya iwe vigumu sana kwa mtu yeyote kushtukia kwamba ni watu wa namna gani waliokuwa wakisafirishwa. Bila hata kumueleza chochote, dereva aliwasha pikipiki na kutoka getini, kisha tukaondoka kwa kupitia barabara ile iliyokuwa inaenda kukutana na ile inayotoka Bagamoyo.
Wakati safari ikiendelea, nilitoa simu yangu mfukoni na kutafuta namba ya Saima, nikaipiga, ndani ya muda mfupi tu akawa ameshaipokea.
“Niko njiani natoka Kigamboni, vipi wewe uko wapi?”
“Niko nyumbani.”
“Vipi tunaweza kuonana,” nilimwambia Saima, kauli ambayo aliipokea kwa shangwe kwelikweli, akaniambia alikuwa anaisubiri sana nafasi ya mimi kuonana naye. Kwa sababu ya upepo wa bodaboda, hatukuzungumza mambo mengi zaidi ya mimi kumwambia kwamba nitakuwepo Sinza, akaniambia na yeye anaenda kujiandaa kisha nikakata simu.


ITAENDELEA
 
SEHEMU YA 49




“Vipi tunaweza kuonana,” nilimwambia Saima, kauli ambayo aliipokea kwa shangwe kwelikweli, akaniambia alikuwa anaisubiri sana nafasi ya mimi kuonana naye. Kwa sababu ya upepo wa bodaboda, hatukuzungumza mambo mengi zaidi ya mimi kumwambia kwamba nitakuwepo Sinza, akaniambia na yeye anaenda kujiandaa kisha nikakata simu.
Nilijikuta nikitabasamu mwenyewe, safari ikaendelea huku nikiendelea kutafakari mambo mbalimbali ndani ya kichwa changu. Yule dereva alinipeleka mpaka Bunju, akaniambia wamepewa maelekezo kwamba waishie hapo.
“Kwa nini usinifikishe nyumbani?”
“Hapana! Unatakiwa kupanda daladala kama wenzako wanavyofanya,” aliniambia, akawa ni kama amenikumbusha kitu muhimu sana kwa sababu tulishapewa maelekezo kwamba njia nzuri ya kuingia mjini salama, ni kwa kutumia usafiri wa umma kwa sababu ni vigumu sana kwa askari wa Dar kusimamisha daladala na kuanza kuwapekua abiria, lakini ni rahisi sana kusimamisha magari binafsi, bodaboda au Bajaj.
Basi nilimshukuru kisha harakaharaka nikavuka upande wa pili wa barabara, nikapanda daladala inayoelekea Makumbusho huku begi langu nikiwa nimeligeuzia mbele na kulikumbatia. Safari ikaendelea huku muda mwingi nikiwa mtulivu sana, gari lilipofika Bamaga niliteremka na kupanda lingine ambalo lilienda kunishusha Sinza Madukani.
Ile nashuka tu, simu ya Saima ikawa inaingia, harakaharaka niliipokea, swali lake la kwanza likawa ni kama nimeshafika au bado.
“Nimeshafika, wewe uko wapi kwani?”
“Naelekea kwenye kituo cha Bajaj, kwa hiyo umesema nishukie wapi?”
“Sinza madukani,” nilimsisitiza, akakata simu. Nilitembea harakaharaka kuelekea nyumbani kwangu, huku nikiwa nimevaa kofia na kuishusha machoni, kiasi kwamba haikuwa rahisi kwa mtu yeyote kunitambua.
Japokuwa nilikuwa najua kwamba hakuna mtu anayenifuatilia, lakini moyo wangu bado ulikuwa na hofu kiasi kwambamarta kwa mara nilikuwa nikigeuka nyuma kuhakikisha niko salama.
Nilifika mpaka pale kwangu salama, nikafungua geti na kuingia mpaka ndani, nikalibwaga begi kwenye sofa kisha nikaanza kuvua nguo zangu kwa ajili ya kwenda kujimwagia maji. Muda mfupi baadaye, tayari nilikua nimeshaoga, nikajilaza kwenye kochi na kuwasha runinga, huku muda wote macho yangu yakiitazama simu.
Dakika chache baadaye, ilianza kuita, nikapokea harakaharaka ambapo Saima alinieleza kwamba tayari ameshashuka kituoni, ikabidi nimuelekeze kwa sababu isingekuwa sawa mimi kutoka tena na kwenda kituoni. Basi akawa anakuja huku nikiendelea kumpa maelekezo na muda mfupi baadaye, nilisikia geti likigongwa, tayari Saima alikuwa ameshafika.
Harakaharaka nikaenda kumfungulia mlango, macho yangu na yake yakagongana, akaachia tabasamu na kutanua mikono yake kama ishara ya kunikumbatia. Huwezi kuamini moyo ulipatwa na mshtuko usio wa kawaida, mapigo ya moyo wangu yakawa yananienda mbio kuliko kawaida.
Unajua hakuna mtihani mkubwa kama kukutana na mwanamke mrembo ambaye kwa kumtazama tu unajua kabisa huna hadhi ya kuwa naye! Hicho ndicho kilichonitokea kwa Saima, japokuwa nilikuwa najua kwamba ni mzuri sana, lakini siku hiyo uzuri wake ulikuwa ni kama umezidi kipimo, ungeweza kumfananisha na wale wasanii wa kike wa Kimarekani kwa jinsi alivyokuwa amevaa! Itoshe tu kusema kwamba alikuwa amependeza kwelikweli.
Basi nilijikaza kiume pale, na mimi nikamkumbatia, akanibusu shavuni na kunifanya nizidi kudata. Basi nilimkaribisha ndani na kumuonesha ishara kwamba akae, nikatoka na kwenda kufunga geti vizuri, nikarudi na kufunga pia geti la ndani na kuuacha mlango wa mbao wazi.
“Siamini kama nimekuona tena James,” alisema huku akiniita kwa lilejina bandia nililolitumia kufungulia akaunti.
“Kwa nini Saima jamani? Mimi mwenyewe siamini kama nimekutana tena na wewe,” nilisema huku utulivu ukiwa umeniisha kabisa, nilibaki kuzungukazunguka tu mle ndani, nikiwa hata sielewi nataka kufanya nini.
“Utakunywa nini?”
“Aah James, ndiyo kwanza nimefika unaanza kuhangaika na mimi, kukuona tu kumenifanya nisitamani kitu kingine chochote,” alisema huku tabasamu pana likiwa limechanua kwenye uso wake, basi nikaishiwa pozi na kulazimika kurudi pale kwenye kiti na kukaa pembeni yake.
“Kwa nini unakuwa bize kiasi hicho jamani,” alisema huku akinisogelea na kunikumbatia, na mimi nikamkumbatia huku mapigo ya moyo yakinienda mbio kwelikweli. Japokuwa awali nilikuwa nikimsifia sana Kezia kwamba ana shepu nzuri na ‘pigo’ zake ni za kisistaduu, kwa Saima ilikuwa ni funga kazi.
Manukato aliyokuwa amejipulizia yalikuwa yananukia vizuri kwelikweli kiasi cha kunifanya nizidi kuchanganyikiwa.
“Kazi ndiyo kila kitu mpenzi wangu, bila kazi unafikiri tutaishije mjini hapa? Na afadhali yenu wenzetu mliosoma,” nilisema kwa sauti iliyoonesha kabisa kubabaika, akacheka sana na kuzidi kunikumbatia kwa nguvu.
“Unaishi na nani hapa,” alisema huku akiniachia na kuanza kutazama huku na kule ndani ya chumba changu.
“Peke yangu,” nilimwambia, akawa ni kama anakumbuka kitu. Niliomba isije ikawa majibu yangu yamejichanganya kwa sababu nakumbuka pia kule benki aliniuliza swali hilohilo. Kwa bahati nzuri, hakuendelea kunihoji kuhusu suala hilo, akaanza kunisifia kwamba naishi sehemu nzuri sana.
“Kumbe mwonekano wako wa nje unaendana na maisha yako halisi, ujue wanaume wengi wana kawaida ya ‘ku-fake’ maisha, ukimuona nje anajifanya kupendeza kwelikweli, lakini mahali anapoishi ni vituko,” alisema huku akicheka, moyoni nikaanza kujisikia vizuri.
Mara alisimama, nikapata nafasi ya kulitazama vizuri umbo lake! Saima alikuwa amejaliwa kila kitu, yaani hata sijui nielezee vipi uzuri wake. Upande wa nyuma alikuwa ametanuka sana chini ya kiuno na kukaribia kufanana na namba nane, basi akawa anazunguka huku na kule mle ndani, akiwa anathaminisha kila kitu kilichokuwemo.
“Huku ndiyo chumbani kwako?” alisema huku akiwa anaelekea kule chumbani, basi ikabidi nisimame na kumfuata ili nimuoneshe na kule ndani kulivyokuwa, kama mwenyewe alivyokuwa anataka, kweli nikamfungulia mlango, akaingia chumbani huku akiendelea kuangaza macho huku na kule, tabasamu pana likiwa limechanua kwenye uso wake.
Katika sekta ya kujikamilisha pale ndani, nilikuwa najiamini kwa sababu ni kweli ndani kwangu kulikuwa kuzuri kwelikweli, kukiwa na vitu vingi vya thamani ambavyo ni vigumu sana kwa mtu wa umri wangu kuwa navyo, pengine hata wengine walioanza maisha muda mrefu na wanaonizidi umri, hawakuwa na ubavu wa kuishi maisha kama yale.
“Hapa ndipo unapolala,” alisema huku akijirusha kwenye kitanda kikubwa na cha kisasa kilichokuwa kimechukua sehemu kubwa ya chumba cha kulala, basi wote tukawa tunacheka huku akiendelea kunisifia.
Pale alipojirusha, sketi fupi aliyokuwa amevaa, ilipanda juu kidogo na kunifanya niyaone mapaja yake mazuri, yenye weupe wa kung’aa, mapigo ya moyo yakawa yanazidi kunienda mbio huku moyoni nikijisemea ‘kweli leo nimepatikana’.
Basi nilikaa pembeni yake, tukawa tunatazamana huku bado akiwa ameachia tabasamu pana kwenye uso wake, lililomfanya azidi kuonekana mrembo.
“Pole kwa matatizo yaliyokupata,” nilisema, akashusha pumzi ndefu na kuinuka, tukawa tumekaa kitako, akaanza upya kunisimulia kila kilichotokea huku akiwa ananitazama sana machoni.
“Sijui alinigundua jana tulipotazamana naye kule benki?” nilijiuliza mwenyewe moyoni huku mara kwa mara nikiwa nakwepesha macho yangu, basi aliendelea kunielezea kila kitu, akanionesha mchubuko mdogo aliokuwa ameupata kwenye mguu wake wa kushoto.
“Hapa nilichubuka baada ya kuanguka niliposikia risasi zikipigwa huku watu wote tukiamrishwa kulala chini,” aliniambia, moyoni nikawa nazidi kupata hofu kwa sababu hata huyo mtu aliyeanza kufyatua risasi na kuamrisha watu wote walale chini, nilikuwa ni mimi.
Kuna wakati nilihisi huenda ananieleza hivyo ili kunitega ili aujue ukweli, lakini na mimi nikawa mjanja sana wa kujifanya kila alichokuwa ananisimulia ni kigeni kabisa.
“Vipi kuhusu kidani chako?” nilimuuliza kwa mtego nikitaka pia kujua ni nini alichokuwa anakihisi moyoni mwake, basi akaanza kunielezea jinsi kidani hicho kilivyotaka kumuingiza matatizoni.
“Kwa bahati nzuri baba’angu mkubwa yupo kwenye ofisi ya mpelelezi mkuu, yeye ndiye aliyesaidia sana kulimaliza soo, vinginevyo na mimi ningekuwa ndani sasa hivi,” alisema huku uso wake ukibadilika.
“Nikuulize kitu James?”
“Niulize tu Saima.”
“Unajua mimi bado sijaelewa mazingira yaliyosababisha kidani changu kiokotwe pale nje, au labda kuna mtu ulimuazima?”
“Hapa...na! Hapana Saima, siwezi kumuazima mtu kitu cha thamani ulichonipa, yaani hata mimi sielewi. Nahisi labda pengine nilikiangusha pale nje ile siku uliponipa.”
Je, nini kitafuatia?
 
SEHEMU YA 50






ILIPOISHIA:
“Unajua mimi bado sijaelewa mazingira yaliyosababisha kidani changu kiokotwe pale nje, au labda kuna mtu ulimuazima?”
“Hapa...na! Hapana Saima, siwezi kumuazima mtu kitu cha thamani ulichonipa, yaani hata mimi sielewi. Nahisi labda pengine nilikiangusha pale nje ile siku uliponipa.”
SASA ENDELEA...
“Hilo mimi nakataa kwa sababu kisingeweza kukaa pale siku nzima. Mimi nahisi labda yule dereva wa Bajaj aliyekuleta hapa anaweza kuwa anajua kinachoendelea na ndiyo maana hata baba mkubwa nilimueleza hicho kitu. Inawezekana ulikiangusha kwenye Bajaj, yeye akakiokota na kukivaa au kumpa mtu ambaye anaweza kuwa ndiyo miongoni mwa wale majambazi waliokuja kutuvamia,” alisema huku akinitazama, basi na mimi nikamuungia hapohapo.
“Dah, kweli inawezekana! Unajua hawa madereva wa Bajaj na bodaboda ndiyo haohao usiku wanakuwa majambazi, hicho ulichokisema kinawezekana kabisa.”
“Ni kweli, wote wamekamatwa kwa sababu hata wakati tukio linatokea, huwezi kuamini wote hawakuwepo, lazima watakuwa walikuwa wanajua kinachoendelea,” alisema, angalau sasa nikawa na uhakika kwamba hakuna tena kitu kinachoweza kuniunganisha moja kwa moja na tukio hilo kwa sababu hata yule dereva Bajaj aliishia kituoni na sikumpa nafasi hata ya kuona nimeelekea wapi.
“Cha kumshukuru Mungu ni kwamba uko salama mpenzi wangu, hayo mengine tuviachie vyimbo vya ulinzi vitakuja na majibu,” nilimwambia, akashusha pumzi ndefu na kunisogelea, akanikumbatia kwa nguvu.
“Nilikuwa najua naenda kufa bila kupata nafasi ya kuonana na wewe James,” alisema, safari hii machozi yakiwa yanambubujika, basi na mimi nikawa nambembeleza huku nikimfuta machozi. Kingine nilichokibaini ni kwamba ngozi ya mwili wa Saima ilikuwa laini mno, mithili ya mtoto mchanga.
Basi niliendelea kumbembeleza pale, na yeye akawa anazidi kunidekea. Kitendo cha kuendelea kubembelezana vile, kiliamsha hisia kali za kimapenzi kwenye moyo wangu, nikawa najiona kama nipo kwenye ulimwengu mwingine kabisa.
Baadaye alitulia, kwa kuwa tulikuwa tumekaa, alinisukuma kichokozi, basi nikalala, na yeye akanisogelea na kujilaza pembeni yangu na kunikumbatia, na mimi nikapitisha mikono yangu na kumkumbatia.
“Sijafunga mlango wa nje, ngoja nakuja,” nilisema huku nikiinuka, basi nikatoka mpaka sebuleni. Nikaenda kuufunga mlango wa mbao kwa funguo kisha nikafungua friji na kutoa redbull na boksi la juisi, nikachukua na glasi mbili na kuelekea chumbani.
Ilikuwa ninywe redbull kwa sababu Bonta alinifundisha kwamba ina uwezo wa kuufanya mwili ukawa na nguvu hata pale unapohisi uchovu. Shughuli tuliyoifanya na Kezia kule kambini ilikuwa imenichosha, ukichanganya na uchovu wa usiku kucha, nikaamua kujihami nisije nikaumbuka bure.
Nilipoingia chumbani, nilishtuka baada ya kumuona Saima akiwa amesimama, huku akimalizia kutoa nguo zake za juu na kumfanya abakie na za ndani tu, ambazo sasa zilinifanya niweze kuliona vizuri umbo lake, nikajikuta nikimeza funda la mate kama fisi aliyeona mfupa.
Sikutaka kubaki nyuma, na mimi nilitoa fulana niliyokuwa nimeivaa juu, akanitazama kwa mshangaona kunisogelea, huku mikono yake ikiwa inapita taratibu juu ya kifua changu.
“Kumbe una kifua kikubwa hivi, huwa unafanya mazoezi mazito eeh!” aliniuliza kwa sauti iliyokuwa inasikika kutokea puani, nikatabasamu kwa sababu ukweli ni kwamba mazoezi magumuya kule kambini, yaliufanya mwili wangu ujenge vizuri kwelikweli, basi Saima akazidi kuchanganyikiwa na muda mfupi baadaye, tuligusanisha ndimi zetu.
Kiukweli msisimko niliopata ulikuwa mkubwa mno kiasi kwamba nilihisi kama naelea kwenye ulimwengu mwingine wa tofauti kabisa. Kwa upande wa Saima, naye alionesha kuwa kwenye hisia za juu kwelikweli na haukupita muda mrefu, tayari tulikuwa uwanjani.
Tofauti kabisa na Kezia, Saima alionekana kuwa mgeni kabisa wa mambo ya kikubwa, kila kitu kilikuwa kigeni kwake na japokuwa mwenyewe hakuniambia chochote, niligundua kwamba mimi ndiyo mwanaume wake wa kwanza! Kwa watu wazima watakuwa wanaelewa nini huwa kinatokea unapokutana na mwanamke ambaye hakuwa akimjua mwanaume kabla.
Ilifika mahali Saima akashindwa kabisa kuendelea, basi tukakubaliana kulimaliza pambano lile la kirafiki huku akiniomba sana radhi na kunitaka eti nimsamehe kwa kuwa ameshindwa kunipa kile nilichokitarajia lakini akanisisitiza sana kwamba nisije nikamuumiza moyo wake kwa sababu yeye ni mgeni kabisa kwenye mambo hayo ila mapenzi yake ya dhati ndiyo yalimfanya mpaka akafikia hatua ya kukubali kirahisi kulala na mimi.
Ilibidi nifanye kazi kubwa kumtuliza kwa sababu baada ya hapo, alikuwa akilia tu. Kila alichokuwa akikizungumza alikuwa analia, wakati mwingine mpaka eti akawa anajishangaa kwamba kwa nini ameshawishika na kuutoa usichana wake kwangu wakati hana uhakika kama kweli nina mapenzi ya dhati kwake.
Nilimtoa wasiwasi na kumhakikishia kwamba yupo kwenye mikono salama na lengo langu siyo kumchezea bali nataka kumuoa awe mke wangu wa ndoa, maneno ambayo yaliukosha sana moyo wake. Nilitumia muda mrefu sana kumtuliza na ikafika mahali, kweli akawa ametulia.
Ilibidi nifanye kazi ya kubadilisha mashuka pale kitandani kutokana na kilichotokea. Kiukweli nilifurahi sana ndani ya moyo wangu na nikawa najiuliza maswali mengi ndani ya kichwa changu, iweje msichana mrembo kama Saima, mwenye kila kitu kinachoweza kumfanya mwanaume yeyote aliyekamilika atamani kuwa naye, mpaka umri huo awe mgeni kabisa kwenye mambo hayo ya kikubwa?
Moyoni nilijiona kuwa na bahati kubwa sana, ni kama nilikuwa nimeokota dodo chini ya mwarobaini, nikawa nachekacheka tu mwenyewe huku moyo wangu ukiwa na furaha isiyoelezeka. Basi siku hiyo ilikuwa ya kipekee sana kwenye maisha yangu na kutoka ndani kabisa ya moyo wangu nikajiapiza kwamba ni lazima nije kumuoa.
Tulishinda pamoja siku hiyo, tukazidi kufahamiana naye huku akinisimulia mambo mengi kuhusu familia yao. Kwa maelezo yake, ilionesha kwamba alikuwa akitokea kwenye familia iliyokuwa inajiweza sana kiuchumi, huku yeye akiwa ndiyo mtoto wa kwanza, akiwa na wadogo zake wawili ambao bado walikuwa wakisoma.
Kila alipokuwa akijaribu kunichimba kutaka kujua historia yangu kwa undani, nilikuwa nikimhamisha kwenye topiki mpaka ikafika mahali mwenyewe akaacha, tukawa tunapiga stori za kawaida.
Kingine kilichonishangaza, licha ya usistaduu wote aliokuwa nao, eti alikuwa anataka nisiende kununua chakula badala yake nikanunue mahitaji yote halafu yeye atakuja kupika, hata hivyo changamoto ikawa ni vifaa vya kupikia, sikuwa na kijiko wala sufuria.
Kwa shingo upande akakubali nikanunue chakula, tukaja kula pamoja na kuhamia sebuleni ambapo tulikuwa tukitazama runinga, huku yeye akionesha kuwa mpenzi sana wa tamthiliya za Kizungu pamoja na muziki, basi akawa ananifafanulia tamthiliya mbalimbali kwa kunitajia wahusika na jinsi stori zilivyokuwa.
Muda ulizidi kuyoyoma, giza likaingia, nikawa natarajia kwamba ataniaga na kuondoka ingawa moyoni nilikuwa nataka aendelee kukaa na mimi, mwisho akaniambia kwamba anataka tulale wote.
“Vipi kuhusu wazazi wako?”
“Nimemtumia baba meseji na kumwambia kwamba kuna pati ya rafiki yangu kwa hiyo nitalala hukohuko, kwa jinsi anavyoniamini ameniruhusu,” aliniambia, nikaishia kucheka kwa furaha kwa sababu kiukweli sikuwa nataka aondoke.
Basi tulilala pamoja siku hiyo na usiku tulijaribu tena kwa mara nyingine kushiriki kwenye sanaa ya kikubwa, na taratibu akaanza kuonekana kwenda sawa na mimi.
Ulikuwa ni usiku wa kipekee sana na japokuwa yeye aliwahi kupitiwa na usingizi, mimi nilichelewa sana huku nikiwa najiuliza maswali mengi ndani ya kichwa changu kama kweli kuna haja ya mimi kuendelea na ile kazi hatari ambayo naweza kupigwa risasi muda wowote na kuuawa au kuishia gerezani, nilibaki njia panda.
Keshoyake asubuhi, Saima aliwahi kuamka na jambo la kwanza alianza kufanya usafi nyumba nzima, muda huo mimi nilikuwa bado nimelala. Nilipoamka, nilikuta nyumba ikiwa safi kwelikweli, alisafisha kila kona ya nyumba isipokuwa pale kitandani nilipokuwa nimelala.
“Wewe unakunywa pombe James,” aliniuliza huku akinitazama kwa uso wenye bashasha nyingi baada ya kuwa nimeamka, nikamueleza ukweli kwamba nakunywa ingawa siyo sana.
“Mimi sipendi unywe pombe bwana, hata kama unakunywa basi iwe ni kiasi tu, yaani friji lote limejaa chupa za mipombe? Friji linatakiwa kuwa na maziwa, maji, matunda na vitu vingine lakini siyo pombe,” aliniambia kwa upole huku mkono wake mmoja ukikichezeachezea kidevu changu ambacho ndiyo kwanza ‘vindevu’ vilikuwa vimeanza kuchomoza.
Basi nikaamka na kwenda bafuni ambako alikuwa ameshaniandalia kila kitu, nikaoga na kurudi chumbani, nikamkuta ameshajiandaa, nikashangaa anataka kwenda wapi tena wakati siku hiyo haikuwa siku ya kazi?
“Mimi maisha ya kula vyakula vya kununua siwezi, ngoja nikafanye shopping ndogo ya vitu muhimu vya kupikia,” aliniambia, nikaishia kutabasamu mwenyewe. Nikataka kutoa fedha za kumsaidia kwenye manunuzi yake lakini alikataa, akatoa kadi ya benki kwenye pochi yake na kuniambia kwamba atasimamia shoo yeye mwenyewe.
Kiukweli nilizidi kumshangaa, basi nikamruhusu huku nikimtaka awe makini, akanibusu na kutoka, nikaenda kufunga milango vizuri na kurudi chumbani, nikajilaza kitandani huku bado kichwa changu kikiwa na mtihani mkubwa sana wa maamuzi ya kuchukua kwa sababu sasa nilikuwa nimeshaanza kuiona thamani ya maisha yangu na sikutaka tena kujihatarisha kwa namna yoyote.
“Nitatafuta sababu yoyote ya kuacha kazi, sitaki kuendelea kushika bunduki,” nilijisemea huku nikijigeuzageuza pale kitandani. Muda mfupi tu niliokaa na Saima ulikuwa umenibadilisha kila kitu.
Je, nini kitafuatia? Subiri kitabu!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom