Willy Gamba 1
JF-Expert Member
- Jan 5, 2015
- 352
- 377
- Thread starter
- #21
CHAPISHO LA 12
Siku mbili baadae
JOSEPH Rutashobya alisimama juu ya kilima
kidogo, akatazama eneo lote lililokuwa na kijiji
walichokiishi zamani, mahame, hakukuwa na
nyumba hata moja, hakukuwa na binadamu
aliyeishi, migomba na mibuni vilifanya machaka
ya kutisha. Joru akainama kichwa kwa muda na
kuwaomboleza wapendwa marehemu wote
waliouawa siku hiyo, aliwaombea na wale wote
walijaribu kukipigania kijiji chao. Akamtazama
Kemi aliyekuwa kajifunga lubega, wakaanza
kutelemka kilima kuelekea bondeni. Mkononi
akiwa na upanga na jembe dogo, Kemi alikuwa
na akimfuata kwa nyuma wakati Joru
akikatakata vichaka na kufanya njia.
Haikuchukua muda walikuwa chini kabisa,
kwenye tambarare ya vichaka. Joru alitazama
eneo lile, akakumbuka vipindi vingi sana vya
utoto wake, akamtazama Kemilembe, aktazama
tena eneo lile walilokuwa wakiishi.
Joseeeeee, twende tukacheze !!!!
Aliihisi sauti ya kitoto ya Kemi ikipita masikioni
mwake miaka zaidi ya ishirini iliyopita, hisia kali
zikauteka moyo wake, kumbukumbu ya matukio
mengi ya maisha ikajaa kichwani mwake,
aliwaona mtu mmoja mmoja aliyemkumbuka,
rafiki zake, wazazi wake na memngine mengi.
Machozi ya uchungu yakamtiririka,
akamkumbatia Kemi kwa uchungu.
Kemi, kijiji kilichotulea, kijiji kilichotukutanisha
duniani, kijiji kilichotujengea mapenzi yetu, kijiji
tulichokipenda sana, leo hii si kijiji tena,
mahame na ukiwa Joru alimwambia Kemi.
Kemi akaegama kifuani mwa Joru.
Wewe ni mali ya Mungu na mimi ni Mali ya
Mungu
Sauti iliyofuatiwa na mwangwi, sauti mbaya
iliyomchukiza Joru, na kutia hasira mpya katika
moyo wake, donge lilimshika, Joru alianza
kutetemeka na kupumua kwa nguvu. Kemi
aliyaona mabadiliko hayo ya Joru, akamtazama
kwa woga kijana huyo aliyekuwa na mwili
unaotisha pindi awapo hasirani.
Nini Joru? Kemi aliuliza.
Lazima nilipe kisasi, lazima nimuue kwa mkono
wangu, damu ya Rutashobya na Watanzania
haiwezi kupotea hivi hivi, Joru alimjibu Kemi,
kisha akasogea taratibu kwenye eneo ambalo
alihisi kabisa ndipo alipouawa baba na mama
yake
Aaaaaaaaiiiigghhh!!!!.........
Sauti ya mama wa Joru ilirudi kwa kishindo
moyoni mwa Joru, akashtuka, moyo ukawa
unamwenda mbio, akasimama na kutazama
chini taratibu, akaondoa mguu wake uliokuwa
umevikwa buti la kijeshi, buti la Muamerika,
akaona kitu kinachongaa kwa jua lile la saa
nane mchana, akainama na kufukua udongo ule
kidogo tu, kidani, akakivuta, kikajifukua kutoka
udongoni. Joru alikikumbuka kidani kile,
akakigeuzageauza, kidani cha mama yake.
Alikisafisha kwa nguo yake, kilikuwa na kutu
lakini hazikuwa za kutisha, Joru akamtazama
Kemi, akaitazama shingo ile ya upanga, akampa
ishara ya kuwa asogee, naye akafanya hivyo
aliposogea akamvisha kidani kile shingoni
mwake.
Sasa wewe ndiye mama Rutashobya! Joru
akamwambia, kisha wakaendelea kuelekea eneo
husika.
Asante Joru, Kemi alijibu huku akiendelea
kumfuata nyuma Joru mpaka walipofika eneo
walilohisi ni lenyewe ambalo lilikuwa na choo.
Kemi akavuta hatua chahe, akasimama mbele
kidogo ya Joru, palikuwa na udongo uliodidimia
kiasi na nyasi kavu zilizokuwa eneo hilo.
Akasimama na kutazama mbele, akauona mti
ambao alijificha akimtazama mzee Rutashobya
alipokuwa akifukia mfuko ule, kisha akarudisha
macho yak echini tena na kuonesha kidole.
Joru, ni hapa bila shaka, siku ile mimi nilijificha
pale kwenye ule mti na ndoo yangu kichwani,
Kemi akamwambia Joru. Macho ya joru
yalimtazama Kemi kwa upendo mkubwa.
Wewe ni mtu wa pekee sana kwangu, Joru
akasema, kisha akainua kijembe chake na
kuchimba taratibu. Joru alichimba huku Kemi
akiwa pembeni kuangalia kinachotokea.
Haikuchukua muda, Joru aliunasa mfuko wa
plastiki, akatupa kijembe pembeni, akaushika ule
mfuko mchafu na kuuvuta taratibu kuja nje.
Kesho na keshokutwa utakua kijana mwanangu,
hakikisha unalipa kisasi kwa damu hii
inayomwagika, damu ya familia yako, damu ya
wazazi wako,
Sauti ya baba wa Joru ilimrudia mwanawe
alipokuwa akivuta mfuko ule, wakati mfuko ule
ukichomoka taratibu ardhini, Joru aliukumbuka,
aliukumbuka bila shaka.
Jose, usiutupe mfuko huo una kazi kubwa
baadae,
Maneno hayo yalipata maana siku hiyo kwa
Joru, mawazo yalikuwa lukuki, hakuna
aliyeongea wala kumuuliza mwenzake, kila
mmoja alitaka kuona tu nini kilikuwa kwenye
mfuko huo.
Joru, kuna sumu humo ndani Kemi
alimwambia Joru.
Hakuna sumu, baba alikuwa anakutisha tu,
hakutaka uje uchezee, ngoja uone, joru akajibu
na kumalizia kuuvuta ule mfuko nje kabisa ya
shimo lile, ulikuwa umefungwa vizuri,
umefungwa kifundo. Joru akaupapasa, sasa
alikuwa mtu mzima alielewa nini kilikuwa katika
mfuko huo, akaufungua na kukitoa, bastola ya
kizamani na risasi nne. Tabasamu pana
likaupamba uso wa Joru. Akaigeuzageuza
bastola ile, ilikuwa ya kizamanai kwelikweli, na
risasi zake nne ambazo hazikuwamo katika
magazine, ila pembeni katika kikasha cha
chuma. Kemi alishangaa sana aliijua bastola
kwa kuwa aliwahi kuiona katika senema za
kizungu, na aliiona kwa askari wakati alipokuwa
gerezani.
Joru akaitazama ile bastola iliyokula kutu za
kutosha, hakika ilikuwa ya kizamani. Alipokuwa
mtoto alikiona kitu hiki mara kadhaa ndani kwao
lakini hakuwahi kujua kazi au matumizi yake,
lakini sasa anajua hata kwamba ilitumika katika
vita kuu ya pili ya dunia ambayo kwa simulizi,
baba yake mzee Rutashobya alishiriki, baba
ambaye hata yeye alizoea kumwita babu.
Akachomoa risasi zile nne ailizokuwa ndani ya
kibweta kile cha chuma, ni nne tu na si zaidi,
alizitazama kwa makini, hakujua lengo la baba
yeke kuzifukia, labda hakutaka mtu azione au
hakutaka watu wabaya kama Malyamungu
kuzipata kwa maana wangetumia kwa matumizi
mabaya vilevile.
Kemi, turudi, hakuna la zaidi, Joru
akamwambia Kemi kisha wakageuza na kurudi
walikotoka wakiwa wameshikana mikono.
Joru alifika nyumbani, kazi ya kwanza aliyoanza
nayo ni kuisafisha ile bastola kwa kutumia
mafuta maalumu ili iweze kufanya kazi upya.
Alikuwa kaka peke yake nyumba ya nyumba
wakati Kemi akiendelea na kazi nyingine kwa
mama Shibagenda ikiwamo kumlea Joru mtoto.
Masaa matatu, yaliirudisha ile bastola katika
uhai mpya, ilikuwa ikingaa, ikingaa mpaka
inaumiza macho. Mtutu wake wa chuma
kingavu ulirudi katika uhai, kitako chake cha
mbao ya mpingo kilingazwa kwa mafuta, kila
kitu kilirudi kati uhai. Joru aliziweka sawa
risasui na akahakikisha kuwa zipo sawa kwa
kazi zitakayotumwa, akavuta kikasha kingine
ambacho risasi zake zinaingiliana na ile bastola,
akajaribu kuipachika katika magazine ikakaa
sawa akapachika nay a pili nayo ikawa sawa,
akaichukua ile magazine na kupichika mahala
pake, akajaribu hiki na kile. Joru aliziheshimu
zile risasi nne, hakutaka kuziharibu kwani alijua
sasa kuwa zina kazi maalumu, kazi ngumu ya
kisasi. Akaishika bastola, akafanya kama
analenga, akabana jicho moja, bahati nzuri
kulikuwa na mwewe aliyekuwa anapita,
akaondoa usalama na kufyatua bastola hiyo.
Kwa mara ya kwanzaq alipata ladha ya mlio wa
bastola ya kale, Yule mwewe alijilaumu kwa nini
alipita eneo hilo, kwani ni manyoya tu
yaliyoonekana angani, alipotua chini
hakujulikana ndani ni wapi na nje ni wapi. Joru
akatikisa kichwa kuonesha haamini
kinachotokea.
Asante Rutashobya, risasi hizi nne zitaishia
kichwani mwa Mali ya Mungu kama amekufa
basi nitazifyatua juu ya kaburi lake, Joru
alijiseme kwa sauti ya utulivu, akachukua zile
risasi nne na kuzisweka katika kibweta chake
kama kwanza, akakiweka katika mkoba wake
mdogo wa kijeshi kisha akaiweka ile bastola na
kunyanyuka kutoka pale alipoketi kwa muda
mrefu. Alipogeuka akakutana uso kwa uso na
mama Shibangeda.
Vipi Joru mbona watushtua? Mama
Shibagenda akauliza.
Pole na samahani mama, nilikuwa nafanyia
mazoezi kifaa change maalumu, maana
natakiwa kwenda Uganda siku nne zijazo, Joru
akajibu.
Kikazi au binafsi? mamaShibagenda akauliza.
Kikazi mama, na ni kazi ya hatari sana kuliko
unavyofikiria, Joru akajibu kwa kirefu.
Kazi gani mwanangu? mama Shibagenda
akazidi kuhoji.
Mama, wakati wa vita vya Uganda. Jeshi la
Tanzania lilifanya kazi kubwa sana ya
kumfurusha nduli Idd Amin, lakini kuna kitu
walikuwa hawajamaliza, nimetumwa kwenda
kumaliza hicho kimoja, ila ni hatari, kuna mawili,
kurudi au kuzikiwa huko huko, Joru alimwambia
mama Shibagenda.
Joru! Mama Shibagenda aliita kwa mshangao,
akajishika kiuno na kumtazama mwanajeshi
huyo kijana.
Mbona unashtuka mama? Joru akauliza na
kusimama kutoka pale alipokuwa.
Mimi hiyo kazi yenu inaniuzi, yaani baba yako
angejua unataka kwenda huko angeshakukataza,
bora ulienda kwa kutoroka, ila we Joru ni dume
huogopi, Mama Shibagenda akamwambia Joru.
Kisha wote wawili wakafuatana kurudi upande
wa pili wa nyuma, mwendo wa hatua ishirini,
mama Shibagenda akasimama na kumzuia Joru.
Enhe, nambie, kuhusu Kemi, nimependa sana
stori yenu, sasa unaoa au unaenda kumtafuta
Yule uliyezaa naye? Mama shibagenda
akauliza.
Mama, mimi sijazaa na mtu, Yule kazaa
mwenyewe, kwanza kaniuzi sana, mwanamke
gani mwenye roho mbaya ya kuniletea mtoto na
lkisha yeye kuondoka, je kama asingeniona, si
angeweza hata kumtumbukiza chooni?
Wanawake wa mtindo huu hawafai katika jamii,
wajirekebishe. Lakini nakushukuru mama kwa
kunilelea mtoto, na Mungu alikuongoza
ukampata mpenzi wangu kipenzi, Kemilembe,
huyo ndiye mama wa Joru, nampenda sana
Kemi, Joru aliongea kwa hisia na masikitiko.
Joru akamuona mwanawe akicheza kibarazani
pamoja na mtoto wa Shibagenda.
Kuna watu wamezaliwa na wema wa ajabu na
upendo wa kupindukia, nah ii ni familia ya
Shibagenda, asanteni sana kwa ukarimu wenu
mmenilea, mkatulea mpaka sasa, muendelee
kutulea mpaka tutakaposimama kwa miguu yetu
wenyewe, nitamuoa Kemi pindi nikitoka kwenye
Operesheni Mali ya Mungu huko Uganda, Joru
akamwambia mama Shibagenda na kumnyanyua
mwanawe.
Yalivyofanana basi!!! Kemi akazungumza
kutokea mlangoni alikokuwa amejificha.
Joseph Rutashobya aliitazama kalenda ya
ukutani kwenye ukuta wa nyumba ya
Shibagenda, akahesabu siku zilizobaki kwa
mapumziko yake, hazikuwa haba, zilikuwa saba,
akatikisa kichwa, akaamua moyoni kesho
naanza oparesheni yangu, naipa siku tatu iwe
imekamilika, akajisemea.
.Hakikisha unatimiza hilo kama ulivyosema !
Alihisi sauti kama ya baba yake ikimwambia.
Nitatimiza, aliijibu.
Siku hiyo usiku Joru hakulala vizuri,
alisumbuliwa na ndoto za kutisha, ndoto za
kuogofya na kumkatisha tama, mara kwa mara
alishtuka na kuketi kitandani. Kemi naye alimka
mara zote hizo na kumtuliza Joru, kumfariji
katika mahangaiko yake. Ilipofika saa tisa usiku
Joru akachuku begi lake la kawaida tu sio la
kijeshi, akapanga baadhi ya vitu vyake muhimu.
Aliitazama sana bastola ile aliyoichimba porini,
sasa ikingaa kana kwamba ni mpya lakini
utaijua kwa umbo lake kuwa ni ya kizamanai
sana, Smith and Wesson, hakuwa na uhakika
kwa hilo.
Kemi nakwenda Uganda kufanya kazi
aliyonituma mzee Rutashobya, usimwambie mtu,
lakini nitarudi baada ya siku tatu, Joru
akamwambia Kemi aliyekua amejivuta jirani
naye kabisa.
Joru mpenzi, naamini kabisa utarudi na
utafanikisha kazi yako, sina kinyongo na safari
yako, lakini utuletee zawadi wenzako,Kemi
alimwambia Joru.
Usijali, baba akitoka safari ni vizuri kuleta
zawadi, name nitawaletea zawadi, zawadi ya
ushindi, Joru akamwambia Kemi.
Baba usiende hivi hivi, japo tupeane Baraka
maana nitakukosa kwa muda wa siku kadhaa,
Kemi alisema huku akisimama na kukiacha
kitenge chake kikiuacha mwili nay eye kubaki
kama alivyo, akamfuata Joru pale aliposimama
alipokuwa akiweka vizuri mambo yake,
akamfungua taulo naye akabaki vilevile, wawili
hao wakaingia upya mapenzini, kitanda kikubwa
kikawapokea na blanketi pana likawasitiri.
JOSEPH RUTASHOBYA ANAKUTA BASTOLA YA
KALE IULIYOFICHWA NA MZEE WAKE, SIRI HIYO
ALIIJUA KEMI PEKEE....
RISASI NNE ZINAAMBATANA NA BASTOLA HIYO,
SASA JORU ANAPANGA SAFARI YA KWENDA
UGANDA....
NINI KITAJIRI UGANDA? USIKOSE CHAPISHO LA
13