Riwaya: 'Njama'

burdani sio utuache solemba mambo ya kutiana nyege za hadithi hatutaki ila hongera mdau huo mkwala kuonyesha tuna hamu ya kujikumbusha khabar za vero mtoto wa freetown. kila siku muda gani?
 
burdani sio utuache solemba mambo ya kutiana nyege za hadithi hatutaki ila hongera mdau huo mkwala kuonyesha tuna hamu ya kujikumbusha khabar za vero mtoto wa freetown. kila siku muda gani?

Na akimaliza hii atuletee nyengine ya willy gamba
 
burdani sio utuache solemba mambo ya kutiana nyege za hadithi hatutaki ila hongera mdau huo mkwala kuonyesha tuna hamu ya kujikumbusha khabar za vero mtoto wa freetown. kila siku muda gani?

Usijali mkuu..utaipata hadi mwisho hapa hapa, Kila siku saa 3 asubuhi na saa 1 jioni.
 
Daaah,,, riwaya za Musiba,,,, Njama, kisasi, kufa na kupona, kikomo na Hujuma big up mzee Musiba pamoja na mhuhusika mkuu Willy Gamba Enzi hizo middle 80's nili enjoy sana,,,,,,
kitambo sana hizi burudani, tuombe uzima tutazipata hapa tena
 
NJAMA
VERONIKA NA SHERRIFF II
ILIKUWA saa tatu kamili niliposimama mbele ya
chumba namba 208 katika ghorofa ya pili ya hoteli
ya Kilimanjaro, niligonga mlango mara mbili haraka
haraka, halafu nikatulia kidogo kisha nikagonga
tena. Hivi ndivyo nilivyokuwa nimeelekezwa.
"Karibu", nilisikia sauti kali ya juu ikitokea ndani ya
nyufa za mlango. Nilifungua nikajikuta katika
sebule ya chumba hiki ambamo Veronika alikuwa
amevaa kaputula na sidiria tu akifanya mazoezi ya
viungo. Alikuwa ameelekea upande mwingine na
kunionesha mgongo na kuendelea na mazoezi yake
kama kwamba hakuna mtu aliyeingia. Nilirudisha
mlango, nikauegemea na kutazama jinsi binti huyu
alivyokuwa akichukua mazoezi.
"Karibu Willy Gamba, kaa kwenye kiti upumzike",
alinielekeza bila kugeuka na huku akiendelea na
mazoezi yake. Kisha akaanza kusema kana
kwamba anajizungumzia yeye peke yake.
"Willy Gamba anayejiita mfanyabiashara huku ni
mpelelezi mashuhuri wa Afrika. Afadhali ningejua
mapema naamini ingekuwa furaha kubwa kuonana
na mtu huyu mashuhuri nyumbani kwetu. Lakini
nimekuja kujua mjini London katika ofisi za gazeti
la 'Afrika', hasa ni hii teknolojia iliyoingia
ulimwenguni maana tumeelekezwa na komputa ya
pale ofisini. Sherriff aikuwa na mashaka kuwa
amewahi kusikia jina la Willy Gamba mahali. Hivyo
kufika tu London akailisha komputa hiyo jina la
Willy Gamba. Maana komputa hiyo imeweka
kwenye ubongo wake waandishi wote maarufu wa
habari, wapelelezi wote maarufu ulimwenguni,
wakubwa wote wa serikali mbali mbali na watu
wote maarufu katika nyanja mbali mbali.
"Lo! alipoilisha jina hili ndipo ikatutolea maajabu.
Ilionyesha kuwa Willy Gamba mwenye umri wa
miaka ishirini na tisa, mwenye urefu wa futi tano
na inchi kumi na mwenye umbo la kupendeza sana
ni mpelelezi maarufu ulimwengu mzima. Iliendelea
kusema kuwa Willy Gamba amehitimu katika chuo
kikuu cha Dar es Salaam na kupata shahada katika
sheria. Baada ya kutoka chuo kikuu moja kwa moja
aliteuliwa kwenda kujifunza mambo ya upelelezi
kwa kutokana na sifa zake alizoandikiwa na
wakubwa wa Jeshi la Kujenga Taifa, wakati akiwa
katika Jeshi hilo".
"Komputa ilieleza kuwa Willy Gamba anasemekana
amepata mafunzo katika nchi mbali mbali kama
vile Uingereza, Cuba, Urusi, Marekani, China na
Japan. Kutokana na mafunzo haya amejulikana
kama mtu hatari katika kutumia aina yoyote ya
silaha. Vile vile anajua karate na Kung-fu ya hali ya
juu kwani wakati akiwa Japan aliwahi kushindana
na Inoki na kutoka sare naye. Watu wanashangaa
kwanini hakuendelea maana bila shaka sasa
angekuwa bingwa wa dunia. Zaidi ya yote
anaaminika kuwa amehitimu mafunzo ya
kikomandoo. Komputa ilizidi kuonesha kuwa Willy
Gamba ana I.Q ya hali ya juu sana, hivi sasa ni
mtu anayeweza kusokoroa matatizo yaliyojisokota
sana. Na iliendelea kuonyesha kuwa ameifanyia
'OAU' kazi nzuri sana hasa kuhusiana na Ukombozi
wa Afrika Kusini".
Alipofika hapa alinyamaza, kisha kama umeme
alikatisha mazoezi yake na kunigeukia na kurukia
kifuani pangu kwani bado nilikuwa nimesimama
mlangoni nikisikiliza kwa makini.
"Kwanini usinieleze toka mwanzo Willy mpenzi,
kwanini?".
Nilimkumbatia kifuani kwangu na badaa ya kujibu
swali lake nilisema. "Veronika Amadu".
Aliinua macho akaniangalia usoni, mimi bila kusita
niliendelea. "Mwandishi maarufu wa gazeti la
"Afrika", Veronika Amadu mwenye umri wa miaka
ishirini na sita, mwenye urefu wa futi tano na inchi
tano, mwenye macho na umbo la kupendeza la
vipimo 38'-22'-36'. Alihitimu katika Chuo Kikuu cha
Ibadani nchini Nigeria na kupata shahada katika
uandishi, baada ya kuhitimu aiajiriwa na gazeti la
'Newsweek' la Marekani, akiwa mwandishi wao
katika Afrika Magharibi. Kwa vile gazeti lilitaka
kumtumia mwandishi huyu kupata habari zingine
ambazo kuzipata kwake itabidi uhatarishe maisha
yake, lililazimika kumpeleka Japan kujifunza namna
ya kujikinga kwa mikono, hatari yoyote itokeapo,
hivyo mwandishi huyu amehitimu katika Judo na
Karate na kupata mkanda mweusi. Baada ya kuwa
na gazeti hili kwa muda mrefu aliacha na kujiunga
na gazeti a Afrika. Anajuikana kuwa msichana
mwandishi jasiri sana, amewahi kusafiri na majeshi
ya Chama cha wapigania uhuru wa Sahara
Magharibi kiitwacho "The Popular Front for the
Liberation of Saguiet el-Hamara na Rio de Oro"
yaani "POLISARIO", katika mapambano yao dhidi ya
majeshi ya Morocco ambayo yameshika sehemu
hiyo, inasemekana mwandishi huyu alikaa na
majeshi haya na kuandamana nayo katika uwanja
wa mapambano kwa muda wa miezi sita na kuwa
mwandishi wa kwanza kuandika habari kamili za
mapambano haya akiwa shahidi wa macho. Je
unasemaje Veronika Amadu".
"Sasa naamini kabisa wewe ndiye Willy Gamba,
maana mimi nilifikiri tumekutangulia kumbe wewe
ndiye umetutangulia zaidi. Naamini hata Sherriff
sasa umamfahamu kama nyuma ya kiganja chako
hebu nieleze".
Nilimweleza. "Ahmed Sherriff mwandishi mashuhuri
wa gazeri la Afrika hasa juu ya mapambano ya
Kusini mwa Afrika. Ahmed Sherriff mwenye umri wa
miaka thelathini na mbili, mwenye urefu wa futi
tano na inchi kumi na moja na mwenye masharafa
mengi, alihitimu katika Chuo kikuu cha Patrick
Lumumba mjini Moscow, Urusi. Baada ya kuhitimu
kwake alipotea isijulikane aliko kwa muda wa
mwaka mmoja. Lakini habari za kuaminika
zinasema kwamba alikuwa akichukua mafunzo ya
kijeshi katika kambi za kijeshi za Wapalestina huko
Mashariki ya Kati. Baada ya kuonekana alipatiwa
kazi moja kwa moja na gazeti la Afrika ambalo
linaaminika lilipata fununu juu ya mafunzo ya
kijeshi ya Sherriff huko Mashariki ya Kati. Kwani
baada ya kumwajiri tu alipelekwa moja kwa moja
Kusini mwa Afrika ambako aliandamana na majeshi
ya wapigania uhuru wa Frelimo, MPLA na siku hizi
anaandamana na majeshi ya SWAPO katika uwanja
wa mapambano huko Namibia.
"Vile vile kuna habari zinazosema kuwa alikuwepo
katika mkasa uliotokea Soweto na ndiye
aliyeandika habari za kuaminika juu ya tukio hilo.
Hivyo ujasiri wake huu umemfanya kuwa
mwandishi maarufu sana anayechukiwa sana nan
tawala dhalimu za Afrika Kusini na Rhodesia na
nchi zote zinazopinga mapinduzi ya Afrika na
harakati zake za kujikomboa kutokana na ubeberu.
Umeridhika sasa."
"Sasa naamini ukiambiwa mtu ana I.Q ya hali ya
juu, lazima utambue kuwa kwa kila jambo
unalotaka kufanya yeye yuko hatua nyingi mbele
yako", Veronika alijibu na kuanza kunibusu huku
midomo yake ikiwa ya chumvi chumvi sababu ya
mazoezi.
"Ngoja nioge mara moja ili tukaonane na Sherriff
tukaanze mazungumzo yetu ya kwanza."
"Sawa". Aliniacha na kwenda maliwatoni. Mimi
nikabaki katika mawazo makali jinsi ya kuanza
kulishambulia tatizo hili.
INAENDELEA
 
NJAMA
SURA YA TATU
Niiegesha gari langu kwenye maegesho ya Hoteli
ya New Afrika. Nikatelemka na kuzunguka ili
nimfungulie Veronika. Tuliingia New Afrika Hoteli
katika sehemu iitwayo duka la Kahawa tukatafuta
meza tukaa.
"Ulishastafutahi?", nilimuuliza Veronika.
"Kawaida yangu huwa ninastafutahi kabla ya
kufanya mazoezi kila siku, ili kujiweka katika hali
nzuri".
"Ndio sababu umbo lako linapendeza namna hiyo".
"Asante".
Mtumishi wa hoteli alifika na kutuuliza mahitaji
yetu.
"Mimi nitakunywa maji ya machungwa kama
yapo".Veronika alisema.
"Mimi niletee maji ya ndimu". niliagiza.
Alipoondoka mtumishi huyo nilimweleza Veronika
kuwa mimi nitakwenda mapokezi kumwita Sherriff,
ambaye niliamini alikuwa bado chumbani.
"Habari za leo Tom?", nilimsalimia kijana wa
mapokezi ambaye tunafahamiana vizuri sana.
"Aha mzee, shikamoo", alinisalimia.
"Marahaba", nilimjibu.
"Sijui nikusaidie nini mzee?".
"Kuna mgeni wangu hapa anaitwa Ahmed Sherriff,
alifika usiku".
"Ndio ndio, yuko yuko namba 406, unahitaji
kwenda huko au nimpigie simu".
"Mpigie simu nizungumze nae".
Alimpigia simu na alipompata akanipa.
"Hallo Sherriff habari za leo?".
"Ohoo, Willy salama?, nilikuwa ninakusubiri kwa
hamu".
"Oke, telemka chini. Tuko hapa duka la kahawa
pamoja na Veronika".
Oh, amekwisha wahi namna hii?".
"Sana tena".
"Oke nakuja sasa hivi".
"Haya tunakusubiri", nilimjibu na kukata simu.
"Oke Tom asante sana", nilimwambia kijana wa
mapokezi.
"Asante mzee karibu", alijibu Tom.
"Asante niko hapa duka la kahawa".
Niliporudi nilikuta vinywaji tayari.
"Yupo?", aliuliza Veronika.
"Yupo, anakuja sasa hivi", nilimjibu.
Haukupita muda Sherriff alitokea na kuja moja kwa moja mezani kwetu. Tulisalimiana akavuta

kiti na kuketi. Mtumishi aliyekuwa anatuhudumia alipomuona alikuja mara moja.

"Mzee nikusaidie nini?," alimuuliza Sherriff.

"Kuna maji ya nanasi?".

"Ndio, yapo".

"Haya niletee hayo, lakini weka barafu nyingi, maana si joto hili".

"Bila ya wasiwasi mzee".

Mtumishi alipoondoka tulikaa kimya tunatazamana kwanza kila mtu anashindwa kuanza

mazungumzo. Veronika aipoona hivi akatabasamu kisha akasema. Sherriff wewe kidogo uko nyuma

ya habari, lakini nitakueleza kwa kifupi ili kukuweka pamoja nasi katika habari zinazotuhusu

wote".

"Nitakushukuru", alijibu Sherriff.

"Willy nimemweleza yote tunayojua juu yake, na jambo la kushangaza ni kwamba na yeye

anatufahamu sisi huenda kuliko tunavyojifahamu wenyewe".

"Usitie chumvi", nilimuasa.

"Ala!", Sherriff alitamka kwa mshangao mkubwa. "Kama ni hivyo basi ni vizuri sana. Kwani

wote sasa tunafahamiana misimamo yetu. Unajua mimi nilishangaa sana usiku pale uwanja wa

ndege. Waandishi wote wengine wa magazeti mbali mbali ulimwenguni tuliokuja nao wamekataliwa

kuingia hapa nchini, na tumewaacha uwanja wa ndege wakilalamika vibaya sana wakiomba kuonana

na mabalozi wao, lakini sisi tumeruhusiwa kwa urahisi sana, kitu hiki kilinishangaza sana

nikahisi lazima huu utakuwa mpango wa Willy. Sasa nimeamini kabisa. Uongo au kweli".

Sherriff aliuliza huku akiniangalia.

"Bila shaka niliwaahidi toka tukiwa Freetown kuwa mnakaribishwa kwa dhati Tanzania, sasa

nimetimiza ahadi yangu".

"Asante sasa", Sherriff alijibu.

"Mimi naamini unajua tumekuja kwa ajili gani, na vile vile naamini likizo yako imekatishwa

kwa ajili sababu hiyo hiyo tuliyoijia sisi", Veronika aieleza huku macho yake yaking'aa

kuonesha kuwa sasa tulikuwa tunazungumza kikazi.

"Sawa, endelea", nilimjibu.

"Mimi naonelea tungeliungana na wewe, kwani wewe ukiwa mwenyeji itakuwa kazi rahisi kwetu

kuweza kupata habari. Sijui wewe unaonaje?".

"Kwa taarifa yenu lazima niwaeleze kuwa tukio hili lililotokea si la kawaida. Mnaweza kuwa

mmeshiriki katika mambo ya hatari sana kama vile mambo ya vita, lakini lazima

niwatahadharishe kuwa kutafuta habari za aina yoyote zinazoweza kufichua kundi lililofanya

ujahiri wa hari ya juu ni hatari sana kwa maisha yenu kuliko hatari yoyote mliyokwisaha

kuikabiri. Nadhani mmenielewa. Ningewaomba ili kuponya maisha yenu muwe watoto wazuri,

muachane kabisa na kuuliza uliza habari za tukio hili".

"Kabla hatujatoka ofisini kwetu London, tumetahadharishwa kama unavyotutahadharisha sasa,

lakini tulikaa tukaamua kuwa tutaendelea; Lolote baya litakalotupata tutakuwa tumetoa damu

yetu kwa ajili ya ndugu zetu. Kwani sisi tunaamini watu waliofanya kitendo hiki si watu

wengine bali ni mabeberu wapinga ukomboni wa kusini mwa Afrika", alijibu Sherriff kwa nia

moja.

"Kama uamuzi wenu ni huo basi tutashirikiana kwa kadiri tutakavyoweza".

"Mlikuwa na nia ya kuanza kutafuta habari tokea lini?".

"Tokea sasa hivi kama unaweza kutupa fununu tuanzie wapi!", Sherriff alijibu.

Kwa vile katika mpango wangu wa upelelezi nilikuwa nimepanga kuwatumia ndugu hawa. niifurahi

sana kuona kuwa mambo yaikuwa yanakwenda kama nilivyopanga. Hivyo niliamua kuwaeleza kwa

kirefu maelezo aliyokuwa amenieleza Chifu.

"Ili kuwaweka sawasawa ninyi katika picha ya tukio hili mtakuwa wageni wa kampuni yangu. Kwa

hiyo mimi naona tangia sasa nitakuwa ni wakala wa gazeti lenu, kwa kufanya hivi nitapata

kisingizio cha kutembea na kupeleleza na nyinyi mkiwa kama wateja wangu; nafikiri

mmenielewa?".

Wote walitingisha vichwa kuonesha kuwa wamenielewa. Kutokana na mipango yangu ilivyokuwa

nilionelea tokea wakati huo tuanze kazi bila kupoteza muda.

Nilitoa onyo tena "Kukubali kwenu kushiriki na mimi katika upelelezi wa tukio hili mjue

kabisa mmejiwekea sahihi ya kifo. Natoa natoa muda wa mwisho kama kuna mtu anaona wasiwasi

katika moyo wake nampa nafasi aache shughuli hii", niliwaasa na kuwaangalia kwa makini sana.

Mwisho Veronika akasema

"Unajuwa Willy dakika ile mtu anapozaliwa pale pale anapewa huku ya kifo. Nina maana ya

kusema kuwa binadamu hata aishi vipi kufa lazima atakufa. Kule kuishi baada ya kuzaliwa ina

maana kuwa ile hukumu ya kifo inaahirishwa kutekelezwa. ..

ITAENDELEA
 
mkuu jitahid uifikishe hadi mwishp, mwaka juz kuna mtu aliileta hii simulizi ila ilipofika sehem ya 5 hakuendelea tena. vp unayo yote na una uhakika wa kuimaliza
 
NJAMA
HADITHI YA KUSISIMUA YA UPELELEZI
SURA YA TATU

"Unajuwa Willy dakika ile mtu anapozaliwa pale pale anapewa huku ya kifo. Nina maana ya kusema

kuwa binadamu hata aishi vipi kufa lazima atakufa. Kule kuishi baada ya kuzaliwa ina maana

kuwa ile hukumu ya kifo inaahirishwa kutekelezwa.Wengine huahirishwa kwa mwezi mmoja. Hivyo

mtoto anazaliwa na baada ya mwezi mmoja anakufa. Hii si ajabu maana hukumu yake ya kifo

imetekelezwa baada ya mwezi mmoja. Wengine huishi hata miaka mia moja. Hii ina maana kuwa

hukumu yake aliyopewa dakika alipozaliwa imetekelezwa baada ya miaka mia.Hivyo kila mtu na

sehemu yake ya kuishi. Kwa hiyo kuogopa kufa ni ujinga."

"Mimi sina wasiwasi, maana kifo cha namna hii, nitakuwa nimekufa kifo cha heshima", alisema

Sherriff.

"Okke, sasa naamini nina watu. Tokea sasa nyinyi si ndugu tena ila ni makomredi", niliwaeleza.

"Kwani komredi ina maana kubwa zaidi ya ndugu?", Veronika aliuliza.

"Hasa, ina maana kali zaidi. Komredi ina maana mwenzi katika harakati".

"Asante komredi Willy, naona tunywe maji haya katika jina la komredi", Veronika aliomba. Wote

tukagonganisha glasi zetu.

"Sasa mimi naonelea itabidi tuanze upelelezi wetu bandarini. Itabidi tukamuone ofisa

aliyehusina ili na sisi tupate habari toka kwake ana kwa ana ingawaje atakuwa amekwisha

sumbuliwa sana na polisi na maafisa usalama kwa maswali. Huenda sisi tukapata jambo ambalo

huenda wao wameliruka. Halafu tukaendelea hivyo hivyo katika ofisi zote zilizohusika kabla

hatujachukua hatua kali zaidi", mnaonaje.

"Sawa", walijibu kwa pamoja.

Tulinyanyuka na kuelekea kwenye gari langu, nikawafungulia milango. Veronika alikaa mbele na

mimi. Sherriff akakaa nyuma. Nilipotaka kuwasha gari moto niliona kijikaratasi chini,

nikakiokota taratibu nikakisoma. Eddy alikuwa ameniandikia namba zote za magari aliyokodi.

Akionesha namba za magari aliyoacha kwenye maegesho ya New Afrika na Kilimanjaro Hoteli kama

nilivyokuwa nimeamru. Nilianza kusikia msisimko wa damu ikionyesha kuwa kazi imeanza. Nilipiga

gari moto tukaelekea bandarini.

MIWSHO WA SURA YA TATU
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…