kidi kudi
JF-Expert Member
- May 17, 2011
- 2,510
- 2,163
riwaya: MUUAJI ALIYEBAKIA
Mtunzi: RAYMOND MWALONGO
Sehemu ya 1
Ilikuwa Ijumaa ya tarehe kumi mwezi
Desemba ambayo hali yake ya hewa ilikuwa
tulivu kabisa. Nyakati hizo za asubuhi
mambo hayakuwa shwari katika nyumba ya
mzee Kibudo ambayo watu kadhaa
walikuwapo nje wakilia kwa huzuni juu ya
kifo cha mzee huyo aliyeuawa na watu
ambao hawakujulikana. Watu hao wa kijiji
cha Magugu wilaya ya Babati mkoani
Manyara waliungana na familia ya mzee huyo
katika tatizo hilo la msiba. Maswali mengi
yalikuwapo vichwani mwa watu juu ya mtu
aliyefanya mauaji hayo kwa mzee huyo
aliyekuwa mkarimu licha ya utajiri wake
aliokuwa nao kijijini hapo. Jeshi la polisi
lilifanya uchunguzi juu ya kifo cha mzee huyo
na mwishoe familia yake ilihurusiwa kufanya
mazishi wakati wahusika wa tukio hilo
wakiendelea kupelelezwa.
Hatimaye mzee Kibudo ambaye ilielezwa
kuwa aliuawa kwa mapanga alizikwa, tukio
hilo lilishuhudiwa na mkewe na watoto wake
watatu pamoja na ndugu na jamaa waliofika
msibani hapo. Mara baada ya msiba huo
familia ya marehemu Kibondo ilikuwa ikisubiri
maelezo yeyote kuhusiana na wauaji wa
mzee huyo lakini hakuna taarifa zozote
zilizopatikana kutoka jeshi la polisi. James
Kibudo ambaye alikuwa mtoto wa mwisho
wa marehemu ndiye pekee alifanikiwa kupata
nafasi ya kusoma katika shule moja mkoani
Arusha. Kaka yake mkubwa alikuwa
akiwasaidia wazazi wake kazi za shamba na
uchungaji wa ngombe vitu vilivyomfanya
mzee Kibudo kuwa na uwezo kifedha kijijini
hapo.
Baada ya msiba huo James aliondoka
nyumbani kwao kurudi shuleni mara baada
ya kuagana na familia yake akiwamo dada
yake aliyetarajiwa kuolewa. Kichwani alikuwa
na mawazo juu ya mtu aliyehusika na mauaji
ya baba yake jambo lililomkosesha raha mara
kadhaa. Alitamani jeshi la polisi lifanikishe
kukamatwa kwa watu hao na sheria kali juu
yao ichukuliwe. Katika nyakati tofauti
aliwasiliana na familia yake kwa njia ya simu
akiulizia jitihada zilizofanywa na jeshi la
polisi lakini jibu lilibaki kuwa watuhumiwa wa
mauaji hayo hawakupatikana.
Mwezi mmoja baadaye James akiwa
amebakiwa na siku chache ili shule yao
ifunge kwa ajili ya likizo fupi, alishtushwa na
ujio wa mjomba yake shuleni kwao. Jambo
lililompa hofu ni hali ya wazi aliyoionyesha
iliyompa hisia za tatizo nyumbani kwao.
Mjomba yake huyo hakumweleza kitu zaidi ya
kumwambia kuwa ajiandae kwa ajili ya safari
kuelekea kwao, baada ya kubisha kwa muda
mfupi akitaka kujua sababu ya kufanya hivyo
alikubali na kujiandaa. Safari ilianza kuelekea
kwao, muda wote wa safari James alikuwa
na mawazo akiwa haelewi jambo lililokuwa
limetokea hali iliyopelekea aanze tena
kumuuliza mjomba yake huyo. Baada ya
kuona usumbufu ulizidi alimjibu kwa ufupi
kuwa kulikuwa na matatizo nyumbani kwao
hivyo uwepo wake ulihitajika.
Baada ya safari hiyo ya masaa kadhaa
walifika kijijini kwao Magugu, walianza
kutembea taratibu kuelekea nyumbani kwao
muda wote alikuwa na hofu akiwa haelewi
kilichokuwa kinaendelea. Hofu hiyo ilimzidi na
kujikuta akianza kulia baada ya kuona kundi
la watu wakiwa wamezunguka eneo la
nyumba yao na kelele za vilio
zikiendelea.Alijitahitidi kutembea lakini miguu
yake ilimwishia nguvu na hatimaye alianguka
chini kabla ya kusaidiwa na watu
waliokuwapo eneo hilo la msiba. Alipelekwa
mpaka ndani na kuwakuta ndugu zake
kadhaa waliomtaka atulie na kujipa ujasiri
kama mwanamme. Walianza kwa kumweleza
kuwa familia yake yote ilikuwa imeuawa
usiku wa siku hiyo. Jambo hilo lilimfanya
James kulia kwa uchungu baada ya kuelewa
yeye pekee ndiye alikuwa amebakia katika
familia hiyo zaidi hakuelewa chanzo cha
mauaji hayo yaliyofanywa.
Kama kawaida polisi walifanya uchunguzi
wao juu ya tukio hilo na kuondoka na
vielelezo wakiahidi kufanya upelelezi zaidi.
Hatimaye miili ya wanafamilia hao
waliouawa kwa kukatwa na mapanga ilizikwa
kijijini hapo. James alijawa na mawazo juu
ya muuaji wa familia hiyo na wazo la
kuhakikisha muuaji anapatikana linamkaa
zaidi kichwani mwake. Akili yake ilikuwa
tayari kuua katika kulipiza kisasi kwa mtu
yeyote ambaye angethibitika kuhusika na
mauaji hayo. Wakati huo alikuwa kidato cha
nne akiwa amebakiwa na miezi kadhaa ya
kumaliza shule, baada ya likizo aliondoka
akirudi shule akitarajia kupata taarifa za
wauaji kutoka jeshi la polisi.
Mali za familia hiyo ya marehemu Kibudo
zilianza kusimamiwa na mdogo wake ambaye
hakubahatika kuwa na mtoto katika maisha
yake. Zaidi alikuwa ni mtu mlevi ambaye pia
hakuwahi kuoa. Alichaguliwa kusimamia mali
hizo wakati James akisubiriwa amalize shule
ili akabidhiwe, hiyo yote ilitokana na hofu
waliyokuwa nayo ndugu wa familia hiyo ya
kuuawa iwapo wangesimamia mali hizo.
Ndugu wengi waliogopa hata kulala katika
nyumba hiyo ya marehemu mzee Kibudo
wakihofia kuuawa.
George Kibudo alisimamia mali hizo katika
misingi mibovu kutokana na tabia yake ya
ulevi aliyokuwa nayo. Baada ya miezi mitatu
James alirudi kijijini hapo na kuungana na
baba yake mdogo huyo kusimamia mali hizo
akiwa ameshamaliza kidato cha nne. Tatizo
lililomsumbua kichwani mwake lilihusiana na
kutokamatwa kwa mtu aliyehusika na mauaji
ya familia yake. Pia aliingiwa na hofu juu ya
sababu ya mauaji hayo, lakini jambo
lililokuwa kichwani mwake siku zote aliamini
baba yake hakuwa na kosa lolote
alilomfanyia mtu. Aliamua kuanza upelelezi
wake kwa utulivu kumfuatilia mtu aliyehusika
na mauaji hayo kwani aliamini alikuwapo
kijijini hapo. Alianza tabia ya ulevi ambayo
awali hakuwa nayo lengo likiwa ni kuwa
karibu na watu ili kufanikisha upelelezi wake.
Baada ya kipindi kifupi alibaini baba yake
alishawahi kufanya biashara ya pamoja na
mzee mmoja aliyejulikana kwa jina la Samola
miaka mingi iliyokuwa imepita. Katika
biashara yao hiyo walimalizana kwa
kufikishana mahakamani baada ya
kushindana katika kugawana n`gombe
walizokuwa nazo. Baada ya mzozo huo wa
kugawana n`gombe kumalizwa na
mahakama, baba yake hakuwa na uhusiano
wa karibu na mzee huyo ambaye alifilisika
miaka kadhaa baada ya kugawana kwao.
Upelelezi huo uliompa shaka ndiyo ulimfanya
James amweleze baba yake mdogo aliyeishi
naye wakati huo ambaye alipinga kuhusishwa
kwa mzee huyo katika mauaji hayo ya familia
yao.
Waliendelea na shughuli zao za kila siku,
wakati upelelezi wa James dhidi ya muuaji
wa familia yake ukiendelea. Siku moja akiwa
amelewa akirudi nyumbani kwao akitokea
eneo lililouza pombe za kienyeji ikiwa yapata
saa saba usiku, James alishtushwa na kelele
zilizotoka nyumbani kwao za mtu
aliyeonekana alikuwa akipigwa. Kutokana na
hali ya kulewa aliyokuwa nayo hakuingiwa na
hofu zaidi ya hasira zilizompanda akiamini
kuna watu walikuwa wakifanya mauaji.
Alichomoa panga lake aliloliweka kwenye koti
ambalo siku zote alikuwa akitembea nalo
akihofia usalama wake, alianza kukimbia kwa
kasi akielekea nyumbani kwao huku akipiga
kwa sauti ya juu kelele ambazo
hazikueleweka.
Mara baada ya kuukaribia mlango wa
nyumba yao, aliwaona watu wawili wakitoka
kwa kasi, mmoja akiwa na shoka na
mwingine akiwa na panga. Alisimama
pembeni kidogo na mlango wao akiwa
anatafakari afanye nini, punde kidogo alitoka
mtu mwingine kwa kasi ndani kwao akiwa
amebeba panga mkononi. James alitoka
mbio akimfukuza mtu huyo aliyekimbia kwa
kasi ya ajabu, baada ya kuwa mita kadhaa
nyuma akimfukuza akiwa anahisi hawezi
kumkamata aliamua kurusha panga lake
lililompata sawasawa mtu huyo shingoni. Mtu
huyo alianza kukimbia kwa kupepesuka kabla
ya kuishia kuanguka, James alimsogelea na
kuanza kumpiga kwa mateke.
Mtu huyo alianza kujiviringisha chini akipiga
kelele baada ya panga lililompata kutoka
shingoni na damu nyingi ilikuwa ikimtoka.
leo utasema anayewatuma kufanya
unyama alisikika James ambaye alikuwa
na hasira. Akiwa anaendelea kumpiga mtu
huyo katika eneo hilo la giza huku akili yake
ikiwa haijatulia kutokana na kulewa kwake
alishtushwa na kitu kizito kilichotua begani
kwake. Alianguka chini wakati mkono wake
wa kulia akielekeza kwenye bega lake la
kushoto na kushika panga lililomkata
sawasawa. Akiwa anapiga kelele kwa
maumivu aliwashuhudia watu wawili
wakimbeba mwenzao aliyemkata shingoni na
kuanza kuondoka naye kwa kasi eneo hilo
wakielekea katika vichaka vilivyokuwa karibu
na eneo hilo.
ITAENDELEA..