Kindo Emmanuel
Member
- Dec 5, 2021
- 34
- 25
Baada ya kuona kuwa nyumbani kunanichosha jioni ile, nikaamua niende katika baa iliyokuwa mtaa wa nne kutoka katika nyumba niliyokuwa naishi.
Pindi nilipowasili katika lango kuu la baa nililakiwa na sauti ya muziki wa ngwasuma ya Kikongo iliyokuwa ikirindima kutoka katika jukebox. Nilisimama nikiangaza wapi ningeweza kupa nafasi ya kukaa, maana muda ule tayari kulikwisha sheheni watu ukizingatia kuwa ilikuwa ni mwishoni mwa juma. Wahudumu walitingwa wakiranda huku na kule wakiwahudumia wateja wao.
Hatimaye niliigundua kulikuwa meza moja iliyokuwa na kiti chake kipweke ikiwa imejitenga katika kona iliyokuwa na mwanga hafifu wa taa kutokana na kuzongwa-zongwa na maua na miti ya bustani nzuri ya baa ile.
Niliijongelea kwa mwendo usio na taharuki na kwenda kujibweteka, kisha nikachukua simu yangu ya kiganjani na kuanza kuperuzi katika mitandao mbalimbali ya kijamii.
“Karibu kaka. Nikusaidie kinywaji gani?”
Sauti ya ukarimu uliolazimishwa ilinisaili, lakini sikutaka kunyanyua kichwa nimuangalie aliyekuwa akinisemesha kwani tayari nilisha mfahamu.
“Castle Lager baridi na…. anyway! Ni hivyo tu” Nilimjibu kisha nikasikia hatua ziondokazo.
Nikiwa nasubiri kinywaji changu kwa bahati mbaya ile simu yangu ikaisha moto (Charge) nikailaani kwa kuisonya na kuirudisha mfukoni.
Ghafla!........mithili ya sumaku pindi inasapo chuma, ndivyo macho yangu yalipovutwa na kukutana na ya kiumbe kizuri kisichokera mboni za macho ya mtazamaji. Ndiyo! Kiumbe chenye sura tamu maridhawa, isiyo na hatia. Alikuwa ni mwanadada niliyekosa kitu cha kummithilisha kwacho kwa uzuri aliotunukiwa.
Kwa macho yangu ya kimbea nilimkadiria kuwa yawezekana alipata kuingia hapa duniani yapata miaka 25 au 27 iliyopita. Alikuwa amekaa peke yake mita kadhaa toka katika meza niliyokuwa nimekaa mimi. Alitingwa akibofya simu yake ndefu na pana kwa ustadi mkubwa.
Alikuwa amevalia sketi fupi ya kitambaa cha jeans huku kiwiliwili chake kikiwa kimesitiriwa ndani ya blauzi ya rangi nyeupe iliyokuwa imemuacha mgongo wazi. Pasi na shaka ilikuwa imebuniwa na mbunifu wa mavazi aliyefahamu vizuri hali ya hewa ya mji wa Dar es Salaam.
“Labda ungependelea na chakula gani?”
Ilikuwa ni sauti yule mhudumu, sasa alikuwa ameniletea kinywaji changu.
“Ndizi tatu na mishikaki 6 tafadhali”
Ilijibu sauti ya kupendeza ambayo ilikuwa na uwezo wa kumshawishi hata ibilisi akaacha dhambi, sauti iliyotufanya mimi pamoja na yule mhudumu kugeukia kule ilikotoke. Tazama...! Alikuwa ni yule mwanadada mrembo niliyekuwa nikimthaminisha punde.
Mhudumu alinitazama tena kwa ishala ya kuniuliza kama nilimuafiki yule dada au la, nami nikatikisa kichwa juu na chini akaelewa nilimaanisha nini kisha akanukuu katika kijidaftari chake na kuondoka “Na Castle Lite baridi dada.” Yule mrembo aliongeza. Mhudumu hakujibu neno zaidi ya kuongeza tena maneno katika kile kijidaftari chake
“Samahani kwa kukuingilia…..” Alianza yule dada huku akiwa amesimama pale akinitazama. Akaendelea: “Sijui naweza kujumuika nawe hapa, au kuna wifi?”
Aliniuliza maswali mawili kwa wakati mmoja.
“Hapana. Unaweza kukaa tu, nipo mwenyewe”
Nilimjibu naye akaketi. “Ila tafadhali unitetee shemeji akija kuniletea zogo” Nilimwambia kwa masihara.
“Aagh, ondoa shaka nipo peke yangu”
“Inawezekanaje mtoto mzuri kuwa mahali kama hapa bila mtu wa kukusindikiza?”
“Kwanini?” Aliniuliza kwa mshangao uliofichua macho yake makubwa na angavu mithili ya mtoto mchanga.
“Kwasababu utakuwa unawanyanyasa kisaikolojia wanaume kama mimi niliye mpweke” Nilijinadi kiujanja.
“Wala usiwe mpweke, nipo kwaajili yako” Aliniambia huku amenitunuku tabasamu lililofanyiza vijishimo katika mgongo wa mashavu yake na kunizidishia mfadhaiko nafsini mwangu. Nilijua kuwa alikuwa akinitania tu katika namna ya kujenga urafiki. Kwani kwa haiba yake tu alionekana kuwa alikuwa ni 'matawi ya juu' na hakuumbwa kwaajiri ya uwepo wangu.
“Nashukuru sana. Enhee! Hivi unaitwa nani vile? Nilimuuliza.
“Fetty. Wewe?”
“John”
Nilimjibu huku roho ikiniuma kwa kumdanganya jina langu. Ilikuwa ni tabia yangu kutotaja jina langu kwa watu nikutananao juu kwa juu na nisiowafahamu, ila kwa mara ya kwanza nilijikuta najuta kumdanganya mtoto mzuri kama huyu. Lakini nilijiuliza ni kwanini najuta hivyo?
Mhudumu alituletea matakwa yetu na kutukaribisha kisha akaondoa zake. “Jina zuri. Mama yangu aliniambia usiogope kuuliza kwasababu ukiuliza baadaye hautasumbua watu kwa maswali, kwasabubu utakuwa tayari unajua mambo mengi na ndiyomaana napenda kuuliza” Nilianzia mbali kisha nikamuuliza tena: “So, unaishi wapi?”
Kabla hajanijibu simu yake iliita, akaipokea;
“Hallo, Daddy!...... Nilishamwambia dada kuwa leo nitalala huku huku hostel…… Yeah!.....Okay, I will! I love you too, daddy”
Alimaliza na kukata simu. “Aagh! Ni baba. Anapenda kunichunga-chunga utadhani mi’ ni mtoto mdogo” Alilalamika.
“Ana haki wa kufanya hivyo, kwasababu ni jukumu la kila mzazi kuhakikisha kuwa mwanaye yupo salama, hasa kwa mtoto wa kike kama wewe” Nilimwambia.
“Kwahiyo na wewe unam’support ?”
Aliniuliza. “Namaana yupo sawa hata mimi kama ungekuwa ni mwangu ningekuchunga kwasababu……unajua. You are so beau...”
“Okay, Okay! Tuachane na hayo” Alinikata kauli, akaongeza: “ Hivi uliniuliza nini vile?”
“Unaishi wapi?” Nilimuuliza swali ambalo hata sikumuuliza awali naye akanijibu lakini sauti yake ilimezwa ghafla na sauti za risasi zilizopigwa hewani! Wateja wote waliokuwa pale wakataharuki wakikimbizana huku na kule ili kuokoa roho zao, si wanaume wala wanawake kwa vijana…..wote walipaza sauti wakiwaita mama zao na Mungu wao.
Iliogofya mno! Nikiwa pamoja nao katika hamaki huku nikiwa sijui hili wala lile, nilihisi nimepigwa na kitu kigumu mithili ya chuma au nondo maeneo ya kisogo changu na punde ile ile nikaona ulimwengu mzima ukibadilika rangi pole pole na kuwa mweusi tii.
Fahamu ziliponirejea niligundua kuwa nipo ndani ya chumba chenye giza kuu. Chumba hicho kilikuwa kikitikisika sana na kufanyiza muungurumo ndipo nilipobaini kuwa nilikuwa nipo ndani ya gari lililokuwa likitembea katika barabara mbovu.
“Oya, wewe unanipeleka wapi, pumbaff?!” Niling’aka kwa mkwara nikigonga bodi la lile gari huku moyoni nikiwa na woga tele.
“We mbwa funga domo hilo, nitakuja kukurarua sasa hivi. Ohoo!” Ilikuwa ni sauti ngumu iliyojaa shari ikitokea upande wa mbele. Ikanibidi niwe mpole.
“He! Kumbe tupo wote?” Sauti ya kike iliuliza kwa kihoro.
“We nani?” Niliuliza.
“Mi’ Fetty! Ile sauti ilinijibu katika lile gari lenye giza.
“Hawa ni akina nani? Na wanatupeleka wapi?”
Nilimuuliza kwa jazba laiti kama angeona nilivyokuwa nimemtolea macho katika giza lile angezirai kwa woga.
“Mi’ mwenyewe sijui na wala siwajui hakyamungu tena”
Alijitete mfululizo huku akilia mpaka nikamuonea huruma.
“Nyie vinyago acheni kelele huko nyuma, hapa siyo kindergarten!” Ile sauti ya kibabe ilisikika tena ikitokea kule mbele.
“Mungu wangu tumetekwa. Tumetekwa!”
Fetty aliniambia kwa sauti ya chini huku akiendelea kulia.
“Ngoja tuone hatma yetu. Tafadhali naomba usitaharuki”
Nilimwambia huku nikimpiga-piga mgongoni kwa liwazo.
Gari lilizidi kuchanja mbuga tukiwa hatuelewi tulikokuwa tukipelekwa. Wakati mwingine ilinibidi kusimama wima ili kunyosha miguu na wakati mwingine nilipitiwa na usingizi, lakini nilipozinduka gari likikuwa lingali likitembea. Ilikuwa ni safari ndefu iliyochosha.
Baada ya kukaa kwa muda mrefu sana ndani ya lile gari lenye kiza cha mauti huku tukiwa tumekata matumaini ya kuendelea kuvuta punzi, hatimaye gari lilianza kupunguza mwendo mpaka likasimama kabisa. Haraka! Huku nikiwa na kihoro tele cha kutaka kujua ni nini kingejiri niliinuka roho ingali ikinidunda na kwenda mlangoni kutegesha sikio. Vilisikika vishindo vya hatua za watu kadhaa. Kila walipokanyaga ardhi nikahisi kama vishindo vile vikifanyiza mwangwi ndani ya ngoma za masikio yangu na kusababisha tumbo liniungurume kwa hofu. “Kazi iliendaje Victor?” Sauti yenye mamraka iliuliza. “Kila kitu kilienda kama ilivyopangwa boss. Ilikuwa rahisi sana tusivyotegemea ila alikuwa na bwana’ke tukaamua kuwachukua wote maana kama tungemwacha angeharibu mpango mzima” Sauti nyingine ilijibu, bila shaka ndiyo ilikuwa ya huyo aliyeitwa Victor. Hapo ndipo nilipogundua kuwa kumbe lengo lao lilikuwa ni kumkamata Fetty ila waliamua kunijumuisha na mimi kwakuwa nilikuwa pamoja naye wakidhani labda ni mpenzi wake. Lakini nikawa siishwi kujiuliza kuwa huyu binti ninini hasa alichowakosea hawa wakora. “Vizuri sana. Huwa nakupendea hapo tu. Hushindwi jambo. Okay, wapelekeni chumbani kwao”. Ile sauti ya kijivuni iliamuru. Nikasikia vile vishindo vya hatua vikirudi tena garini na injini ikahuishwa tena. Tulilitembea tena kama yapata maili kadhaa hivi kasha mlango wetu ukafunguliwa. Manaume wa miraba minne wali wapatao sita huku wakiwa wamekamatia bunduki walikuwa wamesimama pale nje wakiwa wanatutazama utadhani tulikuwa tu viumbe kutoka sayari nyinngine isiyojulikana.
“Haya, nyie mbwa shukeni faster !” Sauti ya Victor amboyo sasa nilikuwa nimeikariri ilituamrisha. Mithili ya mbuzi apelekwaye machinjioni tulitii amri bbila shurti. Kwa hasira niliyokuwa nayo nilitamani kama ningekuwa na bomu nijitoe mhanga tu ile nife naye pale pale.
Nje ya gari nililakiwa na baridi kali. Wakati ule tayali kulikuwa na giza lililokuwa likikinzana na mbaramwezi iliyokuwa ikinadi mwangaza wake katika anga. Nilitupa macho ya wizi-wizi mahali pale. Mbele kulikuwa na jengo kubwa na kuukuu mfano wa Kasri lililokuwa limejengwa kwa mtindo wa Mashari ki ya Mbali likiwa limezungukwa na ukuta mkubwa madhubuti.
Walinzi waliovalia magwanda kama ya kijeshi hivi sambamba na silaha zao za moto mikononi walirandaranda huku na kule wakitimiza wajibu wao huku wengine wakiwa katika vibanda vyao maalumu vilivyokuwa vimejengwa sehemu za juu juu. Hakika sehemu ile ilitisha mno hata nikajiuliza kama pale tulilepelekwa katika mafunzo ya kijeshi au?.
“Unashangaa nini?” Mmoja wa wale wakora alinibwatia huku akinipiga na kitako cha buduki. Mwingine akatoa kitaamba (Blindfold) na kumfunga Fetty usoni kisha nikafungwa na mimi. “Songa kule!” Kama vile vipofu. Tulitembea kwa kujikongongoja tukiwa hatujui tupelekwako, njiani nilijikwaa na kuanguka mara kadhaa kutokana na kile kitambaa walichokuwa wamenifunga usoni. Baada ya mwendo wa umbali fulani niliongozwa kupanda ngazi, kisha nikahisi nipo katika chumba kilicokuwa na kiyoyozi, halafu tukaingia ndani ya lifti iliyokuwa ikielekea katika vyumba vya chini (Basement). Tuliteremka kutoka ndani ya ile lifti tena kwa mtindo ule ule wa kuongozwa tulizidi kusonga kwa dakika kadhaa mle ndani huku tukikatisha kona nyingi mno mpaka katika chumba Fulani. Humo tulifunguliwa vile vitamba halafu wale wakora waliotuleta wakaondoka pasi kusema neno huku wakitufungia kwa nje.
Nilitazamana na Fetty tukiwa hatujui la kufanya mle ndani. Kilikuwa ni chumba kikubwa na maridadi. Mlikuwa na kitanda cha futi sita kwa sita sambamba na mashuka yake meupe, kochi moja la sofa lililoweza bubeba watu wapatao watatu kwa wakati mmoja sambamba na meza ndogo ya kioo. Upande wa Mashariki kulisimama kabati kubwa la kuhifadhia nguo huku pembeni yake kukiwa jokofu dogo. Upande mwingine wa ukuta palining’inizwa picha nzuri ya sanaa iliyochorwa kwa mkono ikimuonyesha mwanamke wa kiafrika anyonyeshaye mtoto. Zuria la manyoya lenye ragi ya kijani liliowana vizuri na rangi ya kuta na viyoyozi havikusahau kazi yake ya kuhakikisha kuwa mle ndani mnakuwa na hali ya ubaridi wakati wote. Uzuri wa chumba kile ulikosolewa na kitu kimoja tu. Ndiyo! Hamkuwa na dirisha wala tobo lolote lililoruhusu mtu wa ndani kuona nje wala wanje kuona ndani. Macho yangu yakavutiwa zaidi na mlango wingine mdogo uliokuwa mle ndani katika upande wa Kusini. Nikaujongelea taratibu na kwa hadhali, nilipojaribu kuufungua ukatii. Nikageuka kumuangalia Fetty ambaye wakati wote kumbe alikuwa akiniangali. Nilimpuuza na kuendelea na uchunguzi wangu. Niingia ndani ya ule mlango na kumbe kilikuwa ni chumba cha maliwato na bafu nikatoka na kurudi kujumuika na Fetty aliyekuwa amekaa pale kitandani akiwaza alichokuwa akiwaza. “Tutatoka kweli humu ndani?” Aliniuliza baada ya kimya kirefu kupita. “ Tumuombe Mungu. Ninaimani tutatoka tu salama” Nilimjibu kwa liwazo ilhali mimi mwenyewe sikujua hatma yetu. Kutokana na uchovu wa ile safari ndefu na yenye misukosuko hivyo nilipitiwa na usingizi japo sikuwa nimekula chochote zaidi zaidi ya kule bar. Pindi nilipoamka nilimkuta Fetty akiwa macho kando yangu pale kitandani.
“Habari ya asubuhi?” Alinisalimu. “Salama tu” Nilimjibu wakati sikuwa na uhakika kama kweli muda ule ilikuwa ni asubuhi maana mle ndani hamkuwa na saa. Istoshe simu zetu sijui kama tulizidondosha kwenye zile purukushani au walizichukuwa wale wakora.
Tukiwa tunazungumza na kuulizana maswali ya hapa na pale mara mlango ulifunguliwa. Kwapamoja mimi na Fetty tukajikuta tumesimama wima huku tukimuangalia Yule mtu aliyeingia. Alitufuata pale kitandani, akatutazama kwa awamu mithili ya mwalimu wa nidhamu awazae ni adhabu gani inayompasa mwanafunzi aliyekiuka sheria ya shule. Alikuwa ni mweusi kama mti wa mpingo na machoyake yalirembuka kama vile anausingizi au amevuta bangi. Mkono mmoja alishika bastola ndogo huku mwingine akiwa ameshika kijifurushi cha mfuko wa Rambo. Akatabasamu! Na punde lile tabasamu lililofeli kumpamba sura likatoweka kana kwamba alijua kuwa hata kama angecheka kamwe asingependeza.
Alipotosheka ‘kutuchora’ akarusha kile kijimfuko pale juu ya kitanda tulipokuwa tumeketi kisha bila kuongea neno akageuza na kuondoka zake huku akitufungia tena kwa nje.
Tulitazamana tena na Fetty macho ya kila mmoja yakiuliza maswali ambayo si mimi wala yeye alikuwa na majibu yake. Taratibu Fetty alichukua kile kijifurushi na kufungua ili ajue mlikuwa na nini, nikajumuika naye katika kutazama. Naam! Mlikuwa na nguo. Alitoa gauni refu la rangi ya buluu na madoa meupe na nguo za ndani. Pia mlikuwa na suruali ya kitambaa cheusi, mkanda na viatu jozi mbili vya kike na kiume.
Nilitabasamu na kumpongeza yeyote aliyepata wazo la kuleta vile vitu. Maana mavazi tuliyokuwa tumevaa yalikuwa yamechafuka na yalinuka jasho.
Tulioga na kuvaazile nguo tulizo letewa na Yule mkora kidogo nikajisikia mwepesi. Baadaye muda mref kupita mlango ulifunguliwa tena, akaingia yuleyule aliyekuja mwanzo na mavazi. Safari hii hakuingia mapaka ndani kabisa bali kwa mtindo wa kuchungulia. Kidogo nicheke kwa sauti. Maana alionekana kama Sokwe mzee nachunguliaye toka gizani. Sura yake ilitisha na kuchekesha kwa wakati mmoja.
Alichungulia kwa muda kisha akaingiza sinia lililokuwa llimebeba ’hot-pot’ tatu juu yake, kisha akaondoka. Alipokwisha funga mlango nikainuka na kulifuata lile sinia. Kwa njaa niliyokuwa nayo tayali nilishajua mnanini. CHAKULA!.
Mlikuwa na wali mweupe vilivyochanganywa viazi ulaya. Zile hot-pot nyingine moja ilibeba nyama sijui ya nini! Lakini ilivutia kwa macho, nyingine ilibeba njegere na ile ndogo ilichukua mboga za majani ila sikuwa na muda wa kuzifahamu. Sikumbuki kama nilikula kwa mikono au kijiko. Lakini chakula kilikuwa ni kitamu sana kama kile wapikacho katika hoteli za kitalii. Siku zilisonga tungali tukihudumiwa chakula, sabuni za kuogea na kufulia na mahitaji mengine. Wakati mwingine Yule mtu alikuwa akija na kutuuliza kama kuna mmoja wetu alihitaji dawa za matibabu na vitu vingine. Tulipewa kila kitu tulichohitaji mpaka nikahisi kuzoea mahali pale. Lakini ni kitu kimoja tu tulichonyimwa pindi tulipokiomba. Tuligombezwa na kutishiwa kuuliwa endapo tungeomba tena. UHURU. Hatukuruhusiwa kutoka nje ya kile chumba. Hata kwenda kupunga upepo.
Kwa wakati mwingine nilijihisi kupatwa wakati mgumu sana. Kulala chumba na kitanda kimoja na msichana mrembo achilia mbali tulikuwepo katika mazingira yanukayo kifo, ukizingatia msichana mwenyewe alikuwakatunukiwa sifa zote za kike ambazo zingeweza kumzuzua hata mwehu. Pia nilijisikia fedhea pindi alipofika siku zake. Sitaki kuongelea sana hili. Tuliendelea kuishi na kuzoeana huku sekunde na masaa yakikatika. Juma zilikuja na kuondoka aikazaa miezi. Siku moja mlango wa kile chumba tunachoishi ulifunguliwa. Tulisha zoea kutembelewa vile, Kama kawaida akaingi yule mkora ambaye huwa anatuhudumia. Lakini safari hii hakuleta mahitaji yoyote zaidi ya ile bastola ambayo sikuzote huwa nayo kama mavazi yake. Kisha nyuma yake alifuta mwnaume mwingine aliyeonekana kula chumvi kiasi akiwa amevalia mavazi ya ghalama na nadhifu sana. Suti yake nyeupe sambamba na viatu vyake vilirandana na nywele zake zilizouaga ujana. Ngozi ya mwili wake ilitakata kutokana na lishe na maisha mazuri, huku macho yake yalitoa nuru ya furaha muda wote. Alitembea mwendo wa taratibu lakini wenye mamraka na kuridhika na maisha. Akisaidiwa na mkongojo wenye nakshi ya chuma aliingia na kwenda kuketi pale kwenye sofa kubwa.
- ITAENDELEA -