mzaramo
JF-Expert Member
- Sep 4, 2006
- 6,371
- 5,191
MTUNZI: George Iron Mosenya
TUNUKIO!
Simulizi hii ni maalumu kwa kila mtanzania na yeyote anayezungumza na kukisikia Kiswahili. Simulizi hii iondoke na mawazo finyu uliyonayo kuhusu walemavu
wa ngozi yaani Albino. Ufungue moyo wako iruhusu na
akili yako kubadilika sasa!! Badilika wewe mbadili na
mwenzako!!
George Iron Mosenya!!!
SEHEMU YA KWANZA
Mungu akulaze pahala unapostahili Judith!! Najua
wazi kuwa laiti kama ungekuwa hai leo hii basi huu
ungekuwa wakati wako wa kupoteza uhai kutoka na
uchungu ambao ungepitia. Uchungu uleule uliokuwa
ukipitia tangu tulipokuwa watoto wadogo, wanmafunzi
waliponiita kwa jina baya kabisa la Zeruzeru
ulichukizwa na licha ya kwamba ulikuwa msichana
ulijaribu uwezavyo kunipigania na mara nyingi
ulishinda. Walipokushinda kwa nguvu uliwashinda kwa
maneno!!
Laiti kama wangepatikana watetezi mia moja kama
wewe Judith huenda pasingekuwa na simulizi hii.
Naam! Ingetoka wapi sasa wakati pasingekuwa na
tofauti kati yetu sisi Albino na wenzetu wanaoamini
wamebarikiwa na Mungu anawapenda sana kwa
kuwapa ngozi hizo!!
Mungu hana upendeleo hata kidogo jama!!
Alivyokuumba hivyo usijihesabia kuwa wewe ulipendwa
zaidi, kamwe Mungu haumbi kiumbe asichokipenda!!
Looh! Judith ulikufa mapema sana Judy!! Ulikufa
wakati ule hata mauaji haya hayajawa kitu cha
kawaida!!
Ninapoyasimulia haya naamini roho yako ipo hapa
ikitiririkwa machozi na kutapatapa kwa hasira kali!
Nayasimulia haya kwa kuanza na jina lako Judy.
Naamini Judy ulikufa wakati ambao haukustahili
kufa!!
Eti ulikufa kwa homa kidogo tu mara ikawa homa kali
na hata hospitali hukufika!!
Nimeanza nawe Judy katika simulizi hii!!
Mungu aipumzishe nafsi yako pema lakini walau
aiamshe sasa na kuipa nafasi ya kuisikiliza simulizi hii
mwanzo hadi mwisho!!
Nakupenda Judy!!!
*****
Mnamo mwaka 1996 nikiwa darasa la kwanza ndio kwa
mara ya kwanza kabisa nilipiotambua kuwa palikuwa
na tofauti kati yangu mimi na watoto wengine pale
darasani.
Mama yangu hakuwahi kuniweka wazi kuwa nilikuwa
nina tatizo la ugonjwa wa ngozi lakini shule ilinuipa
majibu!!
Shule nzima ni mimi pekee nilikuwa albino.
Nilikuwa sina rafiki hadi pale alipohamia shuleni kwetu
msichana aliyeitwa Judith!!
Sijasahau kitu hata kimoja katika simulizi yangu,
miaka saba niliyokuwanayo inatosha kabisa kukumbuka
kila kitu.
Ninakumbuka hadi maonyo ya mama yangu, kuna
kipindi aliwahi kuniita na kuzungumza nami!!
Alinieleza kuwa kuna fununu zinatapakazwa na
imekuwa mazoea kabisa kuwa eti ni jambo la kawaida
kabisa kwa Albino kupotea hasahasa ukifika wakati
wao wa kuaga dunia!!
Naikumbuka sauti ya mama ambaye alinieleza kuwa
baba yangu alimkimbia baada tu ya kunizaa mimi
nikiwa albino!!!
“Mwanangu Majaliwa nilimuomba Mungu sana na
Mungu hadanganyi kamwe, Mungu akanijibu kuwa
alinipatia mtoto na huyo mtoto ni wewe. Wewe ni
mwanadamu kama wanadamu wengine, Majaliwa!!
Nilikuwa jasiri sana baba yako alivyonikimbia na wewe
jifunze kuwa jasiri pale ambapo watu watakukimbia.
Nitakusimamia mwanangu, utasoma hadi utamaliza
chuo kikuu sawa mwanangu”
Naam! Sijaisahau sauti ile ya mama, sauti
inayozungumza katika masikio yangu hadi leo hii!!!
Yale maneno ya mama yakaanza kutimia, wanafunzi
wakaanza kunitenga. Wakajiweka mbali nami kasoro
Judith tu!!
Naumia sana msikilizaji, naumia kwa sababu Judith
alikufa akiwa bado namuhitaji sana!!
Ila nisilalamike sana isijekuwa nafanya kufuru!!!
Nilifanikiwa kumaliza darasa la saba na kuchaguliwa
kujiunga kidato cha kwanza!!
Nilikutana na changamoto zilezile…. Lakini kwa
kutoka kwa wanafunzi hazikuwa na matatizo kwangu
kwa sababu mama alikuwa akinitia moyo kuwa
wananichukia kwa sababu nilikuwa na uwezo mkubwa
sana darasani kuwazidi.
Maneno ya mama yalikuwa yakiniimarisha sana!!
Lakini sikuweza kuwa imara pale mwalimu wangu wa
darasa siku ile nimechelewa kufika darasani wanafunzi
wakiwa kimya kabisa akanitamkia maneno ambayo kwa
mara ya kwanza yalianza kunipa mashaka katika
maisha yangu na hapo nikaitazama ngozi yangu mara
mbilimbili. Hadi ninaposimulia haya nakiri kuwa
sijawahi kumsamehe Yule mwalimu!!!
Yule mwalimu aliniambia kwa dharau kubwa kabisa.
“Jichunge sana kuchelechelewa huku watu
tunakutafuta sana wewe tuepukane na haka
kamshahara kadogo ka ualimu!!” maneno yake
yaliniingia na nikayashika kama yalivyo.
Yalikuwa maneno magumu kuyaelewa na mama alikuwa
ameniambia kuwa kila nikiambiwa maneno
nisiyoyaelewa nisiste kumweleza. Nikaenda kumweleza
mama kauli ile ya mwalimu wangu!!
Mama alihema juu juu, akajaribu kuongea hakuweza,
akabaki kutupa mikono huku na kule…. Neno pekee
aliloweza kutamka ni ‘yaani….. yaani…’ hakuweza
zaidi akaanza kulia. Ni hapo nikatambua kuwa kauli ya
Yule mwalimu ilikuwa kauli mbaya.
Mama hakulilazia damu, siku iliyofuata tukaenda wote
shuleni hadi kwa mkuu wa shule!!
Akamweleza mashtaka yale!!
Ajabu mkuu wa shule hakuonekana kushtuka!!
Akamtazama mama kasha akamuuliza.
“Mwanamke ni hili tu limekuleta?”
Mama akabaki kushangaa. Yule mwalimu akaendelea
tena.
“Mama tena bora umekuja mwenyewe, kwa sababu
nilikuwa nimepanga kukuita!! Na ninapenda kutoa
onyo mbele ya mtoto wako, mama hapa shuleni ni
mtoto wako pekee ambaye ana hali hii… sasa
nakwambia mama ni ama umtafutie uhamisho lakini
ikitokea shule yangu inapata matokeo mabovu basi
utanijua mimi ni nani??” alizungumza kwa ghadhabu
kasha akatoka nje na kutuachia ofisi.
Nilimtazama mama yangu akiwa na kanga yake
iliyochakaa akikosa la kufanya. Akageuka na
kunitazama nikayaona machozi yakimtoka mama yangu
ambaye alikuwa yu mweusi kabisa si kama mimi.
“Majaliwa mwanangu, Mungu ananiweka hai hadi sasa
ili nikulinde, kama baba yako mzazi alikukataa watu
baki kama hawa wanashindwa nini kukukataa, shule
zipo nyingi mwanangu na hawa wanakuchukui kwa
sababu tu una akili kuwazidi. Utasoma mwanangu
utasoma!!” alizungumza mama huku nikimsikia kuwa
alikuwa analia!!
Chozi la mama likanidondokea katika utosi wa kichwa
changu, likanisisimua nami kujikuta ninatokwa na kilio
huku nikimkumbatia mama yangu kwa nguvu zaidi!!!
Mwalimu mkuu akafika na kutuamrisha tutoke ofisini
kwake!!
Siku iliyofuata sikwenda shuleni bali niliongozana na
mama hadi kwa mkuu wa wilaya. Mama akajieleza
vyema kuhusu maneno makali ya mkuu wa shule na
Yule mwalimu wa darasa.
Mkuu wa wilaya hakuwa muongeaji sana. Akaandika
barua na kuifunga katika bahasha na kisha
akamwambia mama kuwa siku inayofuata aifikishe
barua shuleni.
Barua ile ikawa mwisho wa mwalimu mkuu ya Yule
mwalimu mwenzake kunitamkia maneno mabovu!!!
Hadi namaliza kidato cha nne hapakuwa na matatizo
sana na hiyo ilikuwa ni mnamo mwaka 2006!!
Ilikuwa heri nikachaguliwa kujiunga kidato cha tano.
Nikachagulia kwenda shule iliyopo kanda ya ziwa!!
Siichukii kanda ya ziwa hata kidogop na ninawapenda
sana watu wa kanda ya ziwa hadi ninapousimulia
mkasa huu lakini napenda kuwaeleza waziwazi bila
kificho kuwa ni hapohapo kanda ya ziwa mikono ya
albino wenzangu ilikatwa, sehemu zao za siri zilikatwa
tena bila ganzi, naumia sana naumia kwa sababu
niliona kwa jicho langu!!!
Niliona miguu ikikatwa, nilipata bahati mbaya zaidi
kushuhudia jicho la mwanadamu ambaye hajakata roho
likinyofolewa!!
Walionyofoa walikuwa wakitabasamu na bila shaka
walijiona watu waliobarikiwa sana kupata bahati ile ya
kuvipata viungo vya albino!!!
Zikipitishwa sura zao hapa hao wauaji hata wawe
wamezeeka vipi naapa kwa jina la Mungu
aliyeniumba….. naapa nitawakumbuka!! Akili yangu
haijawahi kuwasahau!!!
Kanda ya ziwa iliimeza damu ya wenzangu wengi tu!!!
Siichukii kanda ya ziwa lakini walaaniwe waliothubutu
kututenda vile!!!
Ni huku nilipochaguliwa kujiunga kidato cha tano na
cha sita!! Nilikuwa sina wasiwasi lakini mama yangu
alikuwa na mashaka tele. Aliniambia kuwa nilikuwa
nimekomaa akili basi nijifunze jinsi ya kujilinda!!
Nilikuwa muoga sana kuchinja kuku, mama
akanilazimisha niwe nachinja kuku. Nilipomuuliza ni
kwanini ananilazimisha alinifokea.
“Yaani wewe wanaweza wakatokea majambazi hapa
wakanipiga halafu wewe una kisu ukashindwa
kupambana nao”
Hayo yalikuwa ni maneno ya mama yangu mzazi!!!
Maneno ambayo ilifika siku nikaijua maana yake!!
Kumbe mama hakutaka tu kuniambia waziwazi kuwa
wapo watu wabaya sana duniani!!
Kule Kanda ya ziwa, nasikitika kuwa sitautaja huo
mkoa moja kwa moja. Sihitaji uuchukie mkoa ule bali
wachukie wale wauaji!!
Nilisoma pale kidato cha tano nikamaliza salama
kabisa, mama alijitahidi kuniandikia barua mara kwa
mara na ikafikia hatua akanunua simu yake ya kwanza
ya mkononi kwa ajili tu ya kuwasiliana na mimi.
Alinisihi sana niishi kwa tahadhari. Maneno ya mama
yalijikita katika kichwa changu vyema.
Kitu kibaya ni kwamba sikuona nini maana ya zile
tahadhari sasa ikiwa sijaona baya lolote likikaribia
kunitokea.
Amakweli mdharau mwiba mguu huota tende asilani!!
Na ni heri nusu shari kuliko shari kamili.
Nilipomaliza kidato cha sita nikajiona ya kuwa mimi
nimekuwa mtu mzima. Ile kujichanganya na watu
wasiokuwa na ulemavu kama mimi nikajiona nipo sawa
kabisa. Sikujua hata kidogo kuwa baya hujificha
likisubiri ukosee maelekezo ndipo liibuke.
Maisha magumu ya mama yangu yakanifanya nijione
mpuuzi sana kuendelea kukaa nyumbani nikiyasubiri
matokeo ya kidato cha sita. Mama hakuuchukulia
uwepo wangu nyumbani kama tatizo badala yake
alifurahia kuwa amekuza mtoto.
Maneno ya marafiki yakaanza kuibomoa akili yangu,
wakanisifia kuwa nilikuwa najua sana somo la hesabu
hivyo nitafute shule niwe nafundisha kwa muda ili
nimsaidie mama yangu.
Nilipomwambia mama akanipinga vikali sana
akaniambia nikae nyumbani.
“Majaliwa mwanangu wewe ndiye mwanangu wa pekee,
tangu baba yako anikimbie unajua wazi kuwa sijawahi
kuolewa tena. Kaa mwanangu tutakachopata tutakula
pamoja, bado unahitaji uangalizi wangu majaliwa we
kaa tu usijali!!” mama alinisihi lakini sikuelewa
nikalazimisha hatimaye akakubali.
Sikuwa na ujanja wa kutafuta shule mimi mwenyewe,
wale marafiki wakanieleza kuwa yupo mtu ana shule
yake anahitaji waalimu. Wakampatia mtu Yule namba
ya mama ili waweze kuwasiliana naye niweze kwenda
kufundisha shule yake!!
Sitazisahau nyakati hizo kamwe!!!