Riwaya:Lazima nikuoe Part-1

Riwaya:Lazima nikuoe Part-1

wiseboy.

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2014
Posts
2,931
Reaction score
4,550
Ilikuwa majira ya saa 9 alfajiri wakati nilipoamka na kukaa kitandani, usingizi ulinigomea kabisa, mtoto wa kiume mie nikaanza kulia kama mtoto mchanga anayechomwa sindano, nilikuwa nikimlilia Lilian binti mrembo ambaye aliamua kuniasi na kwenda kwa mwanaume mwingine ambaye kwa kipato alikuwa ananizidi zaidi ya mara mia, nilikuwa na haki ya kulia, maana bila mimi Lilian asingeweza kuonekana ktk uso wa dunia hii kuwa yu mrembo,sasa Lilian alisahau yote na kuamua kunisaliti,nilikutana na Lilian kwa mara ya kwanza ktk mataa ya mnazi mmoja,Lilian alikuwa ni ombaomba akiwa na kundi la watoto wadogo aliokuwa akiwaongoza,umri wake haukuwa chini ya miaka 15,macho yake kama ya Ray c,umbo lake kama la J.Lo na sura yake nzuri kama ya Alicia Keys na rangi ya chocolate,hakika Lilian alikuwa mrembo,nakumbuka akiwa kasimama kwenye gari langu pale mataa akiomba nilijikuta bila kutarajia nampatia burungu la noti za elfu moja zenye thamani ya sh elfu hamsini,aliruka kwa mshtuko akakimbia akitokomea kama mwizi kwa furaha...inae.
 
ilikuwa majira ya saa 9 alfajiri wakati nilipoamka na kukaa kitandani,usingizi ulinigomea kabisa,mtoto wa kiume mie nikaanza kulia kama mtoto mchanga anayechomwa sindano,nilikuwa nikimlilia Lilian binti mrembo ambaye aliamua kuniasi na kwenda kwa mwanaume mwingine ambaye kwa kipato alikuwa ananizidi zaidi ya mara mia,nilikuwa na haki ya kulia,maana bila mimi Lilian asingeweza kuonekana ktk uso wa dunia hii kuwa yu mrembo,sasa Lilian alisahau yote na kuamua kunisaliti,nilikutana na Lilian kwa mara ya kwanza ktk mataa ya mnazi mmoja,Lilian alikuwa ni ombaomba akiwa na kundi la watoto wadogo aliokuwa akiwaongoza,umri wake haukuwa chini ya miaka 15,macho yake kama ya Ray c,umbo lake kama la J.Lo na sura yake nzuri kama ya Alicia Keys na rangi ya chocolate,hakika Lilian alikuwa mrembo,nakumbuka akiwa kasimama kwenye gari langu pale mataa akiomba nilijikuta bila kutarajia nampatia burungu la noti za elfu moja zenye thamani ya sh elfu hamsini,aliruka kwa mshtuko akakimbia akitokomea kama mwizi kwa furaha...inae....

mtunzi wa riwaya ni nani??
 
Tittle yenyewe imeshapoteza hadhi ya maana halisi ya riwaya, labda uiite tu ndoto yako kwa kuwa umeamka nayo usingizini.
 
Katika maisha yangu sijawahi kupata mshtuko kama niliopata siku hiyo,taa ya kijani iliwaka nikaondoa gari kwa kasi ya ajabu utadhani nilikuwa peke yangu barabarani,mwendo kasi ule nilijikuta naigonga gari ndogo iliyokuwa mbele yangu na kusabisha foleni kubwa nyerere road,jamaa mwenye miraba minne na sura ya kutisha alitoka kwenye gari niliyokuwa nimeigonga mkononi akiwa na bastola,nilifungua mlango wa gari nikatoka na kutimua mbio kuelekea central police ili kuinusuru roho yangu,nilipofika eneo la karibu na stesheni ya treni nilimuona Lilian akiwa peke yake bila ya wale watoto aliokuwa anawaongoza kuomba,Lilian alikuwa analia na hakuwa na lile burungutu la fedha nililokuwa nimempatia,mawazo ya kwenda tena polisi yalitoweka akili yangu yote ikarudi tena kwa Lilian,nilimuuliza ni kipi kilikuwa kimemsibu wakati alipoanza kunielezea tu nilishtuka ghafla kuna mtu nyuma yangu kanielekezea bastola,nilipogeuka ili nimtazame vizuri mwili wote uliishiwa nguvu nikabaki natetemeka....continues.
 
Back
Top Bottom