Riwaya Kali

Riwaya Kali

Man_Sai

Member
Joined
Aug 24, 2016
Posts
8
Reaction score
8
SIMULIZI: Jina
NA: Frank Masai
SEHEMU YA 1.

"Ni siku nisizoweza kuzisahau. Ni siku zilizobadili maisha yangu na kuwa maisha mengine katika dunia hii. Siwezi kusahau, na siwezi kuthubutu kusahau jinsi jina lilivotesa maisha yangu. Jinsi jina lilivyonibadili na kuwa mtu tofauti na nilivyokuwa mwanzo.
Life, is just a beginning of long journey that you'll never know where it will end. (Maisha, ni mwanzo wa safari ndefu ambayo huwezi kujua ni wapi itaishia)
Nachokumbuka jina limenifanya niwe hapa leo. Jina ndio sababu ya mimi kupewa majukumu magumu na dunia hii pamoja na kulitetea taifa langu la Tanzania. Hakuna maisha magumu, bali kuna mapito magumu. Nakuja kupambana na madhalimu waliovamia kisiri nchi yangu pendwa na kuifanya kama genge la wahuni. Ni mimi Frank Masai."
Maneno makali yalikuwa yanatoka kwenye kanda moja video iliyonakiriwa na Frank Masai mwenyewe na kutumwa kwa njia ya mtandao.
Na baada ya maneno hayo, Frank alisimama na kuvaa begi lake la jeshi mgongoni na kuanza kuondoka ile sehemu alipo.
"Atakuwa wapi huyu mtoto?" Montana Juvenile, mkuu wa kitengo cha upelelezi wa siri cha Tanzania, alijikuta akijiuliza swali ambalo kamwe hakupatiwa jibu na mtu yeyote katika ukumbi mkubwa wa jengo lile la kipelelezi.
"Embu rudisha hiyo kanda hapo nyuma kidogo." Montana alitoa ombi na kanda hiyo ikarudishwa nyuma kwa utaratibu ili akiona pale anapopataka aseme.
"Hapo hapo." Montana akamrisha mkanda usimamishwe. “Vuta hiyo picha ya nyuma kwa ukaribu zaidi." Yule opareta akafanya hivyo na kuifanya kile anachokivuta kiwe kama kina mawimbi, hali iliyofanya picha isionekane vema.
"Clear that." Montana aliamrisha pale pasafishwe ili paonekane.
Hapo opareta akabofya bofya kompyuta yake, na kioo cha runinga kubwa iliyopo mle ndani, ikaonesha mistari mistari ikipanda na kushuka. Hatimaye picha ikaonekana safi.
"Chon Ping?" Montana alijikuta akiropoka peke yake. "Ipo wapi hii." Akauliza swali baada ya kuyaona yale maneno yaliyovutwa.
Kitendo bila kuchekewa, mtaalamu mwingine wa kompyuta, akaingiza maneno hayo kwenye kompyuta na kisha kompyuta ikaanza kutafuta.
Sekunde kadhaa, jibu la Chon Ping likawa mbele yao. Na uzuri lilikuwa moja tu dunia nzima.
“Boss, Chon Ping ni mgahawa uliopo Vietnam na unamilikiwa na familia ya Ping ambayo kazi yao kubwa ni kupokea watalii mbalimbali wanaodhulu nchi ile." Kijana mmoja hodari alielezea kwa ufasaha na kwa kifupi kuhusu Chon Ping.
"Huo mkanda umerekodiwa saa ngapi."Montana alimuuliza opareta wa ile runinga, naye kwa utaalamu alioupata kutoka kwenye somo la Jografia, akatoa majibu ya haraka.
"Ni mida ya saa kumi na mbili jioni. Naangalia hapa jinsi kulivyo…." Akarudisha kanda ile nyuma na kuonesha sehemu ya dirishani.
"Kama utaangalia kwa umakini, utaona kivuli cha bati la nyumba akiyokuwamo huyu bwana kikiwa kimeenda mbali na kimefifia kutokana na jua kupungua makali yake.
Na kingine....." Hakumaliza kauli yake, Montana akawa amemkata kauli kwa kukubaliana na kile anachokizungumza.
"Na mkanda huu ulikuja saa ngapi." Montana alitupa swali lingine kwa mtaalamu wake.
“Mkanda uliingia saa moja na nusu jioni, leo hii kwa njia ya satellite na kujirekodi wenyewe kwenye mashine zetu.
"Na sasa hivi saa ngapi?" Montana akauliza swali huku anafunua mkono wake na kuangalia saa.
"Saa tatu na dakika thelathini na tatu usiku." Akajibu opareta wa runinga na kumfanya Montana atikise kichwa kukubali majibu yale.
"Hapa hadi Vietnam ni dakika ngapi kwa kutumia Jet P One Twelve (P 112)" Badala ya kujibu, wataalamu wote walijikuta wametoa mshangao kwenda usoni mwa bosi wao.
"Vipi, mbona hamnijibu?" Montana aliyekuwa anashahuku ya kuonana na Frank Masai, aliuliza huku anawatazama wafanyakazi wake karibu ishirini waliokuwamo katika jumba lile la kipelelezi. Jumba ambalo hadi leo, hata wafanyakazi wake hawajui lipo mkoa gani, wanachojua ni kuwa lipo Tanzania.
"Kwa P 112, ni nusu saa hapa Tanzania hadi Vietnam." Akajibu mwanasayansi mmoja aliyekuwa kavalia mawani ya macho na kumfanya aonekane nadhifu kama si msomi kabisa.
“Nataka vijana wawili tuongozane sasa hivi kwenda Vietnam. Hatokuwa kafika mbali huyu kijana." Montana aliongea huku akiondoka pale ukumbini na kuelekea ilipo ofisi yake.
Akabonyeza namba fulani zilizo mlangoni kwake, mlango wa kioo ambao hauingizi risasi. Na kama upo ndani ya ofisi, huwezi kusikika ukiongea ila wale wa nje wakiongea, wa ofisini anamsikia vema.
Mlango ukafunguka na Montana Juvenile akaingia ndani ya ofisi yake na kukwapua simu ambapo akiipiga moja kwa moja katika kituo kikubwa cha mamlaka ya hali ya hewa cha Marekani (NASA) na kuwapa taarifa za kuonekana kwa Frank huko Vietnam.
NASA nao baada ya kupata taarifa hizo kutoka Tanzania, wakairuhusu ndege maalumu ambayo muda wote hutembea angani kwa ajili ya kuendesha mitambo ya iliyopo duniani. Mara nyingi ndege hizo huwa na kamera maalumu ambazo huchukua picha hata za masafa marefu.
NASA wakairuhusu ndege hiyo iende hadi Vietnam katika eneo ambalo mgahawa wa Chon Ping upo.
Ndege ikiongozwa na wataalam waliobobea wa pale NASA, ikafanya kama inavyoelekezwa.
Ikafika sehemu uliopo mgahawa wa Chon Ping, na kuanza kuvuta picha mbalimbali za eneo lile. Na picha hizo mara moja zilitumwa hadi NASA na shirika la upelelezi la Marekani (FBI) ambalo nalo lilikuwa katika mchakato mkubwa wa kumsaka Frank Masai.
Picha zikazidi kupigwa eneo lile na sasa ndege ile ikavuta zaidi eneo moja ambalo kwa jinsi ilivosadikika, ndipo Frank alimokuwamo kabla hajatoka na kutitia pasipojulikana.
Ndege ile ikavuta zaidi hadi chini ya mlango wa kutokea kile chumba alichokuwepo Frank. Kwa pale chini pakaonekana kuna nyayo fulani za viatu.
Nyayo zile zikaanza kuvuliwa kitaalamu kwa kutumia mitambo ya NASA na FBI, na baadae nyayo zile japo zilikuwa za viatu, zikabaki uchi na kuonekana mmiliki wake.
Zilikuwa ni za Frank Masai, hapo hapo ndege ile ikaachiwa na kuanza kufuatilia nyayo hizo zinapoelekea.
****

FISSA (Federal Intelligence Secret Service Agencies)

Montana Juvenile baada ya kumaliza mawasiliano na NASA, akatoka nje ya ofisi na kwenda kwa vijana wake.
"Tayari mmeiandaa Jet P 112 kwa ajili ya safari yetu." Montana aliwauliza vijana aliowaachia majukumu.
"Ipo tayari mkuu." Alijibu jamaa mmoja kiukakamavu.
"Na wale vijana niliowahitaji wapo?" Montana aliuliza tena.
"Wapo mkuu. Wapo kule kwenye ndege pamoja na vifaa mbalimbali vya kijeshi na mapambano." Alizidi kuonesha utendaji bora wa kazi yule bwana.
"Good. Sasa naweza kwenda kumtafuta huyu mtu." Montana aliongea huku akianza kuondoka eneo lile la ofisi.
Akafika mlango mmoja ambao ulifunguka bila hata kuushika.
Akanyoosha moja kwa moja ambapo kulia kwake akakuta mlango wa chuma na kitasa chake kilikuwa kinafunguliwa kwa kadi maalumu aliyokuwa nayo yeye na baadhi ya wakuu wengine wa mle ndani.
Akaingiza kadi hiyo na mlango ukatii kwa kufunguka huku ukitoa sauti ya juu kidogo.
Humo ndani alilakiwa na vijana wapatao watano. Wawili wakiwa wale aliowaagiza na watatu walikuwa madereva wa ndege ile aina ya Jet P 112.
Ndege hiyo ilikuwa imekaa eneo moja kubwa na sura yake ilikuwa hailezeki kwa jinsi ilivyokuwa kubwa na rangi nyeusi iliyokuwa nayo.
JET P.112, kama ilivyoandikwa ubavuni. Ni ndege iliyobuniwa mwaka 1946 na jeshi la Japan ili wapiganie vita ikiyokuwa inawatazama, nazungumzia vita vya pili vya dunia. Lakini hawakufanikiwa kuitumia baada ya nchi yao kupigwa Bomu la Atomic na nchi onevu ya Marekani.
Bomu hilo lililopigwa Hiroshima, ndilo lilimaliza vita vya pili vya dunia. Na baada ya kupiga bomu hilo, Marekani wakaenda katika makao ya jeshi la Japan na ndipo wakaikuta ndege hiyo ya kijeshi ikiwa katika hatua za mwisho katika ujenzi wake. Wakaichukua, na sasa wameiboresha na kila nchi washirika wa Marekani, waliweza kupatiwa ndege hii ambayo inaaminika hadi hivi usomapo, hakuna ndege yenye kasi kama yenyewe licha ya kuwa kubwa na yenye uzito mkubwa kuliko ndege nyingine za kivita.
Inaweza kubeba mabomu pembeni na katikati kwa wakati mmoja. Na pia inabunduki za hatari katika mabawa yake.
Yote kwa yote, ndege hii inaweza kuzama baharini kama zifanyavyo nyambizi. Sasa Montana Juvenile, alikuwa mbele ya ndege hii ambayo inamitambo maalumu ya kuwasiliana na FISSA, CIA, NASA na FBI.
Montana Juvenile, akameza funda la mate kubwa kabla hajaifata ndege ile akiwa na baadhi ya watu wake.

Watch Out Part 2
 
Back
Top Bottom