Riwaya Kali; Briefcase

Riwaya Kali; Briefcase

Six Man

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2017
Posts
253
Reaction score
893
RIWAYA; BRIEFCASE
MTUNZI; HALFANI SUDY
WhatsApp 0674 395733

Sehemu Ya Kwanza

ILIKUWA ni usiku wa saa sita. Anga la jiji la Dar es salaam lilikuwa limetulia baada ya kunyesha mvua kwa saa mbili mfululizo. Mvua liliyoiacha mitaa kadhaa ya jiji la Dar es salaam ikiwa imejaa maji kutokana na ujenzi wa hovyo wa barabara bila mfumo nzuri wa mifereji.

Katika nyumba moja iliyokuwepo katika mtaa wa Mbagala maji matitu kulikuwa na mtu mmoja akiwa amelala kitandani. Kijana alikuwa anajulikana kwa jina la Alex. Mfanyabiashara wa viatu katika soko la Tandika.

Alex alikuwa amelala fofofo katika chumba kidogo cha kupanga. Ndani ya chumba chake hakukuwa na kitu chochote kile cha zaidi ya kitanda kile dhaifu. Kwa kuangalia mwonekano wa chumba chake tu ilikuwa ni taswira ikiyoonesha hali yake ya kiuchumi. Alex alikuwa ni kijana mbangaizaji pale sokoni akimiliki biashara ya viatu visivyozidi kumi.

Historia ya Alex ilianza miaka ishirini na tano iliyopita huko wilayani Mkuranga. Alizaliwa katika kijiji kidogo cha Kisemvule, kijiji kilichopo wilayani humo. Alimaliza darasa la saba shule ya msingi Kisemvule na kubahatika kuendelea na Sekondari katika Sekondari ya Ally Hassani Mwinyi iliyopo Mkuranga mjini. Kidato cha nne ndio kilikuwa kikomo cha elimu yake ya darasani. Ndipo alipoingia mtaani akiwa na miaka kumi na saba tu. Biashara yake ya kwanza ilikuwa kununua nguo za mitumba mnadani na kwenda kuziuza mitaani. Baada ya miezi kadhaa alihamia Dundani alipokuwa akiishi na wazazi wake na kuhamia Mbagala maji matitu. Mwaka mmoja baadae akiwa anaishi Mbagala alibadilisha biashara ya nguo na kuanza kuuza viatu huko sokoni Tandale.

"Aaah nani tena ananipigia usiku huu" Alex alisema kwa sauti ndogo huku akiivuta simu yake aina ya Nokia ya tochi na kuiweka sikioni.

"Haloo Ha..loo" Alex alisema kwa sauti yenye usingizi.

"Bila shaka naongea na Alex" Sauti nzito iliongea simuni.

"Ndio"

"Sikiliza ninachokwambia kisha utekeleze."

"Wewe ni nani? Naongea na nani?" Alex aliuliza kwa pupa. Usingizi ulianza kumtoka.

"Huna sababu ya kujua jina langu. Una haja ya kujua nini ninachotaka kukwambia.
Ni hivi, kesho, saa nne asubuhi unatakiwa kwenda Posta. Unatakiwa kwenda nje ya ghorofa la RITA lilipo Posta. Unatakiwa kusimama tu pale. Atakuja mtu na kukupa briefcase, na maelekezo ya wapi pa kuipeleka briefcase utaelekezwa katika simu" Sauti ya kwenye simu ilisema.

"Sikuelewi kabisa bila shaka utakuwa umekosea namba brother" Alex alisema.

"Naongea na Alex Manda. Mtoto wa kwanza wa mzee Manda wa huko Dundani, Mkuranga. Elimu yako ya msingi ulisoma Kisemvule na baadae ukajiunga shule ya Sekondari Mwinyi. Ulimaliza. Ulipata daraja la tatu lakini haukuchaguliwa kujiunga na kidato cha tano . Ndipo ulipojiingiza katika biashara ya kuuza nguo, na baadaye ulianza kuuza viatu ulivyohamia Mbagala maji matitu. Hauna mke, hauna mchumba. Kwa sasa umelala kitandani kwako, umevaa bukta bluu ya Chelsea ukiwa kifua wazi. Unataka nikwambie na miaka yako?" Sauti ya kwenye simu ilimaliza kwa swali.

"Mmmmh" Alex aliguna. " Wewe ni nani lakini?" Alex aliuliza tena.

"Utanijua kesho. Fanya nilichokuagiza. Sijataka kukwambia kwamba usipotekeleza hayo hutoliona giza la kesho. Nitakuua saa kumi kamili jioni. Kama unabisha, we bisha tu"

"Kaka, inamaana..." Alex alitaka kuongea. Ndipo alipogundua alikuwa anaongea peke yake simuni. Jamaa alikuwa amekata simu.

Alex aliamka. Alikaa kitandani akiwa haelewi kabisa ni balaa gani linamkuta. Aliwaza na kuwazua.

"Huyu jamaa ni nani? Anajua kila kitu kuhusu mimi. Amejua mpaka hii bukta niliyovaa. Haya ni mambo ya ajabu sana. Eti niende posta kesho kwenye jengo gani sijui, ni nani yule? Kwanini anipe mimi maagizo hayo?" Alex alikuwa anajiuliza mwenyewe.

Mara alisikia mlio katika simu yake. Ulikuwa mlio wa meseji. Alichukua simu yake na kuisoma ile meseji.

"Saa nne kamili asubuhi, mbele ya jengo la RITA. Usimuulize chochote atakayekupa briefcase. Chukua na utapigiwa simu ya maelekezo. Kuwa makini ili ulione giza la kesho"

Hadi anamaliza kuisoma hiyo meseji mwili mzima ulikuwa umeloa jasho. Ilikuwa ni meseji fupi lakini yenye ujumbe uliomtia hofu sana.

Hivi ndivyo simulizi hii inavyoanza, tuwe wote katika sehemu ijayo..
 
Saf sana
 
Naomba utuweke Wapi Mkuu kama unakuja kutupa adhabu bora tujue tuache Kusoma maana kule kwa binunu pamenuna halafu tena tuje kwa Alex hivi utatumudu Mkuu?
 
RIWAYA; BRIEFCASE
MTUNZI; HALFANI SUDY
Mawasiliano 0674 395733

Sehemu Ya Pili

"Saa nne kamili asubuhi, mbele ya jengo la RITA. Usimuulize chochote atakayekupa briefcase. Chukua na utapigiwa simu ya maelekezo. Kuwa makini ili ulione giza la kesho"

Hadi anamaliza kuisoma hiyo meseji mwili mzima ulikuwa umeloa jasho. Ilikuwa ni meseji fupi lakini yenye ujumbe uliomtia hofu sana.

Alex hakupata usingizi hata chembe. Kila akiwaza sauti ya yule jamaa alikuwa anajawa na hofu. Hadi saa kumi na moja alfajiri bado alikuwa macho. Saa kumi na mbili asubuhi alijiandaa na kuelekea Posta kwenye ghorofa la RITA. Njiani, Alex akiwa ndani ya daladala alikuwa na mawazo lukuki. Alifikiria mwisho wa safari ile ya kufuata mzigo asioufahamu.

"Sijui kama nafanya kitu sahihi. Lakini nisipoenda ni hatari kwa maisha yangu, na je nikienda haiwezi pia kuwa hatari kwa maisha yangu?" Alex aliwaza akiwa garini.

Saa mbili kamili asubuhi daladala alilopanda Alex lilifika Posta, lilichelewa kutokana na foleni. Alianza kuulizia kwa watu eneo lilipo jengo la RITA, alielekezwa. Hadi anafika katika jengo la RITA ilikuwa saa mbili na nusu asubuhi. Saa moja na nusu kabla ya muda aliotakiwa awe pale.

Watu walikuwa wanamiminika katika jengo hilo la RITA, huyu anaingia, yule anatoka. Hakutaka kujua mengi, alibaki amesimama tu pale mbele.

Saa nne kamili juu ya alama, ndipo alistukia anaguswa bega, aligeuka kwa fadhaa huku sura yake ukionesha woga usiomithilika. Alikutana na kijana barobaro mwenye kupata umri kama wa miaka thelathini na mitatu. Alikuwa amevaa shati la bluu, katika mfuko wa shati lake kulikuwa na maandishi ya bluu yaliyoandikwa RITA. Chini alivaa suruali safi nyeusi iliyonyooshwa vizuri. Mkononi alikuwa ameshika briefcase!!

Kijana alimkabidhi Alex ile briefcase bila kuongea neno lolote lile. Kisha akaelekea katika jengo lile la RITA. Alex sasa alikuwa na briefcase mkononi, mkono wenye kutetemeka dhahiri shahiri. Ghafla, simu yake ya mkononi iliita. Aliitoa ile simu mfukoni, ilikuwa namba ileile iliyompigia jana saa sita usiku.

"Kazi nzuri Alex. Umeifanya hatua ya kwanza kwa ufanisi mkubwa sana. Sasa ni hatua ya pili ya kazi hii. Mbele yako kuna gari nyekundu, imeshusha kioo kimoja cha mbele, funguo mlango wa nyuma na ingia humo. Sharti ni lilelile, usiongee chochote kile na mtu utakayemkuta ndani ya gari hiyo, maelezo yote utapewa na mimi. Na kweli, Alex aliangalia mbele yake, maelezo yote aliyoelezwa simuni yalikuwa vilevile. Alipiga hatua za kinyonge mbele na kuelekea katika gari nyekundu. Hakuuliza, alifungua mlango wa nyuma wa gari lile na kukaa, briefcase yake akiwa kaipakata. Alipokaa tu dereva alipandisha kioo na gari kutia moto. Dereva wa gari alikuwa ni mzee kidogo. Alitulia katika usukani na kumpeleka Alex mahali kusipojulikana, hakuna aliyethubutu kuongea ndani ya gari. Safari ile iliishia katika jumba moja ambalo Alex hakujua lipo maeneo. Geti kubwa lilifunguliwa na gari lile kujitosa ndani yake. Hiyo ilikuwa saa sita kamili mchana.

Kijana mmoja alikuja kumfungulia mlango Alex. Alex alitoka nje akiwa kaishikilia ile briefcase mkononi. Sura yake, mwendo wake vikiashiria woga mkuu, huku moyo wake ukimdunda isivyo kawaida. Alijiona na mwenye mkosi kuliko mtu yeyote yule hapa duniani. Walienda hadi kwenye sebule ndogo iliyokuwemo mle ndani. Walimkuta mwanamme mmoja tu akiwa amekaa sofani.

"Karibuni sana" yule mwanaume alisema. " Hongereni sana kwa kufikisha mzigo salama. Uweke hapo juu ya meza. John, utamrudisha Alex palepale ulipomtoa. Hamruhusiwi kuongea chochote kile garini. Kama kuna mtu hataki kuliona giza la leo ajaribu kukaidi amri hiyo" Jamaa alisema kwa sauti ya kumaanisha.

Saa mbili baadae Alex alishushwa katika jengo la RITA. Na lile gari jekundu kutokomea. Alex alielekea stendi na kupanda gari lililompeleka Mbagala. Ndani ya daladala alitulia tuli katika kiti, akiwa na maswali lukuki juu ya watu wale, lakini, hakukuwa na wa kumjibu.

Je nini kitatokea, tuwe wote katika sehemu ijayo
 
RIWAYA; BRIEFCASE
MTUNZI; HALFANI SUDY
SIMU; 0674 395733

Sehemu Ya Tatu

Ilikuwa imepita miezi mitatu tangu litokee lile tukio katika jengo la RITA. Alex aliendelea na biashara zake za kuuza viatu bila ya bughudha yoyote ile. Hakupigiwa tena wala kutumiwa meseji tena na ile namba. Aliendelea na maisha yake akiwa anaishi palepale, katika nyumba ya kupanga Mbagala maji matitu. Pamoja na kupita muda mrefu bila kupigiwa tena na yule mtu, lakini ndani ya kichwa chake alilikumbuka lile tukio kila saa. Maswali juu ya wale watu ni wakina nani? Wanafanya nini mjini? Waliipata vipi namba yake na maelezo binafsi kuhusu yeye? Yalikuwa yanamgonga mara kadhaa. Na swali kubwa zaidi, ndani ya ile briefcase kulikuwa na nini?. Mara kadhaa alipuuzia maswali hayo kwa kujionya mwenyewe asifuatilie mambo yasiyomuhusu. Na kweli, hakuthubutu kufatilia wala kumsimulia mtu yeyote yule.

***

Jumatano moja, Alex alikuwa sokoni Tandika akinadi viatu vyake kadhaa kwa makelele. Kulikuwa na umati wa watu wakionunua bidhaa mbalimbali. Simu yake iliita. Alex aliitoa simu yake na kupokea.

"Nambie bosi wangu" Alex alianza simuni.

"Poa Alex. Sasa nilikuwa nahitaji ule. Ila kwa sasa nipo Posta na nina ratiba ya kwenda mkoani leo hivyo sitorudi nyumbani. Kama inawezekana nilitee mzigo wangu huku, nitakurejeshea nauli yako"

"Haina shida bosi, nakuletea sasahivi. Nikifika Posta utanielekeza mahali ofisi yako ilipo" Alex alisema.

"Sawa haina shida, tutawasiliana" Jamaa alijibu.

"Leo nina bahati sana. Asubuhi yote hii nauza pea tano za viatu kwa mkupuo. Nyota njema huonekana asubuhi, bila shaka leo itakuwa siku njema sana kwangu" Alex aliwaza akiwa ndani ya daladala.

Dakika hamsini na tano baadae Alex alikuwa Posta. Akampigia simu mahali ofisi yake ilipo, alielekea huko.
Alikutana nae, na kukabidhi vile viatu. Alex alivuna shilingi laki moja na elfu Ishirini. Mauzo makubwa sana kwa asubuhi ile. Akatoka ndani ya ofisi ya yule jamaa ili aelekee Tandika kuendelea na biashara, alipotoka tu nje alikumbuka kitu.
Jengo la RITA.

"Hivi kwanini nisiende jengo la RITA ili angalau nijue wanahusiana na nini?" Nguvu za hisia za kibinadamu zilimvuta Alex. Bila kufikiria mara mbili alipiga hatua kuelekea katika jengo la RITA. Hatua chache sana kutoka katika ofisi ya yule mteja wake. Kila hatua akiyopiga kuelekea katika jengo la RITA mapigo ya moyo wake yalipiga maradufu. Ndani ya akili yake mambo yote yaliyotokea miezi mitatu iliyopita yalipita taratibu katika kichwa chake. Nguvu ya udadisi ilikuwa inashindana na woga. Lakini miguu iliendelea kupiga hatua kuelekea katika jengo la RITA. Alifika hadi mlangoni.

"Kitambulisho, tunahitaji kitambulisho" Mlinzi aliyekuwa pale mlangoni alisema. Bila kusita, Alex alitoa kitambulisho na kumuonesha yule mlinzi. Mlinzi alikichukua kile kitambulisho, alikiangalia na kumwangalia Alex usoni. Alimruhusu.

"Hili jengo linahusu nini? Wanaangalia kitambulisho na kukuruhusu kuingia bila kukuuliza unaenda kufanya nini?" Alex alijiuliza wakati akipanda ngazi kuelekea ghorofa la kwanza.

Alifika ghorofa la kwanza, akaufuata mlango uliokuwa upande wa kulia. Akaingia katika chumba kipanda kilichokuwa wazi, alikutana na ummati wa watu ukiwa katika foleni. Alex alisogea kwenye meza moja ambapo kulikuwa na madada wawili wakijaza fomu.

"Samahani dada yangu hii ofisi inahusika na nini?"

Yule dada alimwangalia Alex kwa mshangao. Anaingia vipi ofisi asiyoijua inahusika na nini?

"Hapa ni RITA, ofisi inayotoa vyeti vya kuzaliwa na vifo" Dada alimjibu huku akiendelea kujaza fomu yake.

Alex aliangalia mbele, ndipo alipowaona wafanyakazi watatu wakiwa wamevaa mashati mithili ya aliyovaa yule jamaa aliyemkabidhi briefcase miezi mitatu iliyopita. Alex aliwasogelea wale watu huku akiwa na matumaini ya kumwona yule jamaa. Hakumwona.
Alizidi kwenda mbele ya ile foleni. Aliwaona wafanyakazi wawili wengine wakiwa wamekaa kwenye benchi wakiwa wamevaa mashati aina ileile. Yote, juu ya mfuko yalikuwa yameandikwa RITA. Alipoziangalia sura zao, hakuna iliyofanana na ya yule jamaa. Akaona anapoteza muda.

"Hii ni sare ya wafanyakazi wa hapa. Sijui kama nitamwona yule jamaa. Sura yake naikumbuka ila sijui atakuwa wapi? Ngoja nishuke tu niende kibaruani"

Alex alitoka nje ya ile ofisi. Aliifata njia iliyompeleka katika ngazi za kushuka chini. Alipotaka kukanyaga ngazi tu wazo lilimjia kichwani mwake.

"Kwanini nisiende kuchunguza na ofisi za juu. Pengine nitakutana naye yule jamaa" Alex aliwaza tofauti. Akabadilisha uelekeo na kuzifuata ngazi zilizokuwa zinaelekea juu ya jengo lile.

Alikuwa njiani akipanda ngazi. Huku akili yake ikifikiria kama alikuwa sahihi ama alikuwa anakosea kwa lile jambo alilokuwa analifanya. Hali ya uwoga wa kibinadamu bado ikiendelea kumtawala ndani ya moyo wake. Alifika ghorofa ya tatu, mkono wa kushoto aliona ofisi na mlinzi mmoja mlangoni.

"Fomu za RITA zinaletwa humu" Mlinzi alikuwa anawaambia wakina dada watatu waliokuwa wamesimama pale nje. Alex akaona hatakubaliwa kuingia mle kwakuwa hakuwa na fomu yoyote mkononi. Aliamua kupandisha juu kuelekea ghorofa ya nne. Akiwa anapandisha kwenye ngazi akiwa na mawazo lukuki, ghafla alipamiwa na mtu aliyekuwa anashuka kwa kasi. Jamaa alibabaika na briefcase aliyokuwa ameishika ilimtoka mkononi.

"Samahani.." Alisema kwa sauti ya woga.

"Bila samahani" Alex alijibu huku akimwangalia yule mtu aliyefadhahika hasa.

Jamaa aliokota briefcase yake na kushuka chini. Alex alimwangalia kwa nyuma yule mtu, alikuwa amevaa shati la bluu na suruali nyeusi. Kama za yule jamaa aliyekutana naye miezi mitatu iliyopita. Macho yake yakatua tena kwenye ile briefcase.

"Siye yeye lakini ni wao" Alex alijisemea mwenyewe kwa sauti ndogo. Alibaki amepigwa na butwaa pale katikati ya ngazi kwa dakika tatu. Ghafla akili zilimrejea, alipanda juu harakaharaka, akafika katika ghorofa ya nne. Alielekea mbele moja kwa moja, akiitafuta sehemu ambayo ingemuwezesha kuona kule chini. Alipapata. Jicho lake la kwanza tu kuangalia kule chini, aliliona gari jekundu ikiwa imepaki mahali palepale pa siku ile huku kioo cha dirisha moja likiwa limeshushwa. Moyo ulimripuka!
Alex akaangalia sehemu ya mlango wa kutoka katika jengo lile, ndipo alipomwona yule jamaa aliyepamiana nae kwenye ngazi, akimkabidhi mtu ile briefcase. Mithili ya yeye alivyokabidhiwa miezi mitatu iliyopita. Hawakuongea. Wakati jamaa aliyepamiana nae akirudi ndani ya jengo la RITA, yule kijana alielekea moja kwa moja katika gari nyekundu. Aliingia katika mlango wa nyuma, na dakika ileile gari liliondoka.

Kutokana na sehemu na urefu wa maghorofa mengine yalimzuia kuona gari lile lilikuwa linaelekea wapi. Alex alibaki amesimama mahali palepale huku akitafakari maana ya tukio lile. Alex alishuka chini kwa kupitia zile ngazi. Alifika mahali palepale alipogumiana na yule jamaa. Aliona kitambulisho kikiwa kimedondoka. Akajua kitambulisho cha yule jamaa, alikiokota na bila kukiangalia alikitia mfukoni. Na kuendelea kushuka chini. Hadi anafika kule chini kabisa, hakubahatika kukutana na yule jamaa.

"Nina kitambulisho chake, bila shaka nitajua namna gani ya kumpata. Hiki kitambulisho ndio njia itakayonipeleka kuwajua watu hawa ni wakina nani?" Alisema huku akijipapasa mfukoni.

Alex alienda stendi na kupanda gari iliyompeleka kibaruani kwake, Tandika. Hadi anafika Tandika, ilikuwa ni saa nne na dakika hamsini asubuhi. Kwa makadirio yake, akahisi kile kitendo kilifanyika saa nne asubuhi. Muda uleule wa miezi mitatu iliyopita. Aliendelea kufanya biashara hadi jioni.

***

Saa moja kamili usiku, Alex ndio alikuwa ndani ya daladala akielekea Mbagala. Akiwa ndani ya gari bado mawazo na akili zake zilikuwa katika jengo la RITA. Bado matukio yale yalimuumiza sana kichwa.

"Wale ni kina nani?" Alex alijiuliza huku akikitoa kile kitambulisho mfukoni. Alikishika mkononi akikiangalia.

'James Luganda' Ndio jina lililosomeka katika kitambulisho kile cha kura na sura ilikuwa ya jamaa yuleyule aliyepamiana nae kwenye ngazi. Akasoma pamoja na maelezo mengine ya yule mtu aitwaye James Luganda. Kisha alikirejesha kile kitambulisho mfukoni.

Dakika ishirini baadae, gari lilifika Mbagala rangitatu. Alex aliangalia saa yake, ilimwambia ni saa moja na dakika ishirini.

"Ni mapema sana kwenda nyumbani sasahivi. Ngoja nikamjue huyu James Luganda ni nani?" Alex aliwaza huku akirudi kwa miguu Mbagala Zakheim. Alipita ukumbi Dar live, alitembea kidogo na kupita sheli. Upande wake wa kushoto kulikuwa na frem kadhaa. Alitembea huku akiiangalia kila frem, ndipo alipoiona. Ilikuwa ni 'stationery' ndogo ambapo kulikuwa na huduma za 'Internet'. Alex alijitosa ndani ya 'stationery' hiyo.

"Saa moja bei gani?" Alex alimuuliza dada aliyemkuta mle ndani.

"Ni shilingi elfu moja kaka yangu, nusu saa ni mia tano" Yule dada alijibu huku akimwangalia Alex.

"Niwekee saa moja" Alex alisema huku akikaa kwenye kiti kilichokuwa mbele ya kompyuta.

Yule dada mwembamba mrefu alisogea pale kwenye kompyuta aliyokuwa amekaa Alex na kuweka muda atakaotumia Alex kwenye ile kompyuta.

"Karibu sana kaka" dada yule alisema huku akiondoka.

"Ahsante" Alex alisema huku akishika kipanya cha kompyuta. Moja kwa moja aliingia kwenye akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa Facebook. Alipofanikiwa, alienda kwenye sehemu palipoandikwa 'search' akaandika jina, James Luganda. Kisha akaacha ijisachi.
Walitokea watu wawili wenye jina hilo. Mmoja aliweka picha katika akaunti yake, huku mwengine akiwa hajaweka 'profile picture'. Hakupata wasiwasi wowote, yule aliyeweka picha ndiye alikuwa James Luganda akiyemtafuta.
Alifungua na kuanza kusoma habari zake.

**SURA YA PILI**

JAMES LUGANDA ni kijana mwenye umri wa miaka ishirini na minane. Ni mtoto wa kwanza katika familia ya mzee Luganda yenye watoto wawili iliyokuwa inaishi katika kijiji cha Vikindu. James alisoma elimu yake ya shule ya msingi Vikindu na baadae kuchaguliwa shule ya Sekondari Pugu. Baadae alichaguliwa kuendelea na kidato cha tano na cha sita ambavyo alisoma katika shule ya Sekondari ya Tosamaganga huko mkoani Iringa.

Baada ya kumaliza kidato cha sita James alisoma shahada ya kwanza ya uhasibu cha TIA tawi la Mbeya na kutunukiwa shahada hiyo. Kwasasa James alikuwa ni mhasibu katika kampuni ya usafirishaji iliyokuwa inapeleka mizigo sehemu mbalimbali nchini na nje ya nchi.

Siku moja akiwa kazini kwake alipokea mgeni. Mgeni aliyejitambulisha kwa jina la Fred Kabanda.

"Bila shaka naongea na James Luganda. Mhasibu katika kampuni ya usafirishaji ya A & B. Mimi ninaitwa Fred Kabanda, afisa utumishi katika kampuni ya roho mbaya" Fred alisema bila wasiwasi wowote akiwa mbele ya James.

"Roho mbaya? Kampuni yenu inajihusisha na nini? Na na kwanini mkaiita roho mbaya?" James alihoji huku akimwangalia kwa umakini yule mtu.

"Ndio roho mbaya" Fred alijibu huku akikaa vizuri kitini. Swali la kampuni yetu inajihusisha na nini sitolijibu. Swali la kwanini kampuni yetu ikaitwa roho mbaya nitakujibu..ni rahisi tu, ni kwakuwa kampuni yetu imeajiri watu wenye roho mbaya, ili wafanye kazi ya roho mbaya, na bosi wetu ana roho mbaya ile mbaya. Sasa, huyo bosi mwenye roho mbaya ndiye kanituma mimi kwako " Fred alisema kwa kujiamini.

"Mmekosea njia, mmekuja kwa mtu asiye na roho mbaya. Hukukosea jina langu, naitwa James Luganda, lakini ulikosea kwa kuwa hukumalizia, ni mlokole safi mwenye imani isiyotetereka" James Luganda alisema.

"Nafaham James Luganda ni mlokole. Aliyeingia katika ulokole miaka saba iliyopita baada ya kumuua mwanadada Veronika Mushi. Kwahiyo James kwasasa ni mlokole safi baada ya kuwa mhalifu safi kabla ya hiyo miaka saba. Waswahili wanasema asili haipotei, na ni kweli asili kamwe haijawahi kupotea. Kama wewe una asili ya uzinzi wewe ni mzinzi tu, kama una asili ya wizi wewe ni mwizi tu, na kama una asili ya uuaji wewe ni muuaji tu. Damu ya uuaji haitoki, damu ya Veronika Mushi haitotoka kamwe mwilini mwako. Labda utajidai umebadilika, basi kama umebadilika nasi tutakubadilisha na kukufanya mlokole mwenye roho mbaya!" Fred alisema kwa kirefu wakati James woga dhahiri ukineemeka usoni mwake. Katika yote watakayoyazungumza pale hili la Veronika Mushi hakulitegemea katu.

"Naona upo kimya bwana James Luganda. Ngoja nikwambie dhumuni langu la kuwa mbele yako kisha niondoke. Ninaweza nikarejea tena ama nisirejee, inategemea na wewe ufanisi wako katika jambo hili. Ni hivi, wewe ni kati ya watu watano mlioajiriwa katika kampuni ya Roho mbaya. Na baada ya kuondoka kwangu tu andika barua ya kujiuzuru hii kazi yako ya uhasibu hapa A & B"

"Haiwezekani, haiwezekani" James alikataa.

"Inawezekana na itawezekana. Kesho asubuhi njoo katika jengo la RITA ofisi namba 105 saa mbili asubuhi kuyajua majukumu yako mapya" Fred alisema huku akinyanyuka.

"Na nisipokuja?" James Luganda aliuliza.

"Sikwambii utauwawa kwa mateso makali sana. Nakwambia picha zako wakati ukiufukia mwili wa Veronica Mushi kule Mabwepande zitakuwa juu ya magazeti ya kesho, unajua nini kitafuatia baada ya hapo..." Fred aliachia kauli hewani na kutoka nje. Akimwacha James Luganda akibubujikwa na jasho. Alikuwa amepatikana.

***

Siku moja baadae James alijiunga katika kampuni ya Roho mbaya, na kazi yake kuu ni kila siku kumkabidhi mtu mmoja briefcase ambayo hakuna aliyekuwa anajua kuna nini ndani yake. Kazi iliyomlipa vizuri sana mara tano ya ile ya awali.

Baada ya miezi sita James alihama Vikindu kwa wazazi wake na kuhamia Bunju mahali ambapo alipanga nyumba nzima. Maisha yake yalibadilika haraka sana, alipata pesa nyingi sana, na alijua kuzitumia pesa. Lakini siku zote alibaki na maswali mawili kichwani mwake, zile briefcase zilikuwa zina nini ndani yake? Na watu wale walimpigaje picha wakati anamfukia Veronica Mushi kule Mabwepande?.

***

"Nimepata kila kitu hapa" Alex alisema. "Kumbe haikuwa na haja ya kuja hapa. Kilekile kitambulisho kilimaliza kila kitu. Jamaa anaitwa James Luganda, kwa mujibu wa kitambulisho alijiandikishia katika serikali ya mtaa katika kijiji cha Vikindu. Nilichokipata katika Facebook ni jamaa alikuwa ni mpenzi wake, Veronica Mushi ambaye kwa jinsi alivyoandika alifariki ghafla. Na mwili wake kupotea hadi leo. Veronika Mushi, alikuwa mrembo wa viwango vya kimataifa" Alex alikuwa anaongea peke yake.

Alifika nyumbani kwake saa nne na dakika tano usiku baada ya kupitia kwa mama lishe alipokula chakula. Alikuwa amechoka mwili, amechoka akili, alifika na kujilaza kitandani, usingizi ulimpitia palepale.

Aliamka saa moja kasoro asubuhi. Alienda bafuni kuoga, kisha alirejea ndani na kuvaa suruali yake ya jeans ya bluu mpauko na t-shirt nyeusi iliyoandikwa Nike kifuani. Chini alivaa raba nyeupe. Alihamisha zile hela laki moja na ishirini kutoka suruali aliyovaa jana yake na kuziweka katika hii suruali aliyovaa sasa pamoja na kitambulisho alichokiokota jana. Alitoka nje, safari yake ilimfikisha Mbagara rangi tatu, alienda katika banda moja na kupata kifungua kinywa. Sasa alijisikia yupo vizuri. Alienda stendi na kupanda gari iliyokuwa inaelekea Vikindu. Nyumbani kwa James Luganda.

Haikuwa safari ndefu. Saa mbili na dakika kumi alifika Vikindu getini. Alisimama wakati akifikiria aanzie wapi kumtafuta James Luganda. Alex alitumia dakika tano kuzungukazunguka pale stendi, akimtafuta mtu angalau mwenye kuonekana mwenyeji wa eneo lile, hakumwona. Alipoangalia, akakumbuka kitu.

Je nini kitatokea? Tuwe wote katika sehemu ijayo
 
Mkuu story yako insonesha Ni Nzur ila unatoa vpande vifup sana ongeza ongeza iwe ndefu
 
Naomba utuweke Wapi Mkuu kama unakuja kutupa adhabu bora tujue tuache Kusoma maana kule kwa binunu pamenuna halafu tena tuje kwa Alex hivi utatumudu Mkuu?
Wala usiwe na hofu mkuu tutasoma tu zote kwakuwa nina ruhusa ya MTUNZI mwenyewe..
 
Back
Top Bottom