Riwaya: Janga

Dam55

JF-Expert Member
Oct 8, 2015
5,592
11,831
RIWAYA: JANGA
MTUNZI: richard MWAMBE

SEEMU YA 1
I
Saa 5: 7usiku…

DAR ES SALAAM

MVUA ILIYOAMBATANA NA RADI iliendelea kunyesha kwa hasira katika jiji la Dar es salaam, hakukuwa na nyota hata moja iliyong’aa siku hiyo wala mbalamwezi yenye nguvu ya kulishinda wingu zito lililofunga anga la jiji hilo.

Kila mmoja alijifungia ndani ya nyumba yake, kimya, akisikiliza sauti kali za radi na mng’ao mkali wa radi uliongaza ndani na kufukuza giza nene lililovijaza vyumba vya nyumba hizo. Michoro ya kutisha ilionekana angani kana kwamba mbingu ilikuwa ikipasuka, hofu.

“Ngrrrrrrrrrr! Ngrrrrrrrrrrr! Ngrrrrrrrrrr!” kelele ya simu ilisikika katika nyumba moja kubwa ya iliyo kandokando tu mwa barabara na kumkurupusha mwenyenayo toka kitandani, akaiendea meza ndogo na kuinyakuwa simu iliyokuwa ikifanya fujo hizo.

“Hallo!” akaita na kutulia akisubiri upande wa pili uongee. Badala ya kusikia jibu alihisi kupumua kwa nguvu kwa mtu aliye upande wa pili.

“Nilikuahidi kukupigia simu usiku huu kama unakumbuka, nimetimiza ahadi yangu. Nafikiri sasa utakuwa tayari kunisikiliza tofauti na mara zote nilizokuwa nikija ofisini kwako,” sauti ya upande wa pili ikaongea kwa kukwaruza.

“We ni nani? Na mbona unanifuatafuata sana? Nimeshakwambia sitaki na siwezi,” yule mmiliki wa nyumba ile akajibu.

“Sikiliza!” ile sauti ikaendelea kusema, “Huwa hatubahatishi katika kazi yetu, lakini inaonekana unataka kuwa kikwazo. Kwa nini unataka kufa masikini ilhali utajiri unakuja mpaka mlangoni kwako na unaukimbia?

Unataka mwisho wa siku umlaumu Mungu kuwa hakukupa? Acha ujinga! Hii ni nafasi yako ya mwisho,” ile sauti ikasema. Na yule jamaa akatulia na simu yake mkononi alipotupa jicho dirishani alishuhudia tu matone ya mvua yakigonga kioo cha dirisha na kugeuka kuwa michirizi mingi ya maji, hakuweza kuona taswira sahihi ya nje.

“Nisikilize…” akamwambia huyo wa upande wa pili, “kama ninyi mmezoea kufanya hayo, fanyeni na hao. Si kwamba sijui, najua vyema kuwa huo ni mchezo mliouzoea, mnaumiza wananchi kwa sababu ya pesa zenu, mnaua mamia ya watu kwa sababu ya uchu wenu wa utajiri, mnadhulumu na kupora haki ya wananchi kwa sababu yakutaka ufahari wa maisha…”

“E! E! E! E! umekuwa mhubiri siyo? Acha upumbavu, wewe ni mtu muhimu katika hili na unajua, sheria ya nchi katika hili iko juu yako ni kusema neno tu na roho zetu zitapona, unajifanya una shingo ngumu.

Hebu sogea dirishani, sogea kabisa,” ile sauti ilimwomba mwenye nyumba hiyo kusogea, akaitii na kulifikia lile dirisha kubwa la alluminium, “Fungua dirisha,” ile sauti ikamwambia naye akafungua na nje ya nyumba yake akakuta gari imeeegshwa, gari ya kisasa BMW 605 mpya kabisa hata haikuwa na namba bado.

“Umeona hiyo gari? Hiyo ni ya kwako na kesho unaweza kuichukua na kuitumia, nitakuelekeza wapi utapata namba zake,” ile sauti ikamwambia na yule bwana akabaki kapigwa butwaa, akatazama huku na huku hakuona mtu eneo lile, akili yake ikauma kujiuliza yuko wapi huyo anyeongea lakini hakumuona.

“Nimesema sitaki! Sitaki! Sitaki! Nitasimamia haki na haki ndiyo itaamua kila kitu katika hili…” akaongea kwa kelele huku akirudi katika ile meza ndogo.

“Sawa! Swala la mwisho usipokubali hili basi utakuwa umekubali lingine, nenda karibu na mlango wako wa kuingia sebuleni,” ile sauti ilimwamuru lingine, akasukuti na kuitii, akaufikia mlango… “ angalia chini, kuna nini … okota!”

Yule mwenye nyumba akaokota kitu kama broshua, akaigeuza geuza, sasa hiki ni nini? Akajiuliza, mbona sielewi, akahofu.

“Usijiulize, ila hapo una uchaguzi mmoja tu, unaona nini kwenye kurasa ya juu?” ile sauti ikauliza na yule jamaa akaitazama ile broshua ndogo, kulikuwa na picha ya nyumba nzuri , nyumba ya kisasa, nyumba iliyosheheni kila kitu.

“Itakuwa yako hiyo kesho tu ukikubali kutekeleza hili nilitakalo mimi…”

“Sitaki na nitahakikisha nakutia katika mkono wa sheria,” yule jamaa akaongea kwa ukali huku akirudi mahala pale palipokuwa na kile kitako cha simu.

“Basi, kama hutaki na hicho bila shaka umechagua kurasa ya pili, kwa heri,” ile sauti niliposema hayo tu simu ikakatika. Yule bwana akageuza nyuma ile broshua na kukuta picha mtu mwenye fuvu tupu aliyevalia kanzu jeusi na mikononi mwake kashikilia msalaba uliondikwa jina lake yaani la mmiliki wa nyumba hiyo. Hofu ikamwingia, mwili ukamtetema, macho yake yapepesa kama mtu anayetaka kuona kitu kisichoonekana.

Wazo likamjia kupiga simu polisi, alipobofya ile simu na kuweka sikioni hakusikia chochote, simu haifanyi kazi, akakimbilia ile ya mkononi alipoiinua chaji imekwisha na wakati huo umeme umekatika, akabaki kabutwaika huku sura yake ikisawajika kwa mawazo.

Mchoro wa kutisha ukakatiza anga na mng’ao wake ukafanya mwanga mkali ulioangaza hata sisimizi yule ambaye yuko kwenye ardhi akitembea kwa tabu, kisha ukafuata muungurumo mkali na mzito wa radi uliotetemesha nyumba kwa sekunde kadhaa. Kisha mti mkubwa uliokuwa nje ya nyumba hiyo uling’oka na kuanguka na kufanya kishindo kikubwa.

Wazo lililomjia mwenye nyumba ni kutoka nje na kuangalia, maana ile gari aliyoooneshwa pale nje ilikuwa imeegeshwa eneo hilo ulipo huo mti. Itakuwaje kama gari ya watu imeangukiwa na mti? Akawaza huku hofu na mashaka vikimtawala, alipofungua mlango akatanabahi kutoikuta ile gari mahali pale.

Akiwa bado haelewi kinachotukia, akahisi mkono ukimshika begani.

“Eeeeeeeee! Nooooooo!” akapiga kelele na alipogeuka nyuma alikutana uso kwa uso na mke wake kipenzi Bi. Zuhura.

“Nini mume wangu, kimekupata nini? Mbona sikuelewi?” aliingiwa na mashaka na kumuuliza mumewe ambaye bado alikuwa ndani ya pajama.

“Aaaaaah! Aaaaaaah! Mke wangu, aaaaaah! Wanataka kuniua,” akalalama.

“Akina nani? Mbona hapa uko peke yako?” akauliza Bi. Zuhura.

“Siwajui mke wangu ila wanataka kuniua, toa taarifa polisi,” akaendelea kulalama.

Bi. Zuhura akakumbuka kuwa mumewe tangu utoto wake alikuwa na ndoto mbaya za kumfanya atoke chumbani na kutembea peke yake usiku wa manane nje ya nyumba yao, tatizo hili aliambiwa kuwa limekwisha baada ya mumewe huyo kufanyiwa dawa za kienyeji za kwao Tanga lakini akashangaa leo hii kwa mara ya kwanza tangu aoelewe naye anakutana na haya. Atakuwa amerudia ndoto zake za utotoni, akawaza na kumshika mkono mumewe.

“Twende tukalale mume wangu” akamwambia.

“Nimekwambia toa taarifa polisi kuna watu wanataka kuniua,”

“Nitatoa mume wangu subiri pakikucha,” Bi. Zuhura akajibu huku akimkokota mumewe mpaka kitandani na kumliwaza kwa mahaba mazito ili kumsahaulisha masaibu hayo ya ndoto aliyokuwa akiota.

SIKU ILIYOFUATA
JUA TAMU LA ASUBUHI lilipenya kwenye mapazia mazuri ya nyumba ya Jaji Shekibindu na mkewe Bi. Zuhura. Mvua ilikatika usiku wa manane na kuacha mito ya maji ya asili ambayo ilisahaulika na wakazi wa mji huu ikitiririka kuelekea baharini. Ilikuwa ni adha, adha kubwa isiyo kifani. Nje ya dirisha hilo Bi. Zuhura aliweza kuona watu wakitembea viatu mkononi, magari yakiwa yamekwama kwenye madimbwi makubwa ya maji, maduka yakiwa bado hata kufunguliwa.

Akatazama saa ya ukutani, ilikuwa saa moja na nusu ya asubuhi, akarudisha macho kwa mumewe, akakuta bado anakoroma akiwa katikati ya usingizi mzito. Polepole akamwamsha na mtu mzima huyo akaamka pasi na pingamizi lolote.

ITAENDELEA
 
RIWAYA; JANGA
MTUNZI: Richard MWAMBE
SEHEMU YA 2

ILIPOISHIA
Akatazama saa ya ukutani, ilikuwa saa moja na nusu ya asubuhi, akarudisha macho kwa mumewe, akakuta bado anakoroma akiwa katikati ya usingizi mzito. Polepole akamwamsha na mtu mzima huyo akaamka pasi na pingamizi lolote.

Endelea…

“Kumekucha mume wangu, uamke, kazini je?” akamwambia.

“Aaaaaaahhhhhhnnnnnnnn!” Shekibindu akapiga mwayo na kujinyoosha huku akijivuta pembeni mwa kitanda na kuyatwaa makubazi yake kabla ya kuingia maliwato. Dakika ishirini baadae alikuwa tayari ndani ya suti yake safi, nyeusi, iliyotanguliwa na shati jeupe na tai ndefu ilimfanya aonekane nadhifu. Bi. Zuhura alikuwa tayari keshaandaa chai nzito pale mezani, supu ya kuku wa kienyeji iliyochanganywa na viazi mviringo na pilipili hoho ndani yake, pembeni kukiwa na pilipili mbuzi na vipande vya limao.

“Jana umeota ndoto mbaya sana mume wangu, pole!” akamwambia. Shekibindu akamtazama usoni mkewe kisha akendelea kula, “Naona zile ndoto zako sijui zimekurudia tena!” akaongea kwa shaka.

“Sio ndoto mke wangu, ilikuwa kweli, jana nimepata simu mbaya sana usiku ule, lakioni kinachoshangaza mambo yote niliyoonesha hapa sasa siyaoni, kulikuwa na gari hapo kwenye huo mti uliodondoka lakini silioni limeondoka saa ngapi,” Shekibindu akamjibu.
“Ndiyo maana nakwambia ni ndoto tu hiyo! Itabidi tufanye dawa zile ulizoniambia,” akashauri mkewe na Jaji huyo akatikisa kichwa juu chini bila kuongea lolote.

Kengele ya mlango ikalia, tayari dereva alikuwa amewasili kumchukua mzee huyo kwenda kwenye majukumu ya kulijenga taifa.

SIKU HIYO HIYO
MGAHAWA WA HARD-ROCK
DAR ES SALAAM
“Kwa hiyo tunafanyaje katika hilo? Jamaa amekuwa mgumu kwelikweli,” kijana mmoja mwenye asili ya Kiasia alimwambia mtu wa pili aliyekuwa naye mezani hapo wakipata kahawa.

“Ana shingo ngumu, anajifanya anaijua sheria? Basi sisi ndiyo tupo juu ya sheria hiyo,” yule bwana mwenye tumbo kubwa na mashavu mapana yaliyojaa nyama za kutosha alijibu. Kikao hicho cha watu wawili kilifanyika asubuhi ya siku ileile iliyotanguliwa na mvua kubwa usiku. Haikuwa kawaida kwa kibopa kama huyu kuja kufanya mkutano au kukutana na mtu eneo kama hilo na hii ilitokana na hadhi na wadhifa wake serikalini. Alikuwa mnene, mwenye pesa, amekaa serikalini tangu enzi za Mwalimu.

Ilikuwa ngumu kujua kama wananchi wa jimbo lake la ubunge wameshindwa kumpigia kura ya ‘hapana’ ili asiendelee au amewapumbaza kwa namna moja au nyingine nao wakasema ‘ndiyo’ kwa kauli moja? Hakuna aliyekuwa na jibu la swali hilo, kila mtu alibaki kutazama na kulaumu tu.

Alikuwa akimiliki majumba makubwa makubwa au tungeita ‘estates’ nyingi tu ndani na nje ya jiji la Dar es salaam. Alikuwa na magari ya kutosha familia yake yote ilielimikia ughaibuni, hakuwa na shida kama yako, shida yake yeye ilikuwa ni pesa nyingi na mawazo yake yalikuwa ni jinsi ya kuzitumia. Hakuna Changudoa aliyekuwa hajawahi kulala naye katika miji mikubwa ya Afrika Mashariki, wanafunzi wengi wa vyuo walimjua kibopa huyu na walimfaidi sana kila aingiapo bungeni huko Dodoma.

Pamoja na yote hayo, hakutosheka na pesa hasilani, kila siku alitaka kukwapua nyingi zaidi, biashara zake haramu zilizipita hata zile halali, lakini si polisi wala mgambo aliyethubutu kuinua pua yake kusema lolote baya juu yake. Shule kadha wa kadha za kisasa zilimilikiwa naye, hoteli chungu mbovu na kampuni za kitalii zilikuwa mali yake. Alikuwa na uwezo wa kufanya lolote alilotaka kwa maana pesa ziliongea.

“Sikia Ngishu! Katika nchi hii, asikudanganye mtu sheria inauzwa na haki inanunuliwa kama yeye hajui hilo basi ataona kile alichojichagulia, nahitaji ufanye kazi hiyo mapema, kumbuka keshokutwa ni hukumu ya kesi hii, siwezi kupoteza mamilioni ya pesa huku nayaona,” yule Mheshimiwa alimaliza sentensi hiyo na kujiweka vizuri katika kiti ambacho kilionekana kupata shida ya kumbeba ila kilishindwa tu kusema kwa kuwa hakikupewa uwezo huo.

Nusu saa baadae waliagana na kila mmoja akashika njia yake, huyu kibopa akaingia kwenye ndinga yake iliyokuwa ikipepea bendera ya taifa na kukata mitaa kuelekea eneo lingine ambalo nalo halikuwa eneo la kazi yake aliyopewa na serikali.

Ilikuwa hoteli kubwa yenye hadhi ya nyota tano, alimwacha dereva wake garini akisoma magazeti na yeye akaingia ndani ya hoteli hiyo ya kifahari ambayo huingiwa aghalabu na watu wenye fahari zao kama huyu. Katika moja ya chumba cha mikutano nyeti kulikuwa na watu wengine watatu waliokuwa wameketi wakimsubiri kwa shauku.

“Vipi?” wa kwanza akauliza.

“Nasikia amegoma kabisa, hasikii chochote na kasema ataisimamia sheria na kuhakikisha inafanya kazi kusudiwa,” yule Kibopa akawaeleza wenzake. Ukimya wa sekunde kadhaa ukapita kati yao, hakuna aliyeongea.

“Ile ishu ni ya bilioni 500,” mwingine akadakia huku akiweka koti lake vyema, “Uhai wa mtu mmoja asiye na akili hauwezi kutufanya sisi tukose pesa hiyo iliyotakata,” akamaliza kusema huku akiinua bilauri yake na kupiga funda la maji.

“Lazima tucheze draft, mmoja analiwa na mwingine anaingia kingi,” yule kibopa akakandamizia hoja ya mjumbe wa kwanza.
2
HODI ILIBISHWA KATIKA ofisi ya Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Amana.

“Karibu, pita ndani,” akakaribisha. Yule mtu aliyegonga akaingia ndani ya ofisi hiyo, akaketi juu ya kiti alichooneshwa.

“Ndiyo, karibu sana, sijui nikusaidie nini?” yule Mganga akamwuliza huyo mgeni. Alikuwa ni kijana wa makamo, kati ya miaka thelathini na arobaini hivi, mkononi mwake alikuwa na mkoba wa ngozi wa wastani ambao kwa kuutazama tu haukuzidi kilo tano, sati la kahawia lilichomekewa ndani ya suruali nyeusi na mikanda iliyoibana suruali hiyo kwa mbele ilienda kutua upande wa nyuma na kuudhihirisha unadhifu wa kijana huyo. Macho maangavu yalitua usoni mwa Mganga huyo aliyekuwa akisubiri jibu la swali alilouliza.

“Naitwa Mustafa Bashiru, ni mwandishi wa habari kutoka gazeti moja binafsi linalotoka kila wiki,” akajitambulisha huku akimkabidhi kitambulisho cha kazi.

“Unatokea gazeti la Mbalamwezi?” akauliza yule mganga.

“Ndiyo mheshimiwa,”

“Mustafa Bashiru, nimekukumbuka, ndiyo wewe uliandika ile habari ya kuhusu meno ya tembo kukamatwa ughaibuni? Iliyopelekea wale waheshimiwa kuondolewa serikalini?” yule Mganga akaruhusu.

“Haswaaaaaa! Ndiyo mimi,” Mustafa akajibu.

“Sawa, karibu sana, nakusikiliza maana nyie waandishi ndiyo wambea wenyewe, lazima umenusanusa na kuona kuna cha kuandika, haya jimwage…”

“Aaaaaa usiseme hivyo, sisi kazi yetu ni kuihabarisha jamii juu ya habari mbalimbali za sasa na zile za uchunguzi. Nimekuja hapa kwa kuwa nimepata taarifa kuwa kuna akinamama watatu wamefariki hospitalini hapa kwa ugonjwa usioeleweka.

Inasemekana ugonjwa huu umewapata akina mama hao kwa nyakati tofauti na pia wapo wasichana wengine wawili ambao wanaumwa uo huo. Haja yangu ni kutaka uthibitisho kutoka kwako kama Mganga Mkuu wa hospitali hii…” yule mwandishi alimjulisha mwenyeji wake lililomleta.

“Unataka kwenda kuandika hilo?” akadakiza yule mganga.

“Ndiyo!”
“Mbona halina maana kwa kuwa hapa kila siku watu wanakufa, kwa nini akinamama hao wamekuvutia kwa vifo vyao? Labda mwenzangu una jingine ndani yake nijuze kwanza,” yule mganga akageuza swali kwa Mustafa.

“Huko nilikosikia habari hii inasemekana kuwa hawa marehemu walipata ugonjwa mbaya wa ngozi ambao uliziharibu ngozi zao kuanzia usoni na sehemu zingine za mwili, isitoshe inasemekana kuna kemikali zilizosababisha hali hiyo. Je hili liko sawa au…?”

“Ni kweli, akina mama hao wamekufa hivyo usemavyo, na uchunguzi wa ugonjwa huo unaendelea kufanyika, sampuli ya ngozi zao imekwenda kwa Mkemia Mkuu na tunasubiri majibu,” yule Mganga akajibu kwa ufasaha kabisa.

“Je; unaweza kufikiri kwa harakaharaka ni kitu gani kilichowasababishia tatizo hilo?” Mwandishi akazidi kuhoji.

“Siwezi yaani sina uhakika lakini labda vipodozi au aina fulani ya mafuta kwa kuwa akinamama hupenda kujipodoa mara nyingi,” akajibu.

“Asante sana, ni hayo tu Mheshimiwa,” Mustafa akashukuru na kuaga.

Mustafa alipotoka katika hospitali ile, moja kwa moja alielekea katika kituo kikuu cha polisi kwa minajiri ya kuonana na Mkuu wa kituo hicho. Kwa bahati mbaya hakumkuta lakini alisubiri kwa dakika kadhaa na Mkuu huyo alirudi na kuingia ofisini ambapo alipewa taarifa ya ugeni huo, naye bila kusitasita alimruhusu Musatafa kupita ndani.

Itifaki ya utambulisho ilifanyika kati yao na mazungumzo yakaendelea.

“Naitwa Mustafa kutoka gazeti la Mbalamwezi…”

“Gazeti la Mbalamwezi!” Yule afisa wa polisi akajibu huku akiandika kwenye kijitabu chake, kasha akainua uso wake.

“Karibu sijui nikusaidie nini?”

“Asante! Kuna vifo navifanyia uchunguzi, wanawake watatu wamefariki hospitalini kwa ugonjwa usiojulikana, na wengine wanaumwa uo huo, ninataka kujua je ninyi kama polisi mnataarifa ya vifo hivi vya utata?” akauliza.

Yule afisa, akashusha pumzi na kumtazama kijana huyo kwa jicho kali.

“Kuhusu vifo vya magonjwa, kaulize hospitali, hapa tunadili na usalama wa raia na mali zao. Umenielewa?” Yule afisa akauliza. Mustafa akabaki kimya kwa nukta kadhaa akimtazama.

“Sikia Mkuu, sijafanya kosa kuja kwako kwa kuwa, kama watu wanakufa kwa maradhi yasiyojulikana, inakuwaje ninyi msijue ilhali ndiyo wenye dhamana ya usalama wa raia?” swali hilo ikagonga kwa nguvu ngoma za masiki ya afisa huyo. Hakutabasamu, ila sura yake ilichukua muonekano mwingine wa kutisha kiasi fulani.

“Unanifundisha kazi?” akauliza.
“Hapana…”

“Sasa kwa nini unauliza maswali wakati majibu unayo?” wakatazamana, “Nenda, usiniharibie siku,” akangeza kusema kisha akainua simu upepo na kuendelea kuongea na vijana wake kutoka sehemu mbalimbali.

Mustafa alitoka katika afisi ile huku kichwani akiwa na maswali lukuki ambayo hayakupata majibu. Akiwa nukta chache kabla ya kuvuka barabara, akasita, akili yake ikawambia kitu.

Kwa nini nisiende kuongea na wae wagonjwa? Akajiuliza, akasonya na kugeuka kurudi alikotoka. Miguu yake ilimfikisha katika hospitali ile ile ya Amana, kwa bahati mbaya au nzuri, akakuta ni muda wa kuona wagonjwa hivyo hakupata usumbufu wa kuingia katika wodi aliyohitaji.

Msongamano ulikuwa mkubwa wa ndugu na jamaa kuja kuona wagonjwa wao, Mustafa alifanikiwa kujipenyeza mpaka kufika katika moja ya kitanda ambacho yule aliyemhitaji alikuwapo baada ya kuuliza hapa na pale.

ITAENDELEA ……
 
RIWAYA: JANGA

MTUNZI: richard MWAMBE







Kwa nini nisiende kuongea na wae wagonjwa? Akajiuliza, akasonya na kugeuka kurudi alikotoka. Miguu yake ilimfikisha katika hospitali ile ile ya Amana, kwa bahati mbaya au nzuri, akakuta ni muda wa kuona wagonjwa hivyo hakupata usumbufu wa kuingia katika wodi aliyohitaji.

Msongamano ulikuwa mkubwa wa ndugu na jamaa kuja kuona wagonjwa wao, Mustafa alifanikiwa kujipenyeza mpaka kufika katika moja ya kitanda ambacho yule aliyemhitaji alikuwapo baada ya kuuliza hapa na pale.



SEEMU YA 03

Shuku alilala kimya katika kitanda hicho cha chuma huku watu kadhaa wakiwa wamemzunguka katika hali ya huzuni.

“Karibu baba!” sauti ya mwanamke mmoja wa makamo ikamkaribisha kijana huyo.

“Asante!” akaitika na kusogea karibu na kitanda alicholala Shuku, “Mgnjwa anaendeleaje?” akauliza.

“Hivyo hivyo tu baba yangu, anababuka ngozi anakuwa kama na malengelenge…”

“Amepatiwa matibabu?” akamwuliza Yule mama kwa mtindo wa kumkatisha kauli yake.

“Wanapita tu wanamtazama na kuondoka, wanasema hakuna dawa,” Yule mama akajibu kwa uchungu.

“Mimi ni mwandishi wa habari, nimekuja hapa kujua kiundani shida ya mgonjwa huyu na hatua iliyokwishakuchukuliwa na mamlaka husika,” akajitambulisha na kuwaambia zaidi ni kipi kilichmeta mahala pale.

Waliposikia kuwa ni mwandishi wa habari, kila mmoja alitaka kuongea maana alikuwa na dukuduku lake moyoni. Baada ya kusikiliza kila mmoja, Musatfa aligundua kuwa chanzo cha ugonjwa huo ni vipodozi ambavyo binti huyo alivitumia saa chache kabla hali yake haijawa mbaya. Akaandika katika kijitabu chake na kuendelea kukusanya habari. Alipomtafuta mgonjwa wa pili, majibu hayakuwa na tofauti sana na ya kule alikotoka.

Vipodozi! Akawaza.

Kwa nini serikali inaruhusu vipodzi hivi kuingia nchini? Akajiuliza swali ambalo halikupata jibu kwa kuwa hakuwapo mtu wa kujibu.

Ina maana haijui au mamlaka husika za kuruhusu hiki ni salama na kile si salama imelala usingizi? Bado maswali hayo yalikuwa yakiumiza kichwa chake huku akipita katikati ya ujia ambao watu wotw walikuwa wakiutumia kwenda na kutoka katika wodi za hospitali hiyo. Akiwa anavuka geti a kutokea nje mara akakutana na Mganga Mfawidhi wa ile hospitali, ambaye ni asubuhi ya siku yiyo hiyo alitoka kumhoji juu ya swala lile.

Macho yakagongana, wakatazamana kwa nukta kadhaa.

“Ina maana majibu niliyokupa hayakukutsha hadi uingie na wodini?” akamwuliza kwa sauti ambayo walisikiana wao tu wakati walipokuwa wakipishana bila kusikiwa na mtu wakati ni wengi walikuwa wakipita eneo hilo. Musatafa alimtazama yule daktari pasi na kujibu kitu, ni kama alimjibu ‘haikutosha’ huku akiyageuza macho yake mbele na kupita eneo hil na yule daktari akiendelea kumsindikiza kwa macho.



03



VIPODOZI HATARI VYAINGIA NCHINI, ilikuwa ni kichwa cha habari cha gazeti la Mbalamwezi lililochapishwa siku iliyofuata. Habari hiyo ambayo chini tu ya kichwa chake kulikuwa na jina la mwandishi, Mustafa Bashiru. Kila mtu aliyeliona gazeti hilo siku hiyo alipenda kujua kulikoni na habari hiyo. Kama ni kundi kubwa la wateja wa siku hiyoi basi akna mama na wasichana waliongoza kwa kununua.

Katika moja ya afisi kubwa za serikali, mtu mmoja aliyekuwa na tumbo lililomtangulia alikuwa akibembea juu ya kiti chake cha magurudumu manne huku kiyoyozi kikimpepea kwa nguvu. Mkononi mwake alikuwa na gazeti la hilo, alipomaliza kuisoma habari ile akalifunga na kulitupa mezani kasha akashusha pumzi ndefu.

“Mustafa Bashiru, once again!” akasema kwa sauti ndogo, akazungusha kiti chake na kuielekea simu iliyokuwa hapo jirani, akiinua na kuibonya tarakimu kadhaa kisha akaiweka sikioni.

“Fika afisini hapa mara moja!” alipomaliza kusema hayo katika simu ile akakata na kuirudisha katika kitako chake. Akajiegemeza kwa nguvu mpaka kile kiti kikapiga kelele ‘kwiiiin’.

“Belinda! Belinda!” akamwita katibu wake na mara tu mwanadada huyo akaingia ndani ya afisi ile.

“Yes Boss!”

“Mtu yeyote akija mwambie nina kikao, akifika yule rafiki yangu mhindi koko, mruhusu apite mara moja, sawa?” akampa maagizo.

“Sawa Boss!” Belinda akajibu na kutoka katika afisi ile, moja kwa moja akaketi katika kiti chake, afisi ndogo ya kwanza kabla hujaingia ile ya mheshimiwa. Dakika kumi na tanoi zilikuwa nyingi sana, Ngishu alifika katika afisi ile kama alivyotakiwa na ile simu aliyopigiwa, Belinda alimkaribisha na kumwambia apite ndani, naye bila kuchelewa akingia na kumkuta mnene huyo katulia tu juu ya kiti chake huku akingalia luninga iliyokuwa ikirusha habari za kimataifa. Alipomwona kijana huyo, akajioweka sawa kitini na kumkaribisha katika kiti cha wageni.

“Ngishu! Umesoma gazeti la leo?” akamtupia swali hata bila ya salamu.

“Gazeti gani?”

“Mbalamwezi!” akamjibu na Ngishu akajibu kwa kutikisa kichwa kushoto na kulia akiwa na maana ya ‘hapana’. Yule mzito akamrushia lile gazeti.

“Mustafa Bashiru, once again!” akairudi ile kauli yake huku akijiweka sawa kitini kurekebisha tai yake iliyokaa sawia shingoni mwake. Ilichukua dakika kama tano hivi za ukimya na baada ya hapo Ngishu akakunja lile gazeti na kuliweka mezani.

“Umeona ee?”

“Nimeona! Huyu anamtafuta nyoka miguu,” Ngishu akamwambia swahiba wake.

“Hivi anajua anachokiandika au anajitafutia umaarufu tu?” yule mheshimiwa akamuuliza Ngishu huku mara hii akijiegemeza mikono yake mezani.

“Anatafuta kiki…”

“Basi ataipata, tena muda si mrefu,” akamkata kauli Ngishu, kasha akatulia kidogo na kumtazama kijana huyo wa kihindi aliyetulia kitini kimya.

“Ok tuliache hilo, lakini unaona katika habari hiyo akijitapa kuwa kaongea na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Amana na Mkuu wa Kituo Cha Polisi Buguruni,” akamwambia Ngishu.

“Ndiyo, lakini hakumaanisha kuwa wao wamempa habari kamili juu ya tatizo lenyewe,” Ngishu akajibu kwa kueleza kile alichokielewa.

“Kama yeye ni mwandishi si akaandike huko Syria! Sasa sikiliza achana na mpumbavu huyo mmoja, tuzungumzie swala la kesho,” Yule mhesimiwa akabadili mada.

“Mhmhhh! Sikia kiongozi, swala hili la Mustafa usilione dogo, kumbuka sisimizi ana uwezo wa kumuua tembo, lazima tulifanyie kazi tena haraka iwezekanavyo,” Ngishu akatoa ushauri.

“Ok! Fanya juu chini huyu kiumbe umlete bandani usiku wa leo, tumfundishe adabu kasha tutamrudisha uraiani,” maagizo yakatolewa, “Lakini sasa kuhusu kesho, Yule mshenzi anatoa hukumu kesho na unajua pesa tuliyowekeza pale kwenye zile kontena si za kitoto. Ngishu, kwenye pesa bwana hakuna ubinadamu, tunacheza vipi na huyu mtu?” akauliza kwa wasiwasi mkubwa.

“Kiongozi swala la kesho ni gumu sana, nashindwa kujua naliwekaje, kama jana tulivyoongea, jamaa mgumu mgumu mgumu sijapata kuona!” Ngishu akaongea huku akigongagonga meza.

“Sikia Ngishu, kesho ile hukumu isisomwe!” akasema.

Kauli ile ikamfanya Ngishu kutoa macho huku akimwangalia yule kibopa. Angalio lake lilionesha wazi kuwa hakuwa ameelewa maana ya kauli ile.

“Tuna uwezo gani wa kuzuia mahakama kesho? Tusubiri asome hiyo hukumu kasha tukate rufaa,” Ngishu akapendekeza.

“Ngishu, kwa ishu kama hii usije ukajidanganya kwa hilo, eti ukate rufaa, utakata rufaa wakati mzigo wako ushateketea? Ah! Weeeee!” akatulia kidogo, kasha akendelea, “sikia, we nenda kashughulike na huyo anayejiita mwandishi then nityakwambia ni vipi tutafanya kuhusu kesho,” akamaliza kusema na kuagana na swahiba wake.

Ngishu alitoka katika ile afisi na kuagana na Belinda kasha akaondoka zake na kuingia mtaani. Akili yake yote sasa ikawa inacheza na jinsi ambavyo ataweza kumnasa Mustafa kama alivyoagizwa. Aliitazama saa yake tayari ilikuwa mchana mwingi. Najua mida mizuri ni kuanzi saa kumi nambili jioni, akajiwazia huku akiingia kwenye gari yake aliyokuwa ameiegesha mbali kidogo na afisi ya Yule kigogo wa serikali.

Ukimya ulitawala katika chumba kikubwa kilichokuwa kikiendelea kubeba kikao cha watu kadhaa walioonekana wazi wakifanya majadiliano huku wakiwa wamejawa na wasiwasi mkubwa. Walikuwa kama kumi hivi, yule aliyeonekana kama mkubwa wao aliketi mwisho kabisa wa meza ile huku wengine wakiwa pembeni yake. Tumezoea kikao kama hiki mwishoi wa pili wa meza utakuta kamera za aina mbalimbali zikiwa zinafanya kazi yake ili kuwapa wananchi kile kilichonenwa ndani ya nyumba.

“Hivi tutafikiriwaje?” yule kiongozi akauliza.

“Siyo tutafikiriwaje, sema tunafikiriwaje kwa sababu habari imeshatoka kwenye gazeti, na ni kweli hao inaosemekana wamekufa kwa tatizo hilo wamekufa na watu wanajua tu kuwa ni ugonjwa usiojulikana,” akazungumza mkemia wa Mamlaka hiyo, “Na sampuli za ngozi za marehemu wale zipo kwa Mkemia mkuu wa serikali…”

“Janga!” yule kiongozi akatamka huku akijifuta jasho kutokana na kutohisi hata ubaridi wa kiyoyozi. Kilikuwa kikao cha ndani ambacho wahusika walikuwa wakijaribu kuweka mambo yao sawa kabla ya kufikiwa na rungu la serikali katika kadhia hiyo ya vipodozi vyenye sumu. Idara hii nyeti ambayo ilikuwa ni idara tanzu inayokagua bidhaa zote zinazohusiana na ubora wa bidhaa kabla havijatumia na binadamu ilijikuta haina budi kukutana kwa kikao hicho ili ‘kuyajenga’.

“Lakini sampuli ya vile vipodozi si ilikuja hapa au?” mjumbe mmoja akauliza.

“Ndiyo ilikuja na ikakaguliwa ikaonekana vile vipodozi vina kemikali hatari …”

“Sasa nini kikatokea?” akauliza mjumbe yuleyule.

“We acha tu! Hapa cha muhimu ni kuona nini tunafanya,” yule kiongozi akakatisha hoja hiyo na hapo sasas ndipo palipotokea na sintofahamu. Wajumbe walilalamika wanahujumiwa, wakati wao wanafanya kazi vizuri lakini bado huko nje wanaonekana kuwa na matatizo. Kikao kikavunjika bila muafaka.

Hodi ikabishwa katika mlango wa afisi ya Mkurugenzi wa idara ile, Mkurugenzi Bwana Kilimbana akashtuka kidogo kasha akajifanya yuko sawa kabla ya kuruhusu ugeni huo. Kijana mmoja mtanashati, aliyevalia shati la drafti kahawia, suruali ya cadet ya khaki, mgongoni alikuwa na kijibegi kidogo alichokuwa akihifadhia vitendea kazi vyake. Hakuwa mwingine ni Yule aliyeushtua umma asubuhi ya siku hiyo kwa kuchapa ile habari iliyohusu vipodozi.

“Naitwa Mustafa Bashiru,” akajitambulisha na kuonesha kitambulisho chake cha kazi. Bwana Kilimbana, akatulia na kukisoma kwa chati kasha akakirudisha kwa mhusika.

“Ndiyo bwana Bashiru! Karibu sana, sijui unapenda tuongelee hapa au twende nje kidogo,” KIlimbana akamwuliza kijana yule.

“Aaaa mkuu haina haja, maadam nimekuja afisini na ni muda wa kazi nafikiri hapa pangefaa,” Bashiru akaeleza.


Itaendelea
 
RIWAYA: JANGA
MTUNZI: Richard MWAMBE

SEHEMU YA 04
ILIPOISHIA
“Aaaa mkuu haina haja, maadam nimekuja afisini na ni muda wa kazi nafikiri hapa pangefaa,” Bashiru akaeleza
Endelea…
“Ok, karibu nakusikiliza,” akamruhusu huku akiona kama viungo vyake vikiishiwa nguvu, kwa maana alikwishamjua kijana huyo ni nini anachokitaka kutoka kwake.
“Kilinichonileta kwako ni kutaka kuuliza juu ya vipodozi vile vya sumu ambavyo leo hii gazeti letu limechapa ile habari. Kiukweli nimekuja kwako ili nipate sehemu ya pili ya ukweli ule, je sampuli ya vipodozi vile ilipita hapa kwenu katika uchakataji ili kujua kama ni salama kwa matumizi ya binadamu?” lilikuwa swali ambalo Kilimbana alilitarajia, na sasa alitakiwa kulijibu, muda huo tayari Mustafa alikuwa kashika kalamu na kijidaftari chake.
“Unajua kijana, hii ishu ni kubwa sana, hivi punde tu tumemaliza kikao cha dharula baada ya kusoma ile habari yako. Kiukweli umetusaidia sana katika kugundua hilo, laity ungekuja kwangu kabla hujaandika mambo yangekuwa mazuri zaidi…”
“Unamaanisha nini?” Mustafa akamdakiza swali.
“Nina maana kwamba ile sampuli ya vipodozi haijapita hapa kwetu kuchunguzwa, imeingizwa tu kinyemela huko madukani,” Kilimbana akajibu kwa kujitutumua huku jicho kali la Mustafa lilikuwa likimtazama.
“Ok, kwa hiyo wananchi unawaambiaje? Maana hii ni habari ya kesho…”
“Aaaa unajua kijana, enheeee!!! Hapo hapo sasa, kiukweli ni kwamba vile vipodozi havijapita hapa, na hata mkemia wangu hajawahi kuviona wala kuwa na kumbukumbu ya kazi hiyo. Hao ni wajanja tu ambao wameingiza kinyemela.” Akaeleza.
“Sawa, sasa bidhaa hiyo imejaa madukani, mnasemaje iondolewe au iendelee kuuzwa?”
“Sikia, tukisema bidhaa iondolewe sokoni, siyo fare eeenh, si unajua! We umesoma! Na tukisema iendelee kuuzwa bado nayo haikai sawa hapo, sasa hapo kitu ambacho tumekiona ni kuwa inawezekana walioathirika walitumia chupa ambazo zimeeksipoaya au ndiyo zenye sumu lakini sidhani kama vyote vina tatizo hilo. Na wakati mwingine inawezekana ni ule uchanganyaji wa madawa yao kule saluni au nyumbani, maana mwanamama anapaka hiki anachukua na kile anachanganaya kikemia ile tunaita chemical reaction, ndicho kilichotokea,” akaeleza.
“Sawa mimi sina utaalamu wa mambo hayo lakini ninyi mnatoa tamko gani katika hilo?” Mustafa akataka apate tamko hasa la Mkurugenzi huyo.
“Aaaa tunawashauri wananchi wanapotumia vipodozi hivi wasipende kuchanganya na product nyingine ni hatari kwa afya zao kama hivi,” akaeleza kasha wakaagana na Mustafa. Mlango wa afisi ile ulipofungwa tu, sura yake ikatoka kutoka katika tabasamu la uongo na kurudi kwenye muoinekano wa hasira kali.
“Huyu dogo ataharibu sasa hivi!” akajisemea kwa sauti ndogo, akachukua simu na kupiga namba fulani.
“Ndiyo mzee, naweza kuja kukuona ofisini…”
“Hapana tuonane palepale Bushtracker,” akajibiwa namna hiyo.

Mara tu Mustafa alipotoka kwenye ile afisi, akaingia kwenye kigari chake kilichochoka sana, Toyota Celica na kukiwasha kwa taabu. Kilipowaka akawasha na redio kujiliwaza kasha akaingia barabarani nakuondoka zake. Wakati yeye anaodoka tu pale maegeshoni, gari nyingine aina ya Lexus ikaingia bartabarani na kumfuata taratibu huku katikati kukiwa na gari kama mbili hivi zilizowatenganisha.
Saa kumi na mbili jioni Mustafa alikuwa akikaribia eneo la nyumbani kwake, lakini kabla ya kuifikia nyumba hiyo ilimpasa kuvuka kichaka cha chenye matete mengi kwakuwa eneo hilo kulikuwa na maji yaliyotuama miaka na miaka. Akapunguza mwendo na kuingia kwenye kolongo hilo taratibu kwa kuihurumia gari yake. Akiwa katika kufanya hivyo ndipo alipoiona ile gari, Lexus, ikimpita kwa kasi bila kujali mashimo ikasimama mbel;e yake ghafla. Watu wawili waliovali sox usoni ili kujiziba wasijulikane wakateremka haraka, wakazubguka upoande wa dereva na kumchomoa Mustafa. Kijana huyo alishindwa kujitetea kutokana na shambulio hilo kuwa la ghafla sana, alijitahidi kupiga kelele lakini wapi, konde moja lilitua midomoni na kuchana vibaya mdomo wa juu, akakamtwa na kuburuzwa mpaka kwenye ile gari, harakaharaka, akafungwa kamba na kupakiwa kwenye buti ya gari hiyo, kisha likafungwa na ile gari ikaondoka kwa kasi na ile gari ya Mustafa ikabaki palepale kolongoni.
Ndani ya banda kubwa lenye makolokolo mengi ya aina mbalimbali, lililotumika kama stoo au ghala sijui tuliiteje, Mustafa alibwagwa sakafuni. Alipoinua macho yake kutazama juu, hakuweza kuwaona sawasawa wale watu waliomletaq mle ndani, kutokana na mwanga hafifu sana wa banda lile ilimchukua muda macho yake kufunguka sawasawa na kutambua kilichomo mle ndani. Pembeni ya wale jamaa kulisimama ile gari iliyomteka, na lango la banda lilikwishafungwa, hakujua hata ni wapi alipo. Mara ghafla akaanza kushambuliwa na mateke kutoka huku na kule. Jamaa hao walimpiga bila huruma mpaka Mustafa akawa hoi, damu zikimtoka kinywani, akihema kwa taabu sana.
“Mwacheni!” sauti nzito ilisikika kutoka katika moja ya kijichumba kidogo ndani ya banda hilo. Mtu mmoja aliyevalia kaptula ya jinzi alisimama karibu yake, usoni naye alikuwa kavalia soksi kama wale wengine ila huyu alionekana wazi kuwa ni kiongozi wao kutokana na unene aliokuwa nao na tumbo lililotangulia mbele.
“Ha! Ha! Ha! Mwandishi…” akacheka na kuongea kwa kejeli, “Nimesoma habari yako leo, ilikuwa nzuri sana, na hiyo lazima utambue kuwa ndiyo iliyokuleta hapa. Kwa nini unapenda kuingilia mambo ya watu wewe? Hivyo vipodozi we vinakuhusu nini?” akamuuliza huku akimsukuma uso kwa mguu wake na Mustafa akapindukia upande wa pili kasha na wale vijana nao wakamsukuma vilevile akarudi upande wa kwanza.
“Hili ni onyo, nakuacha hai, ukijifanya mjanja wa kuandika tena kinachohusiana na hivyo vipodozi sijui nini nitakushughulikia, kunguni wewe!” yule mtu akauguruma kwa hasira wazi.
“Koh! Koh! Koh!” Mustafa akakohoa na kutema damu zilizokuwa kinywani mwake, “Uki-ni-u-a mi-mimi, she-ri-a i-ta-ku-a-dhi-dhibu!” akaongea kwa taabu.
“Oooh! Kumbe! Ok, kaandike tena ujinga wako na hiyo kesho utaona sheria jinsi tunavyoichezea. Mtoeni hapa mkamtupe huko!” akatoa amri na wale vijana wakamsulubu tena Mustafa mpaka akapoteza fahamu. Wakambeba na kumpakian kwenye gari, mara hii haikuwa ile ya kwanza. Wakatoka pale na kuendesha kwa kasi mpaka katika bonde la Msimbazi eneo la Segerea, sio mbali sana na nyumbani kwake, wakamtupa hapo kolongoni ambako gari yake waliiacha, lakini mara hii hawakuikuta.
Sauti za watu waliokuwa wakiongea kwa mbali zilisikika kwenye masikio ya Mustafa, lakini hakuweza kuwaona, fahamu zake zikampa taarifa kuwa ajitahidi kufumbua machjo naye akafanya hivyo na mara akaanza kuona nuru ya taa ndefu iliyofungwa juu yake, akafinmya macho na alipotaka kuinua mkono ili afunike macho yake ndipo alipogundua kuwa katika kiganja cha mkono huo kulikuwa na sindano ya drip iliyounganishwa. Akadakwa mkono na mkewe kipenzi aliyekuwa jirani hapo, hapo akagundua kuwa kati ya anaowajua ni mkewe tu aliyekuwa jirani na kitanda hicho.
“Mus’ umeamka mpenzi?” sauti nyororo ya mwanadada huyoi ikpenya katika masikio ya Mustafa, akaitaika kwa kichwa, kwa kinywa kizito akauliza, “Niko wapi?”
“Hospitali hapa! Amana,” mkewe akaqmjibu na wakati uohuo muuguzi akafika na bkumpa huduma za hapa na pale.
“Jina lako nani?” Yule muuguzi akamuuliza mgonjwa wake. Mustafa kabla hajajibnu akamtazama kwanza.
“Mustafa Bashiru,” akajibu na Yule muuguzi akaitikia kwa kichwa na kuondoka. Baada ya dakika mbili akarudi akiwa na mtu mwingine aliyevaa koti jeupe na kuning’iniza stethoscope shingoni mwake, mara moja akamtambua kuwa huyo ni daktari. Sura yake haikuwa ngeni kwa Mustafa, alimtambua mara moja.
“Pole Mustafa!”
“Asante dokta,” akaitika. Yule muuguzi akashika kitu fulkani chini ya kitanda na kukizungusha kile kitanda kikajiinua upande mmoja na kumfanya Mustafa kuketi kwa kiasi Fulani.
“Asante nesi,” akashukuru.
“Unajisikiaje?” Yule daktari akamuuliza.
“Nina maumivu sana tumboni,” akajibnu.
“Ndiyo, uliumizwa sana maeneo hayo, ulipigwa au ilikuwaje?” swali hilo la daktari likamfanya Mustafa kujaribu kukumbuka matukio ya nyuma, akili yake ilirudi mpaka jinsi alivyotekwa na kipigo kile alichokipata, akiwa pale bandani, hakukumbuka tena nini kilitokea. Akatikisa kichwa juu chini akiwa na maana ‘ndiyo’. Daktari aliyekuwa akimhoji Mustafa hakuwa mwingine bali ni Mfawidhi wa ile hospitali. Dakika hiyo hiyo askari watatu wakafika na Mkuu wa Kituo cha Polisi cha Mabatini Stakishari akawasili akiwa na swahiba wake yule OCD wa Buguruni.
“Pole sana Mustafa!” wakamsabahi naye akawajibu kwa kichwa.
Mmoja kati ya wale vijana aliyevalia nadhifu kabisa sare yake ya kijani kikavu akawa tayari na kalamu na faili mkononi mwake.
“Sisi ni maafisa wa polisi, usishangae kwa nini tumekuja sisi na si wale wa chini yetu hii ni kwa sababu swala lako liko toifauti kidogo na mengine. Tunapenda kujua ni nini kimekusibu hata kukupelekea kuwa hivi,” Yule OCD wa Mabatini akamuuliza.
“Nime-pi-gwa,” akaongea kwa shida kidogo huku akikatakata maneno.
“Pole, ina maana ulipigwa palepale au ilikuwaje?”
“Waliniteka, wakanipe-le-ka sijui wapi, wakanipiga sana,” akawaeleza.
“Sababu ya kukupiga ni ipi? Walikwambia?”
“Gazeti la leo!” akajibu. Wale askari wakatazamana kwa nukta kadhaa.
“Gazet la leo!” OCD wa Mabatini akamwambia Yule mwenzake kwa mshangao. Akachukua gazeti la siku hiyo na kumwonesha kurasa ya juu kabisa iliyobeba maandishi mazito meusi.
‘AJALI MBAYA YACHUKUA MAISHA YA JAJI SHEKIBINDU’ ndicho kilichosomwa na macho ya Mustafa. Akashtuka na kutazama vyema lile gazeti, akawaangalia wale askari.
“Mbona sielewi?” akauliza.
“Huelewi nini Mustafa? Hili ndilo gazeti la Mbalamwezi la leo na hakuna linguine,” akajibiwa.
“Kwani leo lini?” akauliza.
“Leo ni tarehe 26 Mei 2012, na wewe ulipatikana tarehe 25 alfajiri,” Yule afande aliyekuwa anaandika akamweleza Mustafa. Hapo ndipo alipogundua kuwa amekuwa pale hospitali kwa saa nyingi sana, akashusha pumzi na kujaribu kujiweka sawa lakini maumivu katika sehemu za kiuno yalikuwa makali sana.
“Unawakumbuka waliokuteka?” akaulizwa.
“Walikuwa wamevaa soksi usoni, sikuwatambua hata mmoja wao” akajibu. Baada ya wale maafisa kuongea machache wakaagana na yule daktari kisha wakaondoka zao wakiahidi kurudi siku akipata nguvu zaidi.
Mustafa alijiegemeza kichwa godoroni, akaomba gazeti la siku hiyo akaletewa, akaanza kuliperuzi hapa na pale. Mkewe alimwona mpenziwe akiangusha chozi kutoka pale alipokuwa amejioegemeza.
“Usilie mume wangu, nini tena,” mkewe akambembeleza.
Kutokana na jinsi mwanamke huyo alivyomzoe mumewe kwa jinsi anavyopenda kazi yake ya uandishi wa habari, alielewa ni kipi hasa kinachomliza. Mtu mwingine kwa haraka haraka angeweza kusema kuwa analia kwa kuwa Jaji huyo amekufa ajalini, mwingine angesema analia klutokana na maumivu anayoyapata. Siku hiyo hata mkewe alikosea kuotea kwani yeye alijua waqzi kuwa mumewe analia tu kwa nini si yeye aliyeiandika habari ile. La bali jibu alikuwa nalo moyoni mwake.
Akaliweka gazeti papo hapo kitandani na kujaribu kuyafumba macho yake kwa nguvu lakini usingizi haukuja mara hiyo.
“Ina maana kesi imeahirishwa?” akamuuliza mkewe.
“Kesi?” mkewe akauliza.
“Ndiyo, kesi,”
“Kesi gani?”
“Huyu Jaji aliyekufa kwa ajali, ndiye aliyekuwa anaendesha kesi ya yale makontena ya vipodozi vyenye sumu, na jana ilikuwa ndiyo siku ya hukumu ya wale watu, dah!” akaeleza. Mkewe alisikiliza lakini kutokana na kwamba yeye hakuwa mfuatiliaji wa mambo ya habari, hata hilo hakuling’amua kutokana na kwamba hata gazeti lenyewe hakulisoma.
“Ha! Kumbe ndiyo huyu!” naye akashtuka, “Aaaaaa kweli, picha yake hii hapa,” akasema huku akiwa na lile gazeti mkononi mwake.
“Lazima niiandike upya hii habari, huyu karashiarashia tu, hajawaambia Watanzania ukweli,” akasema…
“M’me wangu unaumwa upumzike, wengine wataandika!” mkewe akalalama.
“No! hii lazima ifanyiwe uchunguzi iandikwe tena, kwa nini huyu Jaji apate ajali wakati ni saa chache tu zilikuwa zikimsubiri kutoa hukumu ya kesi ile nzito? Nani yuko nyuma ya swala hili? Watanzania lazima wajue, na kama ni njama sheria itamhukumu anayehusika,” kasha akajifunika shuka kwa taabu na kuutafuta usingizi akimwacha mkewe kajiinamia kimya.

ITAENDELEA...............
 
RIWAYA: JANGA

MTUNZI: richard MWAMBE






“M’me wangu unaumwa upumzike, wengine wataandika!” mkewe akalalama.

“No! hii lazima ifanyiwe uchunguzi iandikwe tena, kwa nini huyu Jaji apate ajali wakati ni saa chache tu zilikuwa zikimsubiri kutoa hukumu ya kesi ile nzito? Nani yuko nyuma ya swala hili? Watanzania lazima wajue, na kama ni njama sheria itamhukumu anayehusika,” kasha akajifunika shuka kwa taabu na kuutafuta usingizi akimwacha mkewe kajiinamia kimya.



SEHEMU YA O5



04

SIKU MBILI BAADAE

“Mwanadamu kumbuka, wewe ni mavumbi na mavumbini utarudi…” sauti ya Kasisi ilisikika huku ikifuatiwa na harufu ya ubani ulichomwa. Sanduku lililbeba mwili wa Jaji Shekibindu liliteremshwa taratibu kaburini huko kwao Raskazoni Tanga, kisha taratibu za kuweka udongo kaburini zilifuatia, nyimbo za huzuni zilizindikiza tukio hilo lililkusanya watu wengi wakiwamo viongozi wa serikali ngazi mbalimbali.

“…Marehemu alikuwa mtu mwadilifu…” maneno haya machache ndiyo yaliyobaki kwenye kichwa cha Madam S. Alikuwa wa kwanza kuingia katika gari kabla ya mtu mwingine yoyote. Ndani ya gari hiyo Scoba alikuwa katulia tuli nyuma ya usukani akimsubiri bosi wake.

“Ifuate hiyo gari,” akamwambia Scoba naye akafanya hivyo. Ilikuwa Land Cruiser VX nyeusi, iliyoondoka makaburini pale kabla ya tukio lile kwisha. Scoba hakuuliza aliwasha gari na kuanza kuifuata hiyo aliyoambiwa.

Katikati ya jiji la Tanga, Hoteli ya Mkonge, ndipo gari ile iliegeshwa, nao wakaingia hapo dakika nne tu baadae, Scoba alifanya vile makusudi tu.

“Nisubiri,” Madam akamwambia dereva wake kasha yeye akatokmea ndani ya hoteli ile, ilimchukua kama dakika tano hivi kurudi katika gari.

“Vipi?” Scoba akauliza.

“Twende,”

“Wapi?”

“Makaburini,” Madam akajibu na kijana huyo akachukua barabara na kurudi walikotoka. Walipofika katika eneo lile la makaburi walikutana na ukimya wa ajabu, hakukuwa na mtu, tayari aliyekuwa Jaji Shekibindu alibaki peke yake kaburini. Scoba aliendesha gari kwa mwendo mdogo na baadaye akasimama baada ya Madam S kumpa ishara ya kufanya hivyo.

Gari moja nyeupe, Subaru, ikatokea mbele yao na kusimama karibu na lango a kuingilia katika makaburi hayo. Watu wawili wakashuka, kijana mmoja na mwingine alionekana mtu mzima, mwenye mwili mkubwa, kwa jinsi alivyovaa hakuweza kumtambua hata sura yake.

WIKI MBILI BAADAE

Bi Zuhura, mjane, aiketi sebuleni kwake, jioni hiyo alikuwa peke yake kwani watoto wake wawili walikuwa masomoni, na mfanyakazi wake wa ndani alikuwa amepumzika baada ya kazi nyingi za mchana huo. Mbisho wa hodi ndiyo uliyomgutusha kutoka katika wimbi la mawazo.

Akainuka kwa kujivuta na kuuelekea mlang huo huku moyo wake ukipiga haraka haraka, daima muda huo iikuwa na hodi ya mumewe ambaye sasa alikwishakuwa marehemu.

Mungu wangu! Nangi huyu? Akajiuliza huku akitupa jicho lake kwenye saa kubwa iliyopachikwa ukutani, juu tu ya mlango huo. Alipofungua mlango ule akakutana macho na watu asiyowajua. Akina nani? Akajiuliza.

“Karibuni!” akawakaribisha baada ya kugundua kuwa kwanza ni wanawake wenzake.

“Asante sana!” mmoja aliyeonekana mtu mzima kuliko mwingine aliitikia na kuingia ndani. Wakaketi kwa mtindo wa kutazamana na mjane yule.

“Pole sana wifi!” ndiyo sentensi ya kwanza iliyotoka katika kinywa cha Madam S ambaye alikuja na Jasmine kumtembelea mjane huyo.

“Asante, ni kazi ya Mungu!” akaitika.

“Naitwa Selina, na huyu ni binti yangu Rose. Nimesikitishwa sana na msiba huu, sikuwahi maazishi lakini pia sikuna vyema kukaa bila kuja kukupa pole, mimi na Shekibindu tumesoma wote Uingereza,” akaeleza maelezo yaliyojaa uongo mtupu. Mazungumzo kati yao yaichukua nafasi, na watatu hao walizungumza mengi sana. Bi. Zuhura alieleza mengi sana juu ya mazingira ya kifo cha mumewe. Madam S kwa utaalamu wake wa kuhoji kirafiki aikuwa anazidi kumrudisha nyuma kaba ya kifo ili angalau apate chochote, lengo lake ikafanikiwa.

“Siku mbili kabla ya kifo, nilishtuka usiku sana nikakuta mume wangu hayupo kitandani, kama unakumbuka siku ile kulikuwa na mvua kubwa sana…”

“Ndiyo ndiyo!” Madam akadakiza kiitikio.

“Nilipotoka sebuleni nikamkuta akiwa anaweweseka, anaongea na mtu asiyeonekana, nikamchukua na kumrudisha chumbani. Shekibindu alikuwa na matatiz ya kuota ndoto kama hizi tangu utoto wake, wazazi wake walikwishanieleza,” akazidi kueleza.

“Oh pole sana, kaba ya kuota hiyo ya mwisho, ni lini tena aipatwa na ndoto kama hiyo?” Madam akapiga swali.

“Aaa ni muda tu, nakumbuka ni kama miaka saba hivi, hata nilishasahau kwanza,” akamjibu.

“Hakuwa na maadui? Labda majirani au marafiki,”

“Mh! Sina uhakika, mume wangu alikuwa mtu wa watu sana,” akanyamaza kidogo, kasha akaendelea, “lakini nakumbuka siku ile alikuwa akirudiarudia kuniambia ‘wanataka waniue’ mi nikamtuliza tu na kumpeleka chumbani”.

Baada ya saa kadhaa Madam na binti yake waiagana na Bi. Zuhura huku akimwachia namba ya simu akimtaka kwa muda wowote kama kuna tatizo amjulishe, ili waitatue kwa pamoja.



UKUMBI WA MIKUTANO – MAHAKAMA KUU

Jopo la majaji wa Mahakama ya Tanzania lilikutana asubuhi na mapema, kikao hicho kiliitishwa baada ya wiki mbili tangu kitokee kifo cha Shekibindu. Jaji Mkuu alikuwa mmoja wa majaji hao na ndiye alikuwa msemaji wa kikao hicho.

Kabla ya kuanza lolote walisimama kimya kwa dakika moja ili kumkumbuka mwenzao aliyetangulia mbele ya haki. Baada ya hapo wakaketi na kila mmoja akaweka sawa kabrasha lake tayari kuandika yale yanaytakiwa kuandikwa tu.

“Waheshimiwa majaji, tumeitana hapa kama mnavyojua ni dharula tu na hii imetokana na kifo cha mwenzetu kilichotokea kwa ajali ya gari. Kama mnavyojua Mheshimiwa Shekibindu, alikuwa mbioni kumaliza ile kesi nzito yenye utata ya zile kontena za vipodozi hatari, lakini kama mlivyosikia na kushuhudia kilichotokea,” akakohoa na kuendelea, “sasa dhumuni la kikao hiki ni kumchagua mtu mwingine wa kumalizia kesi ile”. Aliposema hayo, wakaanza kutazamana kana kwamba kila mtu hakuwa tayari kwa hilo.

“Waheshimiwa tunapiga kura za kupata jina moja,” akawaambia na zoezi hilo likaanza mara moja huku makarani walioteuliwa wakihakikisha linaenda vyema. Baada ya saa mbili hivi walikuwa wamekamilisha zoezi hilo na Mh. Jaji Tulabayo akachaguliwa. Alipotangazwa jina lake, alijikuta akitazamana na Jaji Mkuu kwa nukta kadhaa kabla hajatakiwa kusema lolote.

“Mheshimiwa Jaji Mkuu na waheshimiwa majaji wote, najua jukumu mlilonipa ni zito, lakini sauti ya wengi ni sauti ya Mungu, ninalipokea lakini nitahitaji sana msaada wenu wa kiushauri kwani wenyewe mnaelewa uzito na ugumu wa kesi hii,” Tulabayo aliongea huku chozi likimtoka, hakuna aliyejua kwa nini mheshimiwa huyo kakumbwa na hali kama hiyo isipokuwa yeye na nafsi yake. Baada ya Jaji Mkuu kufunga kikao kile waheshimiwa walitawanyika na kubaki Mheshimiwa Tulabayo na Jaji Mkuu.

“Sasa Mkuu, hii kesi ninaianzia wapi?” Tulabayo akauliza.

“Usijali mheshimiwa, upelelezi ulishafanyika na ushahidi wote upo, Shekibindu alikuwa tayari keshaandika hukumu ya kadhia hii lakini wakati wa ajali ile kila kitu kimeibwa hakuna chochote tulichokikuta.

“Viliibwa?” akauliza.

“Ndiyo, laptop, mafaili yote ya kazi ambayo alikuwa nayo hayakupatikana,” Jaji Mkuu akajibu.

“Lo! Hii ni kazi ngumu sana,”

“Usihofu, utauona ushahidi wote kisha utaandika hukumu inayostahili kadiri ya kesi yenyewe ilivyo,” jaji Mkuu akamtoa hofu Tulabayo.

Jioni ya siku hiyo, ilimkuta Jaji Tulabayo katika moja ya hoteli kubwa jijini Dar, akipata kinywaji yeye na rafiki zake. Habari za kuchaguliwa kwake kuendesha kesi hiyo tayari zilisambaa kila kona na wengi walikwishamjua.

Wakati yeye akiwa na rafiki zake katika hoteli hiyo, watu wengine walikuwa wakimwongelea yeye katika hoteli nyingine.

Mtu mnene, aiyeniga tai ndefu iliyoshuka mpaka chini ya mkanda wa suruali yake, waliyomzunguka wote walivaa kama yeye, walionekana kushiba pesa, walitakata haswa.

“Tunaingia awamu ya pili ya huu mchezo,” sauti ya Kigogo wa serikali mwenye cheo katika serikali alisikika akiwaambia wenzi wake.

“Ile imekwisha, sasa hii tunafanyaje, tukubali kupoteza pesa?” mwingine akadakia.

“Hapana, lazima tumvae, nimepata taarifa kuwa Jaji Tulabayo ndiye kapewa mikoba,” Yule Kigogo akaeleza.

“Ndiyo ni yeye, sasa inabidi afanyiwe utaratibu mapema,” Mjumbe mwingine akasema.

“Haina shida wajumbe, kijana atamtafuta usiku huu huu”.

Kikao hiki kilichofanyika Bushtracker kiiwakutanisha watu wenye pesa zao, wenye madaraka serikalini na kwenye idara zake nyeti. Vigogo wale waliokuwa wakifanya biashara nyingi haramu na watu mbalimbali walipewa wakati mgumu sana na Marehemu Shekibindu, na sasa walikuwa wakijipanga nini cha kufanya. Kikao hicho kilipmalizika, Ngishu aliingia katika chumba hicho cha VIP na kumkuta yule mtu mnene, kibopa ambaye yeye ndiye kila kitu katika michezo hiyo.

“Kuna hii hundi hapa, ya milioni kumi, kesho ifikishe kwa Mheshimiwa Tulabayo,” akamwambia Ngishu.

“Sawa mzee, hii imefika, kwa nini kesho? Mbona hata leo inawezekana. Mheshimiwa yupo na maswaiba zake pale Hoteli ya Belmont …”

“Wanafanya nini?”

“Wanakunywa tu!” Ngishu akajibu.

“Ok, ifikishe hapo kama unaweza, kisha unipe taarifa. Kumbuka njia yetu salama ya kuwasiliana siyo kwa simu,” Kibopa akasisitiza.

“Done!” akajibu Ngishu na kuondoka zake.

HOTELI YA BELMONT

Vinywaji viliendelea kumiminika, waliopo hapo walikuwa wakiendelea kuburudika, walipofika walikuwa wakiongea Kiswahili, na wakati huu walikuwa washabadili lugha karibia tatu, sasa ilikuwa kifaransa.


ITAENDELEA....
 
RIWAYA: JANGA
MTUNZI: RICHARD MWAMBE

SEHEMU YA 06

ILIPOISHIA
.....Vinywaji viliendelea kumiminika, waliopo hapo walikuwa wakiendelea kuburudika, walipofika walikuwa wakiongea Kiswahili, na wakati huu walikuwa washabadili lugha karibia tatu, sasa ilikuwa kifaransa.



Mheshimiwa Tulabayo alishikwa bega, akageuka na kutazama nyuma kwa kuinua macho yake juu kidogo. Ndipo alipokutana na sura hiyo ya Kihindi, sura asiyoijua, macho aliyoyaona yalikuwa mekundu, yaliyolegea, moja kwa moja akaelewa kijana huyo ni mtumiaji mzuri wa kubeil.
“Kijana, mbona sikufahamu!” Jaji Tulabayo akamwambia Ngishu.
“Usijali, utanifahamu tu, ila mimi ninakufahamu, na nimetumwa kwako,” Ngishu akamwambia Tulabayo kwa sauti isiyofanana na mwili wake, yaani alikuwa na sauti nyembamba ilhali mwili wake ulikuwa mkubwa wa wastani.
“Umetumwa kwangu?” akamwuliza.
“Ndiyo Mheshimiwa, na hii ni barua yako,” akamkabidhi ile bahasha, mzee Yule akaipokea na kuitia mfukoni mwa koti.
“Imefika,” akasema, na wakati huo Ngishu akawa anaondoka eneo lile. Tulabayo aliitazama ile bahasha lakini hakuifungua kwanza, akaiweka mfuko wa ndani kabisa wa koti lake. Usiku mkubwa airudishwa na dereva wake ambaye muda wote ambao mheshimiwa huyo alikuwa akigonga cheers yeye alikuwa ndani ya gari kalala.
“…Chaupele mpenzi, hayo usemayo,
Kama ni malazi yapeleke kwa dakitari…”
“Yaani ukirudi kila mtu atajua tu!” mkewe alimwambia huku akiwa anajigeuza upande wa pili kuendelea na usingizi. Mheshimiwa huyo alipolitoa tu koti lake kabla ya kujitupa kitandani akakumbuka ile bahasha, akaichomoa na kuifungua, ndani yake kulikuwa na karatasi ya mstatili, ngumungumu kidogo, akaivuta nje kwa uwoga na kukaribishwa na maandishi ya kuvutia ‘EXIM BANK’. Akaitazama ile hundi huku macho yamemtoka, akaigeuza na kuigeuza, akafikicha macho labda amelala, hapana, ni hundi ya Milioni kumi.
“Come on! Mama Jesca! Mama Jesca!” akaita huku akimtikisa mkewe kwa fujo.
“Nini bwana ah! Mi nimelala,” Mkewe akajibu huku akiusukuma mkono wa mumewe upande mwingine.
“Amka! Hebu soma hapa hii ni shin’ ngapi?” akamwambia. Mwnamke huyo wa kichaga aliposikia ‘shin’ ngapi’ akakurupuka na kuinyakua ile hundi, akaisoma.
“Milioni Kumi,” akamwambia huku akimkabidhi.
“Ok, Mungu hujibu kila mtu kwa jinsi yake lo! Nyumba yetu ya Salasala itaisha sasa,” akasema huku akionekana wazi kutokwa na pombe alizokunywa kwa furaha ya ile hundi.
“Umalizie nyumba wewe! Wewe? We nyumba zako si unajenga baa,” Mkewe akamwambia kwa ukali huku akijifunika gubigubi.

05
KIFO CHA JAJI SHEKIBINDU, NI AJALI ILIYOKUSUDIWA? Gazeti la Mbalamwezi asubuhi ya siku iliyofuata lilipambwa kwa kichwa hicho cha habari, lakini badala ya kuandikwa pale juu kuliwekwa maelekezo tu kuwa habari hiyo inapatikana kurasa ya ngapi. Kila aliyetupia jicho katika meza za magazeti alivutiwa na gazeti hilo.
Katika kurasa hiyo iliyotajwa habari ile ilikuwa imeandikwa na mwandishi maarufu wa kufichua maovu, Mustafa Bashiru. Ndani ya habari hiyo kulikuwa na maswali kadhaa ambayo yalihoji juu ya mazingira yaliyzunguka kifo hicho.
‘Mazingira ya ajali ya Shekibindu yanatuachia maswali mengi kama kwa nini itokee siku moja kabla ya yeye kutoa hukumu ya kesi ya kifisadi?’
Ilikuwa ni moja ya maswali ambayo yalimshtua kila aliyesoma habari hiyo. Mustafa Bashiru alikuwa ni kama mtu aliyetoka mafichoni baada ya kuwa kimya kwa takribani wiki mbili ambazo alikuwa akijiuguza.
Moja ya watu ambao gazeti hilo lilitua mikononi mwao ni yule kigogo wa Serikali. Akiwa afisini kwake hasubuhi hiyo ilikuwa ngumu sana kwake.
“Kwa nini huyu jamaa ananiweka roho juu hivi?” akajiuliza kwa sauti ndogo lakini hakuna wa kujibu. Alijiegemeza kitini na kuweka mikono yake kichwani.
“Sasa namuua, mshenzi huyu!” akangeza kusema na kuinua simu yake, akaongea na mtua fulani kisha akatulia kusubiri.
Nusu saa haikupita, Ngishu aliingia ndani ya afisi ile ile aliyoingia wiki mbili zilizopita na kupata maagizo hayo hayo.
“Safari hii tafuta njia ya kumpoteza kabisa, sitaki hata kumwona, huyu kimbulu ataharibu mambo yote,” akamwambia.
“Haina shaka, leo jua la kesho hatoliona,”
“Good! Go ahead!” akamwambia na kijana huyo akaondoka akiwa na hari ya kutekeleza hilo.
“Bastard!” Ngishu alijisemea wakati akiubamiza mlango wa gari yake na kuondoka kwa kasi.
AFISI ZA GAZETI LA MBALAMWEZI
Mustafa Bashiru aliketi mkabala na Mkurugenzi wa gazeti hilo, ulikuwa ni wito kutoka kwa Mkurugenzi huyo.
“Ndiyo boss,” akatamka.
“Nimekuita, nimekuita kwa sababu maalumu, najua wewe u mwandishi bora sana na habari zako zinauza sana gazeti letu, lakini tumepata barua hii ya onyo ya kuwa tuache kuandika habari za uchochezi…”
“Mkuu! Habari ya uchochezi iko wapi?” akauliza.
“Hizi unazoandika …”
“Hizi? Hizi ni habari za uchunguzi jamani, uchochezi uko wapi?” Mustafa akaunguruma.
“Sikiliza Mustafa, mimi ni mwandishi kama wewe najua miiko na misingi, wewe huandiki uchochezi, hizi ni za uchunguzi kama ulivyosema, lakini wenye mamlaka na nchi yao wamesema na wamekutaja kabisa, soma barua hii,” akampa ile barua, Mustafa akasoma kwa makini na kuirudia rudia.
“Umeelewa?” mkurugenzi akauliza.
Mustafa hakujibu, akabaki kimya kabisa na baada ya dakika kama tatu hivi akajibu, “Nimeelewa, lakini kwa nini serikali inatufunga midomo? Kwa nini inakandamiza uhuru wa vyombo vya habari?”
“Wote tunajiuliza swali hilo hilo,” mkurugenzi akajibu.
“Mimi sintoacha kuandika, kama wewe hutotaka niandike kwenye gazeti lako basi nitaandika kwingine…”
“Hapana Mustafa, si hivyo!”
“Vipi sasa?”
“Ipo hivi, makala zako ninazihitaji sana, lakini tunajiwekaje mbele ya hawa watu wenye matumbo makubwa?” Mkurugenzi akauliza kwa shaka.
“Waliniteka, wakanipiga sana, sasa waache waje waniue,” Mustafa akamwambia mkurugenzi wake na kuinuka kitini, “Kuna habari naifuatilia naenda kwenye afisi fulani na hii tunaichapa kesho. Akiwa tayari kuiacha afisi ile akazuiwa na bosi wake.
“Mustafa!”
Akasimama, na kugeuka nyuma.
“Inahusu nini hiyo habari?” akaongeza swali.
Mustafa badala ya kujibu, akarudi tena mpaka pale karibu na meza ile, akaegemeza mikono yake miwili juu ya meza ile ya Ki-China.
“Hii ndio itawamaliza, si waliniteka ndiyo nakamilisha habari ya kiuchunguzi, ili hata wakiniua, Watanzania wajue kuwa kwa nini nimekufa,” Mustafa akamwambia Yule Mkurugenzi.
“Aliyekwambia atakuua nani?” akaulizwa.
“Huyo aliyeniteka, sina alama ya kumtambulisha kwako lakini kama ukipata bahati ya kumuona akiwa na kaptula basi yeye ana kovu kubwa ugokoni kwenye mguu wa kushoto,” akamaliza kusema na kutoka huku jicho la bosi wake ikimsindikiza. Yule mkurugenzi, Bwana Kisinini akatikisa kichwa kwa masikitiko na kujiweka sawa kitini kwake huku akiendelea kupitia habari mbalimbali zilizokuwa juu ya meza yake.
Jua la utosi lilikuwa likimchoma Ngishu bila huruma, akiwa ameegemea gari yake eneo la Mwananyamala Komakoma mbele yake kulikuwa na vijana watatu walioshiba kimazoezi.
“Mtu wetu si mnamkumbuka?” akawauliza.
“Yupi? Maana tunao wengi,” mmoja wao akauliza.
“Mwandishi…”
“Mustafa?”
“Yes!” akakubaliana na jina alilopewa.
“Enhe vipi?”
“Amepona, na sasa keshaanza makeke yake, makala yake ya leo inafukunyua vya uvunguni,” Ngishu akawaeleza.
“Kile kipigo hakijamtosha ee?” mwingine akauliza kwa shauku.
“Hata kama kilimtosha, safari hii …” akasema na kuonesha alama ya kidole gumba kukatisha shingo, akiashiria ‘kifo’. Ukimya wa sekunde kadhaa ukatawala kati yao, hakuna aliyeongea kana kwamba walitakiwa kukaa kimya kumkumbuka marehemu fulani.
“Yule bwege, tusipomuwahi leo, kesho analipua bomu lingine baya zaidi, tutakuwa pabaya,” Ngishu akawaambia, “kwa hiyo auawe na maiti yake hakikisheni wanaipata kwa tabu,” akamaliza kusema na kuingia garini mwake.
“Sawa!” wale vijana wakaitikia kwa pamoja na kurudi kuendelea na vinywaji vyao. Ngishu, aliondoka eneo hilo huku akijua wazi ni jinsi gani ambavyo atakutana na vijana wake kwa kazi waliyopewa, waliizoea, haikuwa mara ya kwanza kuua au tuseme kumdhulumu mtu roho yake. Ngishu aliijua vyema kazi hiyo, aliifanya katika mazingira mbalimbali kadiri ya mteja wake alivyotaka. Ukimuona, ni kijana mtanashati, hana mwili mkubwa, ana macho ya kulegea kutokana na ulevi wake wa kubeil. Hata kama mtu angekwambia kuwa ‘huyu ni muuaji hatari’ usingekubali abadan. Huyo ndiyo Ngishu, kijana wa Kihindi kutoka mitaa ya katikati ya jiji, mtaa ule waliuteka na kuugeuza kama kwao, Mtaa wa India.

ITAENDELEA
 
RIWAYA: JANGA

MTUNZI: richard MWAMBE
SEHEMU YA 7






“Hata kama kilimtosha, safari hii …” akasema na kuonesha alama ya kidole gumba kukatisha shingo, akiashiria ‘kifo’. Ukimya wa sekunde kadhaa ukatawala kati yao, hakuna aliyeongea kana kwamba walitakiwa kukaa kimya kumkumbuka marehemu fulani.

“Yule bwege, tusipomuwahi leo, kesho analipua bomu lingine baya zaidi, tutakuwa pabaya,” Ngishu akawaambia, “kwa hiyo auawe na maiti yake hakikisheni wanaipata kwa tabu,” akamaliza kusema na kuingia garini mwake.

“Sawa!” wale vijana wakaitikia kwa pamoja na kurudi kuendelea na vinywaji vyao. Ngishu, aliondoka eneo hilo huku akijua wazi ni jinsi gani ambavyo atakutana na vijana wake kwa kazi waliyopewa, waliizoea, haikuwa mara ya kwanza kuua au tuseme kumdhulumu mtu roho yake. Ngishu aliijua vyema kazi hiyo, aliifanya katika mazingira mbalimbali kadiri ya mteja wake alivyotaka. Ukimuona, ni kijana mtanashati, hana mwili mkubwa, ana macho ya kulegea kutokana na ulevi wake wa kubeil. Hata kama mtu angekwambia kuwa ‘huyu ni muuaji hatari’ usingekubali abadan. Huyo ndiyo Ngishu, kijana wa Kihindi kutoka mitaa ya katikati ya jiji, mtaa ule waliuteka na kuugeuza kama kwao, Mtaa wa India.



06

HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI

Chumba cha Kuhifadhi Maiti

Shabani Mtemanyongo aliishusha kwa nguvu chupa ya pombe, Jack Daniel, aiyokuwa akiinywa kwa fujo. Kila aliyemuona kwa jinsi alivyokuwa anakunywa alimuacha kama alivyo maana waliamini kuwa ni kazi yake inayomfanya awe hivyo. Ni kweli, kufanya kazi katika idara hiyo, ya kuhifadhi maiti au tuiite miili ya marehemu yataka moyo. Hakuna mtu anayeipenda kazi hiyo lakini cha kushangaza kijana huyu aliyejulikana kwa jina moja tu la ‘Mtemanyongo’ aliipenda sana kazi yake, daima kila unapomkuta yeye anatabasamu tu akiwa ndani ya suti safi hata kama kuna joto.

Lakini wiki hizi mbili, Mtemanyongo alikuwa tofauti sana, hakuwa na tabasamu lile walilolizoea, macho yake mekundu daima yalionekana kutona machozi. Alipoulizwa, hakujibu, bali alimtazama tu aliyemuuliza.

Katika moja ya droo nyingi zilizop kwenye kabati kubwa ambalo wafanyakazi wa chumba hicho walitumia kuhifadhi nguo zao, Mtemanyongo alihifadhi magazeti mengi ambayo alikwishayasoma. Akalichukua na hilo alilomaliza kulisoma siku hiyo, akalisweka katika droo iyo hiyo huku akitikisa kichwa chake kwa masikitiko na kuvuta kamasi jepesi lililotaka kudondoka na kulirudisha ndani ya pua zake.

“Ipo siku hata wewe utalala hapa!” akajisemea huku akiifunga ile droo ya kabati na kutoka nje katika chumba chake cha kupumzika. Siku hii hakukuwa na watu wengi waliokuja kuchukua ndugu zao hivyo hali hiyo ilimpa nafasi kubwa ya kupumzika na kujisomea gazeti lake kwa raha bila bugudha.

NDANI YA JENGO LA MAHAKAMA KISUTU

Simu ya mezani iliita kwa fujo, Mheshimiwa Jaji Tulabayo aliinyakua na kuiweka sikioni.

“Hello!” akaita.

“Hello! Mheshimiwa hongera sana kwa uchaguzi wa jana,” sauti ya upande wa pili ikampongeza.

“Uchaguzi! Uchaguzi upi?”

“Aaaa Jaji, si umechaguliwa kuendesha kesi…”

“Ha! Sasa hilo ndiyo swala la kunipongeza?” akauliza.

“Ndiyo!”

“Hili ni jukumu langu, na ni lazima nilifanye. Ingekuwa nimepandishwa cheo sawa, lakini kupewa kesi kuongoza ndiyo unipongeze?” Tulabayo akang’aka.

“Sikiliza mheshimiwa, mimi ninayekupongeza siyo kwamba sina akili au sijielewi, ninakupongeza kwa sababu umefika kwenye njia panda ya kuwa Milionea,” ile sauti ikamwambia.

“We n’nani kwanza?” akauliza.

“Usijali mheshimiwa, jana nilimtuma kijana wangu mmoja hivi, nafikiri alikuletea mzigo,”

“Aaanhhhh, mmmmh, ok, ok, nimemkumbuka, yule shombe shombe?” akaulza.

“Huyo huyo,” ile sauti ikajibu.

“Ndiyo mzigo nimeupata, ni wewe ulituma?”

“Naam wewe wasema. Sasa Mheshimiwa ile ilikuwa ni bakshishi tu, ila leo tunaweza kuonana?” ile sauti ikauliza.

“Nitaonanaje na mtu nisiyemjua?” Tulabayo aliingiwa na shaka.

“Usijali, we njoo pale Bushtracker saa kumi na moja jioni,” baada ya kusema hayo tu ile simu ikakatika. Tulabayo akaduwaa kidogo kisha akaiweka ile simu mahala pake.

Muda wa kazi wa serikali ulipokwisha tu, Tulabayo aliingia katika gari yake ya afisi na kumtaka amfikishe katika eneo hilo. Ijapokuwa foleni ilikuwa kubwa kutoka Barabara ya Bibi Titi mpaka ile ya Ally Hassan Mwinyi, bado haikumkawiza kufika katika club hiyo iliy pembezoni mwa Barabara ya Bagamoyo.

Alipokanyaga tu eneo hilo tayari alipokelewa na mwanadada mrembo aliyepewa kazi hiyo, akaongozwa mpaka ukumbi wa ndani kabisa ambao waliingia watu maalumu tu. Mara alipingia ndani ya chumba hicho macho yake yaikutana na watu asiowategemea. Wafanyabiashara wakubwa wenye asili ya Kiasia na Kiarabu lakini kati yao kulikuwa na mtu mzito wa serikali, waziri katika wizara nyeti, hakuwa na haja ya utambulisho, aliwatambua wote naye alijiona wazi kuwa akifahamika.

Mheshimiwa Waziri Thomas Kalembo, alikuwa katuna kitini akimtazama Jaji huyo huku akikigeuzageuza kichwa chake.

“Usiwe na hofu Tulabayo, karibu sana, subira hii yote ni kwa ajili yako tu,” wakati anasema hayo, akabnya kitufe fulani, mwanadada mwingine akaingia na chano iliyojaa vinywaji vikali.

“Asante sana, nashukuru, ila sijaelewa juu ya wito huu,” akasema.

“Usijali, jana tulikupngeza kwa hundi ya Milioni kumi, na leo kwa ujio huu tu, tunakupa hundi ya Milioni Hamsini, hatuna nia mbaya ila twataka ufanane na sisi,” Kalembo akamwambia.

“Sijaelewa!” Tulabayo akajieleza.

“Kwa ujumla hiyo kesi uliyopewa ni ya kwetu, ninyi mmezoea kuwaona hawa mahakamani, lakini na mi pia nipo. Mhehsimiwa mimi na wewe kama watumishi wa serikali, inabidi tulindane asee, mzigo ule wa bandarini ni wa kwetu, kila kntena moja ya vipodzi ina thamani ya shilingi Billioni mia nane na hamsini, na zipo kontena tatu, nahitaji ufanye juu chini kadiri ya cheo na nafasi yako hii kesi ipinduke na ushindi uwe wetu nikimaanisha na wewe pia,” Waziri Thomas Kalembo alipkuwa akisema hayo mwanadada mwingine akaingia ndani ya chumba kile na trei ndogo ambay ndani yake kulikuwa na kitabu cha hundi, akakivuta na kuifyatua kalamu yake yenye ncha ya dhahabu, akasaini na kuandika jina la jaji huyo, Manfred Tulabayo. Akaitatua na kumkabidhi.

Mustafa akatafuta njia ya kuliacha jiji hilo ambalo sasa kwake lilikuwa kama kaburi linalomsubiri. Akilini mwake alifikiri kwenda kusikojulikana lakini bad kichwa kilimzunguka ni wapi anapoweza kufichama ilhali aweze kupata mawasiliano ya internet kwa ajili ya kujua nini kinaendelea.



07

NDANI YA BOEING 777

Sauti nyororo ya mwanadada mhudumu wa ndege hiyo ya shirika la Ethiopia iliwataka abiria wa ndege hiyo kufunga mikanda kwani tayari walikuwa wamewasili Dar es salaam na wako tayari kutua. Abiri 280 waliitikia witoa huo na kuanza kujiweka sawa, miongoni mwao alikuwamo kijana shababi, aliyevalia fulana nyeupe yenye mstari mmoja mpana mweusi katikati ya kifua chake na jinzi la buluu. Mwili wake mkakamavu uliojaa nyama kimazoezi haukuonekana kama una wasiwasi na hicho kinachotukia wakati huo. Alitupa jicho dirishani na kuona mandhari nzuri ya jiji la Dar kutoka juu, jiji linalosifika kwa amani.

“Home, sweet home!” akajisemea huku akiipachika miwani yake usoni na kuonekana yu maridadi maradufu. Safari hiyo ndefu iliyowachukua saa tisa angani ilikuwa ikifikia tamati dakika na nukta hiyo.

Nini nakikuta nyumbani? Alijiuliza. Na alipokuwa katika kujiuliza huko aligutushwa na mtikisiko wa ndege hiyo, akatupa jicho dirishani kwa mara nyingine, akaona jengo zuri la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere. Haikuwa na shaka kuwa wamefika, wamewasili na sasa ilikuwa ni mapambano tu na joto la jiji hilo. Baada ya kuruhusiwa kuteremka, kijana huyu alisubiri kwanza wengine watangulie kisha yeye akawa wa mwisho kufanya hilo.

Kamanda Amata, ndani ya jingo la ukaguzi wa mizigo haikumchukua muda kumaliza mchakato huo, nah ii ilitokana na kujulikana kwake kama mfanyabiashara, meneja wa kampuni ya AGI Investment. Ni mtumishi mmoja tu aliyekuwa akijua wazi kuwa Amata ni nani, na huyu aliwekwa hapo kwa kazi maalumu. Yeye alimjua Amata kama mtumishi katika idara ya Usalama wa Taifa Tanzania lakini pia hakujua kuwa kiumbe huyo yupo katika idara nyeti kabisa ya TSA, ‘Invisible’.

Nje ya uwanja huo, moja kwa moja alipita katika kibanda kinachotumika kuuza magazeti, akijua kuwa kwa vyovyote hapo atapata mapokezi yanayomstahili. Akiwa na begi lake dogo mgongoni aisimama kukodolea macho magazeti, na lile lililomvutia lilikuwa ni Mbalamwezi, halikuwako mezani bali muuzaji aliliweka ndani katika meza yake mwenyewe na juu kabisa liligongwa mhuri ‘HALIUZWI’.

“Una nakala ya Mbalamwezi?” akamuuliza huyo muuzaji.

“Aaaa bro, hiyo ni lulu kwa wiki hizi,” Yule kijana akajibu.

“Kwa nini?”

“Kuna habari nzito nzito kiasi kwamba saa tatu mpaka nne asubuhi huwa limekwisha,” akaeleza yule kijana.

“Asee! Basi naomba nakala yako hiyo japo nisome habari hiyo hapo…”

“Haina shaka kaka!” akampatia.

Amata alipekuwa kurasa mpaka ile anayoitaka na macho yake yakatua kwenye makala iliyoandikwa na Mustafa Bashiru juu ya ajali na kifo cha Jaji Shekibindu. Baada ya kuimaliza akajikuta maswali yale ambayo mwandishi huyo alikuwa ameyaandika ndani ya makala yake yanajijenga katika ubongo wake na kuanza kutafuta majibu ndani kwa ndani.

“Asante!” akamshukuru yule kijana na kumpa gazeti lake.

“Ulikuwa unamsoma Mustafa?”

“Yeah, ndiyo” akamjibu.

“Huyo jamaa ni noma sana kwa habari zake za uchunguzi, inasemekana alitekwa huyu wiki iliyopita…”

“Alitekwa?” Amata akadakiza swali.

“Ee aliokotwa huko bonde la Msimbazi akiwa hana fahamu, majeraha kadhaa hapa na pale, wiki mbili hakuwa gazetini,” yule kijana akaeleza kwa hamasa.

“Weeee! Sasa polisi wanasemaje?”

“Waseme nini, si hao hao wanausalama wtakauwa walimteka kama kawaida yao,” yule kijana akazidi kufunguka.

Kamanda Amata alinogewa na mazungumzo ya kijana huyo ambaye alimpa mpaka nakala ile ya habari kuingizwa kwa vipodozi. Ilimchukua takribani dakika arobaini na tano kuzungumza na kijana yule.

Saa tatu usiku ilimkuta bado yupo uwanja wa ndege, alipogundua hilo akaamua kuagana na rafiki yake huyo, kisha akaondoka zake na kuelekea mjini. Katika maegesho ya uwanja huo, gari zaidi ya mia tano zilikuwa zimesimama, nyingine zikiondoka baada ya kuchukua wageni na nyingine zikiingia kuleta wasafiri. Moja kwa moja akazipita gari kadhaa na kuiendea pic-kup moja ya rangi ya silver, Ford Ranger
 
RIWAYA: JANGA
MTUNZI Richard MWAMBE
SEHEMU 8

new model. Akaingia ndani yake na kuiwasha, ile gari ya kisasa ikawaka na kubaki ikiunguruma bila kufanya kelele kwa aliye ndani. Baada ya kuisubiri injini ikae sawa, akaiondoa katika maegesho na kuikamata barabara ya Nyerere kuelekea mjini.
“Ding-Dong!” kengele ya mlango mkubwa wa Madam S ilisikika, bila kujali alijua mgeni huy ni kati ya vijana wake kwa maana kengele hiyo ilikuwa maalumu kwao tu, kila momja alimpa rimoti ya kutumia mara tu akifika hapo. Akauendea mlango akiwa tayari katika vazi la kulalia ila juu yake alijifunga kitenge cha mwenge ili kujiuzuia maana nguo hiyo ilikuwa ya kitambaa laini kinachoangaza.
“We mwanaume, mbona unapenda kuja kwangu wakati wa kulala? Halafu husemi kama unakuja,” Madam akamwambia Amata mara tu alipoufungua mlango na kumruhusu kijana huyo kuingia ndani.
“Babu angekuwepo nisingekuja, sasa si hayupo ndiyo maana nimekuja,” akajibu Kamanda.
“Chizi mwenzio katoka hapa muda si mrefu, naingia kulala tu na wewe unagonga, haya habari za safari!” Madam akaendelea kuongea huku akiliendea jokofu kubwa lililo hapo sebuleni.
“Nashukuru, nimerudi salama! Sijui habari za hapa na poleni kwa msiba wa Shekibindu,” Amata akajibu.
“Tumepoa lakini michakato inaendelea kama nunavyojua…”
“Watu kazini?” Amata akadakiza.
“Kama kawa mwanangu,” akarudi mezani akiwa na mvinyo ya St. Rafael, “Unajua huyu jaji amekufa lakini bado kuna utata juu ya kifo chake…”
“Kwa nini?”
“Hilo sio swali,” akamjibu na kunyanyuka kisha akarudi na gazeti la Mbalamwezi, “unafikiri kifo hiki kinaendana na habari hii huku?” akamuuliza.
‘AJALI MBAYA YACHUKUA MAISHA YA JAJI SHEKIBINDU’ imeandikwa na Rebecca Masaka. Akaiangalia tu haraka haraka, akachukua gazeti lingine.
‘KIFO CHA JAJI SHEKIBINDU, NI AJALI ILIYOKUSUDIWA?’ nayo akaitazama kwa juu juu maana tayari alikuwa ameisoma, hii iliandikwa na Mustafa Bashiru. Akaweka pembeni na kisha akavuta lile la nyuma zaidi na kulitupia jicho.
‘VIPODOZI HATARI VYAINGIA NCHINI’ hii nayo iikuwa imeandikwa na Mustafa Bashiru, akaisoma harakaharaka na kuweka gazeti mezani.
“Ina maana Tanzania nzima ni gazeti hili tu ambalo imeandikwa habari hii?” Amata akauliza.
“No! mengi yameandika, ila Mbalamwezi wameandika vizuri zaidi, na kisa cha kuyakusanya ni kutazama muoano wake. Unaonaje?”
“Shekibindu ndiye alikuwa na kesi hiyo ya zile kontena za vipodozi, kama inavyosema habari hiyo kuwa amekufa saa kumi na sita kabla ya kusoma hukumu hiyo,” Madam akaeleza.
“Asee! Nina swali la msingi ambalo Madam S hujalishtukia…”
“Lipi?” akamkatiza.
“Habari ya vipodozi imeandikwa na Mustafa, na hii makala imeandikwa na huyo huyo, kwa nini hii ya ajali haijaandikwa na Mustafa?” akauliza.
Ukimya wa sekunde nne ukafuatia, kisha Madam S akakata ukimya huo, “swali zuri Kamanda, kweli sikuchunguza hicho”.
“Au mwandishi aliyeokotwa wiki mbili zilizopita ni yeye?” Amata akauliza, swali hilo likawa kama limemgutusha mwanamama huyo.
“Inawezekana! Maana wiki mbili hizo kuna mwandishi kweli ilivuma kaokotwa,” Madam akaongeza kusema huku akiendelea kunywa kinywaji chake.
“Hili swala inabidi kuliangalia kwa faida yetu, isijekuwa michezo ileee imerudi,” Amata akamwambia Madam S.
“Ni kweli, tulikwenda kwa mjane wa Shekibindu kumpa pole, tukajaribu kumhoji hili na lile labda tutaona au kuhisi nani wa kuanza naye katika hili. Kwa maelezo ya mkewe, anasema siku mbili kabla ya kifo chake aliamka usiku mnenen akiwa anaweweseka, akilalama kuwa kuna watu wanataka kumuua, baada ya kumhoji sana akasema kuwa mumewe tangu utoto alikuwa na ndoto za mtindo huo,” Madam akaeleza. Amata akasikiliza kwa makini sana maelezo hayo yote huku kichwa chake kikiunganisha matukio.
“Madam, hiki kifo au ajali hakina budi kufanyiwa uchunguzi, tena wa hali ya juu na wa siri sana, kama mwandishi huyu alitekwa basi ina maana anajua vitu vingi sana katika hili, na huyu ndiyo msaada wa kwanza kwetu kumpata ili tujue kipi ni kipo,” akatoa ushauri.
“Yeah! Ndiyo maana nilikuwa nakusubiri, idea is responsibility! Kuanzia sasa fanya kazi hiyo,” Madam akampa kazi Amata muda huo huo wa kulitazama tukio hilo kwa jicho la tatu.
“Kwa heri, ushaniuzi,” Amata akasema huku akinyanyuka.
“Subiri nikupikie,” Madam akamtania.
“We mwenyewe unakula hotelini, ndiyo unipikie mimi!” Akamjibu na kuanza kuondoka.
“Ukalale kwa Gina ee! Ila angalia usipotee maana nimemhamisha pale, sasa hivi anakaa Msasani karibu na Chiba” akamwambia.
“Tangu lini?”
“Siku tano zilizopita,”
“Ok bye! Huyo atakuwa disco tu saa hii, maana kwa kujirusha, hajambo,” Amata akamaliza kusema na kuondoka zake.
Kamanda akaondoka usiku huo na kuelekea nyumbani kwake Kinondoni huku kichwani mwake tayari akili yake ilikuwa ikiwaza jinsi gani kazi hiyo itaanza. Panga pangua kichwa chake kilianza kupanga kipi cha kwanza na kipi cha pili.
Pambazuko la siku iliyofuata lilimkuta Amata akiwa kandokando ya barabara ya Kinondoni akifanya mazoezi mepesi ya jogging na kujinyoosha hapa na pale. Akiwa katika zoezi hilo bado akili yake ilikuwa ikifikiri juu ya swala lile ambalo tunaweza kusema alilikuta mezani ijapokuwa hakukabidhiwa kama anvyokabidhiwa kazi nyingine.
Saa moja na nusu asubuhi tayari alikuwa nyumbani kwake akijiandalia staftahi inayomfaa, nukta hiyo hiyo kengele ya mlango ikagongwa kwa mtindo anaoufahamu, akaacha anachofanya na kuelekea huko mlangoni. Kama alivyfikiri akili yake haikuwa imemdanganya, Gina alisimama mlangoni.
“Karibu mrembo!” akamkaribisha na kumkumbatia msichana huyo kwa nguvu, “Nilikumiss dear!” akamwambia.
“Nami pia mpaka nilikuwa naumwa,” Gina naye akajibu.
“Umejuaje kama nimerudi?” akamwuliza.
“Nimekuta meseji ya simu kutka kwa mama mkwe,”
“Mmmmmmh na huyu mama mke wako sijui ana nia gani na sisi, jana kanilazimisha nije kulala kwak mi nikachomoa…”
“Aaaaa jamani kwanini, mwenzio jana nilikuwa napigwa na baridi, umenikatili,” Gina akajichomoa kwenye himaya ya Amata na kupita kuingia ndani ya nyumba ile. Amata akabaki kufunga mlango huku akimtupia jicho la wizi mrembo huyo ambaye asubuhi hiyo alivalia gauni refu mtepeto lililokuwa likimshika mwili hasa sehemu za makalio na kuufanya mwili wa rijai huyu kupata shida za kimaumbile.
Kishapo wote wawili walikutana jikoni na kusaidiana kuandaa stafutahi.
“Niambie mpenzi,” Amata akaanza mazungumzo.
“N’na la kukwambia basi! Hapa ni kifo cha Shekibindu tu tulifikiri tukifanyie kazi, mimi na Madam tulishaanza kudodosa mambo fulani, lakini tunajua kuwa umekuja basi harufu zote utazijua zinapotokea,” Gina akaeleza.
“Ninyi mlioanza ndiyo mmalizie muziki wenu, mi simo,”
“Haumo! Hata ukifa tutakufufua ufanye kazi,” Gina akaeleza.
“Kazi ya kifo cha Shekibindu waachieni polisi wa barabarani, wanalipwa hela nyingi sana kwa kazi hiyo,” Amata akajaribu kumkatisha Gina.
“Unasema tu, mama yako hajakwambia? Huu mzigo unaonekana mzito kaka,”
“Haijalishi, sasa nani kapewa kazi ya Shekibindu?” Amata akauliza.
“Jaji Tulabayo,” Gina akajibu.
“Ok, ila Shekibindu alikuwa anafaa sana katika hili”. Gina na Amata wakapata kifungua kinywa pamoja asubuhi hiyo huku wakizungumza hili na lile, wakichekeshana kwa hiki na kile.
“Sasa Amata!”
“Nini?”
“Niweke sawa mwenzio akili yangu inachizika,” Gina akaongea kwa kuegeza sauti huku akiung’atang’ata ulimi wake. Kamanda Amata akanyanyuka na kuondoka mezani hapo.
“Sa’ unaenda ‘api?” akauiza mrembo huy huku naye tayari amesimama.
“Kuoga,” akajibiwa.
Robo saa iliyofuata, Gina alikuwa ndani ya taulo kubwa juu ya kitanda kipana cha Amata, haikupita muda kijana huyo naye alitoka kuoga na kuungana na mrembo huyo, raha ya mahaba ikawameza hata wakasahau kazi.
“Breki ya kwanza wapi?” Gina akauliza wakiwa tayari barabarani kuelekea afisini.
“Kituo cha polisi cha kati, kwa Inspekta Simbeye,” Amata akajibu na Gina akawasha indiketa kunesha kuwa anaiacha Barabara ya Ally Hassan Mwinyi na kuchukua ile ya Bibi Titi kuelekea Mnazi Mmoja.
“Naona umeanza kazi!” Gina akachokoza.
“Hapana, nataka kumsalimia tu mzee huyu, na nafikiri kwa sasa atakuwa ndiyo kazeeka zaidi,” Amata akajibu na kumwacha Gina akiangua kicheko cha nguvu.
“Angalia na mbele sio unacheka tu,” Amata akasisitiza wakati huo Gina tayari alikuwa anaiacha Bibi Titi na kuchukua ile ya Uhuru kuelekea Mnara wa Saa. Dakika kumi tu gari iliegeshwa mbele ya kituo hicho cha polisi, wakateremka na kuingia ndani. Maafande wachache waliokuwa wakimjua Gina walimpa heshima yake kwa kubana mikono wakimsahau Amata kwa kuwa hawakumjua vizuri.
Mlango wa Inspekta Simbeye ulikuwa umefungwa lakini kutoka ndani ya afisi ile kulisikia sauti ya ukali.
Inspekta kachachamaa! Akawaza na kuugonga ule mlango mara tatu, kisha mara mbili, akamalizia mara moja.
“Pita ndani!” sauti ikasikika kutoka ndani ya afisi hiyo na Amata akanyonga kitasa na kuingia akifuatiwa na Gina. Wakampa heshima yake mzee huyo.
“Karibuni sana!” akawakaribisha, “We nenda, tutamaliza baadae,” akamwambia Yule kijana askari aliyekuwa akimfokea.
“Vipi tena mzee mbona unamfokea Constable?” Gina akaulza bila woga.
“Aaah! Vijana hawa wana matatizo kweli kweli,” akajibu huku akiwaonesha viti vya kuketi, nao wakafanya hivyo.
“Ndiyo kijana wangu, habari za siku nyingi…” Simbeye akamsabahi Amata huku akimtazama.
“Mi niko sawa, nikajua nitakukuta ushaacha afisi,” Amata akamtania.
“Namna hii, mi siyo wa kustahafu leo wala kesho, hawataki kabisa na kama unavyojua kilichoniweka hapa. Haya nambie maana hata mrembo wetu umemfundisha tabia mbaya ya kutokuja kutusalimia,” Simbeye naye akatania kisha wote watatu wakacheka.
“Mzee, faili lililpo mezani ni juu ya ajalia ya Jaji Shekibindu…”
“Imefanya nini?” Simbeye akajibu kwa kuikata kauli ya Amata.
“Kilichonileta hapa, ni kutaka kujua ajali ilikuwaje, nini kilipatikana katika eneo la tukio,” Amata akasema.
“Aaaaaa kazi mpya sasa hiyo, wiki mbili zimepita kijana wangu, gari ipo uani huko, ni ya kuikarabati tu,” akajibu.
“Mkewe hajaja kuichukua?”
“Alikuja kwa sababu alikuwa akifuatilia maswala ya bima. Gari haijaharibika sana , imebonyea tu huku mbele basi,” Simbeye akaeleza.
“Sasa kama ni hivyo hushangai kwa nini mtu huyo amekufa?”
“Kijana we si unajua kuwa hawa wazee wanakuwa na presha nyingin sana si ajabu mshtuko ule ndiyo umemwondoa,” Simbeye akajibu na kuruhusu ukimya wa sekunde kadhaa. Yule mzee polisi akainua simu yake na kupiga afisi nyingine akaomba kuletewa kabrasha la taarifa ya ile gari, dakika tatu tu kabrasha ile iiwasiishwa mezani na WP mmoja aliyeonekana mkakamavu haswa.
“Faili hili hapa, tazama mwenyewe,” akamwambia. Amata akalivuta na kupekua karatasi hii na ile, akatazama maelezo yote na kuyasoma kwa makini sana, akatazama mchoro uliyoonesha jinsi ajali ile ilivyotokea. Alipojiridhisha akalirudisha kwa huyo mzee naye akamkabidhi yue WP akaondoka nalo.
“Naomba niione hiyo gari,”
“Twende!” Inspekta akainuka na kundoka na Amata pamoja na Gina, wakazunguka uani na kuikuta ile gari ikiwa imewekwa kando.
“Kumbe ni gari binafsi?” Amata akauliza.
“Sasa ingekuwa ya serikali ningekwambia kuwa mkewe alikuja kuifuatilia, acha uchizi kijana!” Simbeye akamwambia Amata. Gina na Amata wakaitazama gari ile kwa kuizunguka zunguka huku akiwa na simu yake mkononi iiymuwezesha kupata picha kadhaa za gari hiyo. Iikuwa gari ya kisasa, Toyota GX 100 nyeupe, haikuharibika sana, mbonyeo mkubwa ulikuwa katika mlango wa dereva na boneti ilikuwa imefyatuka kiasi. Katika mbonyeo huo, Amata akagundua mabaki ya rangi ya gari ya pili iliyogonga hapo. Yalikuwa ni bluu nyeusi, akapiga picha hilo eneo na kuhakikisha hilo tabaka la rangi linaonekana vyema pichani.
“Gari iliyomgonga ilikuwa ya bluu,” Amata akamwambia Gina, mwanadada huyo akamtazama kisha akatikisa kichwa kuonesha kuwa kaelewa hilo analoambiwa.
Walipomaliza hilo wakaagana na Simbeye, wakarudi ndani ya gari yao na kama kawaida Gina akaketi kuume, nyuma ya usukani.
“Umejuaje kuwa gari iliyognga ni ya bluu?” Gina akauliza huku akiwasha gari.
“Siku zote ni asilimia tisini rangi ya gari la pili kubaki katika gari la kwanza na hapo utagundua japo rangi tu ya gari hiyo endapo ilitoroka,” Amata akajibu.
“Na hili lilitoroka?”
“Sasa si ungeliona au taarifa yake ungeiona kwenye lile jalada, lakini wameshindwa hata kujua japo rangi ya gari ya pili,” Amata akaeleza.
“Ingia hapo,” akamwamuru gina achukue barabara itakayowafikisha makutano ya Bibi Titi na Uhuru yaani Mnazi Mmoja, “Egesha hapo mbele ya duka la vitenge,” akamwambia dereva wake, Gina.
“Ok Boss!” akajibu na kufanya hivyo. Amata akatelemka.
“Unaenda wapi?” Gina akauliza.
“Eh mwanamke we! Naenda kunywa kahawa hapoo kwenye kona, we kachague vitenge,” akamjibu na kuachana naye. Katika moja ya kona hizo kulikuwa na mzee anayeuza kahawa siku nyingi tu, akajiunga na kuketi hapo. Akawalipia kahawa madereva taxi waliokuwa hapo na soga likaendelea.
“Mnajiamini nini kuketi hapa, maana gari ikikosa breki kule inawaishia ninyi,” Amata akawatania.
“Aaaa bro usiombe hayo, hapa Mungu tu,” mmoja akajibu.
“Kama ile iliyogonga gari ya Jaji, asee, ngoma ilikuwa inakuja kutu hapa hivi,” mwingine akadakia na ndipo hapo Amata alikuwa akipasubiri kwa hamu, akawadodosa vya kutosha na kupata habari nyingi juu ya ile ajali.
“Ile gari baada ya kugonga, ilipiga rivasi na kuondoka kwa kasi,” mmoja alieleza.
“Sasa, jaji alifia hapo hapo au ilikuwaje?” akazidi kuwachimba.
“Mwanangu, alifia hapo hapo,”
“Yule itakuwa mstuko tu, lakini kusema ajali ile imemuua! Aaaaa mi nakataa,” mwingine alidakia. Mazungumzo yale yalinoga lakini Amata hakuwa na budi kwenda, akawalipia wale vijana kahawanyingine na kashata kisha akarudi garini.
Gina naye alikuwa tayari kamaliza yake, alisimama nje ya duka akimsubiri kijana huyo.
“Twen’ zetu!” Amata akamwambia.
“Kalipe kwanza,” akajibiwa.
“Nikalipe nini?” Amata akauliza.
“Ukalipe nini! We si umenambia nikachague vitenge, nimechagua doti nne, unadaiwa elfu themanini kwa Mwarabu pale,” Gina akajibu.
“Mwanamke wewe, hutaniwi,” Amata akamjibu na kumpa hizo pesa.

ITAENDELEA…..
 
RIWAYA: JANGA

MTUNZI: richard MWAMBE





Gina naye alikuwa tayari kamaliza yake, alisimama nje ya duka akimsubiri kijana huyo.

“Twen’ zetu!” Amata akamwambia.

“Kalipe kwanza,” akajibiwa.

“Nikalipe nini?” Amata akauliza.

“Ukalipe nini! We si umenambia nikachague vitenge, nimechagua doti nne, unadaiwa elfu themanini kwa Mwarabu pale,” Gina akajibu.

“Mwanamke wewe, hutaniwi,” Amata akamjibu na kumpa hizo pesa.



SEHEMU YA 9



OFISI FULANI YA SERIKALI

Asubuhi hiyo iliwakutanisha Mheshimiwa Waziri Thomas Kalembo na Ngishu kama kawaida yao. Alinda alipewa agizo lile lile la kutokumkaribisha mtu kwa wakati huo, naye alitii.

“Mzee, Jamaa mji mzima hatujamwona!” Ngishu akatoa ripoti.

“Hajaonekana?” Kalembo akauliza kwa upole huku akimtazama kijana huyo wa Kihindi.

“Kabisa, maana vijana walisambaa kila kona, kila klabu, kila kwenye tukio labda wangemwona lakini wapi,” Ngishu akazidi kumnyong’onyeza Kalembo.

“Atakuwa wapi?”

“Swali gumu mzee,” Ngishu akajibu na kutulia kimya.

“Unajua huyu kijana keishakuwa mwiba kwetu, ina maana kagundua njama zetu?” Kalembo akawa na shaka.

“Sidhani, njama atazigunduaje na swala hilo tumeliongea wenyewe tu!” Ngishu naye akatia shaka katika wazo hilo.

“Kwake mlienda?” Kalembo akauliza.

“Oh kweli hatukwenda,”

“Pumbavu sana nyie, sasa mnategemea mtu kama yule kila siku mtampata klabu? Sasa tusiliongee hilo nendeni nyumbani kwake mkambane mkewe au yeyote ambaye mtamkuta ili mpate jibu. Baada ya hapo ndio uje tuongee sasa,” Waziri Thomas Kalembo akatoa maelekezo na muda huo huo yule kijana akaaga na kuondoka.

Hakutembea mwendo mrefu, jirani kabisa na Shule ya Sekondari ya Shaban Robert aliikuta Noah nyeusi imeegeshwa, akaifuata na kuingia ndani, kisha akafunga mlango nyuma yake na kuketi.

“Mnajua tumefanya uzembe sana,” akawaambia vijana wane aliowakuta ndani yake.

“Uzembe gani?” mmoja akauliza.

“Jana tumemtafuta sana Yule mshenzi lakini tumesahau kwenda kumcheki nyumbani kwake,” Ngishu akwaambia.

“Ndiyo hilo tulikuwa tukilizungumza hapa,”

“Aaaaah ok, sasa lifanyike hilo, tukambane mkewe au yeyote aliye nyumbani kwake tupate jibu,” Ngishu akaelekeza.

“Saa hii! Kwa nini tusiliache jua lichwee?” dereva wa gari hiyo akauliza kwa kujawa hofu.

“Muda, muda ndiyo tatizo. Washa gari Kebby twende,” akaamuru na mara injini ikaunguruma na ile gari taratibu ikaingia barabarani kupotea kwenye kona za mitaa hiyo.

Saa moja iliwatosha kufika eneo la Segerea, walipoipita baa ya Migombani wakakunja kulia na kusimama mbele kidogo ya nyumba ya Mustafa Bashiru.

“Lazima watakuwepo!” Yule dereva akawaambia wenzake mara tu baada ya kuona nje ya nyumba hiyo kuna gari imeegeshwa, Ford Ranger.

“Ila tahadhari lazima, maana hujui ndani wapo watu wangapi…”

“Hapana, msiende sasa hivi, subirini ile gari iondoke kwanza kisha ndo mwende,” Ngishu akawaambia na wote wakaafiki.

“Sasa kama na yeye akiondoka je?”

“Si tutamwona hapa, tutamfukuzia ikiwezekana tunafanya mchezo uleule na kazi inakuwa imekwisha,” Ngishu akamjibu kisha wote wakatulia wakikodoa macho kutazama upande huo. Walikaa kimya ndani ya gari ile na baada kama ya dakika tano hivi waliwaona watu wawili, mwanamke na mwanaume wakitoka ndani ya nyumba ile wakaingia katika ile gari na kuondoka zao.

“Let’s go!” Ngishu akawaamuru na ile gari ikapiga rivasi mpaka jirani na ile nyumba. Kebby na mwenzake wakateremka na kuiendea mpaka mlangoni. Wakagonga mara kadhaa, kimya. Wakajaribu kuufungua, haufunguki. Wakazunguka huku na huko, hakukuwa na dalili yoyote ya mtu katika nyumba hiyo. Wakatoka na kurudi garini.

“Vipi?” Ngishu akauliza.

“Hakuna mtu wala dalili,” Kebby akajibu huku akijiweka sawa kitini. Ngishu akashusha pumzi ndefu na kugeuka nyuma kuwatazama vijana wake.

“Ina maana kaztuzidi kete au?”

“Itakuwa!”

“Toa gari, twende tukaegeshe karibu na ofisi yao, atazunguka kooote lakini lazima aje ofisini, tutaanza naye hapo,” Ngishu akasema.

“Ok!”

Ile gari ikaondolewa kwa kasi na kurudi mjini.

“Mi n’na swali,” Kebby akauliza.

“Swali gani?” kijana mwingine akauliza.

“Kama Mustafa ametoroka, ni nani kamjuza kuwa tunamtafuta?” swali hilo lilikuwa kama limewagutusha ndani ya gari ile.

“Nawaza hicho kitu muda mrefu sana, lakini sipati jibu, lazima kuna mmoja ambaye katusaliti, tutalijua hilo kesho, endapo leo tutamkosa tena,” Ngishu alimaliza kwa kusema hayo wakati ile gari ikiegeshwa upande wa pili wa barabara ya Nkurumah. Wakati dereva akiiweka vyema pale kwenye maegesho Keby alimgusa begani Ngishu na kumwonesha kitu fulani upande ule wa pili. Ngishu akapiga macho upande ule, akaiona Ford Ranger ya kijivu ikitoka eneo lile na kuikamata Barabara ya Nkuruma kuelekea Mnara wa Saa.

“Hii si tumeiona kule Segerea?” Ngishu akauliza.

“Ndiyo, nahisi wana uhusiano na Mustafa,” Kebby akajibu.

“Yeah, fanya hivi, Kadoda na Bundala, bakini hapa, mtupe taarifa yeyote ambayo itakuwa ya muhimu kwetu, Kebby na Boi twendeni, ifuate hiyo gari tuone inaishia wapi,” Ngishu akawaambia nao wakafanya hivyo.

“Kuna gari inatufuata!” Gina akamwambia Amata huku akizungua Mnara wa Saa na kuikamata barabara ya Samora.

“Usisimame afisini, waoneshe kuwa wewe ni dereva mzoefu hivyo wasikufuate,” Amata akamwambia Gina. Gina akavuta mafuta na kuziovateki gari kama tatu hivi kisha akakunja kona moja mbaya kushot na kukatiza mbele ya gari nyingine. Breki za dharula zikasikika, honi na kelele za huku na kule, mwanadada huyo tayari akawa keshakamata Barabara ya Morogoro kuelekea Magomeni. Mtaa wa kwanza, wa pili, wa tatu, Gina akawasha indiketa ya kushot na kuingia kwenye kijimtaa hiko. Akapenyapenya na kuibukia barabara ya Kitumbini, akakunja kushot tena akaibukia karibu kabisa na duka la Jeshi la Magereza kisha akaikamata ena barabara ile ile ya Samora.

“Wakinikamata mi naacha kazi,” akamwambia Amata huku akiingiza gari yake katika maegesho ya juu ya jingo la JM Mall.

“Sawa mama!” Amata akajibu. Mara baada ya kuweka ile gari vizuri wakaingia ofisini na kilamtu akachukua nafasi yake.

Asubuhi ile mara tu baada ya kutoka kuongea na wale madereva taxi pale Mnazi Mmja, Amata na Gina waliamua kumfatilia Mustafa Bashiru wakiwa na waz moja tu, wampate awaeleze kile ambacho anakihisi katika sakata lile. Walipofika afisi ya gazeti ya Mbalamwezi wakapata taarifa kuwa Musatafa hakuonekana siku ile, wakauliza mahala anapoishi wakpewa ramani ambayo iliwapeleka bila shida, lakini nako walikuta jumba halina mtu. Hofu waliyoipata ndiyo iliyowarudisha tena pale afisi ya lile gazeti na kukutana na Mkurugenzi ambaye sasa naye aliingiwa na hofu juu ya mfanya kazi wake mahiri. Wote hakuna aliyekuwa akijua nini kimempata kijana huyo, si Mkurugenzi wala Amata na Gina. Kutoka hapo sasa, Amata, damu ilimchemka, kila alipokumbuka kuwa mtu huyo alitekwa ndani ya siku hizo hizo haikumpa amani hata kidogo.

“Gina, lazima Mustafa apatikane, huyu atakuwa ufungu wa jambo hili,” Amata akamwambia.

“Yeah, sure!” Gina akajibu huku akichezea simu yake.

“Sasa tunafanyaje?”

“Sijui, lakini sasa naona kazi hii ina utamu wa pekee sana, lazima ivaliwe njuga,” Amata akasema. Wakati uo huo simu yake ikaita, akaichukua na kuitazama kwenye kioo. Madam S alikuwa akipiga.

“Yes Madam!” akaitika.

“Afisi ndogo tafadhali,”

“Ok!”

08

Jaji Tulabayo alimtazama Bwana Ankit Singh na mwenzake Suleiman Kabba walioketi katika mkao wa huruma. Kesi yao ilikuwa ikitarajiwa kusomwa tena ndani ya saa sabini na mbili.

“Msiwaze, mnachotakiwa kufanya ni hicho nilichowaeleza,” akawaambia.

“Tumesikia, tutahakikisha linawezekana,” wakajibu na kusimama tayari kuondoka.

“Hakikisheni mnanipa jibu leo,” akawasisitizia kisha mlango ukawatenganisha na kumfanya kila mmoja kubaki upande wake.

Watu walikuwa wakisubiri kwa hamu muendelezo wa kesi hiyo, walikuwa wakitaka kujua hasa ni nini ambacho Jaji Tulabayo atawafanyia Walalahoi. Alipanga makabrasha yake kuhakikisha yako tayari. Tafutishi alizozihitaji kutoka kwa wapelelezi wa serikali zilikuwa zimekamilika. Baada ya kubaki peke yake akachakurachakura yale makabrasha, akapitia hiki na kile kisha akaandika mambo yake pembeni na wakati huo karani wake akaingia na kumpatia faili moja.

“Umekamilisha?” akamwuliza

“Ndiyo kila kitu kipo tayari,” akajibu na kumkabidhi kisha yeye akaondoka zake na kumwacha Mheshimiwa huyo, kama alivyozea kuitwa, akiendelea na mambo yake mle ofisini.

Amata na Gina walifika afisini kwa Madam S na kumkuta kajaa kitini kama kawaida yake, wakaingia na kuketi vitini wakisubiri kuambiwa kile walichoitiwa.

“Tumefika!” Amata akasema.

“Hata mi nawaona, haya nipeni ripoti yenu, mmefikia wapi na mmenusa nini?” akawauliza.


ITAENDELEA
 
RIWAYA: JANGA
MTUNZI: Richard MWAMBE
SEHEMU YA 10
“Hata mi nawaona, haya nipeni ripoti yenu, mmefikia wapi na mmenusa nini?” akawauliza.

Endelea

Gina akasimulia kila kitu kuhusu asubuhi yao jinsi ilivyoenda mpaka kufikia hapo, Madam S alifurahi sana.
“Naona mshafika mahala patamu, sasa kazi inayobaki ni moja, ninataka nijue hukumu ya Shekibindu iliandikwa nini, maana kesho kutwa hii kesi inaendelea, na si hukumu tena, hapana, ila inarudi nyuma ili naye huyu Tulabayo apate kujua kama ni hukumu basi ahukumu vipi,” Madam akawaeleza.
“Naelewa, lakini mpaka sasa umeona kuwa hii ishu tumeichunguza tu upande huu wa magazeti, hatujaingia zaidi upande wa hawa wanaotuhumiwa ili kujua hasa ukweli upo wapi,” Amata akaeleza.
“Kwa hiyo unasemaje?” Madam naye akatupa swali.
“Nafikiri sasa inabidi tuwachunguze hawa, mmoja mmoja kisha tujumuishe mambo. Lakini bado nina wasiwasi na upotevu wa huyu Mustafa, maana kila aliye jirani naye hajui kinachoendelea juu yake, nyumbani hakuna mtu,” akaeleza zaidi.
“Kwa nini mnamtaka Mustafa?” Madam S akauliza.
“Kwa sababu, hili fukuto hata sisi tumelinasa kutokea kwenye kazi yake, sasa hapo kiukweli yeye ana jambo kubwa la kutueleza,” Gina akatoa jibu kabla ya Amata.
“Gina yuko sawa!” Amata akaongezea.
“Ok, hii ishu inahusisha watu wawili, mmoja Mhindi na mwingine Mwarabu,” Madam akawaambia kisha akawapatia picha za watu hao, “Mmewaona?” akawauliza.
“Yeah!” Amata akajibu.
“Mnawajua?” akawachapa swali lingine.
“Aaaah kuna mtu asiyewajua hawa? Suleiman Kabba na Ankit Singh…”
“Mabingwa wa kutoa rushwa nchini,” Gina akadakiza sentensi ya Amata.
“Safi, nataka muwafuatilie hawa jamaa na shughuli zao. Kama anavyosema Gina, kama ni kweli kuna kontena zao zimeingia na bidhaa hizo za sumu zipo dukani, je zimeingiaje? Zimepitaje bandarini? Hiyo ndiyo kazi nataka Gina na Amata muikamilishe kabla ya siku ya kesi yaani mna saa kama thelathini hivi,” Madam akawaambia.
“Haina tabu, hilo litakamilika tu tena mapema sana!” Kamanda Amata akasema huku akiwa tayari wima.
“No! Madam, Mustafa hajulikani alipo, hivi kama ametekwa unafikiri tukiacha kufanya uchunguzi juu yake si tutaokota maiati? Mi nafikiri tuendelee kwanza na huyu ambaye tunahisi yuko hatarini zaidi, hawa magabacholi operesheni yao wala haihitaji nguvu,” Gina akapinga agizo la Madam S. Amata akamkazia macho msichana huyo kwa jambo hilo, si kwamba alifanya vibaya bali alimtangulia mbele kimawazo.
Madam S akatulia kimya kwa sekunde kadhaa kisha akawatazama wote wawili kwa zamu.
“Ok! Yote mawili mkayafanye, ndani ya muda niliyowapa hakikisheni muwe mmekamilisha,” akaongeza jukumu.
“Sawa!!” wakajibu na kutoka ofisini mle.
Ngishu akaangaza macho yake huku na kule hakuiona ile gari, “Una uhakika kuwa imepita hapa?” akamuuliza Kebby.
“Imeingia hapa, nina uhakika kabisa nimeiona…”
“Yaani kwenye jingo hili?” Ngishu akauliza ili kuwa na uhakika zaidi.
“Ndiyo,”
“Ok, panda huko juu tutaliona tu kisha tutakachokifanya tunajua sisi,” Ngishu akamwambia dereva naye akavuka barabara ya Samora na kufuata lango la kuingia katika maegesho ya jengo la JM Mall. Ile Noah ikaendeshwa polepole kupanda ghorofa ya juu, ikapita maegesho namba moja hawakuiona ile gari, walipofika ghorofa ya tatu, wakaikuta imeegeshwa.
“Ile paleeee!” Kebby akasema kwa shauku, wakasogea mpaka pale na kusimama, Ngishu na Kebby wakashuka na kuiendea, wakazunguka na kuipiga picha vibao vya namba na mambo mengine.
“Toa upepo,” Ngishu akamwambia Kebby, kijana huyo akachomoa kisu kidogo na kukikunjua kisha akachoma kwa nguvu kwenye kila tairi na dakika hiyo hiyo tu ile gari mpya kabisa ikasimamia rim huku mipira yake ikiwa haina upepo. Waliphakikisha wamekamilisha hilo wakaondoka za na kurudi kwa wenzao pale karibu na afisi za Mbalamwezi.
“Vipi?” Kebi akawauliza akina Kadoda wakati wakiingia garini.
“Hajaonekana wala wanaomjua hawajamuona,” Kadoda akaeleza.
“Ok, sasa ninyi endeleeni na mawindo, kila mnaloliona haliko sawa mnipe taarifa,” Ngishu akashuka kwenye ile gari na kuchukua tax, akaondoka zake.
“Wewe muwahi Ankit mimi nimuwahi Suleiman kisha tuwasiliane saa mbili usiku,” Amata akamwambia Gina na kutoka hapo kila mmoja akakamata njia yake.
Katika eneo la BP Kurasini, foleni ya magari ilikuwa kubwa na haisogei, Gina alitulia akiangalia kila gari inaykuja kutoka upande ule wa Kurasini, alihisi anaweza kumuona Ankit akitokea upande huo maana ndipo ofisi yake ilipo. Alipoona nusu saa nzima imekatika yuko pale, akainua simu yake na kupiga kwa Inspekta Simbeye.
“Enhee binti, wasemaje?”
“Nipo hapa BP kuna foleni kubwa sana, nipo kikazi na muhimu naomba msaada wako ova!” akakata simu na kutulia. Haikupita dakika mbili, pikipiki ya polisi ikapita kasi upande wa pili ikielekea Kurasini na dakika tatu zilizofuata ile foleni ikaanza kutembea na Gina aliwasili pale anapopataka, akaegesha gari na kutulia akijipa moyo kuwa kwa kuwa muda wa kufunga afisi bado basi mtu huyo kwa vyovyote atakuwa ndani.
Kwa nini nisiitembelee afisi yake? Akajiuliza. Na sekunde nyingine zilizofuata zilimkuta tayari kwenye ngazi akipanda kuelekea juu kama alivyoelekezwa na askari mlinzi.
Ankhit Singh, maandishi hayo ya kujinyonganyonga yalimkaribisha katika mlango mkubwa wa alluminium, akausukuma na kukutana na katibu wa afisi hiyo.
“Nina shida na Mr Ankhit, sijui hapa ni afisini kwake?” akauliza kana kwamba hajui anapotakiwa kwenda.
“Ni hapa, ila kwa sasa ana kikao, naomba uje kesho, samahani sana dada,” Yule katibu akamwomba radhi Gina.
“Bila shaka, basi nitakuja kesho asubuhi sana kumwona maana nina shida naye ya kibiashara,” Gina akaeleza.
“Oh vizuri nitampa taarifa lakini nimwambie kutoka wapi?” yule dada akamhoji Gina
“Mimi natokea AGI Investment,” akaeleza huku akitoa kadi ya kibiashara na kumpatia mwanadada huyo, wakaongea kirafiki kisha wakaagana.
Akiwa katika ngazi za kutoka nje simu yake ikaita, akaichukua na kuiweka sikioni.
“Washenzi wamepasua mipira, gari haina upepo!” Amata akang’aka simuni.
“What? Ina maana wametujua,” Gina akaongea mara hii kwa kushusha sauti.

SOMA RIWAYA YA JANGA KWA S 4000 TU. LIPIA SASA KWA MPESA 0766974865 UJIPATIE NAKALA LAINI
“Aaaa shiiiit, tutaongea baadaye,” simu ikakatika. Gina akaingia katika gari na kuketi sawia akisubiri tajiri huyo kutoka afisini. Ilimchukua saa nzima kumwona kwanza yule mwanadada akitoka na kuondoka kisha robo saa baadaye, akatoka mtu ambaye Gina alimfahamu vyema. Meneja wa idara ya kukusanya ushuru wa forodha Tanzania na nyuma yake tu akaibuka Ankith. Hawakuonesha kama wana uhusiano lakini hii kwa Gina ikagonga kichwa. Akachukua kamera yake na kumpiga picha mpaka akiingia garini na kuondoka. Kisha akarudisha macho kwa Ankit na kumuona akiingia katika Jaguar ya rangi ya bluu na kuondoka. Naye akasubiri kidogo kisha akaingia barabarani na kuifuata taratibu. Ankith alipita Kurasini BP akazunguka mzunguko na kukamata barabara ya Railway na kuibukia Psta ya zamani, alipofika kwenye benki ya NBC akakinja kushoto na kuchukua Barabara ya Maktaba. Gina naye alikuwa taratibu akifguata nyayo zizo hizo.
VINGUNGUTI
Upande wa viwanda Kiwalani, Kamanda Amata alitulia kimya katika gari nyingine ya kukodi baada ya ile aliyokuwa akiitumia kutobolewa mipira. Darubini yake ikiwa machoni mara kwa mara alikuwa akiangalia upande wa pili wa barabara ile ambao ulijulikana kwa jina Vingunguti.
SuleiAnkhit Pharmaceutical, kiwanda cha kutengeneza madawa ya binadamu lakini kinyemela ilikuwa ikiingiza vipodozi na kuvisambaza kwa matumizi ya binadamu. Mara hii kontena za kutosha zilifika bandarini kwa meli ya Santorini. Baada ya chache kuweza kutoka, vipodozi hivyo vikagundulika kuwa na kemikali mbaya za sumu nah ii ilijulikana baada ya akina mama na wasichana kadhaa kupoteza maisha kwa ugonjwa mbaya wa ngozi ambao haukujulikana tiba yake.
Kontena zilizobaki zilizuiwa bandarini kwa uchunguzi, watu wakapiga kelele, waandishi wakaandika, hapo ndipo Mustafa Bashiru alipopata umaarufu kwa kisa hicho, alichimbachimba, akaweka vitu hadharani, Watanzania wakafunguka macho. Vipodozi hivyo vyenye sumu viliingiaje madukani? Wakajiuliza. Kwani serikali na idara ya ukaguzi wa ubora wa bidhaa za kutumia binadamu zilikuwa wapi wakati haya yote yakitokea? Maswali hayo na mengine mengi hayakupata majibu. Mahakama ikaamuru kontena hizo zisiingie kwenye mzunguko wa matumizi ya binadamu, kesi ikaunguruma, ikiwa hukumu inakaribia, Jaji aliyekuwa na dhamana ya kesi hiyo akafa kwa ajali ya gari pale Mnazi Mmoja, utata.

ITAENDELEA ……
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom