bobefu zoefu
JF-Expert Member
- Feb 15, 2018
- 565
- 419
Hiv huyu remi si ndiye yule mdada alietokea Rwanda akafikia nyegezi mwanza
Sent using Jamii Forums mobile app
RIWAYA; URITHI WA GAIDI
NA; BAHATI MWAMBA
SIMU; 0758573660
SEHEMU YA KUMI NA NNE
“hakuna mlinzi anaeweza kutembea katikati ya mvua kubwa hii” Alijisemea!!
Ndipo alipoamka na pia akahisi kitu kikiwaka na kuzima kichwani kwake.
Akakitoa kifaa kile na kukibonyeza kikaacha kumweka.
“tatatata…ti….tatatata..ti..”
Bado aliendelea kusikia sauti ile na sasa ilizidi kukaribia kwenye hema lake.
Roho ikamdunda!!
Kule nje yule bwana aliendelea kuhangaika kutafuta mwelekeo wa mawimbi na bado alijua mawimbi yale yalitokea kwenye moja ya mahema aliokuwa amesimama kati yake.
Akawa anapiga hatua moja mbele na hatua moja nyuma,yani bila kutoka pale alipokua lengo likiwa ni kujua mweleko sahihi wa mawimbi mageni.
Hatimae alijua ni upande gani mawimbi yale yalikuwa.
Honda nae kule ndani alikuwa amesimama karibu kabisa na mlango na kwa kusaidiwa na mwanga wa radi, aliweza kuona mtu akiwa hatua chache kutoka mlangoni kwake na alikuwa anahangaika huku na huko.
Honda akili ikamjia na haraka akawasha kidubwasha kile na kukirudisha ndani ya kikasha cha risasi kisha akaruka hatua kubwa na kuangukia kitandani na kulala.
“Aisee hawa watu wana mitambo yenye nguvu sana” Alijiwazia huku akimalizia kujifunika shuka.
Dakika moja badae, yule bwana aliingia mule ndani na bila kujali kama alikuta mtu au la, yeye aliendelea kukagua hapa na pale.
Hatimae kile kifaa kilianza kutoa mlio mkubwa mfululizo na Honda akaamka na kukutana na kisu kikiwa shingoni mwake.
“ulikuja kutupepeleza sio? Alihoji yule bwana huku akitumia mkono mwingine kuwasiliana kwa simu ya upepo.
Hazikupita dakika tatu wapiganaji zaidi ya sita wenye mitutu waliingia mle ndani na kumweka kati Honda.
Isa nae akaingia.
Yule bwana akampa maelekezo kwa lugha ya kienyeji na kisha akamwonesha kifaa kile chenye muundo wa risasi alichokikuta kwenye viatu vya Honda.
“Hii si ni ile ya kule melini?” Alihoji Isa huku akimtizama Honda.
“Ndo yenyewe! Kwani kuna nini mbona navamiwa usiku huu? Alihoji Honda.
“Aah ni usalama tu unazingatiwa ila usijali” Alisema Isa huku akiwapa ishara wapiganaji wake nao wakashusha silaha zao.
“Wale wazungu walikuwa ni mamluki na tulikuwa sahihi kuwapoteza, walituwekea mtego wa kujua tulipo aisee” Alisema Isa huku akimwangalia Honda ambae wakati huo alikuwa anafanya jitihada za kunyanyuka kitandani.
Isa aliongea na vijana wake kuwaelesha na kisha wakasambaratika mle hemani na kukiharibu kifaa kile.
Honda alipumua kwa afueni na kurudi kujilaza na hakulapua lau tone la usingizi hadi ilipotimu ahsubuhi.
***
Ahsubuhi ilikuwa na mengi ya kufanya kwa pande zaidi ya tatu.
Honda na wapiganaji wa AIAI waliamka wakiwa na lengo moja la kufanya mauaji katikati ya Mogadishu huku wadunguaji wakifanya zoezi kwa ajili ya kukamilisha kazi yao mida ya jioni ya siku hiyo.
Upande mwingine ulikuwa ni ule wa Zedi Wimba na Haji Makame ambao wao lengo lao lilikuwa ni kuvuruga mipango ya wauaji na kumuokoa Rais bila uwepo wao kujulikana popote.
Kundi lingine lilikuwa ni kundi la ulinzi na usalama wa viongozi wote watakao hudhuria mkutano huo na bila kujua lolote linalopangwa, wao waliendelea na taratibu zao kama kawaida kuhakikisha usalama upo kwa asilimia zote.
Hatimae wakati uliwadia!!
Maeneo yote yalikuwa na ulinzi wa kutosha kuhakikisha eneo la Lamada na viunga vyake lipo salama.
Misafara ya viongozi mbalimbali ilianza kuwasili kwenye hotel Lamada.
Aliingia Rais wa Somalia kisha akafuatia Rais wa Kenya na wajumbe wake.
Katika majengo matatu yaliokuwa yanatazamana na hotel ile, kulikuwa kuna makundi mawili yenye malengo tofauti.
Kundi la kwanza lilikuwa lile la wadunguaji ambao kila mmoja alikuwa amekaa sehemu yake kuhakikisha mlengwa wao hawamkosi na walitaka kufanikisha azima yao hiyo wakati rais huyo atakapokuwa akitoka ndani ya hotel.
Kundi lingine lilikuwa ni lile ambalo lilikuwa na watu wawili tu na wao walikuwa kwenye chumba cha hotel nyingine wakiwa na chupa yao iliokuwa na unga wa chupa nyingine na vitu vingine kadhaa ambavyo vingehakikisha sauti iliokusudiwa inatoka.
Walikaa wakihakikisha kabisa kila tukio linaloendelea kule chini linatazamwa na wao mubashara bila kukosa hata nukta.
Muda wa kuanza kikao ulianza na watu mbalimbali walikuwa wapo na radio zao wakisikiliza.
Waliongea viongozi kadhaa na hatimae wakati rais wa Kenya anataka kuzungumza; Zedi na Haji walikonyezana.
Na hatua iliofuata ilikuwa ni kufungua dirisha kisha wakapachika chupa ya bia kwenye mdomo wa bunduki aina ya gobole kisha wakafyatua kuelekea kule ilipokuwa Lamada hotel na kilichofuata ni sauti kubwa ilioambatana na moshi mzito.
Ilikuwa ni taharuki iliozuka,walinzi wa viongozi hawakujua kimetokea nini na harakati zao zilikuwa ni kuhakikisha hakuna madhara yanayotokea kwa viongozi hao.
Wadunguaji nao walibaki wakiwa wamebutwaika wasijue kilichotokea.
Isa ambae alikuwa karibu ya eneo la tukio na Honda; walishuhudia mtafaruku usiosemekana.
“Shukeni wote, na msiache alama” Isa alitahadharisha vijana wake kisha akaondoa gari na wakarejea porini huku wakiwa wameshindwa kuekeleza mpango wao.
Zedi na Haji nao walikuwa wako mbali na eneo lile huku wakiwa wanashingilia ushindi wao kwa kuvuruga mpango ule ambao hawakuwa na hakika kama walikuwa sahihi,ila walijua wamefanya kile walichopaswa kufanya.
Na kazi ikabaki ni kumtafuta Imamu Shafi’I wa msikiti wa Masjid nuur.
***
- TANZANIA-
Ahsubuhi ile ilikuwa ni ahsubuhi mbaya kabisa kwa Remi.
Alilia peke yake na kulikuwa hakuna wa kumsaidia wala kumuonea huruma.
Alilia na Mungu wake.
Nchi nzima kulitapakaa taarifa zake na picha zake, mitandao ya kijamii ilikuwa ndio taarifa kuu.
Alikuwa amesahau kuzima simu yake na mara ikaita.
Namba zilikuwa ni za Kagoshima.
“Nadhani kuna haja ya wewe kujisalimisha kituoni”
Alisema Kagoshima.
“Muda ukifika nitafanya hivyo ila sio sasa” Alijibu kinyonge Remi.
“Ila tambua serikali ina mkono mrefu itakufikia tu” Alisema Kagoshima.
“Haina shida” Alijibu Remi na kukata simu.
Alishusha pumzi na kuzishusha, alihitaji kuhama pale mana si pahali salama tena kwake.
Walikuwa na nyumba nyingine mwananyamala kisiwani.
Wakati anatoka kwenye ile nyumba alihisi hayuko peke yake,licha ya kujifunika kanga juu hadi chini.
Licha ya kuhisi huko lakini kamwe hakuona mtu mwenyewe yupo umbali gani nae mana watu walikuwa ni wengi nyuma yake.
Alichukua bodaboda na kwenda kushukia komakoma na kuanza kutupa tena miguu yake kwa hatua za mashaka tele.
Hakufika hata mbali, alihisi kitu kidogo kikipenya kwenye shingo yake na kilichofuata hakujua licha ya kuhisi akiangukia mikononi mwa mtu.
Remi mbio zake ziliishia ukingoni.
***
Tukutane wakati mwingine
Sent using Jamii Forums mobile app