Riwaya: Genge

GENGE
EP20

KICHWA CHA MADAM S hakikupata wasaa wa kutulia. Jambo gumu na kubwa liliendelea kumsumbua kichwani.
Tunakwama wapi? Akajiuliza. Usiku huo alilala chali kitandani, akiwa na vazi la kulalia tu. Taa yenye mwanga wa rangi ya orange iliyowekwa kwenye meza ndogo ilikijaza chumba hicho kwa uhafifu wake. Ungeweza kumletea usingizi, lakini kwake haikuwa hivyo, tuli, alitulia. Alihakikisha ananyamazisha kelele zote ubongoni mwake ili achambue kimoja baada ya kingine.
Mwanamama huyu alikuwa mbobevu sana katika maswala ya kijasusi, daima alijua anachofanya. Uongozi wake katika kitengo cha siri cha serikali ulitambulika vyema na Mkuu wan chi, aliheshimika kwa siri vilevile. Kazi yake ilionesha matunda. Vijana wake hawakumwangusha. Mpaka siku hii alipojilaza kitandani, uzee ulikuwa unapiga hodi. Mvi zilikijaza kichwa chake na kumfanya awe mrembo maradufu. Hakuwahi kuolewa. Ijapokuwa alikuwa na mabwana wa hapa na pale ili kukata kiu yake ya kike, bado hakuwahi kupata mtoto. Si kwamba alikuwa tasa, la, ila majukumua na kazi yake vilimfanya aepuke kushika mimba. Haya yote yalimpa mawazo mengi kadiri umri ulivyokuwa ukienda. Watoto pekee aliyewaona ni wake ni vijana wa TSA na si wengine. Aliwaita wanangu, nao wakamwita mama.
Akili ya Madam S ilizimika na kuacha giza nene katika ubongo wake. Hii alijifunza huko Mongolia katika pitapita zake za mafunzo ya Kiintelijensia. Akarudisha kumbukumbu moja moja za nyuma. Kumbukumbu zake zikamrudisha alipokuwa na umri wa wastani. Siku alipopokea barua ya kutakiwa kuripoti Ikulu katika kitengo cha usalama.
Alipokelewa na watu wawili wacheshi ambao aneweza kumwita mmoja baba na mwingine baba mdogo. James Msambamagoya na Chameleone, walimpokea, wakampa ofisi na kumsimamia kwa ukaribu sana katika kazi waliyompa. Selina akafanya vizuri, aliweza kuratibu vyema safari za ndani za Rais, kupanga makabrasha na mambo mengine ya kiitifaki. Alimheshimu sana Chameleone kwa jinsi alivyokuwa akipanga mambo yake. Akajitahidi kujifunza na kuiba mambo kadhaa. Akafanikiwa. ‘Binti Chameleone’ wakampa jina. Kwa sababu mwishowe alikuwa na tabia kama za mzee huyo. Hakuwa na ukaribu sana na James Msambamagoya, kwa kuwa alimtaka kimapenzi mara kadhaa.
“Sikiliza binti… nakupa kazi ya siri, na uifanye kwa umakini”. Sauti ya Chameleone ilimrudia kwenye kumbukumbu zake.
“Nahitaji umfuatilie au umchunguze James… ila uwe makini sana asijue hili. Nataka unambie, akimaliza kazi hupendelea kwenda wapi, na nani ikiwezekana nipe hata orodha ya marafiki zake anaokutana nao mara kwa mara.” Agizo.
Madam S aliikumbuka siku hii, jinsi alivyoweza kumfuatilia mwanausalama huyo. Aligundua kuwa, baa aipendayo ni Banana. Aliwatambua marafiki zake, aliokuwa anakunywa nao. Wanajeshi. Sura zao aliziona mara kadhaa walipokuwa wakija Ikulu kwa kazi maalumu. Alivuta sura ya mmoja mmoja, alikumbuka wapo waliofungwa kwa kesi ya uhaini, wengine walitoroka. Kati ya waliotoroka alikumbuka Mwanachia aliyejulikana kwa jina la Chatu, alikwishauawa. Alimkumbuka Mwakibinga naye alikwishauawa kwa mkono wa TSA. Bado wawili.
Yuko wapi aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wakati ule? Ambaye iligundulika kuwa ndiye mpanga mipango, anayeitaka nchi, aitwe rais. Uchu wa madaraka.
Madam S alikuwa bado kitandani, chali. Akili yake ilikuwa imepaa mbingu ya saba, nje ya upeo wake wa kawaida. Iliitaji utulivu mkubwa kuweza kuwasha sakiti mpya ya umeme katika ubongo, kucukua tafutishi kutoka kwenye memori za muda za wakati huo. Kutafuta wapi zilitupa kumbukumbu hizo na kuzirudisha kwenye mfumo wa LTM yaani Long Time Memory. Ni zoezi gumu ambalo majasusi ujifunza. Katika zoezi hili mfumo wa kumbukumbu wa Madam S ulirudi kwa Chameleone.
“Nina ofisi yangu ya siri ambayo taarifa nyingi zinapatikana…” sauti ya Chameleone ilimrudia kichwani.
Hospitali ya Ocean Road! Akajikuta akiwaza.
Ding! Dong! Sauti ya kengele ilimgutua. Akafumbua macho na kushusha pumzi kwa nguvu.
Ding! Dong! Ikajirudia tena. Haraka haraka, akachukua kitabu chake cha kumbukumbu. Akafyatua kalamu na kuandika mambo machache muhimu. Akakiacha kitanda na kuliendea kabati la nguo. Akachojoa na kuchukua koti refu na kujitupia mwilini. Akafunga zipu yake mpaka chini. Akaenda sebuleni na kuwasha taa. Alielewa ni nani anayegonga mlangoni kutokana na jinsi alivyoibonya kengele hiyo.
Kabla hajafungua geti akatazama saa yake. Saa sita kasoro robo usiku. Akafungua geti.
Kamanda Amata akajitoma ndani na Madam S akafunga geti lile. Hatua chache wakafika sebuleni, pombe kali ikawekwa kati. Wote wawili, kila mmoja, akajitupa kitini.
“Yes Kamanda!” Madam S akamsabahi kwa namna hiyo mara baada ya kushusha bilauri yenye kinywaji.
“Madam, akili yangu haijatulia kabisa…” akasema na kupiga tena funda moja la kinywaji kile.
“Nini unafikiri?” Madam akamrudishia swali.
“Madam nimetoka kuachana na mtoto wa Mtokambali, nililoambiwa sijalitegemea,”
“Nambie mwanangu…”
“Kibwana Mtokambali alikwishafariki na amezikwa huko Kiev,”
“Nani amekwambia?”
“Mtoto wake wa kwanza, Bwana Onesmo anaishi Mwananyamala,”
“Umeonana naye?”
“Ndiyo, nilimtafuta nikampata nyumbani kwake, nikazungumza naye mengi sana. Anailaumu serikali kwa kutomjali baba yake. Anauliza, ukiachana na kosa alilohukumiwa kama mhaini mbona mmeusahau utumishi wake kwa miaka yote?” Amata akaeleza. Kutoka mfukoni mwake akachomoa rekoda ndogo, akawasha. Wote wawili wakaanza kusikiliza mazungumzo yale kutoka Alfa hadi Omega.
* * *

KIEV 1980

Katika Uwanja wa ndege wa kimataifa wa Boryspil Kyiv, Kibwana Mtokambali alipokelewa na swahiba wake Colonel Ivan Chernyakhovsky. Colonel huyu alimfahamu vyema Kibwana Mtokambali kwa kuwa walikutana kwenye mafunzo ya kijeshi mwaka 1968 huko katika Akademia ya Kijeshi ya Kiev. Ivan alijua fika nini dhamira ya swahiba wake. Tangu wakiwa katika academia hiyo, Mtokambali hakuweza kuficha hisia yake.
“Utakuwa mwanaume kamili ukifanikiwa hilo, hata ukishindwa, utakuwa umejaribu pakubwa…” Ivan alimwambia mara kadhaa wakiwa katika mafunzo yao. Tofauti na Kibwana, Ivan yeye akili yake yote ilikuwa ni kuanzisha chuo cha maswala ya usalama katika Kiev. Ndoto yake haikufa mpaka alipofanikiwa kwa asilimia kubwa na serikali kumsaidia.
Siku hii, ndani ya uwanja wa ndege alimpokea shujaa wake huyu.
“Tovarishch, ya ne smog…” Kibwana akamwambia Ivan kwa Kirusia kuwa ameshindwa jaribio lake.
“Ne volnuysya, moy pokazhu tebe drugoy put,” brat. YA Ivan akamtoa wasiwasi na kumwahidi kumwonesha njia nyingine ya kufanikisha lengo hilo. Wakakumbatiana kwa sekunde kadhaa kisha wakaelekea garini ambako mizigo yote ilikuwa tayari imekwisha pakiwa.
“Karibu tena Kiev komredi…”Ivan akamwambia Mtokambali.
“Nimekaribia, asante sana…”
Wote wawili wakaondoka uwanjani hapo kwa gari maalum la kijeshi. Baada ya mwendo wa takribani dakika arobaini na tano, waliwasili katika kitongoji kimoja mashambani. Lile Fiat likaingizwa ndani ya wigo mkubwa uliuzungukwa na kila aina ya ulinzi. Jumba la kifahari lilikuwa katikati ya wigo huo. Mara tu alipokanyaga ardhi, Kibwana akapokelewa na mwaDanada mrefu wa wastani, mwenye nywele nyeupe zilizomwagika mgongoni mwake. Suruali yake ya kijeshi ilimkaa vyema na kumpendezesha haswa.
“Kutana na Barbier Saratov,” Ivan akamwambia mgeni wake.
 “Nafurahi kukutana nawe Barbier…”wakasalimiana na kuzungumza machache kisha wakaelekea ndani ya jumba hilo. Moja kwa moja walifikia katika meza kubwa ya chakula, iliyopambwa na pombe kali kali. Kijindoo kidogo chenye barafu kilikuwa kikifuka mvuke. Kibwana Mtokambali aliitazama ile meza na kukumbuka miaka ya nyuma alipokuwa katika nchi hiyo kwa mafunzo ya kijeshi. Katika meza hiyo kulikuwa na watu watatu tu, Ivan, Barbier na Mtokamba. Akukuwa na mtu mwingine na wala hakukuonesha dalili ya kuwa na mtu wa ziada katika jumba hilo, ukiachana na walinzi wa nje.
Baada ya glasi mbili tatu kumiminiwa tumboni, ukimya ulivunjwa.
“Kwa katiba ya nchi yetu, nitahukumiwa kifo,” Kibwana alimweleza Ivan.
“Kamanda haogopi kufa, kwa kuwa ni sehemu ya maisha yake hasa anapopigania taifa lake,” Ivan akajibu.
“Najua comrade!”
“Sasa wasiwasi wako ni nini?” Ivan akamuuliza swahiba wake.
“Sina wasiwasi,”
“Hayo ndiyo maneno. By the way, utakuwa na Barbier kwa takriban wiki tatu au mwezi hivi. Yeye atakupitisha katika michakato tofauti ya kukubadili na kukurudisha tena kwenye uwanja wa vita,” Ivana akamwambia Mtokambali.
“Kunibadili?” akauliza.
“Naam, wewe utahukumiwa kufa, na utakufa, sasa sisi tunakuua mapema na kukurejesha vitani,” akamweleza, “Barbier!” akaita.
“Yes Sir!”
“Mweleze kinachoendelea kwa ajili yake,” Ivan akamwambia yule mwanamke. Barbier akavuta droo kubwa chini ya meza hiyo, akatoa kabrasha moja na kuliweka mezani. Alipoifunga ile droo, akalifungua lile kabrasha. Ndani yake kulikuwa na karatasi kama kumi hivi zote zikiwa na sura za watu, wazungu na majina yao. Zaidi ya hapo kuliokuwa na tarakimu nyingi sana.
“Nani unampenda kati ya hawa?” Barbier akamuuliza Mtokambali huku akimsogezea lile kabrasha. Mgeni huyo akachukua lile kabrasha na kuanza kulipekuapekua. Picha namba kumi na moja, akaipenda. Akamrudishia Barbier lila kabrasha kama alivyopewa, yaani kwa kulisukuma.
“Ok!” Barbier akatamka. Akaitatua ile karatasi na kuondoka pale mezani akiwaacha Mtokambali na Ivan, marafiki wawili.
“Don’t worry Kibwana. Hakuna linaloshindikana chini ya jua, utaona tu. Mimi na watu wangu tutakupa kila kitu ili ufanikishe lengo. Mafanikio yako ndiyo yetu kama tulivyopanga,” Ivan akamtoa wasiwasi.
Dakika kumi baadae, Barbier alirudi na kuketi katika kiti kilekile.
“Kila kitu sawa?” Ivan akamuuliza.
“Ndiyo! Kinachofuata ni kujiandaa kwa safari wiki moja ijayo. Dakta Punchkunel yuko tayari na atakuwa kwa ajili yetu siku hiyo,” Babier akatoa maelezo. Wakati yuote haya yakionelewa, Kibwana alikuwa kimya akigugumia vodka yake. Hakuna alichokielewa zaidi ya kusikia tu.

ITAENDELEA
 
GENGE
EP21

Dakta Punchkunel yuko tayari na atakuwa kwa ajili yetu siku hiyo,” Babier akatoa maelezo. Wakati yuote haya yakionelewa, Kibwana alikuwa kimya akigugumia vodka yake. Hakuna alichokielewa zaidi ya kusikia tu.

* * *

Dar es salaam

Madam S aliegesha gari nje ya hospitali ya Ocean Road. Asubuhi ya siku hii, mvua ya rasha rasha ilikuwa ikiendelea kunyesha. Akiwa ndani ya koti kubwa la mvua, akavuta hatua kuelekea jengo moja dogo lililotelekezwa kando tu mwa ukuta wa hospitali hiyo. Mmea mkubwa wa mpaseni ulikuwa umefunika jengo lote. Unetazama tu unejua wazi kuwa hakuna aliyekuwa akilitumia kwa kipindi kirefu. Alipolizunguka upande wa pili akakutana na mlango mdogo uliosonwa na mpasheni ule. Akasimama kwa jozi la sekunde akitazama vizuri ule mlango. Akajipapasa mfukoni na kuchomoa funguo moja aliyoona inamfaa kwa kazi hiyo. Akasukuma huku na huko mpasheni ule na kufanikiwa kupachika ufunguo. Alipouzungusha, kitasa kile cha kizamani hakikuleta ubishi. Akausukuma ndani kwa nguvu kidogo. Mlango ule, ukakwangua chini kutokana na uchakavu wake. Alipopata upenyo wa kuingi akafanya hivyo. Akaurudisha kwa tabu vilevile na kujikuta kasimama kwenye chumba kidogo.
Ndani ya chumba hiki kulikuwa na meza moja nzuri ya mninga. Ilimstaajabisha Madam S kwa usafi wake. Tofauti na alivyotegemea kuwa angekuta buibui na wadudu wengine, haikuwa hivyo. Ofisi ile ilikuwa safi, picha ya Chameleone ilikuwa ukutani ikining’inia. Madam S alishangaa, akatazama huku na huku akitegemea labda atasikia sauti ikimwita.
Nani husafisha humu ndani? Akajiuliza.

Alipoona hilo halina majibu akapitisha macho yake kwenye rafu ya vitabu na makabrasha iliyosimama mbele yake. Akatia mkono kupekuapekua kama aneweza kuona chochote ambacho kingemsaidia. Madam S alijikuta anapekua kila kabrasha. Ndani yake alikutana na mambo mengi sana, mabaya na ya kutisha. Siri nzito nzito za na mipango ya hatari isiyofaa kuonwa kwa macho mepesi. Madam S alijikuta akitetemeka mikono kama mtu anayepiwa na baridi.
Nani anatumia ofisi hii? Akajiuliza mara nyingine. Unafuu ulipomrudia akasogelea tena rafu ile. Mwili ukasisimka, nywele na vinyweleo vikamsimama pindi tu alipokama kabrasha moja lililoandikwa Most Wanteds. Akiwa katika kulivuta, ikaanguka picha moja ya wastani. Macho ya Madam S yakaiona sura ya James Msambamagoya. Akapata shauku ya kufunua zaidi. Kulikuwa na kurasa kama hamsini hivi zenye picha na maandishi. Hakupenda kupoteza muda katika ofisi ile. Akalifutika kabrasha lile kotini na kutoka nje. Mara hii mvua ilikuwa kubwa zaidi. Alipoufunga tu mlango akakimbia kulielekea gari lake. Akafungua mlango na kuketi ndani yake. Akashusha pumzi ndefu na kulivua lile koti, kisha akalitupia kiti cha nyuma. Lile kabrasha akalipachika kati ya kiti na kiti ambapo si rahisi mtu kujua. Akatia moto injini na kuondoka taratibu kutoka katika yale maegesho. Mapigo ya moyo yalikuwa yakimwenda kasi, hali iliyokuwa ikimtia wasiwasi.
Kuna kitu! Akawaza wakati akiingiza gari katika maegesho ya Chuo cha Magogoni. Akazima gari na kusubiri sekunde kadhaa akitazama vioo vyake vya pembeni na kile cha ndani ili kuona kama kuna anayemfuata. Alipojiridhisha kuwa usalama upo wa kutosha, akateremka na kabrasha lile mkononi. Kwa kutumia njia zake za siri, alipita mpaka Ofisi Ndogo. Akalitua mezani na kulitazama bila kulimaliza.
Nina uhakika, siri zote nitazipata humu. Chameleone hakuwa mtu wa mchezo! Akawaza na kuizunguka meza mpaka upande wa pili, akaketi na kuliweka sawa kabrasha lile.
Most Wanteds!
Lilisomeka juu kabisa. Kwa mikono ya kitetemeshi, alifungua jalada lake na kukutana na ukurasa wa juu kabisa ulioandikwa kwa mkono Top Secret. Hii tu ilitosha kujua nini anaenda kukutana nacho. Macho ya Madam S yakatua kwenye kurasa ya pili. Ilikuwa karatasi ile iliyoandikwa tafutishi za mtu asiyejulikana. Tafutishi ambayo Chameleone alipewa na Mkuu wa nchi tangu mwaka 1980, iliyobeba majina ya watu wanaosadikiwa kuwa wana mpango wa mapinduzi. Mpango wa kumuua Rais ili kujitwalia madaraka. Katika kurasa hii ndimo alipokutana na orodha ile chafu. Majina asiyoyategemea ambayo yalivuma wakati yeye akiwa bado mpya kwenye medani ya usalama. Akaiweka pembeni. Akatupa macho kwenye kurasa ya tatu. Hapa akakutana na muhtasari wa kikao cha siri kilichokutanisha watu wa juu kabisa wa jeshi. Kikao kilichofanyika Banana Bar, Ukonga. Akaisoma kwa tuo bila papara. Katika kurasa hii, mpangomzima ulikuwa mezani, nani apewe cheo gani na cheo gani apewe nani. Huku ukimtaja Kibwana Mtokambali kama Rais wa nchi. Ilikuwa ni Syndicate hatari iliyoundwa na watu makini wanaoujua vyema uwanja wa vita. Madam S akatikisa kichwa. Mengi kati ya haya hakuyajua kabla.

Akafungua kurasa ya nne akakutana na orodha ya watu waliohukumiwa kifo baada ya kesi ile. Waliotoroka, wakawekewa alama nyekundu na picha zao zikielezea wajihi wao. Wengine waliofungwa maisha. Na wapo waliouawa. Picha zao zilikuwapo vilevile. Orodha ya chini ilikuwa ya wale wote walioachiwa huru.
Kurasa zilizofuata zilikuwa ni taarifa mbalimbali ya ufuatiliaji wa sakata hilo. Chameleone aliorodhesha njia zote alimopita katika upelelezi wake. Nani na nani alimhoji. Kipi na kipi alikipata. Akuishia hapo, aliweka majina mengine ambayo anayatilia shaka. Madam S hakutegemea kuyaona hapo.
Kurasa tatu za mwisho, zilitanguliwa na karatasi iliyobeba maandishi ‘Orodha Chafu’. Katika kurasa hizi kulikuwa na majina ishirini na mbili. Mpaka tarehe hiyo ambayo kabrasha hilo lilikuwa mikononi mwa Madam S, majina tisa yalikuwa na X nyekundu. Kila moja likielezewa sababu ya kuwekwa X hiyo, vifo. Madam S akavuta kumbukumbu na kung’amua kuwa majina hayo yote yalikuwa ya marehemu.
Kulikuwa na mauaji ya siri! Akawaza. Majina mengine hayakuwa na orodha yoyote isipokuwa manne ya mwisho. Haya yalifunikwa viboksi vyekundu na kuandikwa pembeni ‘Most Wanteds’. Maelezo yaliyofuatia chini yake ni kutaka watu hao wasakwe popote duniani na wauawe pasi na huruma. Madam S akaunganisha matukio ya kazi aliyopewa na Ikulu na hicho anachokiona.
Akagundua kuwa anatekeleza kazi ya Chameleone.
Akiwa katika kufunga kabrasha lile, akakutana na bahasha. Bahasha ile iliyobanwa kwa stepla pini iligongwa mhuri wa serikali wenye neno ‘SIRI’ katikati. Akaichana na kutoa karatasi mbili zilizokuwa ndani yake.
Moyo ulimpiga kwa nguvu, pumzi ikapanda na kushuka. Hakuamini anachokutana nacho.
Hati safi ya mkono ilikuwa imeandika taarifa hiyo fupi.

Wamesema wakimgundua mamluki yeyote anayekwamisha

juhudi zao watamuua bila huruma.

Ni mimi si mwingine, wataniua, lakini lazima niufikishe mpango huu dhalimu mikononi mwa serikali.

Mpango huu ni kigae katika choo changu cha ndani.
Na mengine mengi niliyoyakosa yapo katika nyumba namba 73A Kinondoni Mtaa wa
Galu. Nyumba hii ni mali ya Burushi mmoja mwenye urafiki wa karibu sana na
Kibwana Mtokambali…
Dastan Kihwelo

Madam S alijikuta akipandwa na hasira, alimfahamu kijana aliyeandika ujumbe ule. Dastan Kihwelo, aliyeuawa mara tu baada ya sherehe yake ya harusi. Hasira ziliwaka kichwani mwa mwanamama huyu. Akafunga lile kabrasha na kuliweka katika saraka yake ya siri ambayo ni yeye tu anayeweza kuifungua.


* * *

Mtaa wa Galu, Kinondoni
Sauti ya nukushi ilisikika kutoka katika nyumba namba 73A katika Mtaa wa Galu. Mbele ya mashine hiyo alisimama kijana mmoja mtanashati wa mavazi, mweupe wa rangi, na mrefu wa kimo. Mkono wake ulikuwa tayari kuinyakuwa karatasi iliyokuwa ikupokea ujumbe wa nukushi hiyo. Mkono mwingine ulikamata kikombe kidogo kilichojaa kahawa isiyo na sukari. Sekunde ishirini na nne zilitosha. Ujumbe ule tayari ulikuwa katika karatasi ile. Akaichana na kuitupia macho huku akivuta hatua kuielekea meza kubwa iliyowekwa kando ya nyumba ile, sambamba na dirisha lililoelekea barabarani. Kwa nje, wigo mrefu wa michongoma uliificha nyumba ile karibu robo tatu yake kutoka chini. Ni paa chakavu, lenye kutu na lililoliwa na hewa ya chumvi ndilo lililonekana kiurahisi.
Brian Mkuchu, aliketi kitini na kuiweka karatasi ile mezani. Mara baada ya kupiga funda moja la kahawa, akakitua kikombe na kuivuta ile karatasi karibu na uso wake.

Tafuta mzigo wenye Code 005 Ukiupata, upoteze bila maswali.

Brian akarudia kusoma karatasi ile mara kadhaa.
“Code 005!” akajisemea kwa sauti ya chini huku akiiendea simu ya mezani iliyowekwa kando. Akabofya vinobu kadhaa na kuweka mkonga wake sikioni. Utulivu wa kusubiri amkio la upande wa pili, ukatamalaki.
“Sabini na tatu A nakupata…”
“…Tafuta code 005 haraka unipe jibu,” akamwambia mtu wa pili.
“ Copy”.
Brian akakata simu na kurudi kitini. Alipoinua kikombe cha kahawa, tayari ilikwishapoa. Akasonya na kukisogeza kando. Akarudia tena kuisoma ile nukushi mara kadha wa kadha hasione nini kimejificha ndani yake.
“Code 005!” akajisemea tena. Alipotupa macho nje ya dirisha akaliona gari la kizamani,
Mazda jekundu likiwa limeegeshwa nje tu ya baraza la nyumba hiyo. Brian akatikisa kichwa

akalikumbuka Mazda lile ambalo sasa halikuwa maridadi kama kale. Akiwa bado katika kulitazama, simu ile ile, ikaita, akaiendea na kuinyakua kwa shauku, akaiweka sikioni.
“Sabini na tatu A…” akaitikia.
“Tukutane Ndege Beach tupate bia kidogo!” sauti ya upande wa pili ikamwambia.
“Umesomeka,” Brian akamjibu. Haikumpa tabu kuitambua sauti ile. Haraka akatoka nje na kuingia kwenye lile Mazda. Akaketi na kuufunga mkanda. Akaliwasha mara kadhaa likagoma kuwaka.
“Aaaaaaa shiiit!” akajikuta akipiga kelele peke yake. Alipojaribu mara hii likawaka. Muungurumo wake mzito ulilitambulisha kuwa halikuwa la kawaida. Akalitoa pale lilipoegeshwa na kuliingiza barabarani. Safari ikaanza.
Nusu saa baadaye aliwasili eneo la miadi, Ndege Beach. Akateremka na kuvuta hatua kuelekea kwenye baa ndogo iliyojengwa katika ufukwe huo. Baada ya kuzipita meza kama mbili tatu hivi, akaifikia ile anayoitaka, ambayo mwenyeji wake alikuwa kaketi peke yake, huku mbele yake kukiwa na chupa ya soda. Brian akavuta kiti na kuketi, akaondoa miwani yake nyeusi usoni na kuitia katika mfuko wa shati huku akiacha sikio moja lining’inie nje yake.
“Brian,” akaita yule jamaa kwa sauti ya chini.
“Yes Mic,” Brian akajibu huku akijiweka sawa kusikia alichoitiwa, “umetambua?” akamtupia swali akitaka kujua hasa juu ya kazi aliyompa. Kazi ya kuitambua code 005.
“Jambo jingine kaka, hatari…” akajifikicha jicho la kuume, kisha akaendelea, “faili limetoweka…” Mic akasema.
“What?” Brian akahisi kizunguzungu cha ghafla akajiegemeza kitini na kushusha pumzi ndefu, “Umejuaje?”
“Kama kawaida yangu, niliingia ofisini late sana, ukizingatia kamvua haka. Nafika kwenye shelf kwa minajiri ya kulichukua ili nianze ile kazi, silioni kaka…”
“Mike, Mike, Mike…” Brian akaita kwa sauti ya chini iliyojaa msisitizo huku akimkazia macho, “Kila mara nimekwambia; chunga hilo faili kwa sababu lina taarifa muhimu na tutazihitaji. Ona sasa, hata aliyechukua humjui… we are in trouble my friend,” akamwambia kwa sauti ya kukata tamaa.
“Unajua Brian, ile ni ofisi ya siri sana, haijulikani na watu… lakini ninachoshangaa, huyu mwanamke aliyeingia humu kaijuaje?” Mic akasema huku akitoa picha tatu; moja ikimwonesha Madam S akiwa ameingia mlangoni, ilimwonesha vizuri usoni. Ya pili ilimwonesha akiwa anachomoa kabrasha lile, na ya tatu alipoinama kuokota picha aliyoiangusha.
Brian alizichukua zile picha na kuzitazama kwa tuo, akamwangalia tena Mike.
“Ina maana humjui huyu mama? Na kama ameingia kwenye hii ofisi unayoiita wewe ‘ya siri’ basi ni mmoja wenu,” akamwambia.
“Simfahamu kabisa,” Mike akamweleza Brian.
“Ok, naondoka na hizi picha, naomba tuonane saa kumi na mbili jioni ukiwa na ile kazi yangu na mi nikiwa na majibu ya hizi picha,” Brian akamwambia Mike huku akiwa tayari keshasimama. Wawili hao wakaagana na kila mmoja akashika njia yake.


* * *


Mburahati NH

Nyumba aliyoinunua marehemu Dastan na kuikarabati tayari kuishi na mkewe Egra, ilikuwa Mburahati katika mtaa wa National Housing. Ilikuwa Imepita miaka takribani kumi hivi tangu kijana huyu atoweke. Ndugu na majirani hawakuweza kusema kwamba kafa , kwa sababu hawakuwa na ushahidi. Hivyo neno zuri lilikuwa ‘katoweka’. Kwa sasa nyumba hiyo ilikuwa imepangishwa.
Inspekta Simbeye aliegesha gari lake nyumba ya tano kutoka hiyo, akateremka. Upande wa pili, Madam S naye akateremka. Wote wawili, wakaikabili nyumba moja iliyokuwa mkabala nao. Simbeye, aliyevalia nguo za nyumbani; shati la Bahama na suruari ya kitambaa alikuwa wa kwanza kuzifikia ngazi hizo. Madam S alifuatia kufika hapo, akiwa hatua chache tu kutoka kwa Simbeye. Kama ungewaona, basi bila shaka ungejua kuwa ni mtu na mke wake. Kumbe walikuwa kazini.
Kabla awajaufikia mlango wa nyumba hiyo, ukafunguliwa. Mwanamama mmoja wa makamo akajitokeza. Wakakutana hapo kwa sadfa tu, kila mmoja akasimama na kuacha mita moja hhivi katikati yao.
“Habari yako dada!” Simbeye alikuwa wa kwanza kumsabahi. Umri wao haukupishana sana, ndiyo maana akamsabahi kwa kumwita ‘dada’.
“Salama tu. Karibuni sana…” yule mwanamke akawajibu huku akiifunga kanga yake vizuri.
“Samahani, hapa ndiyo kwa Bwana Kihwelo?” Simbeye akauliza. Yule mwanamke akabaki na butwaa. Hakujua nini anapaswa kukijibu. Baada ya sekunde kama tano hivi akawajibu.
“Kihwelo! Kihwelo yupi? Maana anayeishi hapa anaitwa Chami. Amepanga nyumba hii yote…” akaeleza.
“Ok! Samahani tutakuwa tumekosea, maana tunauliza tangu hukoooo tukaelekezwa hapa. Tuna muda mrefu sana hatujaonana,” Simbeye akasema.
“Ni ndugu yangu ndiyo. Ni miaka kama thelathini hivi tangu tuachane na kiukweli hatukuwa na mawasiliano.” Simbeye akatunga uongo.
“Oh poleni sana, hapa tumehamia miaka sita iliyopita na kwa kweli, simjui mtu huyo, labda uliza kwa majirani au mjumbe nyumbani kwake paleeee,” akawajibu na kuwaonesha kwa kidole nyumba ya Mjumbe wa eneo hilo.
“Asante sana!” Simbeye akajibu. Simbeye na Madam S wakatembea taratibu mpaka kwenye nyumba ya mjumbe. Bahati nzuri wakamkuta kibarazani akicheza bao na wazee wenzake.
Walipojitambulisha kama ndugu wa bwana Kihwelo, yule mzee akawakaribisha ndani na kuketi sebuleni.
“Mnasema ninyi ni ndugu wa Kihwelo?” akawauliza.
“Ndiyo! Na hatujaonana na huyu bwana miaka mingi sana. Na hii inatokana na kwamba hatukuwa na ukaribu sana kimawasiliano…” Simeye akajibu wakati Madam S akiwa kimya kabisa.
“Mh! Mmmmh!”
“Vipi mzee wangu mbona unaguna?” Simbeye akauliza swali.
“Nashindwa nianzie wapi…”
“Usijali mzee, sisi twahitaji kujua ndugu yetu yuko wapi. Laiti tungekuwa na ndugu hapa Dar’ ingekuwa rahisi,” Simbeye akaeleza.
“Mzee mwenzangu! Hapa habari wala si nzuri,” aliposema hayo, Madam S akarudisha macho kwa yule mzee, “Kihwelo bwana, dah! Huyo kijana bwana aaa alitoweka tu katika mazingira ya kutatanisha yeyena mkewe, tena siku ya ndoa yao!” yule mjumbe akeleza kwa kigugumizi kidogo, akatulia. Simbeye na Madam S wakamkodolea macho ya mshangao uliochanganyika na majonzi kwa wakati mmoja.
“Na alikuwa akiishi wapi?” Simbeye akamuuliza.
“Huyu bwana, nyumba yake ilikuwa ile pale, na sasa wameipangisha,” mjumbe akajibu.
“Ok, sawa, tutafanyaje sasa… mi nitaendelea kuwatafuta ndugu wengine huko Iringa ili nipate habari kamaili,” Simbeye akasema huku akionekana wazi kuwa anataka kuaga. Dakika kumi zilizofuata, Simbeye na Madam S walikuwa tayari ndani ya gari lao.
Mpango huu ni kigae katika choo changu cha ndani. Madam S akawaza. Moja ya sentensi
iliyoandikwa katika ule ujumbe wa siri.
“Inabidi vijana warudi baadae kuipekuwa ile nyumba,” Simbeye akasema. Madam S akashusha pumzi na kumtazama mzee huyo.
“Hilo niachie mimi, kesho asubuhi nitakupa habari,” Madam S akamwambia Simbeye.

* * *

ITAENDELEA
 
GENGE
EP22

Mpango huu ni kigae katika choo changu cha ndani. Madam S akawaza. Moja ya sentensi
iliyoandikwa katika ule ujumbe wa siri.
“Inabidi vijana warudi baadae kuipekuwa ile nyumba,” Simbeye akasema. Madam S akashusha pumzi na kumtazama mzee huyo.
“Hilo niachie mimi, kesho asubuhi nitakupa habari,” Madam S akamwambia Simbeye.

* * *

2:35 usiku

MWINYIJUMA SOCIAL HALL

Mwananyamala

Muziki wa bendi ya Vijana Jazz uliendelea kuunguruma ndani ya ukumbi huo mkongwe jijini Dar es salaam. Mmoja kati ya wapenzi wa bendi hiyo aliyekuwa katikati ya umati akilisakata rumba alikuwa Kamanda Amata. Hakuwa na hili wala lile, binti aliyekuwa naye alikuwa hodari pia katika hilo. Alijua kulisakata ‘Air Pambamoto’, alimpagawisha Amata kwa mauno aliyokuwa akiyazungusha. Hata wanaume wengine pembeni yake, walijikuta wakiacha kucheza na kuwatazama wawili hawa.
Honi za gari zilizopigwa nje ya ukumbi huo zikamgutusha kutoka katika lindi la burudani. Honi zile zikarudia tena. Na mara ya tatu ilipopigwa tena, Amata akamshika mkono yule mwaDanada na kutoka naye kwenye kundi lile la watu.
“Aaaaaaa mrudisheee, mwacheeee!” kelele za wanaume walionogewa na unenguaji wake zikasikika. Amata hakujali, akamvuta mkono mpaka katika mlango wa kutokea nje. Akamwacha , kisha yeye akavuta hatua kama tano mbele, karibu kabisa na barabara. Akasimama na kuangaza huku na kule.
‘Piiiiii! Piiii! Pi!’ honi ikasikika tena, mara hii kwa mtindo mwingine. Mara moja akaliona gari lililokuwa likipigwa honi hizo. Alipotaka kuvuka barabara, akashikwa mkono.
“Mbona unataka kunitoroka?” yule msichana alikuwa pembeni mwa Amata akihoji.
“Oooh, tangu lini nikamwacha mrembo kama wewe? Nilitaka nimwone rafiki yangu pale ng’ambo kisha tuendelee na burudani zetu,” Amata akamjibu.
“Mmmmm!”
“Mmmmm nini?” Amata akauliza.
“Wanaume wote baba yenu mmoja. Maneno matamu kinywani lakini hisia hakuna moyoni,” yule msichana akalalama huku kaibetua midomo yake kama anamsuta mtu. Kamanda Amata akavuka barabara na kumvuta yule msichana mpaka upande wa pili.
“Eh, baba utaniangusha! Polepole,” akamwambia Amata. Hakumsikiliza. Akavuta hatua mpaka kwenye lile gari. Alipolikaribia tu, kioo cha mbele kikateremka nusu.
“Vipi?” Amata akamuuliza dereva wa gari hiyo.
“Twende!” Chiba akajibu. Amata hakuuliza tena, akafungua mlango na kumkamata yule msichana, akamnyayua na kumuweka kwenye siti ya nyuma, naye akapanda na kuketi kandoye.
“Mnanipeleka wapi jamani?”
“WE tulia, shida yako nini!” Amata akamtuliza yule mwanamke.
“Vipi Chiba?” akamuuliza.
“Ondo!” Chiba akajibu akimaanisha ‘Ofisi Ndogo’.
“Ok, pita Virginia kwanza,” Amata akamwelekeza Chiba. Naye akatii. Akaiacha barabara ya Kinondoni kuelekea daraja la Salender na kuingia mtaa wa vumbi na mashimo upande wa kulia. Dakika mbili tu ziliwafikisha Virginia.
“Adella, nitakukuta hapa lodge, naenda kucheki kitu Fulani , ninakuja…” Amata akasema.
“Utarudi kweli wewe? Au ndo umekatisha starehe zangu tu?” Adella akauliza kwa mashaka. “Nitarudi, fika mapokezi mwone Lilian!” akamwambia huku tayari msichana yule akiwa chini. Hatua zake za maringo zikamfanya Amata asahau kurudi garini. Alikuwa mfupi, mnene, nywele zake zikiwa katika mtindo wa Afro. Sketi fupi aliyovaa ilitosha kudhihirisha uzuri na utamu wa mguu wake mnene, mapaja yaliyojaa vyema, kiuno kidogo kilichobeba kiwiliwili chenye afya.
“Hivi hizi mbegu unazitoaga wapi?” Chiba akauliza. Amata hakujibu, badala yake akaingia garini na kuketi siti ya mbele. Akamtazama Chiba na kuanza kucheka.
“Nambie Chiba!”
“Bibi yako anakutafuta huko!”
“Nipeleke nikamwone tafadhali,” akamwambia Chiba.
* * *

Ofisi ndogo

Madam S alikuwa kimya ofisini kwake usiku huo. Mbele yake, juu ya meza kulikuwa na kitabu chake cha kumbukumbu, kikiwa wazi. Miwani yake ikiwa imetulia juu ya kurasa hizo zilizo wazi. Akiwa kazama katika lindi la mawazo, sauti hafifu ya kengele ikamgutusha. Alipotazama luninga yake ndogo iliyowekwa mahali pa siri katika meza yake hiyo. Akawaona vijana wake wawili wakiwa mita chache tu kabla ya mlango. Akabofya kitufe katika uvungu wa meza hiyo. Mlango ule ukafunguka na kuwaruhusu kuingia ndani.
“Karibuni, ketini tafadhali,” akawakaribisha na kila mmoja akaketi katika kiti chake. Ndani ya ofisi hii palikuwa na viti sita tu. Kwenye meza zilizofanya T palikuwa na kiti kimoja upande wa mbele na vitano vilikuwa upande mwingine. Viti vyote hivi vilikuwa nadhifu sana, kila kimoja kikiwa na namba na nembo safi ya TSA. Amata na Chiba wakaketi wakimtazama HOT.
“Giza limeingia, usiku umetamalaki… kazi inayotukabili bado ni kitendawili. Nyote mnajua.
Sasa naitaji ifanyike blackbag job usiku huu. Nitakaa hapa hapa nikiwasubiri,” Madam S akawaambia. Amata na Chiba wakatazamana, kisha wakarudisha macho kwa mwanamama huyo.
“Wapi?” Amata akauliza. Badala ya kujibu, mwanamama huyo, mkuu wa idara nyeti ya kijasusi, akamsogezea kijana wake karatasi moja nyeupe iliyo na maandishi machache tu.

Wamesema wakimgundua mamluki yeyote anayekwamisha juhudi zao watamuua bila huruma.

Ni mimi si mwingine, wataniua, lakini lazima niufikishe mpango huu dhalimu mikononi mwa serikali.

Mpango huu ni kigae katika choo changu cha ndani.

Na mengine mengi niliyoyakosa yapo katika nyumba namba 73A Kinondoni Mtaa wa
Galu. Nyumba hii ni mali ya Burushi mmoja mwenye urafiki wa karibu sana na
Kibwana Mtokambali… Dastan Kihwelo

Ni ujumbe uleule ambao Madam S aliukuta katika kabrasha lile. Amata akausoma na alipomaliza akampatia Chiba, naye akausoma.
“Nipe mwongozo mkuu …” Amata akamwambia Madam S huku akijiweka vizuri kitini.
“Maandishi hayo, au niite ujumbe huo umeandikwa na marehemu Dastan Kiwelo. Huyu alikuwa mwanausalama katika idara yetu miaka hiyo ya tisini. Hatujua kama aliuawa au emetekwa na kufichwa mahali Fulani. Hatujui, lakini alitoweka mara tu baada ya harusi yake yeye pamoja na mkewe. Tukio hilo lilitukia mwaka tisini na moja,” Madam akaeleza kwa kifupi.
“Dastan Kihwelo! Sasa blackbag hii inahusiana na nini hasa?” Amata akauliza.
“Swali zuri ila kitoto kuulizwa na mtu kama wewe…”
“Najua…”
“Dastan Kihwelo, alikuwa akifanya kazi kama D.A. Mkuu wake wa kazi kipindi hicho alimruhusu kurubuniwa na kujiuna na kundi la wanamapinduzi waliokuwa wakifanya mambo yao kwa siri sana hapa nchini. Kundi hili liliundwa mara baada ya sakata la kujaribu kuiangusha serikali ya awamu ya kwanza mwaka ule wa themanini na mbili, uliopelekea wengine kufungwa na wengine kutoroka nchi. Hili mnalijua!” akawaeleza.
Amata na Chiba wakatikisa vichwa vyao kuonesha kuwa wanalifahamu vyema. Sifa moja wapo ya mwanausalama katika idara hizi za kijasusi ni kujua historia ya nchi yako, mahali unapoishi na watu wanaokuzunguka. Madam S akaendelea kuwaambia, “Sasa huyu kijana aliweza kupata habari nyingi sana. Mojawapo ndiyo iliyofanikisha sisi kummaliza Mwakibinga, mpo?”
“Tupo!”
“Hivyo basi, katika kutoka pale tulipokwama, nimeipata memo hiyo hapo. Na katika kuichambua kitaalam utagundua kuna maeneo mawili yametajwa. Moja limetajwa wazi kuwa ni ‘nyumba namba 73A Kinondoni Mtaa wa Galu’, na nyingine ameitaja kwa fumbo kwa maneno ‘Mpango huu ni kigae katika choo changu cha ndani’” akawaeleza.
“Kwa hiyo hicho kigae kina mengi!” Amata akasema.
“Yes!”
“Kazi imekwisha,” akamhakikishia mkuu wake akiwa tayari wima.
“Sasa unasimama unajua unaenda wapi?” Madam S akamuuliza Amata ambaye tayari alikuwa
wima.
“Si umeshatuambia ‘ni kigae katika choo changu cha ndani’ au?” akauliza.
“Ndiyo. Mburahati, National Housing, kitalu namba 21B. Nawasubiri hapa hapa…” Madam S akawaamuru. Amata na Chiba wakatoka katika ile ofisi na kuliendea lile gari. Wakaingia na kuketi ndani yake.
Amata akashusha pumzi ndefu, akavuta mkanda wa usalama na kuupachika vyema katika
bako yake. Chiba na Amata, usiku huu walikabiliwa na kazi hiyo ‘blackbag’ yaani uchunuzi ama wa nyumba au ofisi hasa katika nyakati za usiku. Haikuwa kazi kwao kuvamia nyumba isiyo na ulinzi kama hiyo. Wakatazamana, kila mmoja akaelekeza macho yake mbele.
“Twende Kinondoni, nyumbani, tukaandae vifaa kisha usiku wa saa nane tuifanye kazi hiyo,” Amata akamwambia Chiba. Chiba, badala ya kujibu, akaitazama saa yake. Saa tano kasoro usiku.
“Halafu tunapoisubiri saa nane tutakuwa wapi?” Chiba akamtupia swali Amata. Sekunde
kadhaa zikapita bila neno. Ukimya ukatamalaki kati yao.
“Utaniacha kwa Adella, pale Virginia Lodge. Au umesahau kama nimeacha mtoto pale?” Amata akamwambia Chiba, wakati huo tayari ari likiwa juu ya barabara ya Mtaa wa Shaban Robert.
Safari ya Kinondoni.
“Sawa kaka. Ila angalia pia na upande wa pili. Gina anakupenda sana ila umtendei haki…” Chiba akamwambia Amata.
“Chiba, ya Gina yaache. Twende home tucukue vifaa, uje uniache kwa Adella wangu,” Amata
akasisitiza.

ITAENDELEA
 
GENGE
EP23

MBURAHATI

Saa 8:15

Kamanda Amata aliegesha gari mbele ya maduka, mitaa mitatu kabla ya ule waliolekezwa. Walipohakikisha milango yote imefungwa, wakavuta hatua kuilekea nyumba waitakayo. Usiku wa manane, wakiwa ndani ya mavazi meusi, Chiba na Amata waliikaribia kabisa nyumba waitakayo. Ukimya ulitamalaki, walichukua dakika moja kuizunguka nyumba hiyo. Hakuna aliyekuwa akiongea kwa sauti, lugha ya viziwi ilikuwa ikitumika. Walipohakikisha kila kitu kipo sawa, wakauendea mlango wa mbele. Wakapeana ishara, Chiba akapachika funguo na kuzungusha. Mlango ukaitikia. Chiba akausukuma taratibu na kukaribishwa na korido ndefu iliyogawanya vyumba upande huu na ule. Wakapeana tena ishara nyingine. Amata akachomoa makopo matatu ya dawa aina ya Chlorofom yenye ujazo wa mililita mia tano kila moja. Akampa ishara Chiba, kila mmoja akavaa barakoa maalumu ya kuzuia aina yoyote ya gesi kutomdhuru mtumiaji. Akaondoa kifungo cha chupa moja na kuisukumia koridoni huku ikitoa kitu kama majimaji mepesi yakisindikizwa na harufu nzuri. Wakaingia ndani na kufungua kila chumba wakinyunyiza kiasi kidogo cha kuwafanya wenyeji walale kwa saa mbili tu.
Dakika tano zilitosha kuwalaza wote mle ndani. Chumba cha mwisho kabisa ndicho hasa walikuwa wakitakacho. Jinsi kilivyojengwa kilionekana wazi kuwa kingekuwa cha mwenye nyumba. Kilikuwa kikubwa kilichowekwa makochi matatu ya kisasa. Luninga moja ya Hitach na redio kubwa ya Panasonic Double Deck. Upande mmoja kulikuwa na mlango. Amata akahisi kwa vyovyote kitakuwa chumba cha kulala. Akampa ishara Chiba naye akakifuata mpaka mlangoni. Akajaribu kuufungua mlango, ukagoma. Akatumbukiza funguo yake isiyoshindwa, akanyonga mara moja tu. Kitasa kikatii. Akausukuma mlango taratibu na kukaribishwa na watu wawili waliokuwa kitandani wakikoroma. Mwanamke na mwanaume, pembeni ya kitanda kulikuwa na meza ndogo iliyobeba chupa kubwa ya Amarula na pakiti sita za mipira ya Salama.
Amata akampa ishara Chiba ya kuingia ndani ya chumba kile, naye akafanya hivyo na kumuelekeza moja kwa moja kwenye mlango wa chooni kwa kuwa chumba hiki kilikuwa ni self container. Amata akawatazama wale viumbe pale kitandani waliokuwa usingizini bila nguo huku suka likiwa limesongwasongwa kando ya kitanda. Feni lilikuwa likiunguruma na kujaribu kupambana na joto la jiji hilo lakini wapi. Amata akapuliza tena dawa ile karibu nusu kopo kwa kuwa watu wale walikuwa wamekunywa pombe.
* * *
Hakikuwa chumba kikubwa. Sinki la choo cha kukaa na kipande kingine kulikuwa na pazia la plastiki kutenganisha maeneo mawili hayo nyeti. Kamanda Amata akachukua ufagio na kutumia mpiniwe kugongagonga vigae vya sakafu kuona kama kuna yoyote ambayo itaonesha dalili za shimo. Kwa kusikiliza mlio uliokuwa ukisikika, Chiba akaaundua kiurahisi zaidi. Akamwonesha kwa kidole kigae alicho na wasiowasi nacho. Vyote vilitoa mlio sawa wenye tofauti ndogo sana. Ilihitajika masikio makini sana. Bila kuchelewa, Amata akashusha begi lake na kuchukua mashine ndogo ya kukata vigae. Akakiwasha na kukata sawasawa na miungo ya vigae hivyo. Alipofanikiwa akachukua kifaa kingine na kubandua vigae vile. Chini ya kigae kimojawapo kulikuwa na mfuniko mdogo wa mbao. Akaukamata na kuutoa. Chini kulikuwa na mfuko wa plastiki uliofungwa vyema kabisa. Amata akautazama kwa kusaidiwa na kurunzi ndogo iliyokuwa katika paji lake la uso. Akauvuta taratibu na kuutoa, akauweka sakafuni. Ndani ya mfuko ule kulikuwa na bahasha moja ya kaki, iliyofungwa na kugongwa mhuri wa ‘SIRI’. Akampa ishara Chiba kuwa waufungue, naye akajibu kwa kumwambia kuwa wataufunua ofisini.
Kazi ikaisha, Amata akarudisha vile vigae kama vilivyokuwa. Kwa kutumia gundi maalumu akavibandika kiasi kwamba si rahisi kugundua kuwa vilifumuliwa. Wakapakia kila kitu kwenye mkoba wao. Amata akauweka mgongoni na kutoka mpaka pale chumbani. Mtu na bwana wake walikuwa wamelala fofofo. Kila mmoja katupa mguu anapopajua yeye na kuacha siri zote nje.
Joto la Dar’ halina adabu! Amata akawaza. Haraka akauendea mlango, Chiba alikuwa tayari sebuleni. Amata alipoufikia mlango, akasita, akageuka nyuma na kutupa jicho juu ya meza ndogo ya urembo. Macho yake yakaiona pochi ya kike. Akarudi kuifuata na kumwacha Chiba akiwa hajui kinachoendelea. Akaufungua ule mkoba na kupitisha macho kijasusi, vidole vyake viwili yaani kile cha shahada na kati vikapenya na kuchomoa kadikazi, akaitia mfukoni. Alipotaka kutoka, akasita, akamtazama yule bwana pale kitandani. Akili yake haikumpa jibu sahihi, vinyweleo vikamsimama. Akainua mkono na kumpa ishara Chiba. Ishara ya hatari. Kutoka sebuleni, Chiba akachomoa bastola yake ndogo, akapachika kitu kama sindano kwenye mtutu wake. Akaiweka tayari. Kwa kutumia saa yake ya kisasa, Amata akampiga picha yule jamaa. Ni sekunde ileile alipojikuta akitazamana na mtutu wa bastola kutoka kitandani.
“Nilikuwa nakusubiri kwa hamu sana mjinga wewe,” yule jamaa akamwambia Amata, “Lete mlichokichukua!” akang’aka. Amata hakuwa na ujanja kwani domo la Magnum 22 lilikuwa likimtazama kwa uchu. Akataka kuingiza mkno kwenye jaketi lake ili atoa ile bahasha.
“Acha! Weka mikoni yako juu,” yule jamaa akamwamuru Amata huku akiteremka kitandani uchi wa mnyama, “Ninachukua mwenyewe, na ukileta kokolo kuna bastola tatu zinakutazama, zote zitakuchakaza kabisa”. Akamwambia kisha akapachika mkono kuitoa ile bahasha. Chiba hakifanya makosa, akafyatua ile bastola kutoka mafichoni. Kile kisindano kikapaa kwa shabaha malidhawa na kutua shingoni mwa yule jamaa. Yule bwana akatulia kama sekunde tatu hivi, akakichomoa na kumtazama Amata. Macho yake yalikuwa yakirembua kama mwenye usingizi mwingi. Konde moja zito sana kutoka kwa Kamanda likamshukia na kumbwaga chini. Amata akakiendea kile kitanda. Akavuta shuka na kulitupia huko. Kamera ndogo ikaanguka chini akaiokota.
“Mh!” akaguna. Akaitazama saa yake, ilikuwa tayari saa tisa na kitu. Akachomo kifaa chake kingine cha kumwezesha kutambua camera za siri. Akaangaza kila kona, kwenye maua ya urembo, taa ya juu, feni, na kila kona, hakuna kamera.
Haiwezekani! Akawaza. Akazichunguza picha za ukutani, alipoifikia picha ya Monalisa, kile kifaa kikatoa mwanga mwekundu. Akaiende na kuitoa palle ukutani, akakutana na kamera ndogo iliyofungwa kiufundi sana. Akaichomoa na kuitia mfukoni. Kamera nyingine akaikuta nyuma ya kioo cha meza ya urembo. Akaichukua. Alipojiridhisha kuwa kila kitu kipo sawa, wakatokomea zao nje ya nyumba hiyo.
Kwa hatua za haraka haraka wakakata mitaa mpaka walipoliacha gari lao. Wakaingia na kuketi. Chiba upande huu na Amata nyuma ya usukani. Akatia injini moto na kutoka katika ile barabara kuitafuta ile ielekeayo Kigogo. Kwa mwendo wa wastani wakakiacha kitongoji hicho na kuikamata Manzese, wakatokea Barabara ya Morogoro na kutokomea mjini.

ITAENDELEA
 
GENGE
EP 24

WAKIWA KATIKA maficho yao, Mc Tee, Big J na Bi Jesca waliagana wakiwa bado hawajapata ufafanuzi way ale wayatakayo. Walifikia muafaka wa kurudi kila mmoja anakoishi na wasubiri taarifa moja tu kutoka kwa Mc Tee. Kila mmoja alitumia njia yake ya siri kuondoka katika kisiwa hicho. Mc Tee baada ya kuagana na wenzi wake, alirudi ndani na kujitupa kochini. Akaminya kitufe Fulani chini ya meza yake. Sekunde chache tu, yule mwaDanada mrembo akaingia tena katika sebule ile nadhifu. Hakuwa mwingine, Hassna.
“Sikiliza Hassna, ni wewe pekee unayeingia katika chumba hiki. Narudia tena kwako, unachokiona humu kiache humuhumu. Wanaokuja humu wala usiwaulize wanatokea wapi. Ukikaidi, utakufa…” Mc Tee akamuaonya msichana huyo.
“Sawa bwana, kila siku nakuahakikishia kuwa ninakuelewa na siwezi kukaidi maagizo yako,” Hasna akajibu kwa unyenyekevu huku mikono yake kaikutanisha viganja mbele, chini kidogo ya tumbo lake.
Mc Tee alirudi kwenye meza yake ya kompyuta akimwacha msichana yule akitoka na kuingia chumba kingine. Alipohakikisha hayupo, akawasha kompyuta ile na kuunganisha kamera zake za usalama zote. Akachunguza kila kona ya kambi yake kuanzia nyumbani kwake mpaka kwenye hoteli kubwa na ile sehemu iliyojengwa apartment za wageni. Akaingia kila chumba kwa kutumia kameara za siri zilizofungwa katika vyumba hivyo. Akashuhudia yote ya chumbani nay a sebuleni ambayo wageni wake walikuwa wakiyafanya. Akatazama chumba cha mikutano na kusikiliza kila alichotaka na kile alichokuwa na wasiwasi nacho akakiandika kwenye kitabu chake cha kumbukumbu.
Akawatazama wageni wake mpaka walipopotelea kwtika upeo wa macho yake na kubadilika kuwa watalii katika kisiwa hicho. Akiwa ametingwa na kucheza na kamera hizo, simu yake ya mezani ikaita kuashiria nukushi iliyokuwa ikisubiri kuruhusiwa. Akaijibu kwa kuiruhusu, nayo ikaanza kujichapa katika karatasi. Ilipomaliza, akaikata na kuiweka mezani. Ulikuwa ujumbe. Ujumbe mfupi tu lakini wenye ujazo mwingi.

Mshenzi ametuwahi,
hatukuwa tumejua wapi Dastan ameificha ile siri.
Mshenzi ameichukua tukiwa chumbani humohumo.
Tumeinasa picha yake, tumeituma kwako.
Mc Tee alijikuta anaingiwa na baridi kali, hakujua nini anapaswa kufanya. Mwili ukatetemeka kwa hasira, moyo ukadunda woga na nywele zikasimama kwa hatari inayomkabili. Ni kwa miaka mingi walikuwa wakiitafuta siri ambayo Dastan aliificha baada ya kuichukua kwenye mikono ya Bambros. Siri nzito, iliyobeba kila baya kwa serikali na jema kwao. Mikakati, misaada, wahusika na kila kitu kilikuwa humo. Ni siri hii iliyofanya Dastan auawe. Aliikumbati, akaificha kisha maelekezo akayaweka katikaofisi nyeti na ya siri ya Chameleone kule Ocean Road. Pamoja na kupata pandikizi jingine ndani ya serikali, bado walishindwa kujua wapi siri ile ilifichwa. Wakafanya kila njia, wakaiweka mkononi nyumba ya Dastan ilikuona kama kuna chochote kitatukia.
Mc Tee akaigeukia kompyuta yake, ndani ya barua pepe akaipata picha aliyotumiwa. Mtu aliyevaa barakoa ya kuzuia hewa ya sumu. Hakuitazama sana, akaituma kwa rafiki yake Zelda akiomba msaada wa utambuzi wa kiumbe huyo. Alipojiridhisha kuwa imekwenda , akajitupa kitini, akaweka mikono kichwani huku macho akiyakodoa kuitazama picha ya Rais iliyokuwa ikininginia ukutani.
You are dead, Bastard! Akawaza, akiiambia ile picha. Lakini cha kushangaza, ile taswira ndani ya picha ilikuwa ikitabasamu daima kila ikimwangalia.
* * *
SIKU TATU BAADAE

SHAMBA

Kamanda Amata na Madam S walikutana katika chumba cha siri ndani ya jengo hilo. Kikao hicho cha wawili kiliitishwa na mwanamama huyo mara tu baada ya kukamilisha uchunguzi wa tafutishi ile waliyoipata katika nyumba ya Dastan.
“Unajua mpaka sasa hatujui nini kimempata Dastan…” Madam akamwambia Amata na kuiweka miwani yake vizuri, “…si yeye tu, hata mkewe,” akamalizia kusema.
“Miaka yote hii Madam, watakuwa washamuua,”
“Na kilichomuua ni hiki,” akamwambia akimaanisha ile bahasha, “Kama angekuwa hai, huyu kijana angekuwa katika ofisi hii,” akasema.
“Pole!”
“Asante,” akatulia kidogo na kushusha pumzi, “Sasa kuna kazi hapa Amata, inabidi uingie mzigoni. Tumeshapata pa kuanzia ili kuwamalizia hawa wawili waliyobaki yaani Kibwana Mtokambali na James Msambamagoya. Kama Dastan alivyodokeza kuwa ‘mkakati huu ni wa kudumu mpaka chama tawala kitoke madarakani iwe kwa damu au kwa maji’. Kwa maana hiyo lazima hukumu yao itekelezwe kama Jaji Mzava alivyohitimisha,” Madam akamwambia TSA 1 aliyekuwa mbele yake.
“Nakusikiliza HOT…”
“Kuna hii picha hapa ya huyu mwanamke, sijui ni mzungu au mwarabu, mtazame vizuri,”
“Kwani Chiba hakumtambua?”
Badala ya kumjibu, Madam S akamsogezea karatasi nyingine. Amata akaipokea, akaitazama juu yake na kuona picha ya yule mwana mke na maelezo kadhaa chini yake. Maelezo yale yalimtambulisha kwa jina la Babier Saratov, raia wa Jumuia ya Kisoviet ya Urusi ambayo mpaka wakati huu ilikuwa imesambaratika.
“Anaitwa Babier, yupo Saratov, Rusia,” Madam akamwambi.
“Kwa hiyo inabidi nifike Saratov?”
“Ikibidi dear…”
“Sawa Madam, ila naomba saa ishirini nan ne kuna kazi ndogo niimalize, kisha nitakuwa tayari kwenda popote utakapo isipokuwa kuzimu…” Amata akasema na kutia utani wake kama kawaida.
“Sawa, nakuhitaji hapa kesho kama saa hizi, tiketi yako itakuwa ta…,” Madam akakatishhwa na simu iliyoita kwa fujo. Akaichukua.
“Hello!” akaita.
“Wizara ya mambo ya nje inaongea,” sautiya upane wa pili ikajibu.
“Kwa niaba ya ofisi Alfa, Mambo ya nje unasomeka,” Madam akajibu kwa utambulisho huo. “Mwanausalama Dana Kalangila kutoka Lisbon atatua leo na ndege ya shirika la Swizz saa nne kamili
usiku. Ana mzigo wenu pokeeni tafadhali,”
“Copy!”
“Over and Out”
“Out!” Madam akakata simu. Akamtazama Amata usoni.
“Vipi?” Amata akauliza.
“Kumekucha mwanaume. Dana anaingia usiku huu saa nne na Swizz…” Madam akamwambia Amata.
“Habari nzuri hiyo, Gina na Jasmin watashughulika naye…” Amata akajibu.
Baada ya kupanga mikakati na kuiweka sawa, Madam S na Amata wakaagana kwa miadi ya kukutana muda wowote kabla ya hizo saa ishirini na nne kutimia kama ikibidi.
* * *
Kamanda Amata aliegesha gari jirani kabisa na maduka ya vifaa vya ofisini mbele ya chuo cha uandishi wa habari DSJ. Kutoka katika mfuko wake wa Suruali, akachomoa kadi kazi ile aliyoichukua katika kile chumba usiku uliopita.
“Mariam Shemweta,” akasoma jina na kutamka kwa sauti ya chini. Kwenye ile kadi kazi alipata jina na namba ya simu. Kadi ile ilimwelezea Mariamu kuwa ni mkufunzi katika chuo hicho. Hii haikumsumbua Amata kufika eneo hilo tayari kufanya kile anachokitaka. Taswira ya mwaDanada huyo akiwa kitandani usiku uliopita ilimjia Amata, akameza mate. Akachukua simu yake na kupiga namba Fulani iliyokwenda moja kwa moja injinia wa kampuni ya simu.
“Ndiyo kaka nambie!” sauti ya upande wa pili ikajibu.
“Swedi, kama kawaida…”
“Wapi leo nipe codes nifanye kazi,” Swedi akamwambia Amata.
“Nataka unifanyie Carnivore…”
“Lete codes!” Swedi alimwambia Amata. Alishaelewa lugha hiyo ya kijasusi ‘Carnivore’ ikimaanisha kuingilia mawasiliano ya mtu. Swedi, injinia wa simu katika mtandao wa DarCom aliipokea namba ya Mariamu kutoka kwa Amata na kuiingiza katika kompyuta yake. Kwa kutumia njia za kielektroniki akaiunganisha simu ya mwanamke huyo na ile ya Amata.
“Hey man!” akamwita Amatya ambaye alikuwa bdo yupo hewani.
“Yes!”
“Kazi imeisha, wash simu yako ile ya akiba, alafu iache wazi muda wote. Ili upate mawasiliano hayo vizuri, basi tumia blutooth device kaka,” akamwambia.
“Sawa nimekupata,” akamjibu.
“All the best, ukimaliza unipe tone nifunge. Angalia tu usije kuua mtu maana we na hao viumbe, nahisi ushahisi unaibiwa…. Hah hah hah hah” Swedi akamwambia na kumtania.
“Aaaaa ha ha ha … hamna bwana, Man at work!” Amata akamjibu na kuangua kicheko.
“Ok, ova!”
“Ova”.
Kmanda Amata, akawasha ile simu aliyoambiwa na kupachika kwenye dashboard ya gari. Akaingiza tarakimu nne za siri na kuifanya simu ile iwe hewani muda wote. Hivyo mawasiliano yote yanayotokana kuingia kwenye simu ya Mariamu yalisikika hapo bila shida. Akachukua kifaa chake cha masikioni na kukipachika. Ungemuona ungesema ni kiziwi kutokana na kifaa kile kilichofanana kwa umbo.
Mara tu baada ya kupachika, akakuta tayari kulikuwa na simu hewani. Akasikiliza kwa muda na kucheka tu. Ilikuwa simu ya Mariamu akiongea na shoga yake. Mazungumzo yao yalijawa na umbea.
Wanawake bwana, wanaacha kufanya kazi wanapiga umbea! Akawaza huku akiendelea kuwasikiliza. Muda huohuo, mbele ya gari lake kukaegeshwa Jaguar jeupe. Hakuna mtu aliyeshuka. Wakati umbea ule unaendelea kwenye ile simu aliyokuwa akisikiliza Amata, akasikia simu nyingine ikiingia katikati yake.
“Shoga subiri naona hubby ananipigia, nitakucheki baadae,” Mariamu akamuaga shoga yake. Mara tu simu ile ikapokelewa.
“Yes dear nimekumiss… unaendeleaje?” Sauti ya Mariamu ikasikika.
“Niko poa, lakini naapa mbele ya Mungu nikimtia mkononi yule shetani nanyonga,” sauti ya kiume ikasikika.
“Kabisa yani, jizi lile, halafu limetuvamia usiku… mi majizi siyapendi…”
“Usijali, nimekufuata, nipo hapa nje…”
“Sawa mpenzi nakuja, ngoja nifunge ofisi kabisa,” sauti ya Mariamu ikamjibu yule mtu wa kwenye gari. Ile simu ikakatika. Kamanda Amata akacukua kamera yake ndogo na kuitega tayari kupata picha atakazo. Dakika kumi baadae, mwanamke mmoja mwenye mwili wa wastani akajitokeza getini na mkoba mikononi. Suti aliyovaa ilionesha haswa kuwa ni mkufunzi. Hijab , kichwani mwake ilimtambulisha vyema kuwa ni muumini wa dini gani. Badala ya kupiga picha, Amata akajikuta akimkodolea macho. Akamtazama kutaka kujua kama ni yeye au la.
Ni yeye! Akajisemea moyoni, akaweka tena kamera yake vizuri na kupata picha kadhaa. Mlango wa dereva wa lile Jaguar ukafunguliwa. Kijana mtanashati akateremka na kuzunguka upande wa abiria, akafungua mlango. Sekunde hiyohiyo, Mariam akafika, wakakumnbatiana, kisha akapanda garini. Yule kijana naye akarudi upande wake na kuingia. Taratibu lile gari likaanza kuyaacha maegesho na kuingia barabara ya Simple kurudi barabara kuu ya Uhuru. Kamanda Amata akaipachika kamera mahala pake na kuanza kuwafuata taratibu.
Lile gari likaikamata barabara ya Uhuru kuelekea Kariakoo. Kamanda Amata akiwa katika makutano ya barabara ya Amana na Uhuru, akasubiri maari matatu yakae katikati yake na yule anayemfuata. Kisha naye akaingia na kumfuata taratibu. Safari ilikuwa ndefu mpaka mitaa ya Mbuyuni, Oysterbay. Barabara ya kwanza, ya pili, lile Jaguar likakunja kona kulia na kuingia mtaa wa Galu. Amata naye akakunja kwa kuwa njia hiyo pia ingeweza kumfikisha nyumbani kwake. Mita kama mia mbili hivi lile jaguar likasimama getini, Amata akapitiliza na kuendelea mbele. Hakwenda mbali sana, akaegesha gari kwenye mgahawa mmoja kando tu. Akateremka. Akaichomoa ile simu kutoka kwenye dash board na kuitia katika mfuko wa shati. Akavuta hatua taratibu kurudi kule lilikoingia lile Jaguar. Geti la nyumba hiyo lilifungwa, lile gari lilionekana kwa ndani. Akavuta hatua na kuingia mtaa mwingine. Kwa sadfa tu akakuta fundi viatu na mng’arishaji, akaketi.
“Karibu mkuu, karibu sana,” yule fundi akamchangamkia kana kwamba wanajuana miaka mingi. Akaketi kwenye kibenchi huku akihakikisha jicho lake haliipotezi ile nyumba. Akavua viatu kumpatia, akimtaka kufanya haraka kidogo.
“Mtaa wa matajiri,” Amata akasema.
“Aaaaa ndo hivyo, matajiri wapate na masikini tufaidike!” yule fundi akamjibu.
“Hii nyumba ya nani?” akauliza.
“Ipi? Hiyo kubwa ya kizamani?”
“Yap! Napenda sana nyumba kama hizi, haiuzwi?” Amata akauliza.
“Haiuzwi hiyo kaka, kuna kijana mmoja anaishi hapo, zaidi hutembelewa na marafiki tu,” fundi akajibu.
“Watu wana raha zao bwana. Ni mfanya biashara au?” akazidi kuhoji.
“Dah! Hata sijui yaani, namuonaga kaingia, katoka bas…”
Mazungumzo kati ya Amata na fundi huyo yalichukua kama dakika thelathini hivi. Wakiwa wamezama kabisa katika mazungumzo hayo, Mazda jekundu likawasili katika lile geti na kupiga honi. Geti lilipofunguliwaa, gari lile lilijitoma ndani. Amata akaendelea kupiga soga na mwenyeji wake, wakiyasifia haya na kuyaponda yale kule. Kutoka ndani ya nyumba ile, hakuna aliyetoka muda huo wote ambao Amata amekuwa kwa fundi yule.
“Hapa naona sawa kaka!” yule fundi akamwambia Amata wakati akimsogezea vile viatu.
“Oh shukrani sana,” akamshukuru na kumpatia noti ya shilingi elfu mbili. Wakaagana, na Amata akaenda zake. Akiwa katika hatua fupifupi kulielekea gari lake, simu ikaita mfukoni. Akaichomoa. Akaitazama. Chiba.
“Yes!” akaitika.
“Kuna pandikizi…” Chiba akasema kutoka upande wa pili.
“Wapi?”
“Njoo, tukutane Makumbusho ya taifa,” Chiba akamaliza na kukata simu. Kamanda Amata, akasimama kwa sekunde kadhaa, akifikiri jambo. Ushirika kati ya ubongo wake na mwili ukachukua nafasi. Akajitoma garini na kuondoka haraka kuelekea huko kwenye miadi na TSA2.

ITAENDELEA
 
GENGE
EP25

Njoo, tukutane Makumbusho ya taifa,” Chiba akamaliza na kukata simu. Kamanda Amata, akasimama kwa sekunde kadhaa, akifikiri jambo. Ushirika kati ya ubongo wake na mwili ukachukua nafasi. Akajitoma garini na kuondoka haraka kuelekea huko kwenye miadi na TSA2.
* * *

Nyumba namba 73A

Mariamu aliketi kwenye kochi kubwa la vono. Bilauri iliyojaa mvinyo wa Dodoma ilikuwa mbele yake huku TV kubwa ikionesha kipindi cha Jiji letu Dar es salaam. Mbele yake, katika kochi jingine aliketi yule kijana aliyekwenda kumchukua kazini. Na dakika nyingine kama thelathini hivi akawasili mwanaume mwingine, pande la baba, akaungana nao. Hakuwa mwingine zaidi ya Brian Mkuchu.
“Poleni kwa matatizo…” akawaambia huku akiketi vyema kitini. Jicho lake lilikuwa likimwangali Mariam kwa tuo. Labda lilikuwa likiuburudisha moyo kwa uzuri wa mwanamke huyo.
“Tumeshapoa,” akajibu yule kijana.
“Mariamu!” Brian akaita. Yule mwanamke akageuka kwa pozi na kumtazama mwanaume huyo kwa jicho la ubembe.
“Labeka shemeji…”
“Naomba usiniite shemeji kuanzia sasa!”
Bila kutegemea kauli hiyo, Mariamu alijikuta akiangusha bilauri ile sakafuni na kuruhusu mvinyo yote kumwagika.
“…umekuwa adui yangu namba moja,” akamwambia.
“Shem, mbona sikuelewi?” Mariamu akauliza kwa kitetemeshi.
“Narudia, usiniite shem! Kwa nini umeificha siri tunayoitafuta muda wote? Mpaka jana mpumbavu anaingia ndani kwako kuichukua…”
“…Siri! Siri gani Brian?” Mariamu akatahayari.
“Ina maana Andy hajakwambia nini tunataka?” Brian akamuuliza kwa ukali.
“Hapana…” akajibu.
Briana akachomoa bahasha na kuchukua picha tatu akamuwekea mezani, “Nataka unambie huyo ni nani?” akamuuliza.
“Aka! Simjui mimi…”
“Umetusaliti, umetuingiza motoni, utatutambua. Utatueleza huyu ni nani…” Brian akamwambia kwa ukali. Akainuka na kuwasha luninga nyingine ndogo. Mariamu akashuhudia picha ambayo hakuitegemea. Yeye na Andy wakiwa kitandani kama walivyozaliwa, wakioneshana ufundi wote katika sanaa ya mapenzi. Baada ya dakika kama tano hivi picha ikawaonesha wamelala fofofo. Kwa sekunde chache Andy akaamka akionekana mchovu na kuchukua mkoba wake. Akachukua kitu kidogo sana na kukipachika puani kwa jinsi ambayo hakikuonekana kirahisi. Picha ile ikaonesha kila kitu kuhusu Amata na Chiba, walivyoingia mpaka chooni na kufanya kila walichofanya. Mpaka Amata alipoanza kupachua kamera za siri na alipompiga ngumi Andy ndipo ikazimika.
Mariamu akashusha pumzi. Akawatazama kwa zamu. Akavuta mkoba wake na kuinuka, tayari kwa kuondoka. Hakutaka hata kuaga mtu. Lakini azma yake haikufikia lengo, alijikuta kavutwa nyuma na kusukumiwa juu ya kochi. Kwa ukaidi wake akainuka tena, mara hii, Brian akamnyanyua kama karatasi na kumtupa juu ya meza. Mariamu akapiga yowe la maumivu huku meza ile ikipasuka vipande. Kwa kitendo kile, Andy hakuweza kuvumilia. Akainuka na kutaka kumshika Brian, hakuweza. Konde moja la kilo nyingi likamrudisha chini.
“Lazima mjue kuwa nimekuja kwa kazi maalumu, na ninyi wawili mmeniharibia. Andy, kwa nini ulishindwa kuwapiga risasi wale jamaa na hukuwa umelala? Ulidanganywa na huyu Malaya? Tutakufanya kama tulivyomfanya Dastan,” Briana akaunguruma. Mkanda mkononi. Akamtazama Mariamu.
“Unambie wale ni akina nani?” akamuuliza na kuanza kumtandika kwa mkanda ule bila huruma. Hasira iliwaka ndani ya Brian hakukuwa na wakuizuia. Mariam hakuweza kujitetea zaidi ya kulia mpaka sauti kukauka. Mwanaume yule hakujali, aliendelea kumsulubu kwa mikanda mpaka aliporidhika.
“Utamuua Brian, mtu ukishampiga hivyo na hajakwambia kitu ujue ni innocent!” Andy akasema.
“Unanifundisha kazi? Wewe Andy ni mzembe. Ulishindwaje kulichukua lile faili pale ofisini kwako mpaka kile kibibi kinakuzidi maarifa? Sehemu ya pili ya ile siri, je; sote tulijua kuwa imefichwa na Dastan…” akahema kwa nguvu “tukafanya yote kujua anayeishi pale ni nani, tukampata, ukamlaghai kwa mapenzi ukampata, badala ya kufanya kazi mapenzi yakakulevya. Faili linguine linaibwa hapo hapo unaona kwa macho…. You are so stupid. Ninyi wawili mmepanga, sasa mtakiona,” Briana akabwata mpaka Andy akaogopa. “Toa huu mzoga wako, kaufunie stoo, usiku huu tutauzika mimi na wewe!” akamwambia huku tayari mkononi keishakamata bastola. Andy hakuwa na jinsi akamtazama Mariamu akiwa pale chini, nguo yake yote ikiwa imetota kwa damu. Kimya. Dalili ya uhai haikuwapo. Hakuweza kumwinua, akamburuza mpaka stoo. Akiwa katika kumweka sawa, akajikuta akipigwa na kitu kizito. Andy akayumba na kujibamiza ukutani, akaanguka juu ya Mariamu. Brian akaondoka na kutokomea kusikojulikana.



Makumbusho ya Taifa

Kamanda Amata aliegesha gari nje ya lango kuu la jengo hilo. Akateremka na kuufunga mlango nyuma yake. Sekunde tano zikamtosha kutazama huku na kule kama kuna lolote baya kwa upande wake. Hamna. Akavuta hatua na kuingia katika uwanja wa jengo hilo. Hakukuwa na watu wengi kwani tayari muda wa kufungua ulikuwa umekaribia sana. Ni Wazungu wachache tu waliokuwa wakirandaranda na kupiga picha hii na ile. Akazikwea ngazi na kujitoma ndani.
Ndani ya jengo hilo kulikuwa na mambo mengi ya kihistoria hususan juu ya taifa la Tanzania na Tanganyika ya zamani. Historia za watawala na watawaliwa katika uga tofauti. Chiba alikuwa amesimama mbele ya picha kubwa iliyosheheni maandsihi mesngi ya Kiingereza na Kiswahili. Amata akasimama karibu yake.
“Kuna lolote?” akamuuliza.
Chiba badala ya kujibu, akaondoka eneo lile. Amata naye akamfuata. Mguu kwa mguu mpaka
katika chumba kingine, wakaingia ndani. Chumba hicho kilikuwa ni ofisi yenye kila kitu kinachostahili kuwapo ofisini. Palikuwa na viti viwili tu; yaani cha mwenye ofisi na cha mgeni wake. Chiba moja kwa moja akaenda kuketi kwenye kile cha mwenye ofisi na Amata akaketi kwenye kile kingine.
Upande ule, Chiba akavuta droo na kutoa picha nne, akamwekea Amata mezani.
“Unamkumbuka?” Chiba akamuuliza. Amata akatazama ile picha kwa makini sana.
“Si ni yule bwege wa leo!”
“Good! Anaitwa Andrew Makita,” Chiba akamwambia.
“Andrew Makita!” Amata akalirudia jina lile kwa mshangao na kumtazama Chiba.
“Mbona unashtuka? Unamjua?”
“Simjui kwa sura ila kwa jina namjua kuwa ni mwanakondoo…”
“Anafanya biashara…” Chiba akasema. Amata akabaki kimya, akamkazia macho TSA2.
“Unataka kuniambia, huyu dogo ana linki na hawa majahili…”
“Swadakta!” Chiba akaitikia, “Kwa tafutishi nyingine nilizozipata katika ile bahasha… huu mtandao ni hatari,. Bado wana azma ya kuipindua serikali iwe kwa maji au kwa damu. Wamepanga kuwa, kama wameshindwa kwa kutumia bunduki basi watakuja kwa njia nyingine. Mapinduzi yao ni awamu tatu. Awamu ya kwanza walishindwa mwaka 1964, awamu ya pili wakashindwa tena mwaka 1980. Sasa awamu ya tatu wamepanga kuja kivingine. Maadam serikali imeamua kuruhusu mfumo wa vyama vingi, basi wamejificha kupitia humo. Plan A ilikuwa ni kuiangusha serikali kwa kutumia sanduku la kura, inaonekana hii ni ngumu. Plan B ni mbaya Zaidi…”
Amata akabaki kimya kusikiliza kwa umakini wa hali ya juu. Lakini aliposikia kuwa plan B ni mbaya hakuweza kutulia kwani kama kuna kitu kilikuwa hakipendi basi ni wananchi wasiyo na hatia kuingia matamatanui kwa tamaa za watu wachache.
“Ubaya upi?” akauliza.
“Hili genge limejiwekea nadhiri kuwa, endapo litashindwa kwenye sanduku la kura mara tano mfululizo, litaingia msituni…” Chiba akasema na kuweka tuo. Amata akamkazia macho kwa yale anayoyasikia.
“Nchi hii hii au nyingine?” akauliza.
“Hii hii,”
“Aya, ngoja tuone. Enhe… na nani anyewafadhili?” akaongeza swali.
“Amata, hii taarifa haijakamilika. Inaonekana Dastan hakufanikiwa kuipata yote, hivyo hatuna budi kutembelea nyumba namba 73A… kwa sababu kaizungumzia sana katika taarifa hii,”
“Mtaa wa Galu,”
“Yes!”
“Leo leo usiku…”
“Naunga mkono,” Chiba akajibu. Akarudishia droo na kuifunga kwa ufunguo kama mwanzo. Ukimya ukajidai kati yao kwa jozi la sekunde.
“Hayo ni yote kwa leo…” Chiba akamwambia Amata huku mikono yake yote miwili ikiwa juu ya ile meza.
“Andrew Makita, inabidi akacukuliwe apelekwe shamba haraka iwezekanavyo. Hawezi kuidoublecross serikali yake…” Amata akasema, “Leo tuna kazi mbili kubwa, kumtia mkononi Andrew na lazima lifanyike jioni hii. Pili kufanya black bag Mtaa wa alu namba 73A,” akamalizia.
“Haswaa, nilikuwa nasubiri mpango kazi, maana nakujua, ukishasikia haya huwezi sema kesho wala kesho kutwa,” Chiba akamwambia Amata.
“No! Chiba,” Amata akawa kama mtu aliyegutushwa.
“Ndiyo kaka…”
“Twende Galu sasa hivi…” akamwambia.
“Kamanda, kweupe sana,” akaitazama saa yake, ikamwambia ni saa tisa na dakika thelathini alasiri,” Chiba akatia shaka kwa hilo.
“Nina maana yangu kusema hivyo Chiba! Leo mchana nilimuungia mkia huyu bwana, kutokea Ilala DSJ maana mpenzi wake ni staff pale. Na safari yao iliishia kwenye hiyo nyumba. Nafikiri ni vyema twende sasa, la kutokea litokee, twende,” Amata akamwambia Chiba.
“Sawa, ila hapa nimetembea kizembe Kamanda…” Chiba akasema akimaanisha hana silaha.
“Hata mimi, twende ofisi ndogo tukafunge mzigo,” Amata akamwambia.
Wote wawili wakainuka na kutoka nje ya jengo hilo. Wakaingia garini. Moja kwa moja mpaka ofisi ndogo. Madam S alikuwa bado ofisini akiendelea na majukumu ya serikali. Alipowaona vijana hao akapata tashwishwi ya kutaka kujua kulikoni. Kwa maana katika ofisi hii, huja kwa kuitwa au hutoa taarifa.
“Nyie vipi? Mmefumaniwa?” akawauliza.
“Hapana, tunaenda vitani…” akamjibu huku akivuta mlago wa kabati baada ya kuufungua ule wa chuma. Madam S akainuka na kutoka pale mezani, akawafuata.
“Nyi’’ watoto mbona siwaelewi?”
“Tupo kazini mama, tunaenda Mtaa wa Galu, nyumba namba 73A. lolote linaweza tokea, usilale…” Amata akamwambia Madam S huku akimpa Chiba shot gun iliyoshiba risasi na bastola moja. Na yeye akachukua kama hivyo hivyo. Akafunga lile kabati na kumgeukia bosi wake.
“Kuna mjukuu wako anafanya ujinga, tunaenda kukuletea popote alipo…” akamwambia na kumpigia saluti. Madam S alishazoea utani wa TSA 1 hata wawapo kazini. Lakini alimjua vyema awapo sirias na awapo katika utani. Siku hii alimsoma kijana wake na moja kwa moja akajua kuwa kuna jambo zito.
“All te best!” akawaambia. Amata na Chiba wakapotelea nje. Mwanamama huyo akaifuata lunina yake na kuiwasha kamera inayoonesha matukio ya nje kwenye maegesho ya magari. Akawaona vijana wake wakiingia garini haraka haraka na kuondoka.
“Mh!” akaguna na kujishika kidevu kwa sekunde kadhaa, akifikiria jambo. Kilichomtatiza mwanamama huyu ni jisi vijana hao walivyoingia na kuondoka. Ijapokuwa mapambano yote ya silaha hupangwa mezani lakini yapo yanayotokea kwa nasibu tu na haya humtaka mtu kujihami mwenyewe. Hili hakulielewa kabisa. Akavuta hatua na kuiendea simu yake ya mezani. Akaminyaminya tarakimu Fulani na kuiweka sikioni.
“Hello, Gina!” akaita na kuitikiwa upande wa pili.
“…”
“Fika Mtaa wa Galu, nyumba namba 73A, kachunge mikia ya kaka zako kule…” akakata simu na kuirudisha katika kitako chake. Akaiendea meza yake na kuketi kitini.
* * *
Brian alitulia kimya katika ndani ya baa ya Mwanamboka eneo la Kinondoni. Akili yake ilikuwa imetibuka, aliwaza hili akawaza lile. Hakupata jibu. Aliona wazi kuwa Andrew kamfanyia hujuma. Lakini bado akawaza kuhusu Mariamu. Mariamu alijua kuwa pale ndani pana siri akaiuza kwa watu wengine. Hapana.mawazo yaligongana, fikra zikashindwa kuwa kitu kimoja. Brian akagutuliwa na simu yake ya kiganjani iliyoita kwa fujo. Alipotazama kwenye kioo, akasoma, ‘Babu’. Moja kwa moja akajua kuwa mwito huo una maana yake. Akainuka haraka na kuiacha ile pombe yake mezani. Haikuwa na maana tena.
Ndani ya gari lake, Mazda, jekundu, Brian akatulia tuli. Akafyatua simu yakena kuiweka sikioni.
“73A”akaitikia.
“Code 005, Amata Ric, Unstopable human being. Brian, htumepata kumtambua mtu mwenye uficho wa code hiyo ya 005. Yupo hapo hapo Tanzania, ni mtu hatari sana. Tumetazama rekodi zake kwenye kabrasha za mashirika ya kijasusi duniani, MI6 wamemueleza kama mwaDanamu hatari mwenye kasi ya ajabu katika mapambano. Interpol nao wanamfahamu kama ‘Thorn’ yaani mwiba ambao ukikuchoma kupona ni kitendawili…” mtu wa upande wa pili akaeleza kwa sauti ya taratibu.
Brian akajikuta akipatwa na ubaridi mkali kuanzia unyayoni mpaka utosini. Akashusha pumzi ndefu. “Kwa hiyo unaniambiaje? Maana kuna ripoti nilikuwa naiandaa nikuletee ya huyu mpumbavu Makita,” Brian akaeleza.
“Kwanza kabisa, ili tufikie lengo letu mwaka huu, huyu 005 lazima auawe hata kama ni kwa kumroga,” sauti ile ikamwambia ikiwa kwenye mwangwi ili isitambulike kiurahasi. Brian akapumua kwa nguvu. Kisha akamweleza kila kitu kilichotukia siku hiyo.
“Kwa hiyo, Andrew Makita anataka kufanya kama Dastan? Sawa maadam umesema yupo ndani, nenda ukamuue sasa hivi kisha myeyushe kwa tindikali asionekane tena duniani…”
“Ok Sir!” Brian akajibu.
“Shughulika na huyo Andrew, muache huyo mwanamke ili umtumie kama chambo cha kumpata huyo mpumbavu mwingine,”ile sautio ikamwambia.
“Copy!” akakata simu na kulisha gari lake. Akatoka kwenye maegesho na kuingia barabara kubwa ya Kawawa kuelekea Morocco.
* * *

ITAENDELEA
 
Nimeamka nikajua tayari inaendeleea hizi stori za kijasusi nazipendaga sana
 
GENGE
EP26

Shughulika na huyo Andrew, muache huyo mwanamke ili umtumie kama chambo cha kumpata huyo mpumbavu mwingine,”ile sautio ikamwambia.
“Copy!” akakata simu na kulisha gari lake. Akatoka kwenye maegesho na kuingia barabara kubwa ya Kawawa kuelekea Morocco.
* * *
Kamanda Amata na Chiba wakawasili katika ile nyumba. Wakateremka na kuliacha gari umbali mdogo kutoka katika geti la nyumba hiyo.
“Kazi moja tu!” Amata akasema.
Chiba akaitikia kwa kichwa, wakavuta hatua kulielekea geti la nyumba hiyo. Hakuna aliyeongea. Silaha zao zolikuwa zimefichwa kwenye makoti waliyovaa, usingeziona. Walipoukaribia mlango, ghafla kwenye kona, likaibuka Mazda jekundu. Amata akampa ishara Chiba, wakajifanya wapita njia, wasisimame kwenye lile geti. Lile mazda likafika getini. Geti likafunguliwa kwa mtambo maalumu na kisha kujifunga mara tu baada ya gari lile kuishilia ndani. Amata na Chiba wakatazamana. Wakaizunguka ile nyumba na kugundua kuwa ilikuwa imepaka na nyumba nyingine ambayo haikuonekana kuishi watu. Upande huo haukua na mambo mengi. Amata akaitazama ile nyumba pweke, nyasi na magugu viliotea ndani yake. Akauendea mlango na kujaribu kuusukuma, ukafunguka, wakaingia ndani na kupambana na nyasi ndefu, magugu na nyuzi ngumu za buibui. Ukuta wa nyumba hii ulipakana na ule wanaoutaka. Katika yake kulikuwa na uchochoro wa mita moja hivi.
“Hapa panatufaa!” akamwambia Chiba. Wakajiweka tayari kukwea ukuta ule. Haukuwa mrefu sana, kama mita tatu na nusu hivi. Kamanda Amata akajiweka sawa, akakinga mikono yake kwa nyuma. Haraka Chiba akaelewa nini cha kufanya. Akaweka mguu wake katika viganja vya Amata, akajiinua na kuuweka mwingine kwenye bega. Akakamata ukuta ule sawia na kujivuta haraka juu huku akiuacha mguu wake ukining’inia. Amata akaukamata ule mguu na kuutumia kukwea ukuyta ule mpaka juu. Walipokuwa juu, wote kwa pamoja wakajirusha mpaka ukuta wa pia na kutua ndani ya wigo huo kwa ustadi mkubwa na kutulia kimya. Tukio hilo lilichukua sekunde kumi tu. Walipoona kuna ukimya na utulivu wa kutosha wakainuka na kila mmoja akapita upande wake, wakakutana mlango mkubwa.
Ndani ya nyumba hiyo, Brian alisikia mchakacho wa viatu. Nina wageni! Akawaza na kuiendea droo kubwa ya mezani, akatoa bastola na kuiweka sawa, tayari kwa lolote. Akajibanza nyuma ya kabati lilikuwa jirani kabisa na mlango mkubwa.
Nje ya nyumba hiyo, Chiba alikuwa wa kwanza kuufikia mlango. Amata akabaki nyuma na kuiweka tayari ile shot gun yake. Chiba akatoa ishara kuwa anaingia, Amata akatikisa kichwa kumwonesha kuwa yuko sawa kwa kumlinda. Mchezo wa hatari. Akaruka kwa guu lake la kulia na kuvunja mlango ule. Ukaachana vipande viwili, akachomoa bunduki yake na kuiweka sawa. Ndani kulikuwa kimya.
Tunapambana na mjuzi! Chiba akawaza na kuanza kuvuta hatua kuingia ndani. Brian alijibana palepale pasina kutikisika. Alianza kuona kivuli cha mgeni wake kikitangulia kabla ya mwenyewe kuingia ndani. Sekunde chache baadae, akamwona mtu huyo akizama ndani na bunduki yake ikiwa mbele kabisa. Kwa macho ya harakaharaka, Brian aliona jinsi bunduki ile ilivyoshikwa kikakamavu. Taratibu akaamua kuiweka bastola yake kibindoni ili amfanyie shambulizi la kushtukiza. Ikawa hivyo. Brian aliruka na kutua kwenye shingo ya Chiba kwa pigo moja la karate. Chiba hakupata nafasi ya kujitetea kwa pigo hilo. Alipogeuka alikutana na pigo lingine lililotua kwenye chembe ya moyo. Akapepesuka na kuanguka vibaya sakafuni. Brian alikuwa akijipanga kuiendea ile bunduki ya Chiba, hakuwahi. Ghafla alijikuta mikononi mwa Kamanda Amata. Mapigo saba yenye kasi ya ajabu yalimwacha hoi sakafuni akiwa hajiwezi. Brian akiwa chini sakafuni alihisi kama kapigwa kwa chuma. Akakusanya nguvu zake zote na kuinuka kumkabili Amata. Amata akasimama kimya akimtazama jinsi anavyojipanga. Akarusha mapigo mfululizo kumwelekea Amata lakini yote yakaepwa kwa ustadi kabisa. Kamanda Alikuwa akitafuta nafasi tu na alipoipata akapeleka pigo la nguvu kwenye chembe ya moyo. Brian alipotaka kukinga, akachelewa. Pigo lingine la karate likatua kwenye koromeo. Amata akaruka kimo cha ng’ombe na kumtandika teke la mbavu lililompeleka chini. Brian alitambaa mita kama tatu akageuka ghafla na bastola mkononi. Amata akaruka kandona sisasi tatu zikapita nukta chache kutoka pale alipoangukia. Sekunde hiyo hiyo akashuhudia kichwa cha Brian kikifumuka vibaya na mwili wake kusukumwa kando. Amata alipogeuka nyuma, macho yake yakamtazama mwanamke mrembo aliyesimama katikati ya mlango huo. Gina.
“Muwe mnaaga mnapoondoka,” Gina akasema huku akiipachika bastola kiunoni mwake.
“Tungekuwa hatujaaga ungejuaje kama tuko huku?” Amata akamjibu huku akinyanyuka na kumwendea Chiba aliyekua akiinuka taratibu huku bado anakohoa.
“Vipi kaka uko poa?” Amata akamuuliza.
“Yea, mpumbavu aliniotea huyu…” akasema wakati akisaidiwa kuinuka. Amata na Gina wakaanza msako wa chumba kimoja baada ya kingine. Kila kimoja kilikuwa tupu, sanasana ni picha na vijatabu mbalimbali. Kila walipokuwa kitabu cha kumbukumbu walikibeba. Amata alipoutikisa mlango wa stoo akakuta mgumu haufunguki. Akaupiga teke, ukafunguka na kujibamiza upande wa pili. Aliyoyaona hapo, mwili ulimsisimka. Miili ya watu wawili, anaowatambua, aliowafuatili mchana wa siku hiyo. Andrew Makita na Mariamu walikuwa wamelaliana. Wamekufa? Akajiuliza. Akavua saa yake na kuuchukua mkono wa kushoto wa Andrew. Akafanya kama anamvesha. Akabana vyema na kuwasha nobu ya kusoma mapigo ya moyo. Ikamwonesha kuwa kijana huyo bado mzima ila yupo katika mzimio mzito. Akafanya hivyo na kwa yule mwaDanada pia, vivyo hivyo. Haraka akamtaka Gina kuleta gari. Dakika mbili tayari gari ilikuwa pale ndani ya wigo. Wakasaidiana kuwapakia wote wawili.
“Mpigie simu Jasmini, tukutane shamba,” Amata akatoa maagizo. Gina akaingia garini na kuondoka kwa kasi kuelekea shamba na kuwaacha vijana wale wakiwa bado katika ile nyumba. Chiba aliendelea kupekua hapa na pale, akachukua hard disc ya kompyuta na makabrasha mengine muhimu. Akabomoa sefu moja iliyowekwa kwa siri nyuma ya ukuta na kufunikwa na picha kubwa ya kisiwa cha kuvutia. Wakachukua kila kilichomo ndani.
“Safi, unajisikiaje sasa?” Amata akamuuliza Chiba.
“Bado sipo vizuri sana…”
“Ok, Jasmin atakufanyia uchunguzi. Tuondoke zetu!” Amata akamwambia Chiba. Kabla ya kutoka Chiba akatega kamera yake ya siri ambayo aangeweza kuifuatilia kutoka umbali wa mita mia tano na pale ilipo. Wakatokea getini na kulifunga vizuri. Wakaingia garini na kuondoka zao. Amata akapiga simu kwa Madam S.
“Mission clear! Mwambie Simbeye aende kuna mzigo wake. Hiyo nyumba iwe chini ya ulinzi wa siri mpaka tutakaposema,” Amata akamwambia bosi wake.
“Sawa, linafanyiwa kazi… uelekeo wapi? Nataka kupata taarifa ya uvamizi wenu,” Madam S akamwambia Amata.
“HOT, tunaelekea shamba, tuko na wafu wawili tunataka kujaribu kuwafufua ili watugee waliyonayo. Hapa tuna tafutishi za kutosha ambazo nafikiri zitatupa njia sahihi ya kulibomoa hili genge,”
“Safi sana TSA1, tutakutana huko saa mbili zijazo,” Madam S akajibu na kukata simu.
* * *

SAA 6 BAADAE

Akili, moyo na mwazo ya Mc Tee havikutulia kabisa. Katika Utaratibu wa kazi walivyojiwekea ni kwamba, ikipita saa sita simu yako haipokelewi basi maana yake umeshakufa au haupo salama. Kwa mara ya kwanza, hakutaka kukubaliana na hilo ijapokuwa ndiyo Utaratibu wao wa kazi. Akaitazama saa yake, muda unayoyoma. Nini kimetokea hajui. Simu ya mwisho kwa Brian ilikuwa ni kumpa maelekezo ya mtu wa kummaliza, code 005. Na sasa Hakuna jibu. Amekufa? Akajiuliza. No labda amekamatwa! Akajifariji. Akatembeatembea barazani huku akiangalia maji ya bahari yanavyoyumbayumba kwa madaha. Wala hali ile haikumpa ahuweni ya mawazo. Yalisongeka haswa.
Akaamua kurudi ndani na kuketi kwenye ofisi yake ndogo, ambayo kwayo walikutana na watu wake si chani ya saa hamsini zilizopita. Akawasha kompyuta na kuwaita wote. Walipokuwa online mazungumzo yakaanza.
“Bandari salama si salama tena,” akawaambia.
“Kwa vipi comrade?” Big J alikuwa wa kwanza kuuliza kwa shauku.
“Brian hayupo hewani kwa saa saba sasa,” akawaambia.
Wote wakaelewa mara moja nini anamaanisha. Wakasikitika kwa sekunde chache kisha mazungumzo yakaendelea.
“Jesca, nafikiri huna budi kwenda Dar… na kwa kuwa tayari ulikuwa na hilo moyoni, ruksa,” Mc Tee akamwambia.
“Sawa comrade nitafanya hivyo,” Jesca akajibu.
“Yatupasa kuwa makini, maana top ranking tunakwisha. Kama wameweza kunasa zile siri pale ndani mjue kuwa kazi tunayo,” Mc Tee akawaeleza.
“Mkakati upoje?” Big J akauliza.
“Tuwe kimya kabisa, tusubiri Jesca atatuambia nini. Mimi nitaondoka kesho kuelekea Urusi kukutana na mkulu kisha nitawaunganisha kwa tamko la mwisho,” Mc Tee akawaambia wenzi wake kisha simu ikakatwa na kila mmoja akatakiwa kufanya kadiri ya maagizo hayo ya awali.
Mara baada ya simu ile kukatwa, Mc Tee alijitupa kochini na kujinyoosha. Akavuta simu yake na kupekua namba zilizopo. Baadae akafanikiwa kuipata ile aitakayo, kampuni ya ndege. Kwa kuwa pesa haikuwa tatizo kwake, aliweza kupata tiketi ya siku inayofuata katika kampuni ya KLM. Baada ya kuhakikisha kuwa amekamilisha malipo yote, akaandika memo ndogo na kuipeperusha mpaka kwa mwenyeji wake kuwa yupo njiani.





JIJI LA DAR ES SALAAM lilikuwa katika hali ya utulivu. Wingu zito lilitanda na kuleta giza hafifu. Kama kawaida, wakazi wa jiji hilo walianza kujiandaa kwa kuipokea mvua kubwa waliyoitabiri.
Adha ya mvua katika jiji hili huwa ni mbaya hata kupelekea vifo na mafuriko katika maeneo Fulani. Hii yote ni kutokana na miundombinu mibovu isiyoendana na mahitaji ya jiji hilo.
Upande wa pili wa jiji hilo, yaani Kigamboni, Madam S alilitoa gari lake katika pantone na kuanza safari ya kuelekea Gezaulole. Mwendo wake wa wastani ulimcukua takribani dakika arobaini na tano kufika eneo hilo. Akayaaca makazi ya watu na kuanza kupita mashambani mpaka kijiji kidogo ambacho kwacho ndipo waliweka makazi yao ya siri, ‘Shamba’. Alipofika tu getini hakusimama maana geti hilo lilifunguka lenyewe. Magari yote waliyokuwa wakiyatumia kiofisi, yalifunwa kifaa maalumu ambacho kiliwasiliana na sensa ya geti umbali wa mita ishirini na kufanya lifunguke atomatiki.
Ndani ya jumba hilo alikosekana Jasmini pekee, kwa kuwa alikuwa katika kazi maalum.
Madam S akaingia na kupokea heshima zote kutoka kwa vijana wake. Alistahili kwa kuwa alikuwa Spymaster makini katika taifa. Head Of TSA ‘HOT’. Aliyeaminika kubeba ulinzi wa siri wa Rais na urais wake.
Ndani ya jumba hilo hilo, katika vyumba viwili tofauti; kimoja alilazwa Mariamu na kingine Andrew Makita. Wote wawili walilazwa katika vitanda vya Chuma tupu bila hata godoro. Vitanda hivyo vilikuwa na uwezo wa kubadili hali tatu kwa nyakati tofauti. Ama viwe vya baridi sana au moto wa kubandua ngozi au shoti kali za umeme. Mikono na miguu vilifungwa katika mwisho huu na ule. Mwilini kila mmoja alibaki na nguo ya ndani tu. Ngozi ilikutana na chuma moja kwa moja.
Andrew alikuwa wa kwanza kuamka kutokana na ubaridi mkali katika vyuma hivyo vy akitanda. Akavuta mkono huu, umefungwa, akatikisa mwingine , vivyo hivyo. Na miguu nayo alkadhalika. Akagwaya. Akapepesa macho na kugeuza shingo huku na huko, akapambana na maumivu makali. Akakumbuka alivyopigwa na Brian kwa kitu hasichokijua. Chumba kilikuwa na ukubwa wa wastani. Zaidi ya kitanda hicho kulikuwa na mashine nyingine ndogo pembeni. Andrew aliijua vyema mashine ile. Ukuta wa kile chumba, ulitisha. Alama za damu za watu waliouawa kwa risasi zilitapakaa kila kona, hewa nzito iligubika. Hakukuwa na dirisha isipokuwa tundu dogo la kupita kalamu juu kabisa ya paa lake.
“Shiiit!” Andrew alilalamika. Hakuwahi kufika sehemu kama hii tanu azaliwe. Aliogopa. Moyo wake ukaanza kupunguza kasi ya mapigo yake.
Brian amenileta huku? Mshenzi huyu wanataka kuniua! Akawaza. Akajitahidi kupiga kelele, lakini sauti yote alijisikia mwenyewe tu. Mlango mzito wa chuma ulikuwa upande wa kichwa chake, hivyo asingeweza kuona nani anaingia ndani ya chumb hicho.
Katika chumba kingine, Mariamu alishtuka ghafla baada ya kujikuta akipigwa shoti ya umeme. Akapiga ukelele wa nguvu lakini haukusaidia chochote kutokana na kile chumba kilivyojengwa. Mariamu alianza kutetemeka kwa hofu, maumivu makali ya majeraha ya kile kipigo kutoka kwa Brian yalianza upya mara baada ya kurudiwa na fahamu.
“Niko wapi! Niko wapi miye…?” akaanza kuongea mwenyewe. Kila akiutazama ule ukuta alizidi kuchanganyikiwa. Damu mbichi ilikuwa sakafuni, na ile iliyoganda ilikuwa chini sakafuni. Katika moja ya kona ya chumba hicho aliona mkono wa mtu na upanga uliolowa damu chini yake. Akaanza kutweta huku macho yakiwa yamemtoka pima. Hofu ile ikamfanya apoteza fahamu kwa mara nyingine.
* * *
ITAENDELEA
 
GENGE
EP27

Niko wapi! Niko wapi miye…?” akaanza kuongea mwenyewe. Kila akiutazama ule ukuta alizidi kuchanganyikiwa. Damu mbichi ilikuwa sakafuni, na ile iliyoganda ilikuwa chini sakafuni. Katika moja ya kona ya chumba hicho aliona mkono wa mtu na upanga uliolowa damu chini yake. Akaanza kutweta huku macho yakiwa yamemtoka pima. Hofu ile ikamfanya apoteza fahamu kwa mara nyingine.
* * *
Katika chumba maalumu kilichofungwa mitambo mbalimbali ya mawasiliano, Gina alikuwa ameketi huku vidole vyake vikigongagonga meza ambayo juu yake kulikuwa na kompyuta kubwa na ukuta wa mbele yake ulikuwa na luninga iliyokuwa ikionesha chumba kile alichofungwa Mariamu. Ni hapa alipokaa kwenye hii meza palikuwa na kitu kama kichakata cha kompyuta amacho kilibeba batani kumi. Alipoona mwanamke yule bado yupo kwenye mzimio alibonyeza tu batani moja na shoti kali ya umeme ilimchapa, akaamka.
“Safi sana msichana mzuri!” Gina akatamka kwa sauti ya chini, akaanza kuiongoza kamera iliyofungwa kwa siri ndani ya chumba hicho kumwangalia vizuri mwanamke huyo. Gina alitazama mahangaiko yote ya mwanamke huyo na kuanza kucheka kwa hofu waliyomtengenezea.
Katika ofisi hiyo hiyo, meza kubwa ya upande wa pili, Chiba naye alikuwa mbele ya lunina nyingine akamtazama Andrew Makita katika mahangaiko yake ile ndani. Kwa kutumia kamera yake ya siri, iliyofungwa ndani ya chumba hicho, Chiba aliweza kumchunguza kijana huyo atakavyo. Dakika hiyo hiyo, Kamanda Amata na Madam S wakaingia katika ofisi hiyo.
“Haya vijana. Nataka kujua uhusiano wa Mariamu na Andrew,” Madam S akawaambia.
Chiba akamtazama Gina na kumpa ishara. Gina akaminya tenaile swichi na kumpiga shoti ya umeme Mariamu. Akashtuka na kupiga kelele, akajivuta kama anataka kukaa lakini vile vifungo vilimrudisha chini.
“Mariamu!” akasikia sauti ya kike yenye mwangwi ikimwita. Akageuka huku na huko, hakumwona mtu.
“Be-e-e!” akaitika kwa shida.
“Hicho kitanda ulicholalia, kina uwezo wa kukupiga shoti ya umeme, kina uwezo wa kukubanika kwa moto kama kuku na kina uwezo wa kukugandisha barafu… sasa chagua kati ya hivyo vitatu unataka nikufanye kipi sasa hivi?” Gina akamuuliza.
“Ha-ha-pana, usini-fa-nye cho-cho-te…” Mariamu akajibu.
“Sawa, sintokufanya chochote kama utanipa majibu ninayotaka…” Gina akamwambia kwa sauti ya upole.
“Sawa!” Mariamu akajibu huku akitweta kama mbwa aliyekimbizwa.
“Unamjua Andrew Makita?” Gina akaamuliza.
“Ndi-yo, uhhh!”
“Ni nani kwako?”
“Alikuwa mpenzi wangu…” akajibu na kuanza kulia.
“Alikuwa mpenzi wako? Kwani sasa mmeachana?”
“Siiimmmtaki hata kumuona…… ah!” Mariamu akaanza kulia.
“Nyamaza, sitaki makelele yako,” Gina akamkaripia. Mariamu akanyamaza na kubaki na kwikwi za kilio. Alionekana tangu usoni kutomtaka kabisa mwanaume huyo.
“Hebu nambie mara ya mwisho ulimuona wapi?” Gina akauliza.
“Ahaaaa dah, mara ya mwi-sho jana, nime-pi-gwa na rafiki yake, hakunitetea… wewe ni nani kwanzzza?” akajibu. Kitendo cha kuamka ‘jana’ kilimfanya Gina agundue kuwa mwanamke amepoteza kumbukumbu kiasi fulani.
“Wapi ulikuwa ukipigwa nay eye akiwepo?”
“Kinondoni,” Mariamu akajibu kwa utulivu.
“Hapo ndipo ulikuwa unaishi?”
“Hapana…”
“Unaishi wapi?”
“Mburahati NHC,”
“Kwenye nyumba ya nani?” Gina akamtupia swali ambalo lilimfanya Mariamu atulie kidogo.
“Naikiaga jina tu Kihwelo, hata simjui, sijawahi kumuona,” akajibu.
Gina akamtazama Madam S. Madam S akampa ishara aendelee kumuuliza. Wakati huo mashine ya kurekodi sauti ikiendelea kufanya kazi.
“Nikikwambia kuwa Andrew na huyo rafiki yake wana mpango mmoja kwako, utakataa au utakubali?”
“Ntakubali tu…”
“Kwa nini?”
“Yeye ndo amenipeleka kwa rafiki yake, napigwa hanitetei… maana yake nini sasa? wale majambazi kwanza, majambazi kabisa,” Mariamu akaanza kulia tena.
Madam S akampa ishara ya kuzima ile microphone, Gina akafanya hivyo. Madam S akamgeukia Chiba.
“Mpe disprin kwanza, pumbavu huyo!” akamwambia. Chiba akaminya batani na kumpiga shoti moja mbaya ya umeme. Andrew alipiga kelele na kujitikisa huku kauma meno kisha akarudi kitandani na kuanza kutweta kwa nguvu.
“Chiba! Unafanya nini?” Madam S akang’aka.
“Si umenambia nimpe disprin, hii ndiyo disprin Madam!” Chiba akajibu.
“Shenzi kabisa wewe! Unataka kumuua mwenzio!” Madam akamwambia Chiba huku akiketi vyema kitini, “Endelea!” akamwambia.
“Umetugeuka Andrew!” Sauti ya Chiba ikasikika ndani ya chumba kile kwa mwangwi. Andrew aliisikia. “Mimi sijawageuka ila mnahisi hivyo,” Andrew akajibu kwa sauti tetemeshi.
“Sisi tuna akili, na tunajua umetugeuka… na wale uliokwenda kuwapa taarifa zetu juu ya kesi hii wamekugeuka!” Maneno hayo ya Chiba yalimshtua Andrew. Akashindwa kuongea na kubaki akimwemwesa midomo, “Ninyi ni nani?” akauliza huku akihema. Chiba akaangua kicheko kirefu ambacho upande ule wa pili kinakuwa cha kutisha.
“Sisi ni kaka zako tuliokulea, mpumbavu wewe! Haya nieleze kwa Mariamu ulikuwa unafuata mapenzi au kitu kingine?” Chiba akauliza. Andrew akaendelea kuhema na kubaki kimya.
“Hutaki kunijibu! Kumbuka kitanda ulicholalia kina kazi kubwa tatu, kukupiga kwa umeme, kukubanika kama kuku au kukugandisha kama barafu. Usiponipa majibu kimoja wapo kitachukua nafasi,” Chiba akaweka mkono wake kwenye batani tayari kuruhusu kimojawapo. Akaanza kuzungusha taratibu.
“No! no! no! Nooooooo!!!” Andrew akapiga kelele baada ya kuhisi vyuma vya kile kitanda vikipata moto.
“Semaaaaaa!!!” sauti mbaya yenye mwangwi ikasikika masikioni mwake.
“Ravennnnn!” akajibu kwa kutumia lugha ya kiintelijensia.
“Kwa ajili ya nani?” Chiba akauliza.
“Nilitaka yule mwanamke anipe siri iliyofichwa ndani ya ile nyumba…”
“Nani aliyekwambia mle ndani kuna siri?” Chiba akahoji haraka haraka.
“Godfather!”
“Godfather ni nani?”
“Simjui, nimesikia sauti yake mara moja tu! Noooooo tafadhali msinichome!” Andrew akaanza kulia kama mtoto. Kamanda Amata akaukamata mkono wa Chiba na kuutoa kwenye ile batani.
“Acha tafadhali, inatosha!” Amata akasema huku macho yake yakiwa yamejawa machozi yasiyotaka kumwagika. Madam S akamtazama Amata, wakagongana macho.
“Hata wewe una huruma leo?” Madam akamuuliza Amata.
“Sometime yes! Sometime no!” akajibu kisha akageukia tena kwenye ile luninga na kumtazama Andrew akihangaika pale kitandani. Amata akatikisa kichwa kushoto kulia.
“Tuambie wajibu wako kwao, ulikuwa unawanyia nini?” Amata akamuuliza.
“Nilikuwa na kazi ya kuiba siri za serikali dhidi yao… pamoja na yote walikuwa wanataka kabrasha lenye Top Secret kuhusu mapinduzi ya mwaka 1980 dhidi ya serikali,”
“Uliwapa?”
“Sikufanikiwa kulipata, lakini nakala yake ilisemekana imefichwa nyumbani kwa marehmu Dastan Kihwelo,” Andrew akajibu vizuri kabisa.
“Tunaitaka hiyo uliyokuwa unaitafuta kwa Kihwelo,” Amata akamuuliza.
“No! sijaipata pia, iliibwa usiku na watu wasiojulikana. Inaonekana kuna watu wengine pia walikuwa wanaitaka na walijua ni wapi ipo,” Andrew akaeleza kwa uwazi.
“Dastan Kihwelo yuko wapi?” Amata akauliza.
“Huyu jamaa aliuawa miaka kama kumi na mbili nyuma…”
“Nani aliendesha mauaji yake?”Amata akahoji.
“Hawa jamaa wana timu kubwa na mbaya katika mauaji. Mauaji ya Dastan yalisimamiwa na mwanamke wa Kirusi anaitwa Barbier Saratov,” akaeleza. Haraka Chiba akaandika jina lile.
“Maiti yake ilizikwa wapi?” akamuuliza tena.
“Kwa kweli sifahamu, ninachojua ni kuwa wakiua mtu wanamyeyusha kwenye tindikali ili kupoteza ushahidi,” Andrew akaeleza. Amata na Chiba wakatazamana huku Madam S akitikisa kichwa juu chini.
“Umeshawahi kumsikia Kibwana Mtokambali na James Msambamagoya?” Amata akauliza.
“Hao wote ni marehemu, na wanaheshimiwa sana na lile genge…”
“Mkuu uliyeongea naye ni nani?”
“Simjui!”
Madam S akawapa ishara ya kusitisha zoezi. Wakati huo simu ya mezani ilikuwa ikiita kwa fujo.
“Wafungulieni kwa muda, kisha warudishwe uraiani,” madam S akamwambia Chiba. Kwa kidole chake akabonyeza batani moja tu na vile vifungo alivyofungwa Andrew kwenye kile kitanda vikaachia kwa mara moja. Bila kuchelewa akajitupa chini sakafuni huku akiugulia maumivu. Gina naye akafanya vivyo hivyo na Mariamu akawa huru.
Madam S aliifikia simu ile na kuinyakua, akaiweka sikioni, “Ground Zero!” akaitikia.
“D.I.A terminal two. Mzigo umefika, ova and out!”
“Copy!” Madam akajibu na kukata simu. Akawatazama, Amata, Chiba na Gina kwa zamu.
“Dana amefika!” akawaambia.
* * *
Dana aliwasili uwanja wa ndege majira ya saa kumi jioni. Mara baada ya kumaliza taratibu zote za uhamiaji na kuchukua mabegi yake, alijiandaa tayari kwa kutoka nje ya uwanja huo. Aliangaza macho kwenye vioo vinavyoonesha watu walioko nje kwa minajiri ya kuwaona ndugu na jamaa waliokuja kumpokea. Akawaona, japo wao hawakumuona. Dana alijawa na furaha sana kwa kurudi nyumbani baada ya kuondoka kikazi miaka mitatu na kwenda kuhudumu katika ofisi za ubalozi wa Tanzania nchini Ureno.
Akiwa tayari kila kitu kimekamilika alipakia mizigo yake kwenye kitoroli tayari kwa safari ya kuondoka uwanjani hapo. Akiwa ndani ya chumba cha kufikia wageni, Dkt. Jasmini tayari alikwishamuona mwanamke huyo ambaye kwaye ametumwa kuhakikisha anafika shamba. Akaingia msalani, akafungua begi lake na kuchukua koti lake la kidakitari. Akalivaa. Kishapo akachukua sindano yake ndogo, akavuta dawa kidogo na kuifunga. Akaitia mfukoni na mkono wake ukabaki huko. Akatoka na kuangaza macho kujua ni wapi ameelekea. Akamuona. Akavuta hatua kumfuata na alipomfikia akasimama sentimeta chache nyuma yake. Akahakikisha hakuna mtu anayemuona kwa kile atakachokifanya. Akachuku ile sindano kwa siri na kumdunga ubavuni. Dana akasikia kitu kikimchoma, akageuka kutazama akakutana macho na mwanamke huyo.
“Unajisikiaje Dana?” jasmine akamuuliza.
“Ummmennnifanya nnnninnnni?” akamuuliza kwa kuvuta maneno. Tayari dawa ile ilisafiri haraka sana na kuanza kukata mawasiliano ya fahamu za mwaDanada huyo. Sekunde hiyo hiyo, Dana akaanza kutokwa na povu kinywani. Akaishiwa nguvu na kulegea. Dkt Jasmini akachukua simu yake ya upepo.
“Mgonjwa wetu amezidiwa, msaada wa kitanda tafadhali! Ova!” akaita.
“Msaada unakuja mara moja! Ova!” akajibiwa upande wa pili.
Kutoka kwenye maegesho ya magari, nje ya uwanja huo, Scoba akatia moto injini gari lake la wagonjwa alilokuwa nalo siku hiyo. Akapiga king’ora na kupata msaada wa njia haraka mpaka karibu kabisa na mlango mkubwa wa kutokea wageni. Akaupita na kulizungusha gari upande wa ndani wa jingo hilo. Walinzi hawakuwa na shaka kwani walishapewa taarifa ya mgonjwa huyo, lango likafunguliwa. Akaingiza gari na kuliegesha salama. Akateremka na kufungua milango ya nyuma, akatoa kitanda cha magurudumu na kuwahi kuingia nacho ndani. Dana akapakiwa juu ya kile kitanda na kufungwa barabara akiwa hana lepe la fahamu. Kwa haraka kitanda kile kikaingizwa garini. Kikawekwa mahala pake na safari ikaanza.
Nusu saa baadae, gari lile likaingizwa kwenye maegesho maalumu huko Shamba. Madam S, Kamanda Amata, Chiba, Gina, wote walikuwa hapo maegeshoni wakimsubiri mgeni wao.
“Kazi nzuri Jasmini na msaidizi wako Scoba,” Madam S akawaambia huku akiwapa mkono kila mmoja. Dana akaingizwa ndani katika chumba maalumu, akaondolewa kwenye kile kitanda na kuwekwa juu ya kitanda kingine cha chuma. Akalazwa hapo akiwa kafungwa mikono na miguu kwa vifungo maalumu. Baada ya hapo timu nzima ikaingia kwenye chumba maalumu cha mawasiliano. Ndani ya chumba hicho, waliweza kumwona vyema mgeni wao. Wakasubiri aamke.
“Dozi ya saa ngapi uliyompatia?” Madam S akamuuliza.
“Masaa mawili tu,” Jasmini akajibu huku akijiegemeza kitini.
“Nafikiri kutoka kwake, tutapata mengi sana…” Madam S akamwambia Amata.
“Kabisa, huyu alitaka aniuze kule Lisbon,” Amata akajibu.
TSA, wote wakaketi kila mmoja katika kiti chake. Mbele yao kulikuwa na luninga moja kubwa inayoonesha mitaa mbalimbali ya jiji la Dar es salaama hasa zile sehemu nyeti kama
Muhimbili, Uwanja wa ndege, Bandarini, Ikulu na maeneo mengine. Huko shughuli ziliendelea kama kawaida, pilikapilika za watu zilishika hatamu. Wakati mazungumzo hayo yakiendelea katika chumba hicho, Chiba alikuwa ametingwa kwenye kompyuta yake akipekua hili na lile. Cyber Intelligency.
“Hapa tulipokwama, huyu mwanamke atatukwamua tu… anajua mengi sana,” Amata akasema na wengine wakatikisa vichwa kukubaliana naye.
* * *
ITAENDELEA
 
GENGE
EP28

Hapa tulipokwama, huyu mwanamke atatukwamua tu… anajua mengi sana,” Amata akasema na wengine wakatikisa vichwa kukubaliana naye.
* * *
Chiba aliendelea na kazi yake katika kompyuta hiyo bila kubughudhiwa na mtu. Aliendelea kuchimbua mafaili waliyoyapata kwenye ile Hard Disk waliyoichukua kule Mtaa wa Galu. Miongoni mwa hayo yalikuwepo yenye taarifa anuai juu ya mmpango wa mapinduzi. Lakini kila moja lilikosa mambo mengi na kumtaka msomaji apate taarifa kutoka katika faili kuu.
Faili kuu! Chiba akawaza na kujaribu kupekua hilo faili kuu, asilipate. Akamgeukia Madam S aliyekuwa akizungumza na Amata na wengine.
“Madam!” akaita, mwanamama huyo akageuka kumtazama kijana wake, TSA 2, “Naweza kupata sauti ya Kibwana Mtokambali? Kama aliwahi kurekodiwa mahali akiongea…” akauliza.
“Bila shaka, kwa kuwa yeye alikuwa kiongozi wa serikali, lazima RTD watakuwa nayo. Ngoja kidogo,” Madam akamjibu na kuchukua simu yake. Akabofya namba fulani na kuiweka sikioni. Akaongea na mtu wa upande wa pili kwa dakika chache kisha akakata simu ile. Akamgeukia Chiba, “Subiri kama dakika tano hivi, wanaangalia kwenye maktaba yao. Unataka ya nini?” akamjibu na kumtupia swali.
“Kuna sauti hapa nimeipata ya mazungumzo kati ya Andrew na huyo anayemwita mkulu. Ijapokuwa sauti yenyewe ina mwangwi lakini si tatizo. Nataka kuifananisha na hiyo, nione, kama ni ya mtu mmoja au vipi,” Chiba akaeleza. Madam S akaitika kwa kutikisa kichwa juu-chini.
“Ok, unaamini kuwa Kibwana atakuwa hai?” Madam akauliza.
“Ninaamini kwa asilimia sitini. Sikilizeni! Hawa watu wanajua wanachokifanya. Kama wao wangekufa nani sasa anayeplan kuendeleza mapinduzi?” akawajibu kwa swali. Madam S akawatazama vijana wake, kila mmoja alitikisa kichwa kama ishara ya kukubaliana na Chiba.


Saa Tatu Baadae

Bado TSA wote walikuwa kwenye chumba kilekile wakijadiliana hili na lile. Dana akionekana juu ya kitanda kile amelala kwa utulivu.
“Jasmini! Ina maana Dana ulimpa dawa ya muda gani?” Madam S akawa wa kwanza kuingiwa shaka na jambo hilo.
“Nimempa ya masaa mawili tu, nashangaa hili ni saa la tatu hajaamka!” Jasmini akajibu.
Madam S akashusha pumzi ndefu. Kabla hajasema lolote, simu yake ikaita. Akaipokea na kuiweka sikioni, “Yes!” akaitikia.
“Mzigo tayari, unauchukuaje?”
“Namtuma kijana sasa hivi!” Madam S akajibu na kumtazama Scoba. Kijana huyo akainuka mara moja kitini na kusimama, tayari kusikiliza .
“Fika RTD, muone Jamila Msemakweli, atakupatia mzigo, nausubiri hapa…” akamwambia.
“Sawa madam!” Scoba akajibu kwa nidhamu ya hali ya juu na kuiacha ofisi hiyo. Madam S akarudisha akili yake tena kwa hawa waliobaki.
“Huyu inatupasa kumwamsha, hivihivi atajilaza pale kutupotezea muda!” Gina akasema. Madam S akatikisa kichwa kumpa ishara Gina kuwa afanye hivyo. Bila kuchelewa, akaminya kitufe cha kwanza, cha pili na baadae akaminya nobu nyingine. Shoti kali ya umeme ikampiga Dana. Akatoa ukulele wa maumivu. Gina hakuachia nobu ile mara moja mpaka Madam S alipomvuta mkono kwa nguvu.
“Gina! Hivi hujui kuwa unaweza kuua?” akamuuliza.
“Najua!”
“Sasa?”
“Lazima apate adabu kidogo kwa kusaliti nchi yake.
Dana alitulia kimya kitandani baada ya shoku ile ya umeme. Kifua chake kilionekana wazi kupanda na kushuka haraka haraka. Akatazama huku na kule kwa kugeuzageuza kichwa chake.
“Dana!” sauti iikamwita, akatulia kuisikiliza. Hakujibu chochote. Sauti ile yenye mwangwi ikarudia kuita karibu mara tatu, lakini mwanamke yule hakuitika, wala hakuonesha kuwa anajali.
“Jeuri huyu!” Gina akasema na kubonya tena kile kitufe. Shoku nyingine ya volti nyingi ikampiga Dana takribaki sekunde kumi hivi. Kelele kali ikasikika katika spika ndogo ndani ya kile chumba. Gina akaachia ile nobu.
“Dana!” ile sauti ikaita.
Dana akabaki kimya. TSA wakatazamana wote kwa mara moja.
“Amekula yamini, hawezi kusema…” Jasmini akadakiza kwa kauli hiyo. Kamanda Amata akamtazama Madam S aliyekuwa kimya akimtazama msichana huyo kwenye luninga kubwa ukutani.
“Nunda!” Madam S akasema na kumtazama Amata, “Nahitaji wanawake kama hawa kwenye idara yangu,” akamalizia huku akisimama kitini.
Vijana wake wote wakamfuata kwa macho kumtazama. Hawakuwahi kumsikia akisema kitu kama hicho hata siku moja.
“Unataka kumpa kazi?” Kamanda Amata akauliza.
“Mh! Mwanaume hupitwi… haya mi natoka nahitaji Dana azungumze. Nitakaporudi nipewe taarifa ili kazi ianze rasmi muda huohuo!” Madam S akatoa maagizo na kukiacha kile chumba. Kamanda Amata akageuza macho yake na kutazama luninga ile, hakujali alichosema bosi wake. Chiba bado alikuwa akiiweka mitambo yake vyema, tayari kurekodi kila kitu ambacho atakisema mwanamke huyo.
“Dana, kuna mambo matatu tu ambayo naweza kukufanyia endapo hutosema lolote,” Amata akamwambia na sauti ile iliyojaa mwangwi ikamfikia mwanamke huyo vyema kabisa.
“Sina la kuwaambia,” Dana akajibu kwa kauli fupi.
“Tunataka kujua, uhusiano wako kati yako na genge la akina Mwanachia,” Amata akamwambia.
“Mwanachia alikuwa mpenzi wangu, hakuna lingine,” akajibu. Amata akatulia kwa sekunde kadhaa.
“Bob Marley alisema ‘Only your friend know your secret’ kwa maana hiyo unajua siri na nyendo za marehemu Mwanachia,” Amata akamwambia.
“Negative,” Dana akajibu akimaanisha hapana.
“Mara baada ya kuuawa Mwanachia, ulienda kufanya nini pale Rua Camarante, lote 25?” Amata akamtupia swali ambalo lilimfanya ababaike kidogo.
“Wewe! Unapajua Rua Camarante, lote 25?”
“Jibu swali Dana!” ile sauti ikamwambia.
“Nilienda kwa mpenzi wangu,” Dana akajibu kwa sauti kavu kana kwamba hakuna hatari yoyote iliyomzunguka. Alijua, tayari yupo safe house, kwenye mikono ya watu wanaoijua kazi yao. Hakuumiza kichwa kwa maana alijua kati ya waliopo ndani humo lazima Amata anahusika kwa kuwa ndiye aliyekuwapo kule Lisbon.
“Nani alikuwa mpenzi wako?” Amata akauliza kwa sauti ileile.
“Yule uliyemuua!” Dana akajibu. Jopo la TSA likatazamana.
“Amejua anaongea na sisi?” Gina akauliza.
“Bila shaka. Ni mwanausalama huyo, lazima anajua yuko wapi...” Chiba akajibu. Kamanda Amata akatulia kimya akimtazama pale kwenye luninga. Wakati wote wapo kimya, Gina akawasha umeme volteji ya juu. Shoku mbaya ikampiga Dana, akapiga yowe moja na kukata sauti.
“Najua sasa utanieleza,” Amata akamwambia.
“Si-siwezzzzi... siammmini ka-ma nchi ya-ngu inawe-za kkkkunifanya hivi,” Dana akaongea kwa shida. Gina akawasha nobu nyingine. Kile kitanda kikaanza kupata moto.
“Umeisaliti!” Amata akamwambia.
“Nnnnnnoooooooo!!!!” Dana akapiga kelele. Akajaribu kujigeuza, wapi! Vifungo vya kitanda hicho vilimkamata barabara. Vyuma vya moto vikaanza kuichoma ngozi yake kwa uchu.
“Nnnnnnoooooooooooo, nnnnaaaasemmma!” akapiga kelele.
“Niambie, wako wapi washirika wa Mwanachia?”
“Uhhh! Saratov, Russia” akaongea kwa akionekana kuwa na maumivu makali. Dana aliuma meno wakati upande wa pili Gina alikuwa akitabasamu. Kamanda Amata akampa ishara Gina apunguze moto. Akafanya hivyo.
“Saratov, Russia!” Chiba akarudia jina lile.
“Nataka utambue picha mbili, na unipe majibu yake haraka!” Amata akamwambia. Dana akatikisa kichwa juu-chini kuitikia. Amata akamtazama Chiba na kumpa ishara kwa kichwa. Chiba akabonya mahala fulani. Luninga ndogo ikajitokeza katika kile chumba. Picha ya kwanza ikaonekana ya mwanamke wa kadiri ya miaka hamsini hivi, Mzungu.
“Unamjua huyo?” Amata akauliza.
Dana akatulia kwa sekunde kadhaa, kisha akajibu, “Namjua, anaitwa Barbier!”
“Ana uhusiano gani na hili genge?” Amata akauliza.
“Babier ni muuaji mwenye taaluma hiyo. Ni mtu wa karibu sana katika genge hili... ana akili nyingi sana,” Dana akajibu kana kwamba si yule aliyekuwa akilia maumivu dakika chache zilizpita.
“Mfungue!” Amata akaamuru na Gina akabonyeza kitufe cha kufungua vile vifungo vya kitanda. Dana akainua mikono na kujinyoosha, kisha akajiangusha chini sakafuni.

MSOCOW – URUSI

K

kochi kubwa la von o. Kochi lililompakata vyema na kumnyemeleshea usingizi mtamu usi ATIKA HOTELI ya kifahari ya Moscow Mariot Trevaskaya, Mc Tee alitulia kimya juu ya
kifani. Alikuwa ndani ya chumba cha ukubwa wa wastani, chenye makochi mawili tu yanayofanana. Aliletwa ndani ya chumba hichi na mhudumu wa hoteli hiyo, akitakiwa kumsubiri mwenyeji wake. Mbele ya kochi hilo, kulikuwa na meza moja iliyotengenezwa kwa kioo tupu. Juu yake paliwekwa chupa mbili za pombe kali zenye chapa ya Whisky 73.
Nusu saa baadaye, mlango wa chumba kile ukafunguliwa, akaingia mwanamke wa makamo ambaye alitambuliwa mara moja na Mc Tee.
“Mr. Mc Tee karibu sana Moscow!” yule mwanamke akamkaribisha. Akavua gloves zake na kuziweka kando. Jaketi nalo vivyo hivyo. Akachukua chupa moja wapo kati ya zile mbili. Akaifungua na kummiminia Mc Tee kwenye bilauri yake. Kisha vivyo hivyo akafanya kwake. Akaiinua bilauri yake na kuipunga hewani.
“Cheers! Kwa afya yako…” Yule mwanamke akasema wakati wakignganisha bilauri zao. Kisha kila mmja akapeleka kinywani na kugugumia.
“Huko nje kuna baridi kali sana. Huwezi kutka bila kupata Whisky au Vodka”.
“Najua vyema maisha yenu Babier…” Mc Tee akamwambia yule mwanamke. Kisha wakapiga mafunda mengine kadhaa kabla ya kuanza mazungumzo.
“Anasemaje Colonel Ivan Chernyakhovsky?” Mc Tee akamuuliza Barbier.
“Hajambo kabisa, anajiandaa kukutana na wewe kwa dakika ishirini tu. Alikuwa huko Afrika ya Kati amerudi leo,” Barbier akaeleza, “Na vipi maendele ya kazi yetu? Ni Tanzania tu ambako mnatuangusha hatujui mnakwama wapi,” akaongeza swali
“Kuna kazi kubwa!” akajibu. Baada ya kupiga fundwa lingine na kuliskmezea tumboni, akamtazama Barbier, “Umakini wa kwenye maswala ya kiintelijensia unanitia hofu, wanatuchokna mpaka wajue tulipo,” akaongeza jibu. Barbier, akainama chini. Baada ya sekunde kadhaa akainua us wake.
“Ina maana wamewagundua?” akauliza kwa sauti ya chini.
“Bado, ila nana wanapita kwenye njia ambay, tukichelewa, watatutia mkononi,” Mc Tee akaeleza.
“Lakini nyinyi mna makosa! Tuliwaambia kuwa Afrika haiwezi kugeuzwa kirahisi kama yai kwenye kikaango, mkatuhakikishia inawezekana. Look! Mtaingia kwenye mikono ya serikali sasa hivi!” Barbier akazungumza kwa uchungu.
“…Kote tulikopanga mapinduzi, tumemaliza. Tanzania tu, tunakwama. Hebu kuweni wanaume kidogo, mlijaribu kuitikisa nchi kipindi kile, sasa hivi, mmezeeka? Andaeni vijana tulete mzigo mfanye kazi,” Barbier aliongea kwa mamlaka kama anaongea na mdogo wake.
“Najua…”
“Hata Ivan hajafurahi kabisa baada ya kusikia habari ya Brian…” Barbier akamkatisha sentensi yake. Ukimya ukatawala kati yao, hakuna aliyeongea wala kutikisika.
“So?” Mc Tee akauliza kwa kifupi.
“Tuna dakika kumi za kwenda kumwona Ivan… lazima ukubaliane na atakachokisema…” Barbier akamwambia Mc Tee na wakati huo huo kijana momja wa Kizungu akaingia katika chumba kile. Unadhifu wake ulimnadi waziwazi kuwa ni mlinzi wa mwanamke huyu. Mc Tee alimtazama mwanamke yule, akamkumbuka miaka mingi nyuma akiwa msichana mbichi. Akamkumbuka jinsi alivyofanikisha mauaji ya Dastan kwa mtindo wa kipekee kabisa. Alimkumbuka, Barbier, ndani ya Mazda jekundu.
Baada ya mazungumzo machache na yule kijana safari ikaanza. Mc Tee alivaa koti lake kubwa na zito ili kujikinga na baridi kali ya jiji hilo.
Aurus Senat, gari la kifahari, zalisho la Urusi, lilikuwa tayari likiwasubiri. Mc Tee alilitazama kwa makini na uchu jinsi lilivyopendeza.
Huwezi kulimiliki ndinga kama hiiAfrika! Akawaza. Barbier akaingia kwanza na Mc Tee akafuatia. Milango ikafungwa. Mshangao wa Mc Tee haukujificha mbele ya Barbier.
“Utalimiliki ukiwa Rais,” akamwambia.
“Na sura langu hili?” naye akauliza.
“No! kama tuliweza kukuua hatutashindwa kukufufua,” Barbier akamjibu na lile gari likaiacha ile hotel taratibu. Taa za nje, barabarani na majengo yaliyojengewa mapaa mithili ya ice cream zilivutia katika dutu la giza jepesi.
* * *

ITAENDELEA
 
GENGE
EP29

No! kama tuliweza kukuua hatutashindwa kukufufua,” Barbier akamjibu na lile gari likaiacha ile hotel taratibu. Taa za nje, barabarani na majengo yaliyojengewa mapaa mithili ya ice cream zilivutia katika dutu la giza jepesi.
* * *

Iliwachukua takriban dakika arobaini na tano kuwasili katika Msitu wa Khimki, uliyo nje kidogo ya Jiji la Moscow. Msitu wenye takribani ukubwa wa hekta elfu moja. Ndani ya msitu huu kulikuwa na nyumba kadhaa za kupumzikia wageni wanapenda kutembelea uoto wa asili. Babier na Mc Tee waliwasili katika moja ya nyumba kuukuu iliyojengwa ndani ya msitu huo. Utulivu na ukimya vilitosha kumfanya aliyesimama hapo kuingiwa na hofu. Barbier akapiga mbinja mara tatu kisha akafuata mlango wa nyumba hiyo uliyosongwasongwa na mimea itambaayo.
Kuna biDanamu anaishi humu? Mc Tee akajiuliza. Barbier akasukuma ule mlango, nao ukafunguka bila shida.
“Nifuate!” akamwambia Mc Tee. Akaingia ndani ya ile nyumba na kuufunga mlango nyuma yake. Yule mwanamke akachukua taa ya kandili na kuiwasha, akaiweka kwenye kiango na kuendelea mbele kama mita kumi hivi. Hapo palikuwa na mlango mwingine uliofuatiwa na ngazi zilizoteremka chini. Wakateremka pamoja mpaka walipokuta mlango mwingine. Barbier akabofya kengele na ule mlango ukafunguka. Mara tu walipoingia, macho ya Mac Tee yakapokelewa na sebule pana yenye kila aina ya samani za thamani. Taa nzuri za umeme zenye urembo wa aina aina zilikuwa zikining’inia darini. Sebule hii haikuwa na mtu zaidi yaw a wawili tu. Katika ukuta mmoja wapo palitundikwa picha kubwa sana ya mtu ambaye Mc Tee alimfahamu fika, Vladimir Ilyich Ulyanov au wengi walimtambua kama Lenin.
“Keti hapa!” Barbier akamwambia Mc Tee, naye akatii na kuketi mkabala na picha ile kubwa. Picha ya mwanamapinduzi wa Kirusia, mwanasiasa na mnadharia wa siasa aliyeamini katika mapinduzi. Aliyesimika nadharia yake ya Leninism, iliyojikita katika jinsi ya kuunda vyama vya kimapinduzi. Aliyejenga kaulimbiu ya ‘Kifo cha Uhuru’.
Yote haya Mc Tee aliyakumbuka pindi alipokuwa akisimuliwa na rafiki yake huyu, Colonel Ivan, walipokuwa huko Kiev katika mafunzo ya kijeshi na medani za usalama. Mc Tee akajikuta akibebwa na usingizi baada ya kusubiri kwa muda mrefu.
“Pasipo na nadharia ya mapinduzi, hapawezi kuwa na vuguvugu la mapinduzi”. Mc Tee akashtuka kutka usingizini, macho yake yakagongana na yale makali ya Colnel Ivan. Hakujua wala hakuwa na uhakika kama sentensi ile iliyonukuliwa kwenye moja ya hotuba za Lenin ilitamkwa na Ivan au alikuwa ndotoni tu.
“Mc Tee…” Ivan akaita huku akiwa kajiegemeza kwenye kochi lililokuwa mkabala na lile aliloketi Mc Tee.
“Comrade Ivan,” akaitikia.
“Mapinduzi hayawezekani bila kuwa na hali ya kimapinduzi; alikadhalika, siy kila hali ya kimapinduzi itatuongoza kwenye mapinduzi,” Ivan alinukuu manen mengine ya mwanamapinduzi Vladimir Lenin. Mc Tee hakushangaa, alimjua swahiba wake huyo jinsi alivyoishiba falsafa ya Lenin, falsafa ya mapinduzi.
“Kwanini unashindwa kufikia ndoto zako mpaka umri unakutupa?” Ivan akamuuliza. Mc Tee akabaki kimya kwa muda.
“Nashindwa kujua, kama nashindana na serikali ileile ya Tanzania au la!” akajibu.
“Mbinu zote tumekupa, watu wa kuwatumia tumekupa, shabaha tumekunesha, shida nini?” Iva akamuuliza swali jingine.
“Medani ya usalama Tanzania imekuwa na weledi wa hali ya juu sana. Anayetutafuta hatumwoni lakini anatupunguza taratibu,” akajibu.
“Nimekuficheni ninyi wawili, hakuna anayejua mlipo, lakini mpo palepale… sasa kama mbinu zte zimeshindikana, twende msituni…” Ivan akamsisitizia.
“Na ndilo lililonileta,” akajibu Mc Tee. Colonel Ivan akatikisa kichwa kama ishara ya kukubali. Babier akaingia sebuleni hapo akiwa na chano iliyobeba pombe kali na bilauri mbili. Akawamiminia. Wawili hawa wakagonga cheers na kujimiminia matumboni mwao. Walipoweka bilauri zile mezani, wakatazamana.
“Hiyo ndiyo mbinu ambayo washirika wangu wote wameitumia na kufaulu… kwa kuwa umeamua, utafaulu. Tanzania haitaweza kuziona nyayo zetu zilizobaki. Walipofika wamefika ukomo, na katika hili nitajua tu nani yupo nyuma yao…” akapiga funda jingine na kuitua bilauri ile mezani. Mc Tee, akaigiza mkono katika mfuko wa koti na kuchomoa picha moja. Akaiweka mezani. Ivan akainyakua na kuitazama kwa makini, akavuta kumbukumbu ya sura anayoiona kwenye picha hiyo. Akatikisa kichwa kama ishara ya kutokumjua.
“Huyu ndiye anayetutesa, muuaji wa siri anayetumiwa na serikali kukamilisha hukumu yetu,” Mc Tee akamweleza Ivan. Colonel Ivan, akachukua kitu kama simu ya mkononi, akaipiga picha ile picha na kuiingiza katika mtandao wa siri wa utambuzi. Dakika tatu baadaye, kile kifaa kikatoa mlio.
Akakichukua na kutazama majibu gani yamekuja.
“Amata Ric, au Kamanda Amata. Agent wa siri asiyeonekana, code ya kijasusi 005…” Ivan akasoma kwa sauti yale yote yaliyoandikwa kwenye kidubwasha hicho. Akakitua na kushusha pumzi ndefu.
“Kuna lolote?” Mc Tee akauliza.
“Lazima auawe haraka iwezekanavyo. Kuna mambo mawili ya hatari kwa huyu kiumbe, na ndiyo maana nasema lazima auawe; ajenti wa siri na code 005,” akamweleza Mc Tee, “Hizo peke yake zinatosha kumfanya awe kiumbe hatari, kuliko hatari hyenyewe,” akamaliza kusema. Alipobonyeza kitufe fulani chini ya meza yake, Babier akaingia haraka. Ivan akampatia Babier kile kifaa.
“Erase him!'' akamwambia amfutilie mbali. Barbier akainamisha kichwa chake kama ishara ya kutii agizo hilo. Akaondoka na kuwaacha wawili wale wakiendelea na mazungumzo. Alipopotelea katika mlango mwingine, Ivan akamgeukia Mc Tee na kumwambia, “Kuna njia mbili tu za kumwondoa mtawala madarakani”. Mc Tee akamtazama na kumkazia sura.
“Ama kumwondoa kwa kura, au kwa chuma cha moto,” Ivan akamwambia Mc Tee. Wakaendelea kupata pombe kali kama walivyoanza kwa dakika kadhaa zilizofuata. Na baadae wakaagana wakiwa tayari wameweka sawa mikakati ya awali.



Dar Es Salaam Shamba

Madam S alikuwa tuli mbele ya meza yake kubwa. Ukimya wake ulivunjwa na mbisho wa hodi ya Kamanda Amata. Mara baada ya mlango kufunguka, alishusha pumzi ndefu na kumkaribisha kijana huyo kitini.
“Amata…” akaita.
“Yes Mom!”
“Kichwa changu kimevurugika kabisa na hili swala,” Madam S akamwambia Amata huku akijifikicha jicho kwa mkono wake wa kuume.
“Najua, ila nahisi tumekaribia ukingoni…” akasema Amata.
“Kwa nini wasema hivyo?”
“Dana ametupatia funguo nzuri ya kuanzia…” Amata akaeleza.
“Babier?” Madam akauliza.
“Ndiyo… na nimeshatuma taarifa na picha yake katika ubalozi wetu kule Moscow waanze uchunguzi kujua wapi anapatikana,” Amata akaeleza kwa urefu.
“Safi sana, ndiyo maana nakupenda we mtoto, huwa wakati mwingine unanitangulia katika kile ninachotaka kufanya au kusema,” Madam S akaeleza. Akajikohoza kidogo kusafisha koo kisha akarejesha utulivu wa awali.
“Mmemaliza na hao watu?” akamuuliza Amata.
“Ndiyo, kwa sasa hawana la kutuambia,”
“Ok, fanyeni mpango muwarudishe uraiani. Dana mumpeleke Muhimbili ICU aamkie huko. Hawa wengine warudisheni mnapopajua nyie,” akatoa maagizo.
“Timamu!” Amata akajibu.
“Jambo lingine… kama nilivyokudokeza awali, inabidi ufike Moscow. Fanya mbinu zote za kijasusi mpaka mwanamke huyu akupe siri ya anachokijua au mahusiano yake na hili genge,” Madam S akamwambia Amata kisha wakaagana.
* * *
Alfajiri ya siku iliyofuata ikawakuta Mariamu na Andrew wakiwa kitandani katika chumba cha mwanamke huyo kule Mburahati. Wa kwanza kuamka alikuwa Mariamu, akajishangaa. Akainuka na kukimbilia dirishani. Jua la asubuhi lilipendezesha nchi. Hakujua amerudije. Akarudi kitandani na kumwamsha Andrew. Naye alipoamka akajishangaa, akatazama dirishani, akatambua yupo Mburahati kwa mpenzi wake, Mariamu.
“Tumerudi vipi sweetie?” Mariamu akauliza.
“Hata mimi sifahamu, kila kitu kama muujiza!” akamjibu huku akivuta hatua kuelekea bafuni. Mariamu bado hakuamini. Alipovuta kumbukumbu, alijikuta akiishia tu kuvuta kitu kama hewa iliyochanganyika na moshi, akalala.
Dana alirudiwa na fahamu saa sita baadae na kujikuta kwenye chumba cha wagonjwa mahututi. Akapepesa macho huku na kule.
Muhimbili! Akawaza. Amefikafikaje, hajui. Alichokikumbuka yeye ni tukio lililofanyika kabla ya hapo. Dana alifumba macho yake na kuanza kuvuta kumbukumbu.
* * *
Wakati huo huo, Kamanda Amata alikuwa akijiweka tayari kwa safari ya Urusi. Begi lake na mkoba wa mkononi, tayari vilikuwa vikisubiri safari. Wakati yeye akihangaika kuchukua hiki na kile tayari kwa safari Gina alitingwa kwa kujitazama kwenye kioo. Aligeuka huku, akageukia huko, akavaa nguo hii, akavua, akachukua ile, ilimradi tu apendeze. Yote hayo yakifanyika, Amata alikuwa tayari keshakamilika.
“Gina!” akaita. Gina akageuka kama kashtuliwa, alishajisahau. “Tunaenda au unaendelea kuchagua nguo?” akamtupia swali.
“Tunaenda mpenzi!” akajibu huku akijiweka sawa gauni lake. Dakika ishirini baadae, wakaanza safari ya kuelekea uwanja wa ndege.
“Uende salama, urudi salama mpenzi!” Gina akamwambia Amata wakati akiiacha barabara ya Nyerere na kuingia ile ya kufika katika uwanja huo.
“Bila shaka! Cha msingi na kuniombea… maana kazi hii hapa ilipofika ni pagumu kuliko ilipotoka,” Amata akajibu. Gina akaegesha gari vizuri. Wote wawili wakateremka. Gina akamkumbatia Amata, akambusu huku chozi likimtoka.
“Rudi na roho yako!” akamwambia. Amata akajibu kwa kutikisa kichwa. Akachukua mkoba wake na kuuweka begani. Dakika tatu baadae akawa tayari ndani ya jengo la uwanja huo.

ITAENDELEA
 
GENGE
EP30

Rudi na roho yako!” akamwambia. Amata akajibu kwa kutikisa kichwa. Akachukua mkoba wake na kuuweka begani. Dakika tatu baadae akawa tayari ndani ya jengo la uwanja huo.


MOSCOW - URUSI

Alfajiri ya saa kumi na nusu, Kamanda Amata aliwasili katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Sheremetyevo - A.S. Pushkin na kupokelewa na swahiba wake Laabib Hussein.
“Karibu sana swahiba!” Laabib alimkaribisha Amata, wakapeana mikono.
“Shukrani… naona Moscow imekupenda, umetakata sana!” Amata akamtania, kisha wote wakacheka na kugonganisha viganja vyao. BMW 3 Saloon, iliwameza watu hawa na safari ya keulekea mjini ilianza. Iliwachukua dakika kumi na tano tu kufika katika ofisi za ubalozi wa Tanzania nchini Urusi, ndani ya jiji la Moscow, katika barabara ya Nikitskaya.
“Karibu nyumbani!” Laabib alimkaribisha mgeni wake, “Hapa hatukai Swahiba, tuna mazungumzo machache ya kikazi halafu utaamua kama unataka kutalii jiji la Moscow au unaendelea na safari,” akamweleza. Amata akaitikia kwa kutikisa kichwa. Baada ya kusalimiana na maofisa wachache wa ubalozi. Kamanda Amata na mwenyeji wake wakaingia katika chumba kimojawapo. Hakikuwa chumba kikubwa. Kilikuwa kidogo cha wastani, chenye meza moja na viti vinne. Zaidi ya hapo hakukuwa na kitu kingine chochote. Mara tu baada ya kuketi, Kamanda Amata akainua mkono wake na kuangalia muda. Akaishika pete ya saa hiyo na kuizungusha kidogo kisha akaiacha kwa sekunde kadhaa, ikifuatiwa na taa ndogondodo zilizokuwa zikiwaka.
Nipo salama! Akawaza. Muda huo huo mlang ukafunguliwa, Laabib akaingia na kuketi.
“Yes Kamanda Amata,” akasema na kuliweka kabrasha moja katikati yao. Amata akalivuta kwake na kulifungua. Kurasa ya kwanza tu akakutana na picha ya kuvutia ya msichana Barbier.
“Ndiye huyo! Sivyo?” Laabib akauliza.
“Swadakta! Ni yeye… nipe tafutishi zako!” Amata akamwambia Laabib.
“Kazi mlonipa nimeifanya kikamilifu na taarifa zote ndizo hizo… Barbier anapatikana sana kuliko mlivyofikiria. Hajifichi, hata ukitaka kufanya biashara naye, msichana huyu hana tabu. Ni mcheshi, anapendwa na watu na ni mwema sana!” Laabib akaeleza. Amata akatikisa kichwa kushoto kulia.
“Sikubaliani na wewe!” Amata akasema, “Barbier ni mwanamke anayeshiriki njama chafu za kuiangusha serikali ya Tanzania. Amehusishwa na genge hili haramu tangu akiwa na miaka kumi na saba mpaka sasa anakaribia uzee. Taarifa zetu zinamwonesha kama muuaji hatari aliyeshindikana!” akaeleza.
Laabib akashusha pumzi na kujiweka vyema kitini, “Barbier yupi unayemsema wewe?” akauliza. Amata akachomoa picha na kuiweka mezani. Laabib akaitazama, kisha akamtazama Amata. Laabib akaichukua ile ya kwenye kabrasha na kuziweka pamoja. Zinafanana kila kitu.
“Endelea…” Amata akamwambia Laabib.
“Kama ulivyosema. Babier amelelewa katika kituo cha watoto yatima huko Kirov kabla hachukuliwa na Afisa wa jeshi la Urusi aliyekuwa akikaa huko Saratov na kumlea kama binti yake,” akaeleza. Maneno haya yakaanza kumwingia Amata kwa namna fulani. “Katika chunguzi zangu nimeweza kupata mpaka wapi alisoma lakini kuna miaka mitatu au mine nimeshindwa kujua huyu Barbier alikuwa wapi…” akamaliza kusema.
“Sikiliza Laabib, niambie Barbier anapatikana wapi, nitajua mimi kama ni yeye au la…” Amata akasema.
“Sawa! Fika Saratov, mtafute Dimitri Gobenskiv, anapatikana katika casino la Faraon. Ukimpata yeye, habari zote atakupa… isitoshe ndiye aliyenipa habari hii yote. Beba na picha hii umpatie, atakutambua kirahisi zaidi!” Laabib akampatia ile picha Amata. Naye akatia kwenye mfuko wa koti. Dakika chache baadae wakaagana.
* * *

Dimitri Gobenskiv, kijana tajiri katika matajiri wa Saratov, kama kawaida yake, aliketi katika ofisi yake pana nay a kisasa ndani ya Casino Faraon. Hakuwa na makuu kama matajiri wengine wa jiji hilo. Alifikika ijapokuwa alikuwa na ulinzi mkali sana. Siku zote alikuwa na kilio kikubwa ndani yake baada ya wazazi wake wote wawili kuuawa kikatili kwa mkono wa mwanamke hatari, Barbier.
‘Ukijaribu kufanya lolote juu ya maisha yangu, nakuua!’ Ni ujumbe wa mwisho aliopewa na Barbier mara baada ya kugundua kuwa ndiye muuaji wa wazazi wake. Alitamani kulipa kisasi, lakini kila alipokumbuka onyo hilo, aligwaya. Kupitia luninga yake kubwa pale ofisini aliweza kuona kila eneo katika casino hiyo. Kila aliyeingia na kutoka, alimwona. Vijana waliokuwa wakimsaidia upande wa kuongoza kamera hizo waliijua kazi yao vyema. Taarifa zote zilimfikia kwa wakati kama kuna hatari au la. Hakupenda wageni hasiyowajua. Dimitri, alikuwa na wageni wake maalum. Wanawake wazuri wa gharama, matajiri kadhaa kutka nchi mbalimbali wanaopenda kuja hapo kibiashara au kucheza kamari.
Mlango wa ofisi yake ukafunguliwa, kijana shababi, mkakamavu, aliyevalia suti safi nyeupe, aliingia.
“Sir, kuna mgeni amefika anataka kuonana nawe!” akamwambia. Wakati huo, Dimitri alikuwa akimtazama mgeni huyo kupitia luninga ile. Hakuwa na ratiba ya kupokea mgeni yeyote kwa
siku hiyo. Akamtazama vizuri kupitia luninga. Kijana wa Kiafrika, aliyevalia suti safi nyeusi iliyotanguliwa na shati jeupe. Usoni mwake alipachika miwani ya kisasa sana, nyeusi, iliyomkaa vyema.
“Ana namba?” akamuuliza kijana wake.
“Hana, ila amesisitiza kama anaweza kukuona leo hii…” yule kijana akasema.
“Msafi?” akauliza akimaanisha kama hana silaha yoyote.
Kila mgeni aliyekuja kwa Dimitri alipaswa kuwa na namba ya miadi. Naye aliwapokea kwa wakati kadiri ya maelekezo ya namba hizo.
Waafrika! Atakuwa anataka msaada tu! Akawaza.
“Mpeleke chumba namba tatu, nitamkuta huko,” akamwambia. Yule kijana akatoka kwenye kile chumba na kumwacha Dimitri peke yake.
* * *
Kamanda Amata alifikishwa chumba namba tatu. Hakikuwa chumba kikubwa, ila kilikuwa cha gharama sana. Samani zake zilivutia macho, meza lkubwa ya kioo iliyotenganisha kochi la vono upande huu na ule, ilikuwa ya aina yake. Amata akaketi kwenye kochi mojawapo huku nyuma yake kukiwa na vijana wawili wakakamavu, wamesimama. Vijana hawa walikuwa wamefanana kwa sura, vichwa vyao vikiwa havina nywele, hawakucheka wala kuongea chochote. Dimitri akaingia akisindikizwa na yule kijana aliyempelekea taarifa kule ofisini.
“Karibu sana kijana!” akamkaribisha Amata kwa kumwita ‘kijana’ ilhali ukiwatazama, wamekaribiana umri. Pesa tatizo.
Amata hakujibu ile salamu badala yake akaondoa miwani usoni mwake na kuikunja, akaitia mfukoni.
“Tuna biashara ya kuzungumza!” Amata akaongea kwa kiingereza safi.
“Biashara? Unataka kuniletea wanawake kutoka Afrika ili niwauze humu? Au we ni mcheza kamari? Maana hata suti yako huvaliwa na gamblers, wacheza kamari…” Dimitri akaongea kiingereza kilichozungukwa na lafudhi ya Kirusia.
“Afrika hatuna dhambi kama zenu!” Amata akamjibu Dimitri huku akiwa kamkazia macho.
“Dhambi zipi?”
“Za kuwafanya dada zetu kuwa biashara kama ninyi mfanyavyo,” Amata akamjibu.
“Ha ha ha haaaaaaa!” Dimitri akacheka sana na yule kijana wake naye akaangua kicheko. Lakini Amata hakucheka hata kidogo. Alipoingiza mkono ndani ya koti lake, vijana wale wa nyuma yake wakachomoa bastola na tayari zilikuwa zikimlenga Amata. Akachomoa picha na kuiweka mezani.
“Hii ndiyo biashara ambayo nataka tuizungumze, na si upumbavu unaoongea!” Amata akamwambia. Dimitri akawapa ishara vijana wake, wakarudisha bastola kwenye makoti yao. Akaivuta ile picha na kuigeuza.
“Barbier Kermikov!” Dimitri akatamka jina la mwanamke yule wa pichani.
“Namhitaji, nimeambiwa ni wewe tu unayeweza kunambia ni vipi na wapi naweza kumpata…” Amata akamwambia. Dimitri akakunja sura yake na kuikunjua tena.
“Hii picha umeipata wapi?” akamuuliza.
“Uliyempa, ndiye aliyenipa kwa kuwa ni mimi nilimtuma kwako…” Amata akaongea.
“Huwezi kumfikia kirahisi, huyu ni mwanamke hatari sana… analindwa na watu hatari vilevile. Anajua mtu gani wa hatari na mwema. Ni muuaji aliyepitiliza…” Dimitri akasema huku chozi likimdondoka, “Yeyote atakayeweza kumuua mwanamke huyu, nitampa pesa nyingi sana… naaihitaji damu yake,” akamaliziakusema.
“Nimetumwa kwake…” Amata akamwambia Dimitri.
“Wewe ni nani?” Dimitri akamuuliza Amata.
“Mr. Spark!” akajitaja kwa utambulisho bandia kama kawaida yake.
“Mr. Spark, Barbier ni mwanamke kahaba… si ngumu kumpata. Lakini nenda kama mteja wa kawaida unayetaka kufanya naye ngono… japo hapendi watu weusi, tumia ujanja wako. Ni mwanamke mwenye siri nyingi sana, na zote zipo kifuani mwake kazining’iniza kwa mkufu wa dhahabu na kuzifificha kwa jiwe la emerald,” Dimitri akaeleza. Amata alikuwa kimya akisikiliza kila hatua ya maneno ya mwenyeji wake.
“Huwezi kumuua, Spark!” Dimitri akasema.
“Sitaki kumuua… naihitaji information moja tu kutoka kwake,” Amata akasema.
“Nimeshakwambia siri zake anaweka wapi, nina uhakika hata information hiyo itakuwa humo humo. Kifua chake, hubaki wazi awapo kitandani tu… ukiipata hazina hiyo, niletee na mimi kuna kitu nakihitaji pia. Nilishatuma watu watatu na wote wameuawa hakuna aliyerudi… na sasa ananitafuta mimi aniue!” Dimitri akasema na kusimama, “Subiri hapa!” akamwambia Amata na kukiacha kile chumba.
Dakika tano baadae, yule kijana aliyekuwa na Dimitri akarudi na kikasha kidogo mkononi mwake, akamkabidhi Amata.
“Dimitri anakutakia kazi njema sana… anasema kama ukifanikiwa muonane kabla hujarudi kwenu,” yule kijana akasema na kumkabidhi kike kikasha.
“Asante!” Amata akachukua miwani yake na kuivaa, akakipokea kile kikasha na kukikamata vizuri mkononi mwake. Akatoka huku akiongozwa na wale jamaa wawili mpaka mlango mkuu wa jumba lile la starehe.
“Take Care!” jamaa mmoja kati ya wale wawili akasema. Amata akampa ishaya ya dole gumba kwamba anaafiki asemacho. Moja kwa moja akaliendea BMW alilokuja nalo na kuingia ndani yake. Akaketi nyuma ya usukani, na jambo la kwanza, akafungua kile kikasha. Macho yake yakapokelewa na bulungutu la noti, dola za Kimarekani. Chini kabisa ya kikasha hicho akakutana na kadi iliyoandikwa kwa kalamu nyekundu.
Park-Hotel, Vineshvaya Gora
2nd Aptechnyi proezd 11,
410009 Saratov, Russia
Chini ya anwani hiyo kukawekwa maelezo mafupi tu ya kumpa tahadhari. Akakisoma na kisha anwani ile akaiingiza katika kifaa chake kinachoweza kutambua uelekeo wa mahali uendako kwa msaada wa satelaiti. Akatia ufunguo na kuwasha gari. Injini ikakubali. Akalitoa kwenye maegesho na kuingia barabarani taratibu.
* * *

ITAENDELEA
 
GENGE
EP31

Chini ya anwani hiyo kukawekwa maelezo mafupi tu ya kumpa tahadhari. Akakisoma na kisha anwani ile akaiingiza katika kifaa chake kinachoweza kutambua uelekeo wa mahali uendako kwa msaada wa satelaiti. Akatia ufunguo na kuwasha gari. Injini ikakubali. Akalitoa kwenye maegesho na kuingia barabarani taratibu.
* * *
Barbier Kelmikov akatikisa kichwa juu chini na kumtazama dereva wake.
“Vipi?” yule dereva akauliza.
“Apelekwe chaka nakuja kumshughulikia,” Barbier akamwambia yule dereva. Wakati wote ambao Kamanda Amata alikuwa katika casino lile, Barbier alikwishapata taarifa ya ujio wa mtu huyo hatari. Kwake ikawa rahisi kuimaliza kazi kama alivyoamuriwa na mzee wake, Colonel Ivan. Kama ingebidi asafiri kwenda Tanzania basi anayemfuata alijipeleka mwenyewe.
* * *
Kamanda Amata mara tu baada ya kusoma ujumbe na kuweka tayari ramani yake ya safari, alilitoa gari maegeshoni na kuondoka taratibu kuwelekea katikati ya jiji la Saratov. Akiwa tayari kalivuka geti la casino hiyo na kuingia barabara kuu, macho yake yalikuwa kwenye taa kuongozea magari zilizo mbele yake. Hakuwa na wasiwasi, akili yake yote ilikuwa ni kumtia mkononi Barbier na kuweza kujua nini kipo katika sakata hilo. Honi kali na nzito zikamfikia masikioni, alipogeuka kutazama kulia aliliona lori kubwa aina ya Liaz likiwa umbali mdogo kutoka pale alipo yeye. Akajitahi kuepa kwa kukunja kona kushoto, lakini hakufanikiwa kwani lile lori lililigonga gari la Amata sehemu ya nyuma ubavuni. Likaizungusha na kulitazamisha lilikotoka. Matairi ya nyuma ya lori lile yakalikanyaga boneti na kuliharibu vibaya likiacha vyoo vikivunjikavunjika na kutuka huki na huko. Kamanda Amata aliyatazama yote hayo kama mkanda wa filamu.
Sekunde chache tu, gari la polisi likawasili pamoja na lile la kubeba wagonjwa. Haraka sana, wahudumu wa gari lile wakateremka na machela, na kumtoa Amata ambaye alikuwa tayari keshapoteza fahamu. Dakika moja baadae lile gari likaondoka eneo lile. Kutoka katika chumba cha dereva cha gari lile la wagonjwa, Barbier alisogeza kioo cha kumuwezesha kuona katika chumba cha mgonjwa.
“Vipi?” akawauliza vijana wake waliojifanya wahudumu wa afya kumbe la. Kamanda Amata alikuwa tayari mikononi mwa Barbier.
“Amezimia tu, na ana majeraha madogo madogo!” akajibiwa huku gari lile likichanja mbuga kuelekea nje ya jiji la Saratov.


Kumysnaya Polyana

Katika msitu huu mkiubwa ambao watu hupenda kwenda kwa mapumziko na harakati
nyingine, lile gari la wagonjwa likaingia. Baada ya kufuata ujia mrefu unaotosha gari moja tu wakafika mahali penye kizuizi. Mlinzi wa eneo hili alikuwa mzee sana kadiri ya miaka sitini au sabini.
“Safari ya wapi?” akamuuliza Barbier ambaye alikuwa ameketi upande wake.
“Shimoni!” Barbier akajibu. Yule mzee kabla ya kufungu lile geti la mbao, akauendea ufagio wa wima ulioegemezwa katika ukuta wa kibanda chakavu langoni hapo. Akauchukua na kuugeuza, akazungusha pale kwenye kiungo cha mpini na ufagio wenyewe. Kwa ndani hapo palikuwa na simu ya upepo iliyofichwa kiufundi sana. Akaongea maneno machache tu na mara lile geti likafunguka lenyewe. Lile gari likapita na kuendelea na safari.
Haikuwa nyumba kubwa, bali ndogo ya kizamani, iliyochoka kiasi kwamba haikuwa na uhai ndani yake. Lile gari likasimama nje yake, Barbie akateremka na kufuatiwa na yule dereva. Wale vijana wa nyuma nao wakateremka. Amata bado alikuwa kimya kitandani.
Barbier alisimama kimya mikono yake ikiwa kiunoni. Sura yake ya kiutu uzima kwenda uzeeni ilionesha dharau ya paka. Si yule aliyekuwa akijidai na Mazda jekundu nyakati zile za miaka ya themanini, si yule aliyekuwa na sura ya kuvutia ya binti mbichi yenye kuvutia marijali. Huyu alikuwa Barbier mwingine kabisa, mtu mzima, mwenye macho yaliyojaa ukatili wa miongo kadhaa. Akamtazama Amata pale alipolala.
“Mshusheni, mpelekeni shimoni haraka,” akaamuru. Wale vijana wakamshusha Amata na kumbeba akiwa hana fahamu. Wakaingia nae ndani ya ile nyumba chakavu, nyuma yao wakifuatiwa na Barbier. Katika sebule ya nyumba hiyo, kukafunguliwa kitu kama mfuniko wa tanki la maji machafu. Baada ya kufungua mfuniko huo wakateremka chini ambako ghala kubwa liliwakaribisha. Amata akabwagwa chini kama mzigo. Ndoo ya maji baridi ikafuatia juu yake. Akashtuka kutoka katika mzimio huo, akatikisa kichwa na kujaribu kujiinua.
“Waoh! Vizuri sana, umeamka ee?” Barbier akasema huku akimzunguka Amata na alipofika upande wa kichwani , akasimama na kujishika kiuno. Amata akainua uso wake na kumtazama mwanamke huyo. Macho yake yakatua kifuani mwa mwanamke huyo. Kidani cha gharama kilikuwa kikining’inia kifuani mwake. Barbier akayatazama macho ya Amata, kisha akajitazama kifuani.
“Ni mwanamke mwenye siri nyingi sana, na zote zipo kifuani mwake kazining’iniza kwa mkufu wa dhahabu na kuzifificha kwa jiwe la emerald,”
Wakati akiwaza hayo akajikuta ghafla akipokea teke zito lililtua usoni na kumwangusha upande wa pili. Amata akainua mkono na kujifuta damu zilizokuwa zikitoka puani mwake. Barbier akaachia sonyo kali.
“Na utafia ndani ya ghala hili shetani mweusi we!” akasema. Amata hakujibu kitu akabaki kimya.
“Mfundisheni adabu,” akawaambia. Wale vijana wakamwinua Amata na kuanza kumsulubu. Vipigo vizito viliufikia mwili wake. Dakika saba zilimwacha nyang’anyang’a akiwa hana hali.
“Good! Mfungeni kwenye kiti cha ufalme…” Barbier akawaamuru wale vijana, wakamtutusa kutoka pale chini na kumkalisha kwenye kiti. Mikono yake ikafungwa kwa vifungo vya chuma, miguu yake pia na kifungo kingine kikafungwa kuzunguka shingo yake. “Utakaa hapa na kifo chako kitakukuta humu ndani,” Barbier akamwambia na kuwapa vijana wale ishara ya wote kutoka mle ndani. Mara baada ya wote kutoka, ule mlango ukafungwa na giza likatawala chumba kile chote. Kamanda Amata akafumbua macho vizuri, hakuweza kugeuza shingo yake kutokana na kifungo kile kilichowekwa shingoni mwake. Kila alipojaribu kujitikisa, vile vifungo vilimbana na kumpa maumivu makali. Alijaribu kutumia macho yake tu kwa kuyapepesa kwa nyuzi aziwezazo. Mwanga mdogo na mwembamba sana ukapita kati ya macho yake kutoka upande wa kushoto. Akili yake ikasoma haraka sana.
Camera! Akawaza. Kisha akatulia. Hakuwa na cha kufanya kwani alikuwa amefungwa barabara. Hana ujanja. Alitulia kimya akisubiri mwisho wake.
Upande wa juu, nje ya ile nyumba, katikati ya msitu wa Kumysnaya Polyana, Barbier na vijana wake walikuwa wakizungumza jambo. Dakika mbili baadae, kukasimama gari la kisasa, BMW. Ndani yake akatoka mwanaume aliyekula chumvi nyingi, Mzungu, aliyechakaa kichwa chake kwa mvi lukuki. Barbier akamsalimu kwa kumpa mkono. Mzee huyo akapokea salamu hiyo pasi na kusema neno. Fimbo yake ya kutembelea alikuwa ameining’iniza kwenye mkono wake, upande wa nyuma ya kiwiko. Barbier akampa ishara yule mzee ya kuwa ‘amfuate’, akafanya hivyo. Wakateremka shimoni, alikohifadhiwa mateka wao.
Dakika tano baadae, Colonel Ivan Chernyakhovsky, alisimama imara mbele ya Kamanda Amata. Kanali wa jeshi la Kirusi aliyeasi na kuanzisha shughuli zake za siri. Kuwekeza katika tawala nyonge zilizojawa tamaa huko Afrika. Kamanda Amata, akamtazama mwanaume huyo, mzee, mwenye macho makali. Kinywani pake alikuwa na cigar ya gharama sana. Akaibana kwa vidole vyake viwili, akaiondoa katika midomo yake na kuining’iniza vidoleni.
“Finally, hatujatumia nguvu kukutafuta! Umekuja mwenyewe kwenye himaya ya mtu mwenye mikono michafu” Ivan akamwambia Amata huku akitembea huku na kule. Amata hakuweza kugeuza sura yake kumtaza kila upande aliyokuwa akienda. Macho yake yalibaki kutazama mbele tu lakini poopoo zake ziliweza kuzunguka kadiri ziwezavyo. Muda wote huo Barbier alikuwa kasimama kando ya chumba mahali ambapo palikuwa na swichi kubwa ya taa na vibonyezo vingine.
“Nani aliyekudanganya kuja huku? Nani kakutuma?” Ivan akamuuliza Amata. Ukimya ukatawala. Barbier akabonyeza moja ya zile swichi. Vile vifungo vikaanza kukaza kwa nguvu. Kile cha shingoni kikawa kinamkaba zaidi na kuliminya koromeo taratibu. Kamanda alimwagikwa na jasho, akakosa pumzi, akahangaika kuitafuta, akaanza kukoroma huku vidole vyake vya mikono vikiwa vimechanua kutafua msaada.
“Aaaa hah hah hah hahaaa hakuna kitu kizuri kama kumuona biDanamu akikata roho!” Ivan akasema baada ya kutoa cheko lake la kifedhuli. Cheko lile lilimtia hasira Amata lakini hakuweza kufanya lolote. Barbier akaminya swichi nyingine, kile kifungo cha shingoni kikalegea kabisa. Amata akakohoa mfululizo. Nuru iliyoanza kumpotea ikarejea taratibu. Akakohoa na kutema damu iliyochafua shati lake. Akabaki akihema kwa nguvu huku macho yake dhaifu yakimtazama mzee yule katili. Sura yake ikawa inakuja na kutoka katika kumbukumbu za Amata lakini hakujua ni wapi amewahi kumuona.
Sebastiano Moznich! Akamkumbuka. Huyu ndiye key point yetu! Akakumbuka nini walizungumza shamba walipoiona sura hii katika tafutishi zao.
“Amata Ric, mnajifanya mnaweza kuzuia mapinduzi! Nani kawaambia? Na sasa ndugu zako watashuhudia nchi ile inageuka. Vijana wangu wataiangusha kwa mtutu wa bunduki wakati wewe tayari ukiwa nyama ya udongo!” Ivan akasema kwa sauti yake kavu. Akiwa katika kusema yote hayo, Amata alibaki kimya kabisa bila kujibu.
Ivan akainua ile fimbo yake na kuibonyeza kwa juu. Katika ile ncha ya fimbo kikajitokeza kitu kama kisu chembamba. Akamchoma nacho pajani.
“Aaaagh!” Amata akatoa ukelele.
“Hah! Kumbe una sauti?” Ivan akauliza huku akitabasamu, “Haya nambie nani kakutuma kwangu?” akamsindikiza na swali huku akimchomachoma na kile kisu mapajani huku na huko. Kamanda Amata aliuma meno kwa maumivu.
“Mmmnnnnnhhhhh!” akagugumia kwa maumivu, “Aaaaaaghhh Sebastianoooooo!” akapiga kelele na kulitaja lile jina. Ivan akaacha kile alichokuwa akifanya na kukodoa macho, akimtazama Amata. Barbier akatoka pale kwenye ile swichi na kusogea karibun na mzee huyo.
“Umesema nani kakutuma?” Ivan akauliza.
“Sebbbastiano Moznich!” Amata akataja jina lile kwa urefu. Moyo wa Ivan ukabadili kasi ya mapigo. Akili yake ikahama, akamtazama Barbier kifuani, macho yake yakakutana na ule mkufu wa dhahabu.
“Unamjua? Kanipa ujumbe wako!” Amata akamuuliza Ivan kwa kuwa sasa aliona wazi kuwa mzee yule kachanganyikiwa. Sebastiano Moznich lilikuwa ni jina lake la bandia lililoficha mambo mengi sana nyuma yake. Mzee huyu aliyefungua duka kubwa sana la kuuza magari ya Ferarri huko Toscana, Italia.
“Lock him well!!” akamwamuru Barbier amfunge sawasawa. Ivan akatoka kwenye kile chumba na kuelekea katika sebule ndogo upande mwingine. Baada ya kurudisha kile kifungo cha shingoni, Barbier akatoka na kumfuata Ivan. Ivana akageuka na kumtazama mwanamke huyo aiyemlea tangu akiwa na miaka kumi na saba.
“Nataka huyu jamaa afe, sihitaji kuju chochote kutoka kwake, na ile program yetu iharakishwe ili kusudi mipango isiharibike,” Ivan akatoa maelekezo huku mwili wake ukitetemeka. Alielewa kuwa siri yake kubwa imefichwa katika jina hilo la Sebastiano Moznich. Yeyote anayejua jina hilo basi anakuwa ameingia kwenye kiini cha mipango na mikakati yake.
“Na vipi kuhusu mjinga Dimitri?” Barbier akamuuliza Ivan.
“Kill him,” Ivan akajibu bila kusita. Barbier akaondoka zake. Giza lilikwishauvamia mzitu huo, wakati vijana wa Barbier walipokuwa njiani kwenda kumkusanya Dimitri.

SIKU SABA BAADAE

Mc TEE, Big J na Madam Jesca walikutana tena kwa kikao katika kisiwa kilekile. Wenyewe walikiita ‘kikao cha mafanikio’. Kama ilivyo ada, kilikuwa kikao cha siri na cha watu watatu tu huku wakiunganishwa na mfadhili wao Colonel Ivan kwa njia ya mtandao.
“Bwana Ivan amekasirishwa sana na uendeshaji wetu wa mapinduzi, aDanai tumechelewesha mambo ndiyo maana sasa tumeanza kugundulika…” Mc Tee akawaeleza wenzake.
“Analolisema ni kweli… lakini sisi kilichotutawala ni huruma kwa ndugu zetu. Tungemwaga damu, tungeua dada zetu, kaka zetu, shemeji zetu, shangazi na wajomba. Uamuzi wetu wa wakutumia nguvu kipndi kile cha ujana wetu ilikuwa sahihi lakini kwa sasa imekuwa ngumu,” Big J akasema huku sura yake ikionekana wazi kusawajika kwa mawazo lukuki.
“Sasa inabidi tutumie nguvu tu kuiondoa serikali hii madarakani. Tufumbe macho, cha muhimu ni kuwalinda wale wa damu yetu…”
“Nani anakukumbuka wakati wewe umeshakufa?” Jesca akamuuliza Mc Tee. Mzee huyo mtu mzima, mwanausalama wa jeshi aliyehasi, akatabasamu akimwangalia mwanamke huyo.
“Ni kweli usemayo, lakini hata Yesu alipofufuka aliwatambua ndugu zake japo wao wakati mwingine hawakumtambua,” Mc Tee akamjibu Jesca.
“Jesca!” Big J akaita, “Kama kaututambua wangefanya hivyo sasa, lakini wamefeli wakati tumesimama katika miguu yao…” akamwambia.
“Ok, sasa katika mwezi huu, tutegemee mzigo silaha nzito utakaoingia kwa siri, tayari kwa kazi…” Mc Tee akawaambia na taarifa hiyo ikamgutusha kila mmoja. “Jesca, inabidi uende Dar es salaam, nitakupa barua yenye kifungo maalum ukwapatie watu nitakaokuelekeza,” Mc Tee akatoa maelekezo kwa mwanaharakati huyo wa kike. Bi Jesca alijizolea umaarufu sana miongoni mwa Watanzania kwa harakati zake za kuiponda na kuikosoa serikali. Alipoanza kutafutwa akafanikiwa kutoroshwa na Vincent Mwanachia.
“Lazima ubadilike kidoko!” Big J akamwambaia Jesca, “Utatoka hapa utaenda India, pale utafanyiwa mambo yote kisha utaingia Dar’ kama utakavyoelekezwa. Hautatakiwa kufanya lolote kwa maamuzi yako isipokuwa yetu. Ukikiuka hilo, utakamatwa kirahisi, wanausalama wa Tanzania ni wakali sana siku hizi, wananusa kuliko mbwa,” akamwambia.
Wakiwa katika mazungumzo hayo, simu ya mezani ikaita. Simu hii iliyounganishwa na satelaiti iliweza kuwaunganisha hapo Camp Site na Saratov bila kuingiliana na kampuni yoyote ya mtandao. Mc Tee akawasha luninga ndani ya chumba hicho na kuifyatua ile simu. Katika luninga ile, akaonekana mzee wa makamo, nywele nyeupe, fimbo ya kutembelea mkononi mwake. Nyuma yake, mitya kama mbili hivi alisimama mwanamke mwenye umri kidogo, midomo yake myekundu ilimfanya aonekane kama mtu wa kuchora.
“Comrades! Nina habari nzuri sana kwenu na kwetu pia!” Upande wa pili , Ivan alizungumza. Mc Tee na jopo lake wakakaa tayari kusikiliza. “Tunaye huyu bwana hapa!” akageuka nyuma na kutoa ishara. Akaletwa mbele ya camera, mwanaume, mwafrika, akiwa tumbo wazi, damu ilionekana dhahiri shahiri mwilini mwake. Uchovu aliyokuwa nao ulionesha wazi kuwa mwanaume huyo alipigwa na kuteswa haswa.
“Anaitwa Kamanda Amata kutoka TSA huko Tanzania, huyu ndiye mwaribifu wa mipango yetu siku zote. Ndiye aliyepokea kijiti kutoka kwa mshenzi Dastan. Tumemkamata, na leo hii mtakishuhudis kifo chake kupitia luninga hii…” Ivan akaongea kwa uchungu huku akitetemeka kwa hasira. Mc Tee na wenzake walibaki kimya kabisa wakimtazama mtu yule ambaye hata sura haikuonekana sawasawa.
“Nataka mjue kwamba, huyu bwana kufika hapa ina maana kuwa amekwishajua siri nyingi sana za genge hili. Huyu ndiye aliyeiangusha Brussels, huyu ndiye aliyeiangusha Lisbon, na bado alikuwa katyika mikakati ya kuigusa ngome kuu. Ninyi mlikuwa mnamchekea tu wakati mnamjua fika! Nimemtia mkononi na hapa ni kifo tu,” Ivan akasema kwa Kiingereza chake kilichotawaliwa na lafudhi ya Kirusia. Mc Tee, Big J na Jesca hawakuamini nini wanachokiona. Mtu aliyekuwa akiwaumiza kichwa na kuwanyima usingizi alikuwa mikononi mwa jitu katili, Ivan, na mwanmke muuaji, Barbier. Ilikuwa kama ndoto.
“Hakuna jinsi tunasubiri kushuhudia kifo chake!” akasema Mc Tee.

* * *

OFISI NDOGO

Ilikuwa siku ya tatu tangu Kamanda Amata atoweke, Madam S alipopata nukushi ya kujulishwa habari hiyo mbaya. Nukushi hiyo iliingia asubuhi kabisa ambapo ofisi hiyo ilikuwa ndiyo kwanza inafunguliwa. Madam S baada ya kuisoma alijikuta akikaa kitini huku akiwa haamini.
Nini kimetokea? Akajiuliza. Baada ya kutumia dakika kumi za kutafakari, uamuzi ukafika akilini mwake. Akainua simu yake na kubofya namba kadhaa. Baada ya kuongea maneno machache akakata na kutulia akisubiri. Dakika kumi baadae Chiba na Gina walikuwa tayari ndani ya ofisi hiyo. Ukimya ulitawala kwa maana kila mmoja alijua nini maana ya simu ile. Kazi nyeti, kazi nzito.
“TSA!” akatamka.
“For my people. For my nation!” wakaitikia pamoja.
“Kamanda Amata amepotea. Na nyote mnajua ugumu wa mchezo huu… hatutakiwi
kujiuliza wala nini. Gina na Chiba haraka sana mkamate ndege mchana au jioni ya leo, mtapokelewa Moscow na Laabib. Mambo mengine yote tayari huyo bwana keshapanga… na ubalozi utawakirimia yatayobakia,” Madam S akawaambia huku macho yake yakiwa wazi yametona machozi. Alimwamini sana Amata lakini mara nyingi ilikuwa endapo inatokea kuwa katika mikono ya watesi, raha humuondoka. Akajifikicha macho na kuirudisha miwani yake usoni.
“Madam!” Chiba akaita, “Unatukutanisha na ubalozi tena? Umesahau yaliyotokea Lisbon?” akauliza.
“Nakumbuka, lakini nchi ile ipo makini sana na mambo ya usalama na kijasusi. Mkiingia viabaya mnaweza kujikuta pabaya. Lakini kuna mambo ya kidiplomasia ambayo lazima yafanyike, hivyo Laabib ambaye ndiye aliyempokea Amata , atawapokea na ninyi. Mkiona mauzauza basi akili vichwani mwenu,” Madam akawaambia.

Siku iliyofuata

Jioni ya siku iliyofuata iliwakuta Chiba na Gina ndani ya jiji la Moscow. Ndani ya moja ya ofisi za siri katika viunga vya jiji hilo, Laabib aliwakaribisha watu wake.
“Unataka kunambia Spark katoweka au katekwa?” Chiba aliuliza mara tu baada ya salamu na mazungumzo machache.
“Nilichokigundua ni gari lake lilipata ajali, na askari katika eneo lile wanasema alichukuliwa na gari la wagonjwa. Unajua huku kwa wenzetu, magariya wagonjwa yanafanana isipokuwa kuna namba maalumu ambayo hutofautisha kuwa hili ni la wapi na lile ni la wapi…”
“…Enhe, hilo lilikuwa na namba za wapi?” Gina akadakiza swali kwa shauku.
“Lile halikuwa na namba ubavuni, na tumefatilia kwenye camera za barabarani tumeliona likielekea nje ya mji wa Saratov ambako kumejawa misitu tu…”
“…ametekwa, lazima tukafunge kazi,” Chiba akawaambia.
“Kama ametekwa, basi yuko mikononi mwa Barbier…” Laabib akasema.
“Barbier!” Chiba na Gina wakatamka kwa pamoja.


Msitu wa Kumysnaya Polyana

Barbier, mwanamke katili, alisimama mbele ya Amata aliyekuwa amefungwa barabara. Macho yake makali yalikuwa makini kumtazama kijana huyo. Kamanda Amata alikuwa kimya, ingawaje aliteswa kwa kipigo kikali lakini alibaki hivyo pasi na kujibu swali lolote aliloulizwa.
“Endelea kuwa bubu hivyo hivyo… umeshatelekezwa, na humu hutoki. Aliyekuelekeza amekuingiza kuzimu kwenye shimo la mauti, si kwamba alikusaidia. Dimitri ni mshirika wetu na tumemuweka pale makusudi kabisa,” akamwambia Amata huku akitembeatembea ndani ya chumba kile kichafu na cha kuogofya. Kuta zake zilichafuka kwa damu ya biDanamu, sakafu nayo iliganda damu ya muda mrefu. Harufu nzito iliyotokana na damu hiyo ilikijaza chumba hicho. Ndani ya chumba hicho kulikuwa na makolokolo mengi na kukifanya kionekane kana ghala. Amata aliyavumilia yote. Kukaa ndani ya chumba hicho kwa siku saba haikuwa rahisi.
“Leo ndiyo mwisho wako… na huyo mjinga mwenzio Dimitri anakuja hapa kuungana nawe maana anajifanya anajua sana,” Barbier akasema. Sekunde chache baadae, Amata akasikia kelele za mtu anayelia kwa uchungu huku akitukana matusi yote ya Kirusia. Sauti ile haikuwa ngeni sana kwake. Hisia zake hazikukosea. Mita chache mbele yake, Dimitri aliangushwa vibaya na kupigiza uso chini.
“Shiiit!” Amata akatamka kwa sauti ya kichovu. Vijana wa miraba mine, watatu wakafuatia nyuma yake. Wakamwinua Dimitri na kuanza kumsulubu kwa makonde mazito mazito yaliyotua tumboni na kifuani. Dimitri alitapika damu nyingi sana, macho yake yalimtazama Amata kuomba msaada lakini minyororo iliymfunga mikononi na miguuni ilimkatisha tamaa.
“Stop!” Barbier akawaamuru. Wale vijana wakamwacha Dimitri. Akaanguka chini na kulala kimya. Barbier akachutama na kumgeuza kwa kumshika ukosi wa shati lake. Dimitri alikuwa kimya kabisa. Akampapasa kwa mkono wake maeneo ya shingoni, kisha akamtazama Amata, “Bado ana uhai kidogo unaoweza kumfikisha masaa matatu yajayo, hah hah hah…” akatoa cheko lake la kifedhuli. Sekunde chache zilizfuata, akanyamaza na kubadilika sura.
“…saa ya hukumu,” akasema na kutoa tabasamu baya na la kuchukiza. Kamanda Amata alihisi kakutana na shetani. Sura ya mwanamke huyu ilimfanya kusadiki kuwa watu-majini wapo duniani.
Nitakuua vibaya wewe mwanamke shetani! Amata akawaza kwa hasira. Chuki ndani ya moyo wake ikajijenga na kufanya donge kubwa la gadhabu liuzunguke moyo wake. Amata alipogeuza sura kuwatazama wale vijana waliokuwa wakimsulubu Dimitri, akapata ganzi kidogo. Hakuyaamini macho yake yaliyovimba kwa kipigo na kufumbwa kwa damu iliyoganda huku akiachiwa eneo dogo la kuweza kuona. Kati ya wale vijana alikuwapo mmoja ambaye sura yake haikuwa ngeni kabisa. Akajaribu kuvuta kumbukumbu ya wapi amemuona kijana huyo ambaye daima alikuwa akikwepesha kukutana macho na Amata.
Take care! Sauti hii ikamrudia tena. Akamkumbuka, ni yeye aliyemtamkia neno hili pale katika Casino la Pharaon. Mmoja wa walinzi wa Dimitri katika casino lile. Akamtambua bila kificho.
Alijua nini kitanipata, alijua kila kitu. Dimitri ameuzwa na watu wake, ama kweli kikulacho ki ng… Hakumaliza hata kuwaza huko, akashtushwa na taa kali zilizommulika usoni.
“Tungeweza kukuua muda mrefu sana, lakini tulikuacha ili ipatikane saa maalum ambayo wapendwa wako watashuhudia kifo chako kwa njia ya mtandao,” ilikuwa ile sauti kavu ya mzee Ivan, Colonel muasi wa jeshi la Urusi. Sauti yake ilitangulia kabla ya yeye kufika. Barbier akamwendea mzee huyo na kumvua koti la ngozi alilokuwa amelivaa. Moyo wa Amata ukaanza kudunda mfululizo bila mpangilio, kifo kilikuwa dhairi shahiri mbele yake. Minyororo yenye nguvu ilimdhibiti asiweze kufanya lolote. Mbele yake kukasogezwa kitu kama beseni kubwa la kioo ambalo mwaDanamu mwenye urefu wa futi sita angeweza kusimama wima ndani yake. Beseni hilo lilikuwa juu ya kifaa maalumu chenye magurudumu na lilisogezwa pale kwa kuongozwa na mitambo maalumu. Ndani ya beseni lile kulikuwa na kimiminika ambacho Amata alikitazana na kutokuelewa ni cha aina gani. Kijana mwingine, akatega camera ili kuchukua matukio yote. Kompyuta iliyokuwa juu ya meza ndogo ilionesha kuwa matukio yale yanatazamwa mubashara sehemu fulani. Ivan akakusanya mikono yake kifuani na kumtazama Amata.
“Hii ni kemikali itakayotumika kukuteketeza na hutoonekana duniani isipokuwa nguo zako tu ulizoziacha Tanzania. Kwa mkono wa Ivan utateketezwa mwili na roho… kisha ndugu zako watashuhudia mapinduzi yenye umwagaji damu mkubwa katika nchi yako,” akamwambia. Ivan akachukua pande la nyama kutoka katika chano iliyokuwa imeshikwa na kijana mwingine. Akalitumbukiza ndani ya lile beseni. Pande lile la nyama likateketea taratibu na kupotea kabisa. Na kemikali ile ikanbaki safi kama mwanzo. Ni kitendo cha dakika mbili tu jambo lilifanyika.
“Mwili wako utateketea namna hii baada ya ule wa Dimitri,” Ivan akamwambia Amata. Akasogea pembeni na kumpisha Barbier. Mwanamke huyu akatoa amri Dimitri atumbukizwe kwenye ile kemikali.
Ni kemikali hii ilitumika kumteketeza Dastan na mkewe? Amata akajiuliza huku akihema kwa nguvu. Bila kificho, alijua wazi kuwa mwisho wa maisha yake umefika.

ITAENDELEA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom