Riwaya: Code x 3

Madame S

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2015
Posts
17,190
Reaction score
34,526
RIWAYA: CODE X 3:
THE REAL ME 1
MTUNZI: Tariq Haji

SEHEMU YA 1

"Niko wapi, niko mbinguni au" aliongea Alex baada kufumbua macho kutoka katka usingizi wa kifo, "tulia kijana, utafikaje mbinguni wakati hujafa" aliongea mzee mmoja wa makamo huku akitabasamu na kumuekea Alex mkono begani "uko mahali salama kabisa" aliendelea kuongea mzee huyo. Alex alijaribu kuzivuta kumbukumbu zake za mara ya mwisho. Na ndipo akakumbuka kuwa alipigwa risasi na Agent Darling, akaanza kuwaza ikiwa risasi ile hajapigwa yeye , je aliepigwa ni nani?. Swali hilo lilizuka ghafla kichwani mwake, "isije ikawa wamemuuwa hawa". "Alex karibu tena duniani" aliingia mwanamke mmoja aliekuwa amevaa kinyago nusu katika uso wake. "unanikumbuka" aliobgea mwanamke na kukaa pembeni kwenye kiti. "hapana sikukumbuki" alijibu Alex huku akijaribu kukaa, "hahaha kweli Alex umenisahau?" aliuliza tena huku akicheka. "subiri hiyo sauti kama naijua" Alex aliongea huku akivuta kumbkumbu zake vizuri ghafla akaruka "Scarlet ni wewe au". "kumbe bado kichwa chako kipo vizuri" alijibu Scarlet, "wema haupotei" aliendelea kuongea mwanamke huyo mwenye tabasamu lenye kumuweka simba kichaa chini. Alionekana kuwa mchangamfu kupita maelezo lakini kwa mtu ambe na uwezo wa kusoma sura vizuri basi angegundua kuwa uchamgamfu wake pamoja na tabsamu vilikuwa ni danganya toto tu. Mtu pekee alielielewa hilo ni General Griffin, ambae ni baba mlezi wa Scarlet. "Hebu nambie nimeokokaje" aliongea Alex, "usijali nitakwambia kila" alijibu Scarlet na kumuangalia Alex.

"Ni hivi, nilisikia kinachoendelea kupitia vyanzo vyangu vya habari na uchunguzi. Taarifa nilizipata wakati natoka Mexico katika kazi maalum niliyopewa na serekali, ndipo nikaskia kuwa kua mtu anaitwa Alex na ni muuaji mkubwa sana. Nikaanza kufatilia na ndipo nikagundua kuwa Alex mwenyewe ni wewe, na pia nilianza kufatilia kwanini ulikuwa unatekeleza mauji hayo. Sasa siku moja nilifika katika ofisi za kitengo maalum cha upelelezi kama mwandishi wa habari. Wakati nashuka gari niliona vikosi vingi sana vya kuimarisha ulinzi wakati nataka kudadisi ghafla nilipitwa na gari ndogo nyeusi ikielekea upande waliopo wanajeshi na ilipofka ikaripuka. Kwa mbali nikauona ukianza kugawa dozi, bila kuchelewa nilipiga simu makao makuu waniletee chopa niondoke. ilichukua muda kufika, wakati naondoka sasa ndipo nikakuona juu ya jengo ukiwa umepiga magoti na mbele alikuwepo mwanamke aliekuwa ameshikilia bastola. Nilichukua sniper na kabla hajakupiga wewe nikamuwahi yeye, sijui hata nilimpiga wapi maana sikulenga kwa makini. Baada hapo nilikuchukua na kukuleta huku" Alimaliza kuongea Scarlet na kumuangalia Alex ambae macho yalikuwa yamemtoka kam mjusi aliebanwa na Mlango.

*******************************

"mkuu, Christina amemka" aliigia mwanamke mmoja aliejiulikana kwa jina la Martina, jeff aliinuka alipokaa na kuelekea chumba alichokuwa amelazwa Christina. "vipi hali yako" Swali a kwanza kuuliza alipofika ndani ya chumba hicho, "Jeff nimefikaje hapa?" aliuliza Christina. "tulia utajua kila kitu lakini kwanza unajiskiaje" Jeff alimtuliza na kumuuliza tena swali la kwanza. "vizuri kiasi na maumivu kwa mbali katika bega la mkono wa kushoto" alijibu Christina huku akijiangalia mkono ambao ulikuwa umefungwa bendeg. "usijali unahitaji siku chache tu, mkono utapona kabisa" alijibu Jeff huku akimshika mkono, "nilikukuta juu ya gorofa ukiwa unavuja damu huku ukiwa umepoteza fahamu,ndipo nikakuchukua na kukuleta huku katika kambi maalum, na wala usijali hakuna mtu anaejua kama uko hai ama umekufa" aliongea Jeff huku akimuangalia kwa makini, kwa vipi atazipokea taarifa hizo. "na kwanini wasijue kama niko hai ama nimekufa" aliuliza kwa mshangao, "nilikuwa nategemea swali hilo kutoka kwako" alijibu Jeff na kuinuka, alisogea mpaka ukutani na kubonyeza pahali. Ukuta ulifunguka na kulikuwa na TV, "naomba usikilize mwenyewe kabla sijakueleza chochote" aliongea Jeff na kuwasha Tv hiyo kubwa kisha akarudi alipokuwa amekaa wali na kukaa.

"mpendwa mwanangu Christina" iliskika sauti ya Allen James, "wakati utakapoupokea ujumbe huu uenda nikawa sipo tena duniani, nakuomba sikiliza kwa makini na uwatabue marafiki zako na maadui zako usije ukatumika kama nilivyotumika mimi" baada hapo sauti ya Allen ilikata na kuanza kusikika sauti nyingine "ndio baada Allen James kukamilisha kazi inabidi na yey afe, si mnaelwa kuwa kazi hii ni siri ya hali ya juu na hatakiwi mtu mwengien asiehusika afahamu, na kama Allen atashidwa kumuua Alex basi itabidi sisi tumuue yeye halafu kesi hii tunambambikizia Alex. Akirudi Christina na kufahamu kuwa babaake ameuwawa na Alex, nina uhakika hatopumzika mpaka atakapohakikisha Aex amekufa na baada ya hapo na yeye pia tunamuua ili kupoteza ushahidi kabisa. Mapinduzi hayawezi kuzuilika, na mtu na mwanae wote watatumika kama mbwa wa kuwindia"baada ya sauti hiyo kukata ilirudi tena sauti ya Allen "natumai utakuwa umefahamu nani mbaya wako na nani rafiki yako, atakae kuletea ujumbe ni Alex na ni mmoja kati ya watu ambao watakuwa msaada mkubwa kwako katika kukamilisha kazi ntakayokupa kama babaako. Nataka uwasambaratishe kama vumbi wale wote wanaotaka kuitndea nchi yetu mabaya, na kunitenda mimi babaako. Ni matumaini yangu kwamba utafanikisha zoezi hili kwa hali na mali, kama ikibidi ufe ili likamilike basi fanya hivo. Nakupenda sana mwanangu...mimi babaako Allen James" hapo ndio ulikuwa mwisho wa rikodi hiyo na katika kioo cha TV hio kutaoke maandishi mekundu yaliosemeka "THE END IS THE BEGINNING".

Christina alijikuta machozi yakimtoka bila mategemeo na kujisemea kwa sauti ya kinyonge "kwanini hukunipa mapema taarifa hii Alex", "Christina punguza jazba" aliongea Jeff. "najaribu ila nshindwa, kwakweli mtu niliokuwa nataka kumuua ndie mtu aliekuwa bega kwa bega na babangu katika mapambano, unafikiri ningemuua ningeenda kuiweka sura yangu siku ambayo ningekutana na babaangu" alianza kujilaumu sasa. "lakini jambo zuri ni kwamba hujamuua" aliongea Jeff akijaribu kumpa moyo. "una uhakika gani, mi sidhani kama atakuwa amepona baada majeraha yale niliompa" alizidi kujilaumu huku moyoni akijiapiza kulipiza kisasi hata kama itabidi damu yake imwagike. Jeff baada kusikia hivo, ikabidi anyamaze kwanza na kisha akainuka na kutoka na kutoka nje huku akimuacha Christina akiendelea kulia. "mbona umemuacha peke yake" aliuliza Talbot, "ndio inavotakiwa, kwa sasa anajaribu kukabiliana na uhalisia kwamba aliekuwa anamuwinda sie aliemuaa baba ake. Na tujiandae kwa mechi ngumu mbele kwasababu lazima atahitaji msaada wetu kukamilisha kazi yake" Jeff alijibu na kuelekea chumbani kwake kwa ajili ya kupumzika.

Christina aliendelea kulia huku akiwa mwekundu kwa hasira ambayo ilianza kukikitesa kichwa chake, mara kadhaa alipiga kelele na kuangusa vitu chini. Lakini hakuna mtu alieingia katika chumba chake, "hahaha....Christina wewe ni mjinga sana tena mjinga wa mwisho, hukuona muda wote kama Alex alikuwa kiajribu kukufikishia ujumbe". "hahaha... lakini amefanya uzembe mwenyewe kwa kutokupa ujumbe mapema", "General David mpumbavu mkubwa wee, utalipa huu unyama kwa damu yako mjinga mkubwa wewe. Ulidhani mimi ni babaangu, umekosea sana kucheza na baba angu kwani umesaini mkataba wa kifo na mimi...hahaha mshenzi wee". Alikuwa akiongea mwenyewe na kujijibu huku akicheka na baadhi ya wakati alikuwa analia, alionekana kama mtu aliechanganyikiwa tena si kidogo maana chumba kizima alikichafua chafua, alikuwa mevunja kila kitu kilichokuwemo katika chumba hicho kuanzia vitu viukubwa mpaka vidogo vidogo. "THE END IS THE BEGINNING....NDIO KWANZA SAFARI IMEANZA" alisema kwa nguvu huku machozi yakimtoka. "furahia siku zako za mwisho na kila anaehusika na wewe,nitauwa kuanzia sisimizi na kila kitu ambacho kimo katika himaya yako na yoyote atakaekaa mbele yangu na yeye pia atakufa...General David" alijisemea na kusimama kwenye kiti alichokuwa amekaa baada ya kushuka kitandani.
CODE X 3: THE REAL ME 2

***************************

"nimekwambia nenda nyumbani ukanyonye. leo ni siku mbya sana" Alex aliikumbuka sentensi aliomwambia Allen Jr kabla ya kumpa kichapo cha fisi mwizi. "natumai kwa sasa utakuwa ushaujua ukweli" alijisemea huku akijisifu kwa kufikisha ujumbe wa mwalimu wake Allen. Siku ile baada ya kumpiga mpaka kumzimisha, alitoa ile recorder alioambiwa kuwa ni kwa ajili ya Christina na kumtilia katika mfuko wa suruali yake kisha yeye akaondoka na kuendelea na pambano lake. "hivi kwanini hukuniacha nife tu maana tayari nilishapanga kwena kukutana na familia yangu mzima" Alex alimuuliza Scarlet aliekuwa pembeni bize akicheza game ya kivita. "unadhani kila mtu ambae anapata mikosi angetaka kufa, unadhani kungekuwa nawatu amabao wangekuwa tayari kupigania haki ya mtu" Scarlet alijibu na kuacha kucheza game, alionekana kukerwa na swali hilo la Alex. " ni bora ushukuru ulikuwa sehemu ambayo ulikuwa na marafiki na walikuwa wakikujali japo mlikuwa kambini" Scarlet aliongea huku akikaa mbele ya Alex na kumuangalia usoni. "mimi nimeishi maisha ya manyanyaso sana tokea nilipozaliwa" Scarlet aliendelea kuongea huku akionekana wazi kuumizwa na anachokiongea. "hebu nielezee maisha yako" Alex aliomba na kukaa mkao wa kula kusuburi binti huo aanze kumporomoshea mkasa wa maisha yake.

********************

Scarlet alianza kuelezea hadithi ya maisha yake "Jina langu halisi sio Scarlet kama wanavolifahamu wengi, ila jina langu ni Ariella Mark. Ni mtoto wa pekee katika familia yangu, na babaangu alinipa jina hilo kwa sababu mama angu alijifungua katika wakati mgumu sana wa maisha yao. Japo hali ilikuwa duni lakini niliweza kukuwa vizuri tu bila kusumbuliwa na magonjwa kama wengi walivyodhani. Ukweli wazazi wangu walinipenda sana, tena sana kupita maelezo. Nilipata kila kitu nilicholikitaka, taratibu maisha yalianza kunyooka na kuwa mazuri huku kubadilika huko kwa maisha kukiwachukiza ndugu wa karibu wa wazazi wangu. Nikiwa na miaka minne tulihama tulipokuwa tunakaa na kuhamia mjini kabisa ambako baba alikuwa amejenga nyumba mpya na ya kisasa kwa wakti huo. Nilianza shule japo nilikuwa nimechelewa lakini wazazi wangu hawakumsikliza mtu, nilianza shule ya awali na baada ya miaka mitatu niliingia darasa la kwanza. Wakati huo nilikuwa na miaka saba lakini kutokana na mwili wangu kuwa mdogo sana hakuna alieamini kuwa nina miaka hiyo. Lakini nashukuru Mungu kwa kunipa wazazi wenye hekima na busara kama wale, lakini kama tunavojua kuwa duniani tunapita hakuna kiumbe kitakachoishi milele. Basi hivyo ndivyo ilivokuwa kwa babaangu ambae nikiwa na kumi alpoteza ajali katika ajali ya ndege nikabaki na mama yangu tu.
 
RIWAYA: CODE X 3:
THE REAL ME 1
MTUNZI: Tariq Haji

SEHEMU YA 2

Nikiwa na miaka minne tulihama tulipokuwa tunakaa na kuhamia mjini kabisa ambako baba alikuwa amejenga nyumba mpya na ya kisasa kwa wakti huo. Nilianza shule japo nilikuwa nimechelewa lakini wazazi wangu hawakumsikliza mtu, nilianza shule ya awali na baada ya miaka mitatu niliingia darasa la kwanza. Wakati huo nilikuwa na miaka saba lakini kutokana na mwili wangu kuwa mdogo sana hakuna alieamini kuwa nina miaka hiyo. Lakini nashukuru Mungu kwa kunipa wazazi wenye hekima na busara kama wale, lakini kama tunavojua kuwa duniani tunapita hakuna kiumbe kitakachoishi milele. Basi hivyo ndivyo ilivokuwa kwa babaangu ambae nikiwa na kumi alpoteza ajali katika ajali ya ndege nikabaki na mama yangu tu.
Maisha yalizidi kusonga mbele huku ndugu zake baba wakizidi kuleta vita juu ya mali alioacha baba, na taratibu walianza kutupora. Na walipoona mama ameleta ubishi sana wa kuzikabodhi mali, Baba mkubwa alituma vijana wakaja kuchoma nyumba yetu moto. Moto huo ulianzishwa usiku wa manane, na ulitanda kwa kasi ya ajabu. Nilikuja kushtuka baada kuhisi maumivu makali usoni na kugundua kuwa chumba changu kina moshi mwingi sana. Na haukupita muda mama alifika chumbani na kunibeba huku nikilia kwa nguvu. Kwakweli siwezi kuyasahau maumivu nilioyapata usiku ule, na kwa sababu moti ulikuwa umeshaienea sana ilikuwa hakuna jinsi ya kutoka ndani ya nyumba hiyo. Mama alichokifanya alinitia kwenye friza, nikiwa humo ndani nilihisi friza hilo likisogea kwa nguvu huku nikisikia kelele za mama kutoka na maumivu anayoyapata baada moto huo kuanza kumuunguza. Aliendelea kulisukuma friza hilo lakini ghafla nilihisi kama likianguka na kweli kwasababu lilipiga chini kwa nguvu na kunifanya niumie. Baada hapo nilisikia mlipuko mkubwa sana, kutokana na baridi kuwa kali katika friza hilo nilipoteza fahamu. Nilikuja kushtuka niko hospitali, na swali la kwanza lilikuwa ni kumuulizia mamaangu lakini majibu niliokutana nayo yalikuwa ni ya kutisha sana. Huwezi amini ndani ya miezi minne baada kifo cha babaangu, nilimpoteza mamaangu tena kwa kifo cha mateso. Na taarifa nyingine mbaya ambao niliipokea baada kuamka ni kuwa upande wa kushoto wa uso wangu wote ulikuwa umeungua, na kutokana na umri wangu kuwa mdogo sana ilikuwa ni vigumu kufanyiwa plastic surgery. Nilikaa kwa sikukadha hospitali bila hata ndugu yangu mmoja kuja kunitembelea.
Baada wiki kupita huku kukiwa hakuna dalili ya mtu yoyote anaenifahamu kuja kuniona, daktari mkuu wa hospitali hiyo alichukuwa uamuazi wa kunipeleka katika kituo cha kulelea watoto yatima. Na kwasababu alikuwa hanijui jina na mimi sikutaka kumwambia mtu jina kutokana na kutonesha kidonda kibichi kwa sababu kila nnapolitaja jina hilo nawakumbuka wazazi na kuanza kumlaumu Mungu kwa kunitenda. Sasa sikutaka kumkosoa na kuingilia majukumu ya muumba wangu na hivyo ndivyo nilivyofundisha na wazazi wangu kuwa kila linalotokea basi limepangwa na Mungu litokee. Basi aliniandikisha kwa jina la Scarlette. Maisha mapya yalianza baada tu daktari huyo kuondoka, yule mama nilomkuta katika zamu siku niliofika alikuwa na roho nzuri. na alinieleza kuwa nijiandae kwa maisha magumu sana kutokana na tabia za watoto waliekuwepo katika kituo hicho na baadhi ya wasimamizi. Alinipelaka mpaka katiak chumba ambacho ndio nilitakiwa kulala na kunikabidhi kwa kiongozi wa chumba hicho. Yule msichana alikuwa anaitwa Harleen, alikua ni binti mwenye asili ya kihindi aliyechanganyika na muingereza. Yeye pia alikuwa na roho nzuri na alikuwa mchangamfu, alinipeleka mpaka kwenye kitanda ambacho kilikuwa pembeni ya kitanda chake. Alinikabdihi shuka kadhaa pamoja na nguo za kubadilisha, kwakweli nilimshkuru sana. Siku hiyo ilipita huku usiku kucha nikiwa macho bila kupata hata lepe la usingizi na usiku mzima nilikuwa nikilia huku nikijaumu kwa nini sikufa pamoja na mama ili tukaenda kuonana na baba tukiwa pamoja na kuungana tena kwa mara ya pili kama familia nzima. Hapo awali maisha katika kituo hicho yalikuwa magumu kutokana na kuwa mgen wa mazingira hayo, pia waschna wengine walinitenga kutokana na kovu langu usoni. Walinipa majina tofauti tofauti, wapo walioniita laana wakimaanisha kuwa nimelaaniwa. Kuna wengine waliniita jini, wengine waliniita mdudu. Yote kwa yote kila mtu aliniita alivojisikia, kwa kweli nilikuwa najiskia vibaya sana hasa nnapo kumbukua uzuri wangu ulioteketezwa na moto na kuuzika pamoja na jina langu.
Lakini kadiri siku zilivyokwenda nilizoea hali hiyo, baada wiki moja katika kituo hicho. Nilipelekwa shule kwa ajili ya kujiendeleza kimasomo. Nilifurahi sana na wakati huo huo nilikuwa na hofu, kwasababu ya sura yangu ambayo ilikuwa nyeusi upande mmoja na nyeupe uoande mwengine. Siku ya kwanza shuleni watu wengi walinicheka hasa wanaume, hakuna hata mwanafunzi mmoja aliekuwa akiniongelesha darasani. Wote walinitenga na wengine walikimbia mbio waliponiona, kuna baadhi waliziba pua wakati napita. Hali hizo zilinitesa sana lakini ningefanyaje na yote ni mipango ya muumba. Mwaka uliisha na hatimae tukafanya mitihani ya kuingia darasa la nne, nilipasi vizuri tu lakini sikuwa na furaha kabisa kwa sababu hakuna mtu alionekana kuthamini matokeo yangu. Baada likizo kuisha tulirudi shule kwa ajili ya mwaka mpaya wa masomo, niliamua kufanya mabadiliko kwa kuzichukulia changa moto zote zilizonikuta mwaka uliopita kama sehemu yangu ya maisha ya kila siku. Hivyo basi niliondoa wasiwasi kabisa na kuyavaa maisha yangu kwa sura ya kipekee, nilifanya hivo baada kugundua maana ya jina langu halisi kuwa ni SIMBA JIKE LA MIUNGU YA KIGIRIKI.

Niliamua kuwapuuzia wote wanaonikejeli na kuendelea na maisha yangu mweyewe mimi kama mimi bila kuendeshwa na woga uliokithiri. Hali hiyo ilipelekea hata hali yangu ya kimwili kutengemaa kutokana na kudhoofika na mawazo ya mwanzo kuhusu watu wanavonichukulia. "atakae nikimbia na akimbie, atakaeziba pua na azibe nnapo pita, mimi ni mimi na siwezi kubadilika hata kama ntacukia.....
THIS IS THE REAL ME"

Hiyo ndio ilikuwa kauli mbiu yangu.
Basi jitihada zangu zote nilizielekeza kwenye masomo sasa, sikujali tena waliokuwa wakinikera. Japo nikuwa mzito kidogo darasani sikuwa tayari kukubali kufeli, hivyo niliongeza bidii mara dufu katika masomo. Siku moja nikiwa peke yangu nikipata chakula wakati wa mapumziko, nilisikia mtu akiniita. Nilipogeuka nikakutana na kijana mmoja mzuri sana, "samahani wewe ndio Scarlet" aliniuliza. Nikamjibu ndio, wakati huo upande ambao nilikuwa nimeungua na moto ulikuwa umefunikwa kwa nywele. Alitabasamu kidogo kisha akajitambulisha "mimi naitwa Adrian", pia alinambia kuwa yeye ni mwanafunzi mgeni pale shuleni hivyo wakati anaulizia sehemu akaelekezwa aje kwangu. Maskini hakujua kama aliambiwa aje pale ili anicheke kutokana na kovu langu kubwa usoni. "kwangu hukuambiwa uje nikuelekeze, umeambiwa uje kuniangalia usoni, nina kovu kubwa la moto" nilimwambia huku nikimkazia macho lakini cha kushangaza alikuwa kaitabasamu tu kisha akanijibu "unajua kuwa na kasoro si jambo la kujitenga na wengine, we huoni kama Mungu amekupendelea kukufanya hivo. Huoni kama kuna mantiki ya wewe kuwa hivyo labda ungekuwa kama wengine huwezi jua mangapi yangekuwa yamekufika mpaka sasa. Mimi naelewa ni kiasi gani upweke unanyonya na kumiza, muda wowote ukitaka mtu wa kuongea nae usisite kunitafuta rafiki yangu Scarlet" maneno alioongea yalikuwa na busara kubwa ndani yake hasa ukizingatia umri wake na darasa. Adrian ndio mwanaume wa kwanza kujenga nae urafiki, na kila wakati tuliokuwa tunaonana, nilikuwa nasahau kabisa karaha zangu.
Alikuwa mcheshi na muelwa, alifahamu wakati nilokuwa niko sawa na wakati ambao niliko sawa. Na alikuwepo nyakati zote nilizomuhitaji, ukaribu wangu kwake uliendelea kukuwa kadri siku zilivyokuwa zinasonga mbele. Tulimaliza elimu ya msingi na kuanz elimu ya sekondary na kwa bahati nzuri tulipata shule moja hivyo urafiki wetu uliendelea. Wakati tunaingia sekondary mimi nilikuwa na miaka kumi na sita na Adrian alikuwa na miaka kumi na saba, hapo nilianza kuhisi kitu tofauti kwangu lakini nilikipotezea. Urafiki wetu waliwakera sana wanawake wanaotaka sifa kutoka na wanaume tofauti hasa wa kitajiri kama Adrian. Nilianza kupokea vitisho kuwa niache kujipendekeza kwa Adrian. Ukweli maneno hayo yaliniumiza sana na kuamua kumuita Adrian na kumueleza lakini kabla sijamaliza kuongea Adrian alinivuta karibu na kunikumbatia kisha akanambia "mimi na wewe tumetoka mbali sana, hakuna mtu anaekujua vizuri zaidi yangu. Wewe ni rafiki wangu wa damu, wa kufa na kuzikana na wala yasikutishe maneno ya wajinga wewe wa puuze tu" maneno yake yalinipa faraja kubwa sana, ukiunganishe na mkubatio ndio kabisa. Basi maisha yaliendelea hivo hivo huku wenye wivu wakizidi kuumia, siku moja uongozi wa shule ukatangaza sherehe ndogo ya msimu wa joto. Ilikuwa ni sherehe ya kucheza maarufu kama "dancing ball", nikiwa sina hili wala lile Adrian alinifuata na kuniomba niwe mweza wake katika usiku wa sherehe. Nilikataa kwa kisngizio cha kutokujua kucheza lakini akanambia hilo si tatizo na kwa sababu kulikuwa na wiki nzima kabla ya sherehe basi angenufundisha kucheza. Nilijaribu kutoa sababu nyingi ili mradi tu nisiende kwenye sherehe lakini alinizidi ujanja na mwisho nikakubali, basi kunzia siku hiyo tulikuwa tunakutana sehemu na akawa ananifundisha kucheza mchezo aina ya blues. Nilishangaa kuona kwa jinsi nilivyokuwa mwepesi katika mchezi huo wakati darasani nilikuwa mzito sana kupita maelezo kuelewa. Siku moja kabla ya sherehe alikuja na box la wastani na kunikabidhi kisha akanambia natakiwa kilichokuwa humo wakati wa sherehe. Sikulifunua hapo tuliendelea kufanya mazoezi mpaka tukamaliza na kuondoka tukikubaliana nimsubiri nje ya kituo nnacho kaa siku ya pili kwa ajili ya kwenda huko kwenye hiyo sherehe. Nilirudi nyumbani na kukaa kitandani kisha nikalifungua box, macho yalinitoka kama mjusi aliebanwa na mlango baada kukuta gauni kubwa lenye rangi ya dhahabu, lilikuwa zuri kupita kiasi. Pia nilikuta kinyago cha dhahabu kikiwa kiana ujumbe juu "kama unaona aibu kutokana na sura yako, vaa hichi". Nilitabasamu kidogo na kulifunga box hilo kisha nikaliweka pembeni ya kitanda changu.

ITAENDELEA.
 
RIWAYA: CODE X 3:
THE REAL ME 1
MTUNZI: Tariq Haji

SEHEMU YA 3

Sikulifunua hapo tuliendelea kufanya mazoezi mpaka tukamaliza na kuondoka tukikubaliana nimsubiri nje ya kituo nnacho kaa siku ya pili kwa ajili ya kwenda huko kwenye hiyo sherehe. Nilirudi nyumbani na kukaa kitandani kisha nikalifungua box, macho yalinitoka kama mjusi aliebanwa na mlango baada kukuta gauni kubwa lenye rangi ya dhahabu, lilikuwa zuri kupita kiasi. Pia nilikuta kinyago cha dhahabu kikiwa kiana ujumbe juu "kama unaona aibu kutokana na sura yako, vaa hichi". Nilitabasamu kidogo na kulifunga box hilo kisha nikaliweka pembeni ya kitanda changu.
Siku ya pili jioni nilianza maandalizi na kwa msaada wa Harleen nilimaliza mapema, nilipotoka ndani kila mtu alitoa macho huku wakionesha kutoamini wanachokiona mbele yao. Kila mtu aliongea neno lake, yote kwa yote walinisifu kwa kuniambia "umependeza kama sio wewe vile rangi mbili usoni". Tulicheka wote kutokana na kuwa nilishazoea kuitwa majina kama hayo, na huo ulikuwa ni utani tu. Nilitoka mpaka nje ya kituo na wala sikukaa sana, nilishangaa kuona garo aina Rolls Royce nyeusi ikisamama mbele yangu. Mlango ulifunguka na Adrian akashuka, alikuja upande wa pili na kunifungulia mlango. Wakati naingia kwenye gari alininong'neza "umependeza sana", sikuwa na cha kusema zaidi ya kujichekesha tu kama mjinga. Safari ilianza huku kila mmoja akiwa kimya mpaka sehemu ya sherehe, baada ya kushuka nilimsikia akiongea na dereva wakem "Simon unaweza kwenda kujirusha au sio, nikikuhitaji nitakushtua", "sawa mkuu" yule dereva alijibu kwa furaha na kuondoka. Adrian alikuja nilipokuwa nimesimama na kunishika mkono kisha tukaanza kutembea kuingia ndani ya ukumbi, kila tuliepishana nae hakuacha kutushangaa na kutusifu. Kutokana na kinyang'o usoni hakuna alienitambua. Kinyang'o hicho kilikuwa kimeifunika sehemu yangu nlioungua yote, kiufupi kiliugawa uso wangu katika nusu mbili. Baada kuingia humo ndani nilishangaa kuona tunaelekea upande wa V.I.P, nilisita lakini Adrian aliminya kidogo. Tulifika kwenye meza moja iliopambwa vizuri sana na juu ilikuwa ilikuwa imeandikwa "THE GOLD PARTNERS" (marafiki wa dhahabu). Sherehe ilifunguliwa rasmi na ratiba ikawa inaendelea vizuri, Adrian aliniomba tukacheze na mimi nikakubali. Siku hiyo ilikuwa ni miongoni mwa siku nilizokuwa na furaha katika maisha yangu na pia ni miongoni mwa siku nilizopata huzuni kubwa pia. Tuliendelea kucheza kwa kuburudika na baada ya muda kidogo kukatangazwa mashindano ya kucheza wawili wawili. Adrian aliinua mkono na kunionyesha ishara na mimi niinue. Baada ya kupatikana washindani wa kutosha, mashindano yalianza na kuendelea mpaka mwisho. Mshindi alitangazwa kuwa ni "THE GOLD PARTNERS", ambao ni mimi na Adrian. Tulikabidhiwa tuzo na kurudi katika meza yetu kwa ajili ya kupata chakula.
Wakti tunaendelea kula nilianza kuhisi harufu flani hivi ambayo nilishwahi kuihis huko nyuma, moyo ulianza kwenda mbio huku kinyasho chembamba kikinitoka. Adrian alinishika mkono baada kugundua hilo, nilimuangalia na kumwambia kuwa nahisi harufu ya kitu kuungua. Na kweli kabla hata hajanijibu ghfla moto mkubwa ulirupuka na kila akaanza kukimbia upande wake. ukweli mimi na moto ni vitu viwili tafauti kabisha, nguvu ziliniishia na taswira ya uso wangu kuungua ikaanza kunirudia. "Scarlet tuondoke" nilisikia kwa mbali Adrian akinambia lakini hata hivo nilishindwa kinua hata kidole nikamjibu "wewe nenda tu mimi siwezi hata kuinuka hapa". Moto ulizidi kuwa mkali huku mimi na Adrian tukizidi kubishana juu ya swala zima la kuondoka. Adrian alipoona nmekuwa mbishi alininyanyua kwa nguvu na kunibeba kisha akaanza kukimbia, kwa muonekano wake sikutegemea kama angekuwa na nguvu kiasi kile.

Alifika mlangoni na kukuta moto umeshatanda, bila kusita alielekea uoande wenye dirisha na kulivunja kisha akanisukuma nje na yeye akafuata. Alipotua tu alitoa simu yake na kupiga "baba naomba helicopter yangu sasa hivi ije huku kwenye sherehe kuna mgonjwa amezidiwa" nilimsikia akiogea maneni hayo kwa masikio yangu, nilianza kuona kiza kinatanda machoni mwangu, na kabla sijafunga macho nilivua cheni yangu yenye kopa la dogo na kumkabidhi mkononi. Hakuijali aliitia mfukoni mwake na kwa mbali nikaanza kusikia mlio wa helicopter ila kabla haijafika nilipoteza fahamu kabisa. Sikujua nini kiliendelea, mawazo yagu ya mwisho kabla ya kufunga macho nilidhani kuwa ndio siku yangu yamwisho duniani.
Nilikuja kushtuka, na kitu cha kwanza macho alikutana na mwangaza mkali sana na baada kuangaza kulia na kshoyo nikagundua niko hospitali. Nilijivuta vuta ili nikae lakini nesi aliniwahi na kunirudisha kitandani na kunambia sijaruhusiwa kukaa. Baada ya dakika kumi alikuja daktari na kuchukua vipimo kisha akatoka na baada ya nusu saa alirudi tena na kuchukua kiti kisha akakaa pembeni na kuanza kuniuliza maswali. Mengi yalikuwa ni kunijaribu kama kumbukumbu zangu ziko sawa, na baada kurdhika na majibu alioyapata alinikabidhi bahasha nyekundu. Niliifungua ndani na kukuta kuna barua, niliitoa na kuanza kuisoma. "najivunia kuwa na rafiki kama wewe, umenitoa upweke ambao ulikuwa umejizika ndani ya moyo wangu. Kitu ambacho sikuwahi kukwambia ni kwamba mimi nilikuwa mpweke kama wewe baada ya kumpoteza mama yangu mzazi pamoja na pacha wangu wa kike Adriana na kaka zangu wengine wawili na dada mmoja. Lakini baada ya kukutana na wewe upweke huo wote ulinitoka na kujikuta nikiwa huru kabisa, nakushukuru kwa hilo. Pia asante kwa zawadi yako nzuri ulionipa lakini nasikitika kuwa kwa sasa hatutaweza kuonana tena mimi na wewe mpaka pale Mungu atakapo tukutanisha tena kwa mara ya pili lakini kaa ukijua nakupenda sana. Nilipanga nikwambie siku ile ya sherehe na niliweka pete ya uchumba katika chupa yenye kinywaji lakini mambo yakaenda bila kutegemea. Nakuahidi kuwa nitakuhifadhia penzi lako ikibidi hata nizikwe nalo lakini nitakutafuta kwa ajili ukurasa mpya wa maisha yetu. NAKUPENDA SANA ARIELLA......WAKO ADRIAN" barua ilishia hapo na bila kutegemea nikajikuta nanyong'ojea na macho yangu yalishindwa kuhimili hali hio na kuanza kutoa machozi. Nililia kwa muda mrefu lakini jibu nililolipata ni kuwa yote ilikuwa ni mipango ya Mungu na kama amepanga mimi na Adrian tuoanane tena basi hakuna atakaeweza kuzia na kama amepanga vingine basi hakuna atakaeweza kubadilisha.
Baada ya baada ya siku mbili niliruhusiwa na kurudi nyumbani, daktari alinipa dawa fulani hivi ya kuondoa kovu japo alinambia kuwa kovo hilo haliwezi kuondoka lote kutokana na kuwa limekwenda ndani sana ya sura yangu. Hivyo dawa ingesaidia kuondoa ule uvimbe na kuirudisha sura yangu kuwa laini huku ikiacha alama ya weusi wa kimtindo. Nilirudi katika kituo nlichokuwa nakaa na kuanza maisha upya huku nikiwa nimepata funzo kuwa "ukijiona uko mpweke basi jua kuna ambae ni mpweke zaidi kuliko wewe" maisha yaliendelea na baada ya mwaka mmoja alikuja mzee mmoja na mkewe kwa lengo la kutaka mtoto wa kulea. Hivyo tuliitwa wote na kuelezwa kuwa mmoja kati yetu amgepata bahati ya kupata wazazi siku hiyo, hivyo tusiache nafasi hiyo ipite bila kutoka. Baada ya nusu saa alianza kuingia mmoja katika chumba maalum ambcho walikuwepo wanafamilia hiyo. Zamu yangu ilifika na kuingia, nilisalimia kwanza kisha nikakaa kwenye kiti. Yule mzee aliniangalia kisha akatabasamu na kunambia kuwa alikuwa na maswali machache anataka kuniuliza. Nilitikisa kichwa kuashiria nimemuelewa, "unaitwa nani" ndio swali la kwanza kuniuliza. "jina langu ni Scarlette Mark Anderson" nilimjibu jina kamili. "hivi una ndoto ya kuwa nani na kwanini" likuwa swali lake la pili na la mwisho, "nataka kuwa mtu ambae ataitumikia jamii bila kujali rika wala kabila kwa sababu furaha yangu ni kuona watu wakiwa na furaha" nilijibu huku nikimuangalia usoni. Yule mzee alitabasamu na kumuangalia mkewe, yule mama alinigeukia na kuniuliza "usoni umefanya nini". Nilimueleza kila kitu na swali jingine aliloniuliza lilikuwa "hujisikii vibaya au aibu kutembea na njiani na sura kama hiyo". Kwa upande fulani nilihisi kama amenidhalilisha lakini sikutaka kuonesha wazi. "hapana sijiskii aibu kabisa tena nahisi faraja kutembea kama nilivo bila kuificha sura kwa sababu hivi ndivyo nilivo na hata kama nitiaficha siwezi kubadilika....THIS IS THE REAL ME" hivyo ndivyo nilivojibu na kumwanagalia mama yule usoni kwa mbali nikamuona akitabasamu na kumgeukia mumewe kisha akatingiha kichwa. Baada ya hapo waliniruhusu nitoke ili waendelee kuongea na wengine. Baada ya muda kidogo kupita wote tulikuwa vyumbani mwetu. Aliingia msimamizi wetu na kuniita, aliongoza njia na mimi nikafata nyuma mpaka katika chumba kingine. Huku nilimkuta yule mzee na mkewe wakiwa wanaongea, walipotuon waligeuka na kuniangalia huku wakitabasamu. "hongera Scarlette umepata wazazi wa kukulea sasa" aliongea yule msimamizi wetu. Nilifurahi sana japo sikuonesha wazi kiasi nimefurahi, basi taratibu zote zilifuatwa ikiwemo kubadilishwa jina la baba na kuitwa Scarlette G. Jackson ambalo ni jina la mzee huyo.
Niliwaaga wenzangu na kuwaahidi kuwa nikipata nafasi nitawatembelea, tuliondoka hapo kituoni na siku hiyo hiyo tulioanda ndege na kuja America. Tokea siku hiyo maisha yangu yalibadilika kabisa, wazazi hao walinipenda sana kama mtoto wao wa kuzaa. Nikiwa na miaka ishirini Baba alikuja akiwa na karatasi mkononi na kunikabidhi kisha akakaa pembeni kwenye kochi na kuongea "ulisema unataka kuitumikia jamii ili iwe na furaha, basi nafasi hiyo imetoka kujiunga na kitengo cha polisi" aliongea maneno hayo huku akitabasamu. Nilisogea pale alipo na kupiga magoti mbele yake na kwa mara ya kwanza sikumuangalia kama baba bali nilimwangalia katika cheo chake, combat aliokuwa ameivaa ilikuwa imechafuka na vyeo vya kutosha vilivomtanabahisha mbele ya wengine na kuitwa General Griffin Jackson. "hii ndio kazi niliokuwa naitaka ila nilikuwa nashindwa niaizie wapi" niliongea na kuinuka kwa nguvu kisha nikamkumbatia "najua unataka kulinda heshima ya familia yako basi usijali hapa heshima na thamani ya familia hii itadumishwa mpaka mwisho wa dunia" nilimnong'oneza hilo wakati nimemkubatia. kwakweli sikuwahi kuona sikua liofurahi mzee huyo kama siku hiyo tokea nianze kukaa nae. Mama alikuja na kumwambia taarifa hizo nae alionekana kufutahi sana, walianda kijisherehe kidogo kwa ajili yangu. Na baada ya hapo niliijazo fomu ya kujiunga na mafunzo ya polisi, baba aliipeleka inapostahiki.

ITAENDELEA
 
RIWAYA: CODE X 3:
THE REAL ME 1
MTUNZI: Tariq Haji

SEHEMU YA 4

"hii ndio kazi niliokuwa naitaka ila nilikuwa nashindwa niaizie wapi" niliongea na kuinuka kwa nguvu kisha nikamkumbatia "najua unataka kulinda heshima ya familia yako basi usijali hapa heshima na thamani ya familia hii itadumishwa mpaka mwisho wa dunia" nilimnong'oneza hilo wakati nimemkubatia. kwakweli sikuwahi kuona sikua liofurahi mzee huyo kama siku hiyo tokea nianze kukaa nae. Mama alikuja na kumwambia taarifa hizo nae alionekana kufutahi sana, walianda kijisherehe kidogo kwa ajili yangu. Na baada ya hapo niliijazo fomu ya kujiunga na mafunzo ya polisi, baba aliipeleka inapostahiki. Alirudi nyumbani na fomu nyingine na kunikabidhi na kunambia kuwa natakiwa niripoti kituo kikubwa siku ya pili.Basi siku ya pili ilifika mapema na baba alinikabidhi suti nzuri sana na kunambia nivae. Baada hapo tuliungana na mama sebleni tukapata chai ya asubuhi kisha mimi na baba tukatoka kuelekea kituo kikuu. Tulifika na baba akaniacha hapo kisha yeye akaelekea makao makuu ya jeshi ambako alikuwa ameitwa. Niliingia ndani na kukuta atu wengine washafika, kuna baadhi waliponiona walianza kucheka lakini wala sikuwajali kabisa. Niliwachukulia kama wapuuzi tu, baada muda kidogo alikuja mkuu wa kituo hicho na kuanza kutueleza mambo kadhaa. Baada ya hapo wanawake tulielekezwa katika chumba maalum kwaajili ya kuchukuliwa vipimo mbali vikiwemo vya magonjwa. Baada kumaliza mchakato huo tuliambiwa tufike katika kambi maalum kwa ajili ya mafunzo kuanza.
Basi nilirudi nyumbani nikiwa na furaha sana, nilimueleza mama kila kitu na alionekana mwenye kufurahi sana. Baada ya hapo kila mtu aliendelea na majukumu yake na jiobi ilipofika baba alirudi lakini alikuwa tofauti na alivyoondoka asubuhi. Alionekana mwenye huzuni sana, mama alijaribu kumdadisi lakini hakuongea kitu bali alimpatia karatasi. Mama nae baada ya kuisoma alianza kunyong'onyea, ilibidi niichukue na mimi niisome na hapo ndio nikagndua kwanini wote wamenyong'onyea. ilikuwa ni barua ilioandikwa na kusainiwa na raisi wa nchi hii ikimueleza baba kuwa amelitumikia taifa sana hivyo alitakiwa kustaafu na kupumzika ili awaachie wengine waendelee kupeperusha bendera.

Kitu hicho kilmuuma sana baba hata mama pia, basi nilimsogolea na kumwambia kuwa kila kitu kinachofanyika ni mipango ya Mungu. Labda kwa wakati ule alikuwa anatakiwa akae nyumbani aendeshe maisha ya kawaida ili alipe ule muda wote aliokuwa mbali na mama. Niliongea nae sana mpaka mwisho akaelewa na kuchangamka tena, mama aliandaa chakula cha usiku tukala na kila mtu akaelekea chumbani kwake kupumzika. Siku ya pili mapema baba aliamka na kupeleka barua ya kukubali kustaafu, alirudi nyumbani akiwa mchangamfu kama kawaida na kuungana na mimi pamoja na mama. Siku chache mbele iliandaliwa sherehe ya kuagwa na mheshimiwa raisi, na hapi alikabidhiwa medani ya dhahabu ya General bora katika kulitumikia taifa lake.
Siku ya kuripoti mafunzoni ilifika na mapema niliwasili katika kambi tulioambiwa, tulipewa maelekezo yote yaliokuwa yanatuhusu na baada hapo tukaanza mazoezi. Kwakweli yalikuwa mazoezi magumu sana kuliko nilivofikiria, ulifika wakati nilifikiria hata kutoroka lakini kila nilipokumbuka hadi niliompa baba nilipata ujasiri na kuendelea na mazoezi. Nilichunika chunika vya kutosha mpaka basi. Ila mwisho nilizoea maumivu na kuendelea na mazoezi bila shida yoyote ile. Muda wa mazoezi ulimaliza na tulikabidhiwa vyeti vyetu pamoja na nguo za kazi, siku hiyi ilikuwa ni ya furaha sana kwa kila mtu ambae alishieiki katika mazoezi yale magumu. Baada ya sherehe fupi tulipew ruhusa ya kurudi nyumbani huku tukisubiri kupangiwa vituo vya kufanyia kazi. Baba alionesha furaha ya hali ya juu sana, alinifanyia kasherehe kadogo hivi. "mwanangu jukumu ulilobeba sio dogo na sio kila mtu atakua na furaha na wewe, kwa hiyo ujiandae vilivo" maneno yalitoka kinywani mwa baba akinihusia. Nilitikisa kichwa kuashiria nimemuelewa, baada ya siku ya mbili nilipokea simu kuwa nimepangiwa kituo kikuu. Hiyo ilikuwa furaha nyingine kwa sababu sikupangiwa mbali na nnapo kaa. Siku ya pili niliwasili kituoni na kutambulishwa kituoni pamoja na kutambulishwa kwa mtu ambae nitakuwa nashirikiana nae. Alikuwa anaitwa Mike, alikuwa mtu mcheshi sana na alikuwa mchangamfu na mchapa kazi. Mike alikuwa mzoefu katika kazi hio, alikuwa na zaidi ya miaka mitatu. Mwanzo kila mtu alinisangaa kituoni kutokana na kovu langu usoni lakini kadiri siku zilivyokwenda walinizoea na kutokana na kujichanganya kwangu nao basi ilikuwa rahisi sana kupata marafiki wengi. Baada ya wiki moja nilipangiwa kazi ya kwanza nje ya kituo, na ilikuwa ni kuongoza msafara wa waziri mkuu katika eneo karibu na kituo chetu. Haikuwa kazi ngumu kabisa hasa ukizingatia ilikuwa ni kufunga njia tu wakati msafara unapita. Nilimaliza na kuripotu kituonim, Maisha kama askari wa kawaida yaliendelea kuwa mazuri huku kila siku sifa zangu zikizidi kutapakaa kutokana na uchangamfu wangu.
Siku moja nikiwa na Mike katika mgahawa mmoja hivi nikipata chai, ghafla tulisikia mlio wa risasi na bila kuchelewa tulitoka huku mikono ikiwa viunoni ambako kulikuwa na bastola zetu ndogo. Tulishuhudia gari moja likitupita kwa kasi huku mtu mmoja akiwa ametoa kichwa nje na kushambulia, tuliingia kwenye gari yetu na kuanza kuwafukuza. Ukweli Mike alikuwa dereva mzuri sana maana aliweza kumudu gari na kukwepa gari nyingi akiwa katika mwendo kasi. Nilitoa kichwa nje na kuipiga gari tuliokuwa tunaifukuza risasi katika tairi ya nyuma na kusababisha ipoteze muelekeo na kugonga nguzo pembeni. Walishuka watu watatu na kuanza kutushambulia, kwa bahati mbaya risasi moja ilimpata Mike begani. Sikuhitaji kufikiria mara mbili, niliteremka kwenye gari na kujificha pembeni kwenye mlango kisha nikatoa radio call na kuomba msaada. Wakati nasubiri msaada mashambulizi yalizidi kuwa makali kawa sababu wale majambazi walikuwa wanatumia silaha nzito sana. Wakati nikiendelea kushambuliana nao nilishutuka mlango ukifunguliwa na Mike akajiangusha chini kisha akanipa ishara niende nyuma kwenye buti. Nilifanya hivo bila kuchelewa, nilifika nyuma na kukuta buti limeshafunguliwa, nilikuta bastola aina ya shotgun na SMG. Nilibeba zote mbili na kurudi mbele ambako Mike alikuwa akiendelea kupambana nao. Nilimkabidhi SMG lakini akanambia nitumie mimi yeye akachukua shotgun. Hapo sasa moto ulizidi kuwa mkali maana sasa uwezo wa silaha ulikuwa unafanana. Baada ya dakika chache msaada ulifika na hapo tukafaikiwa kuwakamata, gari ya wagonjwa ilifika na Mike pamoja na raia kadhaa waliojeruhiwa katika pambano hilo waliwahishwa hospitali punde baada ya kupatiwa huduma ya kwanza. Niliporudi kituoni, mkuu wa kituo aliniita ndani moja kwa moja nikajua kuwa hizo ni lawama. Lakini haikuwa hivo, mkuu wa kituo alinisifu kutokana na ujasiri wangu hasa ukizingatia bado nilikuwa mgeni kati anga hizo. "karibu katika matatizo" mkuu wangu aliongea maneno hayo ambayo kwa haraka sikuweza kuifahamu maana yake, Baada ya hapo niliruhusiwa kurudi nyumbani kupumzika. Lakini nilipofika nyumbani nilimkuta mzee akiwa amevimba kwa hasira, nilipojaribu kumuuliza kuna tatizo gani hakunijibu kitu na kuinuka akaingia zake ndani. Hapo kichwa kilijaa mawazo, basi niliingia chumbani kwangu na kujifanyia usafi kisha nikatoka. Nilipofika ukumbini nilimkuta mzee akiwa anaangalia taarifa ya habari, nilimsalimia kisha nikakaa pembeni yake. "jemedari mzuri anazuia uhalifu na wakati huo huo ana hakikisha mtu asiehusika hapati jeraha lolote, na pia jemedari mzuri ni yule anaehakikisha mwenzake hajeruhiwi" alianza kuongea maneno hayo kisha akaniangalia na kunambia "umefanya vizuri lakini unatakia ujitahidi na kuhakikisha usalama wa raia". Baada kuongea maneno hayo alinikabidhi karatasi nyeupe ambayo haikuandikwa kitu, kisha akanipa ishara nisiongee kitu na niihifadhi ile karatasi.
Baada maongezi mafupi na baba chakula kilikuwa tayari, wote tulisogea mezani na kupata chakula cha usiku. Tulipomaliza niliaga na kuingia chumbani kwangu kulala, na kutokana na uchovo wa mchana, usingizi ulinizoa nilipogusa tu kitanda. Nilikuja kushtuka baada kuota ndoto mbaya sana, nilipoangalia saa nikagundua ilikuwa saa kum na moja usiku. Niliamka na kujiandaa, niliingia jikoni na kuandaa chai na vitafunuwa vya asubuhi. Nilipomaliza niliandika ujumbe na kuuacha mezani kisha nikatoka. Kitu cha kwanza nilichokifanya, nilielekea hospitali kwenda kumuangalia Mike ambae alikuwa anendelea na matibabu. Baada ya hapo nilielekea kituoni kwa ajili ya kuanza majukumu yangu ya kila siku. Kila mtu kituoni alikuwa akinisifu, na magazeti hayakuwa nyuma nayo. Kila gazeti liliandika linavojisikia "tunahitaji polisi kama huyu", "Waabudu matatizo kaeni pembei, simba jike kaingia mtaani". "mamilioni ya pesa yaoolewa". Hivyo ni baadhi ya vuchwa vya habari vya magazeti machache, niljifanya kama siyashughulikii lakini moyoni nilikuwa nnafuraha na kichwa kilikuwa kikubwa kama dunia kwa sifa. Niliendelea na majukumu yangu ya kila siku kama polisi, baada ya mwezi mmoja Mike alirudi kazini na kuendelea kama kawaida. Wakati huo jina langu lilikuwa lishasambaa na kila mtu alikuwa anataka kunijaribu na kila aliefanya hivo alikutana na kisiki. Baada ya Mike kurudi alianza kunipa mazoezi mengine ya kupigana, kila siku baada ya kazi tulikutana Gym na kuoata mazoezi kadhaa ya kujiweka powa. Maana alinambia kuwa niko hatarini sana kutokana na sifa zangu, mpaka majambazi sugu na wale wanasiasa watakuwa wananiwinda hivyo ni lazima niwe fiti, nisiwe nategemea silaha tu. Na pia alinishauri nihame nyumbani ili familia yangu iwe salama kutokana na mikono ya wabaya. Nililiwasilisha wazo hilo kwa mzee nae hakupinga alikubali na taratibu za kutafuta nyumba zikaanza, haukipita muda nilikuwa na kwangu. Kumbuka hapo nilikuwa na miaka ishirini tu na tayari nilishakutana na vikwazo vingi sana katika kazi yangu.Niliendelea na majukumu yangu huku nikiendelea kupokea mafunzo ya ngumi kutoka kwa Mike, ambae alionekana kama komando. Maana mazoezi aliyokuwa ananipa hayakuwa na tofauti na yale nliokuwa nayaona katika TV na movie mbalimbali wakifanya makomando. Miaka miwili ilipita huku nikiwa nimepandishwa cheo mara mbili, siku hiyo baada ya kumaliza mazoezi. Mike aliniita na kunambia kuwa anataka kuanambia kitu. Mapigo ya moyo yalianza kudunda na kihasho chembamba kikaanza kunitoka. "nimemaliza kazi niliopewa na General, natumai umeiva vya kutosha sasa" aliogea maneno hayo na kuniacha njia panda na kumuomba anielezee. Na hapo ndio akafunguka kuwa yeye ni Leutenant General Mike Kings, na alipewa kazi ya kuhakikisha kuwa naiva vya kutosha katika mafunzo ya kijeshi hasa kwenye mkono.

ITAENDELEA
 
RIWAYA: CODE X 3:
THE REAL ME 1
MTUNZI: Tariq Haji

SEHEMU YA 5

Miaka miwili ilipita huku nikiwa nimepandishwa cheo mara mbili, siku hiyo baada ya kumaliza mazoezi. Mike aliniita na kunambia kuwa anataka kuanambia kitu. Mapigo ya moyo yalianza kudunda na kihasho chembamba kikaanza kunitoka. "nimemaliza kazi niliopewa na General, natumai umeiva vya kutosha sasa" aliogea maneno hayo na kuniacha njia panda na kumuomba anielezee. Na hapo ndio akafunguka kuwa yeye ni Leutenant General Mike Kings, na alipewa kazi ya kuhakikisha kuwa naiva vya kutosha katika mafunzo ya kijeshi hasa kwenye mkono. Na hapo akanitonya kitu kuwa kuwa polisi ni maandalizi ya kuelekea katika jeshi la nchi hiyo. Baada ya mazungumzo hayo aliniaga na kunambia kuwa tutakuja kuonana tena labda jeshini katika mafunzo maalum. Kisha akaondoka, nilikaa kitako kwanza huku nikijiambia mwenyewe kuwa naota na nikiamka kila kitu kitakuwa sawa. Lakini ukweli ulibaki kuwa ukweli tu, maana siku ya pili nilipofika kazini nikakabidhiwa msaidizi mwengine na nilipouliza kuhusu Mike nikaambiwa kuwa amehamishwa kituo. Hapo sasa nikaamini kuwa ndio ulikuwa mwisho wa kuonana na Mike.

Baada ya miezi sita tokea Mike nilipokea barua kuwa nimeitwa katika makao makuu ya jeshi, na bila kuchelewa nilielekea huko. Nilishanga kumkuta baba akiwa katika Gwanda zake za Kijenerali huku pembei akiwa amesimama Mike katika combat takatifu ya Lt. General. Baada ya robo saa waliingia watu wengine sita wakiwa wameongozana na vijana ambao walikuwa mapolisi kama mimi kisha tukaelekezwa katika chumba maalumu cha vikao. Hapo alisimama baba na kutoa salamu kisha akaanza kuonge "najua wengi mtajiuliza kwanini mumeitwa hapa, ila ukweli ni kuwa toke mwanzo nyinyi mlichaguliwa kujiunga na kikosi maalum cha kupambana wahalifu sugu. Natumai wote mumewahi kusikia kikosi kinachoitwa "THE PIRATES". Na wengi mlikuwa mnadhani ni stori lakini kikosi hichi kipo na ndio kinachopambana na wahalifu sugu hapa nchini na je ya nchi. Na sheria, ili ujiunge na kikosi hichi ni lazima uanze katika ngazi za askari wa kawaida. Hivyo basi hongereni na karibuni katika anga za majanga".
Kuna kitu sikukielewa na nlipotaka kuongea kitu, mzee alinipa ishara kuwa ninyamaze. Baada ya kikao kile kifupi cha utambulisho tulipelekwa katika chumba maalum na kupigwa picha kisha tukaruhusiwa turudi katika maeneo yetu ya kazi na kuambiwa kuwa hiyo ni siri na hakutakiwa mtu mwengine zaidi yetu kujua. Nilirudi kituoni kwangu nikiwa na maswali kadhaa lakini wa kuyajibu alikuwa ni mzee tu. Hivyo nilisubiria mpaka zamu yangu ilipokwisha na kuondoka kituoni lakini sikwenda nyumbani kwangu. Moja kwa moja nilielekea nyumbani kwa wazazi wangu na nilipofika tu baba alitabasamu na kunipa ishara nikae. Na kwa sababu mama alikuwa hayupo nikaona huo ndio mwanya pekee wa kumuuliza maswali yangu. Swali la kwanza lilikuwa ni ilikuwaje hasa akarudia gwanda wakati yeye alishastaafu. Nae akanijibu kuwa kustaafishwa kwake ilikuwa ni moja kati ya mipango ya raisi ili amkabidhi majukumu mengine ambayo yalikuwa ni siri. Akasema kuwa ile siku alipokwenda kukabidhi barua ya kukubali kustaafu, mheshimiwa raisi alimwambia kuwa hajastaafishwa bali alipewa majukumu mengine makubwa zaidi ya kuendesha kikosi maalum cha THE PIRATES. Yeye mwenyewe alishangaa baada kusikia jina hilo kwani alikuwa akidhani uwepo wa kikosi kile maalum ni maneno tu ya watu. Lakini mhshimiwa raisi alitaka baba akiongoze kikosi hicho ambacho alikuwa akikiongoza mwenyewe kwa muda mrefu, kutokana na majukumukuwa mengi aliamua kukibadhi kikosi hicho kwa mtu ambae ni mzalendo sana na hakuwa mwengine isipokuwa baba. Baada ya hapo ndio akapewa maelekezo yote yanayostahiki, baada kunieleza hivo kidogo roho yangu ilitulia. Basi tuliendelea na mazungumzo mengine mpaka mama aliporudi nikamsalimia na baada dakika kidogo niliaga na kuondoka. Nilirudi nyumbani nikiwa mwepesi kabisa baada ya maswali yangu yote kujibiwa, nilipumzika kwa amani kabisa usiku huo.
Siku iliofuata mapema niliamka na kufanya mazoezi kisha niakaoga na kupata kifungua kinywa, nilipomaliza kila kitu nilitoka na kuelekea kazini. Nilipofika niliambiwa nahitajika na bosi ofisini, na nilipoingia tu alinikabidhi karatasi ya uhamisho wangu. Nilijua tu mambo yashaiva, niliichukua karatasi ile na kurudi nayo ofisini kwangu. Niliifungua na kuanza kuiosoma mwisho iliandikwa "ukiupata ujumbe huu, mara moja fika makao makuu ya jeshi ukiwa na hii karatasi". Nilitoka ofisini kwangu mbio za ajabu na moja kwa moja hadi kwenye gari yangu na safari ikaanza. Nilikanyaga mafuta kisawa kwa mara ya kwanza sikuheshimu hata sheria za barabara. Baada ya dakika kumi nilifika makao makuu na kuwaonyesha ile karatasi wanajeshi waliokuwa getini. Walinipa maelekezo ni wapi natakiwa nifike, bila asante niliondoa gari na kuelekea sehemu ya megesho. Nilishuka na kuanza kukimbia, nilifika katika koridoo ambayo ndio nilipoelekzwa nikakuta karatasi imeandikwa "una sekunde sitini tu kufika juu kabisa ya jengo hili, ukichelewa helicopter ina kuacha" nilihisi kuchanganyikiwa hasa ukizingatia katika koridoo ile kulikua na watu wengi kweli. Nilianza kukimbia huku nikipigana vikumbo na watu wengine lakini wala sikujali, na nilipoona nazidi kuchelewa ilibidi nitumie mafunzo ya ziada ili kuwapita watu hao. Nilivua viatu huku nakimbia, hapo sasa nilianza kuwaruka kwa kukanyaga kuta za koridoo hio. Wengine niliwasukuma kwa nguvu na kuwatupa pembeni, niliongeza mwendo huku akili yangu ikiwa inafanya kazi kama computer. Nilifika juu ya jengo hilo lakini sikuikuta helicopter, nilianza kujilaumu lakini ghafla alitokea mtu kwa pembeni na kunipa ishara nimfate kisha yeye akaongoza njia. Tulifika katika chumba kimoja hivi na kuwakuta wengine wakiwa wananiangalia, mara walianza kupiga makofi. "umetumia sekunde hamsini na tatu" aliongea Mike huku akitbasamu. Baada ya nusu saa tulipewa mabegi na kuambiwa tuongozane na Mike mpaka juu kule, tulipofika tulikuta helicopter ikitusubiri. Tulipanda na safari ikaanza, tukiwa ndani ya chombo hicho tulipewa maziwa kuambiwa tujwe kwa sababu safari ni ndefu sana. Cha ajabu baada ya kunywa tu maziwa hayo macho yalianza kuwa mazito na mwisho wote tukapitia na usingizi mzito. Mimi nikuja kushtuka baada kuhisi hewa nzito, na nilipofungua macho nilishtuka baada kuona chombo tulichopanda kinawaka moto, niliwaangalia marubani wote walikuwa wakivuja damu. Nilianza kuwaamsha wenzangu wengine ambao kwa ujumla wetu tulikuwa saba, wote tulitoa nje ya chombo hicho. Baada kuridhika kuwa hakuna hata mmoja wetu alieumia sana, tulikaa kwanza huku kila mtu akitafakari kuwa ni jambo gani lililotokea. Kutokana na kiza tulishindwa kugundua tuko wapi, na ilibidi tulale hapo hapo. Siku ya pili mapema tuliamka na kila mtu alichukua begi lake alilopewa na kufungua, ndani ya mabegi hayo kulikuwa na combat pamoja na silaha nyepesi na vifaa vya mawasiliano.
Kila mtu alitoa nguo na kubadili kisha akachukua na vile vifaa maalum vya mawasiliano na kuweka sikioni. "jamani ndio tumepata ajali hivi, tunatakiwa tutafute njia ya kutokea" aliongea mwanaume mmoja kati yetu. Na wote tulikubaliana nae na pia tukakubaliana kuwa tutakaa pamoja hata litokee jambo gani. Kila mtu alijipanga vilivyo na wakati naendelea kukagua begi langu nikakuta ramani, niliitoa na kuitandika chini kisha kwa pamoja tukaanza kuiangalia kwa makini. Mschana mmoja alitoa kampas na kuweka juu ya ramani hio, wakati tunendele kukagua ramani hio tukaona alama ya fuvu. Tukakualiana kuwa tunaelekea hapo kweye hiyo alama, baada hapo tulisimama na safari ikaanza huku tukiwa tunapiga stori mbili tatu ili kupunguza safari. Baada ya masaa sita mfululizo ya kutembea tulifika pahali tukakuta makazi yaliokimbiwa na watu kabisa. Majumba ya eneo hilo yalikuwa yamevunjika na kubomoka, sehemu hiyo ilitawaliwa na vumbi na moshi. "jamani hapa tunatakiwa tuwe makini sana" niliongea huku nikitoa bastola yangu ndogo na kuishika vizuri mkononu. Na wengine wote waliniunga mkono nao wakatoa za kwao na tukaaanza kutembea taratibu kwa umakini wa hali ya juu kabisa. Tulitembea huku macho yetu yakiwa wazi na kuangaza pande zote, ghafla tulianza kusikia milio ya risasi. Ilibidi tujibanze pembeni na hapo sasa kila mtu akawa muoga kukaa mbele, ilibidi nijitolee kuwa kiti moto. Nilishika bastola yangu kisawa na kucungulia, kwa mbali nilimuona mtu akiwa amejibanza sehemu huku akiwa na bastola. Niliwageukia wenzangu na kuwaambia nilichokiona, baada kushauriana tukaaanza kukimbia ukuta baada ya ukuta. Cha ajabu yule mtu alikuwa hashambulii lakini tulipomkaribia zilirindima risasi kama mvua, ilibidi tugawanyike makundi mawili ili kumchanganya. Tukawa tunasogea taratibu, na alipowashambulia wenzangu kundi jingine. Nilichomoka sehemu nilio kwa kasi kubwa na kubirngitia kabla hata hajageuka nilipo nilifyetu risasi iliompata kifuani na kumfanya aanguke kama mzigo.
Tulimsogelea na kumuangalia, baada kuhakikishakuwa ameshakufa tayari. Nilirudisha bastola yangu ndogo kiunoni na kubeba ile AK47 aliokuwa anatumia adui yetu. Safari iliendelea kwa umakini wa hali ya juu huku mara kadhaa tukishambuliana na watu. Kadri muda ulivyokwenda walizidi kuwa wengi lakini tulifanikiwa kupita eneo hilo bila hata mmoja kupata majeraha makubwa zaidi ya michubuko tu. Baada ya kutoka eneo hilo tuliingia porini na kwa vile tulitembea muda mrefu bila kupumzika na hasa baada ya kupata ule mshikemshike tulijikuta tukiwa tumechoka sana na kuamua kupiga kambi ndani ya msitu huo ili siku ya pili. Tuligawana majukumu, wengine walitengeneza mahema na wengine tuliinia vichakani kutafuta kuni za kuwashia moto. Baada ya kazi zote kukamilika, tuligawana majukumu ya ulinzi usiku huo. Wawili walilinda na wengine walila, baada ya masaa matatu wale walikuwa wanalinda walikuja kuniamsha mimi na mwenzangu mmoja tukaendelee na zoezi lile wakati wao wanapumzika. Baada ya masaa matatu mengine tuliwaamsha wengine waendelee na kazi ya ulinzi lakini mimi sikurudi ndani kulala.

Niliendelea na wale wengine mpaka asubuhi, palikucha na kila mtu alijiandaa kuendelea na safari. Kwa kweli njaa ilikuwa inauma sana, siku nzima tulikuwa hatujala baada ya kunywa ya maziwa yaliotulaza. Wenzetu wawili walikuwa wameshaanza kulegea, lakini ilibidi wajikaze tu maana safari haikuwa ndefu tena. Baada ya masaa mawili tulifika katika geti kubwa. Tulishangaa kweli baada kwaona wale marubani ambao tuliamini walikuwa wamekufa katika ajali ya ndege wakiwa wanatusubiri getini. "hongereni kwa kumaliza mafunzo ya awali" waliongea wanajeshi hao na kutukabidhi kila mmoja wetu chupa ya maji. Baada ya hapo tuliingia ndani ya kambi hiyo kubwa na kupelekwa katika sehemu ya kula na kupata chakula. Kila mtu alikula kama chakula kinataka kukimbia, chezea njaa wewe.

ITAENDELEA
 
Madame katika ubora wake.asante ingawa bado sijaisoma.nikimaliza shuhuli zangu nitasoma.ila nakuaminia.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…