Halfan Hamisi
New Member
- Sep 11, 2021
- 4
- 7
BAKI NA MIMI
Email: halfanhamis337@gmail.com
Yusto alimaliza kusoma ujumbe huo kutoka kwa Brandina wenye utani ndani yake, akainua macho yake akamtazama Caren akakuta nae anamtazama.
"vipi"
"mmh poa tu vipi"
Waliongea baada ya kutazama kwa muda kila mmoja akaonyesha kama hamna kilichotokea, lakini haikuwa hivo.
SASA ENDELEA...
Kwa mtazamo hali ilionekana kuwa shwari baina ya wawili hao wanaopendana, lakini uhalisia haukuwa hivyo kuna bomu kubwa lilikuwa kati yao. Yusto hakuwa akifahamu kuwa mwanamke anaempenda Caren, ndiye sababu ya matukio yote yanayowaumiza kichwa chuoni hapo. Ni kweli kuna wakati alihisi huenda Caren anahusika lakini baada ya penzi kuibuka katikati yao ikamfanya ajisahau na kutojishughulisha tena na hisia zake.
Caren nae akiongozwa na hisia za mapenzi kwa Yusto anajikuta kuanza kupoteza umakini katika kazi aliyoagizwa asijue kama Yusto ndiye adui yake mkubwa na wanafanya kazi mbili zinazokinzana.
Yusto anapokea ujumbe kutoka kwa jasusi Brandina akimtaka wakaongee kumuhusu Caren, wakati huo huo Caren nae anapokea ujumbe kutoka kwa wakubwa zake wakimtaka ahakikishe anakata umeme wa dharula uliofungwa chuoni hapo.
Meseji hizo zinawatoa kwenye mudi wote wawili.
"Samahani nina dharula naweza kwenda" alisema Yusto
"Jamani si umekuja sasa hivi lakini" alisimama Caren akionekana kutofurahishwa na kauli ya Yusto lakini ukweli nae alikuwa anataka kuondoka kwa ajili ya mwenda kujiandaa na kazi aliyopewa.
"Noo, nitakutafuta tena baadae Caren usijali" alisema Yusto.
Mwisho walikubaliana na Yusto akaondoka.
********
Majasusi wawili Brandina na Simigo walikuwa ndani ya chuo cha Mark Moon, waliingia kama wapishi wapya ambao huandaa vyakula vya wanafunzi chuoni hapo.
Walionekana wakiwa wamesimama kwenye dirisha kubwa la kioo wakiwa ndani ya jengo moja la kisasa ambalo ndilo lilikuwa jiko la chuo hicho.
Walikuwa wamesimama wakitazama nje huku wakizungumza baadhi ya mambo kuhusu jukumu zito walilokuwa nalo ndani ya chuo hicho.
Kwa mbali Yusto alionekana anaelekea bwenini, wakawa wanamuangalia huku wakiendelea na mazungumzo.
"Unahisi kweli Yusto yupo karibu na Caren kwa ajili tu ya kumpeleleza" aliuliza Simigo
"Sina hakika ndio maana nataka niongee nae kwanza nitajua tu, kwani unahisi wanamahusiano" alijibu Brandina nakuuliza swali huku wakiwa bado wanamuangalia Yusto.
"Sijasema hivo lakini kuna mazingira fulani hivi yananifanya nihisi hivyo"
"Mmh sina hakika Yusto yuko smart sana hawezi" alisema Brandina
Punde meseji ya Yusto iliingia kwenye simu ya Brandina
Uko wapi ,,
Niko huku jikon nakuja nikukute chumbani kwako
Alijibu Brandina kisha akamuaga Simigo na kuanza kuondoka.
"Brandina" Simigo aliita
Brandina akasimama na kugeuka.
"Hakikisha unafanya kazi yako, usilete habari nyingine"
"Unamaana gani Simigo"
"Nimeona macho yako namna unavyomuangalia Yusto"
"Unamaana gani"
"Sipendi uzembe kazini, nina wasiwasi Yusto amechanganya mapenzi na kazi ndio maana hajafanikiwa mpaka sasa ,naona na wewe unataka kudondokea huko, tangu mda nimekuwa nakufuatilia"
" Simigo haujatumwa kunifuatilia Mimi, hebu na wewe focus kwenye kazi najua nini nafanya"
Brandina aliongea kwa ukali kidogo kisha akaondoka, maneno aliyoambiwa na Simigo yalimuudhi ingawa yalikuwa na ukweli ndani yake. Japo hakuwa ameweka wazi jambo hilo lakini tayari jasusi Simigo alisha msoma akampa tahadhali asichanganye mapenzi na kazi.
************
Muda mfupi baada ya Yusto kuondoka, Caren nae alisimama na kuanza kuelekea bwenini chumbani kwake, akiwa bado hajafika mara alikutana uso kwa uso na Sophia.
"Nilikuwa nakutafuta sana, wewe ndio Caren si ndiyo" alisema Sophia huku akimtazama Caren juu mpaka chini.
Kwa mbali alionekana Brandina anaenda zake mabweni ya wanaume kwa ajili ya kwenda kuzungumza na Yusto lakini alisimama ghafula baada ya kumuona Caren kwa mbali, haikuwa sura ngeni kwake kwani tayari alikuwa na picha zake.
Akatamani kujua anafanya nini wakati huo, akaanza kuwasogerea pale waliposimama na Sophia.
**********
Caren na Sophia walikuwa wanatazamana huku kila mmoja akiukumbuka ule usiku walipokutana Caren akiwa na Yusto na Sophia akiwa na John.
"Habari" Caren alivunja ukimya
"Si nzuri Caren, nina shida na wewe ndio maana niko hapa" alisema Sophia huku akimsogelea Caren kwa ukaribu zaidi kisha akaanza kuzungumza
"Caren Mimi kama mwanamke mwenzio niko hapa kwa ajili ya kukuomba unisaidie jambo moja, ni kuhusu Yusto. Sijui ni nini kinaendelea kati yako wewe na Yusto lakini nataka nikwambie kuwa Yusto ni mwanaume wangu, ndoto zangu zote nimezielekeza kwake, Mimi na yeye tumetoka mbali mno tumekuwa tukiishi kama marafiki lakini ukweli tunapenda sana.
Yusto hajawahi kuwa na hisia za kimapenzi na mimi lakini kama mwanamke nimekuwa nikipambana kumfanya anipende hivi karibuni jitihada zangu zilianza kuzaa matunda Yusto alianza kuzielewa na kuziheshimu hisia zangu kwake lakini ghafula umekuja wewe Caren, ujio wako umevuruga kila kitu, yaani kila kitu. tulikuwa tumepiga hatua tatu mbele lakini wewe umeturudisha hatua kumi nyuma. Caren nakwambia yote haya ili unionee huruma mimi kama mwanamke mwenzako, bila Yusto mimi si chochote, nakuomba nakuomba sana Caren niachie Yusto wangu"
Sophia alikuwa akiongea kwa uchungu mkubwa mno kiasi cha kumfanya Caren amatazame kwa jicho la pekee.
Ni kweli Sophia alimaanisha kile alichokisema, lakini ilikuwa ni ngumu sana kwa Caren kufanya hivyo, tayari moyo wake ulishaanza kuota mizizi kwa penzi la Yusto, kumtoa ghafula tena haikuwa ni kazi rahisi hata kidogo.
Ni kweli Sophia alionekana kuhitaji msaada lakini angefanya nini sasa ilihali na yeye pia anampenda Yusto.
Caren alijikuta katika hali ya kujiuma uma asijue atamjibu nini Sophia. Sophia nae aliendelea kumtazama Caren usoni akihisi ni lazima atasema neno lolote angalau kumfariji.
Caren hakuwa na la kusema kabisa, alishindwa hata kumuangalia Sophia usoni. Akawa anawaza na kujijibu mwenyewe.
'''hapana Caren usimuonee huruma, usikubali kumuacha Yusto, ni mwanaume wako tena anakupenda""
Aliwaza Caren.
Mwisho akamua kuondoka bila kujibu chochote. Hakufika mbali Sophia alimkimbilia na kumshika begani akamzuia asitembee.
"Inamaana hujanisikia Caren, inamaana nilichoongea umeona ni upuuzi Caren kweli" alisema Sophia safari hii chozi likamdondoka,
Caren alimtazama usoni kwa masikitiko huku roho yake ikimuuma pia, hakutaka aendelee kujiumiza zaidi.
Akaanza tena kuondoka huku akiutoa mkono wa Sophia begani kwake lakini Sophia alimng'ang'ania kwa nguvu kiasi cha kufanya aichane nguo yake.
Caren alipigwa na butwaa baada ya kuona nguo yake imechanwa kiasi cha kufanya bra aliyovaa ndani ionekane, aligeuka haraka na kumsukuma Sophia kwa nguvu akadondoka chini.
Kilikuwa ni kitendo ambacho Caren hakuwa ametarajia kukifanya ilitokea tu ghafula, Sophia alianguka chini vibaya mno akaumia mguu wake.
"Hey hey hey ninyi vipi" mara sauti ya mwanamke ilisikika nyuma ya Caren
Caren akageuka kuangalia ni nani, hakuwa mwingine bali Brandina jasusi mkenya aliyekuwa chuoni hapo kwa kazi maalum. Kwa muonekano wake wala usingezani anafanya kazi hiyo hatari na ngumu. Brandina alikuwa mrembo haswa na alijua kutunza urembo wake.
"Wewe, ni nini kumsukuma mwenzako hivyo bila hata haya, vipi kama ukimuumiza" alisema Brandina huku akimsogelea Caren.
Caren alibaki kimya bila kuzungumza chochote akawa anamtazama Brandina akizidi kumsogelea na mwisho akafika karibu kabisa wakawa wanatazamana uso kwa uso.
"Nakuliza unaniangalia nini" alisema Brandina huku akilini mwake akijua ni nini anafanya jasusi huyu.
"Don't try me, better to ask before judging" (usinijaribu, ni vema kuuliza kabla ya kuhukumu)
Caren aliongea kwa kiburi kisha akampisha Brandina na kuondoka zake.
Hali akitabasamu Brandina alimsindikiza Caren kwa macho hadi alipopotelea jengo la hostel (bweni).
"She is smart" (yuko vizuri)
Alisema Brandina akiwa tayari amepata jibu la alichokuwa anakitafuta kwa Caren. Hii ilikuwa ni moja ya mbinu za kijasuji kusoma saikolojia ya mtu.
Brandina aligeuka na kumtazama Sophia pale chini, akamsogelea na kuchuchumaa pembeni yako.
"Pole mpenzi umeumia" alisema Brandina.
"Asante dada, mguu kidogo umeshtuka, watu wengine bwana, nasema atalipa kwa hili, lazima alipe" Sophia aliongea kwa hasira kiasi.
Brandina aliyekuwa pembeni yake alijikuta anatabasamu.
"" Wewe ndo utakuwa kete yangu ya kumpata Yusto,,, oooh mwanaume anabahati huyu inakuwaje tukampenda wote watatu""" aliwaza Brandina huku akitabasamu akawa anamsaidia Sophia kunyanyuka pale chini.
"Naitwa Brandina, ni mpishi wenu mpya hapa chuoni"
" Ooh kumbe, wageni wengi hapa chuoni na ulivyo ulivyo nikajua wewe mwanafunzi mwaka wa kwanza"
"Noo, mimi ni mpishi tu bana,"
"Karibu sana eti"
"Asante dia"
Alisema Brandina hali wakiwa wameshikana mikono na Sophia.
ITAENDELEA...
==> Mambo yanazidi kukolea
==> Mapenzi bado ni changamoto kwa vijana hawa watano Caren, Sophia, Brandina, Yusto na John
==> Nani ni nani na nani ataibuka mshindi?
==>John/brandina atafanya nini?
==>Vipi sekeseke lililopo kati ya Frank, Yusto na majasusi dhidi ya Caren
ENDELEA KUFUATILIA MKASA WA KUSISIMUA NA LOVE STORY KALI NDANI YAKE
Phone: 0754021538