Mie nilishajivumbulia utamaduni wetu waswahili wa kuthamini wageni zaidi. Nikiingia mahali nikahisi watanimind mavazi yangu, najidai sijui kiswahili. Nawatania kidhungu nalegeza ulimi slang kama Nyani Ngabu, wananipa priority huyooo naishia zangu! Cha kufia! Hamna ufanisi, hamtimizi ahadi kwa wateja mnataka wavai wardrobe zenu! Eboo!
..
..binafsi nadhani wangekataza mavazi yanayo-expose viungo vya siri, kama matiti, kitovu, etc etc. .
Hivi 'la saba' maana yake nini? Nauliza tu!... Hajafika hata la saba huyu, mie nakataa kuwa kafika
Hiyo namba 1 sio sahihi kabisa. Ku-list nikab kama mavazi yasiyofaa ni uonevu.
Sasa hata wateja wanakuwa monitored, kama natoka kukaanga samaki ferry napitia vyeti vyangu inabidi nibebe suti kwenye kirambo? Badala ya kukazania ufanisi wanaangalia mavazi, bongo bwana!
Hiyo namba 1 sio sahihi kabisa. Ku-list nikab kama mavazi yasiyofaa ni uonevu.
Sasa hata wateja wanakuwa monitored, kama natoka kukaanga samaki ferry napitia vyeti vyangu inabidi nibebe suti kwenye kirambo? Badala ya kukazania ufanisi wanaangalia mavazi, bongo bwana!
Yaani huyo muandishi kwanza hajui kuandika Kiswahili fasaha, hajui kanuni za uandishi, hana mantiki ya kuweza kujua namna ya kutenganisha mavazi ya kiimani na mavazi yasiyofungamana na imani, hana mantiki ya kuelewa kuwa pale ni ofisi ya serikali na haiwezi kunyima watu huduma kwa sababu tu ya "maadili" ambayo hayajaainishwa popote kwenye waraka wa serikali
Hajafika hata la saba huyu, mie nakataa kuwa kafika
Hiyo namba 1 sio sahihi kabisa. Ku-list nikab kama mavazi yasiyofaa ni uonevu.
Sasa hata wateja wanakuwa monitored, kama natoka kukaanga samaki ferry napitia vyeti vyangu inabidi nibebe suti kwenye kirambo? Badala ya kukazania ufanisi wanaangalia mavazi, bongo bwana!
Kwenye ofisi za RITA kuna hili tangazo.
TANGAZO
Ndugu wapendwa wateja wetu, mnakumbushwa kwamba hii ni taasisi ya Serikali ambayo inaendeshwa kimaadili hivyo basi hatutapendelea baadhi ya mavazi yasiyofaa na yasiyo na heshima kuvaliwa ofisi kama yafuatayo:-Wateja wetu mnakumbushwa kwamba atakayekiuka maagizo hayo hapo juu hataruhusiwa kuingia ndani kupata huduma zinazotolewa na Wakala.
- Mavazi yanayofunika uso wote - Kininja "Nikab".
- Singet (fulana zisizo na mikono)
- Kaptula
- Suruali zinazolegea "Mlegezo"
- Kofia kubwa "Parma"
- Vitop vya kike vinavyoonyesha vitovu
UTAWALA
08 Februari 2011
Kwa hiyo RITA walikuwa sahihi kukataza kuvaa 'Kininja' kwa kuwa kuna joto kali sana !!!Pale makao makuu RITA joto kali, ... sasa ukivaa kaptula na fulana ingefaa sana.
Wakuu wangu ni lazima tutambue kwamba ofisi za serikali na taasisi zake siyo sehemu za starehe,nyumbani kwako ama vijiwe ambako unaweza ukajivalia unavyotaka wewe. Kuhusu nikab mimi nasema ni sahihi kabisa. Haiwezekani uende ktk taasisi muhimu kama RITA umeziba uso. Ikiendekezwa tabia ya kuacha mambo eti tusihudhi dini ama dhehebu fulani kuna siku wengine watajitokeza watadai dini yao ama dhehebu lao hawavai nguo.
Jamani acheni jazba zisizo na mpango. Kila ofisi lazima iweke taratibu za kimaadili kulingana na hadhi ya ofisi hiyo ua sababu za kiusalama. Nendeni basi Ikulu au ofisi ya waziri mkuu muone kama mtaruhusiwa kuingia Ninja style.
Ofisi ya waziri mkuu kuna tangazo kama hilo na ukienda na kimini au singlet yako haupiti hata kama unapeleka magazeti.
Naomba kuwauliza swali mnaosema watu wanaoenda na Nikab waruhusiwe kuingia RITA. Wakifika mbele ya Ofisa mtoa cheti na mtu kaja anataka kupewa cheti cha kuzaliwa, unathibitishaje kuwa huyu ndo mhusika kwa kutazama picha yake na sura yake halisi? Imagine ndiyo wewe umesimamiwa na mtu mbele yako hauoni kitu zaidi ya macho, je unamwambia jifunue au?
Kila ofisi ina taratibu zake kama unajisikia sana hamu ya kuvaa mlegezo au singlet Dar ni joto sana nenda kavae wanakoruhusu. Ofisi zote za umma zinafanya kazi kwa niaba ya Mkuu wa Nchi hata kama ni ofisi ya kata. Kama mtu anadhani anaweza kwenda mbele ya Mkuu wa Nchi akiwa maziwa yako nje au na singlet au Nikab basi atetee hoja hii.
Tuvae jeans na tops huku ambako wanaruhusu kujirusha maofisini tuwaachie wengine na ofisi na masharti yao.
Nimeshaelewa nia yenu nyie Wasomali mnaokazania kufunika nyuso. Mnataka janja ya kuwachukulia ndugu zenu vyeti kimtindo. Basi poleni, serikali imeshtuka. Ukitaka cheti, weka uso wazi ujulikane wewe ni nani