Mwene chungu
JF-Expert Member
- Nov 12, 2016
- 915
- 752
Habari wanajamvi!
Nimebahatika kutembelea ofisi za RITA pale posta Mara kadhaa kufuatilia VYETI vya kuzaliwa vya vijana wangu.
Mara ya kwanza nilifuatilia Cha kijana wangu mkubwa nikafanya malipo ya 10,000 wakanipangia tarehe ya kukifuata lakini nilipoenda wakadai stakabadhi haisomeki kwenye mfumo (invalid receipt) yaani malipo si halali hivyo niamue moja ama kulipa tena au nisubiri hadi zitakapofanyiwa kazi.
Na kwa mjibu wa maelezo ya aliyekuwa ananihudumia hakusita kusema inaweza kuchukua miezi kadhaa..akanishauri nilipie tena ili kupata cheti haraka! Nilifanya hivyo mara ya hivyo,awamu hii nikakipata!.
Mapema mwa mwezi wa tatu mwaka huu nilienda kuandaa kingine,nikalipia 3500/= kwani mtoto bado mdogo.Kama kawaida nilipokifuata nikaambiwa invalid receipt na hivyo Kama nakihitaji haraka nilipie tena au kiwekwe foleni hadi receipt itakapohakikiwa kuwa ni halali!!
Kwa shingo upande nililipia tena huku nikagundua siko pekee yangu wenye tatizo Hilo,mathalani kwa wakati ule tuliolipia tena hatukuwa chini ya 20.
Nikakumbuka mwezi mmoja nyuma tulilipia tena karibu watu 7 au nane hivi kwa muda niliokaa pale Ofisini..nikajiuliza siku zingine wangapi wanalipia tena?.
Nikajiuliza hizi hela za Mara ya pili zinaenda wapi? ..Je viongozi tuliowapa dhamana ya kutatua matatizo hili hawajaliona? Kwanini waache litutese?
SIKUONA BOX LA MAONI PALE OFISINI
LAKINI NAAMINI KUPITIA MTANDAO HUU RITA MTALIFANYIA KAZI TATIZO HILI..
SIKU NYINGINE SITAANDIKA KWA LUGHA LAINI KAMA LEO.SITAKI KUTOA MAONI MAANA NYIE MNALIJUA ZAIDI HILI NI TATIZO KWA KIWANGO GANI.