RITA imekuwa kero kwa wananchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

RITA imekuwa kero kwa wananchi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tikerra, Jan 29, 2009.

 1. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #1
  Jan 29, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mimi ni mkazi wa mkoa wa Morogoro,na makazi yangu yapo kwenye kijiji kiitwacho Dakawa.Ni kijiji cha wakulima,wafanya biashara ndogondogo pamoja na wafugaji.Wafanyakazi wa serikali kama sisi tupo, lakina idadi yetu ni ndogo sana.Sijawahi kufanya tathmini ya kina lakini,sidhani kama pamoja na taasisi kama sita hivi zilizopo, idadi yetu inafika hata asilimia moja ya wakazi wote.Hali ya wafugaji na wafanyakazi kwa kimaisha kwa ujumla inaonekana kidogo ahueni.Wakazi wa hapa walio wengi ni maskini sana,maisha kwa kweli ni ya kuunga unga tu.Siku moja nilimtembelea jirani yangu ambaye naye kama wengine hali yake kimaisha anaijua mwenyewe.Nyumbani kwake nilimkuta mjomba wake ambaye yuko mwaka wa pili kwenye chuo elimu cha Muhonda,nadhani chuo hiki kipo wilaya ya Mvomero.Alikuwa ametokea Morogoro,na kwa kumtazama alionekana kukukosa matumaini.Kawaida yangu ninapo ona hali ya namna hii, huwa nauliza kunani.Nilipomuuliza kwa nini alionekana kuwa na majonzi sana, aliniambia walikuwa wamefukuzwa chuoni kwa vile wengi wao hawakuwa na vyeti vya kuzaliwa sasa apokwenda Morogoro aliambiwa anatakiwa kulipa Sh.40,000 kwa ajili ya cheti hicho na kwa vile mzazi wake ni maskini,na ndio tu amempa hela za kulipa chuoni kwa ajili ya ada, haoni uwezekano wa kupata fedha hizo kwa sasa.Na kwa vile mkuu wa chuo amewaambia wasipopata vyeti vya kuzaliwa wajihesabu kama wamejifukuza wenyewe chuo,anaona ndoto yake ya kuwa angalau kuwa na na maisha bora kidogo imefika ukingoni.Nilijisikia kama mwili wangu umetiwa maji kwa maneno yale.Mfukoni mwangu nilikuwa na Sh.60,000.Nilimpa Sh.40,000 nikabaki na Sh.20,000!Aliniangalia kwa macho ya mshangao na furaha,mara akaja akanikumbatia,huku akitoa machozi.Niliona kama mbingu zimefunguka.Kisa hiki kinaonyesha jinsi gani jamii yetu isivyo na huruma.Jamii inayofanya maamuzi ya zima moto,ambayo mengi ukiyaangalia ni ya kifisadi tu.Nilijiuliza,hivi vijana hawa kutokuwa na vyeti vya kuzaliwa ni kosa lao?Hivi kweli walistahili kufukuzwa chuo?Hivi tuamini kwamba hata kama kweli vyeti vya kuzaliwa ni vya lazima kiasi hicho, hapakuwa na njia mbadala ya kufanikisha adhma hiyo,isipokuwa kufukuzwa chuo?Maswali ni mengi ambayo nina hakika hayawezi kutolewa majibu sahihi.Na ninaamini tatizo hili halikuishia Muhonda tu,liko sehemu nyingi hapa nchini.Nimesikia katika vipindi vyao RITA wakisema zoezi hili ni la nchi nzima,na litakumba hata shule za msingi .Sina ubishi katika hilo.Tatizo langu liko katika matatizo ambayo wananchi wanapata.Kama ambavyo nimeshagusia hapo awali,wananchi wetu walio wengi ni maskini wa kutupwa.Uwezo wa kuandikisha wanafamilia wote hata kwa awamu,kama RITA wanavyoshauri ni mdogo sana ukizingatia gharama zilizopo sasa.Wananchi wanavyo ona ni kwamba, huu ni mradi wa serikali, tena wa wajanja wachache,lakini haupo kwenye nia hasa ya kusaidia wananchi.Kwa nini uandaliwaji wake uwe wa hovyo kiasi hiki?Kama kweli serikali ina nia ya kusaidia wananchi,na vyeti hivi ni kwa faida ya wananchi, basi kiwango cha kuandikisha vizazi kiwe ambacho kila mwanachi anaweza kumudu,vinginevyo wananchi wataona kwamba mradi huu upo kwa nia ya kuwaibia tu.Isitoshe ni nani mwananchi wa kawaida anaweza kutoka kijijini kwake aende wilayani kwenda kusajili kizazi, hasa ikizingatiwa kwamba kazi sio ya siku moja, kwa hiyo inahitaji fedha nyingi?Napenda kumalizia kwa kusema kwamba, nia ya RITA sio mbaya,lakini utendaji wake unahitaji uboreshaji wa hali ya juu.Vinginevyo RITA wataonekana kama ni wababaishaji,wanyanyasaji na wanyang'anyi tu wanaotaka kuwakomoa wananchi.Nashauri kila mbinu zitumike ili huduma zipelekwe karibu na wananchi, ikiwezekana hata kuwa na "mobile services."
   
 2. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #2
  Jan 29, 2009
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mimi ni mkazi wa mkoa wa Morogoro,na makazi yangu yapo kwenye kijiji kiitwacho Dakawa.Ni kijiji cha wakulima,wafanya biashara ndogondogo pamoja na wafugani.Wafanyakazi wa serikali kama sisi tupo, lakina idadi yetu ni ndogo sana.Sijawahi kufanya tathmini ya kina lakini,sidhani kama pamoja na taasisi kama sita hivi zilizopo hapa, idadi yetu inafika hata asilimia moja ya wakazi wote.Hali ya wafugaji na wafanyakazi kwa kimaisha kwa ujumla inaonekana kidogo ahueni.Wakazi wa hapa walio wengi ni maskini sana,maisha kwa kweli ni ya kuunga unga tu.Siku moja nilimtembelea jirani yangu ambaye naye kama wengine hali yake kimaisha anaijua mwenyewe.Nyumbani kwake nilimkuta mjomba wake ambaye yuko mwaka wa pili kwenye chuo elimu cha Muhonda,nadhani chuo hiki kipo hapa hapa wilaya ya Mvomero.Alikuwa ametokea Morogoro,na kwa kumtazama alionekana alikuwa anaonekana kukukosa matumaini.Kawaida yangu ninapo ona hali ya namna hii, huwa nauliza kunani.Nilipomuuliza kwa nini alionekana kuwa na majonzi sana, aliniambia walikuwa wamefukuzwa chuoni kwa vile wengi wao hawakuwa na vyeti vya kuzaliwa.Alisema anatakiwa kulipa Sh.40,000 kwa ajili ya cheti hicho na kwa vile mzazi wake ni maskini,na ndio tu amempa hela za kulipa chuoni kwa ajili ya ada, haoni uwezekano wa kupata fedha hizo kwa sasa.Na kwa vile mkuu wa chuo amewaambia wasipopata vyeti vya kuzaliwa wajihesabu kama wamejifukuza wenyewe chuo,anaona ndoto yake ya kuwa angalau kuwa na na maisha bora imefika ukingoni.Nilijisikia kama mwili wangu umetiwa maji kwa maneno yale.Mfukoni nilikuwa na Sh.60,000.Nilimpa Sh.40,000 nikabaki na Sh.20,000!Aliniangalia kwa jicho la mshangao,mara akaja akanikumbatia,huku akitoa machozi.Niliona kama mbingu zimefunguka.Kisa hiki kinaonyesha jinsi gani jamii yetu isivyo na huruma.Jamii inayofanya maamuzi ya zima moto,ambayo mengi ukiyaangalia ni ya kifisadi tu.Nilijiuliza,hivi vijana hawa kutokuwa na vyeti vya kuzaliwa ni kosa lao?Hivi kweli walistahili kufukuzwa chuo?Hivi tuamini kwamba hata kama kweli vyeti vya kuzaliwa ni vya lazima kiasi hicho, hapakuwa na njia mbadala ya kufanikisha adhma hiyo,isipokuwa kufukuzwa chuo?Maswali ni mengi ambayo nina hakika hayawezi kutolewa majibu sahihi.Na ninaamini tatizo hili halikuishia Muhonda tu,liko sehemu nyingi hapa nchini.Nimesikia katika vipindi vyao RITA wakisema zoezi hili ni la nchi nzima .Sina ubishi katika hilo.Tatizo langu liko katika matatizo ambayo wananchi wanapata.Kama ambavyo nimeshagusia hapo awali,wananchi wetu walio wengi ni maskini wa kutupwa.Uwezo wa kuandikisha wanafamilia wote hata kwa awamu,kama RITA wanavyoshauri ni mdogo sana katika gharama zilizopo sasa.Wananchi wanavyo ona ni kwamba, huu ni mradi wa serikali, tene wa wajanja wachache,lakini haupo kwenye nia hasa ya kusaidia wananchi.Kama kweli serikali ina nia ya kusaidia wananchi,na vyeti hivi ni kwa faida ya wananchi, basi kiwango cha kuandikisha vizazi kiwe ambacho kila mwanachi anaweza kumudu,vinginevyo wananchi wataona kwamba mradi huu upo kwa nia ya kuwaibia.Isitoshe ni nani mwananchi wa kawaida anaweza kutoka kijijini kwake aende wilayani kwenda kusajili kizazi, hasa ikizingatiwa kwamba kazi sio ya siku moja, kwa sababu ya kuna foleni, kwa hiyo inahitaji fedha nyingi?Napenda kumalizia kwa kusema kwamba, nia ya RITA sio mbaya,lakini utendaji wake unataji uboreshaji wa hali ya juu.Vinginevyo RITA wataonekana kama ni wanyanyasaji na wanyang'anyi tu wanaotaka kuwa komoa wananchi.Nashauri kila mbinu zitumike ili huduma zipelekwe karibu na wananchi, ikiwezekana hata kuwa na "mobile services."
   
Loading...