Risk taking ilimcost Madenge kula wali

Sky Eclat

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2012
Posts
58,636
Reaction score
220,438
Madenge ana miaka nane na ni mtoto wa kwanza katika familia ya watoto wane, baba ni mfanyakazi katika ofisi za serikali, wanaishi katika nyumba ya kupanga.

Wazazi wamemudu kuchukua vyumba viwili. Mshahara wa baba si mkubwa ki vile, mara nyingi unaishia kulipa kodi ya nyumba, na pesa nyingine inayobaki ni nauli ya baba kwenda kazini.

Matatizo mengi ya nyumbani mama anayatatua kutokana na biashara zake ndogo ndogo. Mama anasupply maandazi kwenye migahawa kama mitatu hivi, anatengeneza pia visheti na bajia anapeleka kwenye maduka.

Mama anajitahidi sana kuhakikisha watoto wamekula mara tatu kwa siku, lakini kwa kipato chake mara nyingi anamudu kununua ndoo ya mahindi, inakobolewa na kusagwa.

Kwahiyo msosi mkubwa nyumbani ni ugali. Kwenye nyumba wanayoishi kuna familia zinazomudu kula wali mara kwa mara, jambo alilolitamani sana Madenge.

Sikumoja mama biashara zilikwenda vizuri, aliamua awatreat watoto, Madenge alipotoka shule alipewa pesa akanunue mchele gengeni, kulikua na wingu zito lakini wengi walitabiri mvua itanyesha usiku.

Madenge alikimbia gengeni, akapimiwa mchele kilo mbili, mchele uliwekwa kwenye mfuko wa karatasi, Madenge alipotoka tu gengeni matone ya mvua yalianza kunyunyuzika.

Madenge mawazo yake yote yalikua kwenye sahani ya wali mara tu mchele huu ukiiva! Aliamua kukimbia awahishe mchele, mvua ilizidi, mvufo wa karatasi ukalowana, mchele ukaanza kumwagika.

Madenge alijitahidi kuzuia mchele kwa shati lake. Alipofika nyumbani alikua Analia mchele uliobaki ulikua ujazo wa kiganja cha mkono. Mama akamuambia Madenge ungerudi gengeni ungoje mvua ipungue mwanangu.
 
Madenge alikosea sana hapo kwa akili alizonazo hakutakiwa kukosea kama hivyo
 
Madenge alikosea sana hapo kwa akili alizonazo hakutakiwa kukosea kama hivyo

Focus ya Madenge ilikua kwenye sahani ya wali tena uliopikwa nyumbani kwao!
 
Madenge kidume cha kutake risk lakini mvua ilimuahi this time.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…