Risiti Halali ya TRA, mbona wao hawatumii

chumvichumvi

JF-Expert Member
May 6, 2010
1,207
309
Wanajamvini wenzangu inashangaza sana na kustaajibisha pale mmoja wa mhimili wa serekali hafanyi au kutekeleza kile ambacho raisi wa nchi anasisitiza swala la ulipaji kodi na utolewaji wa risiti Halali za TRA.

Traffic kanda ya kaskazini haswa Arusha na Moshi wao wamekuwa wakitoza faini bila kutoa risiti na wamekuwa wakilazimisha faini ilipwe hapo hapo tofauti na hivyo uache gari. Na ikatokea ukalazimisha upewe risiti wanakuzungusha tu na ukienda ofisini wanakupa risiti ambayo sio ya TRA. Sasa hapa mi napata ugumu sana kuelewa inakuwaje traffic hawatoi risiti husika na hamna hatua yeyote wanayochukuliwa

Mwenye uelewa zaidi tafadhali naomba nipe mwanga zaidi
 
Mkuu hata mimi najiuliza kuhusu hilo hata mzani wa Arusha hawatoi risiti za efd ukiuliza sababu wanakuzungusha hawana majibu yanayoeleweka.
 
Inabidi TRA WAINGILIE kati swala hili sababu sioni umuhimu wa wao kukagua magari ambayo hayana motor vehicle kila mwezi ili hali wanaokagua nao nao niwakwepa sheria kama sio wavunjifu
 
Back
Top Bottom