RISE UP (AMKA) sehemu ya kwanza-01

Nteko1

New Member
Sep 14, 2021
0
0
RISE UP ( AMKAA) sehemu ya kwanza
***********************************
***********************************

Niliendelea kukimbia huku nikianguka na kusimama maana nilikuwa najikwaa kwenye mawe yaliyoijaza hii njia ndogo, giza nene lililotanda juu ya uso wa nchi lilikuwa ni kikwazo kikubwa katika hii safari ya kuinusuru roho yangu.
Niliendelea kuwakimbia hawa watu nisiowajua ambao walikuwa wamezifunika nyuso zao kwa vitambaa vyeusi, kwaharaka nikajibanza kwenye ukuta huku nikijiaminisha kuwa nimekwisha kuwapoteza wale watu ambao walihitaji kunidhuru.

Nikaingiza mkono mfukoni na kutoa simu kisha nikaitafuta namba ya rafiki yangu mmoja ambaye ni mkuu wa kituo cha polisi cha hapa mjini kisha nikabonyeza kitufe cha kupiga simu,lengo langu kubwa lilikuwa ni kutoa taarifa haraka juu hili jambo ili nipate msaada wa haraka kabla sijawa kwenye wakati mgumu zaidi, haikuchukua muda sana ikaanza kuita

Taratibu nikaipeleka sikioni kisha nikatazama mbele yangu, nikashituka baada ya kuwaona watu watatu wakiwa wamesimama mbele yangu, nikayakaza macho yangu ili nitazame vizuri maana giza lilinifanya nisione vizuri kile kilichokuwa mbele yangu.

Nikaona ngoja nimwilike na mwanga hafifu wa simu yangu ambayo iliendelea kuita bila kupokelewa
Mapigo ya moyo yalianza kwenda kasi baada ya kutambua kuwa hawa ndio wale watu walikuwa wakinikimbiza, nikaangalia mikononi mwao na kuona wameshikilia panga

Kabla sijazungumza chochote nilishitukia nikishikwa mikono yangu kwa nyuma na mmoja wao kisha akaanza kunifunga kwa kamba huku mwingine akiniziba mdomo kwa kutumia gundi ya karatasi, na mwingine wa tatu alinivisha kichwani kitambaa kizito Kama kofia ndefu iliyoshuka hadi shingoni na kunifunika uso wangu wote, hivyo sikuweza kuona chochote kinachoendelea.

Nilijaribu kupiga kelele lakini sikuweza kufanya hivyo maana mdomo wangu ulibanwa barabaraa na ile gundi.
Baada ya muda mfupi nilikuwa tayari ndani ya buti ya gari la hawa watu wakinipeleka nisipopajua

Hakika wakati nikiwa kwenye buti niliwaza mambo mengi nisipate majibu, kwanini hawa watu waniteke?, Ni kipi kibaya nilichokifanya mimi? ,Hayo yalikuwa baadhi ya maswali yaliyoisumbua akili yangu, taratibu nikaanza kuvuta kumbukumbu ya matukio ya nyuma ambayo huenda ndo sababu ya haya yote.

Mimi naitwa Elia Simon ni daktari wa hospitali ya taifa ya CHIGO, lakini pia ni Mwenyekiti wa vijana wa chama tawala TDP (Tonzombia Democratic Party)

Rais wangu wa nchi ya Tonzombia ambaye pia ndiye Mwenyekiti wa chama cha TDP ni rafiki yangu ambaye namchukulia kama baba yangu mzazi maana ananipenda sana na huwa ananishirikisha kwenye mambo yake mengi ya nchi, hii ni kutoka na uaminifu wangu na juhudi ambazo nimekuwa nikizionyesha kwa watu wote tangu alipokuwa mwalimu wangu wa sekondari kabla ya kuwa Rais wa nchi.

Nimekuwa nikiwahamasisha vijana wengi juu ya kuujua wajibu wao kama vijana kwenye nyanja mbalimbali za kimaendeleo kijamii na kitaifa kwa ujumla

Elimu niliyokuwa nikiitoa kwa vijana wenzangu imewasaidia kufungua fahamu zao na kuweza kupambanua mambo mengi ya ajabu yaliyokuwa yakiendelea hapa nchini.

Rais wetu alisimama katika haki lakini alipata upinzani mkubwa kwa viongozi wenzake ambao hawakuonyesha kuijali thamani wa raia wa nchi,zaidi sana walileta mijadala mipya kila kuitwapo leo ambayo haikuwa na manufaa yoyote kwa wananchi tofauti na kuwakandamiza

Mimi pamoja na vijana wenzangu hatukukubaliana kabisa na hali iliyokuwa ikiendelea hivyo tulizidisha kasi ya kuhamasishana tukihitaji kuleta mabadiliko hapa nchi ,

Tulihitaji kusimama kwa ajili ya kuwatetea wanyonge ambao sauti zao zilikuwa kama kelele mbele za viongozi wetu.
Sisi vijana ndio nguzo ya taifa la leo na kesho, kijana asiposimama,basi taifa kusimama ni ndoto
Je nikae kimya wakati nauona mwisho wa taifa langu kuwa ni mbaya kuliko mwanzo wake?
Hapana lazima tusimame sisi kama vijana kuipigania haki yetu na haki ya wananchi.
Wazee wetu watapataje haki zao za msingi Kama tusiposimama sisi vijana kuwatetea?
Watoto wetu watatimizaje ndoto zao kama tusiposimama sisi vijana na kuwatetea?
Jamii zetu zitapataje huduma bora za afya kama tusiposimama sisi vijana kuwatetea?
Je nguvu yetu kama vijana iko wapi leo?

"Huu ni wakati wa kusimama sisi Kama vijana na kuuthibitishia ulimwengu kuwa tunayonguvu na uwezo mkubwa wa kuleta mabadiliko ya kweli kwa ajili ya watoto wetu,wazee wetu pamoja na mali zetu zote.
Tuzitumie rasilimali zetu kwa ajili yetu sisi wenyewe"

Hayo ni baadhi ya mambo ambayo tumekuwa tukihamasishana sisi kama vijana wa nchi ya Tonzombia siku za nyuma kabla ya hili tukio la kutekwa kutokea,

Kwa haraka akili yangu ikanituma kuwa huenda hii ndio sababu kubwa ya haya yote kutokea.
Nikamkumbuka mama yangu kipenzi ambaye ndiye mzazi wangu pekee niliyebakiwa naye, je nitamwacha mama katika mazingira gani kama hawa watu wakinidhuru?

Nilijiuliza sana juu ya hili jambo huku nikiendelea kuvuta vumbi zito ambalo liliingia kwenye buti kwa kasi ,taratibu nikaanza kukosa hewa maana nilikuwa nimefunikiwa kitambaa kuzito sehemu yote ya kichwa huku mdomo wangu ukiwa umefungwa kwa gundi ya karatasi na kunifanya nishindwe kupumua kabisa.

Nilianza kuishiwa nguvu huku nikikiona kifo changu kikiwa mbele yangu, je Kama nikifa leo nchi yangu ya Tonzombia nitaiacha katika hali gani?,Je ni Nani atakae simama kutetea wanyonge ambao kadri siku zinavyozidi kwenda ndivyo wanavyozidi kunyanyaswa?.

Niliwaza sana huku nikikosa hewa kabisa na baada ya muda mfupi sikujua chochote kinachoendelea.
***********************************
Taratibu nikaanza kufumbua macho baada ya kumwagiwa maji ya baridi sana usoni, hakika macho yalikuwa mazito sana,nikajaribu kuisogeza mikono pamoja na miguu yangu nikashindwa kabisa,ikanibidi nijitahidi hivyo hivyo kufumbua macho ili niweze kuona kile kinachonizuia nisiweze kusogeza miguu pamoja na mikono yangu, nilishangaa kuona miguu pamoja na mikono yangu ikiwa imefungwa kamba kwenye kiti. Nikanyanyua kichwa changu ili kutazama ni nani aliyekuwa amesimama mbele yangu maana nilihisi uwepo wa mtu mbele yangu
Nilipata mshituko mkubwa,huku nisiamini kile nilichokiona mbele yangu...

ITAENDELEA...(kesho)
Je Elia aliona nini mbele yake?
Na je, kwanini ametekwa?

Je atafanikiwa kutoka salama au ndo mwisho wake?

Usikose kufuatilia simulizi hii,utajifunza mambo mengi ya kisiasa kupitia mkasa huu wa kijana Elia ambaye anapambana kwa ajili ya kuitetea haki ya wanyonge
 
Hadithi zinazoishia njiani
 
Back
Top Bottom