Sababu za watu wengi kuacha kupiga pasi ukuta na hatimae kupiga kibao tu
1. Ukuta ukiupiga pasi ukiwa hauja kauka unatengeneza mabonde nahata ukikauka ukitaka kupiga pasi utatumia nguvu nyingi kupiga pasi nayo pia itatengeneza mabonde kwenye ukuta maana utakua unakandamiza pasi
2. Hii inasemekana fundi rangi akija kufanya skimming haishikani vizuri na ukuta sababu ukuta unateleza kama kioo hatimae huko mbeleni rangi pamoja na skimming hubanduka kwenye huo ukuta
Plasta nzuri ni ile inayo wekwa timanzi alafu pia uwe na lati nzuri ya aluminum epuka fundi anaefanya kazi kubwa kwa siku ili amalize haraka achukue hela aondoke atalipua hiyo kazi
Ili ukuta usiwe na mabonde mabonde baada ya kupiga kibao ukamaliza chukua lati jikague kuangalia makosa kabla ukuta hauja kauka kama kuna sehemu haiko sawa irekebishe kwa kuikwangua na lati alafu nyunyiza maji kidogo piga kibao hiyo kazi itakuwa safi