Ripoti ya utekelzaji wa mikataba ya taaisi za umma huwa haifiki kwenye kikao cha baraza la mawaziri?

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
48,684
149,887
Hivi taasisi za umma zikishaingia mikataba mikubwa, mikataba hiyo na ripoti za utekelezaji wake huwa hazifikishwi kwenye baraza la mawaziri?

1.Kama hazifikishwi,je hili si kosa?

2. Na litakuwa ni kosa la nani kama sio watunga sheria/sera wa nchii hii?

3.Kama zinafikishwa na kupata baraka za baraza la mawaziri,kwanini baraza nalo lisiwajibike?

4.Hakuna Mawaziri/Makatibu Wakuu ambao husaini mikataba ya aina hii?

5.Kama baadhi ya mikataba huwa hawasaini, je,hata nakala huwa hawapelekewi?

6.Kama wanapelekewa,hawawajibika kufuatilia utekelezaji wa mikataba hii?

5.Hivi katika awamu hii kweli tumeamua kabisa kuchora mstari kati ya watumishi wa umma na wanasiasa linapokuja swala la watu kuwajibika?
 
Mkuu nchi ya ccm, waliokuwa wanaila nchi hii ni ccm, hapa kinachofanyika ni kuwahadaa watanzania kuwa ccm ni safi kumbe ni ileile, kinachotakiwa katiba ya warioba baada ya hapo buruza mahakamani viongozi wote wakuu wa serikali wastaafu na waliopo serikalini, hivi vinavyoitwa vijipu ni vile vilivyopo kwa wanyonge wasio na C/O ya wakubwa.
 
Wenye akili fupi wanapiga makofi bila hata kutafakari na kujiuliza!!
 
Wenye akili fupi wanapiga makofi bila hata kutafakari na kujiuliza!!
Na muhusika amejua wengi akili zao ni fupi ndio maana akiona hazungumziwi anazua jambo mradi watu wamuone wamchekee na kumpungia mikono. eg. kwenda CRDB kwa style ile ilikuwa ina umuhimu?
 
Inaelekea hujui mengi.
Zipo sheria zilizounda mashirika/makampuni na wakala wa serikali.
Zilipitishwa na wabunge wakiwemo mawaziri.
Humo ipo miundo ya taasisi kuanzia bodi mpaka menejimenti iweje.
Raisi anateua mwenyekiti wa bodi na waziri anateua wajumbe wa bodi.
Baadhi ya wakuu wa hizi taasisi ama wanateuliwa na Raisi au bodi ya wakurugenzi.
Menejimenti na bodi zina mamlaka kamili na wakati mwingi mwenyekiti wa bodi anashauriana na waziri au wizara husika kabla ya kufanya maamuzi kwenye vikao.
Pia yupo msimamizi anayeitwa msajili wa Hazina.
Nadhani hata hao waopima kila jambo ki ccm au ki ukawa watakuwa wamenipata.
 
Hakuna instrument iliyoundwa kuendesha baraza la mawaziri katika serikali hii ya awamu ya tano.
Kwa muktadha huo mpaka sasa hakuna waziri rasmi zaidi ya Pombe na Samia.
Sasa Pombe na Samia kama mawaziri pekee watapitia utekelezaji wa kila mkataba Saa ngapi?
 
Mawaziri hewa?!!!!
 
Back
Top Bottom