Ripoti ya soko la mikopo ya nyumba 2015.

DarProperty Tz

Senior Member
Apr 24, 2011
168
29
Tanzania Mortgage Refinance (TMRC) imetoa ripoti ya soko la mikopo ya nyumba Tanzania kwa mwaka 2015.

Ufuatao ni muktasari wa ripoti ya TMRC;

Soko la mikopo ya nyumba limeandikisha ukuaji mdogo wa 1% tu katika robo ya nne mwaka 2015. (Robo ya tatu ya 2015 ukuaji ulifikia 6.7%) Mlinganisho wa mwaka kwa mwaka ulishuhudia ukuaji wa 45% kwa miezi 12 iliyopita mpaka 31/12/2015. Kiwango cha ukuaji kimeshuka kutoka 59% mwaka 2014.

Wakopeshaji wa mikopo ya nyumba wamefikia 26 mpaka mwishoni mwa 2015. Tumeshuhudia wakopeshaji wapya wanne wakiingia sokoni katika robo ya nne ya mwaka 2015 (robo ya tatu ya mwaka 2015 walikuwa wakopeshaji 22). Wakopeshaji wapya ni NBC, Amana Bank, Peoples Bank of Zanzibar na Commercial Bank of China.

Kiwango cha mkopo mpaka 31/12/2015 kilifikia TZS 359 billioni sawa na USD 166.5 millioni (kimeongezeka kutoka TZS 248 bilioni manamo 31/12/2015)

Wastani wa mikopo ya nyumba ilifikia TZS 106 milioni, inakaribia USD 49,112.35 (imeongezeka kutoka TZS 69 milioni mwaka 2014)

Asilimia 64 ya mikopo ya nyumba iliyotolewa mwaka 2015 imetolewa na wakopeshaji wakubwa wanne .

Kiwango kikubwa cha riba na kukosekana kwa nyumba za bei nafuu bado ni kikwazo kikubwa katika ukuaji wa soko la mikopo nchini.

Soma ropoti kamili bofya; http://www.darproperty.co.tz/downloads/TANZANIA MORTGAGE MARKET UPDATE 2015.pdf
 
Kiwango kikubwa cha riba kinatokana na inflation. Sidhani kama mtu ukikopa in terms of Dollars utalipa riba kubwa...
 
Back
Top Bottom