Ripoti ya sensa ya kilimo na mifugo yatoka | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ripoti ya sensa ya kilimo na mifugo yatoka

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by JOHN KITABI, May 28, 2012.

 1. J

  JOHN KITABI Member

  #1
  May 28, 2012
  Joined: Nov 10, 2007
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hatimae Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) imetoa ripoti ya Sensa ya kilimo na mifugo (gonga hapa),
  Kwa muda mrefu sasa ofisi hii imekuwa katika malumbano makubwa na vyombo vya habari kuhusiana na sensa ya kilimo na mifugo kwa kile ambacho kimekuwa kikionekana kama ufujaji wa fedha ambao ulifanywa na Uongozi wa ofisi hii hadi kushindwa kutoa ripoti hii.
  Mara ya mwisho sensa ya kilimo na mifugo ilifanyika mwaka 2002/2003. Na hivyo sensa hii ilipaswa ifanyike mwaka 2007/2008. Lakini cha ajabu sensa hii haikufanyika na ikafanyika mwaka 2009. Ripoti ambazo zimetoka zinaonyesha kuwa sensa hii imefanyika mwaka 2007/2008 kitu ambacho sio kweli!.
  Kuna uwezekano mkubwa Ofisi ya Taifa ya Takwimu ikaingia kwenye kashfa nyingine kwa udanganyifu huu. Pamoja na hayo kwa matukio kama haya inakuwa inaiongoza vibaya serikanli kufanya mipango yake. Na hii inaonyesha dhahiri kuwa Takwimu zinazotoka kwenye ofisi hii zina uwalakini mkubwa. Kwa mfano imekuwa ikionekana kuwa mfumuko wa bei wamekuwa wakiurekebisha tofauti na hali halisi ilivyo. Inasadikika kuwa hii ni kutokana na maelekezo ofisi hii inayopewa toka ikulu ili kutokuufanya mfumko wa bei kuonekana uko juu.

   
 2. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #2
  May 28, 2012
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,223
  Likes Received: 1,412
  Trophy Points: 280
  Ikulu tena?, inapika mambo yafuatayo: Mfumuko wa bei?!, kuwaandalia watu kesi za ufisadi?!, kudhibiti upinzani ndani na nje ya bunge.
   
 3. r

  rodrick alexander JF-Expert Member

  #3
  May 28, 2012
  Joined: Feb 12, 2012
  Messages: 4,109
  Likes Received: 1,499
  Trophy Points: 280
  kuna mtu alitoa post ya namna maliasili zetu zinavyoliwa na wajanja alionyesha wakati takwimu za Taifa zinaonyesha Tanzania iliuza cubic meter za magogo 19,000 nje ya nchi Takwimu halisi za China zinaonyesha magogo zaidi ya mara tano ya idadi iliyotajwa yaliingia toka Tanzanaia hii inaonyesha jinsi gani wasivyo makini kwani tofauti iliyopo ni kubwa mno kwa sababu kuna watu wa It walioandaliwa kutoa majibu ya kumtetea Boss wao naomba watupe takwimu halisi za magogo yaliyouzwa nje ya nche na hasa China
   
 4. Bamukunda

  Bamukunda JF-Expert Member

  #4
  May 29, 2012
  Joined: Jul 3, 2011
  Messages: 401
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  John Kitabi umeandika:
  Mara ya mwisho sensa ya kilimo na mifugo ilifanyika mwaka 2002/2003. Na hivyo sensa hii ilipaswa ifanyike mwaka 2007/2008. Lakini cha ajabu sensa hii haikufanyika na ikafanyika mwaka 2009. Ripoti ambazo zimetoka zinaonyesha kuwa sensa hii imefanyika mwaka 2007/2008 kitu ambacho sio kweli!

  Jibu:
  Ni vyema ukafahamishwa kuwa sensa inayohusu mifugo ni tofauti na sensa inayohusu binadamu. Katika sensa za wanyama ukusanyaji wa takwimu huwa unafanyika mwaka mmoja baada ya 'reference period'. Kama ukidodosa zaidi utajua ukweli kuwa sensa ya mwaka 2002/2003 ilifanyika mwaka 2004. Hivyo mwaka wa ukusanyaji na reference period huwa ni tofauti.
   
 5. Bamukunda

  Bamukunda JF-Expert Member

  #5
  May 29, 2012
  Joined: Jul 3, 2011
  Messages: 401
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  kwa ufahamisho zaidi, fungua ripoti inayoitwa:-

  [h=2]Technical_And_Operation_Report - Census of Agriculture 2007/2008 [/h]ukurasa wa 8 imeandikwa:
  2.8 Data Collection
  Data collection activities for the 2007/08 Agricultural Sample Census lasted for three months from June to August, 2009.

  Kwa hiyo si kweli kuwa wamedanganya umma!!!!!!!
   
Loading...