Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,684
- 149,887
Ukisoma hii ripoti utagundua kuwa imekosa kugusuia mambo machache ya muhimu na ambayo yangeweza kabisa kupunguza mshituko wa watu uliotokana na taarifa hiyo na pia kuwapunguzia lawama wawakezaji.
Sijui ni kwa bahati mbaya au makusudi,ripoti hii imejikita zaidi katika kueleza viwango tofauti vya wingi wa madini unaotokana na uchunguzi wao na data za TMAA bila kugusia maswala ya gharama za uzalishaji,mrabaha tunaostahili kupata,n.k bali wao walilenga kueleza kiasi cha madini na gharama zake tu.
Pamoja na kuonyesha uwepo wa tofauti kubwa ya kiasi cha madini kilichopo katika makontena ukilinganisha na data za TMAA,tofauti inayopelekea kuonekana kuwa fedha nyingi zinapotea,kamati ilipaswa pia kuwasiliana na kampuni ya ACASIA na wadau wengine ili kujua ni gharama kiasi gani kampuni hiyo inatumia kuchimba madini hayo,kuuhifidha mchanga huo,kuusifirisha pamoja na gharama za uchenguaji wa huo mchanga nje ya nchi.
Kwa mtazano wangu, gharama hizi zilipaswa kutajwa/kuonekana katika ripoti ile unless mrabaha tunaolipwa haujali gharama hizo za uzalishaji bali unaangalia tu thamani halisi ya madini tu kama kamati ambavyo ripoti ya kamati inavyojaribu kutuonyesha /kutujengea picha.
Na kama mrabaha wa asilimia 4 wanaotulipa haujali gharama ya uzalishaji basi hapa inabidi tujiulize ilikuwaje wakakubali jambo kama hili kama kweli hamna namna wanavyotuibia kurudisha gharama zao na pengine kutengeneza faida zaidi unless huu ndio utaratibu uliopo dununiani kote katika kukokotoa hiyo mirahaba
Naamini ukichukua gharama halisi ya madini hayo ukatoa gharama za uchimbaji,uhifadhi,usafirishaji na gharama ya uchenguaji na kisha ndio ukaweka asilimia ya mrabaha tunayostahili kuwatoza,hasara tunayopata isingefika kiasi kile kilichotamkwa na kusababisha mshutuko mkubwa kwa watu.
Pia nimeshindwa kuelewa ni kwanini ripoti haikutamka wazi kuwa baadhi ya madini ambayo hatupati chochote msingi wake ni mkatataba tulioingia sisi wenyewe.
Yaani wameorodhesha aina ya madini hayo na viwango vyake vilivyopo katika mchanga na fedha tunazopoteza bila kufafanua kuwa kwa mujibu wa mkataba sisi hatuna chetu katika madini hayo(sijui walikua wanafichi nini na kwa faida ya nani)
Hata hivyo, tatizo hapa huenda linatokana na wao kutoa summary tu hivo kupelekea taarifa zingine muhimu tusizipate kulingana na uchunguzi wao.
NB:Kuhusu viwango vya madini vinavyopatika katika huo mchanga kulingana na findings za kamati ,binafsi sitaki kuzipinga wala kuzikubali mpaka pale uchunguzi huru utakapofanyika.