Ripoti ya pili ya mchanga itamuacha uchi Tundu Lissu

Beira Boy

JF-Expert Member
Aug 7, 2016
18,716
28,623
Amani ya bwana iwe nanyi wakubwa wa jukwaa hili kina iparamasa na wengineo

Ni ukweli usioacha shaka kuwa sasa ile kampuni ya kinyonyaji ya ACACIA wameanza kutapa tapa yaani hawajielewi, kila siku wanakuja na matamko mapya hiyo yote ni baada ya mbinu yao ya kumuhonga rais kukwama, na kukimbilia kwenda kumuhonga Tundu Lissu

Kamati ya pili iliyoundwa kuja na suluhisho kamili ambayo itakabidhi riport yake hapo week ijayo kwa ngosha inaenda kumuacha uchi bila taulo Tundu Lissu na genge lake la kutetea mafisadi na wakwepa kodi wa ACACIA.

Unafiki wa Lissu kujulikana hapo wiki ijayo

Nawasilisha karibuni
 
Maisha vile yalivyo magumu sasa hivi hapa Tanzania mtu anakuonyesha dhahiri kwamba anachukia kma vile mtoa Post
 
Kuandika tu maneno ya lugha unayozungumza kila siku ya Kiswahili, haujui! itakuwa ya mambo haya yanayohitaji akili kubwa kuyajadili. Kwa kuonesha wewe usivyo makini, na usivyo mtu wa kutafakari, tayari umeshakuwa brain washed kwamba, kuna watu walitaka kumhonga huyo uliyemtaja; nina hakika haujui ni kiasi gani inachosemekana kuhongwa huyo uliyemtaja.

Kama umesahau ama haujui, inasemekana ilikuwa ahongwe bilioni 300/-. Sasa, kama kweli ilikuwa ahongwe hizo bilioni 300/- na akashindwa kuchukua hatua dhidi ya hao watu, na ameendelea kukaa kimya hadi dakika hii, basi ni tatizo. Ningeshauri, ubaki kuwa observer tu wa haya mambo instead of involving in it, for, you may become a figure of fun.
 
Nadhani watu hawajamuelewa Lissu. siyo kwamba anawatetea acacia. Lissu amesimama kwenye mikataba zaidi. Kuzuia mchanga bila kudeal na mikataba haitatusaidia sana na mfano mzuri ni sakata la IPTL na yule mhindi sethi. Tena siku hizi hasikiki kabisa baada ya kuchota ile mihela na TANESCO wameachwa solemba.

Ile benki iliyowakopesha IPTL hela za kuinvest hapa kwetu inaidai TANESCO walipe hilo deni wakati TANESCO hela walishazipeleka benki kuu kwenye ESCROW account (zisitumike hadi hapo utata wa capacity charges utakapopata ufumbuzi), na wajanja wakazichota.

Lissu kasimamia mikataba zaidi. Tatizo la Lissu ni jinsi anavyowasilisha hiyo mada yake kwa hasira etc na inaonekana kama yuko upande wa acacia. Kwanza suala hili la wizi wa madini halijaanza leo. Wapinzani wamepiga kelele sana kuhusu ubovu wa mikataba inayosababisha tuibiwe. Wabunge wa upande mwingine waliwabeza na kukejeli sana.

Leo wanajifanya kushituka kuwa tunaibiwa na wanawakebehi waliolianzisha suala hili miaka mingi sana juu ya ubovu wa mikataba inayosababisha tuibiwe. Leo walioandaa hiyo mikataba tunawaona wazuri na walioipigia kelele tunawaona wezi (na wanendelea kuipigia kelele) .
 
Huyo Lissu ndiyo alisaini Mikataba na Sheria Mbovu za madini??Nadhani ulitaka kusema akina Kalemani waliotayarisha hiyo mikataba wakiwa State Attorneys na baada ya kusainisha mikataba mibovu na sheria mbovu wakapewa vyeo ndani ya makampuni hayo pamoja na shares??

Kama kweli wazalendo kwanini mumuondoa MUHONGO ambaye hahusiki hata kidogo mkamuacha Kalemani aliyekuwa State Attorney ndani ya Wizara anayoiongoza leo??

Kuwa MZALENDO si kupiga makofi,mmeambiwa tufuate njia sahihi kuvunja mikataba siyo kukurupuka
 
Sasa Ripoti Kakabidhiwa Ama Wewe Ni Mwanakamati Ile
Maana Inaonekana Kilichomo Ndani Unakijua
 
Back
Top Bottom