Ripoti ya mauaji ya mwandishi Mwangosi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ripoti ya mauaji ya mwandishi Mwangosi

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Shuju, Sep 9, 2012.

 1. S

  Shuju Member

  #1
  Sep 9, 2012
  Joined: Jun 22, 2012
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Wadau kipindi cha kuelezea kifo cha mwandishi wa channel ten kinatarajiwa kuonyeshwa mlimani tv j3 kuanzia saa 2.30 usiku usikose,naomba kuwasilisha.
   
 2. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #2
  Sep 10, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  kwa tulio madongo kuinama tunaomba juhudi za kipekee tuweze kupata clip mapema kwenye mtandao
   
 3. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #3
  Sep 10, 2012
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ile ya Ch 10 imeyoyo hatukuiona. Huku Ar hakuna Mlimani TV.
   
 4. Gele vaheke

  Gele vaheke Senior Member

  #4
  Sep 10, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mlimba kilombero hakuna mlimani tv
   
 5. Gele vaheke

  Gele vaheke Senior Member

  #5
  Sep 10, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mlimba kilombero hakuna mlimani tv
   
 6. zukuboy

  zukuboy Member

  #6
  Sep 10, 2012
  Joined: Aug 26, 2009
  Messages: 25
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 5
  Hope itaeleweka
   
 7. Mzee wa ngano

  Mzee wa ngano Senior Member

  #7
  Sep 13, 2012
  Joined: May 3, 2012
  Messages: 179
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mimi sijawahi kusikia kitu kinaitwa mlimani TV hebu waambie hao jamaa zako wakanunue airtime TBC ili tz yote tuone. Hiyo mlimani TV hata Nyololo sidhani kama inaonekana.
   
 8. j

  jaje Member

  #8
  Sep 15, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 10
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  cc wa huku kishumundu hamna mliman tv
   
 9. King'asti

  King'asti JF-Expert Member

  #9
  Sep 15, 2012
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 27,507
  Likes Received: 2,248
  Trophy Points: 280
  Asante kwa kutujuza
   
 10. J

  Julius Kahangwa New Member

  #10
  Sep 16, 2012
  Joined: Jun 22, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwakeli hii Mlimani TV inapatikana DAR tu.Rusheni kupitia ITV au KWA MUHANDO.
   
 11. T

  Toshack Kibala Member

  #11
  Sep 16, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jaribuni kuangalia namna nyingine ya kutuwezesha na sie tusio ipata mlimani tv tupate taarifa kwa wakati.
   
 12. S

  Swamidu kakome Member

  #12
  Sep 18, 2012
  Joined: Sep 11, 2012
  Messages: 11
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ww ndugu yangu TBC hawawezi kuonyesha kipindi kama hiki hujui yaliyomkuta TIDO
   
 13. kiplagati26

  kiplagati26 JF-Expert Member

  #13
  Sep 22, 2012
  Joined: Jul 24, 2012
  Messages: 277
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 35
  Mm hk makao makuu ya afrc mashariki sitakipata salamu mkuu tulushie clips hapa javini.
   
 14. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #14
  Sep 22, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  Huko mlimani TV anakotokea benson Bana?
  Kama amehushwa kwa namna yoyote tutegemee maudhi kupindukia.
   
 15. Arushaone

  Arushaone JF-Expert Member

  #15
  Sep 24, 2012
  Joined: Mar 31, 2012
  Messages: 14,357
  Likes Received: 616
  Trophy Points: 280
  Angalieni YouTube - Broadcast Yourself. then andika VURUGU ILIVYOANYA NYORORO. Kumbuka panaitwa NYOLOLO na siyo NYORORO lakini wameandika hivyo.
   
 16. W

  Wakwe2 Member

  #16
  Sep 28, 2012
  Joined: Sep 28, 2012
  Messages: 91
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  kwa sisi tuliopo mabondeni city mfanye mchakato na sisi tuweze kupata nyiuzi na kwa nini mtumie tv ambayo iko limitedi kwenye kavareji
   
 17. b

  bagwell Senior Member

  #17
  Oct 2, 2012
  Joined: Sep 19, 2012
  Messages: 113
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ripoti ya uchunguzi wa mauaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari mwakilishi wa kituo cha televisheni ya Channel Ten, mkoani Iringa, marehemu Daudi Mwangosi, uliofanywa na timu ya waandishi wa habari watatu kutoka Baraza la Habari (MCT) na Jukwaa la Wahariri Tanzania (TEF), itawekwa hadharani Oktoba 9, mwaka huu.

  Azma hiyo ilitangazwa jana Katibu Mtendaji wa MCT, Kajubi Mukajanga, baada ya timu hiyo kukamilisha uchunguzi wake hivi karibuni.

  Mukajanga alitangaza azma hiyo alipotakiwa na NIPASHE kueleza lini ripoti hiyo itatangazwa.

  Akijibu swali hilo kwa njia ya maandishi, Mukajanga alisema kwa kifupi: “Jumanne Oktoba 9, 2012 Inshallah.”

  Awali, NIPASHE ilizungumza na Katibu Mtendaji wa TEF, Neville Meena, ambaye alisema uchunguzi wa timu hiyo umeshakamilika na kwamba, ripoti yake imekabidhiwa kwa Bodi ya MCT.

  Timu ya waandishi hao iliyoundwa Septemba 4, mwaka huu, iliongozwa na Meneja wa Utafiti na Machapisho wa MCT, John Mirenyi, wajumbe wakiwa ni Mhariri wa masuala ya siasa wa gazeti la Mwananchi, Hawra Shamte na Mkufunzi wa Chuo Kikuu cha Tumaini, Kitivo cha Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma, Simon Berege.

  Timu hiyo ilipewa siku nane na ilianza kazi yake Septemba 6, mwaka huu, kubaini ukweli wa tukio hilo na kuweka kumbukumbu sahihi ya tukio hilo.

  Wakati huo huo, Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini, Advera Senso, alikataa kuzungumzia timu ya jeshi hilo iliyoongozwa na Mkuu wake, Inspekta Jenerali (IGP), Said Mwema, umekwisha au nini kinaendelea, akisema hawaruhusiwi kufanya hivyo kwa kuwa liko mahakamani kisheria.

  “…Waziri wa Mambo ya Ndani alishalisemea,” alisema Senso.

  Mwangosi, ambaye alikuwa pia Mwenyekiti wa Klabu ya Waandishi wa Habari mkoani humo (IPC), aliuawa kwa kupigwa na bomu lililosambaratisha mwili wake wakati polisi wakiwatawanya wafuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kuwazuia kufungua tawi la chama hicho, katika Kijiji cha Nyololo, Wilaya ya Mufindi, mkoani humo, Septemba 3, mwaka huu.

  Tayari askari polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), mwenye namba G2573, Pasificus Cleophace Simon (23), amefikishwa mahakamani akituhumiwa kwa mauaji ya Mwangosi.
   
 18. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #18
  Oct 2, 2012
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,294
  Likes Received: 22,072
  Trophy Points: 280
  Hizi ni stori tu, zamani zilikuwa zikiandikwa kwenye khanga, lakini sasa hata kwenye ma tshirt na madaladala zinaandikwa kila siku na hakuna kipya kinachotokea.
  Hivi ziko wapi ripoti za mabomu ya Mbagala na Gongo la Mboto?
   
 19. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #19
  Oct 2, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,799
  Trophy Points: 280
  Ripoti imekamilika na imekabidhiwa, inakaa ofisini kwa zaidi ya siku tano kabla ya kutangazwa, Pasco tuambie mmeshanunuliwa?
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 20. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #20
  Oct 2, 2012
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Do you expect something different!?
   
Loading...