Ni ripoti nyepesi mno.
Haikidhi kwa vigezo vyovyote uzito wa tukio na kilichomo katika taarifa, sana sana inaonyesha kiwango cha uandishi wa kuripoti badala ya kuhoji na kupata undani wa tukio. Baadhi ya mapungufu nilioyaona katika taarifa hii kwa muda mfupi wa kuipitia ni haya yafuatayo:-
1. Ripoti badala ya kujielekeza katika kiini cha tatizo inatoa taarifa na maelezo yale yale ambayo tayari yanafahamika. Hakuna uchunguzi wa kina kubaini chanzo, tukio lilivyokuwa, vielezo vya ushahidi?
2.Hadidu za rejea ni nyepesi mno na hazijibu maswai ya msingi:- Mfano, ilikuwaje akauwawa? Nani alitoa amri? Kwa nini?Mchakato mzima ulikuwaje?
3. Wahusika wakuu ambao wanahusishwa na mauaji haya, say Polisi, wamehojiwa?
4. Hojaji ziko wapi? Kina nani walihojiwa? Lini na wapi?
5. Mapendekezo ni ya jumla mno, hayalengi wahusika mbalimbali wa tukio hilo: Wanasiasa? Polisi? Waandishi wa habari? Wananchi?
6. Hatua zipi za kuchukua katika vipindi mbalimbali: Nini kifanyike sasa na kwa haraka? Baada ya muda mfupi? Mapendekezo gani yanatolewa kuzuia hali hii katika kipindi cha muda mrefu? Sera za utendaji? Usimamizi na
uendeshaji wa vyombo husika?
7. Wajumbe wa timu yenu wanakidhi mahitaji ya kazi mliyofanya? wana sifa na vigezo?
Kwa style hii, hakika mtaendelea kuburuzwa.
Labda kama mnayo nyingine, na hii ni kwa matumizi yenu ya ndani. Ni duni interms of quality, content, coverage, methodology, review, findings and recommendations and many others. Dont share it, improve it first.