Ripoti ya CAG inaonesha kuwa, Halmashauri 3 za CHADEMA zimepata Hati chafu

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
988564_859868967438130_2118649736318904539_n.jpg

Ripoti ya CAG inaonesha kuwa Halmashauri 3 zilizopata Hati chafu ni;

1. Karatu DC (CHADEMA)
2. Hai DC (CHADEMA)
3. Kigoma/Ujiji MC (CCM)

Halmashauri 1 iliyopata Hati Mbaya ni Halmashauri ya mji wa Tunduma (Town Council) inayoongozwa na CHADEMA. Hawa walificha vitabu 79 vya mapato, Walificha hati za malipo (voucher) zenye thamani ya SHS.178,511,580, Na walitumia SHS.17,158,500 kufanya malipo yasiyo na viambatanisho. Pia wakati wanakaguliwa hawakuandaa vitabu vya hesabu.

#MyTake:
Nimesikitika sana kuona Halmashauri zilizo chini ya CHADEMA zimeongoza katika kufanya vibaya. Hivi kama tumepewa Halmashauri chache na tukafanya vibaya tukipewa nchi itakuaje?

Tulipaswa kuwa mfano kwa wengine. Wananchi wanakata tamaa kuona tunafanya yaleyale yanayofanywa na CCM. Halmashauri ya Wilaya ya Hai ni nyumbani kwa Mwenyekiti wetu wa chama. Tunaongoza halmashauri hii kwa mara ya pili sasa, hii ilipaswa kuwa mfano. Lakini imetia aibu kwa kupata hati chafu?

Halmashauri ya Karatu alikua anatoka Katibu Mkuu wetu wa Chama Dr.Wilbroad Slaa. Wakati ukaguzi unafanyika alikua bado hajajiuzulu. Maana yake ni kwamba ikiwa Dr.Slaa asingejiuzulu tungekuwa na Halmashauri mbili zenye hati chafu. Moja nyumbani kwa Mwenyekiti wetu na nyingine nyumbani kwa Katibu Mkuu. This typical shame.!

Tutapata wapi moral authority ya kukemea CCM ikiwa tunaruhusu ujinga wa aina hii uendelee kujitokeza kwenye halmashauri tunazoongoza?

Watendaji waliofanya ubadhirifu Hai, Tunduma na Karatu na kutusababishia doa kwenye chama chetu wamechukuliwa hatua gani? Au madiwani wanaendelea kuwalea? Nilitegemea baraza la madiwani Hai, Karatu na Tunduma wawe wameshawang'oa wakurugenzi wa Halmashauri hizo pamoja na watendaji wote waliohusika.

Lakini mnakaa kimya bila kuchukua hatua yoyote then mnategemea wananchi waendelee kutuamini? Kama madiwani wa halmashauri husika mmeshindwa kuchukua hatua mnategemea wananchi ndio wajimobilize na kufanya mobb justice au? Kama ndivyo, nini maana ya nyie kuwepo sasa?

Watanzania wametuamini, wametupa mamlaka ya kuongoza jiji la Dar na Manispaa zake mbili pamoja na majiji ya Arusha na Mbeya. Je ripoti ya CAG inatoa taswira gani kwny haya majiji tuliyopewa kuongoza kama tumeanza kuteleza kwenye halmashauri za wilaya?

Ni aibu kwamba katika Halmashauri 4 zilizofanya vibaya, 3 zinaongozwa na CHADEMA na moja CCM. Hii ni sawa na kusema robo tatu (75%) ya mafisadi waliopo kwenye Halmashauri, wamejaa zaidi kwenye Halmashauri zinazoongozwa na CHADEMA. Hii si sawa hata kidogo na inakatisha tamaa sana.

Nategemea chama kitoe tamko kuhusiana na jambo hili na kwa kuwa halmashauri zote 3 bado zipo chini ya CHADEMA hadi sasa, basi mabaraza ya madiwani yaagizwe kufanya kuchukua hatua kali kwa watendaji wote waliohusika ikiwa ni pamoja na kuwang'oa wakurugenzi.

Haiwezekani kila siku tunakemea wizi serikalini lakini sisi tunalea wezi kwenye halmashauri tunazoongoza. Kama Mayor/Mwenyekiti ameshindwa kuzuia ufisadi kwenye halmashauri yake ni bora ajiuzulu na atoe nafasi kwa wengine wenye uwezo wa kupambana na ufisadi.

Huu sio muda wa kubembelezana, ni muda wa kazi. Wananchi wametuamini na kutupa kazi tusiwaangushe. Ikiwa tunashindwa kuwa waaminifu katika haya madogo hivi, itakuaje kwa makubwa? Tujisahihishe.!

Nimeyasema haya kwa nia njema kbs ya kusaidia chama changu. Marehemu Mohamed Mtoi aliwahi kusema "Tusiwe wepesi wa kutetea uozo kwenye chama chetu, maana tutakuwa hatukisaidii chama wala wabunge wake"

Na ktk hili nimeamua kusimamia maneno ya Mtoi. Siwezi kutetea uozo huu kwa sababu tu umefanywa na chama changu. Never.!

NB: Najua kuna watu wangependa nitoe maoni haya kwenye vikao vya ndani, lakini nimelazimika kuyasema hadharani kwa sababu ufisadi wa halmashauri hizi ulifanyika hadharani na CAG ametoa taarifa yake hadharani na Tanzania nzima inajua kuw ktk halmashauri 4 zilizofanya vibaya, 3 zinaongozwa na CHADEMA na 1 ilikua chini ya CCM lakini kwa sasa ipo ACT.

Narudia maneno ya Marehemu Mtoi kuwa "Tusiwe wepesi wa kutetea uozo ndani ya chama chetu, tutakua hatukisadii chama wala wabunge wake". Penye mazuri tusifie lakini penye makosa tukosoe na kukemea. Chama kwangu ni muhimu lakini Tanzania ni muhimu zaidi.

Malisa GJ.!
 
NYUMBA YA MH MBOWE IMEANZA KUUNGUA MOTO BAADA YA TAARIFA YA CAG

HABARI ZA ASUBUHI NDUGU ZANGU NAONA FAYA WAPOKIKAONI ILI KWENDA KUUZIMA MOTO ASUBUHI HII

MTOA TAARIFA ANASEMA:

TUJISAHIHISHE.!

By Malisa GJ,
Ripoti ya CAG inaonesha kuwa Halmashauri 3 zilizopata Hati chafu ni;
1. Karatu DC (CHADEMA)
2. Hai DC (CHADEMA)
3. Kigoma/Ujiji MC (CCM)

Halmashauri 1 iliyopata Hati Mbaya ni Halmashauri ya mji wa Tunduma (Town Council) inayoongozwa na CHADEMA. Hawa walificha vitabu 79 vya mapato, Walificha hati za malipo (voucher) zenye thamani ya SHS.178,511,580, Na walitumia SHS.17,158,500 kufanya malipo yasiyo na viambatanisho. Pia wakati wanakaguliwa hawakuandaa vitabu vya hesabu.

Nimesikitika sana kuona Halmashauri zilizo chini ya CHADEMA zimeongoza katika kufanya vibaya. Hivi kama tumepewa Halmashauri chache na tukafanya vibaya tukipewa nchi itakuaje?

Tulipaswa kuwa mfano kwa wengine. Wananchi wanakata tamaa kuona tunafanya yaleyale yanayofanywa na CCM.

Halmashauri ya Wilaya ya Hai ni nyumbani kwa Mwenyekiti wetu wa chama. Tunaongoza halmashauri hii kwa mara ya pili sasa, hii ilipaswa kuwa mfano. Lakini imetia aibu kwa kupata hati chafu?Halmashauri ya Karatu alikua anatoka Katibu Mkuu wetu wa Chama Dr.Wilbroad Slaa. Wakati ukaguzi unafanyika alikua bado hajajiuzulu. Maana yake ni kwamba ikiwa Dr.Slaa asingejiuzulu tungekuwa na Halmashauri mbili zenye hati chafu. Moja nyumbani kwa Mwenyekiti wetu na nyingine nyumbani kwa Katibu Mkuu. This typical shame.!

Tutapata wapi moral authority ya kukemea CCM ikiwa tunaruhusu ujinga wa aina hii uendelee kujitokeza kwenye halmashauri tunazoongoza?
Watendaji waliofanya ubadhirifu Hai, Tunduma na Karatu na kutusababishia doa kwenye chama chetu wamechukuliwa hatua gani? Au madiwani wanaendelea kuwalea? Nilitegemea baraza la madiwani Hai, Karatu na Tunduma wawe wameshawang'oa wakurugenzi wa Halmashauri hizo pamoja na watendaji wote waliohusika.Lakini mnakaa kimya bila kuchukua hatua yoyote then mnategemea wananchi waendelee kutuamini?

Kama madiwani wa halmashauri husika mmeshindwa kuchukua hatua mnategemea wananchi ndio wajimobilize na kufanya mobb justice au? Kama ndivyo, nini maana ya nyie kuwepo sasa?Watanzania wametuamini, wametupa mamlaka ya kuongoza jiji la Dar na Manispaa zake mbili pamoja na majiji ya Arusha na Mbeya. Je ripoti ya CAG inatoa taswira gani kwny haya majiji tuliyopewa kuongoza kama tumeanza kuteleza kwenye halmashauri za wilaya?

Ni aibu kwamba katika Halmashauri 4 zilizofanya vibaya, 3 zinaongozwa na CHADEMA na moja CCM. Hii ni sawa na kusema robo tatu (75%) ya mafisadi waliopo kwenye Halmashauri, wamejaa zaidi kwenye Halmashauri zinazoongozwa na CHADEMA. Hii si sawa hata kidogo na inakatisha tamaa sana.

Nategemea chama kitoe tamko kuhusiana na jambo hili na kwa kuwa halmashauri zote 3 bado zipo chini ya CHADEMA hadi sasa, basi mabaraza ya madiwani yaagizwe kufanya kuchukua hatua kali kwa watendaji wote waliohusika ikiwa ni pamoja na kuwang'oa wakurugenzi.

Haiwezekani kila siku tunakemea wizi serikalini lakini sisi tunalea wezi kwenye halmashauri tunazoongoza. Kama Mayor/Mwenyekiti ameshindwa kuzuia ufisadi kwenye halmashauri yake ni bora ajiuzulu na atoe nafasi kwa wengine wenye uwezo wa kupambana na ufisadi.

Huu sio muda wa kubembelezana, ni muda wa kazi. Wananchi wametuamini na kutupa kazi tusiwaangushe. Ikiwa tunashindwa kuwa waaminifu katika haya madogo hivi, itakuaje kwa makubwa? Tujisahihishe.!

Nimeyasema haya kwa nia njema kbs ya kusaidia chama changu. Marehemu Mohamed Mtoi aliwahi kusema "Tusiwe wepesi wa kutetea uozo kwenye chama chetu, maana tutakuwa hatukisaidii chama wala wabunge wake"Na ktk hili nimeamua kusimamia maneno ya Mtoi. Siwezi kutetea uozo huu kwa sababu tu umefanywa na chama changu. Never.!

NB: Najua kuna watu wangependa nitoe maoni haya kwenye vikao vya ndani, lakini nimelazimika kuyasema hadharani kwa sababu ufisadi wa halmashauri hizi ulifanyika hadharani na CAG ametoa taarifa yake hadharani na Tanzania nzima inajua kuw ktk halmashauri 4 zilizofanya vibaya, 3 zinaongozwa na CHADEMA na 1 ilikua chini ya CCM lakini kwa sasa ipo ACT.

Narudia maneno ya Marehemu Mtoi kuwa

"Tusiwe wepesi wa kutetea uozo ndani ya chama chetu, tutakua hatukisadii chama wala wabunge wake". Penye mazuri tusifie lakini penye makosa tukosoe na kukemea. Chama kwangu ni muhimu lakini Tanzania ni muhimu zaidi.

Malisa GJ.!
 
Hapo kwa katibu mkuu umechemka,kwani katibu wa chama na halmashauri vinaingiliana vp?
 
Mimi kwa sasa namwamini Magufuli pekee... Wengine wote nawaona wanafki tu...

Tena kama inawezekana hata mawaziri awafute nchi aongoze yeye na wasaidizi wake wa Ikulu, TISS, Takukuru na Wakurugenzi wa Taasis za serikali... CDM imeniboa inavyotaka kukwamisha kasi ya Magufuli kwa sababu za kijinga kabisa..
 
Mh! Imefika kwa wahusika wale wanaoita wenzao mafisiem.

Lakini suala siyo Halmashauri iko chini ya chama gani chama gani cha siasa. Ukweli unaojitokeza katika utumbuaji wa majipu ni kuota mizizi ya uhujumu uchumi ndani yetu sisi Watanzania.

Nadhani hatua ya kutumbua majipu ni msingi kwa kurudisha uwajibikaji ndani ya nafsi zetu ndipo mifumo irekebishwe. Mifumo iwe ni pamoja na ufuatialiaji na udhibiti (monitoring and control) wa shughuli za kila siku za utendaji serikalini.

Hatua ya Rais Magufuli kuwaasa viongozi wa CCM, katika ngazi zote, wafanye kazi ya kufuatilia watendaji wa Serikali, ni njia mojawapo itakayosaidia kudhibiti uzembe na uhujumu uchumi. Ila chama kinapaswa kujipanga vizuri kutimiza hilo, ikiwa ni pamoja na kuwa na wataalamu.

KUPANGA NI KUCHAGUA. TUJISAHIHISHE
 
Sichezi mbali, nasumbiri tu kuona hii match

Alafu wamilik wa JF... Weken sehemu ya viewers, tuwe tunaona idadi ya waliosoma... najua hapa wataparuka sana
 
Watafanya nini wakati kilichoandikwa kiko wazi?

Wewe ni mpumbavu. Unaanzaje kuzomea DC 3 zenye matatizo ukaacha mamia za CCM zilizooza? Huoni aibu wewe? Hivi wewe ni kiumb wa aina gani uliyetengenezwa bila haya? Hujisikii uchi kwamba tangu Magufuli aiengie madarakani amejikita kuhangaika na mizoga yenye uozo unaunikisha nchi ya CCM? Ungeilikuwa na chembe ya ubinadamu japo kidogo, na kama kweli ungelikuwa umegeuka hilo bichwa lako na kuanza kuona uhalisia, ungejikita kutengeneza mtandao na mfumo wa kuhalisisha utumbuaji wa majibu yenu yaliyosesekela ndani hadi nje ya CCM!.

Mijitu ya CCM na ubaradhuli ni sawa na kambale kwenye maji. Kama umeweza kuona mbali si uisaidie serikali kumaliza majipu yenu ili angalau ipate muda wa ku focus kwenye maswala ya maendeleo badala ya ukarabati wa ufirauni wa CCM?

Mbwaha marehemu!.
 
Huu uzi unakosa kabisa wachangiaji. Wabunge wengi wa CHADEMA wapenda kiki za kwenye media majimboni hakuna wanachokifanya ndo maana wanalia na bunge lionyeshwe live njooni majimboni tuwaone live. saizi kero zetu nyingi tunazikimbiza kwa wakuu wa wilaya maana at least wanaonyesha nia ya kutusaidia
 
Back
Top Bottom