Ripoti maalum hii ya kukojoa porini.,

ngoshwe

JF-Expert Member
Mar 31, 2009
4,131
931
ITV wanaonyesha tatizo la kukosa vyoo barabarani na wananchi kujisaidia porini. Inasikitisha ITV wanaonyesha pia wanawake wakiwa wamevua nguo wakijisaidia! Kma nia ni kurekebisha tatizo sidhani kama kitendo cha kuwafunua miili wanawake wanaojisaidiA porini ni suluhisho! Bwana Monyo!!
 
Waziri wa uchukuzi alikurupuka....alipaswa kwanza kutengeneza miundo mbinu...akaitangaza...akaangalia ufanisi wake...kisha angepiga marufuku wanaokwenda kinyume nayo!!
 
Hata nami nimeona wamama wakidhalilishwa na kamera zao. Si vizuri kabisa.
 
Hivyo vyoo huko barabarani vitakua vinasafishwa na nani?!! Sehemu nyingi hapa tanzania hakuna maji so mtu akienda toilet atajisafishaje? Na vyoo vitasafishwaje.. Vitakua vichafu mno kiasi kwamba abiria au wasafiri wengi bado watakua wanaenda misituni
 
[/COLOR]]ITV wanaonyesha tatizo la kukosa vyoo barabarani na wananchi kujisaidia porini. Inasikitisha ITV wanaonyesha pia wanawake wakiwa wamevua nguo wakijisaidia! Kma nia ni kurekebisha tatizo sidhani kama kitendo cha kuwafunua miili wanawake wanaojisaidiA porini ni suluhisho! Bwana Monyo!!

Taabu ya nchi yetu kuna tabia imejengeka ya ku-divert akili ya wananchi toka kwenye ISSUES KUBWA na kuwa kama zima moto; kila siku kunaibuliwa kitu chakutufanya tuwe busy kujadili, kubishana, hadi kutukanana...wakati siku zinakwenda na serikali haifanyi lolote la maana kutatua matatizo yaliyokuwa ya msingi kwa wananchi!!!!

Mwakyembe hakuwa na sababu ya kuibuka bungeni kuchimba mkwara juu ya KUCHIMBA DAWA wakati anajua wazi hakuna utaratibu wowote uliokwisha wekwa kukabiri tatizo hili!!!! Hizi ni SANAA TUU ZA WANASIASA WETU......DELAYING TACTICS muda wa mchezo uishe....

TAFAKARI....
 
Mi nlikuwa nachimba dawa tangu nikiwa mtoto hadi sasa nimezoea hii tamaduni mpya mwakyembe ameitoa wapi watz tumeshazoea kujichimbia dawa majanini hatukuwa na tamaduni ya vyoo porini tangu enzi ya mwl.
 
Niliangalia il mkuu kwa kweli jinsi camera ya ITV ilivyokuwa inawafata akina mama na dada wakichimba dawa. Ingawa walijaribu kuweka shade kuzuia lakini kuna wakati walionekana wazi sidhani kama ilikuwa lazima kuonyesha picha za wale wanawake....Huenda mpiga picha picha naye alikuwa anavutiwa na mazingira yale....!!!:eek2:
 
Hivyo vyoo huko barabarani vitakua vinasafishwa na nani?!! Sehemu nyingi hapa tanzania hakuna maji so mtu akienda toilet atajisafishaje? Na vyoo vitasafishwaje.. Vitakua vichafu mno kiasi kwamba abiria au wasafiri wengi bado watakua wanaenda misituni

Chifu, hii ni nafasi ya biashara. Si lazima serikali ifanye hili jambo.
Kama una pesa,basi jenga vyoo vya kulipia katika maeneo ambayo watu hupenda kuchimba dawa. Weka miundombinu ya maji,weka wahudumu na walinzi. Kisha toza Tsh. 500 kwa huduma hiyo. Hakika nakwambia utatengeneza pesa za kutosha. Ukiweka huduma hii katika njia zote za mabasi - Dar-Mtwara, Dar-Arusha, Dar-Mwanza, Moro-Mbeya-Sumbawanga n.k. kazi yako itakuwa kucheka tu ukielekea benki.
 
Taabu ya nchi yetu kuna tabia imejengeka ya ku-divert akili ya wananchi toka kwenye ISSUES KUBWA na kuwa kama zima moto; kila siku kunaibuliwa kitu chakutufanya tuwe busy kujadili, kubishana, hadi kutukanana...wakati siku zinakwenda na serikali haifanyi lolote la maana kutatua matatizo yaliyokuwa ya msingi kwa wananchi!!!!

Mwakyembe hakuwa na sababu ya kuibuka bungeni kuchimba mkwara juu ya KUCHIMBA DAWA wakati anajua wazi hakuna utaratibu wowote uliokwisha wekwa kukabiri tatizo hili!!!! Hizi ni SANAA TUU ZA WANASIASA WETU......DELAYING TACTICS muda wa mchezo uishe....

TAFAKARI....

pamoja mkuu, wanasiasa wetu bado wana yaleyale tu, blah blah. binafsi nilishangazwa na hii kauli ya mwakyembe, lakini nadhani ni kwa vile anadhani ishu sio unachokiropoka, but bora umeropoka ili nafasi ijae maneno japo hayana maana yoyote. kwa sababu hakuna maandalizi yoyote yaliyofanyika kuhakikisha wasafiri wanapata sehemu ya kujihifadhi, lakini dkt anaropoka tu, nadhani ni kutokana na ma-confidence ya u-dkt na uwaziri. you can utter anything meen!!!
 
Chifu, hii ni nafasi ya biashara. Si lazima serikali ifanye hili jambo.
Kama una pesa,basi jenga vyoo vya kulipia katika maeneo ambayo watu hupenda kuchimba dawa. Weka miundombinu ya maji,weka wahudumu na walinzi. Kisha toza Tsh. 500 kwa huduma hiyo. Hakika nakwambia utatengeneza pesa za kutosha. Ukiweka huduma hii katika njia zote za mabasi - Dar-Mtwara, Dar-Arusha, Dar-Mwanza, Moro-Mbeya-Sumbawanga n.k. kazi yako itakuwa kucheka tu ukielekea benki.

Kwa hiyo mtu akishikwa na haja mara nne itamcost shs 2000??!! Hivi unajua 2000 kwa mwananchi wa kawaida ni nyingi? Alafu hiyo ni kwenda bado kurudi kwa hiyo safari nzima igharimu shs 4000 hata ka ni mimi ni bora nitumie msitu na ninakuhakikishia hata ka ukiweka walinzi hivyo vyoo vitakua vichafu kupindukia watu wataweka hela mfukoni badala ya kuzihudumia. Nimeshaona hapa tz watu hawajali wananchi na afya zao kila mtu anajali tumbo lake.
 
Chifu, mimi nimeongea katika msingi wa kibiashara na kistaarabu. Sasa kama unaweza kuupa ustaarabu thamani ya kifedha, basi fanya hivyo; lakini naamini huwezi kutoa thamani ya kifedha kwa ustaarabu.
Hivyo kama wewe unaweza kulinganisha ustaarabu na kuupa thamani ya Tsh, 2000 au 4000, basi kila la heri.

Ninachosema hapa ni kwamba kitendo cha kuchimba dawa si cha kistaarabu katika jamii ya binadamu - waliopewa utashi na busara.

Hilo ni wazo la biashara, hivyo si lazima kwako wewe ukaona ni viable, lakini mimi naona ni viable; suala la vyoo kuwa vichafu, watu kuweka pesa mfukoni inategemeana na biashara itakavyoendeshwa.
 
Waziri wa uchukuzi alikurupuka....alipaswa kwanza kutengeneza miundo mbinu...akaitangaza...akaangalia ufanisi wake...kisha angepiga marufuku wanaokwenda kinyume nayo!!

Nionavyo mimi mwakyembe kaandika jibu swali halijui(kadesa). Kwanza angeweka utaratibu wa kuwa na community toilets kadhaa kwa kila njia either kwa serikali kijenga au kushirikisha wadau wengine. Kukataza watu wasichimbe dawa ghafla bila njia mbadala naona ni kituko, tutaendelea kama kawa....
 
Back
Top Bottom