RIPOTI MAALUM: HATARI KUBWA KWA WANANDOA.

RIPOTI MAALUM: HATARI KUBWA KWA WANANDOA.

Kingsmann

JF-Expert Member
Joined
Oct 4, 2018
Posts
5,564
Reaction score
21,070
Na Bollen Ngetti

HUU ni utafiti ambao umenichukua takriban miezi 6! Ilikuwa niikabidhi kwenu wadau na Serikali wiki mbili zilizopita lakini haikuwa hivyo kutokana na sababu zilizokuwa nje ya uwezo wangu!

Nitumie ukuta huu kutoa ripoti japo kwa mhutasari ila kwa kirefu itachapishwa katika moja ya gazeti la kila siku next week baada ya sikukuu hizi za Idd!

Baada ya Tume ya TACAID kutoa taarifa ya hali ya UKIMWI nchini ya mwaka 2017/18 na kutaja mikoa inayoongoza kwa maambukizi mapya ikitaja Njombe na Iringa kuwa vinara niliamua kutafiti suala Zima la mahusiano ya kingono jijini Dar es salaam. Nilichokibaini kina ukakasi kwa wanandoa na familia kwa ujumla.

Jambo la kwanza lililonisukuma kufanya utafiti ni mlipuko wa ujenzi wa hoteli, nyumba za kulala wageni (lodge) jijini Dar nikiuliza hasa wateja wakubwa ni kina nani? Je, nyumba hizi wanalala wageni kama zinavyoitwa??

Utafiti ulihusisha Manispaa za Ilala, Kinondoni, Ubungo na Kigamboni. Katika Manispaa ya Ubungo zilihusisha "lodge" 7, Kinondoni (11), Ilala (3) na Kigamboni lodge 1. Nitoe shukrani kwa mameneja wa hoteli na loji hizi na wadau wengine ambao walinipa ushirikiano mkubwa.

Jambo la kwanza mjue kwamba 87.2% ya wanaoingia kupumzika ndani ya loji hizi kwa kile kinachoitwa "short time" ni wanandoa. Katika hiyo 87.2 asilimia 91 ni wanawake na mida yao ya kuingia kufanya ngono ni Kati ya saa 2:30 asubuhi hadi saa 8 na tisa mchana. Hawa ni wale ambao waume zao hudamka makazini na kurejea jioni huku wengi wao wakiwa ni mama wa nyumbani. Wachache miongoni mwao ni wafanyakazi. Mfano: nimekutana na kesi ya mke wa mtu kudamka alfajiri ya saa 11 'kuwahi kazini" Kariakoo kumbe saa 12am anakutana kwanza na mtu wake dereva wa bajaji wanajamiiana hadi saa mbili ndipo huingia ofisini bila mume kujua anayebaki nyumbani kwenda kazini saa 2!

Wanaume wanaoingia na michepuko mida hiyo wengi wao 68% ni waliojiajiri binafsi. Pete nyingi za ndoa huvuliwa endapo mmoja si mwanandoa ku-balance situation!

Wanawake single lakini wafanyakazi huingia kwenye nyumba hizi Kati ya saa 10 alasiri na kurejea nyumbani Kati ya saa 4 na 5 za usiku, hii imekithiri mno maeneo ya Tabata, Sinza na Kigamboni.

Ni asilimia Kati ya 9 na 14 tu ya vijana walio chini ya miaka 22 wanaoingia katika nyumba hizi na sababu iliyotajwa ni uchumi maana ili kulala katika lodge hizi unahitaji Kati ya Sh 50,000 hadi 120,000 kutegemeana na mazingira maana hapo kuna kula, kunywa, malazi na "posho" inayolewa ama na mwanaume au mwanamke kwa mwanaume!

Uchunguzi umebaini kuwa mathalan siku za sikuu kama kesho ndoa nyingi huvunjika kwa maana kuchepuka kuliko idadi ya kondom zinazopasuka. Kinachosikitisha ni kwamba matumizi ya kondom yameshuka sana kwa michepuko wanandoa!

Sehemu nyingi mara ya kwanza baada ya kujamiiana ungekuta kondom zilizotumika ndani ya kapu la taka lakini kuanzia ngono ya tatu kuendelea kondom ziliwekwa pembeni. Ama tulizikuta nzima chini ya Mito au ndani ya kapu la taka.

Kwa mantiki hii maambukizi ya magonjwa ni makubwa na hata mimba zisizotarajiwa wamesakiziwa wenza wao bila kujua.

Matumizi ya magari ya tinted ni makubwa mno katika zoezi hili huku bodaboda nao wakiwa ni wasiri wakubwa katika mchakato huu wa aibu. Mfano mahali tulibaini mke akiwa na bodaboda wake special kumpeleka kwa mchepuko na kumrudisha!

Kina mama wengi wanaochepuka mfano 53% waliohojiwa walidai ni kutotosheka nyumbani kwenye game hasa Sinza lakini uchunguzi ukabaini pia si kwamba waume zao hawana nguvu Bali nao humalizwa nguvu na michepuko akirudi nyumbani Yuko hoi bin taaban akimpanda mke ni kama kuku! Hakuna maandalizi (fore play)!

Kwa mantiki hiyo tunaweza kukuta mnyororo wa ngono nje ya ndoa ulivyo mrefu.

Lakini linalosikitisha sana ni wake za watu ndio wameongoza kwa kuingiliwa kinyume na maumbile maarufu kama 0713. Utafiti umebaini kuwa wengi wa wake hawa 72% Kati ya 25 waliohojiwa waliwahi kufanya kazi ya ukahaba lakini hata baada ya kuolewa hawakusitisha mawasiliano na wateja wao. Hata hivyo kwa waume zao ni wakali kama pilipili wakiulizwa 0713!

Kinondoni na Ubungo ni vinara wa biashara hii ya 0713 ikifuatiwa na Kigamboni. Hata hivyo uchunguzi umebaini mpishano wa maeneo kasoro Kinondoni. Kwamba mtu wa Kinondoni huenda kufanya ngono Ubungo, wa Ubungo ataenda Ilala nakadhalika. Alimradi awe mgeni eneo husika na hili lilirahisisha kuchunguza. Wengi lodge moja ndio maskani ya kudumu na wengine wana vyumba maalumu!

Utafiti unaonesha kuwepo kwa gesti bubu kuliko hata maduka ya dawa au maktaba ya vitabu katika mtaa mmoja. Mfano Tabata unaweza kutembea sana kutafuta bookstore lakini si guest house na bar! Hii imefanya waliokuwa na nyumba za kupangisha badala ya kusubiri kodi ya miezi 6 anaona apageuze gesti italipa kwa haraka!

Kwa kifupi wadau suala la ngono jijini Dar liko juu sana kiasi kwamba kama hatutachukua hatua jiji hili litazama na kupotea kama Sodoma maana maeneo mengine hadi watoto tumewakuta wakiwa mijibaba ndani. Hii ni hatari! Tunadhani maambukizi ni kidogo lakini ukweli ni kwamba Njombe na Iringa waliitikia sana kupima kuliko Dar.

Ninashauri tuwe na Sheria kali kidogo na Gavana Makonda lichukue hili. Mtu yeyote mume na mke wasiruhusiwe kuingia gesti bila kuonesha Cheti au uthibitisho wa uhalali wa uhusiano wao. Kila lodge ifunge CCTV camera zinazokuja kukaguliwa mwisho wa siku endapo tatizo litatokea. Hii ni kwa sababu tumekutana na ya watu mara akifika tu swali la kwanza ni kama Kuna CCTV basi haingii tena! Nini kama si uhalifu wa kingono? Vitambulisho vikaguliwe na kinachoitwa 'short time" iwe ni marufuku kabisa. Ukichukua chumba LALA! Ni mapumziko gani ilhali huko ndani ni miguno tu hakuna kupumzika?

Ripoti kamili next week. Ndoa nyingi hatarini. Vitabu vya wageni vikionesha unatoka wapi uoneshe Ticket na si From Dar to Dar! Tujadili!
#AchaWoga2020
0786 791 229
Bollen Ngetti

C&P.
 
Ukishatoka Ilala ukaenda temeke si tayari umeshakuwa mgeni basi ni ruhusa kulala nyumba ya wageni.

Ila swali unalala na nani na usalama wa huyo unae lala nae ukoje.

Kiukweli kabisa maambukizi ya UKIMWI sidhani kama ni ukweli kuwa ni makubwa zaidi huko mikoani kuliko hapa Dar, kwa wimbi la ngono lilolopo hapa ni ushadi tosha kuwa maambukizi hapa nimakubwa zaidi.
Labda muitikio wa watu kupima Dar ni mdogo hivyo kuonekana kuna asilimia chache, lakini kiukweli huu mkoa ndio unaongoza kwa UKIMWI mimi nadhani hivo.
 
Research nzuri sana hii. Lakin mheshimiwa ungetoa na solution ya hiki jambo ili watu wajue la kufanya. Maana unzinzi unakua maradufu kuliko kitu kingine.
 
Wewe acha masikhara Dar ndio kuna uchafu wa ngono kupindukia

Lakini mikoani kunaongoza hasa kwenye hizi boda zetu ndio balaa tembelea Tunduma,Namanga,Horohoro n.k

Huko watu wanafanya ngono muda wote hasa madereva na watu wanaohusika kwenye seka ya usafirishaji, kumbuka watu hawa wote wameacha familia zao huko

Utafiti wako ni mzuri lakini naona umebase zaidi kwenye sample aina moja wenye kipato, uku kwetu uswahilini ngono is very cheap mtu hawezi kutoa 50,000 au laki kwa ajili ya ngono ambayo iko available

Malaya kibao wanajiuza katika mitindo mbalimbali kuna kisa kimoja miaka ya 2000 nilikuwa naishi buguruni kwa mnyamani, jamaa alikuwa anamuuza mke wake live bila chenga tena kwa dau la tsh 1,500/ by that time
Mimi nilikuwa Mteja mzuri sana yaani kipindi icho bado sijaoa

So ngono ni hitaji muhimu sana kwa binadamu na huwezi kumcontrol
 
Hapo mwisho ndio umezingua, sijui itungwe sheria Kali mala wafunge CCTV, mala Wateja wwonyeshe cheti cha ndoa, hv kwa ufahamu wako unaona hicho ni kitu kirahisi kweli? Mbona madawa ya kulevya yamepigwa marufuku lakini watumiaji wako chungu tele? Mbona biashara ya ukahaba inaendelea?

Angalia ushoga hauruhusiwi lkn umejaa itawezekana kuzuia mwanaume na mwanamke kuingia lodge? Utafiti wako siupingi lkn solution uliyokuja nayo ni ngumu, nenda mawilayani gest sio nyingi sn lkn kuna ngono balaa wanafanyia wapi?

Nenda vyuoni na mshuleni ngono zimejaa nadhani ungeshauri matumizi ya Mpira zaidi km kinga lkn kuzuia watu kwenda gest ni ngumu kumbuka hata hao wamiliki hawatakubali kupoteza wateja
 
Watu wanaroho mbaya......hiv hadi unamuhoji mke aliyechepuka na anakwambia eti amechepuka kwasabab haridhiki......kweli mwanamke(mgoni) awe na ujasir wakufanyiwa enterview haaaa hili liweke sawa labda hakumpata muhusika au umewajazia sehem yao
 
Back
Top Bottom