Ripoti iliyotuhumu Tanzania si rasmi-UN | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ripoti iliyotuhumu Tanzania si rasmi-UN

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Ng'wanza Madaso, Dec 3, 2009.

 1. Ng'wanza Madaso

  Ng'wanza Madaso JF-Expert Member

  #1
  Dec 3, 2009
  Joined: Oct 21, 2008
  Messages: 2,278
  Likes Received: 60
  Trophy Points: 145
  Ripoti iliyotuhumu Tanzania si rasmi-UN [​IMG] [​IMG] [​IMG] Thursday, 03 December 2009 07:01 Na Tumaini Makene

  UMOJA wa Mataifa (UN) umetoa taarifa rasmi kuhusu ripoti inayoituhumu Tanzania kuwasaidia waasi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Congo (DRC) kuwa ililalamikiwa wakati haijachapishwa rasmi.

  Pia umoja huo umejitenga na ripoti hiyo, ukieleza kuwa ilitolewa na jopo la wataalamu walioteuliwa na kupewa mamlaka ya kutafiti iwapo maamuzi ya kuviwekea vikwazo vikundi vya waasi vilivyoko DRC yanatekelezwa.

  Taarifa ya UN iliyolifikia gazeti hili jana ilisema ripoti hiyo haipaswi kuhusishwa moja kwa moja na Sekretarieti ya UN wala mashirika yake yaliyopo nchini, bali ihusishwe na jopo hilo chini ya Mwenyekiti wa Kamati ya Vikwazo vya DRC, ambayo kwa sasa inaongozwa na Uturuki.

  Taarifa hiyo iliyosainiwa na Afisa Habari wa UN, Bi. Usiah Ledama imekuja siku chache baada ya Waziri wa Mambo ya Nje, Bw. Bernard Membe kutoa tamko la kulaani ripoti hiyo kwamba ni ya uongo na kuitaka UN kuiomba radhi Tanzania.

  Ufafanuzi huo wa UN unamaanisha kuwa Bw. Membe alilalamikia taarifa hiyo kabla ya kuchapishwa wala kujadiliwa na Baraza la Usalama la umoja huo, hivyo kuondoa uhalali wake.

  Tayari Chama cha Demokrasia na Maendeleo kimetoa tamko la kumkosoa Bw. Membe, kikimtaka kujibu hoja moja moja na kuwaacha waliotajwa katika taarifa hiyo kuwajibika badala ya 'kufunika kombe mwanaharamu apite'.

  Hata hivyo, pamoja na UN kujitenga na ripoti hiyo, imesema baada ya kukamilika itajadiliwa na Baraza lake la Usalama.

  "Kundi hilo wa wataalamu limekuwa likitoa taarifa mara kwa mara juu ya utafiti wao kuhusu masuala ya vikwazo vya silaha huko DRC, ripoti ya sasa ambayo imezua mjadala katika vyombo vya habari haijachapishwa wala kupitishwa rasmi, ingawa hatua hiyo itafanyika hivi karibuni.

  "Kwa hiyo kikundi hicho cha wataalamu kimepewa mamlaka ya kufanya utafiti wa mara kwa mara na kutoa mapendekezo katika taarifa ambayo inajadiliwa na Kamati ya Vikwazo na Baraza la Usalama ambako kikundi hicho kinawajibika," ilisomeka sehemu ya taarifa hiyo ya UN nchini huku ikiongezea kuwa wataalam hao wameongezewa muda wao wa kufanya kazi kwa mwaka mzima.

  "UN inafanya kazi kama kitu kimoja kwa kujumisha idara, mifuko, mashirika, na mipango mbalimbali bado kuna umuhimu wa kutofautisha kati ya mihimili ya utendaji kama Baraza la Usalama na ile inayohusika na utekelezaji wa sera kama vile sekretarieti ya UN na mashirika yake yaliyoko nchini yakishirikiana na serikali katika shughuli za kimaendeleo," ilisema taarifa hiyo.


  Source: Majira
   
 2. Bluray

  Bluray JF-Expert Member

  #2
  Dec 3, 2009
  Joined: Mar 25, 2008
  Messages: 3,446
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 135
  Naona Mahiga na Migiro wana work magic zao UN !

  Hapa kuna politics kibao zishaanza kuingia, Ban ki-moon mwenyewe ni suspect kama a Tanzania goon.
   
 3. Semenya

  Semenya JF-Expert Member

  #3
  Dec 3, 2009
  Joined: Sep 5, 2009
  Messages: 572
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 35
  Ndo maana akina Mnyika et all, wasikurupuke. haya mambo ni mazito. All in all pia emage ya TZ inabdi tuilinde, sio tu kushangilia eti UN wametoa report basi na watanzania nao wako kipaumbele kuiunga mkono.........UN hawa au mataifa ya magharibi, wana destroy sana amani Africa, ni kuwa nao waangalifu sana, na si kuwa entertain au kuwashangilia.

  Katika mambo haya bwanamdogo MNYIKA, maslahi ya taifa hayana chama. Jifunze hata marekani, walipompiga Saddam Hussein...Bush alipata kura kutoka republican na democrats. Hii inamaana USA walikubaliana wote kuilinda interest ya USA, na kuondoa uchama. Sasa wewe bwa mdogo MNYIKA katika swala hili pia maslahi ya TZ yalinde na uuondoe uo u CHADEMA.

  Sawa?
   
 4. Jayfour_King

  Jayfour_King JF-Expert Member

  #4
  Dec 3, 2009
  Joined: Nov 15, 2009
  Messages: 1,142
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Cha msingi hapa ni kwamba tujitahidi pale inapowezekana tuwe wasafi kama nchi. Na tusikubali wajanja wachache wapige deal kwa kutumia udhaifu au uzembe tulionao kama nchi. Tukikaa kimya siku mambo yakiharibika sifa mbaya zitakuja kwa nchi nzima. Tusaidiane kuwanyooshea vidole wahalifu kama wapo miongoni mwetu.
   
 5. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #5
  Dec 3, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Kwa hiyo Membe alichofanya ni pre-emptive attack against the UN?
   
 6. Barubaru

  Barubaru JF-Expert Member

  #6
  Dec 4, 2009
  Joined: Apr 6, 2009
  Messages: 7,162
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 0
  Mnyika wacha kutafuta umaarufu. Weka maslahi ya Taifa mbele.
   
 7. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #7
  Dec 4, 2009
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  UN, YALIYOMO KWENYE RIPOTI NI KWELI AU SIO KWELI??????? FULL STOP.

  ikiwa ni kweli lakini sio rasmi na ikiwa ni kweli lakini rasmi kutakuwa na tofauti yoyote????? Wasitufanye mazoba hawa.
   
Loading...