RIPOTI: Athari ya COVID-19 katika Biashara ukanda wa Afrika Mashariki

OLS

JF-Expert Member
Oct 12, 2019
419
670
COVID19 iliyotokea tangu Desemba mwaka 2019 imeleta matatizo kati nyanja za kiafya, kijaii na kiuchumi. Janga hili lilitangazwa kuwa janga la kidunia tarehe 11 Machi 2020

Wanachama wote wa jumuia ya Afrika Mashariki, Burundi, Kenya, Uganda, Rwanda, Sudani Kusini na Tanzania wameripoti kuwa visa vya virusi hivi. Hatu mbalimbali zimechukuliwa ili kuzuia tatizo hili ikiwemo kuzuia safari, zuio la wananch kutoka nje na kuleta matokeo hasi kwenye biashara na uwezekezaji kwa ujumla

Baraza la Biashara la Afrika Mashariki (EABC) limefanya tafiti ilikuonyesha madhara ya COVID19 kwenye biashara kwa ujumla, tafiti ililenga kungalia sekta zilizoathiriwa kimapato sana

Katika taarifa hiyo imeonyesha kuwa mapato katika sekta ya Utalii imeathirika kwa asilimia 92, wakati sekta ya afya ikiwa haijaathirika kwa maana ina asilimia 0.

2020-05-09 (5).png


Kutokana na hilo, baraza limeshauri namna ya kufanya ili kuzuia madhara zaidi kwenye sekta ambazo ziko negatively affected hadi hivi sasa
  • Kwanza kutenga hela za kutosha ili kuwarudishia kodi ya ongezeko la thamani (VAT) na kuwalipa watu wanaodai serikali(Madeni ya ndani) . Hatua hii itaongeza ukwasi kwa biashara na kukuza mitaji yao kwa kipindi hiki cha corona virus
  • Benki kuu kuongeza mikopo kwa benki za biashara
  • Benki kuu kupunguza kiwango cha riba, ili kufanya benki za biashara ziweze kukopa katika riba ndogo ili nao pia wakopeshe wafanyabiashara kwa riba ndogo
  • Kupunguza kodi za makampuni hadi 20% hii itawasaidia wafanyabiashara na makampuni kuwa na ukwasi wa kuweza kuwekeza kwenye biashara ili kuzikuza
  • Ni muhimu kutoa muda wa kutodai VAT, PAYE na malipo mengine ili kuleta unafuu kwa wafanya biasahra na makampuni
  • Kuruhusu makampuni yatakayofuata miongozo ya kujikinga na COVID19 kuendelea na shughuli zao badala ya kuweka zuio la moja kwa moja

NAMNA BIASHARA ZILIVYOATHIRIKA

Tafiti hiyo imeonyesha kuwa 55.9% ya walioshiriki ktika utafiti huo wameonyesha kuathirwa na zuio la kutovuka mipaka ya nchi zao. Na 55.9% nyingine wakiwa wameathiriwa kwa upungufu wa mauzo

2020-05-09 (6).png


BARAZA LIMESHAURI
  • Kuruhusu biashara (Free movements) ndani ya nchi wanachama
  • Pia kufuta tozo na malipo ambayo yana madhara, kwa malighafi, na bidhaa muhimu. Hii itafanya wazalishaji kuleta bidhaa katika bei nafuu
  • Pia Kodi ya ongezeko la Thamani kushuka hadi 12% kwa kipindi hiki cha COVID19. Hii yote ni namna ya kupunguza bei za bidhaa kwa kipindi hiki cha covid19 hii itafanya kuongeza mauzo ya bidhaa

MAAMUZI YA KAMPUNI KUPUNGUZA WAFANYAKAZI

Tafiti imeonyesha 36.4% ya makampuni yamesema wako tayari kupunguza idadi ya wafanyakazi. Makapuni 18.2% yamesema hayatapunguza wafanyakazi huku 45.5% wakisema hawajui kama wanaweza kupunguza wafanyakazi au la

Katika hilo baraza limeshauri kuondoa tozo/ushuru wa ajira.

2020-05-09 (7).png


Pia tafiti imeonyesha 44.7% ya makampuni yako tayari kuzisaidia serikali kwa kutoavifaa ili kupambana na COVID19

Baraza limehitimisha kwa kuwataka wanajumuia wa afrika mashariki kuchukua hatua zilizoshauriwa ili kulinda ajira, mauzo ya nje na kuongeza hali ya mchangamano wa shughuli ndani ya nch wanachama
 
Hapo kwenye tourism Hali ndio mbaya kabisa kuwahi kushudiwa, ila ninaimani serikali sikivu itaimaliza corona nchini
 
Back
Top Bottom