Riport ya pili ya makinikia ilitakiwa ikasomewe uwanja wa Taifa!

Nichumu Nibebike

JF-Expert Member
Aug 28, 2016
8,658
15,791
Hii riport ya pili ya makinikia ilitakiwa ikasomewe kwenye uwanja wa taifa, maana huu mpambano ni mkali zaidi ya mechi ya Yanga na Simba...
Hili lingetoa wigo mkubwa wa wananchi wengi kuishuhudia riport hii muhimu katika uchumi wa nchi yetu!
Hawa majamaa wametunyonya vya kutosha.
Pesa ya tozo la VAT kwenye utalii ya mwaka mmoja inayokadiriwa kufikia trilioni nne za kitanzania ni zaidi ya pesa ambayo nchi imepata kwenye madini kwa miaka kumi!
 
Tafuteni mafundi watengeneze bombardier moja imelala chini mwezi wa tatu huu.mna kazi ya kushadadia umbeya.
 
Hii riport ya pili ya makinikia ilitakiwa ikasomewe kwenye uwanja wa taifa, maana huu mpambano ni mkali zaidi ya mechi ya Yanga na Simba...
Hili lingetoa wigo mkubwa wa wananchi wengi kuishuhudia riport hii muhimu katika uchumi wa nchi yetu!
Hawa majamaa wametunyonya vya kutosha.
Pesa ya tozo la VAT kwenye utalii ya mwaka mmoja inayokadiriwa kufikia trilioni nne za kitanzania ni zaidi ya pesa ambayo nchi imepata kwenye madini kwa miaka kumi!

Hilo halitawezekana mkuu kwa sababu za kiusalama zaidi.
 
Kila aliyehusika anaitwa hapo hapo ajisalimishe, na waliokuwepo risasi..
 
Halafu baadae mpige kelele kuwa Rais wetu mpendwa ametumia pesa nyingi namba moja kwenye ulinzi n.k
 
Kwanini kesho isiwe siku ya mapumziko ili watu wengi wafuatilie, ila wasisahau kuwataja walioingia mikataba hii mibovu.
 
Mnaboa sana nyie watu; katiba mpya amtaki kuiweka ili mwanachi apate nguvu ya kuilinda nchi yake bali mnataka makofi kutoka kwa mwananchi huyo. DPP mmempa nguvu nyingi kwenye katiba iliyopo sasa wala amsikii.

Tuanze kitu from grassroots nyie mnaanzia sijui wapi ili tu tupige makofi. Tatizo ni Katiba>Mikataba>Sheria>Mamlaka; yaani umeshasema kwenye katiba kua Fisi atashitakiwa baada ya kumaliza muda wake wa kula kondoo aliochukua kwenye zizi alafu unarudi kulialia si unaonekana kichaa
 
Back
Top Bottom