Ni lazima uchunguzi ufanyike ili ijulikane wazi nani hasa alikuwa mshindi wa uchoraji nembo yetu ili isije kuwa hata washiriki walioingia tatu bora nao wakajiita ni washindi wa nembo ya TaifaRip mzee wa watu
Hii nchi ya viwanda ina maana haina kumbukumbu sahihi mkuu?Lakini Bado tunahitaji kumbukumbu ziwekwe sawa kwa manufaa ya historia
Shida ubabaishaji mwingiHaina ingekuwepo wasingehaha na marehemu mzee Ngosha na huu mkanganyiko uliotokea
stempu ya posta
Wazo lako ni kubwa sana. Mkuu historia ya nchi yetu kwa siku za karibuni inapotea kwa kasi! Ninafikiri moja ya sababu ni kutokana na kutofanya maadhimisho ya matukio ya kihistoria; mfano sikukuu za uhuru,hazifanyiki ipasavyo au kuheshimiwa hadi vijijini kama ilivyokuwa zamani. Kulikuwa na viwanja karibu kila kijiji,Wilaya hadi Mkoa vya maadhimisho haya na kuliwekwa kumbukumbu mbalimbali za kihistoria kukumbusha watu tulikotoka. Pia hapo nyuma tulijifunza mambo mengi ya kihistoria achilia mbali ile ya darasani, ila kupitia nyimbo,maigizo na hotuba wakati wa sherehe za kumbukumbu za kihistoria,mfano kina Seth Benjamin,Bibi Titi Mohamed,Lucy Lameck,Mh.Kawawa bila kusahau kina Morisi Mnyusa (mpiga ngoma),tuliwajua kupitia nyimbo mashuleni n.k. Ukiniuliza leo kazi walizozifanya kupigania uhuru wetu,nitakueleza bila kusoma mahali. Pia viongozi wetu sijui niseme wamekuwa wa kisasa zaidi;mfano utakuta lugha zinazotumika na wakuu haziashirii utaifa kutokana na baadhi kutojua historia. Au unakuta mahali,bendera ya Taifa inashushwa,watu wanatembea tuu,hawasimami kwa heshima kama ilivyokuwa hapo nyuma,na wasiposimama hakuna hatua yeyote inachukuliwa. Na wanaojua,wanakaa kimya au wanabezwa!Lakini Bado tunahitaji kumbukumbu ziwekwe sawa kwa manufaa ya historia